Tuesday, 4 June 2024

UHAKIKI WA NHIF YABAINI WANACHAMA ZAIDI YA 13O SIO HALALI KWENYE VITUO VYA KUTOLEA HUDUMA TANGA

Na Oscar Assenga, TANGA


MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoa wa Tanga katika zoezi la uhakiki wa wanachama kwenye vituo vya kutolea huduma umebaini uwepo wa wanachama zaidi ya 130 ambao sio halali

Hayo yalibainishwa na Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mkoa wa Tanga Evans Nyangasa wakati akizungumza na waandishi wa habari katika maonyesho ya biashara na utalii yanayoendelea kwenye viwanja vya shule ya Sekondari Usagara Jijini humo

Alisema uhakiki huo ulifanyika kati ya mwezi June 2023 mpaka sasa na katika udanganyifu huo kuna baadhi ya waliotumia huduma hizo wameweza kuzilipia gharama ambazo walitumia ndivyo sivyo huku wakitoa wito kwa watoa huduma kutoa kwa mwanachama sahihi na kwa wakati sahihi na huduma halali.

“Kwa kwa wakati sahihji mna huduma halali na wamejipanga kutoa huduma kwa wananchi kwenye nyumba za ibada,mashule na vijiji ili waweze kujiunga na bima ya afya lengo lao ni kuhakikisha kila mwananchi anajiunga na mfuko huo"Alisema 

Alisema lengo lao ni kuhakikisha wanaendelea kutoa elimu juu ya matumizi mazuri ya kadi ya bima ya afya kutokana na kwamba siku za karibuni kumeibuka miongoni mwa wanachama wanashiriki udanganyifu kutumia kadi zao ndio sivyo jambo ambalo linapelekea mfuko kutumia gharama nyingi.

“Tunaendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhakikisha wanatumia kazi zao vizuri wanapokwenda kwenye vituo vya kutolea huduma ndio maana Tanga tumejipanga kuendelea kuweka watalaamu kwenye vituo vya kutolea huduma kwa lengo la kudhibiti udanganyifu ambao unaweza kutokea wakati wa utoaji wa huduma na nisisitize wananchi waendelea kuzingatia miongoozo na taratibu za huduma”Alisema

Hata hivyo alisema wameamua kushiriki kwenye maonyesho hayo kwa lengo la kutoa elimu kwa watanzania juu ya huduma zinazotolewa ikiwemo umuhimu wa kuwa na bima ya afya kwa wananchi kutokana na kwamba inawapa uhakika wa kugharamia gharamaza za matibabu bila kulipia gharama za ziada.

“Pamoja na kutoa elimu lakini pia tunapokea malalamiko na maoni kutoka kwa wanachama wetu juu ya huduma zinazotolewa na mfuko na kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu na kuwa na huduma bora kwa wanachama wa pale wanaponufaika na huduma hizo”Alisema

Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Evans Nyangasa akizungumza Mkurugenzi wa Bodi ya Mkonge Tanzania Saady Kambona na Meneja wa Tarura Mkoa wa Tanga kulia wakati walipotembelea banda lao katika viwanja vya Usagara Jijini Tanga kunakoendelea maonyesho ya Biashara na Utalii 
Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Evans Nyangasa akizungumza Mkurugenzi wa Bodi ya Mkonge Tanzania Saady Kambona na Meneja wa Tarura Mkoa wa Tanga kulia wakati walipotembelea banda lao katika viwanja vya Usagara Jijini Tanga kunakoendelea maonyesho ya Biashara na Utalii 
Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Tanga Shymaa Kwegyir kulia akipatiwa huduma kwenye Banda la NHIF 
MKUU wa Mkoa wa Tanga Balozi Batilda Burian kulia akisalimiana na Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Evans Nyangasa wakati alipokwenda kufungua maonyesho ya biashara na utalii yanayoendelea kwenye viwanja vya Usagara Jijini Tanga
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE JUNI 4,2024

 Magazeti ya leo











Share:

Sunday, 2 June 2024

Video Mpya : NG'WANA SALA - NENGILEKO

Share:

A4K APARTMENTS AND LODGE - KIKUYU, CHIDACHI - DODOMA



A4K APARTMENTS AND LODGE - KIKUYU, CHIDACHI - DODOMA 

Our prices are;
1. Tsh. 35,000, 45,000 or $ 50
2. Tsh 110,000 or 60$, this is an apartment with two master bedrooms.

3.50,000 and 60,000 rooms

All our rooms are Master bedroom fitted with clean mosquito net, Televitions, Furnished sitting room, Functional kitchen,  warm water in the bathrooms and Air condition.

Complimentary
Washing facility - fixed with washing machine, -Ironing facility, 
-Fee Wifi, 
-Parking space, 
-Ectric security fance; and CCTV Camera.

Book Now:
Mobile: +255 755 989 556      +255 746 573 787

Follow us:
Instagram: a4k_aperttment and lodge

Share:

DC MTATIRO AZINDUA HOTELI MPYA IJULIKANAYO KAMA AZAT HOTEL - TINDE

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro amezindua hotel iliyopo kata ya Tinde wilayani Shinyanga ijulikanayo kama AZAT HOTEL.

Hafla hiyo ya uzinduzi imefanyika leo Juni 1, 2024 katika viwanja vya hoteli ya AZAT HOTEL vilivyopo jirani na kituo cha mzani wa Tinde wilayani Shinyanga.

Awali akizungumza wakati wa hafla hiyo ya uzinduzi mmiliki wa AZAT HOTEL Mhe. Azza Hilal Hamad amebainisha huduma zitakazotolewa hotelini hapo baada ya kuzinduliwa siku ya leo.


"AZAT HOTEL ni sehemu sahihi kwa ajili ya kupumzika kwa wageni na hata wenyeji, huduma zitakazotolewa hapa AZAT HOTEL ni pamoja na malazi na chakula kwa gharama nafuu kabisa, vyumba vyetu ni bora, rafiki na vyenye viwango bora, lakini pia mbali na kutoa huduma hii ya hoteli tunajihusisha na ukodishaji wa Tents kwa ajili ya shughuli mbalimbali, karibuni sana ukifika hapa Tinde hoteli ni moja tu AZAT HOTEL kwa mawasiliano zaidi unaweza kutupigia kupitia simu namba 0742 565 555", amesema Mhe. Azza Hilal Hamad.


Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude ambaye alikuwa mgeni mualikwa katika hafla hiyo amempongeza Mhe. Azza Hilal Hamad kwa kutoa ajira kwa vijana kupitia ujenzi wa hoteli hiyo na kuwasihi vijana kufanya kazi kwa bidii pindi wapatapo nafasi na kutoa wito kwa jamii kushirikiana vyema na wawekezaji ili kuwatia moyo waendelee kuwekeza kwenye maeneo yao.


"Sisi tunakupongeza sana wewe na familia yako kwa jitihada hizi, hatuna budi kushirikiana na wawekezaji kama hawa ili kuwatia moyo waendelee kuwekeza kwenye maeneo yetu, na kutoa nafasi kwa vijana wetu ili waweze kujikwamua kiuchumi", amesema DC Mkude.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro amepongeza uwekezaji uliofanywa na Azza Hilal Hamad kwa kuthamini wageni na kuongeza pato, uchumi na maendeleo kwenye halmashauri hiyo, na kuahidi kuendelea kushirikiana vyema na wawekezaji.


"Hongera sana dada yetu Azza Hilal Hamad kwa uwekezaji uliyoufanya kwenye kata hii ya Tinde ukizingatia ni miongoni mwa maeneo yanayopokea wageni wengi kutoka sehemu mbalimbali, niseme tu ni hatua kubwa kwako kama mwanamke, kama serikali tunaendelea kuunga mkono jitihada zinazofanywa na wawekezaji hususani sekta binafsi, niwahakikishie wakazi wa maeneo haya kuwa ile changamoto ya bei kubwa ya maji ukilinganisha na maeneo mengine sasa imekwisha, nimeshaongea na viongozi husika kwenye sekta ya maji na kwanzia sasa bei itakuwa sawa na maeneo mengine" , amesema Wakili Julius Mtatiro. 

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro akizungumza wakati wa hafla hiyo.

Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude akizungumza wakati wa hafla hiyo.
<<<TAZAMA PICHA MUONEKANO WA AZAT HOTEL>>>

Muonekano wa ndani hoteli ya AZAT HOTEL.










Muonekano wa nje hoteli ya AZAT HOTEL.



Baadhi ya watu walio udhuria kwenye hafla hiyo ya uzinduzi wa hotel ya AZAT HOTEL.












Zoezi la kukata utepe kuashilia uzinduzi kwenye hoteli ya AZAT HOTEL.

Mhe. Azza Hamad akiwaonesha wageni muonekano na huduma za hoteli hiyo. 
Share:

Saturday, 1 June 2024

UDSM YAWAALIKA WADAU KATIKA MAONESHO YA WIKI YA UTAFITI NA UBUNIFU MSIMU WA 9 YATAKAYOFANYIKA JUNI 5-7, 2024


Chuo Kikuu cha Dar es Salaam- UDSM kinakualika katika maonesho ya wiki ya Utafiti na Ubunifu msimu wa 9 - 2024 yatakayofanyika 5 -7, June 2024 katika ukumbi wa Maktaba Mpya. 

 Akizungumza katika Ukaribisho huo, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo - Utafiti, Profesa Nelson Boniface amesema mwaka huu wamejipanga vyema hivyo washiriki wajitokeze kwa wingi.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger