Wednesday, 5 June 2024

SHUWASA YAENDESHA WARSHA KWA MADIWANI, YAANIKA HATUA ZILIZOFIKIWA UJENZI MRADI MKUBWA WA MAJI SHINYANGA


Katibu Tawala Wilaya ya Shinyanga, Ndugu. Said Kitinga akizungumza wakati akifungua warsha kwa Madiwani, Maafisa Tarafa na wadau wa maji wilaya ya Shinyanga iliyoandaliwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA).

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) imeendesha warsha kwa Madiwani, Maafisa Tarafa na wadau wa maji wilaya ya Shinyanga kwa lengo la kueleza utekelezaji wa majukumu ya SHUWASA na hatua zilizofikiwa kuhusu ujenzi wa mradi mkubwa wa Majisafi na Usafi wa Mazingira kwa eneo linalohudumiwa na SHUWASA.


Warsha hiyo imefanyika leo Jumatano Juni 5,2024 katika Ukumbi wa mikutano Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga ambapo mgeni rasmi alikuwa Katibu Tawala Wilaya ya Shinyanga, Said Kitinga
kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mheshimiwa Wakili Julius Mtatiro.

Katibu Tawala Wilaya ya Shinyanga, Said Kitinga amesema mradi huo mkubwa unaenda kumaliza tatizo la maji Shinyanga huku akiishukuru serikali kwa kuwezesha utekelezaji wa miradi ya maji ili kutatua changamoto za wananchi.

Mkurugenzi Mtendaji wa SHUWASA, Mhandisi Yusuph Katopola ameeleza kuwa kupitia mradi huo ambao tayari utekelezaji wake unaendelea wanaenda kumaliza tatizo la huduma ya maji katika maeneo yote ya Shinyanga.

Mhandisi Katopola ameeleza kuwa hali ya upatikanaji wa maji safi na salama kwa sasa ni nzuri katika maeneo yote wanayoyahudumia na kwamba SHUWASA imeendelea kupanua mtandao wa maji safi, kuongeza mapato yatokanayo na mauzo ya maji, kuongeza idadi ya wateja, kupunguza upotevu wa maji na inaendelea na ujenzi na utekelezaji wa miradi ya maji.

Ameeleza kuwa, SHUWASA inajihusisha na utoaji wa huduma ya maji safi na usafi wa Mazingira katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga na Miji midogo ya Tinde, Didia na Iselamagazi iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.


Mhandisi Katopola amesema mnamo tarehe 20.06.2022, Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Fedha ilisaini Mkataba wa fedha na Shirika la Maendeleo la Ufaransa (French Development Agency - AFD) kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa Majisafi na Usafi wa Mazingira wenye thamani ya EURO milioni 76 (Euro 75 ni mkopo wa riba nafuu toka Shirika la Maendeleo la Ufaransa na Euro milioni 1 zinatolewa na Serikali ya Tanzania).


Nao washiriki wa warsha hiyo, mbali na kuipongeza serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika utekelezaji wa miradi ya maji ili kumtua mama ndoo kichwani huku wakishauri mradi huo utakelezwe kwa wakati ili kutatua changamoto ya maji kwa wananchi wa Shinyanga.


Aidha wameshauri wananchi waendelee kushirikishwa kuhusu hatua mbalimbali za utekelezaji wa mradi huo ikiwa ni pamoja na utoaji elimu kwa jamii.
Katibu Tawala Wilaya ya Shinyanga, Ndugu. Said Kitinga akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mheshimiwa Wakili Julius Mtatiro leo Jumatano Juni 5,2024 katika Ukumbi wa mikutano Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga wakati akifungua warsha kwa Madiwani, Maafisa Tarafa na wadau wa maji wilaya ya Shinyanga iliyoandaliwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) kwa lengo la kueleza utekelezaji wa majukumu ya SHUWASA na hatua zilizofikiwa kuhusu ujenzi wa mradi mkubwa wa Majisafi na Usafi wa Mazingira kwa eneo linalohudumiwa na SHUWASA. PICHA na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Katibu Tawala Wilaya ya Shinyanga, Said Kitinga akizungumza kwa niaba na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro leo Jumatano Juni 5,2024 wakati akifungua warsha kwa Madiwani, Maafisa Tarafa na wadau wa maji wilaya ya Shinyanga iliyoandaliwa na SHUWASA
Katibu Tawala Wilaya ya Shinyanga, Said Kitinga akizungumza kwa niaba na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro leo Jumatano Juni 5,2024 wakati akifungua warsha kwa Madiwani, Maafisa Tarafa na wadau wa maji wilaya ya Shinyanga iliyoandaliwa na SHUWASA
Katibu Tawala Wilaya ya Shinyanga, Said Kitinga akizungumza kwa niaba na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro leo Jumatano Juni 5,2024 wakati akifungua warsha kwa Madiwani, Maafisa Tarafa na wadau wa maji wilaya ya Shinyanga iliyoandaliwa na SHUWASA
Mkurugenzi Mtendaji wa SHUWASA, Mhandisi Yusuph Katopola akizungumza wakati wa warsha kwa Madiwani, Maafisa Tarafa na wadau wa maji wilaya ya Shinyanga iliyoandaliwa na SHUWASA
Mkurugenzi Mtendaji wa SHUWASA, Mhandisi Yusuph Katopola akizungumza wakati wa warsha kwa Madiwani, Maafisa Tarafa na wadau wa maji wilaya ya Shinyanga iliyoandaliwa na SHUWASA
Mkurugenzi Mtendaji wa SHUWASA, Mhandisi Yusuph Katopola akizungumza wakati wa warsha kwa Madiwani, Maafisa Tarafa na wadau wa maji wilaya ya Shinyanga iliyoandaliwa na SHUWASA
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Ramadhan Masumbuko akizungumza wakati wa warsha kwa Madiwani, Maafisa Tarafa na wadau wa maji wilaya ya Shinyanga iliyoandaliwa na SHUWASA
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Ramadhan Masumbuko akizungumza wakati wa warsha kwa Madiwani, Maafisa Tarafa na wadau wa maji wilaya ya Shinyanga iliyoandaliwa na SHUWASA
Washiriki wa warsha wakiwa ukumbini
Washiriki wa warsha wakiwa ukumbini
Washiriki wa warsha wakiwa ukumbini
Washiriki wa warsha wakiwa ukumbini
Washiriki wa warsha wakiwa ukumbini
Washiriki wa warsha wakiwa ukumbini
Washiriki wa warsha wakiwa ukumbini
Washiriki wa warsha wakiwa ukumbini
Washiriki wa warsha wakiwa ukumbini
Washiriki wa warsha wakiwa ukumbini
Washiriki wa warsha wakiwa ukumbini
Washiriki wa warsha wakiwa ukumbini

Share:

Tuesday, 4 June 2024

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATANO JUNE 5,2024

Share:

WAKAZI WA KIGOMA WASHAURIWA KUWEKEZA KWENYE HATI FUNGANI ZA SERIKALI



Na,Chedaiwe Msuya-Wizara ya Fedha-Kigoma.

Wananchi Mkoani Kigoma wametakiwa kujenga utamaduni wa kuwekeza fedha zao kwa kununua Hati Fungani mbalimbali zinazouzwa na Serikali ili iwe moja ya vyanzo vya kujiongezea vipato badala ya kuweka fedha zao katika mfumo usio rasmi.

Akizungumza na Timu ya watalaamu kutoka Wizara ya Fedha, Katibu Tawala Mkoa Kigoma, Bw. Hassan Abassi Kaigwa alisema kuwa uzoefu unaonyesha watu wengi wanaonunua Hati Fungani za Serikali hunufaika kwa kupata faida muda mfupi huku mtaji wao ukiendelea kuwepo na kutoa wito kwa wananchi wanaomiliki fedha kuchangamkia fursa hiyo.

“ katika Hati Fungani za serikali kwa mwaka unaweza kupata faida kati ya asilimia 12 hai 15 ambapo kwa mtu aliyenunua bondi za thaman ya shilingi million 200 anauwezo wa kupata zaidi ya shilingi milioni 24 kwa mwaka huku mtaji wake ukiwa palepale, mzunguko huu wa fedha sio jambo la kulipuuzia hivyo ni muhimu kila mwananchi achangamkie fursa hii adhimu” Alisisitiza Bw. Kaigwa.

Alisema kuwa sio lazima watu wote wawe wafanyabiashara bali wengine wanaweza kuwa wadau au wabia wa benki ama uwekezaji ili wanaojua kufanya biashara wafanye shughuli hiyo kwa kutumia fedha za wale wasiojua kufanya biashara wakaamua kuwekeza.

Naye Afisa Usimamizi wa Fedha Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha Wizara ya Fedha, Bw. Stanley Kibakaya, alisema kuwa kutokana na umuhimu wa elimu ya fedha katika kuwakomboa wananchi katika umaskini, Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi mahiri wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Raisbwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imeamua kuweka mkazo wa kutoa elimu ya fedha kwa wananchi ili waweze kunufaika.

Bw. Kibakaya alisema kuwa mpaka sasa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametoa maelekezo kwa Wizara ya Fedha kutumia watalaam wake wazunguke nchi nzima kutoa elimu kwa wajasiriamali, wakulima na watumishi wa umma kuwajengea uwezo wa mambo muhimu ya kuzingatiwa kwenye elimu ya fedha ikiwemo umuhimu wa uwekezaji na namna ya kulinda mitaji

“Ndio wakati muafaka sasa ambapo Serikali yetu imeona kupitia huu mtaala mpya wa elimu ya fedha ifundishwe kuanzia shule za msingi hadi vyuo vikuu na Wizara imepokea maelekezo kupitia Mhe.Rais kuhakikisha tunapita katika mikoa yote kuwapatia elimu wananchi wote ambao hawakufanikiwa kuipata katika mfumo rasmi”

Bw. Kibayakaya amebainisha kuwa katika kutekeleza agizo la Rais tayari awamu ya kwanza imekwishafanyika na sasa ni awamu ya pili imeanzia mkoani Kigoma ambapo jumla ya Halmashauri nne zitafikiwa na mpango huo.

Timu ya Wataalam wa Wizara ya Fedha imeanza ziara ya kutoa mafunzo kwa wananchi kwa makundirika mbalimbali Mkoani Kigoma ili kuwajengea uwezo na kutambua fulsa za kuwekeza, kujiongezea kipato, kufanya uwekezaji na kujiwekea akiba.




Share:

JINSI YA KUJISAJILI 888bet TANZANIA

 

Kujisajili 888bet Tanzania 

Historia ya 888bet 

888bet Tanzania ni kampuni ya kuweka madau mtandaoni iliyoanza kufanya kazi Tanzania tangu mwaka 2022. Ukitoa huduma Bora kwa wateja wake. 888 bet inafanya kazi pia katika nchi mbalimbali Africa na duniani kwa jumla. 888bet imesajiliwa kwa mujibu wa Sheria za michezo ya bahati nasibu Tanzania 

Kwa taarifa zifuatazo "Tovuti hii inaendeshshwa na Port Achia Tanzania Limited kwa kibali kutoka Gaming Board of Tanzania (GBT) namba SB1000000046"


Yaliyomo 


1. Jinsi ya kufungua account ya 888bet tz

2. Ku download 888bet apk Tanzania

3. Jinsi ya kuweka pesa 888bet Tanzania 

4. Faida za kubeti na 888bet 

JINSI YA KUFUNGUA ACCOUNT YA 888BET TANZANIA


Zifuatazo Ni Hatua za kufungua account yako ya 888bet Tanzania

1. Hatua ya kwanza Bofya link ya 888bet >HAPA> 👇👇https://media.888africa.com/C.ashx?btag=a_28b_2c_&affid=27&siteid=28&adid=2&c=

2. Jaza namba yako ya simu na password 

3. Bofya jisajili

Hapo tayari utakuwa umeshafungua account yako ya 888bet Tanzania. Unatakiwa kudeposit kwenye Account yako ya 888bet na kuanza kufurahia huduma za kampuni Bora zaidi ya kubeti mtandaoni nchini Tanzania 888bet tz


JINSI YA KUPAKUA 888BET TZ APK 

kupakua app ya 888 bet Tanzania inapaswa kufuata Hatua zifuatazo 

Jisajili na pakua 888bet app hapa 👇https://media.888africa.com/C.ashx?btag=a_28b_2c_&affid=27&siteid=28&adid=2&c=


Kwanza unatakiwa ujisajili ndipo upakue APK ya 888bet 

Pili hakikisha umeseti katika simu yako kupokea app ambazo zipo nje ya playstore (allow from unknown source)


Tatu Sasa unaweza kudakinisha program ya 888bet na kufurahia kubashiri mtandaoni nchini Tanzania 

Tembelea kiungo hiki kuweza kupakua 888bet APK


JINSI YA KUWEKA PESA 888BET TANZANIA

Unaweza kuweka pesa (kudeposit) katika account yako ya 888bet Tanzania kwa njia mbalimbali. Ikiwemo njia ya kudeposit kwa ussd ambapo Playbill ya 888bet Ni 880888 (namba ya kampuni)

Vile vile unaweza kudeposit kwa njia ya moja kwa moja ambapo utatakiwa kuingia katika account yako na kubofya sehemu ulivyoandikwa deposit, Bofya hapo Jaza kiasi , chagua mtandao kulingana na namba uliyotumia kujisajili Kisha endelea , utapokea pop sms kwenye simu yako ikikutaka kuingiza password ili kulamilisha muamala


NB : Njia zote za kudeposit 888bet Ni njia za haraka na pesa itaingia kwenye account yako kwa haraka


JINSI YA KUTOA PESA 888BET TANZANIA

Ikiwa unataka kutoa pesa katika account yako ya 888bet Tanzania unatakiwa kuingia sehemu ulivyoandikwa (with draw) au TOA pesa Kisha fuata maelekezo pesa itaingia katika account yako ya simu kwa haraka.


FAIDA ZA KUBETI NA KAMPUNI YA 888 BET TANZANIA

Zipo faida mbalimbali ambazo huwezi kuzipata Kama ukibeti na kampuni nyingine. Zifuatazo nifaida mbalimbali zilizopo 888bet Tanzania


Malipo ya haraka

Jackpot ya bure yakushinda Hadi milioni 500 bure

Zaidi ya michezo 2000 ya kasino za mtandaoni Tanzania ambapo unaweza Kushinda mkwanja

Mchezo wa Aviator

Huduma nzuri kwa wateja


Hitimisho 

Ikiwa utaka kuwasiliana na 888bet Tanzania unaweza kufanya hivyo kwa njia ya moja kwa moja live chat katika tovuti au app ya 888bet. Vilevile unaweza kuwasiliana na 888bet Tanzania kupitia barua pepe support@888bet.tz

Soma zaidi www.kampunizakubeti.com

Share:

UHAKIKI WA NHIF YABAINI WANACHAMA ZAIDI YA 13O SIO HALALI KWENYE VITUO VYA KUTOLEA HUDUMA TANGA

Na Oscar Assenga, TANGA


MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoa wa Tanga katika zoezi la uhakiki wa wanachama kwenye vituo vya kutolea huduma umebaini uwepo wa wanachama zaidi ya 130 ambao sio halali

Hayo yalibainishwa na Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mkoa wa Tanga Evans Nyangasa wakati akizungumza na waandishi wa habari katika maonyesho ya biashara na utalii yanayoendelea kwenye viwanja vya shule ya Sekondari Usagara Jijini humo

Alisema uhakiki huo ulifanyika kati ya mwezi June 2023 mpaka sasa na katika udanganyifu huo kuna baadhi ya waliotumia huduma hizo wameweza kuzilipia gharama ambazo walitumia ndivyo sivyo huku wakitoa wito kwa watoa huduma kutoa kwa mwanachama sahihi na kwa wakati sahihi na huduma halali.

“Kwa kwa wakati sahihji mna huduma halali na wamejipanga kutoa huduma kwa wananchi kwenye nyumba za ibada,mashule na vijiji ili waweze kujiunga na bima ya afya lengo lao ni kuhakikisha kila mwananchi anajiunga na mfuko huo"Alisema 

Alisema lengo lao ni kuhakikisha wanaendelea kutoa elimu juu ya matumizi mazuri ya kadi ya bima ya afya kutokana na kwamba siku za karibuni kumeibuka miongoni mwa wanachama wanashiriki udanganyifu kutumia kadi zao ndio sivyo jambo ambalo linapelekea mfuko kutumia gharama nyingi.

“Tunaendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhakikisha wanatumia kazi zao vizuri wanapokwenda kwenye vituo vya kutolea huduma ndio maana Tanga tumejipanga kuendelea kuweka watalaamu kwenye vituo vya kutolea huduma kwa lengo la kudhibiti udanganyifu ambao unaweza kutokea wakati wa utoaji wa huduma na nisisitize wananchi waendelea kuzingatia miongoozo na taratibu za huduma”Alisema

Hata hivyo alisema wameamua kushiriki kwenye maonyesho hayo kwa lengo la kutoa elimu kwa watanzania juu ya huduma zinazotolewa ikiwemo umuhimu wa kuwa na bima ya afya kwa wananchi kutokana na kwamba inawapa uhakika wa kugharamia gharamaza za matibabu bila kulipia gharama za ziada.

“Pamoja na kutoa elimu lakini pia tunapokea malalamiko na maoni kutoka kwa wanachama wetu juu ya huduma zinazotolewa na mfuko na kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu na kuwa na huduma bora kwa wanachama wa pale wanaponufaika na huduma hizo”Alisema

Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Evans Nyangasa akizungumza Mkurugenzi wa Bodi ya Mkonge Tanzania Saady Kambona na Meneja wa Tarura Mkoa wa Tanga kulia wakati walipotembelea banda lao katika viwanja vya Usagara Jijini Tanga kunakoendelea maonyesho ya Biashara na Utalii 
Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Evans Nyangasa akizungumza Mkurugenzi wa Bodi ya Mkonge Tanzania Saady Kambona na Meneja wa Tarura Mkoa wa Tanga kulia wakati walipotembelea banda lao katika viwanja vya Usagara Jijini Tanga kunakoendelea maonyesho ya Biashara na Utalii 
Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Tanga Shymaa Kwegyir kulia akipatiwa huduma kwenye Banda la NHIF 
MKUU wa Mkoa wa Tanga Balozi Batilda Burian kulia akisalimiana na Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Evans Nyangasa wakati alipokwenda kufungua maonyesho ya biashara na utalii yanayoendelea kwenye viwanja vya Usagara Jijini Tanga
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE JUNI 4,2024

 Magazeti ya leo











Share:

Sunday, 2 June 2024

Video Mpya : NG'WANA SALA - NENGILEKO

Share:

A4K APARTMENTS AND LODGE - KIKUYU, CHIDACHI - DODOMA



A4K APARTMENTS AND LODGE - KIKUYU, CHIDACHI - DODOMA 

Our prices are;
1. Tsh. 35,000, 45,000 or $ 50
2. Tsh 110,000 or 60$, this is an apartment with two master bedrooms.

3.50,000 and 60,000 rooms

All our rooms are Master bedroom fitted with clean mosquito net, Televitions, Furnished sitting room, Functional kitchen,  warm water in the bathrooms and Air condition.

Complimentary
Washing facility - fixed with washing machine, -Ironing facility, 
-Fee Wifi, 
-Parking space, 
-Ectric security fance; and CCTV Camera.

Book Now:
Mobile: +255 755 989 556      +255 746 573 787

Follow us:
Instagram: a4k_aperttment and lodge

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger