Monday, 7 August 2023
Sunday, 6 August 2023
DKT SIMEO: MICHEZO NI NGUZO MUHIMU YA UTULIVU NA USALAMA KWENYE NCHI
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dkt Japhet Simeo akizungumza wakati alipozindua zoezi la wanachama,wapenzi na mashabiki wa timu ya Simba kuchangia damu katika Zahanati ya Kisosora Jijini Tanga kulia ni Mwenyekiti wa Matawi ya Simba Mkoa wa Tanga Edgar Mdime |
Mwenyekiti wa Matawi ya Simba Tanga Edgar Mdime akizungumza kushoto ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dkt Japhet Simeo |
MKUU wa Idara ya Maabara katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga -Bombo Sinde Mtobu akieleza umuhimu wa uchangiaji damu |
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dkt Japhet Simeo akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kulia ni Mwenyekiti wa Matawi ya Simba Mkoa wa Tanga Edgar Mdime |
Na Oscar Assenga, TANGA.
MGANGA Mkuu wa Mkoa wa Tanga Japhet Simeo leo amezindua zoezi la wanachama,wapenzi na mashabiki wa timu ya Simba kuchangia damu katika Zahanati ya Kisosora Jijini Tanga huku akieleza kwamba michezo ni moja ya nguzo muhimu katika utulivu na usalama kwenye nchi.
Simeo ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba kwenye uzinduzi huo alisema kwamba michezo ina tija sana katika maisha ya binadamu ikiwemo kuwaunganisha jamii na kutengeneza undugu.
Alisema kwamba uchangiaji wa damu ni muhimu ili kuokoa maisha ya wagojwa wahitaji wa damu wakiwemo waluopata ajali, wakina mama wajawazito na watoto waliopo katika hospital mbalimbali mkoani Tanga.
Mganga Mkuu huyo aliwapongeza wanachama hao kwa utayari wao wa kuona umuhimu wa kuchangia damu ambayo itakwenda kusaidia jamii yenye uhitaji huku akizitaka Taasisi, Vikundi na watu binafsi kuendelea kuwa na utamaduni huo ili kuweza kuokoa maisha ya watu wanaofika hospital kupata huduma hiyo.
"Nawapongeza mashabiki wa timu ya Simba SC kwa utayari wenu kuja kuchangia damu mimi nawaambia hii ni sadaka na thawabu kubwa sana mliyoitoa kwa wenzenu wenye uhitaji wa damu " Alisema Simeo.
Awali akizungumza Mwenyekiti wa Matawi ya Klabu ya Simba SC Edgar Mdime alisema kwamba zoezi la uchangiaji wa damu imekuwa ni utaratibu waliojiwekea kila mwaka lengo likiwa kuhakikisha wanakuwa sehemu ya kuokoa maisha ya wahitaji.
Alisema bado wanasukumwa kuchangia damu katika hospitali wakitambua kuwa uhitaji wa damu ni mkubwa kwa wagonjwa wanaohitaji kuongezewa damu hivyo licha ya kushiriki siku hiyo adhimu kwao bado wanaendelea kuhamasishana kujitoa kwa pamoja katika zoezi hilo.
Aidha alisema walianza na zoezi la usafi kubwa zaidi ilikuwa ni kuchangia damu na hamasa kubwa sana ambayo imetokea kwa mkoa huo kwa wana Simba na matawi yote wameungana kwa pamoja kwa ajili ya zoezi hili la kuchangia damu
Hata hivyo alisema kwamba wanajua damu ni muhimu sana kwa kila mmoja hasa ukizingatia wapo wakina mama wanaojifungua katika hospitali ikiwemo ajali zinatokea watu wanahitaji kuwekewa damu kwa hiyo wao wamehamasika kama wanajamii ukiachana na suala la michezo.
Tambo
Katika hatua nyengine, Mdime alituma salamu kwa watani zao timu ya wananchi Yanga kuelekea mechi za Ngao ya jamii zitakazo chezwa Mkwakwani Tanga ambapo ametamba kwa kusema kuwa hawatakuwa tayari ngao hiyo aichukue tena mtani mbele yao.
Mchezo huo unatarajiwa kucheza Agosti 9 mwaka huu katika uwanja wa CCM Mkwakwani Yanga ambao ni mabingwa watetezi wa Ngao ya jamii watakutana na matajiri wa Chamanzi Azam FC huku Simba SC wao wakiminyana na Singida Fountain Gate katika hatua ya nusu fainali timu zote zikitafuta nafasi ya kuanza vyema msimu 2023/2024 .
TBS yatoa elimu kwa wananchi kwenye Maonesho ya Nanenane Mwanza
SUWASA YATAJA MIKAKATI YAKE YA KUIMARISHA UPATIKANAJI WA MAJI
Saturday, 5 August 2023
PESA IPO UKICHEZA MICHEZO YA VIRTUAL NA MERIDIANBET
Michezo ya Virtual safari hii imekuja na bonasi ambayo itatoka siku ya Jumatatu saa 05 asubuhi kwa wale wateja ambao watakuwa wameshinda na kwa wale wateja ambao hawajashinda, watapata rejesho la 15% ya pesa ambayo utakuwa umepoteza kulingana na dau ambalo uliweka.
Ni rahisi kabisa wewe ingia www.meridianbet.co.tz uweke pesa na uanze kucheza michezo mbalimbali ikiwemo ile ya kasino inayopatikana kwenye Virtual kama vile Luck Looty, book of gold, keno na mingine kibao.
Aviator, poker, Roullette, Wild Icy Fruits, Piggy Party na mingine kibao upige pesa na Meridianbet. Ingia www. Meridianbet.co.tz.
Masharti ya Mchezo wa Virtual
❖ Promosheni hii imeanza siku ya Alhamisi tarehe 03 na itaisha hapo kesho tarehe 06 saa 6 usiku hivyo mteja wa Meridianbet kama bado hujaanza kucheza michezo ya Virtual muda ndio sasa.
❖ Promosheni hii itahusisha michezo ya Virtual tuu na sio mingine. Kwahiyo ukishaingia pale Meridianbet chagua michezo ya Virtual na ucheze sasa.
❖ Na wale ambao watakuwa ni washindi watapata bonasi zao siku ya Jumatatu saa 05 asubuhi. Ingia sasa www.meridianbet.co.tz na ucheze Virtual.
❖ Promosheni hii ni kwa wachezaji wote waliojisajili kwenye tovuti na APP ya Meridianbet.co.tz.
❖ Kwa kujisajili na Meridianbet.co.tz, kila mchezaji atakubaliana na sheria za promosheni.
❖ Ofa hii ni halali kwa mtumiaji mmoja, anuani ya IP au kaya.
❖ Meridianbet inahifadhi haki ya kubadilisha sheria za promosheni hii wakati wowote pamoja na kusitisha promosheni hii.
❖ Vigezo na Masharti kuzingatiwa
Baada ya kusoma vigezo na masharti sasa ni wakati wa kukusanya maokoto, weka pesa kwenye akaunti yao ya Meridianbet halafu kucheza ni rahisi tuu kwani utacheza kile ambacho unakipenda.
Pesa inapatikana ndani ya saa chache sana baada ya ushindi kwani pia hauhitaji muda mrefu sana kutumia kwenye kuucheza huu mchezo. Cheza sasa Virtual na Meridianbet ujikusanyie mpunga kabla ya Ligi mbalimbali hazijaanza.
Beti na Meridianbet kwa odds kubwa na machaguo kibao, pia unaweza kubashiri mubashara.
Meridianbet wameamua watoe ofa ya 15% kwa wale ambao watakuwa wamepata hasara ya kile ambacho wamekiweka, vilevile faida ni kupata bonasi siku ya Jumatatu yake baada ya kuwa wikendi umetumia muda wako vizuri kucheza Virtual.
Pia kumbuka kuwa kama ukiwa umeshinda Meridianbet wanakuhaikishia kuwa siku ya Jumatatu saa 5 asubuhi watakuwekea bonasi ambayo nayo pia utaitumia kuchezea michezo mingine uipendayo ndani ya Meridianbet. Kazi ni kwako wewe mteja wa Meridianbet. Muda ndio huu ingia www.meridianbet.co.tz.
NB: Ukijisajili Meridianbet unapewa bonasi ya mizunguko ya bure kucheza michezo ya kasino ya mtandaoni. Jisajili na Cheza.