Saturday, 3 December 2022
KIJANA ANUSURIKA KUUAWA BAADA YA KUNASWA AKIWAFUNDISHA WATOTO USHOGA....AKIRI KUWA NI SHOGA
Friday, 2 December 2022
WAZIRI DKT. GWAJIMA AONGOZA KONGAMANO LA WANAWAKE NA MAENDELEO
ZIARA YA MTENDAJI MKUU TARURA YALETA FARAJA KWA WANANCHI- KALIUA
VYUO VYA ELIMU YA JUU VYATAKIWA KUWAPA VIJANA UJUZI ,MAARIFA NA STADI ZINAZO WAWEZESHA KUJIAJIRI
Katibu Mkuu Wizara ya elimu,sayansi na teknolojia Dkt. Francis Michael akizungumza wakati wa utiaji saini wa makubaliano ya ruzuku ya Mradi wa HEET kwa Taasisi za Elimu ya Juu zilizo chini ya Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam..
Na mwandishi wetu,WEST-DAR.
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imetoa wito kwa Vyuo vya Elimu ya Juu vinavyotekeleza Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) kuhakikisha vinatekeleza azma ya Serikali ya kuwapatia vijana ujuzi, maarifa na stadi zitakazowawezesha kujiajiri ama kuajiriwa.
Wito huo umetolewa jana Desemba 1, 2022 Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Francis Michael wakati wa utiaji saini wa makubaliano ya ruzuku ya Mradi wa HEET kwa Taasisi za Elimu ya Juu zilizo chini ya Wizara ya Fedha na Mipango.
Kiongozi huyo amesema mradi huo unatarajiwa kuleta mageuzi makubwa katika mawanda ya elimu ya juu nchini kwa kuwaandaa vijana watakaokuwa na uwezo wa kushindana katika soko la ajira la ndani na kimataifa kwa kujiajiri ama kuajiriwa.
"Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Benki ya Dunia wanataka kuona mradi huu ukiwaondoa vijana barabarani kwa kuwapatia ujuzi, maarifa na stadi zitakazowawezesha kujiajiri ama kuajiriwa, hivyo twendeni tukatekeleze mradi huu kwa mtazamo huo" amesisitiza Dkt Michael
Katibu Mkuu huyo amezitaka Taasisi hizo kuhakikisha wanatekeleza mradi huo kwa kufuata sheria na taratibu zilizowekwa, huku akisisitiza matumizi makini ya fedha.
Kwa upande wake Mratibu wa Mradi huo kwa Wizara ya Fedha na Mipango Amani Ngedu ameishukuru Wizara ya Elimu na Benki ya Dunia kwa kuzipatia Taasisi hizo mradi huo kwa kuwa unakuwa mradi wa kwanza mkubwa kwa taasisi hizo.
Ameongeza kuwa ushirikiano uliopo kati ya Wizara hizo mbili utasaidia katika kusimamia utekelezaji wa mradi huo katika taasisi hizo kwa ufanisi na weledi.
Taasisi za Elimu zilizo chini ya Wizara ya Fedha na Mipango zinazonufaika na Mradi huo ni Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Chuo cha Mipango (IRDP), Chuo cha Takwimu (EASTC), Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) na Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA).