Saturday, 9 March 2024

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI MACHI 10, 2024


Share:

GRUMETI FUND YAZINDUA MRADI WA NG'OMBE WA MAZIWA SERENGETI , BUNDA WA MIL. 52

Shirika la Grumeti Fund limetoa ng'ombe wa maziwa 15 wenye thamani ya Mil. 52 kwa vijiji vya Motukeri na Nyichoka wilayani Serengeti na vijiji vya Mugeta na Tingirima wilayani Bunda,ikiwa ni awamu ya kwanza ya mradi huo unaolenga kuhamasisha ufugaji wenye tija na unao tunza mazingira.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo, Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii kutoka Grumeti Fund Bi. Frida Mollel amesema lengo la mradi huo ni kuondoa changamoto za kimazingira na mabadiliko ya tabia ya tabia nchi sambamba na kuhamasisha ufugaji wenye faida na kuongeza kipato na lishe Bora katika kaya.

"Mradi huu uliobuniwa na Grumeti Fund unalenga kupunguza changamoto za kimazingira kwakuwa na ufugaji wenye tija kwa kutumia nafasi ndogo lakini matunda yake ni makubwa na wanufaika wa mradi huu wapo 15 ambao 8 ni kutoka vijiji vya Serengeti na wananchi 7 wakitoka katika vijiji vya Wilaya ya Bunda" alisema Bi. Frida

Aidha Bi. Frida amesisitiza utunzaji wa ng'ombe hao sambamba na kuzingatia taratibu za mradi ili kuufanya kuwa endelevu na wenye manufaa kwa wananchi wengi. 

Vilevile, ameongeza kuwa Ng'ombe wote 15 wanamimba na wamepatiwa chanjo muhimu, ambapo pia Grumeti Fund imetoa mbegu za majani ya malisho kwa wanufaika wote ili kuhakikisha upatikanaji wa malisho kwa mwaka mzima.

Mgeni Rasmi katika uzinduzi huo Mkuu wa Wilaya ya Serengeti Dkt. Vincent Mashinji  amewataka wananchi kuzingatia taratibu zote za mradi na kuwataka kuutumia mradi huo kama darasa la mabadiliko kuachana na ufugaji holela na kuingia katika  ufugaji wa kisasa.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Bunda Dkt. Vicent Anney amewataka wanufaika wa mradi huo kuutumia vizuri ili kujikwamua katika umasikini kwa kupitia mazao yatakoyopatikana katika ng'ombe hao huku akiwataka wanufaika wa mwanzo kuwa chachu ya ushawishi kwa taasisi ya Grumeti  Fund kuleta Mradi wa awamu ya pili.

Sambamba na hayo, baadhi ya wanufaika wa mradi huo wameeleza shukrani zao kwa Kampuni ya Grumeti Fund huku wakiutaja Mradi huo kama chanzo cha kukata mnyororo wa umasikini katika familia zao na kuahidi kuwatunza ng'ombe hao ili kuongeza idadi ya wanufaika.

Grumeti Fund katika awamu ya kwanza ya Mradi imetoa ng'ombe kwa Wananchi  15 huku katika awamu ya pili wakitarajia kutoa ng'ombe 15, awamu ambayo itategemea mafanikio yatakayopatikana katika awamu ya Kwanza.


Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI MACHI 9, 2024


Share:

Tazama Video : SHANGWE WANAWAKE MAADHIMISHO SIKU YA WANAWAKE SHINYANGA

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme amewaongoza wanawake katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Mkoa wa Shinyanga.. Tazama Video hapa wakiimba na kucheza 

@malundeblog

Shangwe Maadhimisho Siku ya Wanawake Duniani Mkoa wa Shinyanga.... Wanawake wakicheza live

♬ original sound - Malunde
@malundeblog

Shangwe Maadhimisho Siku ya Wanawake Duniani Mkoa wa Shinyanga.... Wanawake wakicheza live

♬ original sound - Malunde
@malundeblog

Vibe la askari Polisi Wanawake Shinyanga siku ya wanawake duniani

♬ original sound - Malunde
@malundeblog

RPC Shinyanga akicheza na askari polisi

♬ original sound - Malunde
Share:

WANAWAKE EWURA WATOA HUNDI YA MIL.5/- KWA SHULE YA BUIGIRI


 
MWENYEKITI wa Wanawake wa Chama Cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania (TUGHE) Tawi la EWURA,Bi. Herieth Kasilima (kushoto),akiwaongoza baadhi ya Wafanyakazi Wanawake wa EWURA wakikabidhi hundi ya sh.Milioni tano katika Shule ya Msingi ya Wanafunzi wenye mahitaji maalum ya Buigiri Wilayani Chamwino wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika leo Machi 8,2024 Kitaifa kwenye viwanja vya Chinangali II, Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma.

MWENYEKITI wa Wanawake wa Chama Cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania (TUGHE) Tawi la EWURA,Bi. Herieth Kasilima pamoja na Wafanyakazi Wanawake wa EWURA wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhi hundi ya sh.Milioni tano katika Shule ya Msingi ya Wanafunzi wenye mahitaji maalum ya Buigiri Wilayani Chamwino wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika leo Machi 8,2024 Kitaifa kwenye viwanja vya Chinangali II, Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma.
MWENYEKITI wa Wanawake wa Chama Cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania (TUGHE) Tawi la EWURA,Bi. Herieth Kasilima akiwaongoza baadhi ya Wafanyakazi Wanawake wa EWURA waliojitokeza katika maandamano kusherehekea kilele cha Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika Kitaifa kwenye viwanja vya Chinangali II, Wilaya ya Chamwino, mkoani Dodoma leo Machi 8,2024.

Baadhi ya Wafanyakazi wanawake wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) wakishangilia katikati ya viwanja vya Chinangali II jijini Dodoma eneo ambalo maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yanafanyika Kitaifa.


Baadhi ya Wafanyakazi wanawake wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), wakimsikiliza Mgeni Rasmi, Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima (hayupo pichani) katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, yaliyofanyika Kitaifa katika viwanja vya Chinangali II wilayani Chamwino mkoani Dodoma


MWENYEKITI wa Wanawake wa Chama Cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania (TUGHE) Tawi la EWURA,Bi. Herieth Kasilima,akizungumza na Waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kushiriki Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika leo Machi 8,2024 Kitaifa kwenye viwanja vya Chinangali II, Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma.

Na Alex Sonna-CHAMWINO

WAFANYAKAZI Wanawake wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) wametembelea Shule ya Msingi ya wanafunzi wenye mahitaji maalum ya Buigiri wilayani Chamwino na kutoa hundi ya Sh.Milioni tano ili kusaidia kununua vitu mbalimbali ikiwamo karatasi za nukta nundu.

Akizungumza leo baada ya kutembelea shule hiyo, Mwenyekiti wa wanawake wa Chama Cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania (TUGHE) Tawi la EWURA, Herieth Kasilima, amesema fedha hiyo pia itanunua chakula.

Herieth amehimiza taasisi zingine kuwasaidia wanafunzi wa shule hiyo kutokana na kuwa na mahitaji mengi ili watoto hao wafikie ndoto zao kielimu.

Pamoja na kutoa msaada huo, wanawake hao wameungana na wengine katika kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani yaliyofanyika kimkoa mkoani Dodoma katika Wilaya ya Chamwino.

Katika hotuba ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa iliyosomwa kwa niaba na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt.Dorothy Gwajima, amesisita matumizi ya Nishati safi na salama ya kupikia ambapo EWURA wanajukumu la kudhibiti huduma ya nishati ya gesi.
Share:

Friday, 8 March 2024

GGML YATAJA SIRI KUONGEZA IDADI YA WANAWAKE KWENYE MADINI


Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa (wa pili kushoto) akimpatia tuzo Mjiolojia kutoka GGML, Janeth Luponelo kutokana na mchango wa kampuni hiyo katika masuala ya jinsia. Kushoto ni Waziri wa Madini, Anthony Mavunde na kutoka kulia ni Makamu Rais wa AngloGold Ashanti – GGML anayeshughulikia miradi endelevu na masuala ya ushirika Afrika, Simon Shayo, Mkuu wa Kagera, Fatma Mwassa na Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Adam Malima.


NA MWANDISHI WETU

KAMPUNI ya Geita Gold Mining Limited (GGML) imesema mojawapo ya siri iliyouwezesha mgodi huo kuongoza nchini kwa kuongeza idadi kubwa ya wanawake walioajiriwa kwenye sekta hiyo ya madini, ni kubuni na kutekeleza kwa vitendo sera na miongozo inayohamasisha usawa wa kijinsia maeneo ya kazi.


Hayo yamebinishwa mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam na Makamu Rais wa AngloGold Ashanti – GGML anayeshughulikia miradi endelevu na masuala ya ushirika Afrika, Simon Shayo katika sherehe za awali za kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani.

Shayo alisema hivi sasa asilimia 13 ya nguvukazi ya kampuni hiyo ni wanawake ilihali kwa upande wa kimataifa ushiriki wa wanawake katika sekta ya madini takwimu zinaonesha ni kati ya asilimia 14 na 16.

“Kwa hivyo hatufanyi vibaya. Tuliendesha mgodi bila uwepo wa wanawake katika nafasi za juu za uongozi lakini sasa wapo na wengine wamevuka mipaka na kwenda kuwa wasimamizi wa sekta hiyo katika kampuni mbalimbali nje ya nchi,” alisema.

Alisema sera na miongozo ya GGML iliyowekwa sio kwamba imeongeza idadi ya wanawake kushiriki kwenye shughuli za mgodi huo, bali pia hata kubadilisha hulka za wanaume waliopo kwenye kampuni hiyo na kuona umuhimu wa wanawake kuwepo kwenye sekta ya madini.

Shayo alitaja baadhi ya miongozo hiyo kuwa ni pamoja na kuweka utaratibu wa kuajiri ambao unatoa kipaumbele kwa wanawake.


“Katika ajira asilimia 50 ni wanawake na asilimia inayobaki 50 ni wanaume na kama watalingana ufaulu katika usaili anayepewa kipaumbele ni mwanamke,” alisema.

Alisema pia kampuni hiyo hutoa ufadhili kwa wafanyakazi wake wanawake kwenda kupata mafunzo ya juu ya uongozi yanayotolewa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) ambapo tangu mafunzo hayo yaliyopewa jina la Female Future Program (FFT), yaanze mwaka 2016, wanawake 23 kutoka GGML wamefadhiliwa na kuhitimu mafunzo hayo.

“Pia ndani ya mgodi tuna muongoo unaoitwa ‘don’t cross the line’, kwamba usivuke mpaka au mstari kwenda kumghasi, kumtendea ukatili wowote mwanamke na kama kukitokea jambo lolote kuna namba za simu za kutoa taarifa kwa njia ya siri na hatua kuchukuliwa,” alisema.

Akizungumza kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassan kwenye hafla hiyo, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa alisema kampuni za madini zinatakiwa kuzingatia kanuni ya ‘Local Content’ iliyopo kwenye mabadiliko ya sheria ya madini kwa kuzingatia ushirikishwaji wa wanawake kwenye masuala ya ununuzi.

Alisema kipengele hicho cha ushirikisha wazawa katika mnyororo wa thamani, pia ni fursa nzuri kwa kampuni za madini kushirikisha wanawake katika manunuzi mbalimbali ambayo yanatengewa bajeti kubwa kuliko hata kodi zinazolipwa kwa serikali.

"Wanawake wanaojishughulisha kwenye shughuli za sekta ya madini wamekuwa na mchango mkubwa katika kujenga uchumi wao na pato la Taifa," alisema Slaa.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger