Tuesday, 4 July 2023

TEMBELEA DUKA LA HALOTEL UJIPATIE ZAWADI KEMKEM MSIMU HUU WA SABASABA

Mkurugenzi wa Malunde 1 blog, Kadama Malunde akiwa ndani ya Duka la Halotel Mjini Shinyanga 

****
Jipatie zawadi kemkem ukitembelea Duka la Halotel katika msimu huu wa Sabasaba 2023!! Ukihudumiwa katika duka la Halotel kuanzia Juni 30,2023 hadi Julai 30,2023 utapata Kuponi ambayo ukirudi mara nyingine tena na ukanunua vocha ya kuanzia 5,000 utapata nyongeza ya sh. 1,000/=! , Jipatie Ofa motomoto ikiwemo Laini, Vocha na Keyholder buree kwa kila mteja!! Pia utapata kifungua kinywa bureee!!!
Ndani ya Duka la Halotel Mjini Shinyanga mteja akipata huduma ya kifungua kinywa bure kabisa leo Jumanne Julai 4,2023
Ndani ya Duka la Halotel Mjini Shinyanga mteja akipata huduma ya kifungua kinywa bure kabisa leo Jumanne Julai 4,2023
Ndani ya Duka la Halotel Mjini Shinyanga mteja, Mkurugenzi wa Malunde 1 blog, Kadama Malunde akipata huduma ya kifungua kinywa bure kabisa leo Jumanne Julai 4,2023
Ndani ya Duka la Halotel Mjini Shinyanga Mkurugenzi wa Malunde 1 blog, ndugu Kadama Malunde akipata huduma ya kifungua kinywa bure kabisa leo Jumanne Julai 4,2023
Mkurugenzi wa Malunde 1 blog, Kadama Malunde akiwa ndani ya Duka la Halotel Mjini Shinyanga 
Huduma zikiendelea kutolewa ndani ya Duka la Halotel Mjini Shinyanga 
Huduma zikiendelea kutolewa ndani ya Duka la Halotel Mjini Shinyanga 
Huduma zikiendelea kutolewa ndani ya Duka la Halotel Mjini Shinyanga 

Share:

Monday, 3 July 2023

KAIBA CHUPI YANGU ILI NISIOLEWE BAADA YA KUMKATAA


James alikuwa kijana ambaye anaishi mtaani kwetu Buza, tuliweza kujuana na kuonana mara kwa mara, siku moja natoka Stand ya Buza ili niende nyumbani, nikakutana na James na kuniomba namba yangu ya simu, bila tatizo niliweza kumpatia.


Usiku huo James aliweza kunipigia simu na kuniomba tuwe wapenzi, maneno hayo yalinishtua kwa sababu alikuwa miongoni mwa vijana wanaosifika kwa kuwa na tabia mbaya mtaani kwetu.


Sikuweza kumkubalia ombi lake kutokana na tabia yake, pia hakuwa na sifa ambazo nilizipenda, baada ya kukataa ombi lake ilikuwa vita kwangu, mara kunitumia marafiki zake na kusema maneno machafu juu yangu, na muda mwingine kunifanyia fujo hadi kunipiga.


Siku moja nilifua nguo zangu hadi za ndani na kuzianika nje, baada ya masaa kadhaa kupita nilitoka nje kwa ajili ya kuanua nguo zangu, nilishangaa kuona nguo yangu moja ya ndani haipo pale nje katika kamba.

Sikuweza kufuatili sana maana sikudhani kuwa kuna mtu anaweza chukua nguo yangu ya ndani, kesho yake muda wa saa tano asubuhi Bibi yangu aliniagiza dukani, njiani nikakutana na Alex ambaye ni miongoni mwa marafiki wake James.


Alex alinisimamisha kisha kunipatia mfuko mweusi na kuniambia ni ujumbe kutoka kwa James, mwanzo nilikataa kuupokea lakini Alex aliniomba nichukue, basi hapo hapo nikafungua na kukuta chupi yangu imekatwa katwa.

Sikufika hata dukani niligeuza na kurudi nyumbani haraka kabla sijafika nyumbani nikakutana na James na marafiki zake wawili, hapo James ndio akasema; “Naapa hutowahi kupata Mume maishani mwako, wewe ni wangu".


Sikujibu chochote zaidi ya kwenda kumsimulia Bibi na kumuomba Mungu ili aniepushe na visa vya James, maana niliweza kufika hatua ya kuogopa kutoka nje.

Baada ya miaka minne wenzangu wote waliweza kuolewa na James kupata mwanamke ila mimi sikuweza kupata mtu hata wa kuniomba uchumba. Nilipofikisha miaka 30 nikaanza kujiuliza mbona siolewi, pia nikaanza kukumbuka maneno ya James alivyosema na kujiuliza kwa nini aliiba chupi yangu na kuitoboa vipande vipande.


Nilipofikisha miaka 32 bila kupata Mume na mtoto moyo wangu ulijaa na wasiwasi na kujiuliza kwa nini mimi tu, wapi nimekosea mbona wenzangu wote wana watu wao!.

Nikiwa kwenye mitandao ya kijamii, napitia pitia nikaona mtu mmoja ametoa ushuhuda alivyoweza kusaidiwa na African Doctors hadi kupandishwa cheo kazini kwake.

Nilichukua namba ya African Doctors ambayo alikuwa ameiweka kwenye ushuhuda wake, niliamua kuchukua uamuzi wa kuwasiliana naye, nilimwambia shida yangu kubwa sipati mwanaume na umri wangu unazidi kwenda.

Baada ya saa moja kupita, nilimpigia simu African Doctors, aliweza kunieleza maisha yangu yote na vikwazo nilivyokuwa nakumbana navyo, bila kusahau kuhusu tukio la Chupi yangu iliyoibiwa nikiwa na miaka 20. African Doctors akaniahidi kuwa atanisaidia na Love Spells, ndani ya siku nne nitapata matokeo mazuri.

Siku ya tatu asubuhi niliweza pata mtu ambaye nilitamani kuwa naye ila sikuwa na uwezo ila kwa nguvu ya African Doctors, leo hii yupo kifuani mwangu katika ndoa.

Katika mazungumzo African Doctors alisema anatibu mtu popote pale alipo na anatatua changamoto nyingine kama kurudisha mpenzi, kushinda michezo ya bahati nasibu, kutatua shida za familia.

Wasiliana na African Doctors kwa namba; +254 769 404965, tembelea tovuti yao; www.african-doctors.com




au watumie email; africandoctorheals@gmail.com.

Mwisho.


Share:

SERIKALI YAMPONGEZA DUNNAGAN KWA KUTANGAZA UTALII DUNIANI KUPITIA KUPANDA MLIMA KILIMANJARO MARA 50.


Na John Mapepele

Serikali imetambua na kumpongeza Balozi Nguli wa utalii wa Tanzania nchini Marekani mwenye umri wa miaka 63 bwana Macon Dunnagan kwa kuandika historia ya kukamilisha kupanda mlima Kilimanjaro mara 50 hivi na kuendelea kuitangaza Tanzania kimataifa hususan Marekani.

Akizungumza kwenye mkutano na Waandishi wa Habari akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii nchini leo mjini Moshi siku moja baada ya kumaliza kushuka katika mlima huo kwenye safari yake ya mara ya 50 Dunnagan ametoa wito kwa watanzania na wageni kutoka sehemu mbalimbali kuwa na tabia ya kutembelea vivutio vilivyopo nchini Tanzania ili kujionea utajiri wa vivutio mbalimbali ambavyo havipatika sehemu nyingi duniani.A

Aidha amesema Tanzania imebarikiwa kuwa na vivutio vingi ikiwa ni pamoja na wanyama wa aina zote wakiwemo Simba Tembo Twiga na Chui pia kupanda Mlima Kilimanjaro.

Balozi Dunnagan ambaye alianza kupanda mlima Kilimanjaro toka mwaka 1999 amesema ataendelea kuiamasisha Dunia kuja kuona maajabu ya vivutio vya Taifa la Tanzania.


Akiongea kwa niaba ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mohamed Mchengerwa, Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Nchini amesema Serikali itaendelea kutambua michango ya watu wote wanaotangaza utalii wa Nchi wa ndani na wanje akiwemo Macon.

Amempongeza balozi huyo kwa kutoa hamasa kubwa wa watanzania na wamarekani kupitia vyombo mbalimbali vya habari vya nchi hiyo ambapo amefafanua kuwa Dunnagan alianza kuhamasika kupanda mlima Kilimanjaro mwaka 1967 baada ya kuangalia movi ya “Snow of Kilimanjaro”.
Share:

VIJANA 182 WAPIKWA KUTUMIKIA JESHI LA JADI SUNGUSUNGU ITWANGI RPC MAGOMI ATAKA WAZINGATIE MAADILI


Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoa wa Shinyanga Janeth Magomi akizungumza kwenye Mkutano wa Sungusungu katika Kijiji cha Imenya Kata ya Itwangi,ambapo ametumia fursa hiyo kuwataka kuacha kujichukulia sheria mkononi.
Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Itwangi Kamuli Makomango akizungumza kwenye Mkutano wa Jeshi la Jadi Sungusungu Tarafa ya Itwangi Halmashauri ya Shinyanga wakati wa kufunga mafunzo kwa vijana 182 kutoka Vitongoji vya Imenya na Igomelo Kata ya Itwangi ambao wameingizwa rasmi Jeshi la jadi Sungusungu.


Na Elias Gamaya - Shinyanga 
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga ACP Janeth Magomi amelitaka Jeshi la jadi maarufu Sungusungu kutoka Vitongoji viwili vya Imenya na Igomelo Kata ya Itwangi kuzingatia maadili ya kazi yao ikiwemo kujiepusha na vitendo vya kihalifu.


Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya mwezi mmoja ya vijana 182 ambao wameingia katika Jeshi la jadi Sungusungu rasmi ili kusaidia kudhibiti wahalifu wiki iliyopita, Kamanda Magomi amewasihi kuzingatia sheria na kuacha kujichukulia sheria mkononi badala yake wawafikishe polisi.

"Jeshi la jadi lipo kisheria kupitia sheria ya Mgambo na linatambulika kisheria na lilianza kupata umaarufu, sisi Jeshi la Polisi hatutoshi kama polisi mmoja anatakiwa kulinda raia 450 tu katika suala zima la ulinzi na usalama lakini kinachotokea sasa kutokana na uchache wetu askari mmoja analinda raia 1700”, amesema Kamanda Magomi.
Kamanda Magomi amesema Mkoa wa Shinyanga bado unakabiliwa na mauaji,ndoa za utotoni, mimba kwa wanafunzi,ubakaji,kulawiti na baadhi ya watu kujihusisha na mapenzi ya ndoa za jinsia moja mambo ambayo yanatakiwa kukemewa katika jamii ili kukomesha vitendo hivyo.


Awali akielezea historia ya Jeshi la Jadi Muelimishaji ambaye pia ni Mhasibu wa Tarafa ya Itwangi, Philipo Malongo amesema kabla ya kuitwa jeshi la jadi lilikuwa linaitwa shirika la kurudisha mali za watu ikiwemo mifugo kutokana na kukithiri kwa matukio ya wezi wa mifugo kwa kipindi cha mwaka 1981.

Amesema malengo na madhumuni ya Jeshi hilo ni kuwaelimisha vijana ili waielewe sungusungu,kuawezesha vijana kubadilika na kuwafundisha nidhamu vijana ambapo mafunzo hayo hufanyika kila baada ya miaka mitano.


“Sungusungu haikuwekwa kwa ajili ya kuwatesa vijana bali iliwekwa kwa nia ya kuwafundisha kuwa na nidhamu na kuwatengeneza kuendana na kanuni na sheria za nchi yetu”,amesema Malongo

Nao baadhi ya sungusungu wa jeshi hilo wamesema mafunzo hayo yatawasaidia kukabiliana na wahalifu,pia kusaidia kupunguza vitendo vya kihalifu ili hatua za haraka zichukuliwe kukabiliana na matukio hayo na kuyakomesha.
Sungusungu wakiwa kwenye Mkutano
Mkutano unaendelea
Mkutano unaendelea
Mwezeshaji wa mafunzo kwa vijana walioingizwa rasmi Jeshi la jadi Sungusungu Tarafa ya Itwangi Philip Malongo akizungumza kwenye Mkutano
Diwani wa Kata ya Itwangi Sonya Jilala akizungumza kwenye Mkutano wa Sungusungu
Mkutano unaendelea
Mkutano wa Sungusungu unaendelea
Viongozi wakifuatilia Mkutano
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger