Sunday, 8 January 2023
KAMATI YA UTATUZI WA MIGOGORO VIJIJI NA MITAA 975 NCHINI YAHITIMISHA KAZI DAR ES SALAAM.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendelo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula akiongea na viongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani kuhusu zoezi la utatuzi wa migogoro ya ardhi ya Mitaa na Vijiji 975 zoezi ambalo limehitimishwa leo Mkoani Dar es Salaam.
Waziri wa TAMISEMI Angela Kairuki akiongea na viongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani kuhusu zoezi la utatuzi wa migogoro ya ardhi ya Mitaa na Vijiji 975 zoezi ambalo limehitimishwa leo Mkoani Dar es Salaam.
Sehemu ya viongozi wa Wizara na wa Mkoa wa Pwani na Dar es Salaam wakifuatilia kwa makini maamuzi ya Kamati ya Mawaziri wa Kisekta kuhusu zoezi la utatuzi wa migogoro ya ardhi ya Mitaa na Vijiji 975 zoezi ambalo limehitimishwa leo Mkoani Dar es Salaam.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendelo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula katikati, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amosi Makala kushoto na Waziri Kairuki kulia wakiongea na viongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani kuhusu zoezi la utatuzi wa migogoro ya ardhi ya Mitaa na Vijiji 975 zoezi ambalo limehitimishwa leo Mkoani Dar es Salaam.Saturday, 7 January 2023
MINZA MAYENGA; MAMA ALIYEKATWA MAPANGA NA MUMEWE KISA NG’OMBE NA MASHAMBA
WADAU SMZ NA SMT WAJADILI ANDIKO LA MAPENDEKEZO YA SHERIA YA UTAFUTAJI NA UOKOAJI

Dkt. Devotha Mandanda, Mwanasheria kutoka TASAC akifanya wasilisho la mapendekezo ya andiko la Sheria ya Utafutaji na Uokoaji.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Sekta ya Uchukuzi, Ndg. Shomari Omar Shomari (aliyekaa katikati) akiwa katika picha ya pampja na baadhi ya wadau walioshiriki katika kikao cha kujadili andiko la mapendekezo ya Sheria ya Utafutaji na Uokoaji. Wadau mbalimbali wa sekta ya usafiri kwa njia ya maji na anga wamekutaka kwa siku mbili kujadili kuhusu andiko la mapendekezo ya sheria ya utafutaji na uokoaji katika ukumbi wa ZURA uliopo Zanzibar tarehe 5 na 6 Januari, 2023.
Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa wakati wa kikao hicho Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Usafirishaji na Mawasiliano Zanzibar Ndg. Shomari Omar Shomari amesema sheria hiyo ni mihimu kwa pande zote mbili kwani usafiri wa anga na majini umeongezeka kwa kasi kikubwa hivyo ni wakati muwafaka kukamilisha sheria ya utafutaji na uokoaji.
“Kutokana na majanga yanayotokea majini na angani basi hivyo matoke yanayotokea ni muongozo mzuri wa kufanya na kufuatia miongozo hiyo ya utafutaji wa anga na kubainika kuwepo na changamoto katika anga na bagarini" alisema Bw.Shomari.
Aliongeza kuwa anatambua juhudi za Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Sekta ya Uchukuzi kupitia katibu Mkuu kwa utamaduni wake wa kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na kuwezesha kufanyika kikao hiki muhimu Zanzibar ili kupata maoni ya pande zote mbili.
“Tunafahamu changamoto kwa sheria kama hizi zinazohusu Muungano kupata maoni mpaka kukamilisha utaratibu wa kutunga sheria, jambo hili alilolifanya ni muhimu sana pia inaonyesha ushirikiano wetu ulivyozidi kuimarika, aliongeza" Bw. Shomari.
Pia alisema mbali na kuwa kumekuwa utungaji wa sheria hii unafuatia makubaliano na maelekezo yaliyotolewa na Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga (ICAO) na Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Majini (IMO), hivyo kuwataka washiriki kuhakikisha sheria hiyo inasimamia masuala ya utafutaji na uokoaji kwa kuzingatia miongozo ya kimataifa.
Naye Mkurugenzi wa Idara ya Sera, Mipango na Utafiti kutoka Wizara ya Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi - Zanzibar, Bw. Makame Machano Haji amesema ni vyema kuwe na mfumo rasmi wa kisheria utakao toa nguvu kwa pande zote mbili kushirikiana kama Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pindi kunapotokea janga katika anga au majini.
“Suala hili linahitaji rasilimali fedha, watu na vifaa, nguvu ya upande mmjoja haiwezi kufamikisha kutatua tatizo hili hivyo tukiungana pamoja tunaweza kutatua tatizo kwa pamoja" alisema Bw. Machano.
Naye Mkurugenzi wa Sera na Mipango kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Sekta ya Uchukuzi Bw. Maseke Mabiki amesema jambo la muhimu ni wadau kuwa wazi kuelezea changamoto ili kuweza kuwa na sheria itakayosaidia pande zote mbili.
Wadau mbalimbali wa Sekta ya usafiri kwa njia ya anga na maji kutoka Serikali ya Muungano Tanzania (SMT) na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) ambao ni Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi – Zanzibar, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Mamlaka ya Usafiri Baharini Zanzibar (ZMA), Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TCAA) pamoja na Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar (KMKM) wamekutana kujadili andiko la Mapendekezo ya Sheria ya Utafutaji na Uokoaji.
CCM SHINYANGA WAJIPANGA MIKUTANO YA HADHARA..."HII PIN ILITUATHIRI PIA... SASA VYAMA RAFIKI VIKASEME UKWELI VISIFUNIKE MIWANI YA MBAO"
Friday, 6 January 2023
WAHUNI WASHIRIKIANA NA WANAFUNZI KUVUTA BANGI SHINYANGA MJINI

AJALI YA BASI LA LORI YAUA WATU 16
IGP WAMBURA AFANYA MABADILIKO YA MAKAMANDA WA POLISI
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Camillus Wambura, amefanya mabadiliko ya Makamanda wa Polisi wa mikoa katika kuboresha na kuongeza ufanisi wa utendaji kwenye mikoa mitatu.BABA AJIUA BAADA YA KUUA MKE, MAMA MKWE NA WATOTO WATANO































