Wednesday, 12 April 2023

DART KUPANDA MITI 1,000 KWENYE MIUNDOMBINU YAKE DAR ES SALAAM

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Hashim Komba, Mwenyekiti wa Bodi DART Dkt. Florens Turuka,Mkurugenzi wa DART, Dkt. Edwin Mhede pamoja na viongozi wa NMB wakiwa katika uzinduzi wa upandaji wa miti 1000 kwenye kituo cha mabasi ya mwendo kasi Ubungo. Uzinduzi huo umefanyika leo Aprili 12,2023

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Hashim Komba akipanda mche wa mti katika kando ya barabara ya mabasi yaendayo kasi wakati wa uzinduzi wa upandaji wa miti 1000 kwenye kituo cha mabasi ya mwendo kasi Ubungo. Uzinduzi huo umefanyika leo Aprili 12,2023



Mwenyekiti wa Bodi DART Dkt. Florens Turuka akipanda mche wa mti katika kando ya barabara ya mabasi yaendayo kasi wakati wa uzinduzi wa upandaji wa miti 1000 kwenye kituo cha mabasi ya mwendo kasi Ubungo. Uzinduzi huo umefanyika leo Aprili 12,2023
Mkurugenzi wa DART, Dkt. Edwin Mhede akipanda mche wa mti katika kando ya barabara ya mabasi yaendayo kasi wakati wa uzinduzi wa upandaji wa miti 1000 kwenye kituo cha mabasi ya mwendo kasi Ubungo. Uzinduzi huo umefanyika leo Aprili 12,2023
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Hashim Komba akizungumza wakati wa uzinduzi wa upandaji wa miti 1000 kwenye kituo cha mabasi ya mwendo kasi Ubungo. Uzinduzi huo umefanyika leo Aprili 12,2023
Mwenyekiti wa Bodi DART Dkt. Florens Turuka akizungumza wakati wa uzinduzi wa upandaji wa miti 1000 kwenye kituo cha mabasi ya mwendo kasi Ubungo. Uzinduzi huo umefanyika leo Aprili 12,2023.
Mkurugenzi wa DART, Dkt. Edwin Mhede akizungumza wakati wa uzinduzi wa upandaji wa miti 1000 kwenye kituo cha mabasi ya mwendo kasi Ubungo. Uzinduzi huo umefanyika leo Aprili 12,2023

************


WAKALA wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART), imepanga kupanda miti zaidi ya 1,000 kwenye kilomita 154 ambayo miundombinu ya mabasi yake inapita jijini hapa.


Hayo yalisemwa leo Aprili 12,2023 jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa DART, Dkt. Edwin Mhede, wakati wa uzinduzi wa upandaji wa miti hiyo kwenye kituo cha mabasi ya mwendo kasi Ubungo.


Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Hashim Komba na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Dar es Salaam wamiwemo wa benki ya NMB.


Dk. Mhede alisema kabla ya ujenzi wa miundombinu ya mwendokasi kulikuwa na uoto wa asili na miti ya aina mbalimbali hivyo DART inawajibika kuirejesha hali ilivyokuwa.


“Sisi tunapojenga barabara kwa kiasi kikubwa tunaharibu uoto wa asili na miti kwasababu kama kulikuwa na mti tunaukata na nyinyi mliokuwa Dar es Salaam wakati huo naamini mnakumbuka hali ilivyokuwa hapa Ubungo kabla ya ujenzi huu, ile hali haipo tena ndiyo sababu tunaona tunawajibika kuirejesha,” alisema Dk. Mhede


Alisema asilimia 45 ya wakazi wa Dar es Salaam wanatumia njia za kwenda kwa miguu (shoroba), ambazo kwa sasa hazina miti ambayo zamani iliwasaidia kupita kivulini hali ambayo alisema lazima irejelezwe.


“Nitoe wito kwa watumiaji wa hizi njia za kwenda kwa miguu waitunze hii miti kwasababu itakuwa msaada mkubwa kwao tumeanza kupanda miti leo lakini tutaendelea mpaka kufikia miti zaidi ya 1,000,” alisema


Naye Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Hashim Komba, alisema uzinduzi wa upandaji miti hiyo ni jambo kubwa na la kihistoria kwa wakazi wa Ubungo na jijini Dar es Salaam kwani itasaidia kwa kiwango kikubwa kurejeleza mazingira yaliyoharibiwa kutokana na shughuli mbalimbali za ujenzi.


“Mazingira ni uhai hivyo ukiyahifadhi mazingira na yenyewe yatakuhifadhi ukiyaharibu na yenyewe yatakuadhibu kwa hiyo natoa wito kwa wananchi wa Ubungo waunge mkono kampeni hii kwa kutunza miti itakayopandwa, kila mtu ambaye miti hii itapandwa mbele ya nyumba yake au eneo lake la biashara atawajibika kuitunza” alisema


Mkuu huyo wa Wilaya alisema alishatoa maelekezo kwa viongozi wa mitaa na kata kuitambua miti hiyo na kuitunza kwa hali na mali itakapopandwa na DART na wafanyabiashara ndogo ndogo wafanye biashara zao sehemu ambazo hazina miti.


“Wafanyabiashara ndogo ndogo lazima wajue umuhimu wa kutunza mazingira kwaajili yao na vizazi vijavyo na wakumbuke kwamba ukiyalinda mazingira na yenyewe yatakulinda kwa hiyo kila mmoja wetu awe mlinzi wa mazingira kwa kuhakikisha miti hii inastawi,” alisema


Aliwataka watanzania kuona fahari ya kupanda miti kwa kushiriki vyema kwenye kampeni ya upandaji miti kwa Mkoa mzima akisema kuwa hata yeye binafsi amekabidhiwa mti ambao ameupanda na kuuwekea alama kwaajili ya kuhakikisha anafuatilia ukuaji wake.


“Huu mti ambao nimeupanda leo nimeagiza wauwekee alama ili niwe naupitia mara kwa mara kuumwagilia na kuuwekea mbolea na mti huu utakapokuwa nitakuwa nimetoa mchango mkubwa kwa taifa katika kuhifadhi mazingira,” alisema


Alisema viongozi wa kitaifa, Rais Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais, Dk. Phillip Mpango na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, wamekuwa mstari wa mbele kuhamasisha upandaji wa miti kwaajili ya kuhifadhi mazingira hivyo wananchi wanapaswa kuiga mfano huo na kupanda miti.




Share:

WANNE WATUPWA JELA MIAKA 20 KWA KUKUTWA NA PEMBE ZA NDOVU


Watu wanne wamehukumiwa kifungo cha miaka 20 kwenda jela baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kukutwa na vipande tisa vya pembe za ndovu, kinyume cha sheria ya wanyama pori ya mwaka 2005 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2016 wakiwa katika hatua za mauzo ya nyara hizo za serikali.

Hukumu hiyo imetolewa katika mahakama ya hakimu mkazi Mkoa wa Shinyanga na hakimu mkazi Yusuph Zahoro, baada ya kupitia ushahidi wa pande zote mbili na kuwatia hatiani washitakiwa wote wanne waliokuwa wanakabiliwa na Kesi ya uhujumu uchumi namba 1 ya mwaka 2022.

Washitakiwa hao walikutwa na vipande 9 vya pembe za ndovu vyenye thamani ya milioni 69.21 ambapo washitakiwa walikamatwa wakiwa katika hatua za kuuza nyara hizo kata ya Solwa wilaya ya Shinyanga.

Waliohukumiwa kifungo cha miaka 20 jela ni Emanuel Shija Basu, Shija Kaswahili, Revocatus Mtara na Daud Ndizu ambao walitenda kosa hilo July 13 , 2022 baada ya kukutwa na nyara za serikali kinyume cha sheria.

Chanzo - EATV
Share:

Tuesday, 11 April 2023

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATANO APRILI 12,2023





























Share:

MAKABIDHIANO YA BOTI MBILI ZA DORIA TRA NA KAMPUNI YA AMIKAN VENTURES

Boti za doria ambazo zimekabidhiwa na kuzinduliwa katika kituo cha forodha cha TRA leo Aprili 11,2023 Jijini Dar es Salaam 
Kamishna Mkuu wa TRA, Bw.Alphayo Kidata akizungumza katika hafla ya makabidhiano na uzinduzi wa boti za doria na kampuni ya Amikan Ventures katika kituo cha forodha cha TRA leo Jijini Dar es Salaam Jijini Dares Salaam
Kamishna wa Forodha na Ushuru wa TRA Bw. Said Athumani akizungumza 
katika hafla ya makabidhiano na uzinduzi wa boti za doria na kampuni ya Amikan Ventures katika kituo cha forodha cha TRA leo Jijini Dar es Salaam Jijini Dares Salaam


*****************


NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

MAMLAKA ya mapato Tanzania (TRA) wamefanya makabidhiano ya boti za doria na kampuni ya Amikan Ventures katika kituo cha forodha cha TRA Jijini Dares Salaam ambapo boti mbili zimekabidhiwa na kuzinduliwa kwaajili ya kuanza kazi.

Akizungumza na Waandishi wa habari leo Aprili 11,2023 Jijini Dar es Salaam katika hafla hiyo, Kamishna Mkuu wa TRA, Bw.Alphayo Kidata amesema boti hizo zitafanya kazi ya doria katika pwani ya Tanzania na maziwa kupambana na vitendo vya magendo ambavyo vinahatarisha mipango ya TRA katika kukusanya mapato ya nchi.

Amesema waingizaji wa bidhaa bandia na bidhaa za magendo wamekuwa wakitumia mwanya wa urefu wa mpaka wa pwani ya bahari ya hindi kwa kuingiza bidhaa bandia ikijumuisha dawa, vyakula, mavazi, viatu, vifaa vya elektroniki, na vinywaji vyenye pombe.

"Uingizaji wa bidhaa kama hizi zinaathiri vibaya uchumi wa nchi kupitia kukosa mapato, kukwamisha ukuaji wa viwanda vya ndani na biashara halali, na kuathiri afya na usalama wa watumiaji". Amesema Bw.Kidata.

Aidha amesema gharama za ununuzi ya boti hizo zilipitishwa wakati wa bajeti ya mwaka wa fedha 2021/22 ambapo Serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania ilitenga bajeti ya Tsh 2.5 Billioni kwa ajili ya ununuzi wa boti mpya za doria. Hivyo basi boti hizo mbili ambazo wamekabidhi wameona wazipeleke zikafanye kazi za doria kwa mikoa ya Dar es salaam na Kigoma ambapo kuna matukio mengi ya magendo.

Kwa upande wake Kamishna wa Forodha na Ushuru wa TRA Bw. Said Athumani amesema boti hizo ambazo zimekabidhiwa ni sehemu ya bajeti ya Tsh. Billioni 2.5 iliyotengwa katika mwaka wa Fedha 2021/2022.

Amesema Mchakato wa Manunuzi katika bajeti hiyo umehusisha boti tatu za wazi na moia va kufungwa, ambapo Kampuni ya Amikan Ventures Limited ilishinda kandarasi ya kutengeneza boti tatu za wazi kwa thamani ya Tshs 1,589, 109,302.82 yaani kila boti thamani yake ni Tsh. 529,703, 100.94.

"Kamishna Mkuu, leo tutakuomba upokee na kuzindua boti 2 badala ya boti 3 kwani boti moja ilianguka wakati wa kushusha bandarini na kupata hitilafu kubwa. Mkandarasi ametakiwa kuleta boti nyingine mpya kwa gharama zake. Amepewa muda wa miezi 8 kuanzia mwezi wa Machi 2023 awe amekabidhi boti hiyo". Amesema Bw.Athumani.

Share:

PATA ODDS KUBWA UCL LEO



Jisajili Meridianbet leo upate mizunguko 50 ya bure kucheza moja ya mchezo uupendao ya kasino ya mtandaoni kuna Aviator, Poker, Titan Roulette na mingine mingi. Kujisajili bonyeza hapa https://a.meridianbet.co.tz/c/NpUbSL

 

 

Zilianza timu 32, zikafika 16, na hatimaye zimebaki 8 tu hatua ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa, unatabiri timu zipi zitafuzu hatua ya Nusu fainali? Meridianbet inakuhakikishia unapata Odds kubwa na machaguo Zaidi ya 1000+ Tembelea www.meridianbet.co.tz kubashiri soka na kucheza kasino ya mtandaoni.

 

Odds kubwa za Jumanne ya Mabingwa

 

Ni vita vya mbinu kati ya Mwanamitindo na Bisho wa Kikatalunya Pep Guardiola akiliongoza jeshi lake la Man City, huku Luteni Jenerali Erling Haaland atasaidiana na Kapteni Kelvin De Bruyne kusaka ushindi dhidi ya Jeshi la Thomas Tuchel aliyekimbilia mafichoni Bayern Munich kwenye jiji la Munich nchini Ujerumani, huko kuna kijana mdogo tisho sana Kingsley Coman ni hatari wanapaswa kumchunga Zaidi. bashiri mubashara kupitia duka la ubashiri la Meridianbet.

 

Meridianbet wakali wa odds kubwa na kasino ya mtandaoni yenye michezo pendwa ya sloti kama Aviator, Poker na Roulette wameongeza machaguo Zaidi 1000+ kwenye mechi hizi za Ligi ya Mabingwa. Bonyeza hapa kuona machaguo Zaidi na mchanganuo wa odds kubwa bashiri mubashara.

 

Ni mechi ya kwanza ya robo fainali UCL Lisbon itachafuka kwa shangwe au giza litatanda kwa kipigo? ni Benfica vs Inter Milan miamba kutoka Jiji na Milan Italia. Odds za ushindi ni 2.25 vs 3.33 Meridianbet CHAGUA TUKUPE iwe odds kubwa watakupa, Kasino ya mtandaoni, kubashiri mubashara unaweza, michezo ya sloti kama Aviator, poker na Roulette yote unaipata kubwa Zaidi ukiona jamvi lako linataka kuchanika unaweza kucash out/Kuturbo.

 

Jumatano ya Mabingwa

 

Dimba la Giusepee Meazza litawaka moto ni vita ya wanaume 22, chini ya viongozi 2 ni Pioli Stefano na Spalletti Luciano. Ni AC Milan vs Napoli kila mmoja anataka kusonga mbele hatua ya nusu fainali utamu wa mechi hii imenogeshwa na odds kubwa za Meridianbet 2.74 vs 2.65 huku sare ina 3.14

 

Big Match Big day! katika dimba la Santiago Bernabeu ni Real Madrid vs Chelsea mara nyingi Chelsea huwa anafufukia kwenye timu kubwa lakini mabingwa hawa watetezi na mara nyingi Zaidi wa UCL linapokuja suala la Ligi ya Mabingwa huwa hawana jambo dogo, Mechi hii unaipa matokeo gani.  Kama sio mpenzi wa kubashiri soka, Chagua tukupe michezo ya kasino ya mtandaoni yenye sloti pendwa kama Aviator, Poker na Roulette. Bashiri na Meridianbet.

 

NB: Meridianbet imekuja na Jackpoti kubwa ya mechi 13 kwa dau dogo la kuanzia 1,000/=TZS mshindi atajinyakulia donge nono la Tsh 85,000,000/= PIGA *149*10#

 

#MERIDIANBET CHAGUA TUKUPE



Share:

DC SAME ATANGAZA KIAMA NA MAJANGILI AWAFANANISHA NA WAUJUMU UCHUMI

 


MKUU wa wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Kasilda Mgeni akizungumza na waandishi wa Habari baada ya kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi lengo likiwa ni kuhamasisha utalii wa ndani
MKUU wa wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Kasilda Mgeni  kushoto akizungumza na Afisa Utalii wa Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi Happiness Kiemi wakati alipofika kwenye hifadhi hiyo kuitembelea ikiwa ni  kuhamasisha utalii wa ndani
Afisa Utalii wa Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi Happiness Kiemi akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu maboresho makubwa yaliyofanywa kwenye Hifadhi hiyo na Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu 



Afisa Utalii wa Hifadhi wa Taifa ya Mkomazi Happiness Kiemi  kulia akimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Same Kasilda Mgeni wakati wa ziara yake kwenye hifadhi hiyo
Mkuu wa wilaya ya Same Kasilda Mgeni katika akiwa ni Meneja wa Benki ya CRDB wilaya ya Same kulia  
Watalii wakifurahia utalii katika Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi wilayani Same Mkoani Kilimanjaro
Faru katika Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi
Faru katika Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi
Faru katika Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi
Tembo akiwa na mtoto wake katika Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi


Twiga akiwa katika Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi





Na Oscar Assenga aliyekuwa KILIMANJARO

MKUU wa wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Kasilda Mgeni ametangaza vita mpya baada ya kuwatahadharisha majangaili ambao wanafikiria kupitia ujangili wanaweza wakanufaika kuachana na biashara hizo kutokana na kwamba wao wamejipanga kuhakikisha wanawashughulikia vilivyo.

Vita hiyo aliitangaza mwishoni mwa wiki wakati alipotembelea Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi ikiwa ni kuhamasisha utalii wa ndani ambapo alisema watahakikisha wanashughuliwa ili kuhakikisha hawagusi hifadhi ikiwemo kuwataka wajiandae kutafuta kazi nyengine .

Mkuu huyo wa wilaya alisema kwamba kama walifikiria hiyo ndio ajira yao wajiandae kutafuta kazi nyengine kwa sababu yenye ni mhifadhi na anafahamu umuhimu wa hifadhi na ndio Mwenyekiti wa Kamati ya usalama wa wilaya hiyo.

“Hifadhi nyingi zimekuwa zikikabiliwa na vitendo vya ujangili hivyo sisi kama Kamati ya Ulinzi na Usalama wa wilaya tumejipanga kuhakikisha tunashirikiana na hifadhi kutokomeza ujangili mikakati hiyo ni pamoja na tunapokuwa kwenye mikutano yao ya vijiji vinavyozunguka hifadhi hiyo miongoi mwa mambo tunaowaeleza ni umuhimu wa hifadhi na athari za kuwa na ujangili”Alisema

Mkuu huyo wa wilaya wanapokuwa kwenye ziara katika vijiji hivyo wanawaelimisha wananchi umuhimu wa hifadhi na kuwaonya waache kufanya biashara za ujangili kwa sababu wanapoendelea kuifanya serikali kupitia vyombo vyake itaendelea kuchukua hatua kali za kisheria.

“Kwa sababu wanakuwa kama wahujumu uchumi kutokana na kwamba hifadhi hizo zinafanya uchumi wa nchi unaweza kuimarisha hivyo kunapokuwa na majangili wanaoua wanyama ambao watalii wanakuja kuangalia hiyo ni hujuma hivyo serikali ya wilaya tumejipanga vizuri kushirikiana na hifadhi kuhakikisha havijitokezi”Alisema Mkuu huyo wa wilaya

Alisema kwamba Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi ndio Hifadhi muhimu kwa Kanda ya kaskasini na kuna wanyama wengi wanaopatikana kwenye hifadhi nyengine nchini lakini ukifika eneo hilo una uhakika kuweza kumuona mnyama Faru kiurahisi sana na imesaidia wilaya ya sama kuwa na watalii wengi wanaokwenda kumuona mnyama huyo.

Hata hivyo alisema kwamba wanamshukuru Rais Dkt Samia Suluhu amefanya mambo makubwa sana kupitia Royal Tour imewasaidia sana hifadhi kutokana na kwamba baada ya ziara hiyo wataalii wanaoingia kwa mwaka kwenye hifadhi hiyo kwa sasa ni zaidi ya 7000 hiyo ni faida kubwa walioipata kupitia ubunifu huo.

Mkuu huyo wa wilaya alisema kwamba Rais Dkt Samia Suluhu kupitia Fedha za Tozo na Fedha za Covid ameweza kuimarisha miundombinu ya hifadhi nchini ambapo miongoni mwa hifadhi ambazo zimenufaika ni mkomazi ambapo kuna majengo ya utawala na barabara nzuri ambao zinahamasisha watalii hivyo Rais amekuwa mfano nzuri wa uhifadhi nchini.

Aidha pia alisema wanapokuwa na hifadhi inayofikika kirahisi wanapata watalii wengi ambazo wanasaidia kukuza uchumi wa nchi yetu

Hata hivyo aliwahimiza watanzania kutembelea hifadhi za hapa nchini ili kuweza kujionea vivutio mbalimbali vya utalii ikiwemo kuwataka pia wananchi wa wilaya ya Same watumie wikiendi zao kuweza kufika mkomazi kuweza kuona vivutio vilivyopo na hivyo kusaidia serikali kuingiza mapato ambayo yatasaidia maendeleo kwenye wilaya yao.

Awali akizungumza wakati wa ziara hiyo, Afisa Utalii wa Hifadhi wa Taifa ya Mkomazi Happiness Kiemi alimshukuru Rais Dkt Samia Suluhu kutokana na kupelekea fedha za Uviko ambapo waliweza kuzitumia kujenga lango maalumu ambalo ni la kuingilia wageni wanaofika kutembelea hifadhi hiyo na kuweza kupata huduma nzuri za utalii.

Alisema kwamba kupitia fedha hizo wameweza kujenga barabara nzuri yenye utefiu wa zaidia ya kilomita 140 na pia kutengeneza viwanja vya ndege na hiyo imetoa fursa kwa wageni ambao hawana muda wa kutembea kwenye magari kwa muda mrefu wakati wa safari zao kutoka maeneo mbalimbali kwenda kuitembelea hifadhi hiyo

Happiness alisema kwa kujengwa uwanja huo kumesaidia wageni kusafiri kutumia ndege kufika hifadhi ya Taifa ya Mkomazi moja kwa moja kutoka kwenye viwanja vyengine
Share:

Monday, 10 April 2023

SIMBA SC YAENDELEZA UBABE WA YANGA KWA IHEFU


Na Alex Sonna

SIMBA SC wameendelea kuitafuta Yanga SC katika mbio za Ubingwa baada ya kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji Ihefu mchezo wa Ligi Kuu ya NBC katika uwanja wa Highland Estates jijini Mbeya .

Mabao ya Simba yamefungwa na Mshambuliaji hatari Jean Baleke dakika ya 83 na 87 na kuvunja mwiko wa Ihefu wa kuendelea kuzifunga timu kubwa katika uwanja wao ambapo Yanga na Azam zote zilipata kichapo huku Singida Big stars ikiambulia sare.

Kwa Matokeo hayo Simba SC imefikisha Pointi 60 ikiwa imecheza mechi 25 huku Yanga SC bado anaongoza Ligi akiwa na Pointi 65 akiwa amecheza mechi 24.

Ligi hiyo itaendelea kesho kwa mechi moja Mabingwa Watetezi wa Kombe hilo Yanga SC itakuwa kibaruani kucheza na Kagera Sugar kutoka Mkoani Kagera mchezo utakaopigwa uwanja wa Chamazi Complex Azam majira ya saa moja usiku.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger