Thursday, 21 December 2023
Wednesday, 20 December 2023
WAREMBO WANASWA NA SIMU 61 WALIZOIBA MINADANI NA KWA WANAUME WALIOLALA NAO
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akionesha simu zilizoibiwa na wanawake kwenye minada na wanapolala na wanaume
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akionesha simu zilizoibiwa na wanawake kwenye minada na wanapolala na wanaume
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akionesha simu zilizoibiwa na wanawake kwenye minada na wanapolala na wanaume
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akionesha simu zilizoibiwa na wanawake kwenye minada na wanapolala na wanaume
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akionesha fedha za bandia zilizokamatwa
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akionesha vifaa vya kufanyia ramli chonganishi vilivyokamatwa
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akionesha mali zilizokamatwa
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akionesha mali zilizokamatwa
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga limefanikiwa kukamata simu 61 ambazo zimekamatwa kutoka kwa wanawake watatu (akina dada/mabinti) waliokuwa wanafanya shughuli za wizi kwenye maeneo ya minada na pale wanapolala na wanaume.
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo Jumanne Desemba 20,2023 Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi amesema simu hizo na watuhumiwa watatu wamekamatwa kufuatia doria na misako inayofanywa na jeshi la polisi kwa lengo la kuimarisha Usalama wa Raia na Mali zao hasa katika kipindi hiki cha kuelekea Sikukuu za Chrisms na Mwaka mpya ili kuhakikisha wananchi wa Mkoa wa Shinyanga wanasherekea Sikukuu hizo kwa amani na utulivu.
"Tunawashikilia wanawake watatu raia wa Burundi ambao wameingia nchini kwa njia haramu na wamekuwa wakifanya wizi, tumewakamata wakiwa na simu 61 walizoiba kwenye minada ya Kahama, Mwanza na Shinyanga. Lakini akina dada hawa pindi wanapolala na wanaume huwaibia na kuwatoroka wanaume hao",amesema Kamanda Magomi.
"Kufuatia Doria na misako hiyo iliyofanyika katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Shinyanga, Mwezi Novemba 30, 2023 hadi Disemba 19, 2023 Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga limefanikiwa kukamata Simu 61 ambazo zimekamatwa kutoka wa akina dada waliokuwa wanafanya shughuli za wizi, pombe ya moshi Lita 173, mafuta ya dizeli Lita 260, Pikipiki 07, TV 04, vyuma vya kuchimbia visima 09, Goroli za Karasha 106, Bangi misokoto 15, Subwoofer 02, Difu 01 ya Gari aina ya Toyota Hiace pamoja na noti bandia 09 zenye thamani ya Tshs.85,000/=",ameeleza Kamanda Magomi.
Amevitaja vitu vingine vilivyokamatwa ni pamoja na Pipe 11 za kunyonya mafuta, Baiskeli 01, vipande vya nondo 06, Keyboard 01, Chesess 01 ya Pikipiki, Spika 02, na vifaa mbalimbali vya kupigia ramli chonganishi ambavyo ni mikia 08 idhaniwayo kuwa niya mnyama aina ya Nyumbu, kipande 01 cha Ngozi ya mnyama kidhaniwayo kuwa cha mnyama aina ya Simba.
Katika upande wa mafanikio ya kesi Mahakamani, Kamanda Magomi amesema jumla ya kesi 08 zilipata mafanikio ambapo kesi 01 ya kubaka mshitakiwa alihukumiwa kifungo cha miaka 30 jela, kesi 02 za kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu washitakiwa walihukumiwa kwenda jela kati ya miezi 06 hadi miaka 03.
"Nyingine ni kesi 01 ya kuharibu mali mshitakiwa alihukumiwa kwenda jela miezi 05, kesi 02 za wizi wa pikipiki washitakiwa walihukumiwa kwenda jela kati ya miaka 02 hadi 03, kesi 01 ya kupatikana na mali idhaniwayo kuwa ya wizi mshitakiwa alihukumiwa kwenda jela mwaka 01, Kesi 01 ya wizi wa kuaminiwa washitakiwa 06 walihukumiwa kutotenda kosa lolote kwa mwaka 01. Kesi 01 ya kutishia kuua kwa Silaha panga mshitakiwa alihukumiwa kutotenda kosa lolote kwa mwaka 01",ameongeza.
Aidha katika kudhibiti ajali za Usalama Barabarani Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga limefanikiwa kukamata jumla ya makosa mbalimbali 2806, kati ya hayo makosa 05 yalikamatwa kwa kusababisha ajali, kuendesha mwendokasi na matumizi mabaya ya barabara na madereva kulipa faini.
"Pamoja na hatua mbalikmbali tunazoendelea kuzichukua katika kudhibiti ajali za barabarani pia Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Shinyanga kimefanikiwa kutoa elimu kwa makundi yote yanayotumia barabara kwa lengo la kupunguza ajali za barabarani na linawasisitiza madereva kufuata sheria wenyewe bila kusimamiwa na askari, dereva yeyote atakayevunja sheria atashughulikiwa kwa mujibu wa sheria",amesema.
Tuesday, 19 December 2023
MWENYEKITI WA BODI YA EWURA AKAGUA MIUNDOMBINU YA MAMLAKA YA MAJI TUKUYU
Mhandisi Barnabas Konga ( kushoto) kutoka Mamlaka ya Maji Mbeya, akimweleza Mwenyekiti wa Bodi ya EWURA, Prof Mark Mwandosya( aliyeketi kulia) kuhusu maendeleo ya mradi wa maji Mbaka, wakati kiongozi huyo alipotembelea chanzo cha maji cha Mto Mbaka, 18 Desemba 2023. Mamlaka ya Maji Mbeya, ndiye msimamizi wa mradi huo.
.............
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya EWURA, Prof Mark Mwandosya, amefanya ziara ya kikazi katika Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira ya Mji wa Tukuyu ( Tukuyu WSSA), Jumatatu, 18 Desemba 2023 kwa lengo la kukagua miundombinu ya maji na kufuatilia utekelezaji wa mradi mkubwa wa maji Mbaka, wenye thamani ya bilioni 4.5 uliopo Kitongoji cha Mbaka juu, Kijiji cha Isebe, Kata ya Itagata, Tukuyu, Rungwe.
Mradi huo, unatajiwa kuimarisha huduma ya maji kwa asilimia 95 na kuongeza upatikanaji wa maji katika mji wa Tukuyu, ambapo kwa sasa huduma inapatikana kwa saa 13 tu kwa siku.
EWURA husimamia utendaji wa mamlaka za maji nchini ili kuhakikisha huduma zake zinakidhi ubora, kanuni za afya, utunzaji wa mazingira na zinapatikana kwa uhakika na kwa gharama nafuu.
Mhandisi Barnabas Konga ( kushoto) kutoka Mamlaka ya Maji Mbeya, akimweleza Mwenyekiti wa Bodi ya EWURA, Prof Mark Mwandosya( aliyeketi kulia) kuhusu maendeleo ya mradi wa maji Mbaka, wakati kiongozi huyo alipotembelea chanzo cha maji cha Mto Mbaka, 18 Desemba 2023. Mamlaka ya Maji Mbeya, ndiye msimamizi wa mradi huo.
Mwenyekiti wa Bodi, Prof. Mark Mwandosya ( mwenye mkongojo) katika picha ya pamoja na watendaji wa EWURA, Mamlaka ya Maji Tukuyu na Mamlaka ya Maji Mbeya, katika chanzo cha maji Mbaka, wakati wa ziara ya kikazi ya kufuatilia na kutathmini utendaji wa Mamlaka ya Maji Tukuyu na maendeleo ya mradi wa maji Mbaka.
Mwenyekiti wa Bodi ya EWURA, Prof Mark Mwandosya akiwa amesimama mbele ya chanzo cha maji Mbaka, kinachotumika kuhudumia mradi wa maji Mbaka, uliopo chini ya Mamlaka ya maji ya mji wa Tukuyu, alipotembelea mradi huo, 18 Desemba 2023, kufuatilia utekelezaji wake.
Mweyekiti wa Bodi ya EWURA, Prof. Mark Mwandosya ( kushoto) akiwa na Mhandisi Mwandamizi wa Maji EWURA Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Dickson Semkuyu ( katikati) na Mha. Barnabas Konga ( kushoto) kutoka Mamlaka ya Maji Mbeya , katika bonde la Mto Mbaka, ambapo ni chanzo cha maji cha Mradi wa Maji Mbaka, kijiji cha Isebe, kitongoji cha Mbaka Juu, Tukuyu, wakati wa ziara ya kikazi ya watendaji hao kufuatilia maendeleo ya mradi huo, 18 Desemba 2023.
Mwenyekiti wa Bodi ya EWURA, Prof Mark Mwandosya ( aliyeketi) akisisitiza jambo kwa watendaji EWURA, Mamlaka ya Maji Mbeya na Tukuyu, wakati wa ziara ya kikazi kijijini Isebe, kata ya Itagata, Mbaka Juu, 18 Desemba 2023; kilipo chanzo cha maji cha mto Mbaka kitakachohudumia mradi wa maji wa Mbaka, wenye thamani ya bilioni 4.5, unaotekelezwa na Serikali ya Awamu ya sita, ili kuimarisha huduma ya maji kufikia asiliamia 95, katika mji wa Tukuyu.
Chanzo cha Maji cha Mto Mbaka, nje ya kidogo ya mji wa Tukuyu, katika kitongoji cha Mbaka Juu, kijiji cha Ibese, kata ya Itagata, kitakachohudumia mradi wa maji Mbaka.
Chanzo cha Maji cha Mto Mbaka, kilichopo kitongoji cha Mbaka Juu, Kijiji cha Isebe, kata ya Itagata, nje kidogo ya mji wa Tukuyu. Chanzo hicho kitahudumia mradi wa maji wa Mbaka, unaotekelezwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa lengo la kuimarisha huduma ya maji katika mji wa Tukuyu na maeneo ya jurani.