Sunday, 7 May 2023

SHULE YA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM YA BUHANGIJA YAPATA MSAADA WA DOLA 10,000 KUTOKA SHIRIKA LA NVeP KWA UFADHILI WA BARRICK


Meneja Mkuu wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu,Cheick Sangare (wa pili kutoka kulia),akimkabidhi msaada wa hundi ya dola 10,000 kwa Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi ya watoto wenye mahitaji maalum ya Buhangija iliyopo katika manispaa ya shinyanga,Fatuma Gilalah (wa nne kutoka kulia) na Afisa elimu ya msingi,Mary Maka (wa tatu kutoka kushoto mwenye miwani) . Msaada huo umetokana na sehemu ya fedha zilizotolewa na taasisi ya Nos Vies en Partage (NVeP), inayofadhiliwa na Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Barrick Gold Corporation, Mark Bristow.Wengine pichani ni wafanyakazi wa Barrick na wawakilishi wa wanafunzi wa shule hiyo.Hafla ya kukabidhi msaada huo ilifanyika katika mgodi wa Bulyanhulu.
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Cheick Sangare (wa pili kutoka kulia), akimkabidhi msaada wa hundi ya dola 10,000 kwa Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi ya watoto wenye mahitaji maalum ya Buhangija iliyopo katika manispaa ya shinyanga,Fatuma Gilalah na Afisa elimu ya msingi,Mary Maka ( mwenye miwani) .Msaada huo umetokana na sehemu ya fedha zilizotolewa na taasisi ya Nos Vies en Partage (NVeP), inayofadhiliwa na Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Barrick Gold Corporation, Mark Bristow.Wengine pichani ni wafanyakazi wa Barrick.
Afisa Mwandamizi wa Mahusiano ya Jamii wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu akitoa utambulisho kwa wageni wakati wa hafla hiyo.
Meneja Mkuu wa Barrick Bulyanhulu,Cheick Sangare akiwa na Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Buhangija, Fatuma Gilalah na Afisa Elimu ya Msingi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga,Mary Maka (Kushoto)
Baadhi ya wanafunzi wanaosoma katika shule ya Buhangija pia walihudhuria katika hafla hiyo.
***

Shirika la ya Nos Vies en Partage (NVeP) kwa kushirikiana na kampuni ya Barrick,wametoa msaada wa dola za Kimarekani 10,000 kwa shule ya msingi ya watoto wenye mahitaji maalum ya Buhangija iliyopo mkoani Shinyanga kwa ajili ya kuboresha mazingira ya kusomea ya wanafunzi wa shule hiyo.



Msaada huo umetokana na sehemu ya fedha zilizotolewa na taasisi ya Nos Vies en Partage (NVeP), iliyoanzishwa na inayofadhiliwa na Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Barrick Gold Corporation, Mark Bristow, kwa ajili ya kusaidia makundi maalum kama vile Wanawake,watoto na makundi mengine yenye uhitaji yasiofaidika na ukuaji wa kiuchumi barani Afrika.



Akiongea wakati wa hafla ya kukabidhi msaada huo iliyofanyika katika Mgodi wa Bulyanhulu wilayani Msalala, Meneja Mkuu wa Mgodi huo,Cheick Sangare, alisema kila robo ya mwaka,taasisi imeweza kutoa misaada yenye tija na manufaa ya moja kwa moja kwenye jamii zenye uhitaji.



"Hadi sasa tumeweza kutoa msaada kwa zaidi ya mashirika 10 nchini Tanzania kupitia taasisi ya NVeP, leo tuko hapa kuleta mabadiliko kwa shule ya msingi Buhangija ambayo inatoa elimu kwa watoto wenye mahitaji maalum kwa kuipatia msaada wa dola za kimarekani 10, kwa ajili ya kuboresha mazingira ya wanafunzi kupata elimu", alisema Sangare.

Akiongea baada ya kupokea hundi ya fedha za msaada huo, Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Fatuma Gilalah, aliyeongozana na na Afisa Elimu ya Msingi wa Manispaa ya Shinyanga Mary Maka, alishukuru  kwa msaada huo ambao alisema kuwa utasaidia kutatua changamoto mbalimbali kwa ajili ya kuboresha mazingira ya wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo.

Alisema pamoja na jitihada kubwa zinazofanywa na Serikali kuboresha mazingira ya kuwapatia elimu watoto wenye mahitaji maalum wanaosoma katika shule hiyo bado kuna changamoto mbalimbali kwa upande wa miondombinu na vifaa vya kufundishia.

“Tunashukuru kwa msaada huu tuliopokea siku ya leo kutoka Barrick na utasaidia kuboresha mazingira ya kusomea ya wanafunzi wetu”, alisema Gilalah.

Alisema shule hiyo inatoa elimu elimu kwa wanafunzi wenye ulemevu wa ngozi (wenye ualbino), wasioona na wenye usikivu hafifu vizuri (viziwi).


Share:

Saturday, 6 May 2023

SERIKALI KUENDELEA KUFANYA MABORESHO KWENYE SEKTA YA MISITU NA NYUKI .


SERIKALI imesema itaendelea kufanya maboresho mbalimbali kwenye Sekta ya Misitu na Nyuki ikiwa ni pamoja na kufanya marekebisho kwenye Sera, Sheria, Miongozo na Kanuni ili kuongeza ufanisi na mchango wa sekta hizo kwenye Pato la Taifa.

Kiongozi wa ziara ya Mafunzo ya Utekelezaji wa Sera ya Misitu na Sera ya Ufugaji Nyuki kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, Emmanuel Msoffe amesema hayo wakati wa mafunzo ya Wadau wa Sekta za Misitu pamoja na Nyuki katika Wilaya za Kibiti, Rufiji na kilwa na ambapo amewataka wadau hao wayatumie mafunzo hayo kuleta mabadiliko chanya yenye kuongeza mchango kwenye uchumi wa nchi.

“Tumekamilisha mafunzo ya kutoa elimu na kuangalia maeneo ambayo kisera, kisheria, kimuongozo na kikanuni yapo lakini hayafanyi vizuri Kuna mambo mengi ambayo tumeyaona yanahitaji maboresho, kurudiwa ama kubadilishwa kabisa ili kuendana na hali halisi ya ndani”

Kwa upande wake Mkazi wa Kilwa Masoko, Hashim Hassan ameipongeza TFS kwa kuwapa elimu ya Ufugaji nyuki ambayo imewaongezea kipato huku Mwanaidi Issa ambaye ni Mdau wa Misitu Wilayani Kilwa akiishukuru Wizara ya Maliasili na Utalii kwa mafunzo hayo ikizingatiwa kuwa kwa sasa mazao ya misitu yamesaidia kubadilisha maisha yao na kuwawezesha kununua usafiri, kuweka mifumo ya umeme wa jua na kujenga Zahanati.

"Tunaishukuru sana Serikali kwa kututhamini na kutujali kwani elimu hii tunayoipata tutaisambaza kwa wenzetu ambao hawajapata bahati ya kushiriki mafunzo haya" amesema Mwanaidi

Aidha, ameongeza kuwa kitendo cha Wizara kuendelea kuwapatia mafunzo kinawaongezea elimu ambayo inawasaidia kufanya vizuri zaidi katika sekta hiyo.



Share:

ORYX GAS KUENDELEA KUIUNGA TULIA TRUST MASHINDANO YA MBIO ILI KUPATA FEDHA KUSAIDIA WATOTO WA KIKE MBEYA




Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Oryx Gas Tanzania Arama Benoit akishiriki mbio za kilomita tano katika mashindano ya Tulia Marathoni yaliyofanyika jijini Mbeya kwa lengo la kukusanya fedha kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya afya na elimu yaliyofanyika jijini Mbeya na kampuni ya Oryx Gas wakiwa wadhamini wenzi katika mashinadno hayo ukiwa ni msimu wa saba.

******************

Na Mwandishi Wetu, Mbeya

KAMPUNI ya Oryx Gas imesema itaendelea kuiunga mkono Taasisi ya Tulia Trust katika mashindano ya riadha inayoyaratibu kwa kuwa malengo yake yanafanana na ya kampuni hiyo katika kuisaidia jamii.

Mkurugenzi Mtendaji wa Oryx Gas Tanzania Benoite ameeleza hayo leo Mei 6,2023 baada ya kuwaongoza wafanyakazi wa kampuni hiyo kushiriki mashindano ya riadha yaliyoratibiwa na Taasisi ya tulia Trust na yaliyofanyika jijini Mbeya.

Amesema kuwa Oryx Gas kwa kipindi kirefu imejikita katika huduma za jamii hususani zinazohusu kuisaidia jamii ya Watanzania na zaidi mtoto wa kike kwa kuhakikisha anaondokana na changamoto mbalimbali ,hivyo wameona iko haja kuungana na Tulia Trust katika kumsaidia mtoto wa kike katika afya na elimu ndani ya Mkoa huo.

Akieleza zaidi kuhusu ushiriki wao katika mbizo hizo Araman amefafanua kuwa Kampuni ya Oryx Gas imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha wanashirikiana na Serikali katika kumuondolea changamoto mwanamke ,hivyo kwenye mashindano ya mbio hizo ni wazi malengo ya taasisi hiyo yanafanana na yao,hivyo wataendelea kuunga mkono.

Amefafanua katika kutekeleza hilo kwa vitendo Kampuni ya Oryx imekuwa na kampeni ya kuhamasisha nishati safi ya kupikia kwa kugawa majiko na mitungi ya gesi kwa wanawake wa mikoa mbalimbali ambapo hadi sasa wamewafikia zaidi ya 5,000, lengo ni kuhakikisha wanaachana na matumizi ya kuni na mkaa.

"Hivyo tunapoona Taasisi ya Tulia Trust inandaa mbio za kuchangisha fedha kuisaidia jamii ya mtoto wa kike, sisi tunaona ni wajibu wetu kusaidia kwa kufadhili ili mambo yaende kama yalivyopangwa na fedha zinazopatikana zinakwenda kugusa maisha ya wenye uhitaji, tutaendelea kushirikiana na taasisi hii itimize malengo yake," amesema

Baadhi ya Wafanyakazi wa Oryx Gas wakiongozwa na Benoite wameshiriki mbizo hizo huku mkurugenzi mtendaji huyo akieleza jinsi Kampuni hiyo inavyofurahishwa na hatua zinazochukuliwa na Tulia Trust katika kusaidia kutatua changamoto zinazoikabili jamii ya Watanzania.


Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Oryx Gas Tanzania Arama Benoit kulia akivishwa medali baada ya kukimbia mbiop za kilomita tano katika mashindano ya Tulia Marathoni yaliyofanyika jijini Mbeya kwa lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya afya na elimu Mkoani Mbeya na kampuni ya Oryx Gas wakiwa wadhamini wenzi katika mashinadno hayo ambayo ni msimu wa saba.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Oryx Gas Tanzania Arama Benoit wa pili kushioto akiwa na baadhi ya wabunge baada kushiriki kilomita tano katika mashindano ya Tulia Marathoni yaliyofanyika jijini Mbeya kwa lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya afya na elimu yaliyofanyika jijini Mbeya na kampuni ya Oryx Gas wakiwa wadhamini wenzi katika mashinadno hayo ukiwa ni msimu wa saba.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Oryx Gas Tanzania Arama Benoit akiwa na baadhi wa watumishi wa kampuni hiyo walioshiriki mbio za kilomita tano katika mashindano ya Tulia Marathoni yaliyofanyika jijini Mbeya kwa lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya afya na elimu yaliyofanyika jijini Mbeya na kampuni ya Oryx Gas wakiwa wadhamini wenzi katika mashinadno hayo ukiwa ni msimu wa saba.
Share:

WAZIRI JAFO ARIDHISHWA UTEKELEZAJI MIRADI YA KUHIMILI MABADILIKO YA TABIA NCHI WILAYANI KISHAPU

 


Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Seleman Jafo akiwa wilayani Kishapu kuangalia utekelezaji wa miradi ya kuhimili mabadiliko ya tabia nchi.

Na Marco Maduhu, KISHAPU

WAZIRI wanchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dk. Seleman Jafo, ameeleza kuridhishwa na utekelezaji wa miradi ya kuhimili mabadiliko ya tabia nchi (EBARR) wilayani Kishapu.

Jafo amebainisha hayo leo Mei 6,2023 wakati alipofanya ziara wilayani Kishapu, kutembelea kuona utekelezaji wa miradi hiyo ya kuhimili mabadiliko ya tabia nchi.

Amesema katika ziara yake wilayani Kishapu ya kutembelea miradi hiyo ya kuhimili mabadiliko ya tabia nchi, ameridhika nayo baada ya kuona imetekelezwa vizuri, huku akiagiza kwa ile ambayo bado haijakamilika ikamilike haraka kabla ya mwaka wa fedha mwezi Julai iwe tayari na kuanza kutumika.

“Nimeridhika na ziara yangu hapa Kishapu nimeona miradi iko vizuri, na Rais Samia anapoona miradi ambayo anatoa fedha inatekelezwa vizuri anafarijika sana,”anasema Waziri Jafo.

“Naomba wananchi muitumie vyema miradi hii kwa tija, pamoja na kutunza mazingira kwa kupanda miti,”ameongeza.

Aidha, Miradi ambayo Waziri Jafo ameitembea ya kuhimili mabadiliko ya tabia nchi pamoja na mingine kuweka jiwe la msingi na kuzindua ni Mradi wa unenepeshaji Mifugo katika Kijiji cha Muguda, na kuweka jiwe la msingi katika jengo la kusaga mahidi na kukamua Alzeti, Bwawa la Maji Kijiji cha Kiloleli na Kiwanda cha kutengeneza bidhaa za ngozi vikiwamo viatu.

Miradi mingine ambayo inatekelezwa ni ujenzi wa Majosho, Majiko Banifu yatakayosaidia kupunguza matumizi ya kuni, ufugaji wa nyuki, na kilimo zao la Mkonge,

Anesema Serikali imetoa fedha kwa ajili ya kutekelezwa miradi hiyo ya kuhimili mabadiliko ya tabia nchi, ili wananchi wawe na shughuli mbadala za kufanya ambazo zitawaingizia kipato na kuacha kuharibu mazingira kwa kukata miti hovyo ikiwamo kufanya biashara za kuchoma mikaa.

Katika hatua nyingine Waziri Jafo, ameziagiza halmashauri zote hapa nchini kutekeleza agizo la upandaji miti Milioni 1.5 kwa kila mwaka, pamoja na kuihamasisha kampeni ya soma na mti ambayo kila mwanafunzi anapaswa kupanda mti.

Naye Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude, amesema Serikali ilipeleka kiasi cha fedha Sh.bilioni 1.4 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hiyo ya kuhimili mabadiliko ya tabia nchi. ambayo inatekelezwa katika Kata mbili ya Lagana na Kiloleli, na imekuwa na tija kwa wananchi katika suala zima la utunzaji wa Mazingira.

Nao baadhi ya wananchi ambao ni wanufaika wa miradi hiyo, wameishukuru Serikali kwamba licha ya kutunza mazingira, pia imekuwa ikiwasaidia kuwaingizia kipato na kuendesha maisha yao.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Seleman Jafo akizungumza wilayani Kishapu akiwa kwenye ukaguzi wa miradi ya kuhimili mabadiliko ya tabia nchi, pamoja na baadhi kuweka jiwe la msingi na mingine kuizindua.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Seleman Jafo akizungumza wilayani Kishapu akiwa kwenye ukaguzi wa miradi ya kuhimili mabadiliko ya tabia nchi, pamoja na baadhi kuweka jiwe la msingi na mingine kuizindua.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude akizungumza kwenye ziara hiyo ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Seleman Jafo ya kutembelea na kukagua utekelezaji wa miradi ya kuhimili mabadiliko ya tabia nchi.
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu Anderson Mandia akizungumza kwenye ziara hiyo ya Waziri Jafo.
Mratibu wa mradi wa kuhimili mabadiliko ya tabia nchi (EBARR)wilayani Kishapu Godwin Everygist akitoa taarifa juu ya utekelezaji wa miradi hiyo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Seleman Jafo (kushoto) akiweka jiwe la msingi katika Jengo la Mashine ya Alizeti na kusaga Mahindi katika kijiji cha Muguda, mradi ambao utatumika pia kunenepesha mifugo kupitia mapumba.
Muonekano wa jiwe la msingi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Seleman Jafo akipanda mti mara baada ya kumaliza kuweka jiwe la msingi jengo la mashine ya kukamua Alizetu na kusaga Mahindi, katika mradi wa kunenepesha mifugo kupitia pumba.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Seleman Jafo (kushoto) akizindua kwianda kidogo cha kutengeneza bidhaa za ngozi.
Muonekano wa jiwe la msingi la uzindizi wa kiwanda hicho cha kutengeneza bidhaa za ngozi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Seleman Jafo (kushoto) akiangalia bidhaa mbalimbali ambazo zimetengenezwa kwa ngozi.
Muonekano wa viatu ambavyo vimetengenezwa kwa kutumia ngozi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Seleman Jafo akiangalia kiatu ambacho kimetengenezwa kwa ngozi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Seleman Jafo akiwa amevaa viatu ambavyo amevinunua vilivyotengenezwa kwa ngozi na kutoa wito kwa wananchi wa Kishapu na Taasisi za Serikali kukiunga mkono kikundi hicho na kununua viatu.
Muonekano wa bwawa la maji ambalo limetekelezwa katika kijiji cha Kiloleli katika mradi wa kuhimili mabadiliko ya tabia nchi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Seleman Jafo (kushoto) awali akiwasili wilayani Kishapu akisalimiana na viongozi mbalimbali (kulia) ni Mkurugenzi wa Halamshauri ya Kishapu Emmanuel Jonhson, akifuatiwa na Makamu mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Anderson Mandia.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Seleman Jafo (kushoto)akiendelea kusalimiana na viongozi mbalimbali alipowasili wilayani Kishapu.
Share:

TEKELEZENI MAJUKUMU KUINUFAISHA SERIKALI

Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Boniphace Luhende akifunga mafunzo elekezi kwa waajiriwa wapya (hawapo pichani) wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kuhusu sheria, taratibu na kanuni za utumishi wa umma. Mafunzo hayo ya siku mbili yamefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Cha Uongozi wa Mwalimu Nyerere Kibaha mkoani Pwani.

****************

Watumishi wapya wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali (OWMS) wametakiwa kutumia elimu waliyoipata na fursa ya ajira ya Serikali kutekeleza majukumu yao kwa manufaa ya Serikali na Taifa kwa ujumla.

Hayo yameelezwa leo na Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Boniphace Luhende wakati akifunga mafunzo ya siku mbili yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Nyerere kilichopo Kibaha mkoani Pwani kwa lengo la kuwajengea uwezo watumishi wapya kuhusu masuala mbalimbali ya kiutumishi ikiwa ni pamoja na kufanya kazi kwa kufuata sheria, taratibu na kanuni za utumishi wa umma.

Dkt. Luhende amesema kuwa ni muhimu kwa kila mtumishi kuendelea kujikumbusha masuala yote waliyofundishwa katika mafunzo hayo watakapokuwa katika vituo vyao vya kazi kwa kuwa mafunzo ndio dira kwa watumishi wote wa Serikali hasa watumishi wapya.

Amesisitiza kuwa ili utumishi wao uweze kuwa na tija, ufanisi na kuheshimika kwa Ofisi na Taifa kwa ujumla, kila mtumishi anapaswa kufanya kazi kwa kufuata Kanuni za Maadili ya Utumishi wa Umma kwa kuwa na tabia na mienendo inayozingatia utoaji wa huduma bora, utii kwa Serikali, utoaji wa huduma bila upendeleo, kufanya kazi kwa uadilifu, kuwajibika kwa umma, kuheshimu Sheria za nchi na kuepuka vitendo vyote visivyofaa ikiwemo kushawishi na kupokea rushwa.

Ameongeza kuwa OWMS inatarajia kuwa baada ya mafunzo hayo watumishi hao wataweza kutekeleza majukumu yao ipasavyo hivyo kuiwezesha Serikali kunufaika na matokeo chanya yatakayopatikana na kuwa chachu katika kuratibu, kusimamia na kuendesha mashauri ya madai na usuluhishi kwa niaba ya Serikali na taasisi zake ndani na nje ya nchi.

Naye Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Bi. Sarah Mwaipopo amewashukuru watumishi hao kwa umakini walioonesha katika kufuatilia mafunzo hayo ambapo amewataka kuzingatia mambo yote waliyofundishwa katika mafunzo hayo ili kufikia malengo yaliyowekwa na OWMS katika uendeshaji wa mashauri.

Ameeleza kuwa mafunzo hayo yameendaliwa kwa lengo la kuwapatia nyenzo watumishi hao kwa lengo la kuwanoa ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa wakati huku akisisitiza kuwa mafunzo hayo yatakuwa endelevu kwa watumishi wote watakaojiunga na Ofisi hii.

Akizungumza kwa niaba ya watumishi wenzake Bi. Kumbukeni Mwinyimadi, Wakili wa Serikali ameishukuru OWMS kwa kuandaa mafunzo hayo muhimu huku akiongeza kuwa mafunzo hayo yatawaongezea morali katika kutekeleza majukumu yao kwa bidii ikiwa ni pamoja na kuzingatia utawala wa sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma.

Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi, Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, Emil Ntwanga akiwasilisha majukumu ya Kitengo cha Manunuzi na Ugavi kwa waajiriwa wapya wa Ofisi hiyo (hawapo pichani) katika mafunzo elekezi yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Chuo cha Uongozi cha Mwalimju Nyerere kilichopo Kibaha mkoani Pwani


Waajiriwa wapya wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali wakimsikiliza kwa makini Dkt. Boniphace Luhende, Wakili Mkuu wa Serikali (hayupo pichani) wakati akifunga mafunzo elekezi kwa wajiriwa hao kuhusu sheria, taratibu na kanuni za utumishi wa umma yaliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Nyerere kilichopo Kibaha Mkoani Pwani.
Wakili Mkuu wa Serikali Dkt. Boniphace Luhende (aliyeketi katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Menejimenti na waajiriwa wapya wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali baada ya kufunga mafunzo elekezi kwa watumishi hao yaliyofanyika Kibaha mkoani Pwani. Aliyeketi wa pili kushoto ni Naibu Wakili Mkuu wa Serikali Bi. Sarah Mwaipopo.

Share:

KITANDULA AKUMBUSHIA FIDIA ZA WANANCHI WALIOPISHA UJENZI WA KIWANDA CHA SARUJI MKINGA


Na Mwandishi Wetu ,Dodoma

MBUNGE wa Jimbo la Mkinga (CCM) Dastan Kitandula ameikumbusha Serikali fidia za wananchi Vijiji vya Kwale na Mtimbwani cha kiasi cha zaidi ya Milioni 570 kwa ajili ya kutoa ardhi kwa ajili ya uwkezaji wa kiwanda cha Saruji cha Hengya kilichokuwa kijengwe wilaya ya Mkinga mwaka 2017.

Kitandula aliyasema hayo Jijini Dodoma wakati wa kikao cha Bunge kinachoendelea  ambapo alisema mwaka 2017 alijitokeza Mwekezaji Hengya alionyesha nia ya kuwekeza kwenye sekta ya Sariuji nchini na kiwanda kilikuwa kije kujengwe mkinga na mwaka 2019 Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) ilimpa leseni aje awekekeze.

Alisema kwamba baada ya kupatiwa leseni mwaka 2020 akaanza kutoa fidia kwa ardhi aliyoitwaa kule mkinga wananchi wakaachia maeneo yao tokea wakati huo mpaka leo hakuna fidia stahiki iliyotolewa hivi na kwa sasa wako wananchi 143 wa Mkinga kutoka Kwale na Mtimbwani wanadaiwa Zaidi ya Milioni 570 hazijalipwa.

Alisema kwamba na serikali ilituma timu ikaja kukaa na uongozi wa mkoa na wilaya na mwekezaji wakakubaliana aifanyike kazi ya tathimini isiyo na shaka ili watu hao walipwe na kazi imekamilika na mwekezaji amepelekewa amegoma kulipa viwango stahiki vya kisheria.

Alisema kwamba na hao ni wananchi wamepoteza ardhi zao hawana ruhusa ya kuingia kwenye maeneo hayo mpaka leo hawalipwi kwa nini mwekezaji alipi kwa sababu ana machungu na aliwahi kusema jamani uwekezaji wa hengya ambao wakati ule kama ungefanyika mwekezaji angekuja kiwanda chenye thamani ya Trilioni 2.3 uzalishaji wa saruji alikuwa azalishe tani Milioni 7 kwa mwaka.

Aidha alisema amesikia taarifa ya wizara hapa kwamba leo viwanda 14 vinazalisha tani milioni 10 walikuwa na mwekezaji alikuwa tayari uwekezaji wa tani Trilioni 2.3 azalishe tani milioni 7 kwa mwaka wamemvuruga na alikuja kusema maneno hayo hapo kwamba kuna watendaji hawana nia njema wana wanamvuruga mwekezaji wapo ndani ya viwanda vya saruji.

Alisema wawekezaji hao hawamtaki mwekezaji huyo kutokana na kwamba ataleta ushindani leo wamepoteza uwekezaji huo watu wa Tanga wana machungu wanaiomba Serikali na Waziri Simamia watu wa Mkinga 143 walipwe stahiki zao.

Akizungumzia suala la uuzwaji wa hisa Tanga Cement alisema wao hawapingi lakini wanachokitaka ni kwamba taratibu zifuatwe watu wa Tanga leo hii kuna viwanda 8 baada ya kubinafsishwa vimegueka kuwa magodauni havifanyi kazi, magofu hivyo hawatakuwa tayari kuona Tanga Cementi inabinafishishwa inageuka kuwa godauni au magofui na mtu anakwenda kuchukua malighafi Tanga anakwenda kuzalisha Dar hilo hatutaki .

Mbunge huyo alisema kwamba viwanda 8 wamehangaika ndani ya serikali ili wawekezaji waheshimu mikataba yao wanapokuwa wakiuziwa hiyo ndio hofu yao watu wa Tanga wanaiomba Serikali taratibu za uwekezaji ufanyike wajenga confedence ya wawekezaji kwani hata wanapata shida kwenye sekta madini kila mwekezaji akija anagaganiza kukiwa na dispute waenda kuamuliwa maamuzi hayo nje ya Tanzania .

Alisema kwa sababu wanasema mahakama zetu haziaminika kama kuna jambo limeamulkiwa kisheria tusikiuke maamuzi hayo yaliyoamulkiwa kila mwekezaji anayekuja anakwenda kujisajili kampuni kwenye mikataba ya kimataifa hivyo wakiendelea kukiuka maamuzi.

Mwisho.
Share:

ALIYENIPORA KSH200,000 AZIREJESHA AKIWA AMEVIMBA NYETI ZAKE

Siku moja nilienda Nairobi kwa ajili ya kuchukua mkopo Benki ili niweze kuikuza biashara yangu ya kuuza nguo za kike, nilivalia gauni lenye mvuto sana, kila aliyekutana na mimi alisema kuwa vazi lile lilikuwa limenipendeza sana na mara nyingi walikuwa wanavaa watu wenye fedha.


Niliingia Benki na kuchukua fedha zile na kuondoka zangu, nikiwa barabarani nikingoja gari kijana mmoja mtanashati alinifuata kama ananisalimia, nikajua kuvutiwa na uzuri wangu ingawaje nilikuwa na mume nyumbani.

Ghafla tu alinivamia na kunipora begi langu lilokuwa na Ksh200,000 kisha kukimbia, sikuwa na la kufanya kwani hata kukimbia nilishidwa, nilibaki nalia sana huku watu wakiniangalia kama sanamu.

Unajua Nairobi mtu anaweza kukupora kitu chako na kukimbia mbio na hakuna mtu hata mmoja anaweza kujitokeza kukusaidia kwani kila mmoja anakuwa na shughuli zake za kutafuta maisha.

Nilianza kuwaza na kuwazua jinsi ningelipa mkopo ule wala sikupata jibu, nakumbuka mara nyingi mume wangu aliwahi kuniambia nikiwa natembea Nairobi niwe makini kwani wezi na matapeli ni wengi.

Nilipofika nyumbani na kumwambia mume wangu kuhusu hilo alipatwa na hasira sana, alinilaumu sana na kusema nimekuwa na tabia ya kutosikiliza kile ambacho anakuwa akisema kila mara. Fedha zile Ksh200,000 ziliniuma sana hadi nikawa nashindwa kula chakula na kuja kuugua vidonda vya tumbo.

Kila siku nilipokuwa nikitembea kuelekea kazini nilikuwa na mawazo sana, kila aliyepishana na mimi alifahamu kuwa kuna jambo halipo sawa kwangu.

Kuna Bibi mmoja alinifuata na kuniuliza kwanini ninaonekana nina mawazo sana, nilimueleza yote yalitokea, basi alinipatia namba ya Afrika Doctors na kuniambia wanaweza kunisaidia.

Niliporejea nyumbani niliwapigia simu na hapo wakanipa maelekezo jinsi ya kuwafikia, siku iliyofuata nilielekea katika Ofisi zao na hapo walinihoji kwa muda mfupi na kunishughulikia, huku wakiniahidi kuwa nitapata fedha zangu.

Nilirejea nyumbani huku mume wangu hajui nilipokuwa nimetoa, siku tatu baadaye nilishangaa mtu aliletwa kwangu akiwa hajielewi kabisa, alikuwa amevimba sana sehemu za siri, kumbe ni yule ambaye alikuwa ameniibia fedha zangu.

Kilichonishangaza zaidi alikuwa na fedha zangu Ksh200,000, niliwapigia African Doctors ili wanipe maelekezo ya kufanya, walimtaka mwizi yuli  kufika katika ofisi zao zilizopo pande za Nakuru, mara moja familia yake ilimchukua na kumpeleka huko na mimi kuchukua fedha zangu.

Kumbuka African Doctors pia wanatibu magonjwa kama vile kisukari, kisonono, kifafa na mengineo, wana uwezo wa kukukinga na maadui zako, kuikuza biashara, kupata kazi, kupandisha cheo na mshahara kazini n.k.

Wasiliana na African Doctors kwa namba; +254 769 404965, tembelea tovuti yao; www.african-doctors.com au watumie email; africandoctorheals@gmail.com.



Share:

Friday, 5 May 2023

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI MEI 6,2023


























Share:

WALIOKUFA KWA UJAMBAZI DODOMA WATAMBULIWA

 


Na Dotto Kwilasa, DODOMA.

MIILI ya watu wanne  waliokufa Kwa tuhuma za ujambazi Aprili 25,2023 majira ya saa 03:10 Jijini hapa tayari imeshatambuliwa na kufanyiwa taratibu za maziko na ndugu zao.

Kwa mujibu wa Msimamizi wa Kitengo cha kuhifadhi maiti(Mochwari) Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Dodoma Beda Anthony miili hiyo yote imetambuliwa na ndugu zao na kwamba wote walikuwa wenyeji wa Mkoa wa Mbeya.

Akizungumza na Jamhuri jijini hapa leo Mei 5,2023 amewataja marehemu hao kuwa ni pamoja na Godfrey Athman Mwashinga ambaye alitambuliwa Mei 1,2023 ambapo alizikwa Mailimbili-Dodoma  na  Baraka Lusekelo aliyetambuliwa na ndugu zake Mei 5,2023 kisha kusafirishwa Mkoani Mbeya kwa taratibu za mazishi .

Wengine ni Timothy Kabuje aliyetambuliwa Mei 1,2023 na kuzikwa Mkonze-Dodoma pamoja na Shukrani Gambi aliyetambuliwa tangu Aprili 4,2023 na kuzikwa Ntyuka Jijini hapa.

Mnamo Aprili 26,2023,Kamanda wa Jeshi la Polisi Dodoma Martine Otieno aliwaeleza Waandishi wa habari kuwa Jeshi hilo  limewathibiti majambazi wanne wa kiume wenye umri kati ya 25-30 waliokuwa katika harakati za kufanya tukio la unyang'anyi wa kutumia silaha nyumbani kwa  Edna Joseph Kashashari (41), mfanyabiashara.


Kamanda Otieno alieleza kuwa majambazi hao walivamia nyumbani kwa Bi. Edna Joseph Kashashari (41), mfanyabiashara, mkazi wa Kisasa wakiwa wamevaa barakoa usoni na kufanikiwa kunyang'anya pesa taslim 1,100,000/= simu ya Samsung moja na simu ndogo tatu baada ya watu hao kumtishia kumkata mapanga ndipo mhanga alipiga kelele za kuomba msaada.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger