Wednesday, 11 January 2023
MAKAMANDA WA POLISI WATANGAZA KIAMA KWA WEZI WA MAFUTA, VIFAA VYA UJENZI RELI YA KISASA 'SGR'
ASKARI POLISI AKUTWA AMEFARIKI KWENYE NYUMBA YA KULALA WAGENI ARUSHA NDUGU WAKIMUUA KIJANA ALIYETUKANA MAMA YAKE MZAZI
Na mwandishi wetu Jeshi la Polisi
Jesh la Polisi mkoa wa Arusha limesema kuwa tarehe 08 Januari mwaka huu Jeshi hilo lilipokea taarifa ya matukio ya watu wawili kufariki dunia katika maeneo tofauti tofauti katika Mkoa wa Arusha.
Akitoa taarifa hiyo leo Januari 11 kamanda wa Palisi Mkoa wa Arusha kamishina Msadizi wa Polisi ACP JUSTINE MASEJO amesema kuwa Tarehe 08.01.2023 muda wa saa 08:30 usiku Jeshi la Polisi Mkoani hapa lilipokea taarifa ya uwepo wa mtu mmoja ambaye alifariki maeneo ya nyumba ya kulala wageni ijulikanayo kwa jina la Mrina Shine iliyopo kata ya Levolosi Jijijini Arusha.
Kamanda Masejo amebainisha kuwa mara baada ya kupokea taarifa hiyo, Polisi walifika eneo hilo na kuukuta mwili huo ambao waliutambua kuwa ni Mkaguzi wa Polisi Stewart Kaino (47) Askari Polisi wa wilaya ya Arumeru.
Aidha amesema kuwa jeshi hilo bado linaendelea na uchunguzi wa kina ili kubaini mazingira mazima ya kifo hicho.
Sambamba na hilo Kamanda Masejo ameelezea tukio jingine ambapo amesema kuwa Tarehe 08.01.2023 huko katika Hospitali ya Rufaa ya Mount Meru Arusha mtu mmoja aitwaye Nelson Mollel (33) mfanyabiashara, mkazi wa kata ya Moivo, Wilaya ya Arumeru na Mkoa wa Arusha alifariki dunia wakati akiendelea kupatiwa matibabu baada ya kujeruhiwa kwa kupigwa.
ACP MASEJO amebainisha kuwa Uchunguzi wa awali wa Jeshi hilo umebaini kuwa mtu huyo alifariki dunia baada ya kujeruhiwa kwa kupigwa na watu wanaodaiwa kuwa ni ndugu zake tarehe 03.01.2023 wakimtuhumu kumtukana mama yake mzazi (jina limehifadhiwa) na kumuibia.
Kamanda Masejo aliendelea kufafanua kuwa baada ya kupigwa, ndugu hao waliendelea kukaa na majeruhi bila kumpeleka hospitali hadi ilipofika tarehe 08.01.2023 alifikishwa hospitali akiwa mahututi na kufariki dunia wakati akiendelea kupatiwa matibabu.
Amesema kuwa Jeshi hilo linaendelea na upelelezi ili kuwakamata watu wote waliohusika katika tukio hilo ambao walikimbia baada ya kuona hali ya marehemu kuwa mbaya.
DKT MABULA ATAKA WANA CCM KUTUMIA FURSA YA MIKUTANO YA HADHARA KUJIBU HOJA
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi ambaye ni Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akivishwa Scarf mara baada ya kuwasili ofisi ya CCM mkoa wa Mwanza ilipofanyika sherehe ya kuwakaribisha wajumbe wa NEC Taifa tarehe 11 Januri 2023.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi ambaye ni Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza na wanachama wa CCM waliojitokeza katika sherehe za kuwakaribisha wajumbe wa NEC Taifa tarehe 11 Januari 2023 mkoani Mwanza.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa Bi. Ellen Makungu Bogoje akizungumza kwenye sherehe za kuwakaribisha Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa zilizofanyika ofisi ya CCM mkoa wa Mwanza tarehe 11 Januari 2023.
Baadhi ya wana CCM waliojitokeza katika sherehe za kuwakaribisha wajumbe wa NEC Taifa ambao ni Dkt Angeline Mabula na Ellen Makungu Bogoje tarehe 11 Januari 2023.
Vijana wa hamasa wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Mwanza wakifurahia wakati wa sherehe za kuwapokea wajumbe wa halmashauri Kuu ya CCM Taifa zilizofanyika ofisi ya CCM mkoa wa Mwanza tarehe 11 Januari 2023.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza Adam Malima akizungumza katika sherehe za kuwapokea wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa CCM zilizofanyika ofisi ya CCM mkoa wa Mwanza tarehe 11 Januari 2023.MWONGOZO WA KUDHIBITI VVU, UKIMWI NA MAGONJWA YASIOMBULIZWA WAHUISHWA KULINDA AFYA ZA WATUMISHI




Mkurugenzi Msaidizi Anuai za Jamii na Mratibu wa VVU, UKIMWI na Magonjwa Yasiyoambukiza, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Mwanaamani Mtoo akiwasilisha mada kuhusu Umuhimu wa Ujumuishwaji wa Anuai za Jamii mahali pa kazi wakati wa kikao kazi cha kujadili Mwongozo wa Kudhibiti VVU, UKIMWI na Magonjwa Yasiyoambukiza kilichofanyika jijini Dodoma.Tuesday, 10 January 2023
NAIBU WAZIRI KASEKENYA AKAGUA MRADI WA UJENZI WA NYUMBA ZA WATUMISHI MAGOMENI
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi. Godfrey Kasekenya (kulia mwenye miwani) akiwa pamoja na watumishi wa Wakala wa majengo (TBA) akikagua mradi wa ujenzi wa nyumba za watumishi ' Magomeni Kota Phase 2 A' uliokamilika kwa asilimia 96 leo Januari 10,2023 Jijini Dar es Salaam.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA,) Arch. Daud Kondoro (kulia)akimueleza jambo Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi. Godfrey Kasekenya mara baada ya kutembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa nyumba za watumishi ' Magomeni Kota Phase 2 A' uliokamilika kwa asilimia 96 leo Januari 10,2023 Jijini Dar es Salaam.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA,) Arch. Daud Kondoro (kushoto) akimueleza jambo Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi. Godfrey Kasekenya mara baada ya kutembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa nyumba za watumishi ' Magomeni Kota Phase 2 A' uliokamilika kwa asilimia 96 leo Januari 10,2023 Jijini Dar es Salaam.
Kaimu Meneja wa Wakala wa Majengo (TBA) Mkoa wa Dar es Salaam, Arch.Bernard Mayemba akimueleza jambo Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi. Godfrey Kasekenya mara baada ya kutembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa nyumba za watumishi ' Magomeni Kota Phase 2 A' uliokamilika kwa asilimia 96 leo Januari 10,2023 Jijini Dar es Salaam.
Kaimu Meneja wa Wakala wa Majengo (TBA) Mkoa wa Dar es Salaam, Arch.Bernard Mayemba akimueleza jambo Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi. Godfrey Kasekenya mara baada ya kutembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa nyumba za watumishi ' Magomeni Kota Phase 2 A' uliokamilika kwa asilimia 96 leo Januari 10,2023 Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi. Godfrey Kasekenya akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 10,2023 Jijini Dar es Salaam mara baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa nyumba za watumishi ' Magomeni Kota Phase 2 A' uliokamilika kwa asilimia 96.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA,) Arch. Daud Kondoro akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 10,2023 Jijini Dar es Salaam mara baada ya Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi. Godfrey Kasekenya kukagua mradi wa ujenzi wa nyumba za watumishi ' Magomeni Kota Phase 2 A' uliokamilika kwa asilimia 96.ASHIKILIWA NA POLISI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA NA KUMTISHIA KUMUUA MTOTO WAKE WA KUZAA MWENYEWE
















