Monday, 8 May 2023

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE MEI 9,2023















Share:

Sunday, 7 May 2023

WAKAZI WA MBEYA WAIOMBA TCRA KUTOA ELIMU YA UTUMAJI USAFIRISHAJI WA MIZIGO NA VIPETO

Meneja wa Nyanda za Juu Kusini wa Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) Mhandisi Asajile John akizungumza na wananchi wa Jiji la Mbeya kuhusiana Utumaji wa Vifurushi na Vipeto ikiwa ni Kampeni ya TCRA Tuma Chap kwenye viunga vya jiji hilo la Mbeya.

*************

Na Mwandishi Wetu, Mbeya

WAKAZI wa mkoa wa Mbeya wameiomba Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) kusambaza zaidi elimu juu ya utumaji rasmi wa mizigo na vifurushi ili kuwanusuru wananchi wengi zaidi na upotevu wa mizigo.


Wakizungumza katika kampeni ya wazi ya uhamasishaji wa matumizi ya watoa huduma rasmi wakati wa kutuma mizigo wananchi hao wamesema mizigo migo inapotea kutokana na kutojua taratibu rasmi za kuwatambua watoa huduma wenye leseni.


Akizungumzia elimu hiyo mfanyabiashara Anangisye Mwakyoma amesema mara nyingi anapotaka kutuma mizigo huangalia basi ambalo analijua lakini baada ya kupata elimu hii atazingatia maelekezo ambayo yametolewa.


Akizungumzia faida ya elimu Bibi kisa Mwaipyana amesema iwapo angepata elimu hii tokea awali asingepoteza mzigo ambao alituma kwenye basi kupitia wakala ambaye hakuwa na ofisi.


Mch Elibariki Mmari ameishauri TCRA kuweka wazi sifa na vigezo vya wasafirishaji rasmi ili wananchi wawe wanaangali hivyo kabla ya kutuma mizigo yao.


Awali akitoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa kutumia watoa huduma wenye leseni wakati wa kusafirisha mizigo Meneja wa TCRA wa kanda ya nyanda za juu kusini Mha. Asajile John amesema TCRA inapotoa leseni hutoa pia masharti na vigezo ambavyo watoa huduma hao hutakiwa kuvizingatia.


Amevitaja vigezo hivyo kuwa ni pamoja na kampuni kiwa ofisi rasmi na kutoa risiti wanapoagiza ya mizigo wanauosafirisha.


Elimu hii ni sehemu ya kampeni ya tuma chap kwa usalama inayoendeshwa na TCRA nchi nzima kuelimisha wananchi umuhimu wa kutumia wasafirishaji wa mizigo waliosajiliwa.
Afisa Habari na Uhusiano Mwandamizi Mkuu Mabel Masasi wa Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) akigawa vipeperushi kwenye basi la Abiria (Daladala) Jijini la Mbeya ikiwa ni kampeni ya Tuma Chap ya Utumaji wa Vifurushi na Vipeto kwenye viunga vya jiji hilo la Mbeya.
Wananchi wakiangalia simu baada ya kupewa elimu kuhusianq na utumaji wa vifurushi na vipeti jijini Mbeya.
Afisa mkuu wa Abel John Masuala ya posta wa TCRA akitoa elimu kuhusiana na usafirishaji wa vifurushi na na Vipeto katika Viunga vya Mbeya ikiwa ni Kampeni ya TCRA Tuma Chap


Share:

MBUNGE MTATURU ATENGA MUDA KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI WAKE


MBUNGE wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu Mei 5,2023, amefanya ziara katika Vijijiji vya Choda na Mkiwa vilivyopo jimboni humo kwa lengo la kukagua miradi ya maendeleo,kuzungumza na kusikiliza kero za wananchi kupitia mikutano ya hadhara.

Ziara ya Mtaturu ni muendelezo wa utaratibu aliojiwekea wa kukagua miradi ya maendeleo na kuzungumza na wananchi ili kutoa fursa kwa wananchi kubainisha changamoto zao na yeye kwenda kuzisemea bungeni.

Akiwa katika ziara hiyo amekagua miradi kwenye shule ya sekondari Mkiwa ikiwemo ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa na chumba kimoja cha maabara vyote vikiwa na thamani ya Sh.Milioni 90.

Akizungumza na wananchi Mtaturu amesema serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan itaendelea kutoa fedha ili kutekeleza miradi kwenye sekta za Elimu,maji,Afya,miundombinu ya Maji,Umeme na barabara kama ilani ya uchaguzi inavyoelekeza.

Aidha,amesikiliza kero mbalimbali za wananchi zilizolenga hasa sekta ya ardhi ambapo wananchi wameeleza uwepo wa sintofahamu ya maeneo yao kutwaliwa bila wenyewe kushirikishwa na serikali ya Kijiji.

Katika mkutano huo wananchi walitaka kujua faida ya Mpango wa Matumizi Bora ya Ardhi na hasara zake na pia walitaka kujua faida za wawekezaji kwenye maeneo yao.

Baada ya kupokea maswali hayo Mbunge Mtaturu alimpa nafasi afisa ardhi wa wilaya ya Ikungi Ambrose Ngonyani ili atoe ufafanuzi wa kero na maswali waliyouliza wananchi.

Mzee Mathayo Dedu ambaye ni mkazi wa Kijiji hicho amelalamikia eneo lake kutwaliwa bila ridhaa yake na mwekezaji.

“Mzee wangu nimepokea kilio chako nimuelekeze Mtendaji Kata kumuandikia Mkurugenzi wa halamashauri kero hizo zilizotolewa ili zipatiwe majibu ndani ya siku saba,”amesema Mtaturu.

Kupitia mkutano huo amewahimiza wananchi kutunza ardhi kwa manufaa yao na vizazi vijavyo.

“Viongozi wa vijiji fanyeni mikutano ya kisheria ili kuwajulisha wananchi mipango ya serikali pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua nah ii ndio dhana ya utawala bora,”amesisitiza.

Akitoa neno la shukrani kwa niaba ya wananchi,Diwani wa Kata ya Mkiwa Petro Mtiana amemshukuru Rais Samia kwa kuwapelekea fedha za miradi mingi katika kata yao ikiwemo Sh Milioni 310 za kutengeneza barabara za Mkiwa hadi Damaina na Mkiwa hadi Choda zilizokuwa kero sana hasa kipindi cha mvua.

“Nikushukuru pia mbunge wetu Mtaturu kwa kutuwakilisha vyema bungeni,umekuwa mdomo wetu wa kutusemea,na kupitia wewe umeomba fedha za miradi ambapo kupitia mfuko wa jimbo tumeletewa Sh Milioni 3.5 kwenye shule za msingi za Choda na Darajani,ahsante sana,”ameshukuru Diwani Mtiana.
Share:

BABU ACHOMA NYUMBA, APOTEZA MAISHA NA WATOTO WAKE WATATU

 

Watu wanne familia moja wamefariki dunia kwa kuteketea na moto baada ya baba wa familia hiyo Aman Madumba (72), kujifungia chumbani na watoto hao kisha kuchoma nyumba moto.


Familia hiyo ya kijiji cha Malolo B kilichopo Wilayani Kilosa mkoani Morogoro inajumuisha baba huyo na watoto wake watatu ambao ni Habibu Aman (10), Sadick Aman (8) wote wa darasa la tatu na Bahati Aman (5).

 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, ACP Alex Mkama amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa uchunguzi unaendelea ili kubaini chanzo cha tukio hilo.

Mjukuu wa marehemu, Mwanjaa Madumba amesema majira ya saa saba usiku wa kuamkia leo Mei 5, 2023 akiwa amelala aliona moshi mkubwa chumbani kwake na alipotoka aligundua ulikuwa ukitokea upande wa chumba cha babu yake.

“Nilipiga kelele Watu wakafika na kuzima moto huo na walipofungua mlango wa chumbani walikuta wote wanne wameteketea na moto,” alisimulia mjukuu huyo huku ikidaiwa huenda msongo wa mawazo umesababisha hali hiyo kwani marehemu huyo alitengana na mkewe.
Share:

DUBE AIPELEKA AZAM FC FAINALI ASFC, YAITANDIKA SIMBA SC 2-1


NA EMMANUEL MBATILO

KLABU ya Simba imeondolewa kwenye hatua ya nusu fainali na Azam Fc kwa kupokea kichapo cha mabao 2-1 kwenye mchezo huo ambao uliopigwa kwenye dimba la Nangwanda mkoani Mtwara.

Katika Mchezo huo Azam Fc walianza kupata bao dakika ya 22 kupitia kwa mlinzi wao wa kulia Lusajo Mwaikenda kabla ya Simba kusawazisha kupitia kwa Sadio Kanout dakika ya 28 ya mchezo na kwenda mapumziko matokeo yakiwa 1-1.

Kipindi cha pili Azam Fc waliingia uwanjani kwa kushambulia zaidi kwani walitengeneza nafasi nyingi za magoli bila mafaniko.

Azam Fc ilifanya mabadiliko kwa baadhiya wachezaji wao ambapo mbadiliko yalizaa matunda kwani alitoka Idris Mbombo na nafasi yake kuchukuliwa na Prince Dube ambaye alipachika bao kali ambalo liliwapa matokeo ya ushindi wa 2-1 na kutinga hatua ya Fainali ambayo itapigwa kwenye dimba la Mkwakwani Tanga.


Share:

WAZIRI DKT MABULA ATAKA WANANCHI TARIME KUACHA KUISHI KWA MAZOEA NA KUFUATA SHERIA

Mkuu wa mkoa wa Mara Meja Jenerali Suleiman Mzee (wa pili kushoto) akiwaonesha Mawaziri Dkt Angeline Mabula, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi (wa tatu kushoto), Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Angellah Kairuki (wa kwanza kushoto) na Naibu Waziri wa Maliasili Mary Masanja (wan ne kushoto) wakati mawaziri hao walipofanya ziara wilayani Tarime tarehe 6 Mei 2023.


****************

Na Munir Shemweta, WANMM TARIME

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amewataka wananchi wa Kegonga na Karakatonga wilayani Tarime mkoa wa Mara kuacha kuishi kwa mazoea na kufuata sheria ili kuepuka migogoro baina ya vijiji hivyo na maeneo ya hifadhi.

Dkt Mabula amesema hayo tarehe 6 Mei 2023 katika kijiji cha Kegonga kitongoji cha Lisolya kata ya Nyanungu wilayani Tarime, wakati timu ya mawaziri watatu ilipotembelea eneo hilo ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya waziri Mkuu Mhe. Kasim Majaliwa kuwataka mawaziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Maliasili na Utalii pamoja na Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwenda kutafuta ufumbuzi wa migogoro ya ardhi kwenye wilaya za Tarime na Serengeti mkoani Mara.

Mawaziri waliotembelea vijiji hivyo ni Angellah Kairuki, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula pamoja na na Naibu Waziri wa Malisili na Utalii Mary Masanja.

Vijiji vilivyopo kwenye mgogoro na eneo la Hifadhi ya Serengeti wilayani Tarime mkoa wa Mara ni Kegonga, Nyandage, Masanga, Karakatonga, Gobaso, Nyabirongo pamoja na Kenyamosabi.

Dkt Mabula amewaambia wananchi wa vijiji hivyo kuwa, kitendo cha timu ya mawaziti watatu kwenda eneo la mpaka lenye mgogoro ni ishara kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan amewaheshimu wananchi wa maeneo hayo.

‘’Hivi ni vijiji vingapi tumekwenda mpaka kwenye alama za mpaka (Beacon), mnakaa mezani mnasoma then watu wanajua hapa ni pale lakini hapa tumekuwa akina tomaso tumekuja hadi hapa lakini hilo hamlioni kama Mhe. Rais amewaheshimu sana, ndugu zangu hebu tuache kuishi kwa mazoea tufuate sheria’’ alisema Dkt Mabula.

Amewataka wananchi wa mkoa wa Mara kuacha ubishi na kufuata sheria huku akiwatahadharisha dhidi ya watu wanaokwenda kuwadanganya na kueleza watu hao wana lengo la kutafuta kura wakati wa uchaguzi na kueleza kuwa iwapo wataishi kwa kukubali kudanganywa waelewe kuwa mpaka baina ya vijiji hivyo na hifadhi utaendelea kubaki kama ulivyo.

Amewaomba wananchi wa vijiji hivyo kuheshimu kile ambacho kipo kwa mujibu wa sheria na kueleza kuwa GN 265 ya mwaka 1968 ambayo wao wanaitambua ndiyo iliyotafsiriwa na si vinginevyo na kuhoji wanachoshangaa ni kitu gani.

Aidha, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi alisema, eneo la ukingo yaani Buffer zone la mita 500 ambalo Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassana ameridhia kuachiwa vijiji husika katika eneo hilo ambapo ameagiza kufanyiwa mpango wa matumizi bora ya ardhi kupitia wataalamu.

Amewaonya wananchi wa maeneo yenye mgogoro na hifadhi kuwa kwa kuwaeleza kuwa, iwapo wataendelea kubishana kuhusiana na mpaka kila siku basi hakutakuwa na maendeleo na kusisitiza kwamba ni vizuri kuacha kufanya kazi kwa mabishano.

Kwa mujibu wa Dkt Mabula, tafsiri sahihi kuhusiana na alama ya mpaka imetolewa na kusisitiza kuwa alama hiyo inapaswa kuheshimiwa ingawa baadhi ya wananchi wanaweza kuuma lakini hiyo ndiyo tafsiri sahihi iliyosomwa neno kwa neno na kuweka wazi kuwa, kinachotakiwa ni kutokuwa na ubishi na kukubali uanzishwaji wa hifadhi na mipaka iliyowekwa sambamba na ile inayoenda kubadilika.

Serikali kupitia wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeweka jumla ya alama 176 za mipaka katikati ya Alama Kuu Nane zilizotangazwa kupitia GN 235 ya mwaka 1968 ili alama za mipaka ziweze kuonekana vizuri kwa wananchi.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula (katikati aliyevaa miwani) akiwaongoza mawaziri wenzake kuangalia ramani wakati walipotembelea eneo lenye mgogoro la Kegonga wilayani Tarime mkoa wa Mara tarehe 6 Mei 2023.
Waziri wa Ardhi Dkt Angeline Mabula (wa tatu kulia), Waziri wa TAMISEMI Angellah Kairuki (wa tatu kushoto), Naibu Waziri Maliasili na Utalii Mary Masanja (wa pili kushoto), Mbunge wa jimbo la Tarime Mwita Waitara (wa kwanza kulia) wakielekea kukagua alama ya mpaka katika kijiji cha Kegonga wilayani Tarime mkoa wa Mara.
Waziri wa Ardhi Dkt Angeline Mabula akielekea kijiji cha Kegonga kitongoji cha Lisolya kata ya Nyanungu wilayani Tarime mkoa wa Mara wakati timu ya mawaziri watatu ilipokwenda kutafuta ufumbuzi wa mgogoro wa mpaka katika eneo hilo tarehe 6 Mei 2023.
Waziri wa Ardhi Dkt Angeline Mabula na Waziri wa TAMISEMI Angellah Kairuki wakitoka kukagua alama ya mpaka katika kijiji cha Kegonga kitongoji cha Lisolya kata ya Nyanungu wilayani Tarime mkoa wa Mara wakati timu ya mawaziri watatu ilipokwenda kutafuta ufumbuzi wa mgogoro wa mpaka katika eneo hilo Mei 6, 2023.
Waziri wa Ardhi Dkt Angeline Mabula na Mkuu wa mkoa wa Mara Meja Jenerali Suleiman Mzee wakiangalia muelekeo wa mpaka katika kijiji cha Kegonga wilayani Tarime mkoa wa Mara wakati timu ya mawaziri watatu ilipokwenda kutafuta ufumbuzi wa mgogoro wa mpaka katika eneo hilo tarehe 6 Mei 2023. (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)
Share:

SHULE YA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM YA BUHANGIJA YAPATA MSAADA WA DOLA 10,000 KUTOKA SHIRIKA LA NVeP KWA UFADHILI WA BARRICK


Meneja Mkuu wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu,Cheick Sangare (wa pili kutoka kulia),akimkabidhi msaada wa hundi ya dola 10,000 kwa Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi ya watoto wenye mahitaji maalum ya Buhangija iliyopo katika manispaa ya shinyanga,Fatuma Gilalah (wa nne kutoka kulia) na Afisa elimu ya msingi,Mary Maka (wa tatu kutoka kushoto mwenye miwani) . Msaada huo umetokana na sehemu ya fedha zilizotolewa na taasisi ya Nos Vies en Partage (NVeP), inayofadhiliwa na Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Barrick Gold Corporation, Mark Bristow.Wengine pichani ni wafanyakazi wa Barrick na wawakilishi wa wanafunzi wa shule hiyo.Hafla ya kukabidhi msaada huo ilifanyika katika mgodi wa Bulyanhulu.
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Cheick Sangare (wa pili kutoka kulia), akimkabidhi msaada wa hundi ya dola 10,000 kwa Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi ya watoto wenye mahitaji maalum ya Buhangija iliyopo katika manispaa ya shinyanga,Fatuma Gilalah na Afisa elimu ya msingi,Mary Maka ( mwenye miwani) .Msaada huo umetokana na sehemu ya fedha zilizotolewa na taasisi ya Nos Vies en Partage (NVeP), inayofadhiliwa na Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Barrick Gold Corporation, Mark Bristow.Wengine pichani ni wafanyakazi wa Barrick.
Afisa Mwandamizi wa Mahusiano ya Jamii wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu akitoa utambulisho kwa wageni wakati wa hafla hiyo.
Meneja Mkuu wa Barrick Bulyanhulu,Cheick Sangare akiwa na Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Buhangija, Fatuma Gilalah na Afisa Elimu ya Msingi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga,Mary Maka (Kushoto)
Baadhi ya wanafunzi wanaosoma katika shule ya Buhangija pia walihudhuria katika hafla hiyo.
***

Shirika la ya Nos Vies en Partage (NVeP) kwa kushirikiana na kampuni ya Barrick,wametoa msaada wa dola za Kimarekani 10,000 kwa shule ya msingi ya watoto wenye mahitaji maalum ya Buhangija iliyopo mkoani Shinyanga kwa ajili ya kuboresha mazingira ya kusomea ya wanafunzi wa shule hiyo.



Msaada huo umetokana na sehemu ya fedha zilizotolewa na taasisi ya Nos Vies en Partage (NVeP), iliyoanzishwa na inayofadhiliwa na Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Barrick Gold Corporation, Mark Bristow, kwa ajili ya kusaidia makundi maalum kama vile Wanawake,watoto na makundi mengine yenye uhitaji yasiofaidika na ukuaji wa kiuchumi barani Afrika.



Akiongea wakati wa hafla ya kukabidhi msaada huo iliyofanyika katika Mgodi wa Bulyanhulu wilayani Msalala, Meneja Mkuu wa Mgodi huo,Cheick Sangare, alisema kila robo ya mwaka,taasisi imeweza kutoa misaada yenye tija na manufaa ya moja kwa moja kwenye jamii zenye uhitaji.



"Hadi sasa tumeweza kutoa msaada kwa zaidi ya mashirika 10 nchini Tanzania kupitia taasisi ya NVeP, leo tuko hapa kuleta mabadiliko kwa shule ya msingi Buhangija ambayo inatoa elimu kwa watoto wenye mahitaji maalum kwa kuipatia msaada wa dola za kimarekani 10, kwa ajili ya kuboresha mazingira ya wanafunzi kupata elimu", alisema Sangare.

Akiongea baada ya kupokea hundi ya fedha za msaada huo, Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Fatuma Gilalah, aliyeongozana na na Afisa Elimu ya Msingi wa Manispaa ya Shinyanga Mary Maka, alishukuru  kwa msaada huo ambao alisema kuwa utasaidia kutatua changamoto mbalimbali kwa ajili ya kuboresha mazingira ya wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo.

Alisema pamoja na jitihada kubwa zinazofanywa na Serikali kuboresha mazingira ya kuwapatia elimu watoto wenye mahitaji maalum wanaosoma katika shule hiyo bado kuna changamoto mbalimbali kwa upande wa miondombinu na vifaa vya kufundishia.

“Tunashukuru kwa msaada huu tuliopokea siku ya leo kutoka Barrick na utasaidia kuboresha mazingira ya kusomea ya wanafunzi wetu”, alisema Gilalah.

Alisema shule hiyo inatoa elimu elimu kwa wanafunzi wenye ulemevu wa ngozi (wenye ualbino), wasioona na wenye usikivu hafifu vizuri (viziwi).


Share:

Saturday, 6 May 2023

SERIKALI KUENDELEA KUFANYA MABORESHO KWENYE SEKTA YA MISITU NA NYUKI .


SERIKALI imesema itaendelea kufanya maboresho mbalimbali kwenye Sekta ya Misitu na Nyuki ikiwa ni pamoja na kufanya marekebisho kwenye Sera, Sheria, Miongozo na Kanuni ili kuongeza ufanisi na mchango wa sekta hizo kwenye Pato la Taifa.

Kiongozi wa ziara ya Mafunzo ya Utekelezaji wa Sera ya Misitu na Sera ya Ufugaji Nyuki kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, Emmanuel Msoffe amesema hayo wakati wa mafunzo ya Wadau wa Sekta za Misitu pamoja na Nyuki katika Wilaya za Kibiti, Rufiji na kilwa na ambapo amewataka wadau hao wayatumie mafunzo hayo kuleta mabadiliko chanya yenye kuongeza mchango kwenye uchumi wa nchi.

“Tumekamilisha mafunzo ya kutoa elimu na kuangalia maeneo ambayo kisera, kisheria, kimuongozo na kikanuni yapo lakini hayafanyi vizuri Kuna mambo mengi ambayo tumeyaona yanahitaji maboresho, kurudiwa ama kubadilishwa kabisa ili kuendana na hali halisi ya ndani”

Kwa upande wake Mkazi wa Kilwa Masoko, Hashim Hassan ameipongeza TFS kwa kuwapa elimu ya Ufugaji nyuki ambayo imewaongezea kipato huku Mwanaidi Issa ambaye ni Mdau wa Misitu Wilayani Kilwa akiishukuru Wizara ya Maliasili na Utalii kwa mafunzo hayo ikizingatiwa kuwa kwa sasa mazao ya misitu yamesaidia kubadilisha maisha yao na kuwawezesha kununua usafiri, kuweka mifumo ya umeme wa jua na kujenga Zahanati.

"Tunaishukuru sana Serikali kwa kututhamini na kutujali kwani elimu hii tunayoipata tutaisambaza kwa wenzetu ambao hawajapata bahati ya kushiriki mafunzo haya" amesema Mwanaidi

Aidha, ameongeza kuwa kitendo cha Wizara kuendelea kuwapatia mafunzo kinawaongezea elimu ambayo inawasaidia kufanya vizuri zaidi katika sekta hiyo.



Share:

ORYX GAS KUENDELEA KUIUNGA TULIA TRUST MASHINDANO YA MBIO ILI KUPATA FEDHA KUSAIDIA WATOTO WA KIKE MBEYA




Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Oryx Gas Tanzania Arama Benoit akishiriki mbio za kilomita tano katika mashindano ya Tulia Marathoni yaliyofanyika jijini Mbeya kwa lengo la kukusanya fedha kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya afya na elimu yaliyofanyika jijini Mbeya na kampuni ya Oryx Gas wakiwa wadhamini wenzi katika mashinadno hayo ukiwa ni msimu wa saba.

******************

Na Mwandishi Wetu, Mbeya

KAMPUNI ya Oryx Gas imesema itaendelea kuiunga mkono Taasisi ya Tulia Trust katika mashindano ya riadha inayoyaratibu kwa kuwa malengo yake yanafanana na ya kampuni hiyo katika kuisaidia jamii.

Mkurugenzi Mtendaji wa Oryx Gas Tanzania Benoite ameeleza hayo leo Mei 6,2023 baada ya kuwaongoza wafanyakazi wa kampuni hiyo kushiriki mashindano ya riadha yaliyoratibiwa na Taasisi ya tulia Trust na yaliyofanyika jijini Mbeya.

Amesema kuwa Oryx Gas kwa kipindi kirefu imejikita katika huduma za jamii hususani zinazohusu kuisaidia jamii ya Watanzania na zaidi mtoto wa kike kwa kuhakikisha anaondokana na changamoto mbalimbali ,hivyo wameona iko haja kuungana na Tulia Trust katika kumsaidia mtoto wa kike katika afya na elimu ndani ya Mkoa huo.

Akieleza zaidi kuhusu ushiriki wao katika mbizo hizo Araman amefafanua kuwa Kampuni ya Oryx Gas imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha wanashirikiana na Serikali katika kumuondolea changamoto mwanamke ,hivyo kwenye mashindano ya mbio hizo ni wazi malengo ya taasisi hiyo yanafanana na yao,hivyo wataendelea kuunga mkono.

Amefafanua katika kutekeleza hilo kwa vitendo Kampuni ya Oryx imekuwa na kampeni ya kuhamasisha nishati safi ya kupikia kwa kugawa majiko na mitungi ya gesi kwa wanawake wa mikoa mbalimbali ambapo hadi sasa wamewafikia zaidi ya 5,000, lengo ni kuhakikisha wanaachana na matumizi ya kuni na mkaa.

"Hivyo tunapoona Taasisi ya Tulia Trust inandaa mbio za kuchangisha fedha kuisaidia jamii ya mtoto wa kike, sisi tunaona ni wajibu wetu kusaidia kwa kufadhili ili mambo yaende kama yalivyopangwa na fedha zinazopatikana zinakwenda kugusa maisha ya wenye uhitaji, tutaendelea kushirikiana na taasisi hii itimize malengo yake," amesema

Baadhi ya Wafanyakazi wa Oryx Gas wakiongozwa na Benoite wameshiriki mbizo hizo huku mkurugenzi mtendaji huyo akieleza jinsi Kampuni hiyo inavyofurahishwa na hatua zinazochukuliwa na Tulia Trust katika kusaidia kutatua changamoto zinazoikabili jamii ya Watanzania.


Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Oryx Gas Tanzania Arama Benoit kulia akivishwa medali baada ya kukimbia mbiop za kilomita tano katika mashindano ya Tulia Marathoni yaliyofanyika jijini Mbeya kwa lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya afya na elimu Mkoani Mbeya na kampuni ya Oryx Gas wakiwa wadhamini wenzi katika mashinadno hayo ambayo ni msimu wa saba.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Oryx Gas Tanzania Arama Benoit wa pili kushioto akiwa na baadhi ya wabunge baada kushiriki kilomita tano katika mashindano ya Tulia Marathoni yaliyofanyika jijini Mbeya kwa lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya afya na elimu yaliyofanyika jijini Mbeya na kampuni ya Oryx Gas wakiwa wadhamini wenzi katika mashinadno hayo ukiwa ni msimu wa saba.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Oryx Gas Tanzania Arama Benoit akiwa na baadhi wa watumishi wa kampuni hiyo walioshiriki mbio za kilomita tano katika mashindano ya Tulia Marathoni yaliyofanyika jijini Mbeya kwa lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya afya na elimu yaliyofanyika jijini Mbeya na kampuni ya Oryx Gas wakiwa wadhamini wenzi katika mashinadno hayo ukiwa ni msimu wa saba.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger