Thursday, 6 October 2022

WEADO WATAMBULISHA MRADI WA VUNJA UKIMYA, ZUIA NDOA NA MIMBA ZA UTOTONI WILAYANI SHINYANGA



Mkurugenzi wa Shirika la WEADO Eliasenya Nnko akizungumza wakati wa kutambulisha mradi wa vunja ukimya, zuia ndoa na mimba za utotoni wilayani Shinyanga ambao utatekelezwa Kata ya Masengwa na Tinde wilayani Shinyanga.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

SHIRIKA la Women Elderly Advocacy and Development Organization (WEADO) la Mkoani Shinyanga, limetambulisha mradi wa vunja ukimya, zuia ndoa na mimba za utotoni wilayani Shinyanga.
Mradi huo umetambulishwa leo Oktoba 6, 2022 katika Kata ya Tinde wilayani Shinyanga kwenye ukumbi wa Shule ya Sekondari ya wasichana Tinde (Tindegirls).

Afisa mradi kutoka Shirika la WEADO Winnie Hinaya, akiwasilisha utekelezaji wa mradi huo, amesema utatekelezwa katika Kata mbili Masengwa na Tinde wilayani Shinyanga ndani ya miezi nane ambao utekelezaji wake ni kuanzia Septemba mwaka huu hadi Aprili 2023 kwa ufadhili wa Shirika la Foundation For Civil Society wenye thamani ya Sh.milioni 37.8.

“Lengo la mradi huu ni kupunguza kiwango cha mimba na ndoa za utotoni,”amesema Hinaya.

Aidha, amesema Shughuli ambao zitakuwa zikitumika kwenye mradi huo ni kutoa elimu ya kupinga masuala ya mila na desturi Kandamizi, elimu ya malezi bora, makuzi ya mtoto, mafunzo ya ulinzi na haki za watoto,”ameongeza.

Amesema Kata hizo Masengwa na Tinde wamezipelekea mradi huo kwa kutaka ziwa mfano wa kuigwa katika mapambano ya kumaliza tatizo la mimba na ndoa za utotoni mkoani Shinyanga.

Naye Mkurugenzi wa Shirika la WEADO Eliasenya Nnko, amesema malengo ya mradi huo ni kuona jamii inakuwa salama na hakuna tena mimba wala ndoa za utotoni pamoja na watoto kusoma na kutimiza ndoto zao.

Kwa upande Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Nicodemas Simoni ambaye pia ni diwani wa Masengwa akifungua kikao hicho. amelipongeza Shirika hilo la WEADO kwa mradi huo ambao utasaidia kuokoa ndoto za wanafunzi, huku akiahidi Halmashauri itaendelea kutoa ushirikiano kwa mashirika yote ambayo yanaisaidia jamii.

Aidha, Afisa Maendeleo ya Jamii halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Aisha Omary, amesema wadau wa maendeleo wamekuwa na mchango mkubwa katika mapambano ya kutokomeza mimba na ndoa za utotoni, ambapo katika halmashauri hiyo matukio hayo yamepungua kwa kiasi kikubwa tofauti na miaka ya nyuma, kuwa ndoa za utotoni zilikuwa zikifungwa Tisa hadi 10 lakini sasa zinakomea mbili hadi tatu na zote zinatibuliwa.

Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Shinyanga Lidya Kwesigabo, ameitaka jamii wanapozuia mimba na ndoa za utotoni wawakumbuke na watoto wenye ulemavu ambapo wamekuwa wakisahauriwa na kuishia kupewa ujauzito na kuharibu maisha yao.
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Nicodemas Simon na diwani wa Masengwa akizungumza kwenye utambulisho wa mradi wa Shirika la WEADO.

Mkurugenzi wa Shirika la WEADO Eliasenya Nnko akizungumza wakati wa kutambulisha mradi wa vunja ukimya, zuia ndoa na mimba za utotoni wilayani Shinyanga ambao utatekelezwa Kata ya Masengwa na Tinde wilayani Shinyanga.

Afisa mradi kutoka Shirika hilo la WEADO Winnie Hinaya, akiwasilisha utekelezaji wa mradi huo.
Afisa mradi kutoka Shirika hilo la WEADO Winnie Hinaya, akiwasilisha utekelezaji wa mradi huoAfisa ufuatiliaji na tathimini kutoka WEADO John Eddy akizungumza kwenye utambulisho wa mradi huo.

Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Shinyanga Lidya Kwesigabo akizungumza kwenye utambulisho wa mradi huo.

Afisa Maendeleo ya jamii halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Aisha Omary akizungumza kwenye utambulisho wa mradi huo.

Viongozi mbalimbali wa Kata ya Tinde na Masengwa wakiwa kwenye utambulisho wa mradi huo wakiwamo watendaji wa vijiji Kata, Maofisa Elimu, Maendeleo , viongozi wa dini, wazee maarufu, wanafunzi na madiwani.

Kikao cha utambulisho wa mradi kikiendelea.

Kikao cha utambulisho wa mradi kikiendelea.

Kikao cha utambulisho wa mradi kikiendelea.

Kikao cha utambulisho wa mradi kikiendelea.

Kikao cha utambulisho wa mradi kikiendelea.

Kikao cha utambulisho wa mradi kikiendelea.

Wajumbe wakiwa kwenye makundi ya kupanga mpango kazi.

Picha ya pamoja ikipigwa.

Share:

WANAHARAKATI WATAKA SHERIA ZITUMIKE KUKOMESHA UKATILI WA KIJINSIA "MENGINE SIYO MILA NI ULAFI TU"

Afisa Mradi wa Elimu ya Haki za Binadamu kutoka Shirika la Tusonge CDO, Consolata Kinabo.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Jamii imetakiwa kuacha tabia za kumaliza kesi za masuala ya ukatili wa kijinsia kienyeji ikiwemo mimba na ndoa za utotoni kwa kisingizio kuwa ni mila na desturi bali sheria inatakiwa kuchukua mkondo wake ili kukomesha matukio ya ukatili.

Rai hiyo imetolewa leo Alhamisi Oktoba 6,2022 na Afisa Mradi wa Elimu ya Haki za Binadamu kutoka Shirika la Tusonge CDO, Consolata Kinabo kwenye Tamasha la Jinsia Kanda ya Kaskazini wakati wa warsha iliyoongozwa na mada “Mila Kandamizi ni kikwazo cha kufikia haki za uchumi na maisha endelevu” katika viwanja vya Kwasa Kwasa wilayani Same.


“Tunakwepa kufuata sheria na tunamaliza kesi za ukatili wa kijinsia kienyeji. Tuna visingizio vya kusema mila na desturi zetu zinasema hivi matokeo yake wahanga wanazidi kuathirika na yanakuwa ni mazoea katika jamii kwa sababu wanaona hakuna sheria yoyote inayochukuliwa kwa wanaofanya ukatili”,amesema Kinabo.

Naye mmoja wa washiriki wa warsha hiyo,Sauda Hussein Mshana kutoka kituo cha taarifa na maarifa cha Kivule wilayani Same, amesema siyo kila tukio la ukatili wa kijinsia linatokana na mila na desturi kandamizi bali ni tabia tu ya mtu.


“Mambo mengine siyo mila bali ni ulafi tu, unampaje mimba mtoto? Unaoaje mtoto?, sheria zichukue mkondo wake ili haya mambo yakome”,amesema.

Washiriki wa warsha wamekemea vitendo vya ukeketaji kwa wanawake wakisema vinaleta madhara kwa wanawake ikiwemo kukosa ujasiri katika maisha, kupata maambukizi ya VVU, Homa ya Ini kwani vifaa vinavyotumika kufanyia ukeketaji siyo salama.
Afisa Mradi wa Elimu ya Haki za Binadamu kutoka Shirika la Tusonge CDO, Consolata Kinabo akizungumza kwenye Tamasha la Jinsia Kanda ya Kaskazini katika viwanja vya Kwasa Kwasa wilayani Same.
Afisa Mradi wa Elimu ya Haki za Binadamu kutoka Shirika la Tusonge CDO, Consolata Kinabo akizungumza kwenye Tamasha la Jinsia Kanda ya Kaskazini wakati wa warsha iliyoongozwa na mada “Mila Kandamizi ni kikwazo cha kufikia haki za uchumi na maisha endelevu” katika viwanja vya Kwasa Kwasa wilayani Same.
Afisa Mradi wa Elimu ya Haki za Binadamu kutoka Shirika la Tusonge CDO, Consolata Kinabo akizungumza kwenye Tamasha la Jinsia Kanda ya Kaskazini wakati wa warsha iliyoongozwa na mada “Mila Kandamizi ni kikwazo cha kufikia haki za uchumi na maisha endelevu” katika viwanja vya Kwasa Kwasa wilayani Same.

Mwakilishi kutoka  Shirika la NAFGEM Tanzania, Magdalena Mwile akizungumza kwenye Tamasha la Jinsia Kanda ya Kaskazini wakati wa warsha iliyoongozwa na mada “Mila Kandamizi ni kikwazo cha kufikia haki za uchumi na maisha endelevu” katika viwanja vya Kwasa Kwasa wilayani Same.
Mwakilishi kutoka  Shirika la NAFGEM Tanzania, Magdalena Mwile akizungumza kwenye Tamasha la Jinsia Kanda ya Kaskazini wakati wa warsha iliyoongozwa na mada “Mila Kandamizi ni kikwazo cha kufikia haki za uchumi na maisha endelevu” katika viwanja vya Kwasa Kwasa wilayani Same.
Mwenyekiti wa Bodi ya TGNP, Gemma Akilimali akichangia hoja kwenye Tamasha la Jinsia Kanda ya Kaskazini wakati wa warsha iliyoongozwa na mada “Mila Kandamizi ni kikwazo cha kufikia haki za uchumi na maisha endelevu” katika viwanja vya Kwasa Kwasa wilayani Same.
Wadau wakiwa kwenye Tamasha la Jinsia Kanda ya Kaskazini wakati wa warsha iliyoongozwa na mada “Mila Kandamizi ni kikwazo cha kufikia haki za uchumi na maisha endelevu” katika viwanja vya Kwasa Kwasa wilayani Same.
Share:

WAZIRI WA AFYA WA ZAMANI MBARONI KWA RUSHWA

 


Mamlaka nchini Zambia zimemfungulia mashtaka waziri wa zamani wa afya nchini humo kwa makosa ya rushwa.
Bw.Chitalu Chilufya anatuhumiwa kwa ubadhirifu wa fedha za uma kiasi cha dola za kimarekani milioni 17 sawa na zaidi ya shilingi bilioni 3 za Kitanzania , ambazo zilikua ni za kusambaza vifaa vya afya wakati alipokua bosi wa wizara hiyo.

Taasisi ya kupambana na rushwa nchini Zambia imesema Waziri huyo wa zamani anashtakiwa akiwa na katibu mkuu wa zamani wa wizara hiyo Mulalelo Kakulubelwa pamoja na wakurugenzi wengine watatu wa afya.

Wote wamekana mashataka hayo na wameachiwa kwa dhamana. Wanakua ni miongoni mwa watu mashuhuri kutiwa nani siku ya jana kwa tuhuma kadhaa.

Mwanachama wa upinzani Kelvin Bwalya Fube yeye ametiwa ndani kwa makosa ya dawa za kulevya ikiwemo pia utakatishaji w afedha haramu.
Share:

TANESCO SHINYANGA YAADHIMISHA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA KWA KUWAUNGANISHIA HUDUMA YA UMEME WANANCHI WALIOTUMA MAOMBI KUPITIA NI-KONEKT

Share:

Wednesday, 5 October 2022

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI OKTOBA 6,2022









Share:

HII NDIO DAWA YA MGOGORO YA ARDHI KATIKA JAMII NA FAMILIA

Share:

KAMATI YA UKUSANYAJI MAPATO YAIPONGEZA MANISPAA YA SHINYANGA KUTEKELEZA MIRADI YA MAENDELEO KWA UKAMILIFU KUPITIA FEDHA ZA MAPATO YA NDANI

 Wajumbe wa Kamati ya ukusanyaji mapato ya ndani halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye mradi wa machinjio ya kisasa Ndembezi ambao pia una mchango wa fedha za mapato ya ndani.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

KAMATI ya ukusanyaji mapato ya ndani halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, wameipongeza manispaa hiyo kwa kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo itokanayo na fedha za makusanyo ya mapato ya ndani.

 
Wamebainisha hayo leo Oktoba 5, 2022 wakati walipoendelea na ziara yao ya kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo itokanayo na mchango wa fedha za mapato ya ndani.

Katibu wa Kamati hiyo Dk. Kulwa Meshack, akizungumza kwenye ziara hiyo, amesema wamefanya ziara ya kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo Manispaa ya Shinyanga, ili kuona fedha hizo ambazo zinakusanywa zinatumikaje katika kuwaletea maendeleo wananchi.

“Tangu tulipoanza ziara hii na leo ni siku ya tatu tumeona fedha za mapato ya ndani namna zilivyotumika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo, tunapeleka Pongezi kwa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko sababu ndiye aliunda kamati hii, pongeza pia kwa Mkurugenzi na Meya kwa usimamizi mzuri wa fedha hizo na leo tumeona mapinduzi makubwa ya maendeleo,”amesema Dk. Meshack.

Aidha, amesema utekelezaji huo wa miradi mbalimbali ya maendeleo utahamasisha wafanyabiashara kuendelea kulipa Kodi sababu wanaona fedha zao namna zinavyo rudi kwao kwa kutekelezewa miradi mbalimbali ya maendeleo, na uboreshaji wa miundombinu na kufanya biashara zao katika mazingira rafiki.

Pia amewasihi wafanyabiashara kuendelea kulipa kodi kwa hiari yao, ili Serikali ipate mapato mengi na kuwatekelezea miradi mbalimbali ya maendeleo kama inavyofanya hizi sasa ambapo mji wa Shinyanga umeshabadilika ndani ya muda mfupi kutokana na fedha za mapato ya ndani.

Naye Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko, ambaye pi ndiye Mwenyekiti wa Kamati hiyo, amesema kuwa mji wa Shinyanga utajengwa na wananchi wenyewe na kuwasihi kuendelea kulipa mapato ili Serikali ipate fedha na kuwatekelezea miradi mbalimbali ya maendeleo na uboreshaji wa miundombinu zikiwamo barabara, Stendi, na ujenzi wa masoko.


Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati wa ya ukusanyaji mapato ya ndani halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga akizungumza kwenye ziara hiyo.

Katibu wa Kamati ya ukusanyaji mapato ya ndani halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Dk. Kulwa Meshack akizungumza kwenye ziara hiyo.
Wajumbe wa Kamati ya ukusanyaji mapato ya ndani halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye mradi wa machinjio ya kisasa Ndembezi ambao pia una mchango wa fedha za mapato ya ndani.

Ziara ikiendelea kwenye machanjio ya kisasa ndembezi.

Ziara ikiendelea kwenye machanjio ya kisasa ndembezi.
 

Ziara ikiendelea kwenye machanjio ya kisasa ndembezi.

Ziara ikiendelea kwenye machanjio ya kisasa ndembezi.

Muonekano wa machinjio ya kisasa.

wajumbe wakiwa kwenye mradi wa ujenzi wa Stendi ya magari madogo (HIACE) eneo la Kambarage Manispaa ya Shinyanga ,ujenzi ambao utatumia mapato ya ndani Sh..milioni 211.
Muoenako wa Ramani ya ujenzi wa Stendi hiyo itakavyokuwa.

Wajumbe wakiwa kwenye ujenzi wa Soko la Machinja jirani na Ofisi ya CCM wilaya ya Shinyanga, ambapo wafanyabiashara watafanya biashara zao hadi majira ya usiku na linajengwa kupitia mapato ya ndani Sh.milioni 120.

Muoenako wa Stendi ya Magari madogo katika Soko kuu la Manispaa ya Shinyanga ambayo imeboreshwa kupitia mapato ya ndani Sh. milioni 147.
Wajumbe wakiwa katika ujenzi wa Zahanati ya Mwamagunguli Kata ya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga ambayo imeshatengewa fedha Sh.milioni 60 kupitia fedha za mapato ya ndani ili kuendeleza ujenzi wake.
Wajumbe wakiwa katika Zahanati ya Bugweto Kata ya Ibadakuli ambayo nayo imeshatengewa Sh.milioni 30 kupitia fedha za mapato ya ndani ilikuendelea ujenzi wake huku fedha za Serikali ikitengewa Sh.milioni 50.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger