Thursday, 1 June 2023

HEKARI 101 NA MAGUNIA 482 YA BANGI YATEKETEZWA ARUSHA

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na dawa za kulevya (DCEA) imefanikiwa  kukamata gunia 482 za bangi iliyokuwa tayari kusafirishwa kwenye masoko na  imeteketeza jumla ya hekari 101 za mashamba ya bangi yanayokadiriwa kuwa na bangi mbichi gunia 550 katika eneo la Kisimiri Juu kata ya Uwalu, Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha.


Ukamataji huo umefanyika Mei 31,2023 kufuatia agizo la Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kufanya operesheni nchi nzima ili kuhakikisha dawa za kulevya zinatokomezwa nchini.

Akizungumza operesheni hiyo maalumu iliyofanyika mkoani Arusha Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Aretas Lyimo amesema, Mamlaka kwa kushirikiana na vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama itaendelea kufanya operesheni za mara kwa mara katika maeneo hayo ili kuhakikisha bangi inatokomea kabisa na hatimaye wakulima na wananchi kwa ujumla wanaoishi katika eneo ya Kisimiri juu na chini wanaachana na kilimo cha bangi na kujikita katika mazao mengine ya biashara badala ya bangi.


Kamishna Lyimo amesema kuwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb) katika kuhakikisha agizo la Mheshimiwa Rais linatekelezwa, ameelekeza kufanyika kwa utafiti kujua ni mazao gani mbadala yanaweza kulimwa katika maeneo hayo ambayo yamekithiri kwa kilimo cha dawa za kulevya, ili wananchi wa maeneo husika waweze kupewa mbinu mbadala za kulima mazao mbalimbali ya chakula na biashara badala ya kuendelea na kilimo cha bangi. 

‘‘Tumewasiliana na Wizara ya Kilimo na Afisa kilimo wa kata ya Uwalu hapa Kisimiri ambaye ameeleza tayari utafiti huo umefanyika",amesema.


Aidha, Kamishna Lyimo amesema, elimu juu ya athari za biashara na matumizi ya dawa za kulevya itatolewa kupitia shule za msingi na sekondari. 

"Hii inafanyika kufuatia agizo la Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mheshimiwa Jenista Mhagama (Mb) kuitaka Mamlaka kushirikiana na wadau kutoa elimu katika maeno hayo. ambapo tayari maafisa elimu Kata wameanza kutoa elimu kwa wanafunzi, ili baadaye wasijihusishe na kilimo cha bangi na mirungi badala yake wajikite kwenye mazao mengine",ameongeza.

Katika kuhakikisha maagizo ya Waziri Mkuu yanatekelezwa, Afisa kilimo Kata ya Uwelu, Samwel Palangyo, amesema kuwa,utafiti uliofanywa na Wizara ya Kilimo kupitia kituo cha utafiti wa kilimo cha TARI Tengeru, imebaini kuwa yapo mazao yanayostawi katika maeneo hayo kama vile pareto, karoti na viazi mviringo na kuwa mbadala wa zao haramu la bangi ambalo halifai katika jamii.

 Ameiomba Serikali kuangalia namna ya kuwawezesha wananchi wa maeneo hayo kwa kutoa ruzuku ya mazao hayo.


Operesheni hii imefanyika ikiwa ni siku moja baada ya Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mheshimiwa Jenista Mhagama (Mb) kutoa taarifa ya hali ya dawa za kulevya nchini kwa mwaka 2022 ambapo katika taarifa hiyo alitaja mikoa inayojihusisha na kilimo cha Bangi kwa kiasi kikubwa, Mkoa wa Arusha ukiwa kinara ukifuatiwa na Iringa, Morogoro na Manyara.
Share:

Wednesday, 31 May 2023

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI JUNI 1,2023























Share:

UTEKELEZAJI WA SERA YA BAJETI UFANYIKE KUANZIA NGAZI YA SERIKALI ZA MITAA


WADAU wa Maendeleo ya Jinsia wameiomba Serikali kuhusu utekelezaji wa sera ya Bajeti ufanyike kuanzia ngazi ya Serikali za mtaa kabla haijaenda halmashauri na wananchi wajiridhishe vile vipaumbele vyao ili kuleta picha nzuri kwenye jamii na kuleta usahihi wa mambo.

Akizungumza leo Mei 31,2023 Jijini Dar es Salam wakati wa Semina za Jinsia na Maendeleo (GDSS) zinazoandaliwa na TGNP Mtandao wakati wakiichambua Bajeti ya Wizara ya Afya, Mchambuzi wa Masuala ya Kijinsia, Bw.Hancy Obote amesema fedha nyingi hazijakwenda kwenye matumizi ambayo yanawalenga wananchi moja kwa moja .

"Hatujaona fedha ikienda moja kwa moja kwenye vifaa tiba kwa maana kusaidia wanawake wakati wa kujifungua, tumeona fedha imenunua magari 102 ya kwenda kwajili ya matumizi ya ufuatiliaji wa madawa, vitu ambavyo havigusi wananchi moja kwa moja". Amesema

Kwa upande wake masuala ya Bima ya Afya, washiriki wa Semina za Jinsia na Maendeleo wamesema bima ya afya kwa wananchi wa kawaida ni changamoto kwasababu ya gharama kubwa ambazo ni ngumu kuzimudu.

Aidha wamesema suala la Matibabu bure kwa wazee na watoto wenye umri chini ya miaka mitano suala hilo linaonekana halipo kwani kuna gharama lazima aweze kulipia ili apate matibabu.








Share:

WASAFIRI WANAOTUMIA VYOMBO VYA MAJINI WAPEWA NENO NA TASAC

 

Afisa Mfawidhi wa Shirika la TASAC Mkoani Tanga Kapten Christopher Shalua  (kushoto) akitoa maelezo kwa Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji,Viwanda na Biashara Conrad Millinga wa kwanza (kulia)ambaye alimwakilisha Waziri wa Wizara hiyo kuhusu namna ya kutumia vifaa vya kujiokolea wakati alipotembelea banda  la TASAC katika maonyesho ya 10 ya biashara na utalii yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwahako Jijini Tanga
Afisa Mfawidhi wa Shirika la TASAC Mkoani Tanga Kapten Christopher Shalua  (kushoto) akitoa maelezo kwa Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji,Viwanda na Biashara Conrad Millinga wa kwanza kulia ambaye alimwakilisha Waziri wa Viwanda wakati alipotembelea banda lao katika maonyesho ya 10 ya biashara na Utalii yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwahako Jijini Tanga
Afisa Mfawidhi wa Shirika la TASAC Mkoani Tanga Kapten Christopher Shalua  akizungumza na vyombo vya habari katika Banda lao kwenye  maoanyesho ya 10 ya biashara na utalii yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwahako Jijini Tanga
Afisa Masoko Mwandamizi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Martha Kelvin (kushoto) akimkabidhi zawadi Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji,Viwanda na Biashara Conrad Millinga kulia wakati alipotembelea Banda lao


Na Oscar Assenga,TANGA

SHIRIKA la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limetoa wito kwa wasafiri wanaotumia vyombo vya Usafiri majini kuhakikisha wanatumia vyombo vilivyo ruhusiwa kisheria kubeba abiria na sio kupanda vyombo vya kusafirisha mizigo ikiwemo majahazi.

Wito huo ulitolewa leo na Afisa Mfawidhi wa Shirika hilo Mkoani Tanga Kapten Christopher Shalua wakati akizungumza na waandishi wa habari katika maonyesho ya 10 ya biashara na utalii yanayoendelea katika viwanja vya Mwahako Jijini Tanga

Aidha, alisema kwa sababu viwango vya vyombo vipo kwenye madaraja tofauti ni vema kila chombo kikatumika kulingana na matumizi huzika yaliyothibitishwa na amewataka  wananchi wa Tanga kwa ujumla kutembelea Banda lao ili kupata elimu zaidi.

Alisema TASAC imeshiriki maonesho hayo kwa ajili ya kuwafikia wananchi hususani wanaoishi maeneo ya fukwe na kuwaelimisha kuhusu Usalama, Ulinzi na Utunzaji wa Mazingira Majini pamoja na majukumu yanayotekelezwa na Shirika hilo kwa Mujibu wa Sheria. 

Hata hivyo alisema kwamba jukumu lao pia ni kuhakikisha wanasimamia Bandari kuhakikisha wanatoa huduma katika viwango vinavyokubalika kimataifa ili kuweza kuchochea ukuaji wa uchumi nchini .

Mwisho.

Share:

SERIKALI YAKANUSHA TAARIFA ZA NDEGE YAKE KUSAFIRISHA MIZIGO HARAMU

Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Msemaji wà Serikali kwebye ukumbi wa habari Maelezo jijini Dodoma.
Msemaji wà Serikali Gerson Msigwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma.


Na Dotto Kwilasa,Dodoma.

Serikali imekanusha taarifa ya Sekta ya Anga nchini kukumbwa na kashfa nzito ya ndege yake ya mizigo aina ya Boeing767-300F kusafirisha mizigo haramu kwa njia haramu ambayo haijafuata taratibu za kiforodha ambayo inasambaa kwenye baadhi ya mitandao na kueleza kuwa ni  za upotoshaji zipuuzwe.

Hayo yameelezwa leo Mei 30,2023 Jijini hapa na Msemaji wa Serikali na  Mkurugenzi wa Idara ya Habari -MAELEZO Gerson Msigwa wakati akizungumza na Waandishi wa habari na kueleza kwamba  taarifa hizo ni za upotoshaji na kwamba zinalenga kurudisha nyuma juhudi za Serikali katika kukuza sekta ya anga na usafiri wa anga. 

Kutokana na hayo Msigwa amesema Serikali inawafuatilia waliochapisha taarifa hizo na hatua zaidi zitachukuliwa dhidi yao.

Msigwa amefafanua kuwa dege ya mizigo aina ya Boeing767-300F bado haijafika Tanzania, haijaanza kazi rasmi, bado ipo mikononi mwa watengenezaji nchini Marekani. Ndege hii inatarajiwa kupokelewa nchini tarehe 03 Juni, 2023.

"Mheshimiwa Rais, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan tayari ameandaa ndege kubwa aina ya Boeing 787-8 Dreamliner ambayo itabeba wachezaji, viongozi na mashabiki kwenda Algeria kwa ajili ya kuishangilia timu ya Yanga wakati wa mchezo wa pili wa fainali ya Kombe la Shirikisho,"amesema 

Katika hatua nyingine Serikali imewatoa  hofu Watanzania kuhusu  muda wa kuanza kwa majaribio ya treni ya abiria kwa kipande Cha kwanza Cha reli ya kisasa ya SGR kutoka Dar Es Salaam hadi Morogoro na kueleza kuwa haijadanganya bali kilichotokea ni mabadiliko ya ratiba ya mtengenezaji yalioathiri kuja kwa vichwa hivi.

Imesema kutokuanza kwa majaribio ya treni ya abiria kwa kipande cha kwanza cha reli ya kisasa ya SGR kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro ambayo imeshakamilika, kumesababishwa na kutokukamilika kwa wakati kwa utengenezaji wa vichwa vya treni viwili na mabehewa 30.

Akieleza hayo Mkurugenzi wa Idara hiyo  ya Habari -MAELEZO amesisitiza kuwa sababu ya kutokukamilika kwa vichwa hivyo ni kutokana na changamoto katika upatikanaji wa baadhi ya vipuri.

Msigwa amesema,"Vipuri vinavyotumika kwenye ukamilishaji wa vichwa vya treni ambavyo vinatoka nchini Canada ambako kutokana na changamoto ya UVIKO-19, vita na kuharibika kwa uchumi katika nchi nyingi duniani vimefanya viwanda vingi vinavyozalisha vipuri kutorudi katika ratiba za uzalishaji za kawaida,"amefafanua na kuongeza;

Vipuri tulivyotarajia vitafungwa kwenye vichwa viwili ni miongoni mwa vipuri ambavyo vimepata madhara kutokana na changamoto hizo hivyo, mtengenezaji hakuweza kuleta kwa muda aliopangiwa,"anasema Msigwa 

Pamoja na hayo amesema treni hiyo imeshindwa kuanza majaribio kwa sababu  vichwa vya kuvuta mabehewa havijafika na kwamba Serikali inaendelea kufuatilia kwa karibu ukamilishaji wa vichwa hivyo ili vitakapofika kazi ya majaribio ianzie mara moja.

"Kwa makubaliano mapya tuliyoingia na mtengenezaji wa vichwa vya treni, ameahidi kichwa cha kwanza kitafika mwezi Julai na kikifika tu kitaanza majaribio mwezi huo huo. Kichwa cha pili kitafuata baada ya hapo,"amesema

Amesema Kwa upande wa mabehewa, baadhi yake yameshakamilika na kati ya tarehe 2-3, Juni, 2023 huku kukiwa na matarajia kupokea mabehewa sita ya ghorofa kwa ajili ya kutumika kwenye SGR.

Amesema Mabehewa hayo yamefanyiwa ukarabati na kurejeshwa katika upya wake kwa zaidi ya asilimia 85, haya ni mabehewa ambayo yametoka Ujerumani ambapo jumla yake ni 30. Mabehewa 24 yataendelea kuja kwa awamu.

"Kazi ya ukamilishaji wa mabehewa yanayoendelea kutengenezwa nchini Korea ambayo tayari mabehewa 14 mapya yalishafika na mengine 45 kazi inaendelea kukamilishwa,tunatarajia mabehewa yaliyobaki yatafika nchini wakati wowote ndani ya mwaka huu,mabehewa mengine ambayo tumenunua kutoka China, tunatarajia yatafika mwakani,"amesema 


Share:

IFC YAZINDUA PROGRAMU YA JINSIA KUWEZESHA WANAWAKE KIUCHUMI

Mkurugenzi Kanda wa IFC Jumoke Jagun-Dokunmu,



Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na makundi maalumu Dkt.Doroth Gwajima.

Na Dotto Kwilasa,Dodoma.

Katika kuwezesha wanawake kiuchumi, Serikali kwa kushirikiana na Taasisi ya Benki ya Dunia (IFC) imezindua programu mpya ya Jinsia "ANAWEZA" itakayo tekelezwa kwa miaka mitano na kugharimu zaidi ya Dola za kimarekani milioni 10.

Akizungumza leo Mei 31,2023 Jijini Dodoma kwenye uzinduzi huo,Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na makundi maalumu Dkt.Doroth Gwajima IFC ikiwa ni Taasisi tanzu ya Benki ya Dunia ina lengo la kuwezesha wananchi kiuchumi na kuachana na utegemezi.

Katika kuunga mkono juhudi hizo Waziri Gwajima amesema hadi kufikia Aprili mwaka huu serikali ilikuwa  imetoa sh.bilioni 30.9 kwa vikundi 5,120 vya wanawakea katika Halmashauri 184 nchini.

Fedha hizo zimetolewa Kwa lengo la kuboresha kipato na kuondoa umaskini kwa wanawake na wanaume nchini.

Amesema kupitia sheria ya fedha za mamlaka za serikali za mitaa ya mwaka 2018 inayozitaka Halmashauri zote nchini kutenga asilimia 10 ya mapato yake ya ndani kwa ajili ya kutoa mikopo isiyo na riba kwa Makundi maalum ikiwemo wanawake asilimia nne, vijana asilimia nne na watu wenye ulemavu asilimia mbili.

Dk.Gwajima ameeleza kuwa kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake (WDF) unaosimamiwa na wizara anayoisimamia imetoa mikopo yenye thamani ya sh.milioni 664.5 kwa wanawake wajasiriamali 104 katika kipindi cha Julai 2022 hadi Aprili,mwaka huu.

"Tanzania ni miongoni mwa  Mataifa yanayotekeleza malengo ya jukwaa la kimataifa ya kukuza usawa wa kijinsia ambapo Rais  Dk. Samia ni kinara wa utekelezaji wa Jukwaa hilo hususan kuhusu haki na usawa wa Kiuchumi,tumetengeneza programu inayotekelezwa kwa ushirikiano wa Serikali na Sekta binafsi ili ifikiapo mwaka 2026 hali ya Wanawake iwe imebadilika kwa kiasi kikubwa,"amesema 

Pamoja na jitihada hizo amesema Programu hiyo iliyozinduliwa inajumuisha kutengeneza mazingira bora ya malezi ya awali na uangalizi wa watoto katika ngazi ya jamii ikiwemo masokoni lakini pia katika maofisi ili kuhakikisha huduma za msingi kama vile maji na umeme zinafika kwa ukamilifu vijijini ili kutatua changamoto zinazowakumba wanawake,”alieleza

Amefafanua kuwa Programu ya ANAWEZA itachangia kufanikisha utekelezaji programu wa kizazi chenye usawa hapa nchini na kuwezesha wanawake kushiriki katika nafasi mbalimbali za uongozi 

“Ni matarajio yangu kuwa mpango utashirikisha sekta binafsi hapa nchini ili kukuza upatikanaji wa fursa za wanawake katika nafasi za uongozi na ajira bora ili kuchochea ukuaji wa uchumi nchini;

Utafiti unaonyesha kuwa kuziba pengo la kijinsia kati ya ajira za wanaume na wanawake kunaweza kuongeza Pato la Taifa la muda mrefu kwa kila mtu kwa asilimia 4.8.

Kwa upande wake Mkurugenzi Kanda wa IFC Jumoke Jagun-Dokunmu, alisema program ya ANAWEZA itatekelezwa kwa miaka mitano na inalenga kushughulikia changamoto zilizopo ili kuwezesha ushiriki wa wanawake katika sekta binafsi,  nafasi za uongozi na ujasiriamali wenye ufanisi endelevu.

Amesema programu hiyo itakagharimu fedha za Kimarekani milioni 7.5, inaendana na Dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2025, Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano.

“Wanawake wanaweza kuwa injini ya ukuaji wa uchumi wa Tanzania, hivyo kuwawezesha wanawake kunachukua jukumu kubwa la kukuza uchumi na kuwezesha upatikanaji wa maisha bora kwa watu binafsi na familia zao” amesema.

Katika kusisitiza hilo amesema hakuna nchi inayoweza kupata maendeleo bila mwanamke na hivyo kupitia Uwekezaji huo Tanzania inaenda kuwa kinara na mfano wa kuigwa na mataifa mengine kuhusu uwezeshaji wanawake.

"Tunajipanga kusaidia wanawake wengi zaidi kupata Mafanikio kiuchumi ,tutafanya pia na sekta binafsi kuwekeza kwenye kilimo kuongeza ufanisi wa Wanawake kwenye masuala ya kiuchumi na kuweka usawa kwenye masuala ya jinsia,"anasisitiza 

Amefafanua kwa tathmini ya Benki ya Dunia ya mwaka 2022 kuhusu hali ya jinsia Tanzania inaonyesha kuwa  imepiga hatua katika kuongeza usawa wa kijinsia kwa kufanya jitihada za kukabiliana na ukosefu wa usawa wa kijinsia katika Nyanja zote za maisha ya wanawake.

Naye Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Zanzibar, Riziki Pembe amesema kuwa Serikali ya Muungano inathamini kazi zinazofanywa na wanawake Katika kuchochea maendeleo ya uchumi hivyo imekuwa akiwateu kushika nafasi mbalimbali za uongozi.

"Tunatambua juhudi za wanawake katika uongozi na sisi tupo nyuma yenu kuhakikisha hakuna anayebaki nyuma,lazima tushirikiane kufika mbali zaidi,"anasisitiza
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger