Thursday, 6 April 2023

Picha : MATUKIO YANAYOENDELEA MSIBA WA MFANYABIASHARA MAARUFU MUSOMA FOOD..MAZISHI YANAFANYIKA LEO KAMBARAGE

Maelfu ya waombolezaji wamejitokeza kuaga mwili wa Mfanyabiashara wa nafaka mkoa wa Shinyanga Said Makilagi maarufu Musoma Food aliyefariki dunia ghafla jijini Mwanza Jumatatu Aprili 3,2023 akiwa Hotelini.

Mazishi ya marehemu Said Kate Makilagi yanafanyika leo Alhamisi Aprili 6,2023 nyumbani kwake Kambarage Mjini Shinyanga.

Tazama Picha matukio yanayoendelea muda huu...Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Share:

BENKI YA CRDB YAFUTURISHA WATEJA NA WADAU NA KUTOA CHAKULA KWA WATOTO YATIMA TABORA….RC BATILDA APONGEZA HUDUMA YA AL BARAKAH BANKING

Kaimu Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Ndg. Jumanne Wambura Wagana akizungumza wakati Benki ya CRDB ikiwafuturisha Wateja na Wadau wa Benki ya CRDB Mkoa wa Tabora

Na Mwandishi Wetu – Malunde 1 blog Tabora

Benki ya CRDB imewafuturisha Wateja na Wadau wa Benki ya CRDB Mkoa wa Tabora ikiwa ni mwendelezo wa utamaduni wa Benki hiyo kuungana na Waumini wa Dini ya Kiislamu wanaoishiriki Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.


Hafla ya Futari iliyoandaliwa na Benki ya CRDB imefanyika Jumatano Aprili 5,2023 katika Hoteli Ya Ristalemi na kuhudhuriwa na viongozi wa dini, Viongozi wa Serikali, Taasisi za Umma na Binafsi, Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa,Viongozi na Wafanyakazi kutoka Benki ya CRDB, Watoto yatima na wateja na wadau wa Benki ya CRDB ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Buriani.

Akizungumza wakati wa Futari hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Buriani ameipongeza Menejimenti ya Benki ya CRDB kwa kuanzisha na kuendeleza utaratibu huo wa kufutari na wateja, wadau na wenye uhitaji katika jamii katika kipindi cha mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

“Nimefurahishwa na jambo mlilolifanya leo la kutoa msaada wa fulana na kofia kwa Watoto wenye uhitaji maalum katika Shule ya Furaha, hakika lile ni jambo la kuigwa. Nimekuwa nikiwafuatilia kwa muda na kuona namna gani ambavyo mmekua mkitekeleza jambo hili na niliona mwaka huu mlianza jambo hili kwa kufuturu na wateja wa Dar es Salaam mkiongozwa na Sheikh Dkt. Abubakar Zubeir Bin Ally, Sheikh Mkuu na Mufti wa Tanzania. Hongereni sana”, amesema Dkt. Batilda.


“Ushiriki wenu katika kuandaa futari hizi katika mwezi Ramadhani inaonesha ni kwa jinsi gani Benki ya CRDB inatambua kuwa pamoja na kufanya biashara lakini ni sehemu ya jamii na inapaswa kushiriki katika masuala mbalimbali ya kijamii. Hakika hili ni jambo jema linalopaswa kuigwa na taasisi nyingine ambazo ni sehemu ya jamii yetu”,amesema.


Aidha pamoja na mazuri hayo ambayo Benki ya CRDB wamefanya kwa kushiriki na wateja na wadau wao katika futari, Mkuu huyo wa mkoa ameeleza kufurahishwa na uamuzi wa Benki hiyo kuanzisha huduma makhususi za Al Barakah Banking ambazo zinafuata misingi ya dini ya Kiislamu.


“Hakika hii inadhihirisha kuwa CRDB ni Benki inayomsikiliza Mteja kwani mmeweza kutambua mahitaji ya kundi lenye uhitaji wa huduma zinazofata misingi ya dini ya Kiislamu na kuweza kubuni huduma zinazoendana na mahitaji yao.Mafanikio ya huduma ya Al Barakah yatanufaisha sio tu Benki ya CRDB kwani kwa kuanzisha huduma hii mmeweza kuwajumuisha watu ambao mwanzo wasingeweza kujumuishwa katika huduma rasmi za kibenki kwa kuwa huduma zilizokuwepo zilikua haziendani na misingi ya imani yao”,amesema Dkt. Batilda.


“Hivyo kwa kuwajumuisha watu hawa mana yake mmeongeza wigo wenu wa kupokea amana na kwa sababu hiyo mtaweza kutoa mikopo zaidi kwa wafanyabiashara nchini na hivyo kutoa ajira zaidi, kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa pamoja na uwekezaji kwa ujumla wake.

Hivyo kama Mkuu wa Mkoa, nafurahishwa na jambo hili kwani kwa namna moja au nyingine mmtakuwa na mchango katika kutimiza majukumu yangu ya kumsaidia Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuleta mapinduzi ya kiuchumi kwa kuyafikia makundi yote yaliyopo katika jamii”, ameongeza Mkuu huyo wa Mkoa wa Tabora.

Akitoa salamu za benki ya CRDB, Kaimu Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Ndg. Jumanne Wambura Wagana amesema benki hiyo imekuwa na utaratibu huo kila mwaka wakati wa Ramadhan kushiriki Futari na wateja wake na kutoa Sadaka ya vyakula kwa watoto yatima.


Wagana amesema mwaka 2021 benki ya CRDB ilianzisha dirisha la huduma za kibenki ambazo zimefuata misingi ya dini ya kiislamu maarufu kama Al Barakah Banking ambapo mpaka mwaka 2022 benki hiyo imeweza kupata wateja zaidi ya 30,000 na kutoa mikopo isiyo na riba kwa wateja wake kwa kiasi zaidi ya Shilingi Bilioni 73.


Amesema kwa Kanda ya Magharibi yaani Shinyanga, Geita, Kigoma na Tabora amesema mkoa wa Tabora umepokea huduma hiyo mpya ya Al Barakah kwa kasi zaidi hivyo kuwaomba watanzania ambao hawajajiunga wachangamkie fursa kwani ukiweka amana kwa akaunti ya Al Barakah haitengenezi riba na pia ukipewa mkopo hauna riba.

Wagana amewapa uhakika wa huduma wateja wote ambapo amesema benki hiyo kinara nchini yenye kauli mbiu ya benki inayomsikiliza mteja kwa sasa imeendelea kuzifanya huduma zake zipatikane kidigitali zaidi ikiwemo kupitia Mawakala, ATM, Simbanking, Vituo vya malipo n.k huku ikiendelea kupanua mtandao wake nje ya Tanzania ambapo kwa sasa CRDB inafanya vizuri nchini Burundi kama benki namba 2 na hivi karibuni wanatarajia kuanza kutoa huduma nchini Congo.


Mkurugenzi wa NBS na MNEC Tabora Mhe. Mohamed Nasson naye ameguswa na kitendo cha CRDB kutoa sadaka ya vyakula kwa watoto yatima akatoa Tsh 250,000/= huku mkuu wa Mkoa Dkt. Batilda Buriani naye akiguswa na kuongezea Tsh 250,000/= na kufanya iwe 500,000/= ambapo fedha hizo zitakabidhiwa kwa viongozi wa kituo cha kulelea watoto yatima ili wanunue mahitaji kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Buriani akizungumza wakati Benki ya CRDB ikiwafuturisha Wateja na Wadau wa Benki ya CRDB Mkoa wa Tabora
Kaimu Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Ndg. Jumanne Wambura Wagana akizungumza wakati Benki ya CRDB ikiwafuturisha Wateja na Wadau wa Benki ya CRDB Mkoa wa Tabora
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI APRILI 6,2023

 







             

        




Share:

Wednesday, 5 April 2023

ONGEZA USHINDI X1000 YA DAU LAKO KUPITIA VENI VIDI VICI




 Aprili ya Kishua unaambiwaje jisajili Meridianbet upate mizunguko 50 ya bure kucheza sloti ya kasino ya mtandaoni. Kujisajili bonyeza hapa: https://a.meridianbet.co.tz/c/GLd6O8

 

Furahia sloti mpya kutoka Kasino ya Mtandaoni ikielezea Roma ya Kale! Cheza kipekee katika sloti ya Meridianbet Veni Vidi Vici!

 

Mambo ya kale yafuza na kushangaza pia, bila shaka ulishawahi kuisoma historia ya Warumi/Roman kuna mwamba mmoja anaitwa Julius Caesar alikua ni moja ya viongozi wenye nguvu kubwa sana kisiasa na kijeshi. Ili kukurudisha nyuma huku ukipiga hela Meridianbet pamoja na Expanse Studios inakuletea sloti yenye kuelezea mambo ya Roman Empire ni Vedi Vidi Vici.

Ushawishi wa hadithi za Kirumi pia unatambuliwa kwa jina la sloti, lakini mcehzo huu una kitu gani kipya?

Sloti ya Veni Vidi Vici ina Kolamu ambayo inakupa taji la mvinyo, ngao na upanga, mikokoteni, askari wachache, wakati alama ya msingi ya mchezo ni Caesar mwenyewe.

Kadi mbili za porini (Wild) zinakuongoza kwenye mzunguko wa bonasi kutoka Kasino ya mtandaoni ya Meridianbet, wakati kadi tatu au zaidi za porini (Wild) zinaamsha Bonasi ya Sloti ya Veni Vidi Vidi.

 

Kuna msemo mmoja mkubwa wa Gaius Julius Caesar husema ’kete imetupwa’ na katika kasino ya mtandaoni mchezo wa Veni Vidi Vici, Caesar huzungusha kete! Aina hii ya bonasi inakuja katika ngazi tatu, na ya tatu inaweza kukuletea ushindi mpaka mara 1,000 zaidi!

Sloti hii ina bonasi ya ubashiri ambayo inaweza kuongeza kila ushindi mara mbili, pamoja na jackpots tatu zinazoendelea: Mini, Midi na Mega.

 

Sifa kuu ya sloti hii ni chaguo la BONUS NUNUA (Bonus Buy option), ambalo unaweza kuwezesha Bonasi ya Veni Vidi Vici, na RTP nzuri ya 96.28%!

Dhibiti Ufalme/ Kasri ya Roma na upate mafanikio makubwa!


Share:

NEMC YAKIPA SIKU SABA KIWANDA BUBU KUJIBU TUHUMA ZA TAKA HATARISHI

Mmoja wa Maafisa kutoka NEMC akikagua baadhi ya taka za hospitalini zikiwa zimekusanywa katika kiwanda bubu cha kukusanya na kusaga chupa za plastiki eneo la Kisarawe II wilayani Kigamboni leo Aprili 5,2023 Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Maafisa kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) wakitazama baadhi ya taka za hospitalini zikiwa zimekusanywa katika kiwanda bubu cha kukusanya na kusaga chupa za plastiki eneo la Kisarawe II wilayani Kigamboni leo Aprili 5,2023 Jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa Maafisa kutoka NEMC akikagua baadhi ya taka za hospitalini zikiwa zimekusanywa katika kiwanda bubu cha kukusanya na kusaga chupa za plastiki eneo la Kisarawe II wilayani Kigamboni leo Aprili 5,2023 Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya taka za hospitalini ambazo zimekutwa katika kiwanda bubu cha kukusanya na kusaga chupa za plastiki eneo la Kisarawe II wilayani Kigamboni leo Aprili 5,2023 Jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi wa Uzingatiaji na Utekelezaji wa Sheria NEMC, Bw.Thobias Mwesiga akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufanya ukaguzi kwenye kiwanda bubu cha kukusanya na kusaga chupa za plastiki katika eneo la Kisarawe II wilayani Kigamboni leo Aprili 5,2023 Jijini Dar es Salaam.
Meneja wa NEMC Kanda ya Mashariki Kusini Bw.Hamadi Taimuru akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufanya ukaguzi kwenye kiwanda bubu cha kukusanya na kusaga chupa za plastiki katika eneo la Kisarawe II wilayani Kigamboni leo Aprili 5,2023 Jijini Dar es Salaam.


**********************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

BARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limempatia siku saba (7) mmiliki wa kiwanda bubu cha kukusanya na kusaga chupa za plastiki katika eneo la Kisarawe II wilayani Kigamboni kufika katika ofisi za NEMC kujibu tuhuma za kukutwa na taka hatarishi za hospitali katika eneo lake la kiwanda.

Agizo hilo limetolewa leo Aprili 5,2023 Jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi wa Uzingatiaji na Utekelezaji wa Sheria NEMC, Bw.Thobias Mwesiga mara baada ya kufanya ukaguzi wa kimazingira na kutembelea na kushuhudia shughuli mbalimbali zinafanyikakwenye kiwanda hicho kinyume na sheria.

Amesema kwa kuwa wamebaini pia kiwanda hicho hakina vibali muhusika huyo atachukuliwa hatua za kisheria kwa kutozwa faini kwa kukiuka taratibu na ataelekezwa utaratibu wa kwenda kusajili kiwanda chake ambacho kinapaswa kusajiliwa kwa mujibu wa sheria.

"Faini itakayotozwa kwa mwenye kiwanda haitakuwa pungufu ya Milioni 5, na faini hiyo ni ya fedha ambayo anailipa kwa serikali". Amesema Bw. Mwesiga.

Aidha NEMC imetoa rai kwa hospitali zote nchini kufuata utaratibu wa namna ya kuteketeza taka zinazotokana na shughuli zao za mahospitalini.

"Sheria za Mazingira na kanuni zake inazitaka hospitali zote nchini kuwa na mfumo na utaratibu mzuri ndani ya hizo hospitali kuteketeza taka zao wenyewe, kuwa na vifaa ambavyo zile taka zinazozalishwa katika hospitali hazitaweza kurudi kwenye mazingira". Amesema

Kwa upande wake Meneja wa NEMC Kanda ya Mashariki Kusini Bw.Hamadi Taimuru amesema watampa maelekezo kwenye kiwanda pindi atakapofika kwenye ofisi za NEMC ndani ya siku saba, na kuanzia sasa wamesimamisha rasmi shughuli zote ambazo zimekuwa zikifanywa kwenye kiwanda hicho mpaka taratibu zote zitakapofuatwa.

"Hii haiwezi kukubarika kwaani hata hawa wanaofanya kazi kwenye kiwanda hiki wanafanya kazi pasipokuwa na vifaa maalumu hivvyo wanaweza kupata na wao madhara kwenye taka hizo za hospitali, madhara kwasasa ni mengi". Amesema Bw.Taimuru.

Pamoja na hayo amesema watahakikisha wanatembelea katika hospitali kuona takataka zao wanazihifadhi na kuzipeleka wapi na kuonesha uthibitisho unaoonesha sehemu ambayo wanazipeleka takataka hizo.


Nae Mmiliki wa Kiwanda hicho, Bw. Salumu Madongo amekiri kuwa kiwanda chake hakina kibali kutoka NEMC lakini vibali vya kiwanda anavyo hivyo basi atafika katika ofisi za NEMC ili aweze kupewa utaratibu na kuweza kupata kibali cha Mazingira.

Kuhusu taka za hospitali kukutwa katika kiwanda chake amesema ni kutokana na wale ambao wanakusanya chupa za plastiki na kuzipeleka pale ndo walikuja na taka hizo zikiwa ndani ya mfuko wa kubebea chupa za plastiki
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger