Thursday, 5 October 2023

TCRA YAADHIMISHA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA KWA KUTOA ELIMU KWA WADAU WA UTANGAZAJI KANDA YA ZIWA




Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeendesha Programu ya utoaji elimu kwa wadau wa utangazaji Kanda ya Ziwa kuhusu Kanuni Mpya za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta za Kusimamia Huduma za Utangazaji za Jamii ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja.


Mafunzo hayo yamefanyika leo Alhamisi Oktoba 5,2023 jijini Mwanza ambapo Wadau wa utangazaji (Redio na watoa huduma za utangazaji kwa njia ya waya).

Katika Programu hiyo ya utoaji elimu, wadau wa utangazaji wamepewa elimu kuhusu Kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta za kusimamia Huduma za Utangazaji za Kijamii, Mwongozo kwa watoa huduma za utangazaji kwa njia ya waya (Guideline for Cable Operators) na Mawasiliano na TCRA (Tanzanite Portal).

Akifungua mafunzo hayo, Meneja Kitengo cha Huduma ya Utangazaji kutoka TCRA, Mhandisi Andrew Kissaka amesema Watangazaji wana nafasi kubwa sana katika jamii hivyo ni vyema wakafanya kazi kwa weledi kwa kuzingatia Kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta za Kusimamia Huduma za Utangazaji za Jamii ili kuilinda jamii.

"Jinsi jamii tunavyoiona inatokana na mambo yanatotolewa kwenye vyombo vya habari, kama tunafanya vibaya basi pia tunaiharibu jamii, kama tunatengeneza vipindi vizuri basi tunajenga jamii bora. Mna nafasi kuwa sana ya kuitengeneza jamii hivyo ni lazima mtengeneze vipindi vya kujenga jamii ndiyo maana tunatengeneza kanuni za utangazaji  ili jamii iendelee kuwa salama",amesema Mhandisi Kissaka.

"Teknolojia zinakuja lakini umuhimu wa Redio za kijamii unabaki pale pale hivyo ni muhimu mtambue kuwa nafasi yenu katika jamii ni kubwa sana",ameongeza Kissaka.

Kwa upande wake, Meneja wa TCRA Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo amesema wametoa elimu kwa wadau wa utangazaji kuhusu Kanuni Mpya za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta za Kusimamia Huduma za Utangazaji za Jamii ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja.

Mhandisi Mihayo ametumia fursa hiyo kuwahamasisha watoa huduma za utangazaji kutumia zaidi mfumo wa kidigitali 'TCRA Tanzanite Portal' kuwa wasiliana kwa urahisi zaidi na mamlaka hiyo.

"Tunataka mtumie Digitali zaidi kuwasiliana na TCRA badala ya kutumia muda mwingi kuja TCRA. Tumieni mfumo wa Tanzanite Portal ili kuokoa gharama na muda wa kusafiri kufuata huduma, tunataka mtumie digitali kuwasiliana na TCRA. Ukitaka kuwasiliana na TCRA unaingia kwenye ukurasa wetu unaweka kile ambacho unataka sisi TCRA tukione",amesema Mhandisi Mihayo.

Katika hatua nyingine amewataka watangazaji kuzingatia maudhui wanayotoa kwenye vipindi kwa kuhakikisha wanatumia lugha nzuri ili kujenga jamii bora.

"Punguzeni sana kuchanganya lugha, mfano Kiingereza na Kiswahili lakini pia punguzeni kushabikia mambo ambayo hayako vizuri kwenye vipindi. Epukeni kushabikia masuala ya kisiasa. Usianze kutangaza kitu ambacho kina mkwamo kabla ya kuwasiliana na mamlaka husika mfano masuala ya matangazo ya Waganga wa kienyeji, tiba lishe, nguvu za kiume n.k", amesema Mhandisi Mihayo.

"Mwaka ujao ni mwaka wa uchaguzi, msishabikie masuala ya kisiasa, msinunulike, ukialika kiongozi wa chama cha siasa flani hakikisha unaalika na kutoka chama kingine, ukiona umealika mmoja mwingine hajaja acha hadi wawepo wote",ameongeza Mihayo.
Meneja Kitengo cha Huduma ya Utangazaji kutoka TCRA, Mhandisi Andrew Kissaka akizungumza wakati akifungua Programu ya utoaji elimu kwa wadau wa utangazaji Kanda ya Ziwa kuhusu Kanuni Mpya za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta za Kusimamia Huduma za Utangazaji za Jamii. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Meneja Kitengo cha Huduma ya Utangazaji kutoka TCRA, Mhandisi Andrew Kissaka akizungumza wakati akifungua Programu ya utoaji elimu kwa wadau wa utangazaji Kanda ya Ziwa kuhusu Kanuni Mpya za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta za Kusimamia Huduma za Utangazaji za Jamii 
Meneja Kitengo cha Huduma ya Utangazaji kutoka TCRA, Mhandisi Andrew Kissaka akizungumza wakati akifungua Programu ya utoaji elimu kwa wadau wa utangazaji Kanda ya Ziwa kuhusu Kanuni Mpya za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta za Kusimamia Huduma za Utangazaji za Jamii
Meneja Kitengo cha Huduma ya Utangazaji kutoka TCRA, Mhandisi Andrew Kissaka akitoa mada kuhusu Kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta za kusimamia Huduma za Utangazaji za Kijamii
Meneja Kitengo cha Huduma ya Utangazaji kutoka TCRA, Mhandisi Andrew Kissaka akitoa mada kuhusu Kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta za kusimamia Huduma za Utangazaji za Kijamii
Meneja wa TCRA Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo akizungumza wakati wa Programu ya utoaji elimu kwa wadau wa utangazaji Kanda ya Ziwa kuhusu Kanuni Mpya za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta za Kusimamia Huduma za Utangazaji za Jamii 
Meneja wa TCRA Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo akizungumza wakati wa Programu ya utoaji elimu kwa wadau wa utangazaji Kanda ya Ziwa kuhusu Kanuni Mpya za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta za Kusimamia Huduma za Utangazaji za Jamii 
Meneja wa TCRA Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo akizungumza wakati wa Programu ya utoaji elimu kwa wadau wa utangazaji Kanda ya Ziwa kuhusu Kanuni Mpya za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta za Kusimamia Huduma za Utangazaji za Jamii 
Meneja wa TCRA Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo akizungumza wakati wa Programu ya utoaji elimu kwa wadau wa utangazaji Kanda ya Ziwa kuhusu Kanuni Mpya za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta za Kusimamia Huduma za Utangazaji za Jamii 
Mhandisi Mkuu kitengo cha Huduma za Utangazaji TCRA Mhandisi Jan Kaaya akiwasilisha Mada kuhusu Mwongozo kwa Watoa Huduma za Utangazaji kwa Njia ya Waya (Guideline For Cable Operators)
Mhandisi Mkuu kitengo cha Huduma za Utangazaji TCRA Mhandisi Jan Kaaya akiwasilisha Mada kuhusu Mwongozo kwa Watoa Huduma za Utangazaji kwa Njia ya Waya (Guideline For Cable Operators)
Afisa TEHAMA Mkuu TCRA, Irene Kahwili akiwasilisha mada kuhusu Mawasiliano na TCRA (Tanzanite Portal)
Afisa TEHAMA Mkuu TCRA, Irene Kahwili akiwasilisha mada kuhusu Mawasiliano na TCRA (Tanzanite Portal)
Afisa TEHAMA Mkuu TCRA, Irene Kahwili akiwasilisha mada kuhusu Mawasiliano na TCRA (Tanzanite Portal)
Afisa TEHAMA Mkuu TCRA, Irene Kahwili  akiwasilisha mada kuhusu Mawasiliano na TCRA (Tanzanite Portal)
Mwenyekiti wa Umoja wa watoa huduma za utangazaji Tanzania (NIBA), Amos Ngosha akizungumza wakati wa mafunzo hayo
Katibu wa Umoja wa watoa huduma za utangazaji Tanzania (NIBA), Heavenlight Kavishe akizungumza wakati wa mafunzo hayo
Katibu wa Chama cha Umoja wa Cable Tanzania (TACOL), Hirnoy Barmeda akichangia hoja kwenye mafunzo







Share:

PROF. JAY NA MKEWE WATANGAZA KIJIJI CHA NGURUWE DODOMA.... 'KUSANYIKO KUU LA NGURUWE DUNIANI'


Mkurugenzi wa PigInvest International Plc Bi. Grace Mgonjo ambaye pia ni Mke wa Msanii na Mwanasiasa Maarufu ndani nje ya nchi ya Tanzania Joseph Leonard Haule ‘Professor JAY’ Mwana wa Mituringa ametambulisha mradi wa ufugaji wa Nguruwe almaarufu Kitimoto katika kijiji cha Zamahero Mayamaya wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma.


Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Oktoba 3,2023, Bi. Mgonjo amesema yeye na mmewe Prof. JAY wameamua kuja na mradi huo kwa Umma baada ya kuona nyama ya nguruwe almaarufu Kitimoto inaliwa sana na Watanzania.

“Tumeamua kuja na mradi huu wa Kijiji cha Nguruwe ukizingatia kuwa nyama hii inatumiwa na watanzania takribani Milioni 48 na katika Afrika inatumiwa na watu takribani Bilioni 1.4 hii ni takribani asilimia 70 ya watu wote”,ameeleza.

Amefafanua kuwa mtu akiwekeza kwenye Nguruwe mmoja anaweza kupata mpaka mara mbili ya uwekezaji wake ndani ya mwaka mmoja.
Ameongeza kuwa uwepo wa chakula kingi cha nguruwe hususani mashudu ya Alizeti katika mikoa ya Kanda ya Kati imekuwa kichocheo kikubwa cha kuanzisha mradi wa ufugaji wa Nguruwe Mkoani Dodoma katika kijiji cha Zamahero Mayamaya wilaya ya Bahi.

"Ujue miaka mingi watanzania wamekuwa wakifuga nguruwe kienyeji bila kurasimisha shughuli za ufugaji na hivyo serikali inakosa mapato makubwa kwenye mifugo inayopendwa kuliko yote, hivyo tunaamini mradi huu utakuwa na manufaa makubwa katika taifa",amesema Mgonjo.

Aidha ameiomba Serikali iwasaidie kuutangaza mradi huu ambao unaajiri wanawake wenye maisha magumu zaidi ya 200 na tayari wengine wako shambani wakitayarisha shamba la Nguruwe.

Gharama za mradi:

Mradi huo wa ufugaji nguruwe utagharimu zaidi ya Bilioni 270 mpaka kuisha kwake 2026.

“Magari ya Friji zaidi ya 100 yatakuwepo eneo la mradi (site) kwa ajili ya kusambaza nyama Tanzania nzima na duniani kwa ujumla. Tutauza Hisa ili kukuza mtaji na pia tutawaalika wananchi kuwekeza katika mradi huu mkubwa, hii ni fursa kubwa hasa kwa watu wa maofisini na walio busy”,ameeleza.

Amesema Kiwanda cha kuchakata nyama ya nguruwe kitatengenezwa hapo hapo Zamahero Mayamaya Bahi mkoani Dodoma Tanzania ambapo idadi ya Nguruwe ni Milioni 3.

“Endapo kuna mtu anahitaji maelezo zaidi awasiliane naye kwa simu namba 0627122122 au 0627188188",amesema


Katika hatua nyingine Mke wa proffessor Jay ameiomba Serikali pia iangazie mradi wa Kijiji cha Vanilla kwani serikali itapata fedha nyingi sana za kodi na fedha za kigeni kupitia mradi huo.

Share:

GGML YAIBUKA MSHINDI WA JUMLA MAONESHO YA MADINI GEITA

Makamu wa Rais wa pili Zanzibar, Hemed Suleiman (kushoto) akimkabidhi tuzo Mkurugenzi mtendaji wa GGML, Terry Strong baada ya kampuni hiyo kuibuka mshindi wa jumla katika maonesho ya teknoloji ya madini Geita.
Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) wakifurahia tuzo walizozipata katika maonesho ya teknolojia ya madini Geita. GGML iliibuka na tuzo nne ikiwamo ya muoneshaji bora pamoja na mshindi wa jumla.
Mkurugenzi Mtendaji wa GGML, Terry Strong (aliyevaa suti katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafaanyakazi wa GGML baada ya kuwaa tuzo nne katika maonesho ya teknojia ya madini Geita, ikiwamo mshindi wa jumla ya maonesho hayo ambayo pia GGML ilikuwa mdhamini mkuu.

NA MWANDISHI WETU

KAMPUNI ya Geita Gold Mining Limited imenyakua tuzo nne ikiwamo mshindi wa jumla katika maonesho ya teknolojia ya madini yaliyofanyika kwa muda wa siku 10 mjini Geita na kushirikisha washiriki zaidi ya 400.

Katika maonesho hayo ambayo yalianza tarehe 20 Septemba hadi tarehe 30 Septemba mwaka huu, Hospitali ya rufaa ya mkoa Geita kwa kushirikiana na GGML, pia ilitoa huduma za upimaji wa saratani kwa wananchi zaidi ya 1000.

Akifunga maonesho hayo kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassan, Makamu wa pili wa Rais Zanzibar, Hemed Suleiman aliipongeza GGML pia kwa kuibuka na tuzo ya muoneshaji bora kwa mwaka 2023.
Kampuni hiyo pia ilipewa hati maalumu ya shukrani kwa kuwa mdau muhimu tangu kuanzishwa kwa maonesho hayo mwaka 2018 pamoja na hati ya shukrani ya kuwa mdhamini mkuu ambapo kwa mwaka huu ilitoa zaidi ya Sh milioni 150.

Akisoma hotuba hiyo kwa niaba ya Rais Samia katika maonesho hayo, Suleiman alisema Dira ya Sekta ya Madini (Vision 2030) inalenga kumaliza changamoto za muda mrefu kwa wachimbaji wadogo za kukosekana kwa taarifa za kuaminika za maeneo yenye rasilimali hiyo.

Dira ya ‘Madini ni Maisha na Utajiri’ imelenga kuhakikisha hadi kufikia 2030 utafiti wa madini kwa njia za jiofizikia uwe umefanyika nchini wa zaidi ya asilimia 50.

“Serikali inaendelea kuhakikisha wachimbaji wa madini wanapata masoko ya uhakika na itaendelea kuwawezesha wawekezaji wadogo wa sekta hii kwa kuwaunganisha na taasisi za fedha,” asema Rais Samia.

Aidha, Mkurugenzi Mtendaji wa GGML, Terry Strong alisema katika siku 10 za maonesho hayo, anaamini washiriki wakiwa wachimbaji wadogo wamejionea na kujifunza teknolojia mbalimbali ambazo GGML inazitumia katika kuhakikisha kuwa uchimbaji madini unafanyika kwa usalama na tija.

“Dhamira yetu ni kuongeza thamani kwa wadau wetu wote kuanzia shughuli za utafiti, uchimbaji na uchakataji wa dhahabu kwa kuongezea thamani na mambo mengine.

“Ni kwa sababu hiyohiyo kwamba tumefanya juhudi zote kuwezesha uhamishaji wa ujuzi na teknolojia kama inavyoonekana katika maendeleo ya miradi yetu mitatu ya uchimbaji na ushiriki wa wasambazaji wa bidhaa na watoa huduma wazawa,” alisema.

Alisema GGML imekuwa ikitoa kipaumbele kwa wazawa kupata mafunzo na zabuni za utoaji huduma ndani ya migodi ya kampuni hiyo kwa mujibu wa matakwa ya sheria ‘local content’ ambapo kwa mwaka 2015 kampuni hiyo ilitumia dola za Marekani milioni 202 na kiwango kimeongezeka hadi kufikia dolaza Marekani milioni 526 mwaka 2022.

Aidha, Meneja Mwandamizi anayeshughulikia mahusiano ya jamii, Gilbert Mworia mbali na kuishukuru Serikali kwa kutambua jitihada za kampuni hiyo, alisema GGML itaendelea kutoa mafunzo kwa watanzania na wachimbaji wadogo ili waweze kupata fursa mbalimbali ndani ya mgodi huo.

Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, alisema wanaamini ifikapo mwaka 2025 mchango wa sekta ya madini katika Pato la Taifa utafikia asilimia 10.

Share:

Wednesday, 4 October 2023

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI OKTOBA 5,2023

























Share:

IHEFU FC YAICHAKAZA YANGA.....YAIDUNGUA 2-1



Timu ya Yanga Sc imepokea kichapo cha goli 2 - 1 kutoka kwa Ihefu Fc.

Mchezo huo umepigwa leo Oktoba 4, 2023 katika uwanja wa Ubaruku ulioko Mbalali jijini Mbeya.

Ambapo katika mchezo huo uliomalizika kwa dakika 90 na kuwaacha mashabiki wa timu ya Yanga sc midomo wazi wakishuhudia timu yao ikipoteza kwa kichapo cha goli 2 dhidi ya Ihefu Fc.

Goli la kwanza likifungwa na Professor Pacom Dakika ya 3 huku magoli ya Ihefu Fc yakifungwa na wachezaji Kisu Dakika ya 40 na goli la pili likifungwa na Ilanifya dakika ya 67 ya mchezo.
Share:

TBS YATOA ELIMU KWA WAJASIRIAMALI KWENYE MAONESHO YA TIMEXPO


SHIRIKA la Viwango Tanzania TBS wametoa elimu kwa wazalishaji wa Bidhaa za Viwandani na wajasiriamali juu ya dhana ya ubora wa bidhaa katika Maonesho ya Kimataifa ya Viwanda Tanzania 2023 (Times Expo 2023)

Akizungumza katika Maonesho hayo leo Oct 4,2023 katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa TBS,Dkt. Athuman Ngenya amesema maonesho haya yanakutanisha wenye Viwanda Tanzania, Wajasiriamali na watu wengine wanaokwenda kumtembelea maonesho hayo hivyo shughuli yao kubwa ni kuhakikisha Wana elimisha wazalishaji kuzalisha bidhaa bora.

"Bidhaa zikiwa na ubora zinakua na faida nyingi,moja nikujiamini lakini pia zinakuwa na soko kubwa itauzika ndani ya nchi na nje ya nchini". Amesema

Ameeleza kuwa lengo la TBS ni kuhakisha inawafikia wajasiriamali na watuamiaji wa mwisho wa bidhaa kuzitambua na kuchagua bidhaa Bora ili wapate kulingana na thamani ya pesa yao.

Pamoja na hayo ametoa wito kwa wazalishaji wa Bidhaa ambazo hazina nembo ya TBS wakajisajiri TBS ili kupata alama ya ubora na amewasihi wananchi kukagua bidhaa wanazo nunua kama zina alama ya ubora kwa ajili ya usalama wao na thamani ya fedha kulingana na ubora.

"Kisheria kiwanda chochote kinachozalisha bidhaa yeyote ambayo haijapitia TBS ni makosa"amesema


Share:

UWANJA WA CCM KAMBARAGE WAFUNGWA MICHEZO YA LIGI KUU


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger