Sunday, 17 December 2023

IAA YAJIPANGA KUJITANUA KITAIFA NA KIMATAIFA


Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) Prof. Eliamani Sedoyeka amesema Chuo hicho kimejipanga kuongeza wigo wa kutoa mafunzo, kufanya tafiti na kutoa ushauri wa kitaalam kitaifa na Kimataifa.

Prof. Sedoyeka ametoa kauli hiyo Desemba 15 wakati akitoa hotuba yake katika mahafali ya 25 ya IAA yaliyofanyika jijini Arusha.

“Katika Mpango Mkakati (Strategic Plan) wa Chuo wa miaka mitano wa mwaka 2022/2023 hadi mwaka 2026/2027 tumejiwekea lengo la kuongeza wigo wa kutoa elimu Kitaifa na Kimataifa. Kwa sasa tuna Kampasi nne ambazo ni Arusha, Babati, Dar es Salaam na Dodoma na kuanzia mwaka 2024 tunatarajia kuanza kujenga Kampasi Mpya ya Songea mkoani Ruvuma .” amesema.

Ameongeza kuwa pamoja na mpango wa kujenga kampasi ya Songea, IAA inaendela kuboresha miundombinu ya kutoa elimu, ikiwemo madarasa, hosteli, maabara za kompyuta katika Kampasi za Arusha na Babati, na kujenga jengo lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 4500 kwa mara moja kampasi ya Dodoma.

Aidha, amesema IAA imeanza hatua za awali za kuanzisha Kampasi ya kwanza Kimataifa inayotarajiwa kuanzishwa nchini Sudan ya Kusini mjini Juba, katika mwaka wa masomo wa 2024/2025.

Naye Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. David Silinde ambaye aliyekuwa Mgeni rasmi katika mahafali hayo akimwakilisha Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba, ameipongeza IAA kwa hatua hiyo, na kwa namna ilivyoboresha miundombinu katika kukidhi ongezeko la wanafunzi wa elimu ya juu ambalo ni matokeo ya uwekezaji uliofanywa na Serikali katika sekta ya elimu.

Vile vile Mhe. Silinde ametoa wito kwa wahitimu kutumia elimu waliyopata kupambana na umaskini na kuleta maendeleo katika familia zao, jamii inayomzunguka na Taifa kwa ujumla ikiwa ni sehemu ya jitihada za kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na wa nchi pia.

Katika hatua nyingine Mhe.Silinde ametoa rai kwa wahitimu kutumia matokea ya tafiti zao kutatua changamoto za jamii, “Msifungie matokeo ya tafiti zenu baada ya kuhitimu yatumieni shirikisheni jamii ili yaweze kuwa chachu katika kuleta mabadiliko chanya, kuongeza tija kwenye shughuli za kiuchumi na utendaji kazi wa kila siku.”

Dkt. Suleiman Serera (mhitimu shahada ya uzamili) ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro amesema wanafunzi wengi walivutiwa kujiunga IAA kutokana na ubunifu katika utoaji wa elimu bora; huku akiomba jamii, taasisi za umma na binafsi kutumia tasnifu walizoandika ili ziweze kusaidia kutatua changamoto mbalimbali za jamii.

Naye Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo, CPA. Joseph Mwigune amesema idadi ya wahitimu kwa mwaka 2023 imeongezeka kutoka wahitimu 3529 mwaka 2022 na kufikia wahitimu 5387; kati yao wahitimu wa shahada ya uzamili ni 1139, shahada 1027, stashahada 1260 na astashahada 2061.







Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI DESEMBA 17,2023

Share:

Saturday, 16 December 2023

KATAMBI ATEMBELEA MRADI WA UFYATUAJI TOFALI...AIPONGEZA JUMUIYA YA WAZAZI CCM SHINYANGA MJINI KWA KUANZISHA MIRADI YA KIUCHUMI


Naibu waziri Ofisi ya waziri mkuu kazi, vijana, Ajira na wenye ulemavu ambaye pia ni mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Katambi ameipongeza Jumuiya ya wazazi wa Chama Cha Mapinduzi Shinyanga Mjini kwa kuanzisha mradi wa utengenezaji wa tofali kwa ajili ya kujiendeleza kiuchumi.

Katambi ametoa pongezi hizo leo Desemba 16, 2023 wakati alipotembelea mradi huo uliopo kata ya Kambarage manispaa ya Shinyanga.

Awali akizungumza wakati wa kikao cha mwaka cha baraza la Jumuiya ya wazazi ya Chama Cha Mapinduzi Shinyanga Mjini Mwenyekiti wa baraza hilo Fue Mlindoko  amesema wamejipanga kusimamia kikamilifu utekelezaji wa miradi hiyo inayoenda kuanzishwa ili iweze kunufaisha Jumuiya ya wazazi ya Chama Cha Mapinduzi Shinyanga Mjini.

"Sisi kama Jumuiya ya wazazi tumezamilia kuanzisha miradi ambayo kujialisha kisiasa na kiuchumi, kupitia kamati ya utekelezaji tumejipanga kufanya kazi kubwa ya kujenga Jumuiya imara miongoni mwa miradi tuliyoanzisha tumeanzisha kiwanda kidogo cha utengenezaji wa tofali za ujenzi kupitia kamati ya utekelezaji tutaendelea kusimama imara na kufikia malengo tuliyojiwekea", amesema Fue Mlindoko.

Katibu wa  Jumuiya ya wazazi wa Chama Cha Mapinduzi Shinyanga Mjini Doris Kibabi amesema mradi huo umegharimu kiasi cha Shilingi milioni 9,300,000 ikihusisha ununuzi wa mashine mbili za utengenezaji wa tofali, kalo la kuhifadhia maji, umeme, mafundi pamoja na vifaa vingine.

Kwa upande wake Naibu waziri Ofisi ya waziri mkuu kazi, vijana, Ajira na wenye ulemavu ambaye pia ni mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Katambi ameipongeza Jumuiya ya wazazi ya Chama Cha Mapinduzi Shinyanga Mjini kwa kuanzisha mradi wa utengenezaji wa tofali na kuahidi kama mbunge wa jimbo hilo kutafuta masoko kupitia miradi inayotekelezwa maeneo mbalimbali ndani ya manispaa ya Shinyanga.

"Miradi hii inayoanzishwa ni ya kila mmoja wetu kwenye Jumuiya ya wazazi wa Chama Cha Mapinduzi Shinyanga Mjini na msimamizi wa miradi inayotekelezwa na Jumuiya hii, tunao viongozi wazuri wa wa usimamizi wa miradi yetu, nitoe ahadi kwenu kutafuta masoko ya ununuzi wa tofali kutoka kwenye kiwanda hiki kupitia miradi ya ujenzi inayotarajia kuanza utekelezaji ikiwemo ujenzi wa stendi kuu ya Shinyanga, Shule pamoja na soko kubwa la kisasa,"

"Niipongeze sana Jumuiya ya wazazi Shinyanga Mjini kwa kuanzisha mradi huu na kuendelea kujiimarisha kisiasa na kiuchumi, lakini pia kupitia mradi huu vijana wengi watanufaika kwa kupata ajira na wengine kufanya biashara jirani na eneo hilo", amesema Mhe. Katambi.

"Kama mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi tumeendelea kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa barabara, madaraja, shule na masoko, na ifikapo 2025 tutakuwa tumekamilisha yale yote niliyoahidi ndani ya manispaa ya Shinyanga, tuendelee kumuombea Rais wetu Mhe. Samia Suluhu Hassan kupitia serikali ya awamu ya sita kwa kuendelea kutoa fedha za ujenzi wa miradi mikubwa ndani ya mkoa wa Shinyanga", ameongeza Mhe. Katambi.

Aidha katika kikao cha baraza la Jumuiya ya wazazi wa Chama Cha Mapinduzi Shinyanga Mjini kilichoketi leo kimehusisha ugawaji wa vyeti vya pongezi kwa waliofanikisha ujenzi wa mradi huo pamoja na kuunda kamati ndogo ndogo zitakazosaidia jumuiya hiyo katika utendaji kazi.

Mashine ya kutengeneza tofali kwa kutumia umeme.
Mashine ya kutengeneza tofali kwa kutumia mikono.
Kalo la kuhifadhia maji.


Baadhi ya wajumbe wa baraza la Jumuiya ya wazazi ya Chama Cha Mapinduzi Shinyanga Mjini waliotembelea mradi huo.

Baadhi ya wajumbe wa baraza la Jumuiya ya wazazi ya Chama Cha Mapinduzi Shinyanga Mjini waliohudhuria kikao cha mwaka cha baraza hilo.





Zoezi la ugawaji wa vyeti vya pongezi kwa waliofanikisha ujenzi wa mradi huo.






Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger