Monday, 17 April 2023

KANISA LA MLIMA WA MOTO WAENDELEZA MAONO YA HAYATI DK. RWAKATARE UAMSHO WA NDOA

Bishop Rose Mgeta akizungumza kwenye kongamano la uamsho wa ndoa lililoandaliwa na Kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni A jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Wagenimbalimbali wakijipatia chakula kwenye kongamano la uamsho wa ndoa lililoandaliwa na Kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni A jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki
Mchungaji aliyejipatia umaarufu kwenye mitandao ya kijamii, Richard Hananja akifuatilia mambo kwenye kongamano la uamsho wa ndoa lililoandaliwa na Kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni A jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki
Dk. Rose Rwakatare ambaye ni mtoto wa Mwanzilishi wa Kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni A jijini Dar es Salaam akifuatilia mambo kwenye kongamano la uamsho wa ndoa lililoandaliwa na Kanisa la Mlima wa Moto.
Washiriki mbalimbali wakifuatilia mambo kwenye kongamano la uamsho wa ndoa lililoandaliwa na Kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni A jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Askofu Danstan Maboya akifanya maombi kwenye kongamano la uamsho wa ndoa lililoandaliwa na Kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni A jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Wageni waalikwa wakifuatilia kwenye kongamano la uamsho wa ndoa lililoandaliwa na Kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni A jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki


*****************

Na Mwandishi Wetu

ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Mlima wa Moto, Mikocheni jijini Dar es Salaam, Bishop Rose Mgeta amesema Kanisa hilo litaendelea kutekeleza maono ya Mwanzilishi wa Kanisa hilo, Hayati Askofu Dk Getrude Rwakatare kutimiza maono yake kama kuendeleza makongamano ya uamsho wa ndoa kila mwaka.

Hayati Dk. Getrude Rwakatare alianzisha kongamano la uamsho wa ndoa mwaka 2000 kwa lengo la kuhakikisha anaokoa ndoa nyingi baada ya kuona ndoa nyingi zikiingia kwenye mogogoro na kusababisha watoto wengi kuachwa mitaani.

Kongamano hilo lilifanyika mwishoni mwa wiki na Maaskofu waliohudhuria hafla hiyo ni Rose Mgeta wa Mlima wa moto, Dastan Maboya, Richard Hananja, Daniel Mgogo,

Askofu Rose alisema kupitia tukio la uamsho wa ndoa, ndoa nyingi zimepona kutokana na shuduma mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na watu waliokuwa wanahudhuria makongamano hayo.

Alisema hata watoto wa hayati Getrude Rwakatare wamekuwa mstari wa mbele kuhakikisha ndoto za mwanzilishi wa Kanisa hilo zinatimizwa.

Mtoto wa Hayati Dr Getrude Rwakatare, Dk. Rose Rwakatare, ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Morogoro, alisema kongamano la uamsho wa ndoa ilianzishwa mwaka 2,000 kupitia maono ya mwanzilishi wa Kanisa la Mlima wa Moto, Hayati Getrude Rwakatare.

Alisema kutokana na huduma kubwa ambayo Mungu alimkirimia kuhudumia waumini wa Kanisa na katika huduma zote Mungu alizomwitia katika ndoa alitilia mkazo watu kupendana na kuheshimiana na ndipo akaanzisha uamsho wa ndoa.

“Askofu Rwakatare alipenda wanandoa waishi kwa upendo ili ndoa ziweze kudumu na kuwa bora na zilizojaa amani na utulivu kwani hapo ndipo afya ya akili inapokuwepo na kuwa na familia bora,” alisema

Dk. Rose alisema kwa kushirikiana na wazee wa Kanisa hilo na askofu wa kanisa hilo, Askofu Rose Mgeta wamefanikisha kuendeleza tukio la uamsho wa ndoa kwa miaka yote na kwamba wamekusanyika kufanya uamsho wa ndoa ili ziweze kupata uamsho na ndoa ziweze kupona na kuwapa amani ya moyo wana ndoa.

“Kuwa na ndoa yenye masilikilizano inawezekana, Biblia inasema utaacha wazazi wako utaambanana na mwenzako na mtakuwa mwili mmoja sasa mwanaume asimame kwenye nafasi yake na mwanamke naye asimame kwenye nafasi yake kama mama na hapo mtayashinda majaribu yote,” alisma

“Jambo hili linasaidia kuwakumbusha wanandoa kuhusu mambo ambayo yako kinyume na mila na desturi za kitanzania kama mambo ya kuiga yanayoleta mmomonyoko wa maadili kwenye taifa, mfano ukatili wa majumbani unaosabaaisha vifo, kila kukicha unasikia huyu kampiga risasi mwenzake, huku kamchinja mwenzake haya hayakubaliki,” alisema

Aidha, Dk. Rose alisema wimbi jipya linaitesa dunia ni ndoa za jinsia moja na yeye kama Mwenyekiti wa Wazazi Mkoa wa Morogoro amekuwa mstari wa mbele kupinga vitendo hivyo kwani havitaleta mustakabali mwema kwa taifa la Tanzania.

“Tumuunge mkono Rais wetu Samia Suluhu Hassan, hili ni pepo ambalo tunapaswa kulikemea kwa nguvu zetu zote, tunapaswa kusali kwa bidii ili liondoke, kama majanga mengine ambayo tulipiga magoti yakaondoka hili nalo kwanini tusiombe likaondoka, wazazi tusimame kwa umoja wetu kupinga jambo hili, “ alisema

Kwa upande wake, Askofu Daniel Mgogo alisema amekuwa akitoa mafundisho mbalimbali ya ndoa kwenye mitandao ya kijamii lakini kwa muda wa miezi sita hakuandika chochote kwani alikwua nchini Marekani.

“Kumbe yale mafundisho yangu mnayapenda kwasababu nimekuta watu wengi wameniandikia kwenye mitandao yangu ya kijamii kwamba mbona hatuyaoni, lakini kwenye uamsho wa ndoa sitapiga nondo,” alisema

“Katika viumbe ambavyo vinahitaji ustadi wa hali ya juu kukaa navyo ni binadamu, kukaaa na kiumbe kinaitwa binadamu ni kazi kubwa sana hata wachungaji kuchunga watu wanaitwa binadamu mwaka mzima ni kazi kubwa sana na inabidi ukifikisha mwaka upate muda wa kupumzika maana ni kazi kubwa,” alisema
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU APRILI 17,2023


Magazetini leo Jumatatu April 17 2023






Share:

Sunday, 16 April 2023

WAZIRI MKUU ATAKA VIONGOZI WA DINI KUSIMAMIA HAKI NA KUTUNZA AMANI

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza kwa niaba ya Waziri Mkuu Kasim Majaliwa wakati wa ibada ya Harambee ya ujenzi wa shule ya Kanisa la Kiinjili la Kikutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mashariki Ziwa Victoria-Mwanza iliyofanyika kanisani hapo mkoani Mwanza tarehe 16 April 2023
Sehemu ya waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKT) Dayosisi Mashariki ya Ziwa Victoria- Mwanza wakiwa katika ibada ya Harambee ya ujenzi wa shule ya Kanisa la KKKT Dayosisi ya Mashariki Ziwa Victoria-Mwanza iliyofanyika katika Kanisa hilo Ilemela mkoani Mwanza tarehe 16 April 2023.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akipokea zawadi ya picha kwa niaba ya Waziri Mkuu Kasim Majaliwa wakati wa ibada ya Harambee ya ujenzi wa shule ya Kanisa la Kiinjili la Kikutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mashariki Ziwa Victoria-Mwanza iliyofanyika kanisani hapo wilayani Ilemema mkoani Mwanza tarehe 16 April 2023.
Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Dayosisi ya Mashariki ya Ziwa Victoria- Mwanza Andrew Petro Gulle akizumgumza katika ibada ya Harambee ya ujenzi wa shule ya Kanisa la KKKT Dayosisi ya Mashariki Ziwa Victoria-Mwanza iliyofanyika katika Kanisa hilo katika manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza tarehe 16 April 2023.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiwaongoza waumini katika Harambee ya kuchangia ujenzi wa shule ya Kanisa la Kiinjili la Kikutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mashariki Ziwa Victoria-Mwanza iliyofanyika kanisani hapo mkoani Mwanza tarehe 16 April 2023.
Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Karagwe mkoani Kagera Askofu Dkt Benson Bagonza akizungumza mara baada ya kuchangia Harambee ya ujenzi wa shule ya Kanisa la KKKT Dayosisi ya Mashariki Ziwa Victoria- Mwamza tarehe 16 April 2023.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akionesha saa iliyotolewa na Waziri Mkuu Kasim Majaliwa kwa ajili ya kunadiwa ambapo saa hiyo ilinunuliwa kwa shilingi milioni 2.625 wakati wa Harambee ya ujenzi wa shule ya Kanisa la KKKT Dayosisi ya Mashariki Ziwa Victoria- Mwanza tarehe 16 April 2023.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiwa na viongozi wengine wakitoka katika ibada ya Harambee ya ujenzi wa shule ya Kanisa la KKKT Dayosisi ya Mashariki Ziwa Victoria- Mwanza tarehe 16 April 2023.
Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Dayosisi ya Mashariki ya Ziwa Victoria- Mwanza Andrew Petro Gulle akihitimisha Harambee ya ujenzi wa shule ya Kanisa la KKKT Dayosisi ya Mashariki Ziwa Victoria-Mwanza iliyofanyika katika Kanisa hilo katika manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza tarehe 16 April 2023.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiwa katika picha ya pamoja na kamati ya ujenzi wa shule wakati wa ibada ya Harambee ya ujenzi wa shule ya Kanisa la KKKT Dayosisi ya Mashariki Ziwa Victoria- Mwanza tarehe 16 April 2023. (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)

******************


Na Munir Shemweta, WANMM MWANZA

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kasim Majaliwa amewataka viongozi wa dini nchini kuhakikisha wasimamia haki na kuienzi na kusimamia amani kwa manufaa ya wananchi wa sasa na vizazi vijavyo.


"Niwasihi sana ninyi viongozi wetu wa dini kutukumbusha mara kwa mara sisi, waumini na watu wote kuhusu umuhimu wa kusimamia haki na kudumisha amani na kuiombea nchi yetu na viongozi wake" alisema Majaliwa.


Majaliwa alisema hayo leo tarehe 16 April 2023 katika hotuba yake iliyosomwa kwa niaba na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula wakati wa Ibada ya Harambee ya Ujenzi wa shule ya Kanisa la Kiinjili la Kikutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mashariki Ziwa Victoria-Mwanza iliyofanyika katika Kanisa la KKKT Imani wilayani Ilemela mkoani Mwanza.


kupitia harambee hiyo ya ujenzi wa shule ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mashariki ya Ziwa Victoria-Mwanza Kanisa hilo limefanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi 119,563,000 zikiwemo fedha taslimu, ahadi na vifaa.


Kupitia hotuba yake Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amewataka viongozi wa dini nchini kutochoka kufundisha na kulea vijana katika maadili mema na kuthamini kufanya kazi halali.


" Katika nyakati hizi ni ukweli ulio wazi kuwa kuna mmomonyoko mkubwa wa maadili katika jamii yeru, vitendo viouvu na mambo yasiyopendeza mwenyezi Mungu yanazidi kuongezeka mambo ambayo siku za nyuma yalikuwa nadra sana kutokea au kusikia lakini sasa yanakuwa habari za kila siku na wakati mwingine huonekana eti ya kawaida" alisema majialiwa kupitia hotuba yake.


Kwa mujibu wa Waziri Mkuu, kushuka kwa maadili ni jambo lenye athari mbaya kwa jamii na taifa kwa ujumla hivyo kunachangia sana na kurudisha nyuma juhudi za kujiletea maendeleo na kuifanya kazi ya kuondoa umasikini kuwa ngumu.


Amesema, anaamini kwa dhati kuwa viongozi wa serikali, dini na vyama vya siasa wakishika mafundisho ya dini na kuwa na hofu ya mungu maovu mengi yatapungua na nchi kuoongozwa vizuri.


" Naendelea kuwaomba kwa niaba ya serikali, viongozi wa dini zetu zote tusaidiane kukea taifa letu kimaadili na tuweke mkazo zaidi kwa vijana kwa sababu kwanza wao ndiyo wahanga wakuu wa maovu yanayotendeka lakini pia wao ni taifa la leo na viongozi wa kesho" alisema


Kupitia hotuba yake hiyo, Majaliwa alisisitizia pia suala la elimu na kueleza kuwa elimu ni muhimu kwa maendeleo ya taifa lolote na kutaka viongozi wa dini kusaidia kuzungumza na wazazi na kuwaslimisha kuhusu umuhimu wa kusomesha watoto.


Amelipongeza Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mashariki ya Ziwa Victoria -Mwanza na waumini kwa ujumla kwa kujitoa kwa hali na mali kwa kufanya kazi ya Mungu kwa kuhakikisha jengo linakamilikia hasa ikizingatiwa fedha zote ni michango ya waumini na kubainisha kuwa, kitendo kilichofanyika ni chema na kinaleta baraka zote.


Awali Askofu Mkuu wa KKKT Dayosisi Mashariki ya Ziwa Victoria- Mwanza Andrew Petro Gulle alisema ujenzi wa shule ya kanisa hilo unakadiriwa kuwa na gharama ya Shilingi 2,350,000,000 ambapo amesema mpaka sasa kiasi cha 430,000,000 kimetumika kujenga boma la madarasa kumi na boma la jingo la utawala.


Katika harambee hiyo ya ujenzi wa shule Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alichangia shilingi milioni 5 ili kutumika kukamilisha kazi ya ujenzi wa shule huku Dkt Mabula kuchangia milioni 2 katika ujenzi huo.

Share:

UJENZI WA BARABARA YA MIKUMI - IFAKARA WAFIKIA 78%, MIRADI MINGINE MITANO KUJENGWA MOROGORO





Wakati ujenzi wa barabara ya Mikumi hadi Ifakara kwa kiwango cha Lami ukifikia asilimia 78, miradi mingine mitano ya barabara inatarajiwa kujengwa mkoani Morogoro.


Akizungumza na waandishi, Meneja wa Wakala wa Barabara (Tanroads) mkoa wa Morogoro, Alinanuswe Kyamba amesema ujenzi wa barabara hiyo unaohusisha pia ujenzi daraja la Ruaha Mkuu unatarajiwa kukamilika Oktoba mwaka huu.


"Hadi kufikia Aprili 2023, utekelezaji wa mradi kwa ujumla ulikuwa umefikia asilimia 78, kwa sasa Mkandarasi amekamilisha km 43 za lami na kazi zingine zinaendelea kwa hatua nzuri. Madaraja yote yameshakamilika kwa asilimia 83 na daraja la Ruaha mkuu bado kitako cha juu kukamilika," amesema.


Amesema kukamilika kwa daraja la Ruaha Mkuu kutafanya magari mawili kupita kwa wakati mmoja tofauti zamani.


Amesema wa mradi huo ulianza mwaka 2018 lakini changamoto mbalimbali ikiwemo mvua umetajwa kuwa sababu ya kuchelewa kukamilika kwa mradi huo.


"Pia Mlipuko wa homa ya Mapafu (COVID -19) ilichangia kuwapo kwa ucheleweshwaji wa uangizaji wabaadhi ya vitendea kazi kwa ajili ya mradi.

Mbali na barabara hiyo pia mkoa wa Morogoro unakwenda kutekeleza miradi mingine mitano ambayo itakwenda kuunganisha wilaya zote kwa kiwango cha lami na kuinua uchumiwa Wananchi wa maeneo hayo.


Kwa mujibu wa Kyanda miradi yote imekwishatangazwa zabuni na iko katika hatua za mwisho ili kuweza kusaini mikataba


Miradi hiyo ni ule wa barabara ya Ubena Zomozi – Ngerengere (Kizuka Army Camp) yenye urefu wa 11.6km, Mradi wa ujenzi wa barabara ya Ifakara – Kihansi – Mlimba – Taweta – Madeke, Sehemu ya Ifakara – Mbingu, km 62.5.


"Pia kuna Mradi wa ujenzi wa barabara ya Ifakara – Kihansi – Mlimba – Taweta – Madeke, Sehemu ya Mbingu – Chita JKT, yenye urefu wa Km 37.5.


Mradi mwingine alioutaja ni ule wa wa barabara ya Bigwa – Kisaki (sehemu ya Bigwa –Mvuha, km 78, Pamoja na Madaraja ya Ruvu na Mvuha.


"Mradi wa mwisho utakuwa ni wa ujenzi wa barabara ya Ifakara – Lupiro – Mahenge / Lupiro – Malinyi – Kilosa kwa Mpepo – Londo – Lumecha na Malinyi JCT – Malinyi, km 422.54.
Share:

MWONEKANO MPYA NGORONGORO WAVUTIA





•Uoto wa asili, ikolojia vyaanza kurudi kwa kasi katika maeneo yaliyohamwa na wakazi •Matumaini yazidi kuwa makubwa,

•Wadau watoa Ushauri

Baada ya baadhi ya wakazi wa maeneo ya Ngorongoro kuhamia Msomera Mkoani Tanga, Ikolojia na uoto wa asili vimenza kuejea kwa katika maeneo waliyobomoa makazi yao jambo linaloonyesha tija kubwa ya zoezi la Uhamaji Kwa hiyari

Wanahabari na wadau wa Kituo cha wanahabari watetezi wa Rasilimali na Taarifa (Mecira) Veronica Mheta na Dixon Busagaga walijionea mabadiliko makubwa tena ya muda mfupi walipotembelea kwenye baadhi ya zilipokuwa ambazo wamiliki wake waliamua kuhama Kwa hiyari kuhamia Msomera na kwengineko, maeneo hayo ni kwa aliyekuwa Mbunge wa Ngorongoro,Saning'o ole Telele na kwa Foible Lukumay wakazi wa kata ya Enduleni wilayani Ngorongoro na kwengineko katika eneo hilo .

"Kwa macho yangu nilijionea namna eneo hili lilivyokuwa limeathirika. Lakini Leo ninafurahi kuona ikolojia na uoto wa asili vimeanza kurejea kwa kasi kubwa sana" Amenukuliwa Mheta

"Nimeambiwa kuwa hapa pataota hata miti iliyokuweko awali na ikakatwa na wakazi waliokuwa wakiushi Ili kujenga Nyumba na maboma ya mifugo, Kwa kweli kuna tija kubwa sana kwenye zoezi la Uhamaji wa hiyari". Aliongeza Busagaga Miongoni mwa Sababu zilizopelekea wadau wa mazingira na watetezi wa haki za binaadamu kupaza sauti na kuitaka Serikali kutafuta utaratibu mpya wa kufanya Ngorongoro kuwa sehemu Salama kwa ajili ya Wanyama, Mifugo na binaadamu ni pamoja na;-

1.ONGEZEKO KUBWA LA WATU ambapo awali kulikuwa na Watu wasiozidi 8000 lakini sasa hivi wapo zaidi ya watu 120,000

2. ONGEZEKO KUBWA LA MIFUGO ambapo awali ilikuwa chini ya 50,000 lakini sasa hivi imevuka 1.1m

3. Miripuko ya magonjwa Kutokana na kuingiliana kulikopitiliza baina ya wanadamu, Wanyama na mifugo

4. Umasikini uliopitiliza ambapo ni asilimia 3 pekee ndio wanamiliki asilimia 80 ya mifugo yote 1.1m na hivyo kuwafanya wananchi *MANAMBA*

5. Kutokujua kusoma na kuandika ambapo zaidi ya asilimia 63 ya Wananchi wa Ngorongoro *HAWAJUI KUSOMA NA KUANDIKA*

6. Ongezeko kubwa sana la makazi(Nyumba) zisizoruhusiwa kisheria kujengwa hifadhini sambamba na ufungaji wa mitambo, umeme wa sola, nakadharika hivyo kuifanya Serikali kuchukua hatua ya kuruhusu zoezi la Uhamaji wa hiyari kutoka hifadhini humo kwenda Msomera kwa atakayependa na kokote kule atakayetaka mtu anayehama yeye pamoja na mali zake zote ikiwemo mifugo.
Share:

Saturday, 15 April 2023

Video : MBIO ZA BAISKELI NA JESHI LA JADI SUNGUSUNGU WAKITOA BURUDANI KAMPENI YA KATAA UHALIFU, TOA TAARIFA

 

Tazama Video Mbio za Baiskeli na Jeshi la Jadi Sungu wakitoa burudani kwenye Bonanza la Michezo lililoongozwa na Kampeni ya Kataa Uhalifu Toa Taarifa Shinyanga Bila Uhalifu Inawezekana’ katika kata ya Chibe Manispaa ya Shinyanga.

Tazama Mbio za Baiskeli

Tazama Burudani ya Jeshi la Jadi Sungusungu








Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger