Sunday, 3 December 2023

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI DESEMBA 3,2023







Share:

Saturday, 2 December 2023

KITUO CHA UMEME LEMGURU ARUSHA KUANZA KAZI MUDA WOWOTE

 

Mwonekano wa nje wa kituo Kituo cha  kupoza umeme wa mradi wa Kenya Tanzania cha Lemguru kilichopo Mkoani Arusha kilichojengwa na Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA) kwa kushirikiana na Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB). 
Mwakilishi Mkuu wa JICA, Ara Hitoshi  akizungumza na waandishi wa habari, Wakati Wa ziara ya wana habari Jijini Arusha kwenye mradi wa vituo vya kupoza umeme mradi wa Kenya Tanzania cha Lemguru. 
Afisa utawala na Mawasiliano JICA Tanzania, Alfred Zacharia akipewa maelekezo kutoka kwa Meneja mradi wa vituo vya kupoza umeme mradi wa Kenya Tanzania,  Timothy Mgaya,  Jijini Arusha. 






Picha mbalimbali za muonekano wa ndani wa Kituo cha Umeme Lemguru kilichopo Mkoani Arusha. 

Picha ya pamoja Kati ya viongozi wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA) na Viongozi wa Mradi wa Kituo cha Umeme Lemguru kilichopo Mkoani Arusha. 

  (PICHA ZOTE NA JAMES SALVATORY) 
                       
***********
  Na James Salvatory

 Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA) kwa kushirikiana na Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) kimefanikiwa kujenga Kituo cha Umeme Lemguru kilichopo Mkoani Arusha kwa zaidi ya Sh655 bilioni. 
 
Akizungumza na waandishi wa habari, waliofanya ziara eneo hilo, Meneja mradi wa vituo vya kupoza umeme mradi wa Kenya Tanzania ,  Timothy Mgaya, amesema hadi sasa ujenzi wa miundombinu ya kituo hicho umefikia takribani asilimia 99 na kinachofanyika sasa ni uthibitishaji wa vifaa vilivyofungwa kwa kuvipima kabla ya kuwashwa rasmi. 
 
Amesema kukamilika kwa mradi huo utawezesha Tanzania kuwa na uwezo wa kununua umeme pindi kutakapokuwa na upungufu nchini na watu wa nchi za kusini wataweza kutumia mradi huo kupitisha umeme wao pindi wanapohitahi kununua Umeme kwa ajili ya nchi zao.
 
"Hii ni njia muhimu kwa nchi kwani itaweza kutusaidia katika namna zote, tukihitaji kununua umeme itakuwa rahisi au nchi za kusini zikitaka kununua umeme zitatumia njia yetu kwani watakapohitaji kupitisha watalipia," amesema Mgaya.


Mradi huo wa kusafirisha umeme unaounganisha Tanzania na Kenya kwa msongo wa Kilovoti 400 pia utakuwa na uwezo wa kusafirisha MW2,000.
 
Mgaya amesema lengo la mradi huo ni kusafirisha umeme kwa kushirikiana na Kenya kupitia East Afrika Power pool hadi Ethiopia sehemu wanayotegemea umeme huo kutoka na kwa upande wa kusini mradi huo ukiiunganisha Tanzania na Zambia kupitia South African Power Pool.
 
Katika upande wa uthibitishaji wa miundombinu unaofanyika sasa kabla ya mradi kuwashwa Mgaya alisema njia ya kutoka Singida hadi Arusha imeshathibitishwa baada ya kupimwa na kuwa tayari kwa matumizi.
 
"Njia iliyobakia ni Km114 kutoka Arusha hadi mpaka wa Namanga ambao uko hatua za kuthibitishwa vifaa hivyo kwa kupimwa na kuwa tayari kwa matumizi," amesema Mgaya.
 
Tanzania inakamilisha mradi huu wakati ambao tayari Kenya imeshaanza kununua umeme kutoka Ethiopia kwa mkataba wa miaka 25 tangu Novemba mwaka jana.
 
Mkataba huo uliosainiwa baina ya nchi hizo mbili uliifanya Ethiopia kuiuzia Kenya Megawati 600 kutoka mradi wao wa umeme wa Megawati 2,000 wanaozalisha kwa maji.
 
Mbali na Kenya, nchi nyingine zinazonunua umeme kutoka Ethiopia ni Sudan na Djibouti.
 
Akifafanua zaidi kuhusu mradi wa Kenya- Tanzania amesema unahusisha ujenzi wa kilomita 510 wa njia za kusafirisha umeme kwa msongo wa Kv400 kuanzia Singida hadi Arusha kabla ya kufika Kenya kituo cha Isinya.
 
Mradi huo una urefu wa Km414 kwa upande wa Tanzania huku ukiwa na urefu wa Km96 kwa upande wa Kenya.
 
Kwa upande wake Ofisa wa Mambo ya nje daraja la pili Ubalozi wa Japan, Tabochi Tomoyoshi amesema Japan kwa muda mrefu imekuwa ikiisaifia Tanzania katika utekelezaji wa shughuli za nishati huku akieleza kuwa mradi huo ni muhimu katika kufanya maendeleo ya nchi.
 
"Japan tunaheshimu sana umiliki wa shughuli zote chini ya mikono ya Afrika na katika ujenzi huu tunashirikiana na AfDB na tunatumaini kama nchi tutaendelea kushirikiana na Tanzania katika miradi mbalimbali," amesema Tomoyoshi.
Share:

Video : SLYVEPO - HAMO

 

Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI DESEMBA 2,2023

Share:

MBINU NILIYOTUMIA NA KUSHINDA BET, SASA NI TAJIRI MKUBWA

Hapa duniani kuna njia nyingi za kuweza kufanikiwa kimaisha, changamoto inakuwa jinsi gani utaweza kupata hizo njia na kuzitumia hadi kuweza kufanikiwa.

Kibaya zaidi ni kwamba ni watu wachache sana waliofanikiwa ambao hueleza ukweli kuhusu siri za mafanikio yao, wengi husema uongo kuhofia kupitwa kimafanikio au kukutwa na gundu.

Moja ya njia ambazo zinaonekana kuwa nyepesi kufanikiwa kimaisha ni kubashiri michezo (bet), unapoweka fedha kidogo unaweza kuona utashinda fedha nyingi endapo timu ulizochagua zitashinda kama ulivyobashiri.

Hata hivyo, watu wengi hasa vijana hujikuta katika maisha ya kubet kwa miaka mingi bila kufanikiwa kupata fedha yoyote zaidi ya fedha zao kuzinufaisha kampuni za bet na mawakala wao.

Mimi nilikuwa ni mmoja wapo, nilitumia fedha zangu nyingi kwa miaka zaidi ya minne lakini sikuwahi kushinda, nilikuwa naona watu kwenye TV na Magazeti wakitangazwa kuwa wameshinda mamilioni ya fedha kupitia bet nikawa naumia moyoni na kujiuliza wenzangu wanatumia mbinu gani kushinda.

Niliendelea kubet nikiamini kuna siku yangu itakuja, lakini nilijikuta nimemaliza fedha zangu hadi kuanza kuuza vitu vyangu vya ndani kama kitanda, radio, godoro na vyombo vya kulia chakula.

Asubuhi moja nilikuwa nasikiliza kituo kimoja cha Radio nikasikia kuhusu mtu anaitwa African Doctors , walielezea kuwa anaweza kumsaidia mtu kushinda bahati nasibu kwenye michezo ya bet, mtangazaji wa kipindi alitaja namba zake ambazo ni +254 769404965, nilizichukua na kuwasiliana naye.

Katika mazungumzo yetu  African Doctors alinihakikishia kuwa ndani ya siku tatu nitaweza kushinda bahati nasibu na kusahau machungu yote na kuliwa fedha zangu kwa miaka tele.

Siku tatu mbele niliamua kufanya ubashiri wangu wa timu 13 katika Jackpot ya mamilioni ya fedha na kushinda, huo ukawa ndio mwanzo wangu wa kuagana na umaskini ambao umekuwa kinitesa kwa miaka mingi mimi na familia yangu, ndugu jamaa na marafiki.

Kwasasa nimeweza kujenga nyumba mbili, moja nimepangisha na nyingi naishi na mke wangu, pia nimenunua pikipiki nne ambazo zimewapa vijana wananiletea fedha kila jioni. Ama kwa hakika kama sio usaidizi wa African Doctors nisingeweza kufanya haya yote maishani mwangu na wala sikutarajia.

Binafsi kutoka kwenye uvungu wa moyo wangu ningependa kila kijana ambaye amekuwa akibashiri michezo na kuondoka patupu kujua siri hii ya mafanikio. Nayo ni African Doctors ambaye amesaidia wengi.

Kumbuka African Doctors ana uwezo kumfanya mtu kuwa na bahati maishani mwake, kushinda michezo ya bahati nasibu, kukukinga na maadui zako, kukufanya ushinde migogoro kama ya ardhi, kuwa na mvuto wa kimapenzi, kuongeza mauzo katika biashara.

Pia anatibu magonjwa kama kaswende, kisonono, kifua kikuu, presha, kifafa, upungufu wa nguvu za kiume, kuvimba miguu, kaswende, vile vile anawezesha wanawake kubaba ujautizo, wanaume kutungisha mimba n.k.

Wasiliana na African Doctors kwa namba; +254 769 404965, tembelea tovuti yao; www.african-doctors.com au watumie email; africandoctorheals@gmail.com.

Mwisho.


Share:

Friday, 1 December 2023

MTAYARISHAJI WA MUZIKI MASTERKRAFT AREJEA TENA MAJEED & JOEBOY

Mtayarishaji mahiri wa muziki kutoka nchini Nigeria Masterkraft ameingia studio tena na Majeed pamoja na Joeboy.

Baada ya muda mrefu kufanya vizuri na ngoma yake iitwayo Hosanna akiwa ameshirikiana na msanii Chike Masterkraft ameendelea kuwa na uchaguzi bora wa nani amshirikishe kwenye kazi zake.

Kwa mara nyingine Masterkraft ameachia ngoma yake mpya iitwayo FRUIT akiwa amewashirikisha Majeed na Joeboy.

Inapatikana katika mitandao yake yote ya kusambaza na kusikiliza muziki pamoja na unaweza kuwafatilia katika mitandao yao yote ya kijamii.
 
Share:

WATU WENYE ULEMAVU WAWEZESHWA RUFIJI



Na Mwandishi wetu

Watu wenye Ulemavu Wilaya ya Rufiji wamepatia vifaa saidizi ikiwemo Viti mwendo 45 ambavyo vimetolewa na Mbunge wa Jimbo hilo mhe. Mohamed Mchengerwa ambaye pia ni Waziri wa TAMISEMI ikiwa ni sehemu ya uwezeshaji kwa kundi hilo kuendelea kutatua changamoto wanazokabiliana nazo.

Akikabidhi vifaa hivyo wakati wa mafunzo ya watu wenye ulemavu sambamba na mwendelezo wa programu za tamasha la kumbukumbu ya Bibi Titi Mohammed katika Ukumbi wa Ikwiriri Wilaya ya Rufiji, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Ummy Nderiananga amewaasa kutunza vifaa hivyo na kuvitumia kwa manufaa ya ambapo pia alishiriki chakula cha pamoja na watu wenye ulemavu wakati wa mafunzo hayo.

Naibu Waziri huyo amesema kuwa kundi hilo limekuwa likikutana na changamoto nyingi ikiwamo kudharauliwa, kubaguliwa, kutoaminiwa na hata kunyanyaswa kutokana na hali zao na kuitaka jamii kuacha kuwanyanyapaa na kuwaficha watu wenye ulemavu badala yake wawaibue na kuwaunganisha na fursa mbalimbali katika jamii.

Naibu Waziri huyu akikabidhi vifaa hivyo amemshukuru mbunge huyo kwa kuendelea kuwapenda na kuwajali watu wenye ulemavu na kueleza kuwa zoezi la kubaini takwimu za watu wenye ulemavu wote pamoja na mahitaji yao kulingana na aina ya ulemavu walio nao lengo ni kuweza kuwawezesha watu wenye ulemavu kwa kuwapatia mahitaji yao.

“Kipekee nampongeza Mbunge wenu hapa Rufiji Mhe. Mchengerwa kwa namna anavyowapigania na kujali mahitaji yenu na leo ameniomba niwe mgeni rasmi na kukabidhi vifaa hivi, tuendelee kumuunga mkono mbunge wetu kwa moyo wake wa kizalendo kwa wana Rufiji,” alisisitiza Naibu Waziri huyo.

Amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Uongozi mahiri wa Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inawajali na inatambua kundi la Watu wenye ulemavu.

“Serikali imekuwa ikiandaa na kusimamia programu mbalimbali za uwezeshaji kwa watu wenye ulemavu ikiwa ni pamoja na kuweka mazingira wezeshi kama vile kutenga nafasi maalum za ajira, kusisitiza uwekaji wa miundombinu rafiki kwa watu wenye ulemavu katika ofisi na taasisi mbali mbali za umma, kutoa mafunzo mbalimbali ya kuwajengea uwezo watu wenye ulemavu,”Amesema Mhe. Ummy.

Pia ameeleza kwamba kwa mujibu wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya 2020 -2025 ibara ya 94 na 95 imeweka bayana na kuielekeza Serikali kuendelea kuweka mazingira wezeshi na rafiki kwa watu wenye ulemavu ili waendelee kuchangia ipasavyo katika maendeleo ya Taifa.

“Mafunzo haya yatakayotolewa yasaidie kutujenga na kutuwezesha kutambua na kupambanua masuala mbalimbali yanayohusu Watu wenye ulemavu na hii iwe ni fursa na chachu ya kuongeza ushiriki wa kila mmoja wetu katika shughuli za kijamii na kiuchumi,” Ameeleza Mhe. Ummy.

Aidha Mhe. Ummy aliwakumbusha adhma ya Serikali ni kuhakikisha watu wenye ulemavu nchini wanaendelea kupatiwa huduma zote muhimu kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zilizopo huku akieleza kuwa waendelee kujiamini sababu Serikali yao inawajali na kuthamini sana mchango wao katika Taifa.

“Mhe Samia Suluhu Hassan ameendelea kutujali sisi watu wenye ulemavu hivyo tusiwe wanyonge na tuendelee kumuunga mkono katika kujiletea maendeleo yetu ya kila siku.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger