Thursday, 27 April 2023

BARRICK KUENDELEA KUTOA FURSA KWA WANAWAKE KUFANYA KAZI KWENYE SEKTA YA MADINI

Baadhi ya wahitimu wakipokea vyeti kutoka kwa mgeni rasmi

Baadhi ya wahitimu wakipokea vyeti kutoka kwa mgeni rasmi
Meneja Mawasiliano wa Barrick nchini, Georgia Mutagahywa akiongea wakati wa mahafali ya kidato cha sita katika shule ya sekondari ya sekondari ya Jenerali David Musuguri iliyopo wilayani Muleba mkoani Kagera.
Wahitimu wakisoma risala mbele ya mgeni rasmi na wageni waliohudhuria mahafali hayo.
Baadhi ya wazazi wa wahitimu wakifuatilia matukio wakati wa mahafali hayo.
Wahitimu wa kidato cha sita wakitoa burudani wakati wa mahafali hayo.
Wahitimu wa kidato cha sita wakitoa burudani wakati wa mahafali hayo.

Kampuni ya Barrick nchini imeeleza dhamira yake ya kuendelea kutoa fursa kwa Wanawake kufanya kazi kwenye migodi yake nchini ili kuondoa dhana iliyojengeka kwa muda mrefu kuwa ajira za migodini ni kwa ajili ya wanaume na imewataka wanafunzi walioko mashuleni na vyuoni kuchangamkia kusoma masomo yanayoendana na sekta ya madini kwa kujiamini.

Hayo yamebainishwa na Meneja Mawasiliano wa Barrick nchini, Georgia Mutagahywa , wakati wa mahafali ya kidato cha sita katika shule ya sekondari ya Jenerali David Musuguri, iliyoko Kata muhutwe wilayani Muleba Mkoani Kagera ambapo alikuwa ni mgeni rasmi.

Aliwaasa wahitimu hususani wasichana watakapojiunga na vyuo wasiogope kusoma masomo ya Jiorogia na mengine yanayohusiana na sekta ya madini kwa kuwa sekta hiyo bado inazo fursa nyingi na wanawake hawapaswi kuachwa nyuma kuchangamkia fursa hizo kama ilivyo sasa idadi ya wanawake ni wachache katika sekta ya madini kwa kulinganisha na Wanaume.

“Kampuni ya Barrick imedhamiria kwa dhati kuhakikisha inaongeza idadi ya wafanyakazi wanawake katika migodi yake ya Bulyanhulu na North Mara na hivi sasa tunao wafanyakazi Wanawake ambao wanaendelea kufanya kazi zao kwa ufanisi na weledi mkubwa”, alisema Mutagahywa.

Pia aliwataka wahitimu kutobweteka bali watumie elimu waliyoipata na watakayoendelea kuipata kuwa wabunifu ili watakaokosa ajira waweze kujiajiri na kutatua changamoto mbalimbali zilizopo kwenye jamii hususani kipindi hiki ambacho kuna upungufu mkubwa wa ajira nchini na katika nchi nyingi duniani kote.

Mkuu wa shule hiyo, Alchard Kashamba, alisema shule hiyo imefanya mahafali ya sita tangu, kupandishwa hadhi ya kuwa na kidato cha sita mwaka 2007 kwa kuongeza udahili wa masomo ya sayansi na Sanaa na kwa mwaka huu ikiwa na jumla ya wahitimu 264 wasichana.

Alisema kwa Sasa shule ina majengo 26 mabweni matano,bwalo la chakula Moja,maktaba na madarasa licha ya kuwa na changamoto ya baadhi ya vifaa vya kujifunzia na kufundishia kama wahitimu walivyoeleza katika risala yao kwa mgeni rasmi.

Mmoja wa wakazi wa kata ya Muhutwe Ansbert Mushumbushi, ambaye ni miongoni mwa wazazi waliohudhuria katika mahafali hayo alisema wanafurahishwa shule hiyo inavyoendelea kuwa na miundo mbinu mizuri na kufanya vizuri kitaaluma.

Share:

WADAU MBALIMBALI WATEMBELEA BANDA LA NACTVET KWENYE MAONESHO YA WIKI YA UBUNIFU

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET), linashiriki katika maonesho ya wiki ya ubunifu yanayofanyika katika Uwanja wa Jamhuri, Jijini Dodoma.

 Maonesho hayo yameandaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na yanatarajiwa kudumu kwa siku tano, kuanzia tarehe 24 hadi 28 Aprili 2023.

Lengo la ushiriki wa NACTVET katika maonesho hayo ni kukutana na wadau mbalimbali ili kutoa elimu kuhusu majukumu ya Baraza na kutoa ufafanuzi kuhusu mambo mbalimbali yanayosimamiwa na kutekelezwa na Baraza.

Akizungumza katika maonesho hayo, Afisa Habari na Uhusiano wa Baraza , Bi. Casiana Mwanyika, amesema kuwa ushiriki wa NACTVET katika maonesho hayo ni muhimu ili kuwawezesha wadau kufahamu shughuli za Baraza na kujenga uelewa kwa wananchi.

 Hivyo basi, amewakaribisha wadau na wananchi kwa ujumla kutembelea banda la NACTVET ili kupata taarifa mbalimbali zinazofanywa na Baraza, ikiwemo kusimamia ubora wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi Nchini.
Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH Dkt. Amos Nungu akiweka saini alipotembelea banda la Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET), katika Maonesho ya Wiki ya Ubunifu yanayofanyika katika Uwanja wa Jamhuri, Jijini Dodoma.
Afisa Uhusiano wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) Casiana Mwanyika akiwa na mdau katika Maonesho ya Wiki ya Ubunifu yanayofanyika katika Uwanja wa Jamhuri, Jijini Dodoma.
Wadau mbalimbali wakipata maelezo mara baada ya kutembelea banda la Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET), katika Maonesho ya Wiki ya Ubunifu yanayofanyika katika Uwanja wa Jamhuri, Jijini Dodoma.
Baadhi ya wanafunzi walipotembelea banda la Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET), katika Maonesho ya Wiki ya Ubunifu yanayofanyika katika Uwanja wa Jamhuri, Jijini Dodoma.
Share:

POLISI SHINYANGA WAKAMATA KONDOMU, BUNDUKI ZA MAKAMPUNI YA ULINZI ZIKIAZIMWA NA WAHALIFU

Na Halima Khoya  & Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga limefanya ukaguzi wa kushitukiza kwenye malindo ya kampuni mbalimbali za ulinzi na kufanikiwa kukamata Bunduki 5 ambazo hazikufuata utaratibu wa kisheria zikitumika kuazimishwa kwa wahalifu huku likikamata vipodozi vyenye viambata vya sumu ambavyo haviruhusiwi kwa matumizi ya binadamu pamoja na bidhaa mbalimbali yakiwemo maboksi 9 ya kondomu zinazopaswa kutumika kwenye vituo vya afya na mashirika yanayosika na masuala ya kudhibiti UKIMWI.


Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo Alhamisi Aprili 27,2023, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi amezitaja zilizokamatwa kufuatia ukaguzi wa kushitukiza wa malindo ya kampuni mbalimbali kuwa ni Bunduki aina ya MARK IV yenye namba TZ car 89936 na risasi 04 na Bunduki aina ya MARK IV yenye namba K 9239 na risasi 03.


Silaha zingine ni Bunduki aina ya MARK IV yenye namba D 6000 na risasi 01, Bunduki aina ya MARK IV yenye namba MG 564884 na risasi 02 na Short gun Birmingham England na risasi.


“Tumekamata bunduki hizi tano ambazo zilikuwa zikimilikiwa kinyume cha utaratibu chini ya kifungu 10(7) na 60 Cap 38 cha Sheria ya Usimamizi na Udhibiti wa Silaha na Risasi ya Mwaka 2015 pamoja na kanuni zake GN 334 ya tarehe 30/12/2016 kanuni namba 14(2) na (3).
“Pia kupitia misako na Operesheni mbalimbali katika kipindi cha mwezi mmoja kuanzia tarehe 22/03/2023 hadi tarehe 26/04/2023 tumefanikiwa kukamata vitu na vielelezo mbalimbali ambavyo ni magodoro mawili, TV 05, Remote 01 ya Star X, Pard 05, PlayStation PS-3 01, Pikipiki 06 (MC 248 CYP- SANLG, MC 700 AQL-SANYA, MC 815 DQC, MC 494 DCM- KINGLION, MC 909 CEV-HAOJUE na MC 134 DDL-KINGLION), Redio Subwoofer 03, Redio ndogo 02, Sigara aina ya CLUB box 3 na pakiti 15 aina mbali mbali, Computer 02, Vitenge doti 05, Simu smart aina ya Honor, Saa 02 aina ya Titarium, Mtungi wa Gesi, Draya 01, Pombe ya moshi lita 120, Meza ya kuchezea kamari na karata zake tatu, Vifaa vya kupiga ramli chonganishi maarufu MBIGI, Panga 02 kubwa, Viuatilifu vya Serikali vya kuua wadudu wa Pamba”,ameeleza Kamanda Magomi.

Amevitaja vitu vingine vilivyokamatwa ni pamoja na Flash Disk ya 16GB aina ya Toshiba 02, Bhangi Kilogram 327 na kete 85, Mirungi bunda 05, Madumu tupu 14 yenye ujazo wa lita 20, Madumu 16 yenye ujazo tofauti tofauti yakiwa na mafuta ya Petrol Lita 269 yote yakidhaniwa kuibiwa kwenye mradi wa ujenzi wa reli ya SGR.
“Vitu vingine ni Vipodozi vyenye viambata vya sumu ambavyo haviruhusiwi kwa matumizi ya binadamu (Epiderm crème box 01, Betasol crème box 03, CaroLight box 01), Pombe kali aina ya Hakiri box 12, Kondom box 09 zikiwa kwenye maduka ya watu binafsi ambazo zinazopaswa kutumika kwenye vituo vya afya na mashirika yanayosika na masuala ya kudhibiti UKIMWI.
 Mifuko ya plastiki iliyopigwa marufuku pakiti 100, Kiberiti bunda 02, Extention 02, Lita 67 ya mafuta ya kula na bidhaa mbali mbali za madukani”,amesema.


Katika hatua nyingine amesema Jeshi la Polisi kupitia kitengo chake cha Upelelezi kwa kipindi hicho cha mwezi mmoja limewafikisha watuhumiwa 132 mahakamani katika kesi 129 zilizoripotiwa katika kipindi hicho ambapo mpaka sasa kesi zilizopata mafanikio ni kesi 62 ikiwa ni pamoja na watuhumiwa kufungwa jela/kifungo cha nje pamoja na kulipa faini.


Miongoni mwa kesi hizo 62 zipo kesi ambazo zimehusisha makosa ya ukatili wa kijinsia ambazo ni kumpa mimba Mwanafunzi kesi 04, kubaka kesi 02 na kulawiti kesi 01.


Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga linaendelea kuwaasa wananchi kufuata sheria za nchi wakati wote na kutojihusisha na vitendo vya kiuhalifu kwa namna yoyote ile.


Aidha Jeshi la polisi linatoa wito kwa wananchi kutoa taarifa dhidi ya uhalifu na wahalifu ili kutokomeza vitendo hivyo miongoni mwa jamii inayotuzunguka na halitokuwa na muhali kwa yeyote yule ambaye atajihusisha na vitendo vya kiuhalifu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi Aprili 27,2023. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi Aprili 27,2023
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi Aprili 27,2023
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi Aprili 27,2023

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi Aprili 27,2023
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akionesha vitu mbalimbali vilivyokamatwa na Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akionesha vitu mbalimbali vilivyokamatwa na Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akionesha vitu mbalimbali vilivyokamatwa na Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akionesha vitu mbalimbali vilivyokamatwa na Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga

Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI APRILI 27,2023


Magazetini leo Alhamisi April 27 2023

Share:

Wednesday, 26 April 2023

WATU WALIOGOPA KUMSOGELEA; RAIS SAMIA AKAMSHIKA MKONO NA KUOKOA MAISHA YAKE


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitazama maendeleo ya mkono wa Mtoto Hamimu Mustapha Baranyikwa (15) mwenye matatizo ya ngozi ambaye ni mkazi wa Nyakanazi Mkoani Kagera mara baada ya kuzungumza naye na kumpa Mkono wa Eid Ikulu Jijini Dar es Salaam. Mhe. Rais Samia aligharamia matibabu ya mtoto huyo kwa muda wa miezi sita katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam.


* Hatimaye, ndoto ya mtoto Hamimu ya kukutana na Rais yatimia

* "Ni mimi" Rais Samia alimwambia mtoto huyo baada ya kushindwa kuamini macho yake alipofika Ikulu

Mwandishi Wetu

HAYAWI, hayawi... sasa yamekuwa. Ndoto ya mtoto Hamimu Mustapha Baranyikwa (15) aliyokuwa akiililia kwa muda mrefu ya kukutana na Rais Samia Suluhu Hassan hatimaye imetimia. 

Hamimu, ambaye alilazwa kwenye Hospitali ya Taifa ya Rufaa ya Muhimbili kwa miezi 6 akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa ngozi kwa ufadhili wa Rais Samia, aliinama chini na kijishika kichwa baada ya ombi lake la kukutana na Rais kutimia.

Mtoto huyo aliomba akutane na Rais kumshukuru kwa kuokoa maisha yake kwa kumpatia matibabu hadi kupona.

Wakati watu walikuwa wanamnyanyapaa na kumkimbia kutokana na ugonjwa wake wa ngozi, Rais Samia alimshika mkono na kukagua mikono yake kwa upendo wa ajabu.

Mwanzo hakutanabahi kuwa aliye mbele yake ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, lakini baada ya kugundua, mtoto Hamimu alishikwa na hisia kali. 

Mtoto huyo alishikwa na butwaa pale ambapo Rais Samia alipojitambulisha kwake huku akiinama chini bila kuamini.

"Sura inakuja kama ya Mama Samia," alisema Hamimu baada ya kukutana uso kwa uso na Rais.

Rais Samia akamjibu mtoto huyo: "Sasa huyu ndiyo Mama Samia, si ulisema unataka kumuona?"

Huku akiinamisha kichwa chake na kujishika na mikono usoni, Hamimu huku akiwa haamini kama ndoto yake kweli imetimia akamuuliza Rais, kweli "ni wewe?"

Baada ya mtoto huyo kushikwa na butwaa, Rais Samia huku akitabasamu akamuuliza: "Hamimu, vipi sasa? Si ulisema unataka kuniona."

Ndipo Hamimu alipojibu: "Nimefurahi kukuona, Asante."

Hamimu alifika Ikulu Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kumshukuru Rais Samia kwa msaada wa matibabu aliompatia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Rais Samia alimuona mtoto huyo kwa mara ya kwanza wakati wa ziara yake ya kikazi Nyakanazi, mkoani Kagera, tarehe 16 Oktoba, 2022 na kuagiza apatiwe matibabu haraka baada ya familia ya mtoto huyo kuhangaika kwa muda mrefu bila msaada wowote.

Akiwa Muhimbili, Hamimu alisimulia mtihani wa maisha aliopitia akiwa na umri mdogo tu wa miaka 15.

"Nilisikia Rais Samia anapita Nyakanazi na mimi kwetu ni pale pale Nyakanazi. Wazazi walinikataza, wewe usiende na hali hiyo uliyokua nayo watu wanakukimbia. Unaenda kufanya nini, watakupiga," alisema. 

"Kaka yangu akaniambia wewe nenda, itakavyokuwa itakuwa. Ninachojua (Rais) anaweza kukusaidia. Mimi kweli niliamka usiku sana ili wazazi wasinione, maana kama wangeniona wangenikataza."

Hamimu, ambaye wazazi wake walihangaika kumpeleka kwa waganga wa kienyeji na hata kuuza mali za familia bila mafanikio, alikuwa amekata tamaa kama angekuja kupona ugonjwa wake wa ajabu 

Ngozi yake ilikuwa imeharibika, uso wake ukawa hautazamiki hadi watu wazima na watoto wakawa wanamkimbia na alishindwa hata kukunja na kukunjua vidole vya mikono yake kutokana na maradhi hayo.

Wahenga wanasema penye nia pana njia. Rais Samia alipofika Nyakanazi wakati wa ziara yake ya mkoa wa Kagera, alimuona mtoto huyo amekaa pembeni ya barabara akiwa amenyong'onyea akawatuma wasaidizi wake waende kuongea naye wajue tatizo lake ni nini.

Kufuatia ushauri wa daktari, Samia aliagiza mtoto huyo asafirishwe haraka kutoka Nyakanazi hadi hospitali ya Taifa ya Rufaa ya Muhimbili iliyopo Dar es Salaam kwa uchunguzi na matibabu.

Siku chache baada ya maagizo ya Rais, Hamimu akaanza kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Muhimbili tarehe 21 Oktoba, 2022 hadi tarehe 19 Aprili 2023, madaktari wake walipomruhusu kwenda nyumbani baada ya matibabu.

Mwisho
Share:

NIMESHINDA MILIONI TISA YA BAHATI NASIBU KWA KUFANYA HIVI

Frank ndilo jina langu mtoto wa kwanza kwenye familia yetu ya waliosoma, mimi tu ndiye niliyekataa shule mapema wenzangu wote ni wasomi tena waliofanikiwa na wenye kazi nzuri maishani mwao.


Kazi yangu kubwa ni kuuza makava ya simu mtaji wenyewe nilipewa na wadogo zangu angalau na mimi nijitafute kidogokidogo huko, mchana nilifanya kazi hiyo lakini kila jioni nilitembelea kwenye mabanda ya casino hususani meridian bet kutafuta bahati yangu huko.

Nimejifunza kucheza mchezo huu wa bahati nasibu kuanzia nikiwa mwenye umri wa miaka kumi na nane mara tu baada ya kuacha shule.

Nimecheza mara nyingi sana na kila nilipokuwa ninajaribu niliishia kuambulia pesa za nauli tu na vichenji vidovidogo.Kabla ya msaada nilioupata kutoka kwa daktari bingwa BAKONGWA hapo nyuma sikuwahi kupata pesa ya maana ya kufanyia lolote katika shughuli zangu za kubet –ninakumbuka pesa kubwa ambayo niliwahi kushinda ilikuwa ni laki nne na nusu tu pesa ambayo haifikiia hata kwenye mtaji ambao wadogo zangu walinipa nijichangechange.

Jumapili mmoja wadogo zangu walinitembelea ili kujuwa biashara zangu za makava zinaendeleaje lakini kwa bahati mbaya hawakunikuta ofisini walikwenda mahali kukaa kunywa ili kungoja giza liingie kisha wakanifuata nyumbani mida ya saa nne na nusu hivi wakati ambao mimi nimetoka kwenye jukumu langu la kubet.Waliponiuilza niliwaambia nilikuwa meridian bet,mdogo wangu hekima alishangazwa na tabia hii akapuuza kisha akasema kwa ujasiri kama unapenda sana kubet angalau ubet kwa akili safisha nyota yako kwa daktari halafu ndio ubet sio kufanya kienyejienyeti tu.


Kisha akanipa tovuti za daktari https://bakongwadoctors.com nilipomtafuta huko kwenye tovuti zake nikakutana na nambari zake za whatsapp +243990627777 nikazichukuwa na kuzipiga.

Daktari akanipa maelekezo na dawa ya kujisafisha kwa muda wa siku mbili kabla ya kwenda kucheza beti, baada ya muda wa siku hiyo nilikwenda huko meridian nakumbuka siku hiyo ilikuwa ni game la arsenal na tottenham msimu jana wa 2022 mzunguko wa pili, niliweka bet yangu na kumpa hotspurs kisha nikaenda zangu nyumbani.


Siku ya pili baada ya kuisha siku ya kubeti nilipigiwa simu na meneja wa meridian akinitaka nimfuate ofisini kwao HQ dar es salaam na wao wakanikabidhi donge langu nono, nilikuwa nimeshinda milioni tisa za kitanzania.

Kwa uwezo wangu ule wa kubashiri na kwa nguvu ya dawa za daktari nilizotumia meneja akashawishika sana na mimi akaamuwa kuniajiri hapohapo ili niwe mpanga odds kwenye bet zake sasa nina kila kitu kama wadogo zangu walivyo ninasema asante kwa daktari.


Share:

RAIS SAMIA ATOA MSAMAHA KWA WAFUNGWA KATIKA KUADHIMISHA MIAKA 59 YA MUUNGANO





Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger