Tuesday, 26 December 2023

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE DESEMBA 26, 2023

 

Magazeti ya Jumanne December 26 2023
 
 
Share:

Monday, 25 December 2023

ASKOFU SANGU : KANISA KATOLIKI HALIJAWAHI KUHALALISHA NDOA ZA JINSI MOJA... "NI DHAMBI KUBWA, KUWENI MAKINI NA VYOMBO VYA HABARI VINAVYOPOTOSHA"







Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu, amesema Kanisa halijawahi kufundisha au kuhalalisha muungano wa kindoa kati ya watu wa Jinsia moja.

Kupitia salamu zake za Krismasi na mwaka mpya wa 2024 alizozitoa kwa Wakristo na watu wote amebainisha kuwa, madai hayo yanatokana na upotoshwaji mkubwa wa makusudi kuhusu mafundisho ya Kanisa Katoliki, ambapo baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa na kasi kubwa ya kuandaa akaunti za uongo na kuweka taarifa zinazopotosha msimamo wa Kanisa, juu ya muungano hasi wa ndoa za jinsia moja.

Askofu Sangu amefafanua kuwa, msimamo na mafundisho ya Kanisa Katoliki mpaka sasa unabaki kuwa ndoa ni kati ya Mke na Mme na wala si vinginevyo, na linasisitiza kuwa hakuna ndoa inayohusisha watu wa jinsia moja kwa kuwa jambo hilo ni kinyume na mafundisho ya neno la Mungu, mila na desturi za Kiafrika, kinyume cha sheria za Tanzania na ni kinyume cha sheria ya asili ya maumbile (Natural law)

“Nyakati zetu hizi tunashuhudia upotoshwaji mkubwa na wa maksudi kuhusu mafundisho ya Kanisa Takatifu la Mungu. Tumeshuhudia baadhi ya vyombo vya Habari vimekuwa na kasi kubwa ya kuandaliwa kwa akaunti za uongo na kuweka taarifa potoshi, mintarafu msimamo wa Kanisa Katoliki juu ya muungano hasi wa jinsi moja.

Ukweli ni kwamba Kanisa Katoliki halijawahi, kamwe kufundisha au kuhalalisha muungano wa kindoa kati ya watu wa jinsi moja. Huu ni upotoshaji ulioghubikwa na hila za Ibilisi aliye mwovu.

Kanisa linasisitiza kwenye mafundisho yake kuwa ndoa ni kati ya Mke na Mme na si vinginevyo, na linasisitiza hakuna ndoa inayohusisha watu wa jinsi moja na kwamba ndoa za jinsia moja ni kinyume na mafundisho ya neno la Mungu, mila na desturi zetu za Kiafrika, kinyume cha sheria zetu za Tanzania na ni kinyume cha sheria ya maumbile (Natural law)

Askofu Sangu amesisitiza kwamba, Kanisa Katoliki linaamini kuwa ni dhambi kubwa kwa wanaoishi maisha ya jinsi hiyo, kwa wanaoshabikia na kwa wale wanaohamasisha kwa namna yoyote ile.

Askofu Sangu amewatahadharisha wakristo pamoja na jamii nzima kuwa makini na vyombo mbalimbali vya habari ambavyo vinajaribu kupotosha kwa lengo la kuwafanya Wakristo wayaache mafundisho sahihi ya Kimungu.

Wakati huohuo, Askofu Sangu amezishauri mamlaka za Serikali hapa nchini kutilia mkazo suala la uwepo wa vipindi vya dini kwa wanafunzi wawapo shuleni, ili wapate mafundisho sahihi juu ya Imani na kulifanya taifa kuwa na watu wenye hofu ya Mungu, hatua ambayo itasaidia kuwa na viongozi waadilifu, wazalendo na ambao hawatakuwa tayari kuuza utu na heshima ya wanaowaongoza kwa lengo la kujitafutia umahiri bandia na kujinufaisha binafsi kwa gharama za wengine.

Aidha amewaomba Watanzania wote kuendelea kuliombea taifa na hasa viongozi waendelee kuwa na hofu ya Mungu, ili Taifa lidumu na kustawi katika Haki, Amani, Upendo na Mshikamano wa kweli .

Leo, Wakristo kote duniani waadhimisha sikukuu ya Krismasi, ambayo ni kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mkombozi wao Yesu Kristo.

Chanzo - Radio Faraja Fm website
Share:

WABUNGE PATROBAS KATAMBI , SANTIEL KIRUMBA WASHEREHEKEA SIKUKUU YA KRISMASI NA WAFUNGWA SHINYANGA

 


Na Marco Maduhu,SHINYANGA

MBUNGE wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na watu wenye ulemavu, pamoja na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Santiel Kirumba, wametoa Ng’ombe wa Krismasi Magereza ya wilaya ya Shinyanga.

Ng’ombe huyo amekabidhiwa leo Decemba 24, 2023 na Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Samweli Jackson kwa niaba ya Wabunge hao, kwa Mkuu wa Magereza ya wilaya ya Shinyanga Theophil Mulokozi, pamoja na Shilingi Laki 2 iliyotolewa na Mbunge Katambi kwa ajili ya kununua Sabuni za kufulia.
Akizungumza wakati wa kukabidhi Ng’ombe na fedha Sh.Laki 2, Samwel amesema Mbunge Katambi na Santiel, waliahidi kutoa Ng’ombe kwenye Magereza ya wilaya ya Shinyanga, na leo wametekeleza ahadi yao ili askari Magereza pamoja na wafungwa washerehekee Siku Kuu ya Krismasi kwa furaha na upendo.

“Mbunge Katambi pamoja na Santiel waliahidi kutoa Ng’ombe wa Krismasi katika Magereza hii ya wilaya ya Shinyanga, na wametekeleza ahadi yao na thamani ya Ng’ombe huyu ni Sh, Laki 7, nimekabidhi pia na Sh.Laki 2 ambazo zimetolewa na Mheshimiwa Katambi kwa ajili ya kununua sabuni za kufulia ni moja pia ya ahadi yake kwa wafungwa,”amesema Samweli.
“Mheshimiwa Katambi na Santiel wanawatakia Askari Magereza na wafungwa wote, heri ya Sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya 2024,”ameongeza Samweli.

Naye Mkuu wa Magereza ya wilaya ya Shinyanga Theophil Mulokozi, amewashukuru Wabunge hao kwa zawadi hiyo waliowapatia ya Ng’ombe kwa ajili ya Siku Kuu ya Krismasi na kutekeleza ahadi yao, pamoja na fedha Sh.Laki 2 ya kununua Sabuni za kufulia nguo za wafungwa, na kutoa wito pia kwa viongozi wengine wawe wanawakumbuka na wafungwa katika Sherehe mbalimbali.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Samweli Jackson (kushoto) akikabidhi Ng'ombe wa Christimas katika Magereza ya wilaya ya Shinyanga aliyetolewa na Wabunge Katambi na Santiel Kirumba, (kulia)ni Mkuu wa Magereza hiyo Theophil Mulokozi.
Zoezi la kukabidhi Ng'ombe wa Christimas katika Magereza ya wilaya ya Shinyanga likiendelea.
Zoezi la kukabidhi Ng'ombe wa Christimas katika Magereza ya wilaya ya Shinyanga likiendelea.
Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Samwil Jacskon (kushoto)akibidhi Sh. Laki 2 kwa Mkuu wa Magereza wilaya ya Shinyanga Theophil Mulokozi pesa iliyotolewa na Mbunge Katambi kwa ajili ya kununua Sabuni za kufulia.
Picha ya pamoja ikipigwa.


Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU DESEMBA 25, 2023...HERI YA KRISMASI!!!


🌐 Mpendwa Msomaji wetu, Mtandao wa Malunde 1 blog unakutakia Krismasi njema na Kheri ya mwaka mpya wenye furaha na mafanikio

Magazeti ya leo
 
Share:

Sunday, 24 December 2023

JENGA NA MIMI INVESTMENT NDIYO MABINGWA WAUZAJI NA WASAMBAZAJI WA TOFALI IMARA ZENYE UBORA....USAFIRI BUREE



Je? unataka Tofali Imara na Bora? Je unataka kujenga nyumba imara? Karibu katika Kampuni ya Jenga na Mimi Investment ndiyo wakali hizi kazi mtu wangu!! Tunakufikia popote ulipo, Usafiri ni Bure 100%...Tupo Mwime - Mwendakulima Manispaa ya Kahama Mkoani Shinyanga... Tupigie 0763718607

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger