Monday, 10 July 2023

KAMA UNATAFUTA KAZI FANYA HIVI UTAFANIKIWA NDANI MUDA MFUPI!

 
Ni mwaka wa nne sasa tangu nimehitimu masomo yangu ya Chuo Kikuu, nimetafuta kazi na kufanya interview nyingi sana bila mafanikio hali ambayo inaniumiza sana kutokana kuna wadogo zangu wananitegemea sana kwa sababu mimi ndiye kijana pekee katika familia yetu.

Pia mimi ndiye mtoto wa kwanza, hivyo hata wazazi wangu wenyewe wanategemea mengi kutoka kwangu na msaada kwa wadogo zangu ili waweze kufika nilipofika.


Wazazi wangu ni wakulima ila wameangaika sana kunisomesha kuanzia elimu ya msingi hadi kumaliza masomo ya elimu ya juu, jinsi wazazi wangu walivyokuwa wanahangaika kupata ada ya kunisomesha nilikuwa nawaonea huruma sana na kujiwekea ahadi moyoni mwangu kuwa nikimaliza masomo nitahakikisha nawafuta machozi.


Sikuweza kuwaangusha wazazi wangu hata siku moja katika masomo yangu nilijitahidi kadiri niwezavyo kufanya vizuri katika mitihani yangu na mara kwa mara nilikuwa napata nafasi ya kwanza katika matokeo ya mitihani tangu nikiwa elimu ya msingi hadi Chuo Kikuu nilipopata GPA ya 4.5.


Kitendo cha kufanya vizuri shule kilifanya wazazi wangu kuwa na imani kuwa nikimaliza kusoma maisha nyumbani yatabadilika kwa sababu nitapata kazi kumbe mawazo hayo yalikuwa ni kama ndoto ya mchana.

Kila nilipoenda kuomba kazi  walivyokuwa wakitazama CV yangu tangu elimu ya msingi hadi Chuo Kikuu, kisha kupewa siku maalamu ya kufanya interview, lakini kila baada ya interview nilikuwa naambiwa niache namba ya simu kuwa nitapigiwa lakini haikuwa hivyo!.


Nilivyokuwa nawasiliana na marafiki zangu ambao nimesoma nao wengi wao walikuwa wana kazi na wengine wanafanya biashara tofauti tofauti ila mimi sikuwa na chochote muda huo maana nilikuwa sina kazi, pia siwezi kufanya biashara kwa sababu nilikuwa sina sehemu yoyote ambayo naweza kupata mtaji, hivyo sikuwa na chaguo lingine zaidi ya kutafuta kazi ya kuajiriwa tu.


Marafiki zangu wengi walikuwa wanashangaa nikiwaambia kuwa sijapata kazi wala sina kitu ambacho najishughulisha nacho, ila kushagaa kwao mimi sikuweza wafikiria vibaya kwa sababu nilitambua wanashangaa kutokana na jinsi walivyokuwa wananijua Chuo hata sifa ambazo nilikuwa napata kutoka kwa walimu.

Siku moja nilinunua Gazeti kwa ajili ya kuona wapi wanahitaji wafanyakazi, katika kupitia pitia lile Gazeti nilikutana na tangazo kuhusu African Doctors, miongoni mwa huduma ambazo wanatoa ni pamoja na kuwasaidia watu kupata kazi na kupandishwa cheo au madaraja kazini.


Sikuwa na chaguo lolote zaidi ya kuchukua namba yao na kuwasiliana na African Doctors ili nione kama nitaweza kupata msaada, basi nilipiga simu, ilipokelewa kisha nikaanza kujieleza kuhusu maisha yangu na kuomba wanisaidie nipate kazi, basi walinipatia maelezo jinsi ambavyo nitaweza kupata usaidizi.

Nilifuata maelekezo yake kisha nikaambiwa nisubiri ndani ya saa 48 nitapokea simu kutoka sehemu ambazo nimewahi kuomba kazi, basi ndani ya muda nilipigiwa simu na shiriki la serikari na kuambiwa nikaanze kazi mara moja. Hadi sasa hivi nina kazi nzuri, wadogo zangu wanasoma shule nzuri pamoja na wazazi wangu nimewajengea kwa muda mfupi tu.

Wasiliana na African Doctors kwa namba; +254 769 404965, tembelea tovuti yao; www.african-doctors.com au watumie email; africandoctorheals@gmail.com.

Share:

MAAGIZO YA RAIS SAMIA YASHUSHA BEI YA MAFUTA TANZANIA

* Kenya bei ya mafuta yazidi kupaa, wenye magari wavuka mpaka hadi Tanzania kuweka mafuta

* Maagizo ya Rais Samia ya usimamizi wa uingizaji mafuta nchini na ruzuku yaleta ahueni kwa Watanzania


Mwandishi Wetu Dar es salaam

MAAGIZO ya Rais Samia Suluhu Hassan yamesaidia kushusha bei ya mafuta ya petroli na dizeli nchini kwa mwezi wa pili mfululizo, huku nchi jirani ya Kenya wakilia na ukali wa maisha unaotokana na kupanda kwa bei ya mafuta.


Baadhi ya wamiliki wa magari kutoka Kenya wameamua kuvuka mipaka hadi Tanzania ili kuweka petroli na dizeli kwenye vituo vya mafuta vya nchini Tanzania, ambavyo huuza mafuta kwa bei ya chini kuliko Kenya.


Takwimu za EWURA zinaonesha kuwa kwa mkoa wa Dar es Salaam, bei ya kikomo ya petroli mwezi wa Julai imeshuka kwa Shilingi 137 kwa lita hadi kufikia Shilingi 2,736, wakati bei ya dizeli imeshuka kwa Shilingi 118 kwa lita hadi kufikia Shilingi 2,544.


Kwa sarafu ya Kenya, bei ya mafuta Tanzania ni sawa na Shilingi za Kenya, Ksh 147.96 kwa lita ya dizeli, na Shilingi za Kenya Ksh 159.13 kwa lita ya petroli.


Wakati kwa upande wa nchini Kenya, bei halisi ya petroli ni Shilingi za Kenya Ksh195.53 kwa lita wakati bei ya dizeli ni Shilingi za Kenya Ksh179.67 kwa lita.


"Madereva wa magari wengi wa Kenya wanavuka mipaka ya Namanga na Sirari na kuja Tanzania kuweka mafuta ya petroli na dizeli kwenye vituo vya mafuta vya Tanzania kwa ajili ya unafuu wa bei," Aloyce Mushi, mfanyabiashara wa mafuta wa Arusha alisema.

Ahueni ya bei ya mafuta nchini Tanzania imetokana na maagizo mahsusi ya Rais Samia kuwa serikali yake ichukue hatua za kupunguza kupanda kwa gharama ya maisha nchini.


Rais Samia aliagiza kuwa serikali itoe ruzuku ya Shilingi Bilioni 100 kwenye bei ya mafuta kila mwezi ili kudhibiti kupanda kwa bei za petroli, dizeli na mafuta ya taa nchini.


Rais Samia aliagiza pia kuwa Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (PBPA) ihakikishe kuwa inadhibiti ushindani wa makampuni yanayoingiza mafuta nchini kwa lengo la kushusha bei.


Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) nalo limeingia kwenye biashara ya kuagiza mafuta kwa pamoja ili kuleta ushindani kwa kampuni binafsi na kuhakikisha bei ya mafuta inashuka nchini.


Ahueni ya bei ya mafuta nchini Tanzania imeleta manufaa kwenye uchumi na pia kushusha gharama za maisha kwa wananchi wa kawaida.


Gharama za usafirishaji wa mizigo mbalimbali, ikiwemo chakula na bidhaa za nyumbani imeweza kudhibitiwa kutokana na bei ya mafuta kushuka.

Mafuta ya petroli na dizeli ni miongoni mwa bidhaa zinazochangia kupandisha au kushusha mfumuko wa bei nchini.


Mfumuko wa bei kwa mwezi Mei 2023 ulishuka hadi kufikia asilimia 4.0 kutoka asilimia 4.3 kwa mwezi Aprili 2023, kwa mujibu wa takwimu za NBS.


Wakati huo huo, bomba la TAZAMA lililojengwa miaka ya 1960 ambalo lilikua linasafirisha mafuta ghafi kutoka Tanzania hadi Zambia, sasa litaanza kusafirisha mafuta ya dizeli kutoka Dar es Salaam hadi Zambia, badala ya mafuta ghafi kama ilivyokua hapo awali. 

Waziri wa Nishati, January Makamba, amesema kuwa baada ya kuanza kusafirisha dizeli kwenye bomba la mafuta, hali ya usalama na mahitaji ya usalama ya bomba hilo yameongezeka sababu ni rahisi watu kushawishika kutoboa bomba hilo na kuchukua dizeli.


"Tumeshafanya mkutano wa kwanza mwaka jana na tuliweka makubaliano ya kuweza kulilinda bomba hili lenye urefu wa kilomita 1,710 kutoka Kigamboni, Dar es salaam, hadi Indeni-Ndola, Zambia,” alisema.

Makamba alisema kuwa bomba hili limejengwa muda mrefu na lina kipenyo chembamba, wakati biashara ya mafuta imekua na mahitaji ya mafuta yamekua makubwa zaidi.

Alisema kuna haja ya kujenga bomba pana na jipya litakalosafirisha pia bidhaa nyingine zaidi ya dizeli. Serikali zote mbili zimekua zikiongea kuhusu biashara hii ya mafuta na pia ujenzi wa bomba jipya la gesi ili kuiuzia Zambia gesi.


“Haya ni mashirikiano mazuri kati ya nchi zetu hizi na pia ni mwendelezo wa mahusiano mema unaofanywa na viongozi wetu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mhe. Hakainde Hichilema, Rais wa Jamhuri ya Zambia, kama yalivyoasisiwa na Viongozi wetu wa kwanza Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius K. Nyerere na hayati Kenneth Kaunda.”

Share:

Sunday, 9 July 2023

WADAU WAKARIBISHWA KUPATA TAARIFA NAMNA YA KUSHIRIKI JUKWAA LA KIMATAIFA SEKTA YA MADINI MWEZI OKTOBA 2023


Wananchi na wadau wanaotembelea maonesho ya Sabasaba wamekaribishwa kupata taarifa kuhusu namna ya kushiriki katika Jukwaa la Kimataifa la Sekta ya Madini kwa kujisajili katika tovuti maalum ya mkutano.

Mratibu wa Jukwaa la Mkutano wa Kimataifa kutoka Wizara ya Madini Bi. Jacqueline Aloyce  amesema kuwa , jukwaa hilo linatarajiwa kuwakutanisha wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi Oktoba 25 na 26 jijini Dar es salaam.

Amezungumza hayo leo Julai 9, 2023 na kuongeza jukwa hilo litakuwa fursa kwa wenye nia ya kushiriki katika uchumi wa madini, kujifunza, kusikia na kukutana na wadau mbalimbali wa Sekta ya Madini wanaotembelea banda la Wizara ya Madini katika Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) Dar es salaam.

Ameongeza kuwa, jukwaa hilo ni fursa kwa wote walio katika mnyororo  mzima wa shughuli za madini kuanzia wachimbaji wadogo, wa Kati na Wakubwa wa Sekta ya Madini ili kuzungumza kwa pamoja fursa mbalimbali zilizopo katika Sekta ya Madini.

Ameongeza kuwa, ili kushiriki katika jukwaa hilo muhimu wadau wote wajisajili katika tovuti ya mkutano huo https://www.tanzaniamininginvestmentforum.com

Kwa nwaka 2023, Jukwaa la Kimataifa Sekta ya Madini inashirikiana na Kampuni ya DMG events na Ocean Business Partners (OBP) katika kuandaa jukwaa  la Kimataifa kwenye Sekta ya Madini hapa nchini.
Share:

NIMESHINDWA KUMSAHAU MWANAUME WANGU WA KWANZA

Nalinganisha penzi na bustani ambayo huhitaji kumwagiliwa maji mengi na isipopata maji ya kutosha uweza kufifia na hatimaye kufa, hivyo penzi linaitaji maji ya mahaba kila siku liweza kushamiri.


Jina langu Maria, mkazi wa Kinondoni, nilianza kujihusisha na mapenzi nikiwa na umri wa miaka 20 na Boyfriend wangu wa kwanza anaitwa Baraka japo mimi nilimuita jina la Mwalimu kwa sababu yeye ndo aliyenifundisha kila kitu kuhusu mapenzi.

Siku yangu ya kwanza kujihusisha na tendo la ndoa niliumia sana hadi nilipotoka pale nikamchukia Mwalimu na kaapa sitokuja kulala na Mwanaume tena kutokana na uchungu niliopata pale Mwalimu alipokuwa kifuani mwangu.


Ila baada ya siku kadhaa nilishindwa kuvumilia haswa nilipokuwa nakumbuka maneno ya Mwalimu aliyokuwa ananiambia kipindi yupo kifuani mwangu. Mimi mwenyewe nilichukua simu yangu na kumwambia kuwa tuendelee kupendana kama zamani ila hatutashuriki tendo la ndoa tena.

Mwalimu alikubali, tukaanza tena kukutana sehemu mbalimbali na jinsi tulivyokuwa tunakutana nilijikuta nahitaji kushiriki tendo la ndoa kusikia itakuwaje.


Tulipanga siku ya kukutana tena kwa ajili ya kufanya tendo, tulipokutana na kufanya maumivu yalikuwa tofauti sana na siku ya kwanza, hatimaye siku zilivyokuwa zinasonga nikajikuta sasa mimi mwenyewe nahitaji kufanya kabla ya Mwalimu kuniomba kutokana na utamu ambao nilikuwa napata kama mtoto wa kike.


Baada ya miaka tatu tukiwa kwenye mahusiano Mwalimu alianza kubadilika na kuwa tofauti kabisa na jinsi nilivyokuwa nimemzoea, nilisikia Mwalimu ana msichana mwingine anaitwa Judith ndiye anatembea naye.

Hizo habari zilivuruga kichwa changu na kunifanya nichukie wanaume wote duniani na kuwaona ni watu ambao hawajali hisia za mtu haswa katika suala la mapenzi.


Nilivumilia ile hali kisha kuamua kuendelea na maisha yangu, baada ya miezi sita nikaamua kuingia tena katika mahusiano na kijana anaitwa Aivan.

Aivan alinipenda sana ila kila nikiwa naye nilikuwa namfikiria Mwalimu tu hata tukiwa kitandani najikuta nataja jina la Mwalimu, mwisho wake Aivan akaniacha akidhani kuna mtu nalala nae asipokuwepo.

Moyo wangu hukuweza kutulia ikabidi nitafute usaidizi ndipo rafiki yangu wa karibu akaniambia kuwa African Doctors, ana uwezo wa kumfanya Mwalimu turudi kwangu kwa muda wa masaa 48 kutokana na sifa ambazo amezisikia kuhusu African Doctors.

Pia akaniambia kuwa African Doctors wamemsaidia Mama Mdogo wake kupata mwanaume baada ya kukaa kwao kwa miaka kadhaa bila kuolewa.

Nilianza kutafuta mawasiliano ya African Doctors hatimaye nikapata website yao, www.african-doctors.com, kisha nikapata na namba yao ya simu +254 769 404965. Kisha niliwasiliana na African Doctors na kuomba kupata usaidizi wake maana moyo wangu umeshindwa kabisa kumsahau Mwalimu.


Katika mazungumzo nilimwambia kuwa sina uwezo wa kufika mahali alipo ila mimi nahitaji msaada wake kwa sababu sipo tayari kumuona Mwalimu anaoa mwanamke mwingine zaidi yangu.

African Doctors alinipatia mawaidha kisha akaniuliza maswali machache kuhusu Mwalimu na hatimaye akaniambia nisubiri kwa muda wa masaa 48 Mwalimu atanitafuta. Maneno ya African Doctors  yalinipa moyo hatimaye Mwalimu mwenyewe alinipigia simu na kuniambia kuwa amenikosea ila anahitaji tuwe kama tulivyo kuwa mwanzo, nilimsamehe na kwa sasa tunaishi wote kama Mume na Mke.

African Doctors  wana dawa za kukuwezesha kupandishwa cheo kazini, dawa ya kupata kazi, dawa za nguvu za kiume na dawa ya kusafirisha nyota yako.

Wasiliana na African Doctors kwa namba; +254 769 404965, tembelea tovuti yao; www.african-doctors.com au watumie email; africandoctorheals@gmail.com.

Mwisho.


Share:

MWENYEKITI JUMUIYA YA WAZAZI TANGA ATAKA JUMUIYA KUWA NA MAONO YA MAENDELEO NA KIUCHUMI

 

MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Tanga Alhaj Hasani Ramadhani Mbezi  akifungua Kikao cha Baraza la Wazazi la Chama cha Mapinduzi wilaya ya Tanga kilichoketi kupokea Taarifa ya kazi kwa kipindi cha miezi Sita kuanzia Januari mpaka June 2023.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM wilaya ya Tanga Hamza Bwanga  akifuatilia kwa umakini Hotuba ya Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Mkoa wa Tanga 
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM wilaya ya Tanga Hamza Bwanga akizungumza wakati wa ziara hiyo
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM wilaya ya Tanga Hamza Bwanga kulia akigawa daftari la wanachama wapya kwa mmoja wa viongozi wa Jumuiya hiyo ngazi ya Kata wakati wa  Kikao cha Baraza la Wazazi la Chama cha Mapinduzi wilaya ya Tanga kilichoketi kupokea Taarifa ya kazi kwa kipindi cha miezi Sita kuanzia Januari mpaka June 2023.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM wilaya ya Tanga Hamza Bwanga kulia akigawa daftari la wanachama wapya kwa Mwenyekiti wa  Jumuiya hiyo Kata ya Ngamiani Kusini Amour Kasim Salum  wakati wa  Kikao cha Baraza la Wazazi la Chama cha Mapinduzi wilaya ya Tanga kilichoketi kupokea Taarifa ya kazi kwa kipindi cha miezi Sita kuanzia Januari mpaka June 2023.


Sehemu ya Washiriki wa Mkutano huo
Sehemu ya washiriki wa kikao hicho



Na Oscar Assenga,Tanga


MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Tanga Alhaj Hasani Ramadhani Mbezi ameshauri na kuelekeza Jumuiya za Wazazi za wilaya za mkoa huo kuhakikisha zinakuwa na maono ya maendeleo na kiuchumi kwa kuanzisha miradi mbalimbali.

Alhaj Mbezi alisema hayo wakati akifungua Kikao cha Baraza la Wazazi la Chama cha Mapinduzi wilaya ya Tanga kilichoketi kupokea Taarifa ya kazi kwa kipindi cha miezi Sita kuanzia Januari mpaka June 2023.

Alisema kwa sababu haiwezekani Jumuiya kuwa ombaomba wakati wanaweza kubuni na kuweka mikakati ya kuanzisha vitega uchumi ambavyo vinaweza kuwa chachu ya kujikwamua kiuchumi.

“Kwa kweli haiwezekani Jumuiya kubwa kama Wazazi kuwa ombaomba wakati tunaweza kufanya mambo yakatusaidia kiunuka kiuchumi hivyo niagize tuanzisheni miradi ya kiuchumi kwani Tanga kuna ardhi kubwa na miradi mingi hasa kilimo cha Mkonge lakini kubuni na kuanzisha Sheli mbalimbali”Alisema Mwenyekiti huyo.

Aidha alisema pia Jumuiya hizo zinaweza kuanzisha viwanda vidogo vidogo kwa mfano vya kufyetua matofali ambayo vitawasaidia sana wazazi Tanga mjini.

Umoja na mshikamano

Alhaj Mbezi alisema umoja na mshikamano ndio mafanikio makubwa katika jambo lolote hivyo wanapaswa kuuimarisha na kusimama kidete ili uchaguzi 2024/2025 kuhakikisha wanachukuia viti vyote kuanzia ngazi ya chini mpaka udiwani.

Alisema watakapofanya hivyo itawapa dira ya kuelekea 2025 kuhakikisha kura zote za mkoa wa Tanga zinakwenda kwa Rais Dkt Samia Suluhu ambaye ni msikivu mpenda watu.

“Kwa mkoa wa Tanga ametupendelea leo tunajenga daraja mto Pangani ambalo ni kubwa tokea uhuru tuna kila sababu ya kusema Tanga tunakuwa wa kwanza kwa kura za Rais Dkt Samia”Alisisitiza Mwenyekiti huyo.

Awali akizungumza katika kikao hicho Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM wilaya ya Tanga Hamza Bwanga alisema Jumuiya hiyo ipo tayari kuonyesha nguvu yake kwa kutoa mchango wake mkubwa kwenda kushirikiana na viongozi mbalimbali na wananchi kuhakikisha 2024 wanachukua viti vyote katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

“Nikuhakikishie Mwenyekiti sisi Jumuiya ya Wazazi wilaya ya Tanga tutakuwa mstari wa mbele kupigana usiku na mchana kuwa tayari kukitumikia chama na kuonyesha mchango wetu kuhakikisha kinapiga hatua kubwa za kimaendeleo”Alisema Mwenyekiti Hamza.

Aidha Mwenyekiti huyo aliwataka wajumbe wa mkutano huo ukimalizika wahakikishe wanaporudi kwenye kata zao kuhakikisha mabaraza yanafanyika kikatiba,wanaelimisha pamoja na mabaraza ya matawi.

Hata hivyo alisema wahakikishe pia wanaunda kamati ndogo za mazingira elimu na uchumi ili waweze kuwasaidia kuhakikisha jumuiya ya wazazi inakuwa imara na kushika namba moja mkoa huo na itakuwa na mchango mkubwa kwenye Chama cha Mapinduzi.
Share:

RITA YASAJILI CHETI CHA KUZALIWA NDANI YA SIKU MOJA SABA SABA!

Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini [RITA] imesajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa papo hapo kwenye Kilele cha maadhimisho ya sikukuu ya saba saba iliyofanyika tarehe 07/07/2023 kwenye viwanja vya J.K Nyerere jijini Dar es Salaam.

Akiwakabidhi vyeti vyao vya kuzaliwa wananchi waliojitokeza kujisajili kwenye sikukuu hiiyo ya saba saba, Naibu Kabidhi Wasii Mkuu Bi. Irene Lesulie amesema kuwa RITA imejipanga vizuri kuwapatia huduma Wananchi kiurahisi na kuwataka kutumia fursa hii kujitokeza kwa wingi kupatiwa huduma kwenye maonesho hayo.

"Nawasihi wananchi waendelee kujitokeza kwa wingi kwenye maonesho haya ya saba saba ,maana tunasajili na kutoa vyeti hapa hapa uwanjani, yaani unajiandikisha leo na cheti unapata leo",amesema.

Aidha baadhi ya wananchi waliojitokeza kusajiliwa na kufanikiwa kupata cheti kwenye viwanja hivyo vya saba saba ambapo maonesho ya 47 ya maonesho ya biashara yanaendelea wameipongeza RITA kwa kuwarahisishia huduma kwa kuwapatia cheti siku hiyo hiyo!!!

"Hawa RITA wako vizuri kusajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa hapa hapa sio mchezo,kwa watu tulivyojaa sikutegemea kupata cheti leo,"amesema Salma Ubuguyu mmoja wa wananchi waliojitokeza kupatiwa cheti cha kuzaliwa.

RITA inaendela kutoa Huduma ya Usajili wa vyeti vya kuzaliwa,Elimu ya Mirathi Kuandika na kuhifadhi Wosia kwenye maonesho hayo hadi tarehe 13 Julai 2023 .

Share:

DAWA ZA KULEVYA ZILIZOKAMATWA NA DCEA JUNI 2023

 


Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI JULAI 92023

 








         

      


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger