Monday, 1 May 2023

KIOTA KIPYA CHA KISASA KABISA 'FK LODGE' KIMEZINDULIWA MKOANI TABORA

Wafanyakazi wa FK Lodge wakiwa katika picha ya pamoja na Makamu Mkurugenzi wa FK Lodge , Bi Jane Matinde Kanga wakati wa Uzinduzi wa Lodge hiyo

****
Lodge mpya ijulikanayo kama FK lodge imezinduliwa mkoani Tabora na Mwakilishi wa Mstahiki Meya , Diwani wa Kata ya Ipuli, Mh Molo Juma Molo. Lodge hiyo ya kisasa yenye vyumba 13 itaongeza upatikanaji wa malazi kwa wageni wa ndani na nje ya nchi wanaotembelea Mkoani hapo kwa sababu mbalimbali.

Akiongea wakati wa Uzinduzi Mkurugenzi Mkuu wa FK Lodge , Bwana Frederick Kanga amesema maono ya kuwekeza Tabora yameenda sambamba na kukuwa kwa haraka kwa mkoa Tabora hususani kwenye miundo mbinu ya Reli ya kisasa ambayo ikikamilika itaongeza mzunguko wa fedha na shughuli mbalimbali za kiuchumi kipindi cha ujenzi na hata baada ya reli kukamilika.


Uwepo wa barabara nzuri na za lami zinaziunganisha mikoa mingi ya jirani kama shinyanga , Singida, Mbeya, Kigoma, Katavi na Sumbawanga pia kutafanya Tabora kuwa kitovu cha biashara lakini pia kumekuwa na uhaba wa sehemu za malazi zinazoshabihiana na kasi hii ya ukuaji na maendeleo na hivyo tumeona ni vyema kuwekeza kwenye lodge ili kwenda sambamba na mahitaji haya muhimu.


Aidha uwekezaji huu utawezesha kuwepo kwa ajira kwa wakazi wa Tabora na Mikoa ya Jirani na hivyo kuchangia katika kukua kwa uchumi wa mkoa huu na nchi kwa ujumla

Kwa upande wake Mgeni Rasmi Mwakilishi wa Mstahiki Meya , Mh Molo Juma Molo Awapongeza sana wakurugenzi na wamiliki wa FK Lodge kwa kuwekeza Tabora na kuahidi kutoa ushirikiano katika kukuza na kuwepo kwa mazingira bora ya uendeshaji wa biashara na kutoa wito kwa wadau wengine hususani wawekezaji wa ndani kuwekeza katika Mkoa wa Tabora.

Akiongea huduma zinazopatikana Makamu Mkurugenzi wa FK Lodge , Bi Jane Matinde Kanga amesema lodge hii ina vyumba 13 vyenye huduma zote muhimu ikiwemo WiFi , lakini huduma za vyakula na vinywaji pia vinapatika katika lodge hii. Aliongeza kwa kusema”Tunajisikia fahari kuweza kutengeneza Ajira kwa vijana 9 zitakazowawezesha kujikwamua kiuchumi , kadhalika tumeingia mikataba makapuni mbalimbali ya kutoa huduma kama za broadband, ulinzi, maji , umeme na hivyo kuchangia katika ungezeko la mapato yao na hivyo kukuza uchumi na pato la taifa kupita kodi. Matumaini na maono yetu kuwa kuwepo kwa lodge hii ni mwanzo wa nyingine nyingi katika maeneo mbalimbali nchini”.

Kupata taarifa zaidi tembelea tovuti ya FK Lodge :
Mkurugenzi Mkuu wa FK Lodge , Bwana Frederick Kanga akiongea wakati wa uzinduzi wa FK lodge iliyopo Ipuli Tabora
Mgeni Rasmi Mwakilishi wa Mstahiki Meya , Diwani wa Kata ya Ipuli, Mh Molo Juma Molo na Mkurugenzi Mkuu wa FK Lodge , Bwana Frederick Kanga wakikata keki wakati wa uzinduzi wa FK Lodge Tabora

Wamiliki wa FK Lodge Bwana na Bibi Frederick Kanga wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa lodge mkoani Tabora
Mgeni Rasmi Mwakilishi wa Mstahiki Meya , Diwani wa Kata ya Ipuli, Mh Molo Juma Molo akiangalia muonekano wa lodge ndani wakati wa uzinduzi wa lodge hiyo
Mgeni Rasmi Mwakilishi wa Mstahiki Meya , Diwani wa Kata ya Ipuli, Mh Molo Juma Molo akiangalia muonekano wa lodge ndani wakati wa uzinduzi wa lodge hiyo
Wadau wa FK Lodge Joe na Mikidadi wakifungua champaign wakati wa uzinduzi
Wageni waalikwa wakipata chakula cha pamoja wakati wa uzinduzi
Baadhi ya wafanyakazi wa Exim walihudhuria uzinduzi wa FK Lodge mkoani Tabora
Share:

JAMAA AZUA GUMZO MTANDAONI ALIVYOPIGA PICHA KICHWA CHINI AKIFUNGA NDOA NA MKEWE



NA ANDREW CHALE


MWALIMU wa Dance na mcheza dance mjini Arusha ambaye picha zake zimekuwa gumzo mitandao kuanzia Aprili 29, 2023, Kilumbo Steven amefunguka juu ya uwezo wake wa aina mbalimbali ya 'break dance' akiwa amepiga picha akiwa kichwa chini na miguu juu akiwa na Mke wake wa ndoa pembeni.


Akizungumza kwa njia ya simu na Mwandishi Andrew Chale,  Break Dancer huyo kupitia mpango wake wa B Boy Kilumbo anasema kuwa amepata simu nyingi ikiwemo pia kuona wadau wakiposti picha zake hizo mitandaoni.


"Nimefanya densi ndani ya harusi yangu.

Lakini pia picha nyingi tulipiga sema hizo mbili za kusimama kwa kichwa chini ndo imesambaa zaidi mitandaoni,  ila tumepiga picha nyingi " amesema Kilumbo.


Aidha,  amefafanukuwa B Boy Kilumbo ni kwamba B imesimama kwenye Break,  Boy imesimama kama yeye mwenyewe  na Kilumbo ni jina lake.


"Watu wengi wameona picha zile lakini wamekuwa na maoni tofauti, Mie ni kijana ambaye nina malengo makubwa kupitia kipaji changu.


Nataka kuendeleza uwezo wangu huu na hata kuwarithisha wengine."Amesema Kilumbo. 


Ambapo lengo kubwa ni kuanzisha Shule maalum ya Break Dance kwa vijana wote wa kiume na kike ilikuongeza vijana wengine zaidi.


"Hapa Tanzania najulikana kwa vijana wengi na nimekuwa nikiwafunza kwenye Break Dance.


Lakini pia nimekuwa nikishiriki mashindano tofauti, ikiwemo shindano la Hip-hop Hasili na mwaka juzi nilikuwa mshindi wa kwanza.


Pia nimekuwa nikifanya mashindano kwa njia ya mtandao 'Online' Marekani na pia nchi zingine hivyo kwa sasa malengo ni kuona nafika mbali na pia kuacha alama.


Kilumbo anasema kuwa, yeye ni Mngoni aliyeamua kufanya maisha yake Arusha ambapo pia mbali na kufanya Break Dance, lakini pia anajihusisha na masuala ya Utalii akifanya program ya 'Ngondi ya mtembezi' akitembeza Watalii maeneo mbalimbali.



Mwisho.

Share:

MTOTO ALIYEDAIWA KUFARIKI NA KUZIKWA AKUTWA AKIWA HAI


Wakazi wa Kijiji cha Salong’we kilichopo wilayani Magu mkoani Mwanza wamekumbwa na taharuki baada ya mtoto aitwaye Mabilika Wilson aliyefariki na kuzikwa tarehe 17 mwezi huu kupatikana akiwa hai katika Kijiji cha Mwangika wilayani Kwimba mkoani humo.

Wilson Bulabo ni baba mzazi wa mtoto huyo amesema ni kweli mtoto wake huyo aliumwa kwa siku mbili na kufariki hatimaye wakamzika lakini alipoenda kumuangalia huyo mtoto aliyeonekana Kijiji cha Mwangika alimgundua kuwa ndiye mtoto wake aliyezikwa wiki chache zilizopita.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Wilbroad Mutafungwa amefika katika Kijiji hicho na kushuhudia kaburi likifukuliwa kwa ajili ya taratibu za uchunguzi wa tukio hilo ambapo amewataka wakazi wa Kijiji hicho na vijiji vya Jirani, kuwa watulivu kipindi ambacho uchunguzi wa tukio hilo ukiendelea.

Via EATV
Share:

JAMAA MWENYE WATOTO ZAIDI YA 550 APIGWA MARUFUKU KUSAMBAZA MBEGU ZAKE ZA KIUME


Jonathan Jacob Meijer (41) raia wa Uholanzi amepigwa marufuku kusambaza mbegu zake za kiume baada ya kugundulika kuwa ana watoto zaidi ya 550 duniani kupitia utoaji wa msaada wa mbegu za kiume za uzazi.

Mwanaume huyo mwaka 2017 alizuiwa kutoa mbegu za uzazi kwenye kliniki ya masuala ya uzazi nchini Uholanzi baada ya kufahamika kuwa alikuwa amezalisha watoto zaidi ya 100

Inaelezwa kuwa badala ya kuacha kuendelea na utoaji wa msaada huo, Jonathan aliendelea kutoa mbegu zake nje ya nchi yake na kwa njia ya mtandao.

Mahakama ya Uholanzi mjini The Hague imemwambia atoe orodha ya kliniki zote alizowatumia na kuziagiza ziharibu mbegu zake.
Share:

WARUDISHA MALI WAKIWA NA MATUMBO KAMA WENYE MIMBA

Ninaitwa Nathaniel kazi yangu ni uuzaji na usambazaji wa magari kutoka China kuleta Tanzania.Kazi yenyewe siyo kongwe sana kwangu ni kazi niliyoifanya kwa muda wa miaka mitatu sasa kabla sijaacha kujishughulisha na utowaji wa copper kwenye vyuma chakavu.

Kazi yenyewe niliipata baada ya kumfahamu daktari BAKONGWA bingwa wa kutatua shida za wengi mwenye nambari zake za whatsapp +243990627777 na tovuti zake https://bakongwadoctors.com .

Mwaka wa tatu toka nianze kujihusisha na kazi hii ya kuuza magari nilikuwa mwenye kusafirisafiri sana mara kwa mara na hivyo kupaacha nyumbani penyewe bila ya muangalizi, sikuwa mwenye haraka ya kuoa nilitaka kujikamilisha kwanza kwenye kila kona ya maisha yangu.

Sasa nilikuwa nimepanga mara baada ya safari yangu ya mwisho nimhusishe daktari juu ya suala langu la mimi kuoa ili anifanyie wepesi katika jambo hili ambalo vijana wengi huwa linatusumbua.

Uangalizi niliokuwa nao hapo nyumbani ni wa cctv tu ambazo zilifungwa na watu wa kampuni la delmac, kwa hivyo sikuwa na wasiwasi tena, sijui ni kipi walikifanya kwenye ulinzi wangu lakini nilipigiwa simu na delmac nikaambiwa kuwa majambazi wameingia nyumbani kwangu na kuiba kila kitu kwa bahati mbaya walifanikiwa kuzizima cctv na hivyo hazikuwanasa wala hawakujulikana.

Niliogopa sana kwa taarifa hizo tena nilikasirishwa sana nilipokumbuka ni jinsi gani na nguvu kiasi gani nimezitumia kupata mali hizo, nilipokumbuka mtu wa kunisaidia daktari bakongwa , nilimpigia na kumueleza kila lililotokea ,yeye hakuwa na wasiwasi aliniambia kuwa nitakapokuwa nimerudi nyumbani Tanzania mali zangu nazo zitarudi.

Kwakuwa ninamuamini sana sikuwa mtu wa pupa nilifunga mzigo wangu wa magari na kurudi Tanzania , mara tu baada ya kufika nyumbani siku ya pili yake nilishangazwa kuona vijana wanne wamekuja wamevimba matumbo wakiomba msamaha na kurudisha mali walizochukua.

Nilimpigia daktari na kumfahamisha lililotokea yeye akasema nifanye vile mimi ninataka kwa kuwa ni mali zangu nikaamua vijana wale warudishe gharama za kuharibu mfumo wangu wa cctv, mali zangu na kisha kuwasamehe , ninashukuru sana kwa daktari kwa kweli haujawahi kuniangusha katika jambo lolote.


Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU MEI MOSI ,2023




 



Share:

YANGA YATINGA NUSU FAINALI CAF


MABINGWA Watetezi wa Ligi Kuu Tanzania bara timu ya Yanga imewatoa kimasomaso watanzania baada ya kutinga hatua ya Nusu Fainali ya Michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika baada ya kutoka sare ya kutofungana na Rivers United kutoka nchini Nigeria mchezo uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Yanga imepata nafasi hiyo baada ya ushindi wa mabao 2-0 mchezo wa kwanza uliopigwa nchini Nigeria.

Yanga ni kama inataka kufuata nyao za timu ya Simba ambayo Mwaka 1993 ilifanikiwa kutinga fainali za Kombe la CAF ikimenyana na Stella Abdijan Kutoka Ivory Coast ambapo hata hivyo haikufanikiwa kuchukua ubingwa

Simba SC ambayo ilikuwa inashikiriki Kombe la Klabu Bingwa Africa ilishindwa kutinga nusu Fainali ya klabu bingwa Afrika kwa kuondoshwa na Wydad Casablanca kwa mikwaju ya Penalti 4-3
Tanzania Sasa imeingiza timu moja nusu Fainali Katika michuano ya Kombe la Shirikisho ambalo zinacheza timu ambazo hazikufuzu Katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika.

Hivi Sasa rasmi Yanga SC itakutana na Marumo Gallants kutoka Afrika Kusini waliwatoa Pyramids ya Misri kwa jumla ya mabao 2-1 baada ya leo kuibuka na ushindi wa bao 1-0.

Mchezo wa kwanza wa nusu Fainali unatarajia kuchezwa Mei 14 au 15 mwaka huu uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam kabla ya wiki moja marudiano kuchezwa nchini Afrika Kusini.

Timu nyingine ambayo zimefuzu Katika michuano ya Kombe la Shirikisho ni ASEC Mimosas ya Ivory Coastal baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya US Monastir sasa inamsubiri Mshindi kati ya FAR Rabat ya Morocco au USM Alger ya Algeria ambao watacheza majira ya saa nne usiku.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger