Wednesday, 9 November 2022

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI NOVEMBA 10,2022














Share:

RC DENDEGO AITAKA EWURA KUSHUGHULIKIA MASLAHI YA WAFANYAKAZI


MKUU wa wa Mkoa wa Iringa Mhe. Halima Dendego,akizungumza wakati akifungua kikao cha nne cha Baraza la Wafanyakazi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) leo Novemba 9,2022 Mjini Iringa.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), ambayeni Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wa EWURA Mhandisi Modeatus Lumato,akizungumza wakati wa kikao cha Baraza kinachofanyika leo Novemba 9,2022 Mjini Iringa.


KATIBU Tawala Mkoa wa Iringa (kushoto) Mha. Leonard Masanja akipokea mfano wa hundi yenye thamani ya sh. milioni 10 kutoka kwa Mkuu wa Mkoa Iringa, Mhe Halima Dendego, iliyotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) ili kuunga mkono utalii wa ndani kupitia tamasha la Utalii Karibu Kusini 2022, linalofanyika mkoani Iringa


MAKAMU Mkuu wa Shule ya Wasichana Iringa( kushoto) Bw. Mikidadi Rashid akipokea mfano wa hundi ya sh. milioni 10 kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Halima Dendego(wa pili kulia) iliyotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kusaidia ujenzi wa uzio wa shule hiyo ili kuboresha miundombinu ya kusomea


MKUU wa wa Mkoa wa Iringa Mhe. Halima Dendego,(aliyeketi katikati) akiwa katika picha ya pamoja na vVongozi pamoja na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa EWURA mara baada ya kufungua kikao cha nne cha Baraza la Wafanyakazi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kilichofanyika leo Novemba 9,2022 Mjini Iringa.

.................................

Mkuu wa wa Mkoa wa Iringa Mhe. Halima Dendego ameielekeza Menejimenti ya EWURA kushugulikia maslahi ya Wafanyakazi kwa wakati ili kuondoa malalamiko yanayoweza kujitokeza sehemu za kazi kwa lengo la kuimarisha utendaji na ufanisi wa utendaji.

RC Dendego ameelekeza hayo wakati akifungua kikao cha nne cha baraza la Wafanyakazi wa EWURA , leo 9 Novemba 2022 mjini Iringa.

“Menejimenti ya EWURA kuweni karibu na wafanyakazi wenu, shughulikieni maslahi yao kwa wakati ili kuepusha migogoro isiyo ya lazima” Alisisitiza RC Dendego.

Aidha, Mkuu wa Mkoa huyo, amewataka wafanyakazi wa EWURA kuwa na staha wanapodai maslahi yao sanjari na kuwajibika katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.

RC Dendego pia, alikabidhi hundi yenye thamani ya sh. milioni 10 kwa shule ya Sekondari ya Wasichana Iringa kusaidia ujenzi wa uzio na shilingi milioni 10 nyingine kuunga mkono juhudi za kuimarisha utalii kwa Nyanda za Juu Kusini katika kushamirisha tamaha la “Utalii Karibu Kusisni 2022”

Akizungumzia msaada huo, Mkurugenzi Mkuu wa EWURA Mha. Modeatus Lumato, alieleza kuwa, EWURA imekuwa na utaratibu wa kusaidia jamii katika nyanja mbalimbali na kwamba kipindi hiki Mamlaka imetoa kipaumele katika eneo la elimu na utalii.

“Sisi EWURA, tumeona ni vyema tusaidie kuimarisha miundombinu ya elimu pamoja na kuhamasisha utalii wa ndani kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu Hassan katika masuala hayo.

Mwakilishi wa Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Iringa, Mwl Mikodadi Rashid, baada ya kupokea hundi hiyo, aliishukuru EWURA kwa msaada huo na kueleza kuwa utakuwa chachu ya kuboresha mazingira ya kusomea.

Naye Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa TUGHE Taifa Mha.Amani Msuya aliyetoa salamu za TUGHE Taifa kwa niaba ya Katibu Mkuu wake, Henry Mgunda, ameeleza kuwa taasisi zote za umma zinatakiwa kuhakikisha zinakuwa na utaratibu wa kuimarisha maslahi na hali bora za wafanyakazi.

Kwa upande wake Katibu wa TUGHE Tawi la EWURA, Bw. Emmanuel Ndalawa alieleza kuwa, wataendelea kutoa ushirikano kwa menejimenti ya EWURA ili kwa pamoja kuleta tija zaidi katika kuboresha hali bora za wafanyakazi.

Jumla ya wawakilishi wa wafanyakazi 60 wamehudhuria kikao hicho cha nne cha Baraza la Wafanyakazi kitakachofanyika kwa siku mbili mkoani Iringa.
Share:

WIZARA YA ELIMU KUGAWA RASILIMALI NA FURSA KWA HAKI

 



Na Mathias Canal, WEST- Bagamoyo, Pwani.


Serikali imempongeza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Bi Bahati Geuzye pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya mamlaka hiyo Prof Maurice Mbago kwa kazi kubwa na nzuri wanayoifanya kwa utoaji wa rasilimali kote nchini na kuitaka kuendelea kutoa fursa kwa haki katika kusaidia na kugawa rasilimali zinazohitajika katika maeneo mbalimbali mchini.


Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe Prof Adolf Mkenda ameyasema hayo leo tarehe 8 Novemba 2022 wakati akizungumza na wananchi mara baada ya kukabidhiwa nyumba nne za walimu wa shule ya msingi Msinune iliyopo katika Halmashauri ya Chalinze,  Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani zilizojengwa na Taasisi ya Flaviana Matata Foundation pamoja na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA).


Waziri Mkenda ameitaka Mamlaka ya elimu Tanzania (TEA) kuhakikisha kuwa inabainisha vigezo vya kutoa rasilimali na fursa katika jamii kwani uwazi ni jambo la muhimu ili kurahisisha utoaji haki.


"Kwa taasisi zetu zote mnavyo vigezo mnavyovitumia katika ugawaji rasilimali hivyo ni lazima tukae tupitie na kuviboresha ili kubaini maeneo mahususi ya kuvipeleka ili kila mtoto anayezaliwa hapa Tanzania apate fursa sawa" Amekaririwa Waziri Mkenda na kuongeza kuwa


"Fursa zigawanywe sawa sawa na vigezo vitangazwe vya utoaji fursa, hatuwezi kujenga nchi kwa kugawa fursa kwa upendeleo lazima tutoe kwa haki, tatizo uwazi wakati mwingine watu hawapendi lakini lazima tusimamie" Amekaririwa Waziri Mkenda


Prof Mkenda amesema kuwa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliijenga nchi ya Tanzania kwa usawa wa binadamu, na usawa huo utekelezaji wake ni kujifunza hasa kwenye sekta ya elimu bila kuyumba, kutetereka wala kuogopa.


Kadhalika, Waziri Mkenda amempongeza Mbunge wa Jimbo la Chalinze ambaye ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Ridhiwani Kikwete kwa juhudi zake za kuliendeleza Jimbo lake katika sekta mbalimbali ikiwemo kilimo na elimu.


Kwa upande wake Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maemdleeo ya Makazi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mhe Ridhiwani Kikwete amempongeza Waziri Mkenda kwa uthubutu wake wa kuamua kufanya mabadiliko katika sekta ya elimu ambao utakuwa chachu kubwa katika kuikuza na kuiendeleza sekta ya elimu nchini.


"Uthubutu huo ndio ambao una kielelezo cha kutosha kuelekea kwenye maendeleo ambayo kila mtanzania anayataka, Rais yetu Mhe mama Samia Suluhu Hassan alipoamua kumchagua Prof Mkenda kuwa waziri wa elimu, mimi binafsi nilifurahi sana" Amekaririwa Mhe Kikwete


Naibu Waziri Kikwete amesema kuwa kilichomfurahisha kwa kuteuliwa Prof Mkenda kuwa Waziri ni rekodi yake nzuri aliyoiacha Chuo kikuu huku akimtaja kuwa kiongozi wa mfano kwa wanasiasa wanaochipukia.


"Wapo watu wachache ambao wanaweza wakabeza mambo unayoyafanya kwenye nchi hii lakini nia yako itashinda hayo ambayo watu wengine wanafikiri juu yako. Siku zote kwenye maendeleo weka mipango kwanza, tafakari jinsi ya kufanya na tekeleza mipango hiyo na wewe Prof Mmenda umekuwa ukifanya hivyo" Amesisitiza


Mhe Ridhiwani amesema kuwa ataendelea kuunga mkono juhudi za Waziri Mkenda katika utekeleza mabadiliko ya elimu anayoyafanya ikiwa ni pamoja na kuimarisha sekta ya elimu nchini.


"Mimi naamini tukikusaidia wewe maana yake tumemsaidia Mheshimiwa Rais, na amekuteua wewe kwa sababu anajua kabisa kuwa ili ufanikiwe lazima uwe na watu nyuma yako na sisi tupo nyuma yako" Amesisitiza Ridhiwani



Share:

OBASANJO CALLS ON THE PAP TO HARNESS ITS POTENTIAL AND DELIVER ON ITS MANDATE


Rais mstaafu wa Nigeria Olusegun Obasanjo akihutubia Mkutano wa Bunge la Afrika (Pan African Parliament – PAP), Jumanne Novemba 8,2022 ambapo amelihimiza Bunge la Afrika kuchukua jukumu muhimu katika kuhakikisha usalama, amani na utulivu barani Afrika.
Rais mstaafu wa Nigeria Olusegun Obasanjo akihutubia Mkutano wa Bunge la Afrika (Pan African Parliament – PAP), 

Former President of the Federal Republic of Nigeria and African Union (AU) High Representative for the Horn of Africa, H.E Olusegun Obasanjo has urged the Pan-African Parliament (PAP) to play a pivotal role in ensuring security, peace and stability in Africa.

The renowned African Statesman addressed the PAP Plenary at the ongoing first Ordinary Session of the sixth Parliament of the PAP in Midrand, held under the African Union theme for 2022: “Building resilience in nutrition on the African continent: Accelerate the human capital, social and economic development”.


Recalling the context leading to the establishment of the PAP, H.E Obasanjo underscored the significance of the Continental Parliament in the AU governance, peace and security architecture.


“The objectives for which the PAP was established have not changed and the contribution of this Parliament is required now more than ever. Indeed, it must be emphasised that the PAP is not an unnecessary institution. It’s an institution that should be part and parcel of the instruments that will lead us to the Promised Land,” said President Obasanjo.

The AU High Representative further urged the PAP to reclaim its power and rightful place as the voice of the African citizens at a time when the continent grapples with numerous challenges, especially on the peace and security front. He challenged the PAP to harness its potential and be more visible on the continent.


“You have power and you must not let anyone dictate that power. For instance, you can discuss, examine and make recommendations to policy organs on your own initiative. Your Committee on Cooperation, International Relations and Conflict Resolution should be at the forefront of leading initiatives involving peacebuilding across the continent as we try to contain instability in the face of unconstitutional changes of government. There’s a lot to do if we are to achieve peace and this body has a central role to play,” he said.


H.E Obasanjo said that he was encouraged by the issues tackled by the PAP as part of the business related to the first Ordinary Session of the sixth Parliament. Among the other four motions, the PAP Plenary adopted a motion congratulating the Federal Republic of Ethiopia and Tigray People’s Liberation Front on the Signing of the Peace Agreement. The motion also congratulated the AU mediators led by President Obasanjo for their stewardship and impartiality which became a hallmark of this peace agreement.


Describing the process that led to the peace agreement, H.E Obasanjo said:

“It wasn’t easy for us to achieve a Peace Agreement in Ethiopia. The process is challenging, long and frustrating, but because we are determined to see peace and stability in Africa, we managed to bring together the warring parties to the table to convey our vision for a united Ethiopia. We had to be neutral, friendly and appreciative to everyone despite whatever reservations we had. I encourage you as the PAP to also develop that spirit; the spirit that borders around resilience and focus.”

“I am pleased that we have managed to create an environment in Ethiopia whereby people who were foes can now live together. We are glad that all outstanding disputes were resolved in a principled manner. I believe that if we managed to resolve Ethiopian challenges then we can find solutions in other parts of Africa,” he added.

Meanwhile, H.E Hon. Chief Fortune Charumbira hailed the role of President Obasanjo in Ethiopia and across the continent and described his address to the PAP as historic and a testament to the Parliament’s revival.

“As Africans, we celebrate your efforts which have produced very good results in Ethiopia. As the Chief negotiator, you have delivered peace in that country, and this is an incredible achievement. With people of your calibre, Africa is in good hands,” said H.E Hon. Charumbira.


H.E Hon. Charumbira also briefed the former President of the Oil rich nation about motions that the PAP adopted and noted. These include a motion on the DRC-Rwanda conflict, a motion on illegal sanctions imposed on Zimbabwe by the US and its allies, the Mozambique terrorism challenges motion and the Uganda Oil project motion.

-Ends-

Share:

MHUBIRI ASAKWA BAADA YA KUMNAJISI NA KUMUUA MTOTO WA MIAKA 10 AKIFANYA MAOMBI NYUMBANI KWAO


Polisi katika eneo la Rangwe, Kaunti ya Homa Bay nchini Kenya wanamsaka mhubiri anayetuhumiwa kumuua mtoto mwenye umri wa miaka 10, baada ya kumnajisi kisha akamnyonga na kutupa mwili wake katika shamba la mahindi.

Mwanaume huyo anaripotiwa kumnajisi msichana huyo katika kijiji cha Kamuombo katika lokesheni ndogo ya Kamenya, Rangwe, siku ya Alhamisi, 3,2022 jioni. 

Jamaa za Vivian Akoth wanasema alikutana na mshukiwa wakati alipokuwa ametumwa nyumbani kwa bibi yake kuchukua kibuyu cha kuteka maji. 

Nyanya yake alimtambulisha mwanaume huyo kwa jina moja tu Abraham ambaye alisema alikuwa mgeni wake kutoka Kisumu.

Mwanaume huyo aliyekuwa amevalia kanzu ambayo mara nyingi huvaliwa na waumini wa Legion Maria alikuwa katika nyumba hiyo kwa maombi. 

Kwa mujibu wa ripoti ya polisi, mwanamume huyo anaripotiwa kumfuata msichana huyo nje, akamshambulia na kumnyonga katika shamba la mahindi na kumwacha na maumivu makali. 

Mpita njia alitokea na kupiga kamsa ambapo msichana huyo alipelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Kaunti ya Homa Bay, lakini alifariki dunia alipokuwa akipokea matibabu. 

Chifu Msaidizi wa eneo hilo Lilian Ombai alisema kasisi huyo alikuwa kwenye misheni ya kuombea familia. 

Afisa wa Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa Kaunti hiyo ndogo Monica Berege alisema wamemkamata mwanamke mzee ambaye anasemekana alikuwa na mshukiwa wakati tukio hilo lilitokea. 

“Anaweza tu kumtambua mshukiwa kwa jina moja. Lakini alikuwa akifanya nini na mwanaume huyo nyumbani kwake ikiwa hamjui? Tunafanya kila tuwezalo kumkamata mshukiwa mkuu,” Berege alisema.

Chanzo - Tuko News
Share:

JESHI LA POLISI LATAJA MAJINA YA WATU SABA WALIOFARIKI KWA AJALI KITETO


Watu saba ambao ni watumishi wa serikali ya wilaya ya kiteto Mkoani Manyara Idara ya afya na elimu wamefariki kwa ajali baada ya gari waliyokuwa wamepanda kugongana na gari nyingine aina ya Prado katika eneo la Pori namba moja Kata ya Partimbo Kiteto Mkoani Manyara.

Ajali hiyo imetokea Novemba 8,2022  eneo la Pori namba moja Kata ya Partimbo Kiteto Mkoani Manyara.

Kwa mujibu wa kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara RPC George Katabazi ametaja majina ya waliopoteza maisha pamoja na majeruhi.


Waliopoteza maisha ni:
1.Joseph Bizuku (36) Muuguzi
2.Edward Makundi (47) Daktari
3.Agapiti Kimaro (32) Mkuu wa shule ya Esamatwa
4.Kadidi Saidi (36) Nesi
5.Celina Nyimbo 31 Mtumishi wa maabra
6 Katherine Mathei (31) Nesi
7.Nickson Mhongwa Daktari

Waliopelekwa Hospitali ya Dodoma ni
1.Method Malick (55) Dereva Prado
2.Juma Mbaruku (45) Dereba ambulance Kiteto

Waliolazwa hospitali ya Kiteto
1 Ibrahim Selemani (71)
2.Mbaraka Shabani (44)
Share:

Tuesday, 8 November 2022

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATANO NOVEMBA 9,2022







Share:

Live : OBASANJO ANAHUTUBUA BUNGE LA AFRIKA 'PAP' MUDA HUU

Rais mstaafu wa Nigeria Olusegun Obasanjo akihutubia Mkutano wa Bunge la Afrika (Pan African Parliament – PAP), leo Jumanne Novemba 8,2022 katika Ukumbi wa PAP uliopo Midrand Afrika Kusini. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Rais mstaafu wa Nigeria Olusegun Obasanjo akihutubia Mkutano wa Bunge la Afrika (Pan African Parliament – PAP), leo Jumanne Novemba 8,2022

TAZAMA HAPA


Rais wa Bunge la Afrika (PAP), Mhe. Chifu Fortune Charumbira (kushoto) akimkaribisha Rais mstaafu wa Nigeria Olusegun Obasanjo kuhutubia Mkutano wa Bunge la Afrika (Pan African Parliament – PAP), leo Jumanne Novemba 8,2022
Rais mstaafu wa Nigeria Olusegun Obasanjo akihutubia Mkutano wa Bunge la Afrika (Pan African Parliament – PAP), leo Jumanne Novemba 8,2022
Rais mstaafu wa Nigeria Olusegun Obasanjo akihutubia Mkutano wa Bunge la Afrika (Pan African Parliament – PAP), leo Jumanne Novemba 8,2022
Rais mstaafu wa Nigeria Olusegun Obasanjo akihutubia Mkutano wa Bunge la Afrika (Pan African Parliament – PAP), leo Jumanne Novemba 8,2022
Rais mstaafu wa Nigeria Olusegun Obasanjo akihutubia Mkutano wa Bunge la Afrika (Pan African Parliament – PAP), leo Jumanne Novemba 8,2022
Rais mstaafu wa Nigeria Olusegun Obasanjo akihutubia Mkutano wa Bunge la Afrika (Pan African Parliament – PAP), leo Jumanne Novemba 8,2022
Rais mstaafu wa Nigeria Olusegun Obasanjo akihutubia Mkutano wa Bunge la Afrika (Pan African Parliament – PAP), leo Jumanne Novemba 8,2022

Rais wa Bunge la Afrika (PAP), Mhe. Fortune Charumbira akizungumza kwenye Mkutano wa Bunge la Afrika (Pan African Parliament – PAP), leo Jumanne Novemba 8,2022
Rais wa Bunge la Afrika (PAP), Mhe. Fortune Charumbira akizungumza kwenye Mkutano wa Bunge la Afrika (Pan African Parliament – PAP), leo Jumanne Novemba 8,2022
Rais wa Bunge la Afrika (PAP), Mhe. Fortune Charumbira akizungumza kwenye Mkutano wa Bunge la Afrika (Pan African Parliament – PAP), leo Jumanne Novemba 8,2022
Rais wa Bunge la Afrika (PAP), Mhe. Fortune Charumbira akizungumza kwenye Mkutano wa Bunge la Afrika (Pan African Parliament – PAP), leo Jumanne Novemba 8,2022
Rais wa Bunge la Afrika (PAP), Mhe. Fortune Charumbira akizungumza kwenye Mkutano wa Bunge la Afrika (Pan African Parliament – PAP), leo Jumanne Novemba 8,2022.

Picha na Kadama Malunde - Midrand Afrika Kusini

Share:

RAIS MSTAAFU WA NIGERIA OLUSEGUN OBASANJO AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS WA PAP CHIFU CHARUMBIRA


Rais mstaafu wa Nigeria Olusegun Obasanjo (kushoto)amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Bunge la Afrika (Pan African Parliament – PAP), Mhe. Chifu Fortune Charumbira kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu Bara la Afrika leo Jumanne Novemba 8,2022 katika Makao Makuu ya Bunge la Afrika, Midrand Afrika Kusini. Mhe. Obasanjo leo atahutubia Bunge la Afrika. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Share:

MTU MWENYE ULEMAVU AVAMIWA NA WAHUNI, ALAWITIWA NA KUKATWA NYETI ZAKE

Mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 48, anapokea matibabu baada ya kushambuliwa na kulawitiwa na genge lisilojulikana katika Kituo cha Nderu eneo la Ndeiya, Kaunti ya Kiambu nchini Kenya.

Uchunguzi umebaini kuwa mwanaume huyo ambaye ni mlemavu, alivamiwa alipokuwa kwa matembezi ya jioni katika eneo la Ndeiya, lililoko kati kati ya kaunti ndogo za Limuru na Kikuyu.

Wakazi waliohojiwa na Citizen TV, walisema kwamba mwathiriwa alibanwa na majangili hao muda mfupi baada ya kuondoka katika baa moja ya eneo hilo.

 Taarifa zaidi zinasema kuwa mwathiriwa alilawitiwa na wavamizi hao kisha kumkata sehemu zake za siri.

"Tunashuku kuwa kinywaji cha mwathiriwa kilikuwa na dawa za kulevya. Ni lazima washukiwa walitumia dawa ya kumlewesha kabla ya kumtupa barabarani. Inasikitisha," mkazi mmoja alisema. 

Kitendo hicho cha kinyama kimewaghadhabisha sana wenyeji wakitaka hatua za haraka kuchukuliwa na mamlaka husika.

 Akithibitisha kisa hicho, Kamanda wa Polisi wa Kaunti Ndogo ya Ndeiya, Roseline Mnyolmo alisema wanafanya uchunguzi ili kuwakamata wahusika wa kitendo hicho kiovu na kuwashtaki.

Kwa sasa mwathiriwa anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Kiambu Level Five baada ya kupokea huduma ya kwanza katika Hospitali ya Ndeiya Level Three.


Akatwa nyeti zake na majambazi usiku

Katika kisa kingine sawa na hicho, mzee mwenye umri wa miaka 70, alivamiwa nyumbani kwake na watu wasiojulikana ambao walimkata sehemu zake za siri. 

Mzee Uruban Paul, ambaye ni mkazi wa kijiji cha Uru Shimbwe, mkoani Kilimanjaro, Tanzania, alisema alikuwa akitoka kwenda kujisaidia wakati alikutana na watu hao ambao baada ya kumfanyia kitendo hicho walikuwa wakikinga damu yake.


Baada ya kufanyiwa unyama huo, mzee huyo anasema alijiburuza kutoka nje kuomba msaada na bahati nzuri alikutana na jirani yake ambaye pamoja na wenzake walimpeleka hospitalini.
Share:

HII NDIO DAWA YA BOSI ANAYECHELEWESHA MSHAHARA

Share:

Live : KINACHOENDELEA MKUTANO WA BUNGE LA AFRIKA LEO JUMANNE NOVEMBA 8

 

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger