Wednesday, 5 October 2022
RC BABU AFUNGUA TAMASHA LA JINSIA KANDA YA KASKAZINI....AKEMEA UKATILI "TUSIWAPIGE, TUWABEMBELEZE WANAWAKE"
ROMBO KUTUMIA SOKO LA KIMATAIFA KUUZA NDIZI ILI KUONGEZA KIPATO CHA WAKULIMA.
Tuesday, 4 October 2022
WAZIRI WA MADINI ARIDHISHWA KASI YA UJENZI WA KINU CHA KUPOZA UMEME GGML
TBS LIMEFUNGUA MAFUNZO KUHUSU KANUNI YA USHIRIKIANO KATI YA TBS NA HALMASHAURI
RAIS SAMIA KUFUNGUA MKUTANO WA 65 WA SHIRIKA LA UTALII DUNIANI (UNWTO)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan anatarajia kufungua mkutano wa kimataifa wa 65 wa shirika la Utalii duniani (UNWTO) Oktoba 5,2022.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha,Waziri wa maliasili na utalii,Balozi aesema mkutano huo unatarajia kukutanisha mawaziri wenye dhamana ya masuala ya utalii na maliasili kutoka nchi wanachama wa UNWTO wa kanda zaidi ya 50 kujadili kuhusu mustakabali wa ustawi wa maendeleo ya sekta ya utalii barani Afrika hasa baada ya athari za mlipuko wa janga la Uviko 19.
Aidha alibainisha kuwa Uviko 19 umeathiri utalii wa kimataifa kwa wastani wa kati ya asilimia 50 hadi 85 katika nchi mbalimbali ikiwemo nchi yetu ya Tanzania .
Dkt.Chana alisema mkutano huo utakuwa chachu ya kukutana na wadau mbalimbali wakiwemo wataalam wa utalii na ukarimu katika ngazi ya kimataifa na kikanda,watoa huduma kwenye mnyororo wa utalii,wawekezaji pamoja na watu mashuhuri zaidi ya 150.
Alisema kuwa mbali na Rais Samia kufungua mkutano huo pia utahudhuriwa na Katibu mkuu wa shirika la UNWTO,Zurab Pololikashvili ambapo alibainisha kuwa pia patakuwepo na matukio mbalimbali kama jukwaa la uwekezaji kwa ajili ya kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo nchini itazinduliwa Investment Guideline(Tourism Doing Business) sambamba na Marketing Symposium kwa ajili ya kuwajengea uwezo wadau wa utalii kuhusu masuala ya masoko.
Alisema kutakuwepo na uzinduzi wa A tour ofa African Gastronomy pamoja na ziara za mafunzo(FAM Trips) ambapo watapata nafasi ya kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo Tanzania ikiwemo Hifadhi ya Ngorongoro,Jumuiya ya wanyama pori ya Buruge na city Tour ya vivutio mbalimbali katika jiji la kitalii la Arusha,"alisema.
Alibainisha kuwa kulingana na sera ya Taifa ya utalii ya mwaka 1999 mkutano huo ni muhimu kwa kuwa ni mojawapo ya jitihada za serikali katika kuongeza idadi ya watalii nchini pamoja na kutanua wigo wa mazao ya utalii nchini kupitia uendelezaji wa mazao ya utalii kimkakati hususani utalii wa mikutano.
Vilevile alisema kuwa mkutano huo utawezesha kujengea uwezo wataalam wao na wadau wa utalii katika kutangaza utalii,kuendeleza na kufungamanisha mazao ya utalii katika kanda mbalimbali za utalii nchini kulingana na shabaha yao ya kuongeza idadi ya watalii milioni tano na mapato ya dola za marekani bilioni sita ifikapo mwaka 2025.
Waziri Chana alisema Mkutano umebebwa na kauli mbiu isemayo Rebuilding Africa's Tourism Resilience for inclusive socio Economic Development huku aliongeza kuwa hii ni fursa adhimu ya kukuza uchumi wa jiji la Arusha ,mikoa ya jirani na Tanzania kwa ujumla hivyo anatoa rai kwa wananchi katika kuchangamkia fursa zitakazotokana na mkutano huo
UNAKUMBUKA STORI YA MKE ALIYEFARIKI AKIMFUKUZIA MMEWE AKIWA NA MCHEPUKO?? MMEWE NAYE KAFARIKI
NABII MKUU DKT. GEORDAVIE AWAPONGEZA WANARIADHA ZAIIDI YA 500 WALIOSHIRIKI NGURUMO YA UPAKO MATEMBEZI MARATHON
Na Woinde Shizza ARUSHA
Wanariadha zaidi ya 500 kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa wa Arusha wamefanikiwa kushiriki katika mbio za riadha zijulikanazo kama Ngurumo ya upako matembezi marathon.
Mbio hizo ambazo zimefanyika jijini Arusha juzi ambapo washindi wa mbio hizo wameweza kupatiwa zawadi mbalimbali kama fedha taslimu pamoja na medali
Akiongea mara baada ya kuhutimisha mbio hizo mratibu wa mbio hizo Mchungaji Daudi Mashimo alisema kuwa wanafanya marathoni hizo kwa upendo mkubwa sana
Mashimo alisema kuwa wanariadha wamekimbia kilomita 10 na walianzia katika maeno ya Gymkhana kuzunguka katikati ya Viunga vya jiji la Arusha na kuhitimisha Gymkhana.
Alisema kuwa mbio hizo ni msaada mkubwa sana kwa afya kwa kuwa riadha ni mojawapo ya mazoezi ambayo yanafanya mwili uweze kuwa imara.
"Pamoja na kuwa sisi tunahubirk injili bado tuna sehemu kubwa sana ya kuweza kuhimiza michezo kama huu ambapo michezo bado inatakiwa iweze kuendeleza kufanywa ,"alisema.
Katika hatua nyingine alisema kuwa kwa Sasa wanatarajia kufanya mbio nyingine katika mkoa wa Mbeya ambapo napo huenda wanariadha zaidi ya 500 wakashiriki katika marathoni hiyo ijulikanayo kama Ngurumo ya upako marathon.
Aliongeza kuwa washindi katika mchuano huo wa riadha watapata zawadi kama fedha taslimu,lakini hata medali lengo likiwa ni kuwafanya watu wawe pamoja na kuhimiza mazoezi.
Hata hivyo aliwataka viongozi wa dini kuhakikisha kuwa wanaoha mfano wa mbio hizo za Ngurumo ya upako marathon kwa kuaanda michezo pamoja na matamasha mbalimbali ya michezo.
Naye Nabii mkuu wa huduma ya Ngurumo ya upako GeorDavie aliwapongeza sana wanariadha ambao wameshiriki huku akiwapatia zawadi kama hamasa ya kuendelea kufanya vema zaidi.
"Nawapongeza sana sana wote ambao mmeweza kushiriki na ninawashika mkono washindi wote,Huku nikiwasisitiza kuwa michezo ni mizuri kwa afya ,"aliongeza.
Alimtaka mratibu wa mbio hizo kuendelea na hamasa ya kuandaa mbio hizo sehemu nyingine kwa ajili kuimarisha mwili.
Nao washiriki wa mbio hizo walisema kuwa wanamshukuru sana Nabii mkuu,kwa kuwapa zawadi za mshitukizo(surprise)ya kiasi Cha laki moja kwa kila mshindi,ni ishara nzuri na inawajengea njia na mbinu za kujiamini zaidi.
NYUKI WAVAMIA MKUTANO WA UCHAGUZI CCM ...WAJUMBE WAJERUHIWA
Chanzo: Mwananchi