Thursday, 13 July 2023

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO IJUMAA JULAI 14,2023



























Share:

CASINO STUD POKER INAKUPA UTAJIRI CHAP!



 

Kama unapenda mchezo wa karata basi chimbo jipya la kupigia hela limeongezeka pale Meridianbet kasino ya mtandaoni inakuletea mchezo wa karata wenye umaarufu kwa wadau wa michezo ya kubeti duniani kote. Mchezo huu wa poker ni mchezo utakaokupa utajiri haraka, mchezo wenye sifa ambazo haujawahi kuzisikia.

 

Casino Stud Poker ni mchezo mubashara wa poker uliotengenezwa na waandaji wabobefu wa michezo mbali mbali ya kasino waitwao ‘Playtech‘. Katika mchezo huu wa kasino ya mtandaoni, kombinisheni za ushindi zinatengenezwa pekee kutoka kwenye karata tano za kwanza ambazo zitakuwa mikononi mwako.

 

Casino Stud Poker ni mchezo wa kasino ya mtandaoni unaohusisha mchezaji na muuzaji. Lengo la mchezo ni kuwa na mkono wako imara kuliko wa muuzaji, ikitokea umefanikisha hilo basi ushindi ni wako na utalipwa kulingana na dau lako uliloweka.

 

Unaweza kuweka beti zako kwenye aina mbalimbali za beti, beti kuu kati yao ikiwa ni Ante. Ante ni beti inayohitajika na lazima ipigwe mwanzoni mwa kila mkono.

Unaendelea mchezo kwa kubonyeza kitufe cha Call. Unaweka beti zako muda mrefu kama kuna wakati unaendelea. Baada ya kuonyesha chaguo la No More Bets, hakuna tena wakati wa kuweka beti.

 

Unaweza kuongeza maradufu beti yako na kitufe cha X2, na unaweza kurudia mchezo na kitufe cha Rebet.

 

Baada ya kuweka beti zako kwenye beti ya msingi, unaweza pia kucheza kwenye beti mojawapo kati ya beti mbili za nje: 5+1 na Jakipoti.

 

Mchezeshaji atakupa karata tano na yeye mwenyewe. Karata zako zinaonekana wazi, wakati karata ya mchezeshaji ni wazi na karata zilizobaki zimeinama chini.

 

Hakuna karata za ziada kwenye ubao kama ilivyo katika matoleo mingine ya poker. Ili kushinda unapaswa karata zako mkononi zizidi za mchezeshaji wa mchezo wa kasino ya mtandaoni.

 

Ujaribu mchezo huu pendwa kabisa duniani kote Casino Stud Poker ili kujikusanyia maokoto ya kutosha huku ukiburudika na sauti nzuri za muziki.

 

NB: Ukijisajili Meridianbet unapewa bonasi ya mizunguko ya bure kucheza michezo ya kasino ya mtandaoni. Jisajili na Cheza.


Share:

Tazama Hapa : MATOKEO YA KIDATO CHA SITA (ACSEE) 2023 NA UALIMU 2023

Share:

WAZIRI PROFESA MKENDA ASIFU UBUNIFU UNAOFANYWA NA TAASISI YA TOIO

 



Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda akiendesha moja ya baiskeli ya magurudumu matatu iliyotengenezwa na kubuniwa na Taasisi ya Tanzania Open Innovation Organization (TOIO) wakati wa ziara yake


Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda akiendesha moja ya baiskeli ya magurudumu matatu iliyotengenezwa na  kubuniwa  na Taasisi ya Tanzania Open Innovation Organization (TOIO) wakati wa ziara yake  kushoto ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Tanzania Open Innovation Organization (TOIO) Shaukatali Hussein 

 Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda kushoto akiteta jambo na Mkurugenzi wa Taasisi ya Tanzania Open Innovation Organization (TOIO) Shaukatali Hussein  kulia wakati wa ziara yake

Na Oscar Assenga,Tanga

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda amesifu ubunifu unaofanywa na Taasisi ya Tanzania Open Innovation Organization (TOIO) ya kubuni vifaa mbalimbali vya umeme ikiwemo Baiskeli na Pikipiki huku akihaidi kuunga mkono juhudi hizo.

Profesa Mkenda aliyasema hayo wakati alipoitembelea Taasisi hiyo wakati wa ziara yake ya kutembelea Mradi wa pikipiki za umeme,baiskeli ambazo zinazoziunda wenye shule ya Sekondari Tanga Ufundi.

Akiwa katika eneo hilo Waziri Profesa Mkenda alizitaka taasisi zinazojihusisha na teknolojia na ubunifu kuwasaidia wabunifu nchini kuweza kuzalisha bidhaa zenye ubora.

Alisema kwamba kupitia ubunifu ambao unafanywa na taasisi kama TOIO wanaweza kuona namna ya kupata bajeti ambayo wanaitumia kuweza kuitumia kwa ajili ya kununua hivi vitu ili kuwaunga mkono watanzania ambao wanabuni vitu mbalimbali vyenye manufaa.

“Kupitia bajeti hiyo tutaitumia kununua hivi vitu vinavyotengenezwa hapa kitu kimoja tutangeneza mfumo wa kuvifabrikate kwa scale ya haraka”Alisema

Waziri Mkenda alisema kwamba vipaumbele vyao kwa bajeti iliyopo ya serikali ni kuona namna ya kuwasaidia wabunifu hao kununua hivi vitu tayari na serikali itanunua.

Awali akizungumza Mwakilishi wa Botna Foundation  Dkt Hassan Mshinda alisema wao walipata ufadhii wa kujenga ujuzi huo sio kwa wanafunzi tu bali na jamii ya nje.

Alisema  wanachofikiria ile integration kwenye mafunzo kama hayo ni fursa nyengine nzuri wanaweza kuona namna ya kupatna pamoja

Naye kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya Tanzania Open Innovation Organization (TOIO) Shaukatali Hussein alisema  wamekuwa wakitoa ujuzi jinsi ya kutengeneza na kurekebisha vifaa mbalimbali ikiwemo pikipiki za umeme na baiskeli nia ikiwa na ya kuwa mjasiriamali anaweza kutengeneza pia

Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI JULAI 13,2023


 

Share:

Wednesday, 12 July 2023

MBUNGE MTATURU MGUU KWA MGUU JIMBONI



Na Mwandishi Wetu

MBUNGE wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu ameanza ziara yake katika Kijiji cha Nkuhi kwa lengo la kurudisha mrejesho baada ya kumalizika kwa Mkutano wa 11,wa Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara Kijijini hapo Mtaturu amesema Rais Samia Suluhu Hassan amepeleka Shilingi Milioni 544 kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya ya sekondari.

“Ahsante sana wananchi wenzangu wa Kijiji hiki kwa mapokezi yenu na kuupokea mradi wa ujenzi wa sekondari,tunamshukuru Rais Samia kwa kutuletea kiasi hiki cha fedha kwa ajili ya ujenzi wa shule hii mpya,niwaombe wananchi wenzangu tuunge mkono jitihada hizi na kamwe tusimuangushe,”amesema.

Kwa upande wake diwani wa kata ya Issuna Stephano Missai amemshukuru Mbunge kwa kuwasemea na hatimaye Nkuhi wanaenda kupata shule mpya ya sekondari itakayoondoa changamoto ya watoto kutembea umbali wa zaidi ya km 13 kufuata shule.

"Mh Mbunge ahsante sana,hatua hii sio tu itawaondolea adha watoto wetu ya kutembea umbali mrefu,pia itaondoa utoro na mimba zisizotarajiwa kwa watoto wa kike,hapa tumetenga eneo lenye hekta 100 kwa ajili ya ujenzi huu na wananchi wameanza kusafisha na wapo tayari kutoa nguvu zao ili ujenzi ukamilike mapema,"ameeleza.

Nae Afisa Elimu wilaya Mwalimu Ngwano Ngwano amemshukuru mbunge kwa kuendelea kuibeba sekta ya elimu muda wote.

"Tulishajengewa shule mpya MosiMatongo na madarasa mengi kila shule,na hivi karibuni tumepokea Mil 110 ya kujenga nyumba 2 za walimu shule ya sekondari MosiMatongo,"amesema.

Amesema baada ya mapokezi ya fedha kwa ajili ya shule hiyo mpya Nkuhi halmashauri imetoa maelekezo tayari kuunda kamati za ujenzi na wataalam wa idara ya Elimu,Ardhi na Ujenzi wapo tayari kushirikiana na kamati zilizoundwa hapo kijijni ili kuwe na uwazi kwenye utekelezaji wa mradi huo lengo likiwa ifikapo October 30 mwaka huu ujenzi uwe umekamilika tayari kuanza shule rasmi.
Share:

KILA MWANAUME ALINIKIMBIA KISA SURA YANGU ILA SASA WANANITAMANI!

Urembo huwa jambo la muhimu kwa kila mwanamke hasa pale anapotafuta mwanaume wa kuanzisha naye uhusiano, wanaume wengi hupenda mwanamke ambaye kando na tabia nzuri, basi ana mvuto wa sura na shepu yake.

Hiyo ilikuwa ni changamoto kwangu kwa kuwa uso wangu ulikuwa na vidonda vidogo vidogo ambavyo vilikuwa ni tishio katika urembo wangu.


Kila mwanaume niliyekutana naye alisema kuwa vidonda vile vilinifanya kuonekana mwenye sura mbaya isiyovutia kabisa, nilikuwa na kazi nzuri na kipato kizuri lakini suala moja tu ndilo lilinikosesha usingizi nalo ni sura yangu kutovutia.


Marafiki zangu wote walikuwa wamepata wachumba wakati mimi nilikuwa bado nasumbuliwa na vidonda usoni, baadaye vidonda vile vilianza kutoa usaa ambao ulikuwa na harufu mbaya jambo lililopelekea kubakia mwenye upweke muda wote.

Nilijaribu kutumia dawa mbalimbali kutibu ugonjwa huo lakini sikufanikiwa, nilitembea karibu kila sehemu ya nchi kutafuta dawa lakini juhudi zote zilikuwa ni sawa usiku wa giza.


Nakumbuka Eunice ambaye alikuwa rafiki yangu wa siku nyingi alikuja nyumbani na kuniambia kwamba aliwahi kuwatembelea African Doctors na walimpatia mafuta ambayo yalimsaidia kumaliza uvimbe kwenye uso wake.

Alinielekeza kwenye tovuti wao, www.african-doctors.com kuwa naweza kufahamu zaidi kuhusu wao, usiku wake nilitembelea tovuti ile na ndipo nikapata na namba zao ambazo ni +254 769 404965 na kuwasiliana nao mara moja.

Nilifika ofisini kwao kwa ajili ya tiba, alinipa vipodozi fulani mithili ya mafuta, aliniambia nianze kuyapaka muda ule ule na hapo nikanza kuhisi kama uso wangu unayeyuka.

Nilirejea nyumbani na kila siku nilikuwa nikiendeleza kupaka mafuta yale kwenye uso wangu kwani nilikuwa na imani kuwa ngozi yangu ingerudi kama kawaida na kunipa mvuto wa aina yake, nashukuru baada ya siku tatu za kuyapaka mafuta yale, ngozi yangu ilikuwa imebadilika ajabu.

Sura yangu ilikuwa yenye mvuto kweli, ngozi ilikuwa imegeuka kuwa nyororo kabisa, makovu yaliyotokana na uvimbe ule yote yalikuwa yamekwisha.

Tangu siku ile makovu na vidonda vidogo vidogo havijawahi kurejea tena kwenye mwili wangu, baadaye nilirejea kazini, nilipata mchumba na kuanza maisha ya ndoa bila ya shida yoyote hadi wakati huu.

African Doctors  ana uwezo wa kusuluhisha migogoro ya ndoa, kukukinga na maadui zako, pia anatibu magonjwa kama vile kifafa na kisonono kwa siku tatu pekee.

Wasiliana na African Doctors kwa namba; +254 769 404965, tembelea tovuti yao; www.african-doctors.com au watumie email; africandoctorheals@gmail.com.

Mwisho.

 

Share:

SLOTI YA KEOPS WILD NI KAMA MISRI YA FARAO TU!!

Fahamu mengi kuhusu siri za Misri ya kale unapocheza sloti ya Keops Wild kutoka kwa watengenezaji wa michezo ya kasino Spearhead


Katika mchezo huu wa kasino ya mtandaoni, utaona kaburi la Farao, ambalo linaficha siri nyingi, na utajiri wa kumwaga. Ukiwa na mchezo huu unaanza safari ya kuelekea nchi ya ajabu na yenye utajiri sana kupitia.

 

Meridianbet mabingwa wa odds kubwa, bonasi kibao, michezo ya sloti ikiwemo hii ya Keops Wild, na kasino ya mtandaoni imekuwa sehemu pekee ya wachezaji wengi kutengeneza pesa kirahisi.

 

Mipangilio ya sloti ya Keops Wild ipo kwenye safuwima sita katika safu ulalo nne za alama na mistari 40 ya malipo. Kinadharia, sloti hii ina RTP ya 96.04% maana yake ni kwamba inalipa kwa 96.04%, na zawadi yake kuu ni ya thamani mara 7,000 ya dau lako.

 

Sloti zenye mandhari ya Misri ni maarufu sana kwa wachezaji wa michezo ya kasino ya mtandaoni, kwa sababu ya mandhari ya kuvutia na bonasi kubwa inayotoa, pia kuna mizunguko ya bure kucheza kasino ya mtandaoni.

 

Sloti ya Keops Wild ina alama maalum kama vile farao, ambayo ni ishara ya wilds. Piramidi ni ishara ya kutawanya ambayo inatoa mizunguko ya bure.

Mizunguko ya bure ya bonasi huwashwa wakati alama tatu au zaidi za kutawanya zinapoonekana kwenye safuwima kwa wakati mmoja. Alama tano za kutawanya zinaweza kukulipa mara 25 ya dau na kukamilisha utendaji kazi wa bonasi.

Kati ya alama nyingine, utamuona malkia, huenda akawa ni Cleopatra, Anubius, jiwe la bluu, fimbo na kile tunachodhani kuwa ni taji. Sambamba na alama hizi, pia kuna alama za karata ambazo zina thamani ya chini.

 

Upande wa kulia wa sloti hii kuna jopo la kudhibiti na chaguzi zote muhimu kwa ajili ya mchezo huu wa kasino ya mtandaoni. Kubofya kitufe cha Dau +/- hufungua menyu ambapo unaweza kuchagua ukubwa wa mizunguko yako.

 

Kitendaji cha Kucheza Moja kwa Moja (Automatic) kinapatikana pia, ambacho unaweza kukiwezesha wakati wowote. Unaweza kuweka hadi mizunguko 100 kupitia chaguo hili la kukokotoa. Unaweza pia kuweka kikomo kwenye ushindi na hasara zako pindi uchezapo sloti hii kwenye kasino ya mtandaoni ya Meridianbet.

 

NB: Ukijisajili Meridianbet unapewa bonasi ya mizunguko ya bure kucheza michezo ya kasino ya mtandaoni. Jisajili na Cheza.


Share:

SERIKALI YATENGA BILIONI 54 KWA AJILI YA UJENZI WA VYUO VYA UFUNDI STADI VETA 65 NCHINI.

 

Waziri wa Elimu Sayansi na Teklonojia Profesa Adolf Mkenda

Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Elimu, Mafunzo ya Ufundi Stadi Veta Anthon Mzee Kasore



Na Mwandishi Wetu, Tanga

SERIKALI imesema inaendelea na ujenzi wa vyuo 65 vya ufundi stadi Veta utakaogharimu kiasi cha shilingi bilioni 54 katika Mikoa na Wilaya hapa nchini, ikiwa ni mkakati wa kuhakikisha inatoa elimu ya Amali itakayokidhi matakwa ya mabadiliko ya sera ya elimu. 

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teklonojia Profesa Adolf Mkenda alisema hayo  alipotembelea chuo cha ufundi stadi Veta Jijini Tanga ili kujionea namna kinavyotoa mafunzo ya Ufundi Stadi lakini pia kuhakikisha wanatoa huduma zinazostahiki kwa jamii. 

Waziri Mkenda amesema kuwa kati ya vyuo 65 vinavyojengwa Nchini, Vyuo 64 ni za Wilaya na Chuo Kimoja cha Mkoa ambapo hadi sasa tayari imetoa kiasi cha shilingi bilioni 37 huku matumaini yakiwa makubwa katika kila maeneo yanayojengwa vyuo hivyo ambavyo ni mkakati wa serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan. 

"Tukiwa bungeni swali kubwa ambalo limekuwa likiulizwa mara nyingi kuliko maswali mengine yote katika wizara ya elimu sayansi na teknolojia ni kuhusu veta kila mmoja anauliza ni lini veta itajengwa kwake watu wanamatarajio makubwa sana kwenye veta kwa maana hiyo sisi tuna kazi ya kuhakikisha tunakidhi matarajio yao kwa kutoa elimu ya amali ambayo ni bora na ambayo itakidhi matakwa ya vijana, "alisema Waziri Mkenda. 

Prof Mkenda amesema zipo namna mbili za kuendelea kuwapima wahitimu wa Mafunzo ya Ufundi Stadi Veta ambapo moja ya njia ni kuangalia wahitimu wanafanya wapi kazi mara baada ya kuhitimu mafunzo yao na kuwahoji waliowaajiri namna walivyoridhika na utendaji kazi wao. 

Pia Waziri Profesa Mkenda aliwaagiza viongozi wa Veta kuhakikisha wanaandaa bajeti na kuiwasilisha wizarani itakayoomba fedha kwa ajili ya kununulia zana bora zinazokidhi teklonojia ya sasa katika karakana za Ufundi wa magari ili vyuo hivyo vya Veta viweze kuingia sokoni kutengeneza magari ya serikali, mashirika na watu binafsi.

Mkurugenzi wa Veta kanda ya Kaskazini Monica Mbele, alisema wamepokea maagizo hayo ambayo pindi wakipata nyenzo na zana bora za kisasa wataweza kuwa na utayari wa kutengeneza magari lakini pia kuongeza walimu wenye ujuzi wa teklonojia ya kisasa.

Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi VETA Antony Mzee Kasore alisema watahakikisha wanakwenda kutekeleza maagizo ya Waziri ya utoaji wa mafunzo bora na kuhakikisha wanatoa mafunzo yanayohitajika na yanayozingatia ubora unahitajika. 

"Kama tulivyosikia kuna vyuo vinavyojengwa 65 katika wilaya mbalimbali na Mkoa na chenyewe pia tunakwenda kusimamia kama maelekezo aliyotoa ya kuhakikisha tunasimamia ujenzi huo uweze kufanyika tukiamini tutakuwa tumekwenda kutekeleza yale yote yaliyoanishwa, "alisema 

Share:

WAPIGA KURA 74,642 KUPIGA KURA KUCHAGUA MADIWANI KESHO


Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi
Jaji wa Rufaa Jacobs Mwambegele
********
Na Mwandishi Maalum - NEC
Wapiga Kura 74,642 walioandikishwa katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura wanatarajiwa kushiriki katika uchaguzi mdogo wa madiwani katika kata 13 za Tanzania Bara kesho Julai 13,2023.

Jumla ya wapiga kura 74,642 walioandikishwa kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura wanatarajiwa kushiriki katika uchaguzi huu mdogo na jumla ya vituo 205 vya kupigia kura vitatumika.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji wa Rufaa Jacobs Mwambegele katika Risala ya Uchaguzi huo mdogo unaofanyika kujaza nafasi wazi za udiwani.

Jaji wa Rufaa Mwambelegele amewataka wasimamizi wa uchaguzi, vyama vya siasa na wagombea kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za uchaguzi wakati wa Uchaguzi Mdogo wa madiwani katika Kata 13 za Tanzania Bara.

Uchaguzi huo mdogo utashirikisha, Kata ya Ngoywa katika Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Kata ya Kalola katika Halmashauri ya Wilaya ya Uyui mkoani Tabora na za Sindeni katika Halmashauri ya Wilaya ya Handeni, Potwe katika Halmashauri ya Wilaya ya Muheza, Kwashemshi katika Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe na Bosha katika Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga zote za Mkoa wa Tanga.

Kata nyingine ni Mahege katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti mkoa wa Pwani, Kata ya Bunamhala katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi, mkoa wa Simiyu, Kata ya Njoro na Kalemawe zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro, Kata ya Kinyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Makete mkoa wa Njombe , Kata ya Magubike katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa mkoa wa Morogoro na Kata ya Mbede katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe mkoa wa Katavi.

Aidha, amevitaka vyama vya siasa, wagombea na wadau wa uchaguzi kuepuka kujihusisha na matukio yenye viashiria vya uvunjifu wa amani kwani jukumu la kulinda amani ni la kila mmoja, hivyo wahakikishe wanalinda amani iliyopo nchini.

“Jukumu la kulinda amani ya nchi yetu ni la kila mmoja wetu wakiwemo wananchi, vyama vya siasa, wagombea na wadau wengine wa uchaguzi,”alisema Jaji wa Rufaa Mwambegele.

Aliongeza kuwa Sheria na Kanuni za Uchaguzi zimeweka mamlaka na taratibu zinazotakiwa kufuatwa iwapo kutakuwepo na malalamiko yoyote wakati wa uchaguzi, hivyo amevitaka vyama vya siasa na wagombea kufuata taratibu hizo ili uchaguzi huo ufanyike kwa uhuru na haki.

Mweyekiti huyo wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi amewataka wapiga kura wote waliojiandikisha katika Kata 13 za Tanzania Bara kujitokeza kupiga kura ili waweze kuwachagua madiwani wanaowataka.

Amevitaka vyama vya siasa wagombea na wafuasi wao kuzingatia kuwa kampeni za uchaguzi zinakamilika leo Julai 12,2023 saa 12:00 jioni hivyo hawaruhusiwi kufanya mikutano ya kampeni kuanzia muda huo na hawaruhusiwi kutumia alama za vyama zinazoashiria kampeni kama vile vipeperushi, bendera na mavazi.

Aidha Jaji Rufaa Mwambegele amevikumbusha vyama vya Siasa vinavyoshiriki katika uchaguzi huo, kuzingatia wajibu wao wa kuweka mawakala katika vituo vyote vya kupigia, kuhesabu na kujumlishia kura.

“Upigaji kura utafanyika katika vituo vile vile vilivyotumika wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020. Vituo vya kupigia kura vitafunguliwa saa 1:00 asubuhi na kufungwa saa 10:00 jioni. Iwapo watakuwepo wapiga kura katika mstari ambao walifika kabla ya saa 10:00 jioni na hawajapiga kura, wataruhusiwa kupiga kura, mtu yeyote hataruhusiwa kujiunga katika mstari wa wapiga kura baada ya saa 10:00 jioni”alisema Jaji Rufaa Mwambegele.

Aliongeza “Tume kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 62(1) cha Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Sura 292, imeruhusu wapiga kura ambao wamepoteza kadi zao au kadi kuharibika kutumia vitambulisho mbadala”.

Amevitaja vitambulisho mbadala kuwa ni Passi ya Kusafiria, Leseni ya Udereva au Kitambulisho cha Uraia kinachotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).

Mpiga kura aliyepoteza kadi au kadi yake kuharibika ataruhusiwa kutumia kitambulisho mbadala iwapo tu atakuwa ameandikishwa kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na jina lake lipo kwenye orodha ya wapiga kura kwenye kituo anachopigia kura.

Mwambegele amekumbusha kuwa katika vituo vya kupigia kura kipaumbele kitatolewa kwa wagonjwa, watu wenye ulemavu, wazee, wajawazito na akina mama wanaonyonyesha watakaokuwa na watoto vituoni na kutakuwa na majalada ya nukta nundu katika vituo vya kupigia kura kwa ajili ya watu wenye ulemavu wa kuona ili weweze kupiga kura wenyewe. Alifafanua kuwa kwa wapiga kura wenye ulemavu wa kuona ambao hawawezi kutumia majalada hayo wanaruhusiwa kwenda vituoni na watu watakaowachagua wenyewe kwa ajili ya kuwasaidia kupiga kura.

Jumla ya vyama vya siasa 17 vimesimamisha wagombea katika uchaguzi huo mdogo ambapo Tume imevipongeza vyama hivyo na wagombea wao kwa kutumia haki yao ya msingi ya kikatiba kujitokeza kushiriki katika uchaguzi huo mdogo wa Udiwani.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger