Monday, 3 July 2023
Sunday, 2 July 2023
BENKI YA CRDB YAINGIA MAKUBALIANO NA KLABU YA YANGA KUSAIDIA USAJILI WA WANACHAMA NA MASHABIKI
Benki ya CRDB imeingia mkataba wa makubaliano na Yanga kutoa kadi kwa wanachama wa klabu Yanga katika kuongeza ufanisi wa usajili na masuluhisho ya kifedha.
Akizungumza wakati hafla kusaini makubaliano hayo iliyofanyika Julai 1, 2023, Afisa Mkuu wa Biashara Benki ya CRDB, Boma Raballa amesema kadi hizo zitawawezesha mashabiki wa mabingwa hao wa kihistoria wa Tanzania bara kujisajili na kulipia michango yao ya uanachama kupitia mtandao wa matawi zaidi ya 240 wa Benki ya CRDB.
“Kupitia kadi hizi zilizopewa jina la TemboCard Young Africans wanachama wa klabu hii wataweza kufanya miamala kupitia mashine za kutoa fedha (ATMs) hadi milioni 2, kufanya manunuzi kupitia mashine za malipo (PoS), pamoja na malipo ya mtandaoni (online payment) hadi milioni 20,” alisema Raballa huku akibainisha kuwa wanachama hao pia wataunganishwa na mifumo ya kidijitali ya SimBanking na Internet banking.
Raballa pia alianisha kuwa kupitia kadi hizo za TemboCard Young Africans wanachama na washabiki wa klabu hiyo pia watapata bima ambayo inatoa mkono wa pole wa Shilingi milioni 3 pindi mwanachama anapofariki ya milioni 3, Shilingi milioni 2.5 anapofiwa na mume au mke, na Shilingi milioni 2 endapo atapata ulemavu wa kudumu.
Kwa upande wake Rais wa Yanga, Injinia Hersi Saidi ameishukuru Benki ya CRDB kwa kufungua milango ya ushirikiano na klabu hiyo itakayosaidia kuongeza ufanisi katika usajili. Injinia Hersi alisema ukubwa Benki hiyo yenye mtandao mpana ndani na nje ya nchi utakwenda kusaidia kuongeza kasi ya usajili wa wananchama wengi zaidi kulinganisha na sasa hivi.
“Mchakato wetu wa usajili wa wanachama umekuwa na mafanikio makubwa sana ukitufanya kuwa klabu inayoongoza kwa Idadi ya wananchama katika ukanda huu wa jangwa la sahara, lakini ni ukweli usiopingika kuwa bado hatujafikia lengo kwani matawi yetu mengi yamekosa miundo mbinu sahihi. Ni imani yetu ushirikiano huu na Benki ya CRDB utakwenda kuongeza kasi ya usajili,” aliongezea Injinia Hersi.
Akizungumzia kuhusu zoezi usajili wa wananchama kupitia Benki ya CRDB, Injinia Hersi alisema kuanzia tarehe 5 Julai 2023 wanachama wa klabu hiyo wanaweza kufanya usajili katika matawi yote ya benki hiyo yaliyosambaa kote nchini bila gharama yoyote.
Saturday, 1 July 2023
MBIO ZA KIMONDO ZAFANA SONGWE
Mashindano ya riadha, maarufu kama Mbio za kimondo yanayoandaliwa kwa pamoja baina ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), ikiwa ni maadhimisho ya siku ya kimondo duniani kwa mwaka 2023 yamalizika kwa mafanikio makubwa huko Mbozi mkoani Songwe.
Akizungumza katika kilele cha maadhimisho hayo (leo) Juni 30, 2023 kutoka wilayani Mbozi mkoani Songwe, Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Utafiti, Machapisho na Ubunifu wa OUT ambaye pia ni mjumbe wa bodi ya NCAA, Dkt. Harrieth Mtae, amesema shughuli zote zilizoambatana katika maadhimisho ya siku kimondo duniani yamekwenda vizuri lakini mbio za zimondo zimefanya vyema.
“Nasema maadhimisho haya yamefana sana sababu katika mbio hizi za km 5, 10 na 21 yamepata washiriki wengi wa ngazi za kimataifa na kitaifa, kutokana na kufana kwa maadhimisho haya tunategemea taarifa za zao hili jipya la utalii wa anga zitazidi kusambaa sababu ni kitu ambacho hakijazoeleka hivyo jamii inapaswa kuhabarishwa juu ya utalii wa anga ili kuleta matoke chanya.” Amesema Dkt. Mtae
Pia, Kamishna Msaidizi Mwandamizi kutoka NCAA, Joshua Mwamkunda, akizungumzia katika kilele cha maadhimisho hayo, amesema kitendo tu cha wananchi wengi kufika kwa wakati mmoja katika maeneo ya kimondo hayo tayari ni mafanikio tosha kuhusu kueneza habari hizi za utalii wa anga na kimondo.
“Kitendo tu cha washiriki wa hizi mbio kutoka mikoa mbalimbali pamoja na wananchi wa maeneo jirani waliofika kujionea maadhimisho haya ni mafanikio tosha juu ya uhamsishaji na uelimishaji juu ya urithi wa anga na utalii wake, watu wengi wamefika hapa na wametembelea kimondo, wamepiga picha maana yake tayari wamefanya utalii wa ndani lakini kutuma picha mitandaoni hapo matangazo yanasambaa sehemu tofauti.” Amesema Kamishna Mwamkunda.
Aidha, alisisitiza kuwa lengo la maadhimisho haya ni kuelimisha, kuhamasisha na kuendeleza utalii wa anga na urithi wake hasa hivi vimondo vilivyopo nchini ili kuongeza watalii wa anga kutoka ndani na nje ya nchi na kuungana kwa vitendo juhudi za serikali katika kuhamasisha utalii nchini.
Naye, Mkuu wa Idara ya Utalii, Ukarimu na Geographia wa OUT, Dkt. Halima Kilungu, amesema kuhamasisha wananchi kupenda utalii wa anga ni kuwafanya wapende mazingira hayo hivyo watashiriki katika kuyalinda mazingira ya anga dhidi ya uharibifu.
Maadhimisho ya siku ya anga duniani huadhimishwa Juni 30, kila mwaka ambapo kwa hapa nchini yamekuwa yakiadhimishwa katika mkoa wa Songwe ili kuhamasisha utalii nyanda za juu kusini kupitia kimondo kilichopo wilayani Mbozi mkoani Songwe. Taasisi mbili za NCAA na OUT wamekuwa wakishirikiana katika maadhimisho hayo nchini ikiwa ni sehemu ya ushiriki wao katika kutangaza vimondo vilivyopo sambamba na zao jipya la utalii wa anga.
MWENYEKITI UVCCM KISHAPU AFANYA MKUTANO WA HADHARA KUSIKILIZA KERO ZA VIJANA NA KUZITAFUTIA UFUMBUZI
Na Marco Maduhu,KISHAPU
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana ya Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Kishapu Benard Benson Welema, amefanya Mkutano wa hadhara wa kusikiliza kero za Vijana wilayani humo na kuzitafutia ufumbuzi.
Mkutano huo wa hadhara umefanyika leo Julai 1, 2023 katika Mji wa Mhunze wilayani Kishapu.
Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Kishapu Benard Benson Welema akisikiliza kero za vijana.
Amesema amefanya Mkutano huo wa kusikiliza kero mbalimbali ambazo zinawakabili vijana wilayani humo, ili kuzitafutia ufumbuzi, huku akiwataka wachangamkie fursa mbalimbali kupata ajira katika miradi ya kimkakati ambayo inatekelezwa wilayani humo na kujikwamua kiuchumi.
Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Kishapu Benard Benson Welema.
“Kero ambazo vijana wenzangu mmeziwasilisha kwenye Mkutano huu tutazifikisha sehemu husika ili zipate kutatuliwa, katika wilaya yetu ya Kishapu kuna miradi ya kimkakati ambayo inatekelezwa changamkieni fursa hizo ili mpate ajira, vibarua na kujikwamua kiuchumi,”amesema Welema.
Aidha, amewataka vijana wilayani humo kuwa Mstari wa mbele kuomba Ajira ambazo zimekuwa zikitangazwa na Halmashauri, ambapo inaonekana muitikio wao kuwa mdogo, pamoja na kuunda vikundi vya ujasiriamali ili wapate mikopo ya asilimia 4 kwa vijana ya halmashauri na kuinuka kiuchumi.
Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Kishapu Benard Benson Welema.
“Serikali ilisitisha utoaji wa mikopo asilimia 10 ya mapato ya ndani ya halmashauri baada ya kuona haina tija, na vijana wengi mlikuwa mkikopa lakini hamrejeshi, nawaomba mikopo hii itakapoanza kutolewa itumieni vizuri kufanya uzalishaji na kuwaletea maendeleo na siyo kwenda kuzinyewa Pombe.”amesema Welema.
Katibu wa UVCCM Wilaya ya Kishapu Jamal Namanga akizungumza kwenye Mkutano huo.
Nao baadhi ya vijana wakiwasilisha kero zao akiwamo Elisha Elias, wameiomba Serikali wilayani humo kwamba fursa mbalimbali ambazo zinatokea zikiwamo za ujenzi na utengenezaji wa samani wawe wanatoa kipaumbele kwanza kwa vijana wilayani humo.
Naye Kijana Michael Mabula, amewasilisha kilio cha ukosefu wa mikopo ya Bodaboda kutoka kwenye Taasisi za kifedha sababu ya kuwa na masharti magumu ya dhamana, na kuwafanya kuendelea kutumikishwa na kushindwa kumiliki bodaboda zao wenyewe.
Diwani wa Songwa Abdul Ngolomole, akizungumza kwenye Mkutano huo, amempongeza Mwenyekiti huyo wa UVCCM wilayani Kishapu kwa kufanya Mkutano wa kusikiliza kero za vijana na kuahidi atashirikiana naye kama diwani kijana ili kuzitafutia ufumbuzi.
Diwani wa Songwa Abdul Ngolomole akizungumza kwenye Mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Kijana Michael Mabula akiwasilisha baadhi ya kero ambazo zinawakabili vijana wilayani Kishapu
Mkutano ukiendelea.
Elisha Elias akiwasilisha baadhi ya kero ambazo zinawakabili vijana wilayani Kishapu.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Baadhi ya akina Mama wakiwa kwenye Mkutano wa Mwenyekiti wa UVCCM wilayani Kishapu.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Akina Mama wakiimba nyimbo za CCM kwenye Mkutano wa Mwenyekiti wa UVCCM wilayani Kishapu.