Sunday, 1 October 2023

MKUTANO MKUU WA CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI VIJIJINI 'RUJAT' WAFANYIKA DODOMA, MEENA ACHAGULIWA KUWA MWENYEKITI

Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Vijijini (Rural Journalists Association of Tanzania (RUJAT), Neville Meena akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Mwaka wa RUJAT uliofanyika katika ukumbi wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa - TANAPA Kanda ya Kati jijini Dodoma leo Jumapili Oktoba 1,2023

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Chama cha Waandishi wa Habari Vijijini (Rural Journalists Association of Tanzania (RUJAT) kimefanya Mkutano Mkuu wa Mwaka pamoja na uchaguzi wa viongozi ambapo Neville Meena aliyekuwa Katibu wa muda amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa RUJAT, Prosper Kwigize aliyekuwa Mwenyekiti wa muda akichaguliwa kuwa Katibu, Editha Majura Katibu na Zania Miraji Kweka akichaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti. 

Katika Mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa - TANAPA Kanda ya Kati jijini Dodoma leo Jumapili Oktoba 1,2023, pia wajumbe sita kulingana na Kanda wamechaguliwa ambao ni Anne Rhobi (Pwani), Meshack Ngumba (Magharibi), Hamida Ramadhani(Kati), Musa Juma (Kaskazini), Neema Emmanuel (Kanda ya Ziwa) na Felix Mwakyembe (Kusini).

Akizungumza katika Mkutano huo, uliodhaminiwa na Wakala wa Umeme Vijijini REA, STAMICO na TANAPA, Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Vijijini (Rural Journalists Association of Tanzania (RUJAT), Neville Meena amesema kazi kubwa sasa ya chama hicho ni kupata wanachama wengi zaidi ili kujenga RUJAT yenye nguvu. 
 
Kwa upande wake, Katibu wa RUJAT , Proper Kwigize ambaye ni Mwenyekiti Muasisi wa RUJAT, amesema lengo la Chama hicho ni kuondoa utofauti wa vijijini na mijini kwani katika maeneo mengi ya vijijini hawapati taarifa habari mfano pale majanga yanatokea vijijini wananchi hawapati taarifa.

“RUJAT ni chama cha kipekee sana, hivi sasa kina wanachama 38. Tunataka kuandika habari za kusisimua maendeleo vijijini,tunataka kuondoa mitazamo ya kwamba hakuna haja ya kuandika habari za vijijini. Vyombo vya habari vinafanya vizuri kutokana na kwamba kuna waandishi wa habari vijijini. Uandishi wa habari vijijini ni muhimu sana, hakuna Tv, Redio, Gazeti linatukimbia sisi waandishi wa habari za vijijini”,amesema.

Amesema RUJAT imepanga kufungua tovuti ambayo itakuwa inachapisha habari mbalimbali za vijijini ambayo itakuwa inatumiwa na waandishi wa habari kusambaza habari wanazoandika.
Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Vijijini (Rural Journalists Association of Tanzania (RUJAT), Neville Meena akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Mwaka wa RUJAT uliofanyika katika ukumbi wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa - TANAPA Kanda ya Kati jijini Dodoma leo Jumapili Oktoba 1,2023
Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Vijijini (Rural Journalists Association of Tanzania (RUJAT), Neville Meena akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Mwaka wa RUJAT uliofanyika katika ukumbi wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa - TANAPA Kanda ya Kati jijini Dodoma leo Jumapili Oktoba 1,2023
Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Vijijini (Rural Journalists Association of Tanzania (RUJAT), Neville Meena akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Mwaka wa RUJAT uliofanyika katika ukumbi wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa - TANAPA Kanda ya Kati jijini Dodoma leo Jumapili Oktoba 1,2023
Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Vijijini (Rural Journalists Association of Tanzania (RUJAT), Neville Meena akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Mwaka wa RUJAT uliofanyika katika ukumbi wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa - TANAPA Kanda ya Kati jijini Dodoma leo Jumapili Oktoba 1,2023
Katibu wa Chama cha Waandishi wa Habari Vijijini (Rural Journalists Association of Tanzania (RUJAT),Prosper Kwigize akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Mwaka wa RUJAT uliofanyika katika ukumbi wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa - TANAPA Kanda ya Kati jijini Dodoma leo Jumapili Oktoba 1,2023
Katibu wa Chama cha Waandishi wa Habari Vijijini (Rural Journalists Association of Tanzania (RUJAT) ,Prosper Kwigizeakizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Mwaka wa RUJAT uliofanyika katika ukumbi wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa - TANAPA Kanda ya Kati jijini Dodoma leo Jumapili Oktoba 1,2023
Katibu wa Chama cha Waandishi wa Habari Vijijini (Rural Journalists Association of Tanzania (RUJAT),Prosper Kwigize akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Mwaka wa RUJAT uliofanyika katika ukumbi wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa - TANAPA Kanda ya Kati jijini Dodoma leo Jumapili Oktoba 1,2023
Katibu wa Chama cha Waandishi wa Habari Vijijini (Rural Journalists Association of Tanzania (RUJAT), Prosper Kwigize akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Mwaka wa RUJAT uliofanyika katika ukumbi wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa - TANAPA Kanda ya Kati jijini Dodoma leo Jumapili Oktoba 1,2023

Mweka Hazina wa Chama cha Waandishi wa Habari Vijijini (Rural Journalists Association of Tanzania (RUJAT) Editha Majura akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Mwaka wa RUJAT uliofanyika katika ukumbi wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa - TANAPA Kanda ya Kati jijini Dodoma leo Jumapili Oktoba 1,2023

Mwanachama wa Chama cha Waandishi wa Habari Vijijini (Rural Journalists Association of Tanzania (RUJAT) , Felix Mwakyembe akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Mwaka wa RUJAT uliofanyika katika ukumbi wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa - TANAPA Kanda ya Kati jijini Dodoma leo Jumapili Oktoba 1,2023
Afisa kutoka Benki ya NMB, Jastine Bandoma  akitoa elimu kuhusu Bima zinazotolewa na Benki ya NMB
Afisa kutoka Benki ya NMB, Jastine Bandoma  akitoa elimu kuhusu Bima zinazotolewa na Benki ya NMB
 Afisa kutoka Benki ya TCB,Azory Mpungo akitoa elimu kuhusu Bima zinazotolewa na Benki ya TCB
Afisa kutoka Benki ya TCB,Azory Mpungo akitoa elimu kuhusu Bima zinazotolewa na Benki ya TCB
Wajumbe wakiwa ukumbini
Wajumbe wakiwa ukumbini
Wajumbe wakiwa ukumbini
Wajumbe wakiwa ukumbini
Wajumbe wakiwa ukumbini
Wajumbe wakiwa ukumbini
Wajumbe wakiwa ukumbini
Wajumbe wakiwa ukumbini
Wajumbe wakiwa ukumbini
Wajumbe wakiwa ukumbini
Wajumbe wakiwa ukumbini
Wajumbe wakiwa ukumbini
Wanachama wa RUJAT wakipiga picha ya kumbukumbu
Wanachama wa RUJAT wakipiga picha ya kumbukumbu
Wanachama wa RUJAT wakipiga picha ya kumbukumbu
Viongozi wapya wa RUJAT wakipiga picha ya kumbukumbu
Viongozi wakuu wa RUJAT wakipiga picha ya kumbukumbu
Viongozi wakuu wa RUJAT wakipiga picha ya kumbukumbu na mdau kutoka Benki ya TCB
Viongozi na wanachama wa RUJAT wakipiga picha ya kumbukumbu na mdau kutoka Benki ya NMB.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Share:

NEC YASAMBARATISHA TIMU YA TUME YA HAKI ZA BINADAMU SHIMIWI

Timu ya Kamba wanawake ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakimenyana katika moja ya Michezo yao.
Michuano Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali na Mikoa (SHIMIWI) imezidi kurindima katika viunga vya mji wa Iringa ambapo Timu za Kamba za Tume ya Taifa ya Uchaguzi ( ME na KE )zimeendeleza ubabe wao kwa timu katika Makundi yao.

Katika michezo ya leo Oktoba 01,2023 timu ya Kamba ya Uchaguzi wanaume wamewahenyesha na kuchukua alama mbili kutoka kwa timu ya Kamba kutoka Tume ya Haki za Binadamu.

Mchezo huo ambao awali ulikua unaonekana kuwa mgumu kwa pande zote mbili kutokana na aina ya wachezaji waliopo lakini ulikuwa mwepesi kwa miamba ya Uchaguzi.

Katika mchezo mwingi timu ya wanawake wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi imefanikiwa kuingia katika hatua ya 16 bora hii ni baada ya kumaliza mchezo wao dhidi ya Timu ya Mahakama.

Baada ya matokeo hayo sasa timu ya wanaume wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi imebakiza michezo miwili dhidi ya Timu ya Kamba kutoka Ikulu na Timu ya Kamba kutoka TARURA.

Kundi la H la Kamba wanaume lina timu za Ikulu,NEC, TARURA,Tume ya Haki za Binadamu,Pamoja na Maliasili huku upande wa Kundi A timu ya Kamba wanawake kulikuwa na timu za NEC, Tume ya Utumishi, Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi pamoja na Mahakama.
Share:

UBIA WA TWIGA WAONESHA ATHARI CHANYA ZA KIMAGEUZI ZA UCHIMBAJI MADINI NCHINI, YASEMA BARRICK

Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Barrick, Mark Bristow, akizungumza na waandishi wa habari katika Mgodi wa North Mara juzi kuhusu athari chanya za ubia wa kimageuzi katika uchimbaji madini kwa kushirikiana na Serikali kupitia kampuni ya Twiga. Kushoto ni Meneja wa Barrick nchini, Melkiory Ngido.
Mkuu wa Wilaya, Tarime, Michael Mtenjele, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari katika Mgodi wa North Mara kuhusu mipango ya kuimarisha ulinzi na usalama katika Mgodi wa North Mara baada ya kukutana na Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Barrick, Mark Bristow.
Mbunge wa Tarime vijijini,Mwita Waitara,akiongea katika mkutano huo.
Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Barrick, Mark Bristow, akikabidhi mfano wa hundi ya dola za kimarekani elfu 10 kwa taasisi mbalimbali zisizo za Kiserikali kila moja kwa ajili ya kukabiliana na changamoto za kijamii katika hafla iliyofanyika katika Mgodi wa North Mara mwishoni mwa wiki.Fedha hizo ni sehemu ya fedha zilizotolewa na taasisi ya Nos Vies en Partage (NVeP) iliyoanzishwa na inayofadhiliwa na Rais huyo wa Barrick.

Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Barrick, Mark Bristow, akimkabidhi tuzo mfanyakazi bora wa Mgodi wa North Mara,Hassan Marwa katika hafla hiyo.
Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Barrick, Mark Bristow, akimkabidhi ufunguo wa gari Mkuu wa Wilaya Mara, Michael Mtenjele (kulia) lililotolewa na Barrick kwa ajili ya kusaidia ufuatiliaji wa miradi inayotekelezwa kwa fedha za CSR za mgodi wa North Mara katika Halmashauri ya Wilaya hiyo wakati wa hafla hiyo.
Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Barrick,Mark Bristow, akizindua Kamati mpya ya Maendeleo ya Jamii (CDC) ya Halmashauri ya wilaya ya Tarime ambayo kwa sasa Mwenyekiti wake mpya ni Diwani wa Kata ya Matongo, Godfrey Kigoye.
viongozi wa mila kutoka koo zote za kabila la Wakurya wakimpatia Rais na CEO wa Barrick, Mark Bristow, zawadi ya beberu la mbuzi ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wa kampuni hiyo kwa maendeleo ya wananchi wa Tarime.
 ***

Kampuni ya Dhahabu ya Barrick na serikali ya Tanzania zimedhihirisha jinsi uchimbaji madini unavyoweza kuwa na manufaa makubwa pale wachimbaji madini na serikali wenyeji wanaposhirikiana katika kuleta thamani endelevu kwa wadau wote, anasema Rais na Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo Mark Bristow.

Akizungumza na vyombo vya habari mwishoni , Bristow alisema ubia ulioanzishwa na Barrick na Serikali uliyoiunda Kampuni ya Twiga ambamo pande zote mbili zinagawana kwa usawa faida za kiuchumi zinazotokana na migodi ya North Mara na Bulyanhulu, unapaswa kuwa mfano wa kuigwa kwa kuwa ni ubia wenye mafanikio makubwa, hasa katika nchi zinazoendelea. 

Aidha, si tu kwamba Barrick sasa ndiyo mchangiaji mkubwa zaidi katika uchumi wa Tanzania kupitia kodi, mishahara, gawio, malipo kwa wasambazaji wa ndani, na uwekezaji katika miradi ya jamii, bali pia kampuni hiyo imethibitisha kwa makampuni mengine ya kimataifa ya madini kuwa nchini humu kunawekezeka.

Tangu mwaka 2019 ilipoichukua migodi hiyo miwili iliyokuwa imekufa, Barrick imeibadilisha na kuifanya kuwa ya kiwango cha kimataifa na hivyo, kutoa mchango mkubwa katika faida halisi ya kampuni. Aidha, katika kipindi hicho, kampuni hiyo imechangia zaidi ya dola bilioni 3 katika uchumi wa Tanzania, huku mwaka huu Twiga ikitambuliwa kuwa mlipaji mkubwa wa gawio kuliko makampuni yote ambayo serikali ina maslahi nayo. Migodi ya Barrick hutumia asilimia 84 ya bajeti yake ya manunuzi kwa makampuni ya ndani huku asilimia 96 ya nguvukazi yao ikiwa ni wananchi wa Tanzania.

Kwa moyo huo huo wa ushirikiano, Barrick imetoa dola milioni 40 kwenye mpango wa ujenzi wa barabara na dola milioni 30 zaidi katika uboreshaji wa suhula za elimu ya juu nchini.

Migodi yote miwili iko katika mwelekeo mzuri wa kuufikia mwongozo wake wa uzalishaji wa mwaka 2023 na utafutaji wa madini pia. Kwa sasa, utafutaji madini katika maeneo yote ya Barrick yaliyopewa leseni umeonesha fursa mpya za maendeleo katika maeneo hayo, ikiwa ni pamoja na uwezekano wa mgodi mpya wa chini ya ardhi huko North Mara.

“Ubia wetu wa Twiga si tu kwamba unaongeza thamani katika uchumi wa Tanzania bali pia katika ubora wa maisha ya jamii zinazoizunguka migodi yetu na ambayo iaendelea kustawi. Kuendelea kwetu kujihusisha na jamii hizi na viongozi wao wa vijiji, AZISE za maeneo hayo pamoja na mashirika ya haki za binadamu kunaonesha falsafa ya Barrick ya ubia na dhamira yetu ya dhati ya kuzingatia haki za binadamu katika maeneo tunayofanyia kazi,” alisema Bristow.

Bristow pia alikabidhi kwa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime (Vijijini) gari aina ya Toyota Land Cruiser lililotolewa na Barrick kwa ajili ya ufuatiliaji wa miradi ya kijamii inayotekelezwa kutokana na fedha za katika Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) zinazotolewa na Mgodi wa Barrick North Mara. Mgodi wa North Mara kwa sasa unatekeleza miradi zaidi ya 100 ya CSR mkoani Mara.

Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Kanali Michael Mntenjele, alisema gari hilo ni muhimu katika kuhakikisha utekelezaji wa miradi ya CSR kutoka Barrick unaenda vizuri.

Tunashukuru Barrick kwa gari hili, litasaidia wataalamu wetu kufika kwenye miradi kwa wakati na miradi kutekelezeka kwa wakati, ili iweze kunufaisha wananchi wetu,” alisema Kanali Mntenjele.

Mgodi wa Dhahabu wa Barrick North Mara umetumia zaidi ya shilingi bilioni saba kugharimia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kijami kupitia mpango huo wa CSR katika vijiji vyote 88 vya halmashauri ya Wilaya ya Tarime, ambapo asilimia 70 ya kiasi hicho cha fedha kikienda kwenye vijiji vinavyouzunguka.

Katika hafla hiyo, viongozi wa mila kutoka koo zote za kabila la Wakurya walimpatia Rais na CEO wa Barrick, Bristow, zawadi ya beberu la mbuzi ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wa kampuni hiyo kwa maendeleo ya wananchi wa Tarime.

Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI OKTOBA 1,2023

Share:

Saturday, 30 September 2023

MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR ATEMBELEA BANDA LA GGML MAONESHO YA MADINI GEITA

Meneja Mwandamizi wa GGML anayeshughulikia mahusiano ya jamii, Gilbert Mworia akimpatia zawadi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman alipotembelea banda la kampuni hiyo katika Maonesho ya Sita ya Tekonolojia ya Madini Geita. Suleima alikuwa mgeni rasmi katika ufungaji wa maonesho hayo.
Meneja Mwandamizi wa GGML anayeshughulikia mahusiano ya jamii, Gilbert Mworia akimpatia maelezo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman kuhusu shughuli zinazofanywa na kampuni hiyo katika sekta ya madini. Makamu huyo alikuwa mgeni rasmi katika hafla ya kufunga maonesho hayo
Mkurugenzi mtendaji wa GGML, Terry Strong akimshukuru Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman alipotembelea banda la kampuni hiyo katika Maonesho ya Sita ya Tekonolojia ya Madini Geita. Suleima alikuwa mgeni rasmi katika ufungaji wa maonesho hayo.

NA MWANDISHI WETU

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman leo Jumamosi ametembelea banda la Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) katika maonesho ya sita ya teknolojia ya madini Geita na kupata maelezo kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na mgodi huo.

Pia amepata maelezo kuhusu huduma za uchunguzi na elimu ya saratani ya shingo ya kizazi, matiti na tezi dume zinazotolewa na Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Geita kwa ushirikiano wa GGML ambapo hadi jana zaidi watu 1000 wamefanyiwa vipimo.

Akitoa maelezo kwa Makamu Rais huyo wa Zanzibar ambaye ndiye mgeni rasmi anayefunga maonesho hayo yaliyofanyika kwa siku 10, Meneja Mwandamizi wa GGML anayeshughulikia mahusiano ya jamii, Gilbert Mworia alisema kampuni hiyo ndio inayoongoza kwa kuwa muajiri bora nchini.

Pia inaongoza kuwa kuzingatia sheria ya local content Pamoja na kuzingatia masuala ya usalama kazini.

Pamoja na mambo mengine amesema GGML ambaye ni mdhamini mkuu wa maonesho hayo yaliyoanza tarehe 20 Septemba mwaka huu.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa GGML, Terry Strong amemshukuru Makamu huyo wa Rais kwa kutembelea banda hilo na kuahidi kuendelea kushirikiana na serikali katika kutekeleza miradi mbalimbali.

Share:

TPA YAPONGEZWA KUSHIRIKI NA KUDHAMINI MAONESHO YA SITA YA KIMATAIFA YA TEKNOLOJIA YA MADINI MKOANI GEITA.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Prof. Godius Kahyarara ameipongeza TPA kwa kushiriki na kudhamini maonesho ya Sita ya Kimataifa ya Teknolojia ya Madini yaliyofikia tamati leo tarehe 30 Septemba,2023 Katika Viwanja vya EPZ Bombambili Mjini Geita.

Amesisitiza umuhimu wa TPA kufanya Kampeni za Kimasoko ili kupanua Wigo wa biashara na Kampeni za Elimu kwa Umma ili kulinda Taswira ya TPA dhidi upotoshaji unaofifisha umuhimu wa Mamlaka yenye Mchango adhimu kwa Maendeleo ya Uchumi wa Taifa.

Maonesho haya yamefungwa na Makamu wa pili wa Rais Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdullah

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive

Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger