Sunday, 25 February 2024
AJALI YA MAGARI MANNE YAUA WATU 15 ARUSHA
Watu kumi na tano wamefariki dunia katika ajali iliyohusisha lori na magari mengine madogo matatu katika eneo la by Pass Ngaramtoni wilaya Arumeru Mkoa wa Arusha.
Akitoa taarifa hiyo katika eneo la ajali Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha kamshna msaidizi mwandamizi wa Polisi SACP Justine Masejo amesema ajali hiyo imetokea Februari 24,2024 muda wa saa 11 jioni ambapo illmehusisha lori na magari madogo matatu katika eneo la Ngaramtoni Wilaya ya Arumeru Mkoa wa Arusha.
Kamanda Masejo amesema wanaendelea na uchunguzi wakina ajali hiyo ili kubaini chanzo halisi cha ajali hiyo.
Aidha amewaomba wananchi kufika katika hosptali ya rufaa ya mount Meru kutambua miili ya waliofariki katika ajali hiyo.
Saturday, 24 February 2024
DKT. NCHIMBI KUSHIRIKI MAZISHI YA ALIYEKUWA MWENYEKITI WA CCM MKOA WA TABORA
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi baada ya kutua Uwanja wa Ndege wa Tabora mapema leo Jumamosi Februari 24, 2024 asubuhi, akiwasili mkoani humo kushiriki mazishi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Tabora na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Mzee Hassan Mohammed Wakasuvi, yanayotarajiwa kufanyika leo katika Kijiji cha Mabama, Wilaya ya Uyui, ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM, atawakilishwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa.
WAZIRI MAVUNDE ASHUHUDIA URUSHWAJI NDEGE NYUKI ANGANI
*Kusini kuchele, Utafiti wa Miamba na Madini wahamia Mtwara
*GST kufanya tafiti madini mkakati Mtwara
Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde ameshuhudia jaribio la urushwaji wa Ndege Nyuki (Drone) angani kwa ajili ya utafiti wa miamba na madini hususan madini ya Kinywe, Nikeli, chuma na titanium katika Kijiji cha Utimbe kata ya Lupaso wilayani ya Masasi mkoa wa Mtwara.
Waziri Mavunde ameshudia jaribio hilo leo Februari 23, 2024 baada ya kutembelea eneo linalofanyika utafiti huo kwa lengo la kukagua shughuli za utafiti zinazo endelea katika maeneo mbalimbali nchini ikiwa ni utekelezaji wa Vision 2030 "Madini ni Maisha na Utajiri".
Akizunguza katika eneo la utafiti, Waziri Mavunde amesema mpaka sasa Tanzania ina taarifa za kina za tafiti wa miamba na madini kwa asilimia 16 ambazo zimepelekea uwepo wa migodi mikubwa, ya kati na midogo hivyo amesisitiza kwamba nchi hiyo ikifanyiwa utafiti wa kina wa High Resolution Airborne Geophysical Survey wa angalau asilimia 50 ifikapo 2030 itasaidia ongezeko kubwa la uwekezaji katika Sekta ya Madini.
Aidha, Waziri Mavunde amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayo ongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imedhamiria kwa dhati kuhakikisha inawasaidia wachimbaji wadogo wa madini kwa kuwapatia maeneo yenye taarifa za jiolojia ili wachimbe kwa faida na kuondokana na uchimbaji wa kubahatisha.
Awali, Waziri Mavunde alitembelea ofisi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara kwa lengo la kupata taarifa za shughuli za madini zinazoendelea mkoani humo.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Ahmed Abbas, ameipongeza Wizara ya Madini kwa kurusha Ndege Nyuki kwa ajili ya utafiti katika eneo lake na pia, amemuomba Waziri Mavunde kusaidia upatikanaji wa soko la madini ya Chumvi sambamba na kujengwa Kiwanda cha kuchakata madini hayo mkoani humo.
Naye, Mtendaji Mkuu wa GST Dkt. Mussa Budeba amemshukuru Waziri Mavunde kwa kukubari kushiriki na kushuhudia jaribio la urushwaji wa Ndege Nyuki kwa lengo la kutafiti miamba na madini kwa kutumia teknolojia ya high resolution airborne geophysical survey katika kijiji cha Utimbe wilayani Masasi mkoa wa Mtwara.
Sambamba na hayo, Dkt. Budeba amesema GST inashirikiana na Kampuni za Tukutech Company Ltd kutoka Tanzania, Zanifi Enterprise Ltd kutoka Zambia na Radai OY kutoka nchini Finland kufanya tafiti za miamba na madini katika maeneo mbalimbali nchini kwa kurusha Ndege Nyuki angani kwa kutumia teknolojia ya High Resolution Airborne Geophysical Survey.
Katika hatua nyingine, Dkt. Budeba amesema Ndege Nyuki inauwezo wa kufanya uchunguzi wa madini na miamba katika eneo kubwa kwa haraka ambapo hupelekea kupungua kwa muda na gharama zinazohitajika katika tafiti ikilinganishwa na njia nyingine za utafiti.
Mpaka sasa majaribio ya utafiti wa high resolution airborne geophysical survey unaoendelea kufanyika mkoani Mtwara tayari umefanyika katika mikoa ya Dodoma, Shinyanga, Geita, Manyara na Lindi kwa lengo la kutekeleza dhana ya Vision 2030.
*#Vision2030MadininiMaishanaUtajir#*
*#UtafitiTanzania#*
*#GeologicalSurveyofTanzania#*
Friday, 23 February 2024
WAZIRI KIJAJI AZITAKA TBS, BRELA NA WMA KUFANYA UKAGUZI KWENYE VIWANDA VYA MABATI NCHINI
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Dkt, Ashatu Kijaji (MB) amezitaka Taasisi zinazohusika na utoaji Leseni(BRELA) Shirika la Viwango Tansania (TBS) na wakala wa vipimo sahihi (WMA)kupita kwenye viwanda vyote nchini vinavyozalisha bidhaa za mabati na bidhaa nyingine kukagua na kujiridhisha kama bidhaa zinazozalishwa na viwanda nchini zinakidhi vigezo vilivyo vilivyoainishwa na kukubalika na Serikali.
Waziri Kijaji ameyasema hayo leo 22 Febriari ,2024 jijini Dodoma wakati alipofanya ziara katika Viwanda vya kuzalisha mabati vya ALAF na Herosean Interprises inayozalisha mabati ya DRAGON ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Rais Samia Suluhu Hassan kuhakikisha bidhaa zinazozalishwa na Viwanda hapa nchini zinanoreshwa.
Aidha Mhe. Waziri akiwa kwenye kiwanda cha Herosean Interprises kinachozalisha mabati ya DRAGON ameweza kubaini uwepo wa bidhaa nyingine ambazo haziusiani na malengo halisi ya leseni iliyotolewa na BRELA.
"Leo nimetembelea Viwanda hivi viwili lakini cha kusikitisha hiki Kiwanda cha kuzalisha mabati ya DRAGONI kinajihusisha na biashara ya kuuza bidhaa nyingine ikiwemo Friji, PVC, Vigae na Gypsum bord ,
"Nimewataka wanioneshe vielelezo vya usajili wa bidhaa hizo tofauti na bidhaa za mabati kiwandani hapa,sikupata majibu sahihi , naziagiza taasisi zinazohusika na hili suala zilishughurikie ili kupata ukweli wake. Amesema Kijaji
Vile vile Waziri Dkt.Kijaji ametoa wito kwa Viwanda vinavyozalisha bidhaa za mabati hapa nchini kuuzwa kwa bei rafiki ili kunufaisha wanunuaji kwa makundi yote.
" Jambo lingine ninalotaka kuwaambia watanzania kwa bidhaa nilizotembelea leo ,ukilinganisha kwa nchi za Afrika mashariki kwa bidhaa hii ya mabati sisi Tanzania bei yetu ipo chini kuliko nchi yoyote ile ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki hivyo niwatake msisikilize kelele za mtaani endeleeni kujenga kwa wingi na sisi kama Serikali tunaendelea kutekeleza miradi yetu"Ameongeza Dkt. Kijaji.
Kwa nyakati tofauti, wazalishaji wa viwanda hivyo Herry Jailos afsa huduma kwa wateja kiwanda cha mabati ya Alaf na Boniface Lekwasa Afsa Masoko Kiwanda cha kuzalisha mabati Dragon
wameishukuru Serikali kufanya ziara na kubaini changamoto zinazowakabili ikiwemo ukosefu wa masoko kutokana na wazalishaji wa bidhaa hizo kuwa wengi nchini.