Saturday, 22 April 2023

DAWA NILIYOMPA MWANAMKE WA NDOTO ZANGU NA KUMUACHISHA TABIA ZA VILABUNI

Aneth mwanamke mwenye rangi ya kuvutia , mpole mwenye urefu wa wastani na mwenye mazungumzo machache mbele ya kundi la wanaume, kiufupi mwanamke mwenye stara zake anayejuwa nafasi yake kwenye kundi la wanawake.

Mwanamke huyu aliyekuwa anafanya kazi polos, club mpya yenye kutembelewa na kila aina ya wanaume kutoka kila kona ya nchi kwa uzuri na manzari iliyopo club hiyo.Haikuwa rahisi nilipo mshirikisha kila aliyekuwa jirani yangu kwamba nimetokea kumpenda.


Kila niliyemjulisha habari hizo aliitikia na kusema kuwa ni mrembo lakini ni wa bar –wanawake wa bar hawabadiliki tabia na tabia zao huwa ni za kikahaba tu.Nilipo thubutu kumshirikisha shangazi yangu ambaye alikaimu nafasi ya baba mara baada ya marehemu baba kufariki naye pia alijibu yaleyale kuwa hawezi kumpokea mwanamke wa bar kuwa mkwe wake.


Kwa kweli hayo niliyaona mwenyewe kila nilipo mkataza kufanya kazi kwenye vilabu na bar badala yake alibadili na kuhamia kwenye bar za mbali nako kujuwa, hili likanifanya niwaze kuwa haya yote yanapelekeana na tabia za ukahaba na kazi za ubaamedi.


Nilipo mshirikisha mwalimu wangu wa kipaimara , paroko Joshua akatufanyia maombi na kunisisitiza kuwa nifuate msukumo wangu wa moyo na kutokujali hayo alitufanyia maombi na kufunga kwa muda wa wiki tatu lakini hakukuwa na majawabu niliyoyatarajia.


Sasa nilikuwa nimechoshwa na tabia za aneth lakini haikuwa rahisi kumuacha kwa kuwa upendo wangu wa dhati juu yake haukupunguwa hata kidogo, siku mmoja nikiwa nimejituliza kwenye kijiwe tukizungumza kuhusu shida za kila siku nilisikia watu wakimuongekea daktari BAKONGWA kwa tiba zake za muda mfupi na uhakika.

Niliomba nambari zake za whatsapp +243990627777 na kisha kumtafuta akanipa dawa ya kutumia na kumpa mwanamke wangu aneth, mara baada ya kufanya hivyo nilishangazwa kuona aneth anakiri kuacha kazi zake mwenyewe na kisha kunitambulisha kwa familia yake wote.

Asante sana daktari kwa huduma zako nzuri na za uhakika.


Share:

KATIBU MKUU KENYA: TANZANIA IPO MBALI KATIKA USIMAMIZI WA USALAMA NA AFYA


Katibu Mkuu Wizara ya Kazi na Hifadhi ya Jamii Nchini Kenya, Mhe. Geofrey Kaituko akizungumza na baadhi ya viongozi wa OSHA na watumishi wa Wizara yake alioambatana (hawapo pichani) walipotembelea Ofisi za OSHA Dar es salaam kwa lengo la kujifunza jinsi Tanzania ilivyoweza kuwa na Taasisi inayojitegemea kwa ajili ya kusimamia masuala ya usalama na afya mahali pa kazi nchini.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Prof. Jamal Adam Katundu, akimkabidhi zawadi Mtendaji Mkuu wa Idara ya OSHA Nchini Kenya, Dkt. Musa Nyandusi wakati wa ziara yao ya kutembelea ofisi za OSHA Dar es Salaam.
Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi. Khadija Mwenda, akizungumza na Viongozi wa Wizara ya Kazi na Hifadhi ya Jamii kutoka Kenya pamoja na baadhi ya viongozi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakati wa ziara ya viongozi hao kutoka Kenya ambao walitembelea Ofisi za OSHA Dar es Salaam kwa lengo la kujifunza namna OSHA inavyosimamia usalama na afya mahali pa kazi nchini.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Prof. Jamal Katundu, na Katibu Mkuu Wizara ya Kazi na Hifadhi ya Jamii nchini Kenya, Mhe. Geofrey Kaituko (waliokaa) wakikwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Menejimenti ya OSHA na viongozi wa Wizara ya Kazi na Hifadhi ya Jamii nchini Kenya.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Prof. Jamal Katundu (wapili kushoto) na Katibu Mkuu Wizara ya Kazi na Hifadhi ya Jamii Nchini Kenya, Mhe. Geofrey Kaituko (wapili kulia) wakifualia mada mbali mbali kuhusu masuala ya kazi nchini. Wakwanza kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya OSHA Nchini Kenya na wakwanza kushoto ni Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi. Khadija Mwenda.

********************

Na Mwandishi Wetu

Ujumbe wa Wataalam kutoka Wizara ya Kazi na Hifadhi ya Jamii kutoka Kenya umehitimisha ziara yake ya siku nne nchini iliyolenga kubadilishana uzoefu kuhusu sheria na taratibu mbali mbali za kazi ambapo wamesema Tanzania imepiga hatua kubwa katika usimamizi wa masuala ya kazi hususan mifumo ya usimamizi wa usalama na afya mahali pa kazi.

Akiongea mara baada ya kuhitimisha ziara yao katika Ofisi za Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA), Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi ya Kenya, Bw. Geoffrey Kaituko, amesema nchi nyingi za Afrika zimekuwa zikitafuta uzoefu wa mambo mbali mbali ughaibuni ilihali uzoefu huo unapatikana katika nchi zinazowazunguka.

“Ziara yetu hapa Tanzania imekuwa ya kufana sana, tumetembelea Taasisi mbali mbali chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu- Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu. Kwahiyo sisi tumefurahi sana kwa mapokezi mazuri tuliyoyapata pamoja na mambo mazuri tuliyojifunza. Mara nyingi tumekuwa na mazoea ya kwenda Ulaya kujifunza mambo fulani fulani mfano kwa mambo haya ya OSHA tungetaka kwenda Ujerumani wakati hapa Tanzania kuna Taasisi nzuri sana inayosimamia masuala ya usalama na afya hivyo jambo ambalo tunatoka nalo hapa ni kwamba nasisi ni lazima twende tukaanzishe Taasisi kama hii,” amesema Bw. Geoffrey Kaituko.

Kwa upande wake Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Prof. Jamal Katundu, amesema kupitia ziara hiyo ya wataalam kutoka Kenya, Ofisi yake imejifunza mambo mengi ikiwemo jinsi walivyofanikiwa kuwezesha watu wao kupata ajira nje ya nchi yao na hivyo kuliingizia Taifa lao fedha nyingi za kigeni.

“Mfano katika suala la Wakenya wanaofanya kazi nje yan chi yao, Saudi Arabia wana wafanyakazi zaidi ya 120,0000, Qatar zaidi ya wafanyakazi 60,000 na nchi nyingine za Kiarabu zaidi ya 40,000 hivyo nimejifunza kwamba fedha wanayopata kutoka nje kutokana na ajira za nje ni zaidi hata ya fedha zinazotokana na mazao yao makuu ya biashara kama vile Kahawa na Chai. Nimemwelekeza Mkurugenzi anayehusika na Huduma za Ajira aangalie ni kwa jinsi gani tunaweza kujifunza kutoka kwa wenzetu ili nasi tuweze kunufaika na ajira za nje ya nchi,” ameeleza Prof. Katundu.

Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi. Khadija Mwenda, amesema ziara hiyo inafungua ukurasa mpya wa ushirikiano hususan kwenye eneo la sheria na taratibu mbali mbali za kazi baina ya OSHA Tanzania na Kenya jambo ambalo litakuza uwekezaji baina ya nchi zote mbili pamoja na kuleta ufanisi katika utekelezaji wa sera ya soko la pamoja la Afrika Mashariki.

“Tumekuwa na mazungumzo mazuri sana, tumejifunza kutoka kwao na wamejifunza kutoka kwetu lakini tunafahamu kuwa sisi ni Jumuiya ya Afrika Mashariki na katika Jumuiya hii kuna kitu kinaitwa Soko la Pamoja (Common Market) na kuna wawekezaji wa Tanzania huko Kenya na wao wapo hapa kwetu. Hivyo ni muhimu sana kwa nchi hizi kuwa na ulinganifu wa sheria mbali mbali ili kuwezesha uwekezaji na biashara kufanyika katika mazingira mazuri,” amesema Mtendaji Mkuu wa OSHA.

Naye Mkurugenzi wa Masuala ya Usalama na Afya katika Wizara ya Kazi Nchini Kenya, Dkt. Musa Nyandusi, amesema wapo mbioni kuunda Taasisi Mahsusi kwa ajili ya kusimamia masuala ya Usalama na Afya nchini kwao ili kuendana na miongozo ya Shirika la Kazi Duniani (ILO) hivyo wanatarajia kujifunza mengi kutoka Tanzania ambayo imepiga hatua kubwa katika usimamizi wa masuala husika.

Taasisi ya OSHA ilianzishwa rasmi Agosti 31, 2001 ikiwa ni jitihada za serikali ya Tanzania ili kuendana na mabadiliko ya kiuchumi, kiteknolojia pamoja na kukidhi matakwa ya Mikataba ya Kimataifa ya ILO inayozitaka nchi wanachama kuwa na chombo mahsusi cha kusimamia masuala ya usalama na afya mahali pa kazi.
Share:

Friday, 21 April 2023

MRAJIS ATOA WITO KUENDELEZA MICHEZO



Mrajis wa Vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Dkt. Benson Ndiege akiwa amekaa katikati ya Timu ya Watumishi wa Tume ‘TCDC Ushirika Sport’ mara baada ya kikao na Timu hiyo ikiwa katika Mashindano ya Kombe la Mei Mosi 2023 Mkoani Morogoro


Picha mbalimbali za Watumishi wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika (TCDC) wakishiriki michezo mbalimbali Mashindano ya Kombe la Mei Mosi 2023 Mkoani Morogoro

Na.Mwandishi Wetu-MOROGORO

Mrajis wa Vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika (TCDC) Dkt. Benson Ndiege ametoa wito kwa Watumishi wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika kutumia fursa za Michezo zinazojitokeza kujifunza mbinu mbalimbali na kuendeleza Michezo.

Ametoa wito huo alipotembelea kambi ya Michezo ya Watumishi wa Tume ya Timu ya ‘TCDC Ushirika Sports’ wakati wakiendelea kushiriki Michezo ya Kombe la Mei Mosi Mkoani Morogoro Aprili 21,2023

Mrajis amewataka Watumishi wa Tume kuzingatia masuala ya michezo kwa kushiriki na kubuni programu za Michezo zitakazo ongeza wigo wa ushiriki wa Watumishi pamoja na kuongeza ubora na ushindani wa Timu ya Tume, ili kuendeleza Michezo kwa afya na ufanisi kazini.

Mwenyekiti wa Timu ya Tume ‘TCDC Ushirika Sport’ Mrajis Msaidizi Ibrahim Kadudu akiongea kwa niaba ya wanamichezo hao ameshukuru Uongozi wa Tume kwa kuendelea kujitoa katika kuhakikisha Watumishi wanashiriki fursa mbalimbali za michezo zinazoongeza tija katika afya na maendeleo ya Watumishi.

‘TCDC Ushirika Sport’ imeshiriki Michezo ya Kombe la Mei Mosi 2023 katika michezo mbalimbali ikiwemo Mpira wa Miguu, Mpira wa Wavu, kuvuta Kamba na itaendelea na mingine iliyosalia kuelekea Siku ya Kilele cha Sherehe za Wafanyakazi Mei Mosi.
Share:

TCRA YATOA MWONGOZO WA KUSAFIRISHA VIFURUSHI & VIPETO...ZINGATIA MAMBO HAYA KABLA KUSAFIRISHA MZIGO


Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Katika kukabiliana na vitendo vya udanganyifu, utapeli na upotevu wa mizigo wakati wa usafirishaji wa vifurushi na nyaraka mbalimbali (Vipeto), Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imezitaka Kampuni zinazotoa huduma hiyo kutimiza matakwa ya kisheria kwa kukata leseni ya usafirishaji vifurushi na vipeto kutoka TCRA

Kipeto ni mzigo mdogo wa angalau kilo moja au chini ya hapo na kifurushi ni kikubwa kuliko kipeto. Kifurushi huwa na uzito wa hadi angalau kilo 20 au 30.


Akizungumza na Mwandishi wa habari hizi leo Aprili 20,2023 Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo amesema kuwa na leseni ya kusafirisha vifurushi na vipeto ni muhimu kwa sababu inaruhusu mtu au kampuni kufanya biashara ya usafirishaji wa bidhaa hizo za kiposta kwa njia halali na yenye kufuata Sheria na Kanuni za usafirishaji.


Amesema Leseni hiyo inahakikisha kuwa mtoaji huduma ya usafirishaji amefuata taratibu zote muhimu kwa ajili ya usalama wa bidhaa na kuepuka adhabu ya kisheria.


Amezitaja baadhi ya sababu za umuhimu wa kuwa na leseni ya kusafirisha vifurushi na vipeto ni kwamba Leseni inahakikisha Mtoa Huduma/ kampuni au mtu binafsi anayefanya biashara ya usafirishaji wa bidhaa za kipeto vikiwemo vipeto na vifurushi amefuata sheria na kanuni za usafirishaji. 

"Hii ni muhimu kwa sababu Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (2010) Kifungu cha Sita kinaelekeza Dhahiri kwamba Mtu Yeyote au Kampuni inayotaka kutoa Huduma za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta sharti aombe na kupatiwa Leseni inayotolewa na TCRA",ameeleza.
Sababu nyingine ni kwamba Leseni ya usafirishaji vipeto na vifurushi inaweza kuongeza uaminifu wa wateja kwa kampuni au mtu binafsi anayetoa huduma za usafirishaji wa bidhaa. Hii ni kwa sababu leseni inathibitisha kuwa mtoaji huduma anafuata taratibu na kanuni za usalama za kusafirisha vifurushi na vipeto.


Hali kadhalika Leseni inaweza kusaidia kampuni au mtu binafsi anayefanya biashara ya usafirishaji wa bidhaa kuwa na uwezo wa kudhibiti hatari za usafirishaji wa bidhaa. Leseni inaweza kusaidia kampuni au mtu binafsi kuelewa sheria za usafirishaji wa bidhaa na kuzuia uwezekano wa kupoteza au kuharibiwa kwa bidhaa au kusafirisha bidhaa zilizozuiwa kwa mujibu wa sheria.


“Kwa hiyo, kuwa na leseni ya kusafirisha vifurushi na vipeto ni muhimu sana kwa sababu inahakikisha kuwa biashara ya usafirishaji wa bidhaa inafuata sheria na kanuni za usalama na kuongeza uaminifu wa wateja”,ameongeza Mhandisi Mihayo.


Mhandisi Mihayo amesema Leseni ya usafirishaji wa vifurushi na vipeto (Courier Service License) hutolewa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa mujibu wa Sheria ya Mawasiliano ya Elektroniki na Posta ya mwaka 2010.


“TCRA imerahisisha sana upataji wa Leseni za Mawasiliano. Kwa sasa unahitaji kujisajili kwenye tovuti ya Tanzanite ambayo inapatikana kwa kiunganishi cha www.tanzanite.tcra.go.tz . Ukiingia hapo jisajili kisha jaza fomu za maombi ya leseni kwa kuzingatia aina ya leseni unayotaka kuomba”,amesema Mhandisi Mihayo.


Mhandisi Mihayo amesema TCRA imezindua kampeni ya elimu ya umma ili kuwaelimisha watumiaji wa huduma za usafirishaji vipeto na vifurushi kuwa na ufahamu wa kutumia watoa huduma waliosajiliwa/wenye leseni za kutoa huduma husika ambapo kampeni hii inalenga kuwakumbusha watoa huduma kusajili biashara/huduma zao na kuzingatia sheria na kanuni zinazosimamia sekta hiyo.


“Kwa kawaida, watumiaji wa huduma hizi baadhi yao hawajui nani ni mtoa huduma aliyesajiliwa, hivyo kampeni hii inawaelimisha wananchi kwamba mtoa huduma aliyesajiliwa Taarifa zake zinapatikana kwenye dawati la duka lake (kwa kuonesha leseni-inayopaswa kuwekwa mahali panapoonekana aghalabu ukutani). Pia mtoa huduma aliyesajiliwa Taarifa zao zinapatikana kwenye tovuti ya TCRA www.tcra.go.tz ambako kuna orodha kamili ya wenye leseni”,ameeleza Mhandisi Mihayo.

“Tunaposema Tuma Chap kwa Usalam tunamaanisha Mwananchi azingatie kutuma kipeto/kifurushi chake kwa mtoa huduma aliyesajiliwa, kwani kufanya hivyo kunaiwezesha TCRA kufuatilia Haki na Wajibu kwa pande zote mbili mfano mtoa huduma na anayehudumiwa",amesema.
Amesema kuzinduliwa kampeni Tuma Chap kwa Usalama ni sehemu ya majukumu ya TCRA katika kuendeleza kuongeza uelewa wa umma kuhusu umuhimu wa kutumia watoa huduma waliosajiliwa wa kubeba Vipeto na Vifurushi na kuwakumbusha watoa huduma kuzingatia sheria na kanuni za sekta hiyo kwa lengo la kuboresha usalama wa Vipeto na Vifurushi inayosafirishwa na kuimarisha biashara katika sekta ya kubeba Vipeto na Vifurushi nchini Tanzania.


MWANANCHI AZINGATIE NINI KABLA YA KUTUMA KIPETO/KIFURUSHI

“Kabla ya kumkabidhi msafirishaji Kifurushi au Kipeto, mwananchi anatakiwa kuzingatia kama Mtoa Huduma ana na Leseni inayomruhusu kusafirisha vipeto na vifurushi. Pia mwananchi ahakikishe anapatiwa Risiti ya Utumaji mzigo, ahakikishe anamjulisha msafirishaji bidhaa inayosafirishwa na ikaguliwe,ahakikishe anapatiwa namba ya kufuatilia mzigo (tracking number) na ahakikishe kipeto au kifurushi chake kimefungwa vizuri, na kama ni mali ya kuharibika kirahisi kv chupa nk aweke bayana kwa kuweka maandishi yanayotahadharisha wabebaji”,ameeleza Mhandisi Mihayo.

“Mwananchi ananufaika kwa kutumia msafirishaji wa vifurushi na vipeto mwenye Leseni ya TCRA kwa njia kadhaa kama vile Usalama wa vifurushi na vipeto ambapo Msafirishaji mwenye leseni ya TCRA anawajibika kuhakikisha kuwa vifurushi na vipeto vyote vinavyosafirishwa vinawasili salama na katika hali nzuri lakini pia Msafirishaji mwenye leseni ya TCRA anawajibika kutoa huduma ya haraka na kwa wakati kwa wateja wake, hivyo kurahisisha shughuli za biashara kwa wateja wake”,amesema.


“Pia faida nyingine ni kwamba Msafirishaji mwenye leseni ya TCRA hutoa huduma ya kuchukua na kuleta vifurushi na vipeto moja kwa moja kwa mlango wa mteja wake, hivyo kuwapa wateja wake urahisi wa kusafirisha bidhaa. Hali kadhalika Msafirishaji mwenye leseni ya TCRA hutoa huduma za usafirishaji kwa bei nafuu na kwa ushindani mkubwa katika soko kwa kuwa TCRA inasimamia ushindani wa kibishara wenye kuzingatia haki kwa mtumiaji huduma”,ameongeza Mhandisi Mihayo.


Amefafanua kuwa Msafirishaji mwenye leseni ya TCRA hutoa huduma ya kufuatilia vifurushi na vipeto kwa njia ya kielektroniki, hivyo kutoa uhakika kwa wateja wake kuwa vifurushi na vipeto vyao vinawasili salama na kwa wakati uliopangwa.

“Kwa hiyo, kutumia msafirishaji wa vifurushi na vipeto mwenye Leseni ya TCRA kunampa mteja uhakika wa huduma bora, salama, haraka na kwa gharama nafuu, hivyo kumwezesha kufanya biashara yake kwa ufanisi zaidi”,amesema.


“Kabla ya kumkabidhi msafirishaji Kifurushi au Kipeto, mwananchi anatakiwa kuzingatia kama Mtoa Huduma ana na Leseni inayomruhusu kusafirisha vipeto na vifurushi. Pia mwananchi ahakikishe anapatiwa Risiti ya Utumaji mzigo, ahakikishe anamjulisha msafirishaji bidhaa inayosafirishwa na ikaguliwe,ahakikishe anapatiwa namba ya kufuatilia mzigo (tracking number) na ahakikishe kipeto au kifurushi chake kimefungwa vizuri, na kama ni mali ya kuharibika kirahisi kv chupa nk aweke bayana kwa kuweka maandishi yanayotahadharisha wabebaji”,ameeleza Mhandisi Mihayo.
“Mwananchi ananufaika kwa kutumia msafirishaji wa vifurushi na vipeto mwenye Leseni ya TCRA kwa njia kadhaa kama vile Usalama wa vifurushi na vipeto ambapo Msafirishaji mwenye leseni ya TCRA anawajibika kuhakikisha kuwa vifurushi na vipeto vyote vinavyosafirishwa vinawasili salama na katika hali nzuri lakini pia Msafirishaji mwenye leseni ya TCRA anawajibika kutoa huduma ya haraka na kwa wakati kwa wateja wake, hivyo kurahisisha shughuli za biashara kwa wateja wake”,ameeleza.


“Pia faida nyingine ni kwamba Msafirishaji mwenye leseni ya TCRA hutoa huduma ya kuchukua na kuleta vifurushi na vipeto moja kwa moja kwa mlango wa mteja wake, hivyo kuwapa wateja wake urahisi wa kusafirisha bidhaa. Hali kadhalika Msafirishaji mwenye leseni ya TCRA hutoa huduma za usafirishaji kwa bei nafuu na kwa ushindani mkubwa katika soko kwa kuwa TCRA inasimamia ushindani wa kibishara wenye kuzingatia haki kwa mtumiaji huduma”,ameongeza.


Amefafanua kuwa Msafirishaji mwenye leseni ya TCRA hutoa huduma ya kufuatilia vifurushi na vipeto kwa njia ya kielektroniki, hivyo kutoa uhakika kwa wateja wake kuwa vifurushi na vipeto vyao vinawasili salama na kwa wakati uliopangwa.

“Kwa hiyo, kutumia msafirishaji wa vifurushi na vipeto mwenye Leseni ya TCRA kunampa mteja uhakika wa huduma bora, salama, haraka na kwa gharama nafuu, hivyo kumwezesha kufanya biashara yake kwa ufanisi zaidi”,amesema.

“Majukumu ya TCRA katika usimamizi wa usafirishaji wa vifurushi na vipeto ni pamoja na kusimamia watoa huduma za usafirishaji vifurushi na vipeto na huduma za Posta. TCRA ina jukumu la kusimamia na kudhibiti huduma zote za mawasiliano nchini Tanzania, zikiwemo huduma za usafirishaji vifurushi na vipeto kama sehemu ya huduma za posta”,ameeleza Mhandisi Mihayo.


Majukumu mengine ya TCRA ni kutoa leseni kwa wanaohitaji kutoa huduma za Posta ambazo zinahusisha usafirishaji vifurushi na vipeto ambapo TCRA inatoa leseni kwa watoa huduma za mawasiliano kama vile kampuni za simu za mkononi, kampuni za intaneti, na vituo vya redio na televisheni pamoja na Posta. Huduma za usafirishaji vipeto na vifurushi katika mukhtadha huu zimo katika kundi la huduma za Posta.


Pia TCRA ina jukumu la kulinda haki za watumiaji wa huduma za mawasiliano ambapo TCRA inalinda haki za watumiaji wa huduma za mawasiliano kwa kuhakikisha kwamba watoa huduma wanafuata kanuni na taratibu zilizowekwa na TCRA na kutoa huduma bora kwa watumiaji.

“Hapa ndipo unakuja Umuhimu wa Mwananchi kuhakikisha anatuma kipeto chake kwa mtoa huduma aliyesajiliwa ili iwe rahisi zaidi kwa TCRA kulinda haki za Mwananchi kama mtumiaji wa huduma.

“Pia TCRA tuna jukumu la kusimamia usalama wa huduma zitolewazo TCRA inasimamia usalama wa huduma za usafirishaji vipeto na vifurushi kwa kuhakikisha kwamba mtoa huduma anazingatia sheria na Masharti ya Leseni wakati wote anapotoa huduma ya kusafirisha vipeto na vifurushi. Kwa hiyo, TCRA ina jukumu la kutoa leseni kwa watoa huduma za posta nchini Tanzania, kusimamia ubora wa huduma za posta, kushughulikia malalamiko ya watumiaji, na kuhakikisha usalama wa mawasiliano yanayohusisha usafirishaji wa vifurushi na vipeto kama bidhaa za kiposta", amesema.


TCRA pia inaweza kushirikiana na wadau wengine, kama vile Shirika la Posta Tanzania (TPC), katika kusimamia na kuboresha huduma za posta nchini Tanzania, ikiwa ni pamoja na usafirishaji wa vifurushi na vipeto.

Linda thamani ya mzigo wako; tumia Mtoa Huduma mwenye Leseni halali kutoka TCRA. Kwa maelezo zaidi, wasiliana na TCRA kupitia 0800008272 Bure.

TAZAMA ZAIDI HAPA


Share:

MERIDIANBET KASINO KUTOA MGAO WA TSH 2.5M


Kutoka nyumba ya mabingwa Meridianbet kasino ya mtandaoni yaja na promosheni nyingine, baada ya kutambulisha Drops &Wins sasa kuna hii ya Spring Mascot inakupa Mgao wa Tsh 2,500,000/= kwa dau la Tsh 500.

 

Shindano la Spring Mascot linafanyika kuanzia tarehe 21 hadi 27 Aprili kupitia kasino ya mtandaoni ambapo litakupa sababu halisi ya kwa nini Spring ni msimu mzuri zaidi.

 

Furahia michezo iliyochaguliwa na shindania mgao wako wa TZS 2,500,000.

JUMLA YA ALAMA inahesabiwa kwa kujumlisha JUMLA YA MIZUNGUKO ILIYOCHEZWA na mchezaji kwenye michezo ifuatayo:

 

- Fruit Machine x25

- Fruit Vegas

- Fruit Disco: Mega Stacks

- Double-Triple Fruits

- Riot

- Trump Card: Queen

- Fairytale Coven

- Bamboo Bear

- Book of Amaterasu

- The Candy Crush

 

Wachezaji 10 waliofanikiwa zaidi watagawana TZS 2,500,000 kama ifuatavyo:

 

Nafasi ya 1 - TZS 750,000

Nafasi ya 2 - TZS 500,000

Nafasi ya 3 - TZS 375,000

Nafasi ya 4 mpaka 10 - TZS 125,000 kila mmoja

 

Anza safari yako ya kusisismua ya Spring na ufurahie ushindi wako kutoka kasino ya mtandaoni!

 

Vigezo na Masharti:

 

Promosheni itadumu kuanzia 21.04. hadi 27.04., jumla ya siku 7.

 

Promosheni itapatikana tu kwa wachezaji kwenye tovuti na programu ya meridianbet.me, meridianbet.rs, meridianbet.co.tz, meridianbet.pe.

 

Wakati wa promosheni hii ya kasino ya mtandaoni, wachezaji watashindana katika michezo ya sloti ifuatayo ya Mascot:

Fruit Machine x25, Fruit Vegas, Fruit Disco: Mega Stacks, Double-Triple Fruits, Riot, Trump Card: Queen, Fairytale Coven, Bamboo Bear, Book of Amaterasu & The Candy Crush.

 

-Dau la chini ni TZS 500.

 

-Promosheni hii ya kasino ya mtandaoni ya Meridianbet  itahusisha pesa halisi pekee.

 

-Wachezaji watashindana kwa JUMLA YA MIZUNGUKO ILIYOCHEZWA.

 

-Wachezaji wanaweza kuangalia nafasi zao kwenye jedwali ambalo litawekwa kila siku ifikapo saa 10:00 jioni.

 

-Orodha ya mwisho ya washindi itatangazwa tarehe 28.04

 

Zawadi ya fedha itawekwa kwenye akaunti ya mchezaji tarehe 28.04. - siku baada ya kumalizika kwa promosheni. Washindi watapewa taarifa.

 

Meridianbet ina haki ya kubadili au kufuta promosheni hii wakati wowote.

 

Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

 

 

 


Share:

POLISI SHINYANGA LAWAHAKIKISHIA AMANI WANANCHI SIKUKUU YA EID EL FITR.... "MARUFUKU DISCO TOTO, WATOTO KUMBI ZA STAREHE"

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi


Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga limewataka wananchi kusherehekea Sikukuu ya Eid El Fitri kwa amani na utulivu huku likiwaasa wazazi kutowaruhusu watoto wao kwenda kwenye kumbi za starehe kwani kumbi hizo zipo kwa ajili ya watu wazima na si watoto.


Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Ijumaa Aprili 20,2023, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi amewataka wananchi kusherehekea Sikukuu ya Eid El Fitr kwa amani na utulivu huku akisisitiza kuwa Jeshi la Polisi linawahakikishia wananchi kuwa hali ya utulivu mkoani Shinyanga ni endelevu.



Amesema Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga linawahakikishia wananchi wa mkoa wa Shinyanga kuwa tutaendelea kuhakikisha kwamba hali hii ya utulivu iliyopo hivi sasa itakuwa ni endelevu kwa kipindi chote cha sikukuu ya Eid El Fitri na hata baada ya sikukuu.


"Tunaendelea kuwatahadharisha wazazi na wenye kumbi mbalimbali za starehe kwamba Disco toto ni marufuku. Kumbi yoyote itakayokutwa ikichezesha Disco toto itafungwa kwa kipindi chote cha sikukuu kwani Disco toto ni hatari kwa usalama wa watoto", amesema Kamanda Magomi.



"Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga linapenda kuwataarifu wananchi wa mkoa wa Shinyanga kwamba kwa kipindi cha msimu wa mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani hali ya usalama katika mkoa wa Shinyanga ilikuwa shwari kwani tangu kuanza kwa mfungo wa Ramadhani hadi hivi sasa, hakuna tukio kubwa lililojitokeza ambalo limehatarisha au kuleta taharuki katika jamii", ameongeza Kamanda Magomi.


"Nawatakia kila la kheri waislamu wote na wana Shinyanga kwa ujumla katika kusherehekea sikukuu ya Eid El Fitr. Lakini pia napenda kutoa wito kwa madereva wa Magari, Bodaboda, Baiskeli na watembea kwa miguu kuwa makini wawapo barabarani ili kuweza kuepuka ajali ambazo zinaweza kuepukika", amesema Kamanda Magomi.
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO IJUMAA APRILI 21,2023

 


























Share:

Thursday, 20 April 2023

TANZANIA NA UJERUMANI ZAWEKA MIKAKATI KABAMBE KUPUNGUZA MIGOGORO BAINA YA WANYAMAPORI NA BINADAMU


👉 Ujerumani yatoa bilioni 16

Na John Mapepele

SERIKALI ya Ujerumani kupitia Shirika lake la Maendeleo la Kimataifa (GIZ) imetoa msaada wa Euro milioni 6 (16 bilioni) kusaidia juhudi za serikali katika uhifadhi wa bioanuai na kukabiliana na Migogoro ya Wanyamapori (HWC) na binadamu kwenye Maeneo ya Hifadhi.

Tukio hilo la kihistoria limeshuhudiwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mohammed Mchengerwa na Balozi wa Ujerumani nchini, Regine Hess, na wadau mbalimbali wa uhifadhi leo jijini Dar es Salaam, ambapo mkataba huo umesainiwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Hassan Abbasi kwa upande wa Tanzania na Dkt. Mike Falke, Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Ujerumani (GIZ).




Aidha, Mhe. Mchengerwa amefafanua kuwa pamoja na mambo mengine lengo la fedha hizo ni Kupambana na Wanyama Waharibifu katika maeneo ya Kusini ya Kusini mwa Tanzania ambapo ameiomba Serikali ya Ujerumani kuendelea kunisaidia Tanzania kwenye uhifadhi wa raslimali.

Waziri Mchengerwa ameongeza kuwa mradi huo wa miaka mitatu utakaotekelezwa katika mfumo ikolojia wa Selous kusini mwa Tanzania, mbali na kukabiliana na HWC utasaidia katika kulipa fidia kwa jamii zilizoathirika na wanyama.

Mhe. Mchengerwa amebainisha kuwa jamii zitawezeshwa kupitia mafunzo ya mbinu sahihi za kukabiliana na hali hiyo pamoja na kurahisisha matumizi ya teknolojia za kisasa katika kupunguza HWC kama vile kupaka rangi za tembo na uzio wa kijiografia.

Amesema Serikali imekuwa ikichukua hatua mbalimbali za kuimarisha shughuli za uhifadhi ambazo ni pamoja na kuandaa Mkakati wa Kitaifa wa Usimamizi wa HWC-2020/2024.

Amesema kupitia mkakati huo, wizara imeanzisha vituo 154 vya Askari wa uhifadhi nchini kote ili kukabiliana na HWC, na kuongeza vituo vingine 15 vitajengwa kabla ya mwisho wa Juni 2023.

Amesema zaidi ya skauti 180 ngazi ya vijiji (VGS) wamepatiwa mafunzo na kuwezeshwa kukabiliana na HWC, akibainisha kundi jingine la VGS 120 litaanza mafunzo mwishoni mwa mwezi huu.

Ameongeza: “Katika kushughulikia HWC, serikali inafanya kazi na washirika wa uhifadhi na maendeleo katika kujenga uwezo wa taasisi na jumuiya zake.

Mhe. Mchengerwa ameeleza kuwa Serikali ya Ujerumani ni mdau mkubwa katika uhifadhi wa bioanuwai ambapo amekuwa na mchango mkubwa katika suala la uhifadhi kwa zaidi ya miaka 60.”

Kwa miaka sita iliyopita, Serikali ya Ujerumani imesaidia shughuli za uhifadhi kupitia ruzuku zenye thamani ya Euro milioni 124, alisema.

Regine Hess, Balozi wa Ujerumani nchini amepongeza Tanzania katika suala la uhifadhi huku akisisitiza kuwa Tanzania imeweza kuhifadhi sehemu kubwa ya ardhi yake ikilinganishwa na mataifa mengine mengi.




Amesema juhudi za uhifadhi zimesababisha ongezeko la wanyamapori wakiwemo tembo.

“Idadi ya wanyama imeongezeka; lakini kupitia uhifadhi pia tunaimarisha utalii na kutengeneza ajira,” alisema Hess.

Amesema Serikali yake inaunga mkono juhudi za uhifadhi wa bioanuwai na kupunguza HWC kwa sababu wakati mwingine migogoro husababisha watu kuuawa.

Aidha, amefafanua kuwa Serikali yake pia iko tayari kuisaidia Tanzania katika kuandaa Mkakati wa Kitaifa wa Utalii ili kuboresha utalii nchini.

Dkt. Mike Falke, Mkurugenzi wa GIZ nchini Tanzania na Jumuiya ya Afrika Mashariki alisema wamekuwa wakitoa msaada katika kukabiliana na HWC pamoja na sekta nyinginezo kama vile maji, afya, kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi na Unyanyasaji wa Kijinsia (GBV), miongoni mwa mengine.

Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Maurus Msuha amesema kupitia mradi huo jamii zinatarajiwa kunufaika kupitia Maeneo ya Hifadhi ya Wanyamapori (WMAs).

“Uhifadhi ni kwa ajili ya watu; inachangia ukuaji wa uchumi na maendeleo ya watu,” alisema Dkt. Msuha.




Sekta ya utalii inatoa ajira kwa watu milioni 1.5 kote nchini.

“Kusainiwa kwa mkataba huu ni ishawa kuwa Serikali imeanza na itaendelea kulipa uzito suala la uhufadhi na hasa kupunguza athari za wanyama waharibifu kama tembo kwa kushirikiana na wadau kama mnavyoona hapa leo,” alisema Waziri Mchengerwa.
Share:

DC MPWAPWA ATANGAZA OPERESHENI KUKAMATA WAIBA VYUMA RELI SGR, NANE WAKAMATWA, WENGINE WAJISALIMISHA


Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma Mhe. Sophia Kizigo akizungumza na Wananchi Kata ya Berege, kijiji cha Berege


Na Mwandishi Wetu Michuzi TV -Mpwapwa

MKUU wa Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma Sophia Kizigo amesema kwa sasa wanaendelea na operesheni maalum ya kukamata watu wanaoiba vyuma vilivyofungwa kwenye minara ya kupitisha nyaya za umeme kwenye mradi wa reli ya kisasa ya SGR.

Kwa mujibu wa Kizigo hadi sasa jumla ya watu nane katika Kata ya Berege, kijiji cha Berege ambako mradi wa SGR imepita wanashikiliwa kwa tuhuma za kujihusisha na wizi wa vyuma hivyo na kisha kuuza kwa wananchi kwenye baadhi ya Wana kijiji.

Akizungumza hivi karibuni Wilayani Mpwapwa, Mkuu wa Wilaya Kizigo amesema katika ujenzi wa reli hiyo TRC na TANESCO ndio wanaohusika na ujenzi kwa maana ya TRC wanajenga miundombinu ya reli hiyo na TANESCO wanaoweka miundombinu ya minara ya kupitisha nyaya za umeme kwa ajili ya treni ya SGR.

"Sasa kilichotokea kwenye ile minara ya kupitisha njia za umeme wahuni wameiba vyuma kwenye minara,wanafungua vyuma wanaenda kuuza tulivyofahamu hivyo ,tulifanya uchunguzi wa kimya kimya ili tuweze kuwashika hao watu na tukakamata baadhi ya watu.

"Mpaka sasa watu nane wamewekwa ndani na tuliwakamataje, kuna watu tuliwakuta kwenye kuta za nyumba zao wamefunga hivyo vyuma, wengine gereji , na wakiulizwa wanasema wameuziwa , unamuuliza aliyemuuzia hivyo hivyo unamfuata unamkata.

"Kuna watu walikuwa wamefungiwa hivyo vyuma na hawavijui ,wenyewe wamelipa tu fedha lakini hata kama ufahamu si umenunua mwisho wa siku tunaweza kushitaki Kijiji kizima. Kwa hiyo ikabidi Aprili 13 mwaka huu tukafanye mkutano na baada ya kufanya mkutano malengo makubwa yalikuwa mawili,"amesema.

Amefafanua lengo la kwanza aliamua kuchukua watu wa TANESCO kutoka mkoani na akawataka kwanza wakatoe elimu kwa wananchi kwamba vile vyuma kwanza vina namba na vimetengenezwa kwa maombi maalum, kwa hiyo havifanani na vyuma vyovyote.

"Kikiibwa kitajulikana tu kipo tofauti, kwa hiyo nilitaka wawape elimu kwanza madhara ya hicho kilichofanyika kwasababu kwenye zile nguzo unapochomoa machuma unafanya kiwe dhaifu inapofika kipindi treni inaanza kazi ikipita tu pale lazima kutokea ajali kwa sababu zile nguzo ndio zimeshika zile nyaya Kwa hiyo ni changamoto kubwa.

"Baada ya kuwapa elimu nikatoa muda kuanzia saa Saba mchana hadi saa 12 jioni wenye hivyo vyuma wavipeleke kwa Ofisa Mtendaji Kata, tuliwapa nafasi ya kwenda kuvisalimisha kwa Mtendaji wa kata na baada ya hapo tutaendelea na operesheni na tutayemkuta na hicho chuma atakuwa amedhamiria.


Kwa hiyo tukawapa hiyo nafasi ,wananchi wakafurahi kwasababu walikuwa hawana amani lakini pia tulifanya hivyo ili watu waendelee na shughuli zao za uzalishaji mali."



Baadhi ya Wananchi wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Sophia Kizigo (hayupo pichani) wakati mkutano ukiendelea







Moja ya Vyuma ambavyo vimekuwa vikiibiwa kwenye mradi huo kikioneshwa kwa Wananchi
Share:

MBUNGE KITANDULA AISHUKURU SERIKALI KUWAPATIA BILIONI 7 KWA AJILI YA MAENDELEO

 



Na Mwandishi Wetu,Dodoma.

MBUNGE wa Jimbo la Mkinga (CCM) Dastan Kitandula ameishukuru Serikali kwa kuwapatia fedha bilioni 7 kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo  na matumizi mengine kwenye Jimbo hilo .

Kitandula aliyasema hayo leo wakati akichangia Bajeti ya Kitandula-kuchangia bajeti ya Wizara ya Wizara ambapo alisema kwa upande wa barabara na miundombinu ya shule kwenye eneo walipangiwa kupata Bilioni 2 na wanapatiwa Bilioni 1.3 wanaomba fedha nyengine zilizobakia karibia milioni 700 zipatikane ili waweze kukamilisha miradi hiyo.

Alisema kwenye eneo la miundombinu ya shule wana milioni 692 wanakwenda kujenga shule mpya ya Msingi na Ujenzi wa Madarasa na matundu ya vyoo na wanazielekeza kwenye maeneo ya Maramba JKT,Mazola Kilifi,Mtimbwani,Kisiwani A na Perani hivyo wanaishukru sana Serikali

“Mh Spika kwenye eneo la Sekta ya Afya tunaishukuru Serikali kwa kutuanzishia ujenzi wa Hospitali ya wilaya tumeshaanza kutibu wagonjwa wa nje lakini bado changamoto ipo kwenye matibabu ya kibingwa kuwalaza wagonjwa na kufanya upasuaji  ambao bado wanatumia hospitali ya rufaa ya mkoa wa Tanga Bombo”Alisema

Mbunge huyo alisema kwamba wanaiomba Serikali iwapoatie fedha wakamilishe ujenzi wa wodi na vifaa tiba katika Hospitali ya wilaya ya Mkinga ili wananchi waweze kupata huduma katika eneo hilo

Mwisho.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger