Sunday, 2 October 2022

SERIKALI YAONYA UBADILISHAJI MATUMIZI YA ARDHI BILA SABABU ZA MSINGI

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza katika Kikao kazi kilichowaunganisha wakurugenzi wa Halmashauri na watalaam wa Sekta ya Ardhi nchini kilichofanyika jijini Dodoma Oktoba 1, 2022. Sehemu ya washiriki wa kikao kazi kilichowaunganisha wakurugenzi wa Halmashauri na watalaam wa Sekta ya Ardhi nchini kilichofanyika jijini Dodoma Oktoba 1, 2022. Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Allan Kijazi akizungumza katika kikao kazi kilichowaunganisha wakurugenzi wa Halmashauri na watalaam wa Sekta ya Ardhi nchini kilichofanyika jijini Dodoma Oktoba 1, 2022.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula (wa tatu waliokaa mbele ) na viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wakurugenzi wa halmashauri walioshiriki Kikao kazi kati ya wakurugenzi wa Halmashauri na watalaam wa Sekta ya Ardhi nchini kilichofanyika jijini Dodoma Oktoba 1, 2022.

****************************

Na Munir Shemweta, WANMM DODOMA

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Dkt Angeline Mabula amezionya halmashauri nchini kuacha utaratibu wa kubadilisha matumizi ya ardhi bila sababu za msingi.

Dkt Mabula alitoa onyo hilo Oktoba 1, 2022 jijini Dodoma wakati wa kuhitimisha kikao kazi kilichowaunganisha wakurugenzi wa Halmashauri na wataalamu wa sekta ya ardhi kilichofanyika jijini Dodoma.

" Sasa hivi kila mmoja anaondoa open space anataka kupima viwanja anafuta mashamba anataka kupima viwanja hata kama bado yako katika sura ya kijijini ya kimashamba na anataka kila sehemu kuwe fremu"

Akitolea mfano wa jiji la Dodoma, Dkt Mabula alisema, jiji hilo limeanza kusheni fremu wakati ni Makao makuu ya nchi na kusema haiwezekani kuwa na miji ya aina hiyo ambayo haipangwi kwenye sura ya makao makuu kwa kujaza fremu na vituo vya mafuta na kusisitiza kuwa hiyo si sahihi kitaaluma.

Kwa mujibu wa Waziri wa Ardhi, wapo wataalamu wengi katika sekta ya mipango miji na mabadiliko ya matumizi yasiyo na sababu za msingi hayakubaliki kwa kuwa yanawakosesa hata watoto maeneo ya kucheza sambamba na miji kupumua.

"Mipango iliyopangwa awali inatakiwa kubaki siyo kuendekeza mabadiliko ya matumizi kwa kujaza fremu au vituo vya mafuta na kuharibu miji, tunahitaji pia maeneo ya matumizi ya umma". Alisema Dkt Mabula

Kupitia kikao hicho kilichohudhuriwa pia na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Prof Riziki Shemdoe na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Tumushi wa Umma na Utawala Bora Laurean Ndumbaro, Dkt Mabula aliwataka Wakurugenzi ambao halmashauri zao tayari zina mipango kabambe kutoruhusu ujenzi kuendelea kwenye maeneo yao bila kuzingatia mipango hiyo na kusisitiza umuhimu wa maeneo kutunzwa kwa kuzingatia mipango kabambe badala ya kufuata mkumbo wa kutaka kubadili matumizi ya ardhi na kuharibu sura ya miji.

Kikao Kazi kati ya wakurugenzi wa halmashauri na wataalamu wa sekta ya ardhi kimefanyika kwa lengo la kupata maoni juu ya muundo mpya wa utendaji kazi wa wataalam wa ardhi katika ngazi ya Halmashauri.
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI OKTOBA 2,2022








Share:

Saturday, 1 October 2022

KARIBU BUILDING SOLUTION DESIGNING KWA HUDUMA ZA UCHORAJI RAMANI ZA NYUMBA

 


Share:

SAUTI PROGRAMU KUZALISHA MIFUGO BORA KWA MAHITAJI YA SOKO LA NDANI NA NJE YA NCHI


Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki (wa pili kushoto) akizungumza na vijana waliochaguliwa kujiunga kwenye vituo atamizi (hawapo pichani) wakati alipotembelea Chuo cha Mafunzo ya Mifugo (LITA) Kampasi ya Mabuki mkoani Mwanza ambapo amewaeleza vijana hao malengo na matarajio ya serikali ya kuanzisha vituo hivyo, hasa kwa kuhakikisha wanapata ujuzi na uzoefu wa kuweza kufuga mifugo kisasa na kibiashara.


Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo Tanzania (LITA), Dkt. Pius Mwambene (wa pili kulia) akitoa taarifa ya uendeshaji wa vituo atamizi katika Chuo cha Mafunzo ya Mifugo (LITA) Kampasi ya Mabuki na Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) - Mabuki mkoani Mwanza kwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki (wa tatu kutoka kulia) ambapo amesema tayari baadhi ya vijana wameshafika na wanaendelea na maandalizi.


Mkurugenzi wa Utafiti wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI), Dkt. Daniel Komwihangilo (wa pili kutoka kushoto) akiwasihi vijana waliochaguliwa kujiunga na vituo atamizi kuhakikisha wanafanya kazi za ufugaji kwa vitendo kwa bidii ili malengo yaliyokusudiwa na serikali dhidi yao yaweze kutimia.


Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya ufugaji mifugo kisasa na kibiashara wakimsikiliza Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki (hayupo pichani) wakati alipotembelea Chuo cha Mafunzo ya Mifugo (LITA) Kampasi ya Mabuki mkoani Mwanza kukagua kazi zinazoendelea kwa ajili ya uanzishaji vituo atamizi.


Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki (katikati waliokaa) akiwa kwenye picha na Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Mafunzo ya Mifugo (LITA), Dkt. Pius Mwambene (kulia waliokaa), Mkurugenzi wa Utafiti wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI), Dkt. Daniel Komwihangilo (kushoto waliokaa) pamoja na watumishi wa LITA na TALIRI Mabuki na vijana waliochaguliwa kujiunga kwenye vituo atamizi mara baada ya Waziri Ndaki kumaliza kuzungumza na vijana hao kwenye Kampasi ya Mabuki mkoani Mwanza.


Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki (wa nne kutoka kulia) akizungumza na Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Mafunzo ya Mifugo (LITA), Dkt. Pius Mwambene (wa pili kutoka kushoto) wakati alipofika kwenye Chuo cha Mafunzo ya Mifugo (LITA) Kampasi ya Mabuki Mkoani Mwanza kukagua kazi zinazoendelea kufanyika kwenye eneo litakalotumika kwa ajili ya vituo atamizi ambapo amewataka viongozi wa LITA kuhakikisha kazi hizo zinakamilika kwa wakati.

.....................................

Programu ya Samia Ufugaji kwa Tija inakwenda kumaliza changamoto ya upatikanaji wa mifugo bora inayohitajika kwa ajili ya soko la ndani na nje ya nchi.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki wakati anazungumza na vijana waliochaguliwa kujiunga na vituo atamizi kwa ajili ya kupata mafunzo ya ufugaji kwa vitengo katika Chuo cha Mafunzo ya Mifugo Kampasi ya Mabuki mkoani Mwanza ili waweze kufuga kisasa na kibiashara.

Waziri Ndaki amesema kuwa prograu hii kwanza imelenga kuwabadilisha vijana kifikra kwa kuwapatia mbinu mbalimbali za ufugaji wa kisasa na kibiashara ikiwa ni pamoja na kuwaonyesha fursa zilizopo kupitia Sekta ya Mifugo na namna ya kuzitumia kwa tija.

Programu hii imeanzishwa kwa maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan aliyoyatoa wakati wa kuhitimisha sherehe za Wakulima – Nanenane zilizohitimishwa mkoani Mbeya ambapo aliagiza Sekta ya Mifugo kuanzisha vituo kwa ajili ya kuwajengea uwezo vijana ili waweze kujiajiri kupitia ufugaji.

Waziri Ndaki amesema kuwa lengo la SAUTI Programu ni kuwawezesha vijana kuanzisha na kuendesha miradi ya ufugaji wa mifugo kibiashara, kuwapatia vijana stadi rahisi kwa vitendo za namna bora ya kuanzisha na kuwekeza katika miradi ya ufugaji wa mifugo, kuwawezesha vijana kupata ujuzi, uzoefu na ujasiri wa kuanzisha miradi ya ufugaji kibiashara, pia kuwaunganisha vijana kwenye mnyororo wa thamani wa uzalishaji wa mazao ya mifugo kibiashara.

Kutokana na malengo hayo, SAUTI Programu inakwenda kuongeza ajira kwa vijana kupitia Sekta ya Mifugo na hivyo kuifanya Sekta hiyo kuongeza kipato kwa wafugaji wenyewe lakini pia mchango wa Sekta kwenye pato la Taifa.

Hivyo amewataka vijana hao kutumia fursa hiyo vizuri kwa kuwa Wizara imeshawaandalia maeneo ambayo watapatiwa mara baada ya kukamilika kwa mafunzo hayo ili waweze kuanza kufuga kutokana na elimu watakayokuwa wameipata. Pia amewataka vijana ambao wamechaguliwa lakini hawajafika kufika, kwani wasipofanya hivyo watachukuliwa vijana wa akiba kuja kuziba nafasi zilizo wazi.

Aidha, Waziri Ndaki ameendelea kuwasihi viongozi wa mikoa na wilaya kuendelea kusimamia zoezi la uwekaji alama za utambuzi kwenye mifugo katika maeneo yao kwani serikali imeongeza mwezi mmoja ambapo baada ya Oktoba 30, 2022 hatua za kisheria zitaanza kuchukuliwa kwa wafugaji ambao mifugo yao haina alama za utambuzi.

Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo Tanzania (LITA), Dkt. Pius Mwambene amesema kuwa tayari umeshaandaliwa mwongozo utakaotumika kufuga kisasa ambao utawasaidia vijana kama rejea yao hasa pale kutakapokuwa na kitu kinachotaka kuwakwamisha.

Dkt. Mwambene amasema kuwa vijana hao wataanza kujifunza kwa vitendo kuanzia kwenye ujenzi wa mabanda, manunuzi ya chakula na ng’ombe na katika kufanya biashara ili shughuli zote wazielewe.

Mkurugenzi wa Utafiti wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI), Dkt. Daniel Komwihangilo akiwasihi vijana waliochaguliwa kujiunga na vituo atamizi kuhakikisha wanafanya kazi za ufugaji kwa vitendo kwa bidii ili malengo yaliyokusudiwa na serikali dhidi yao yaweze kutimia.

Akizungumza kwa niaba ya vijana hao, Adelina Bilembo amesema ameishukuru serikali kwa kuanzisha vituo hivyo vyenye lengo la kuwajengea kuwe wa ufugaji kwa vitendo na kuona vijana katika sekta ya mifugo wanahitaji kuwezeshwa. Naye Baraka Ezekiel ameahidi kuwa wataweka juhudi kubwa katika kujifunza ili malengo yaliyowekwa na serikali ya kuwajengea uwezo vijana kupitia ufugaji ifanikiwe na matunda yake yaonekane.
Share:

TAMISEMI NA WATAALAMU SEKTA YA ARDHI WATAKIWA KUJIPANGA KUTATUA CHANGAMOTO ZA ARDHI

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza katika Kikao kazi kilichowaunganisha wakurugenzi wa Halmashauri na watalaam wa Sekta ya Ardhi nchini kilichofanyika jijini Dodoma Oktoba 1, 2022. Kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Dkt Allan Kijazi na kushoto ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais –TAMISEMI Prof Riziki Shemdoe. Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Allan Kijazi akizungumza katika kikao kazi kilichowaunganisha wakurugenzi wa Halmashauri na watalaam wa Sekta ya Ardhi nchini kilichofanyika jijini Dodoma Oktoba 1, 2022. Wa pili kushoto ni Waziri wa Ardhi Dkt Angeline Mabula. Wa pili kulia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais –TAMISEMI Prof Riziki Shemdoe na kulia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Laurean Ndumbaro. Katibu Mkuu Ofisi ya Rais –TAMISEMI Prof Riziki Shemdoe akizungumza katika kikao kazi kilichowaunganisha wakurugenzi wa Halmashauri na watalaam wa Sekta ya Ardhi nchini kilichofanyika jijini Dodoma Oktoba 1, 2022. Kushoto ni Waziri wa Ardhi Dkt Angeline Mabula na kulia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Laurean Ndumbaro. Sehemu ya washiriki wa kikao kazi kilichowaunganisha wakurugenzi wa Halmashauri na watalaam wa Sekta ya Ardhi nchini kilichofanyika jijini Dodoma Oktoba 1, 2022. Baadhi ya Wakurugenzi wa Halamashauri wakiwa katika Kikao kazi kilichowaunganisha wakurugenzi wa Halmashauri na watalaam wa Sekta ya Ardhi nchini kilichofanyika jijini Dodoma Oktoba 1, 2022.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza katika Kikao kazi kilichowaunganisha wakurugenzi wa Halmashauri na watalaam wa Sekta ya Ardhi nchini kilichofanyika jijini Dodoma Oktoba 1, 2022. (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)

********************

Na Anthony Ishengoma na Munir Shemweta, WANMM DODOMA

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula amewataka wakurugenzi wa Halmashauri nchini kujipanga na kufanya kazi kwa pamoja na wataalamu wa ardhi ili kuondoa changamoto zinazojitokeza katika utendaji kazi na usimamizi wa sekta ya ardhi katika Halmashauri.

Dkt. Mabula alisema hayo leo Oktoba 1, 2022 wakati wa ufunguzi wa kikao kazi kilichowaunganisha wakurugenzi wa Halmashauri na watalaam wa Sekta ya Ardhi nchini kilichofanyika jijini Dodoma. Kikao hicho kimefanyika kwa lengo la kupata maoni juu ya muundo mpya wa utendaji kazi wa wataalam wa ardhi katika ngazi ya Halmashauri.

Dkt.Mabula alisema, zimeanza kujitokeza changamoto katika utendaji kazi kati ya watendaji wa sekta ya ardhi na wakurugenzi wa Halmashauri hasa katika eneo la usimamizi wa sekta hiyo baada ya kuanza utekelezaji wa rejesho la Waraka wa Utumishi Na 1 wa Mwaka 1998 kuhusu usimamizi wa watumishi wa sekta ya ardhi na maji kutokana na sababu mbalimbali.

Rejesho hilo pamoja na mambo mengine liliwahamisha wataalamu wa sekta ya ardhi kutoka kwenye usimamizi wa Mamlaka za serikali za mitaa Kiajira na kinidhamu na kuwa chini ya usimamizi wa Wizara ya Ardhi.

‘’Watumishi hawa kiajira na kinidhamu wako Wizara ya ardhi mamlaka za upangaji ardhi ziko Halmashauri lakini baadhi ya wakurugenzi wamekuwa wakijiweka mbali na wataalam ardhi na kushindwa kufuatilia utekelezaji wa sekta ya ardhi au kukosa ufahamu katika sekta ya ardhi.’’ Alisisitiza Dkt. Mabula

Kwa mujibu wa Dkt Mabula changamoto hiyo imeleta mkanganyiko kwa kuwa baadhi ya watendaji hasa wakurugenzi hawaoni kama wanawajibu wa kusimamia sekta ya ardhi wakati wao ni mamlaka za upangaji ardhi.

‘’Baadhi ya wakurugenzi hawajui taratibu za ardhi na kutojihusisha zaidi na uelewa wa masuala ya ardhi kwani unakuta Mkurugenzi wa Halmashauri ukimtaka hakupe taarifa anakimbilia kupata ufafanuzi kutoka kwa mtaalamu wa ardhi’’Aliongeza Dkt. Angeline Mabula.

Changamoto nyingine iliyoainishwa Dkt Mabula ni kitendo cha baadhi ya Wakurugenzi wa Halmashauri kushindwa kurejesha fedha za mkopo ya program ya Kupanga, Kupima na Kumilikisha ardhi na kutumia fedha hizo kwenye mipango mengine badala ya kurejesha fedha hizo ili ziweze kutumika katika maeneo mengine.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Allan Kijazi alieleza kupitia kikao hicho kuwa ipo haja ya kuboresha mawasiliano kati ya watendaji wa sekta ya radhi na mamlaka za serikali za mitaa ili kuweka mkakati mzuri wa utendaji kazi kwani wote ni watumishi wa Serikali.

Dr. Kijazi aliongeza kuwa, kumekuwa na changamoto ya kiutendaji kati ya serikali za mitaa na uongozi wa kisiasa ikiwemo madiwani na kusisitiza kuwa, la msingi ni kufanya kazi kwa pamoja kwa kuwa wote ni watendaji wa serikali.

‘’Lengo la kikao chetu ni namna ya kuboresha mawasiliano ili tuweze kujiweka sawa kuboresha utendaji kazi kwani kumekuwepo lugha zinazoleta sintofahamu kuwa baadhi ya wakurugenzi wa halmashauri wamekuwa wakitoa kauli kuwa watendaji wa sekta ya ardhi wako chini ya katibu Mkuu na wao hawahusiki’’. Alisema Dkt Kijazi

Madhumuni ya kikao kazi ni kujadili changamoto, kuibua changamoto zingine zinazojitokeza na kutoa maoni na ushauri kuhusu namna bora ya kusimamia watumishi wa sekta ya ardhi nchini kuwa na ufanisi na kwa maskahi mapana ya nchi.
Share:

SAMAF NA ITEL ZAUNGANA KURUDISHA TABASAMU KWA KITUO CHA WATOTO WENYE ULEMAVU CHA AMANI NA MIHAYO




Na Mwandishi wetu,Morogoro 

UMOJA wa waandishi wa habari wanawake Dar es Salaam chini ya asasi ya sauti ya matumaini Foundation SAMAF kwa kushirikiana na Kampuni ya Simu ya Itel  wametembelea Kituo cha kulelea watoto yatima wenye ulemavu na wanaoishi katika mazingira magumu cha Amani na Mihayo vilivyopo  kata ya Chamwino Mkoani  Morogoro na kutoa misaada mbalimbali ikiwemo taulo za kike pamoja na chakula kwa lengo la kurudisha  tabasamu kwa watoto hao.


Akizungumza wakati wa kutoa msaada huo,Mwanzilishi wa Umoja wa umoja huo,Penina Malundo alisema taasisi yao inaendelea kuhakikisha inarudisha tabasamu kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu na wale wenye ulemavu kwa kuwasaidia vitu mbalimbali ikiwemo kuwapa elimu ya Afya,Kujitambua pamoja na masuala ya ukatili wa kijinsia ili kuweza kuwasaidia katika makuzi yao.


Alisema mbali na elimu hiyo pia wamekuwa wakitoa taulo za kike kwa mabinti hao za kipindi cha miezi sita  ili ziweze kuwasaidia mabinti hao kuweza kupata hedhi salama ambayo itawafanya kutokuwa wanyonge kwa kuendelea na shughuli zao kama masomo.


"Hii sasa ni awamu ya tatu kwa mwezi huu wa tisa kutoa elimu ya afya ya uzazi,kujitambua na ukatili wa kijinsia tumeweza kufikia shule tatu ikiwemo shule ya msingi Buguruni Viziwi,Maweni,Kigamboni,Vijibweni na Kituo cha Amani na Mihayo mkoani Morogoro jumla ya mabinti 200 tumeweza kuwafikia na kampeni yetu ya ithamini na ilinde kesho yangu,"alisema na kuongeza


"Mkoani Morogoro tumeweza kushirikiana na Kampuni ya Simu ya Itel katika kufanikisha shughuli hii na wadau wengine  ikiwemo Shree Jalalam  katika kuwasaidia mahitaji mbalimbali na kuwarudisha katika furaha makundi hayo,"alisema.


Akitaja vitu walivyowakabidhi watoto hao ni pamoja na Mchele,Unga ,Mafuta ya Kula,Maharage,Taulo za Kike Sabuni ya Unga,Maji,Juice na Biscuits ambazo zimetolewa na wadau hao ikiwa na lengo la kuisaidia Samaf kufikia watoto waliokatika mazingira magumu.


Alisema Jamii inatakiwa kuendelea kuwatunza watoto hao na kuwaona nao wanahaki kama wengine ili kuweza kurudisha tabasamu kwao.


Kwa Upande wake Meneja uhusiano wa Kampuni ya Itel,Fernando Mfuole alisema kampuni yao ya Itel inaendesha kampeni ya kurudisha fadhira kwa jamii  katika kila kila faida wanayopata katika Shule mbalimbali au katika vituo vya watoto vya kulelea yatima,wanaoishi mazingira magumu au venye watoto wenye ulemavu.


"Tunafanya hivi katika mikoa yote  mahali popote nchini, tunarudisha fadhila kwa jamii hii ni kuhakikisha tunawasaidia watoto waliopo katika makundi haya leo tumeweza kutoa mahitaji mbalimbali yanayohitajika  ili kuweza kurudisha furaha za watoto hawa wa kituo cha Amani na Mihayo mkoani Morogoro,"alisema 


Alisema Itel imeweza kuguswa na kuhakikisha inawafikia katika kuwapatia kile kitu walichobarikiwa katika faida wanayoipata kwenye bidhaa zake.


Naye Msimamizi wa kituo Amani  ,Padri Beatus Msewando aliishukuru Kampuni ya Itel na Samaf kwa msaada huo na kuiomba jamii kujitokeza kusaidia kituo hicho kwani wanakabiliwa na Changamoto mbalimbali kutokana na wingi wa watoto wanaowapokea.


"Katika huduma zetu hizi tunaona wengine wanaletwa hawana ndugu wala pakukaa,kwahiyo tunawasaidia kuishi nao huku tukiwafundisha mambo mbalimbali kama kazi za mikono,ikiwemo kilimo na Uvuvi ili kuwapa nyenzo za kuja kujitegemea,"alisema.
Share:

MGODI WA BUCKREEF WASHIRIKI MAONESHO YA MADINI GEITA -2022


Afisa Usalama wa Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Dhahabu Buckreef Charles Kafuku (wa kwanza kushoto) akitoa maelezo kwa mgeni aliyetembelea Banda la Kampuni hiyo Bw. Roy Mwinga (wa pili kulia) aliyemuwakilisha Waziri wa Viwanda na Biashara wa Zambia katika Maonesho ya Madini yanayofanyika Mkoani Geita.
(PICHA ZOTE NA: HUGHES DUGILO) GEITA
Mwakilishi wa Waziri wa Viwanda na Biashara wa Zambia katika Maonesho ya Madini yanayofanyika Mkoani Geita Bw. Roy Mwinga (wa tatu kulia) akitia saini katika kitabu cha wageni katika Banda la Buckreef katika maonesho hayo.
Mjiolojia wa Kampuni ya Buckreef Francis Kiyumbi (wa pili kushoto) akionesha sampuli za aina ya miamba inayopatikana kwenye Mgodi wa Buckreef.
Watumishi wa Mgodi wa Buckreef wakiwa katika picha ya pamoja katika Banda lao katika Maonesho ya Teknolojia katika Sekta ya Madini yanayofanyika katika viwanja vya Bombambili Mkoani Geita. (kutoka kushoto) ni, Afisa Usalama wa Mgodi huo Charles Kafuku, Afisa Rasirimali watu wa Buckreef, Domitilla Mang'ondi, (anayefuata), Mjiolojia Francis Kiyumbi, na Mtaalamu wa masuala ya umeme Mgodini Nahom Mramba. Muonekano wa Banda la Buckreef katika Maonesho ya Madini Mkoani Geita.
Share:

Friday, 30 September 2022

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI OKTOBA 1,2022














Share:

UNISURE GROUP, PHOENIX OF TANZANIA (PART OF MUA) AND SMART APPLICATIONS INTERNATIONAL EXTEND THEIR STRATEGIC PARTNERSHIP INTO TANZANIA


Today marked another important milestone for the insurance industry as The Unisure Group, Phoenix of Tanzania Assurance Co. Ltd (PTAL), (Part of MUA) and Smart Applications International extended their official strategic partnership into Tanzania at a media launch in Dar es Salaam.

Industry leaders, regulators, key stakeholders and members of the media came together to learn more about how this partnership in East Africa and the Indian Ocean Islands, which was first launched in Nairobi, Kenya, in May, will help transform healthcare in the region.

“We are extremely proud to be adding the Tanzanian market to the existing partnership countries. Tanzania is a key market in terms of growth opportunities in medical insurance in particular,” said The Unisure Group’s Deputy Executive Chairman, Stephen Conway.

“This partnership is unique in that three independent organisations – one insurance company, an international administration and assistance provider, and a medical services facilitator – have agreed to partner on projects that will provide access to quality healthcare across multiple African countries in a fully regulated way.

We’re incredibly excited for the long-term collaborations and new business opportunities that lie ahead for our Umatter International Private Medical Insurance (IPMI) plans and look forward to adding additional countries to the four existing partnership countries.”

As The Unisure Group’s Head of IPMI, Daniel van der Merwe, explained, this partnership not only addresses the regulatory requirements that exist with cross-border insurance transactions, but it will bring quality medical insurance and service delivery to a larger number of members who previously would not have had access to this level of international cover.

PTAL’s CEO, Ashraf Musbally, echoed this commitment to greater access for all, and world-class service and customer care.

“This partnership greatly increases our operational footprint, and with this wider geographical scope, we can assure our clients’ seamless health insurance services globally,” he said. “At the end of the day, our top priority with the Umatter product is to ensure our clients receive personalised, world-class health insurance services across the globe.”

In partnering with Smart Applications International, The Unisure Group and PTAL members benefit from Smart’s biometric systems, resolving the challenge that many insurers have with regard to direct access to medical service providers, billing, and potential cases of fraud.

“Our goal has been to transform access to healthcare through the use of foolproof digital solutions and to increase medical insurance penetration,” said Grace Gathuri, Country Manager at Smart Applications International, Tanzania.

“For the last 18 years, Smart Applications Tanzania has been a leading pan-African technology player. With access to over 10 countries using our Biometric Smart system, we believe that our partnership with Unisure and Phoenix Assurance will catapult the provision of international private medical insurance coverage, both in Tanzania and throughout the region.”

The Unisure Group, MUA and Smart’s strategic partnership extends across East Africa and the Indian Ocean Islands. This includes Kenya, Tanzania, Mauritius, and the Seychelles, with Uganda and Rwanda following in the new year.


Share:

TBS YAONYA WAFANYABIASHARA WANAOKIUKA TARATIBU ZA UINGIZAJI WA BIDHAA ZA MABATI NCHINI

Kaimu Mkurugenzi Mkuu ( TBS), Bw. David Ndibalema akiongea na waandishi wa habari alipotembelea ghala la kampuni ya URHOME inayoagiza na kusambaza bidhaa za mabati kutoka nchini China. Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara kutoka Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Bw. Christopher Mramba akizungumza na waandishi wa habari leo alipotembelea ghala la kampuni ya URHOME inayoagiza na kusambaza bidhaa za mabati kutoka nchini China. Mkurugenzi wa Utekelezaji na Uzingatiaji wa Sheria TBS, Dkt. Candida Shirima akizungumza na waandishi wa habari alipotembelea ghala la kampuni ya URHOME inayoagiza na kusambaza bidhaa za mabati kutoka nchini China. Meneja wa uthibiti wa Shehena zinazoingia na kutoka nchini Mhandisi Saidi Mkwawa akizungumza na waandishi wa habari alipotembelea ghala la kampuni ya URHOME inayoagiza na kusambaza bidhaa za mabati kutoka nchini China. Mabati yaliyo chini ya kiwango mali ya Kampuni ya URHOME yaliyozuiwa na TBS kwa ajili ya uteketezaji, maeneo ya Sokota, wilayani Temeke, Dar es Salaam mapema leo.

***************************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

SHIRIKA la Viwango Tanzania limeiandikia barua kampuni ya uagizaji na usambazaji wa mabati nchini URHOME Company Limited kuhakikisha ndani ya siku tatu wamewapatia taarifa ya mabati 2176 kati 125280 yapo wapi baada ya kufanyiwa ukaguzi na kugundulika hayajakidhi viwango.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 30 Jijini Dar es Salaam, Meneja wa uthibiti wa Shehena zinazoingia na kutoka nchini Mhandisi Saidi Mkwawa amesema Kampuni hiyo baada ya kuingiza nchini mabati hayo, TBS ilichukua sampuli na kuzipeleka kwenye maabara ya Shirika ili kubaini kama zimeweza kukidhi viwango stahiki kwa mujibu wa sheria .

Aidha baada ya matokeo ya uchunguzi ilibainika kwamba mabati kutoka kampuni hiyo yameshindwa kukidhi viwango vya ubora vilivyotarajiwa, kama ilivyo taratibu za sheria, kulikuwa na njia mbili aidha kurudisha au kuteketeza na mteja alikubaliana na njia ya kuteketeza na zoezi la uteketezaji lilianza.

"Wakati tukiendelea kuteketeza ambapo mabati hayo awali yalikuwa 125280 tukaja tukabaini mabati 2176 hayapo na taratibu za kisheria zimeshaanza". Amesema

Pamoja na hayo Mhandisi Mkwawa amesema watahakikisha mabati yote yanapatikana na zoezi la uteketezaji litaendelea sambamba na mengine.

Nae Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Bw.David Ndibalema amewahimiza wafanyabiashara na waingizaji wabidhaa kutumia vizuri vibali vya masharti kwa kuhakikisha wanazingatia yale masharti ambayo yamewekwa wakati wa kutoa vibali hivyo.

masharti yenyewe ni kwamba kama mzigo bado upo chini ya uchunguzi mzigo huo hautakiwi usambazwe, kuuzwa au kutumiwa kwa njia yoyote ile na tutaendelea kuchukua hatua za kisheria kwa wale ambao wanakiuka akiwemo huyu ambaye ameingiza huu mzigo wa mabati ambayo yamegundulika yapo chini ya viwango

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara Wizara ya Uwekezaji,Viwanda na Biashara Bw.Christopher Mramba amesema wamesikitishwa na tukio hilo na kukemea ukiukwaji wa masharti ya vibali vinavyowekwa na serikali na kuzingatia sheria na kuendelea kujenga utamaduni wakuzingatia masharti ya ubora wa bidhaa na kamwe serikali haitaacha soko la Tanzania liwe dampo kuweka bidhaa zisizo na ubora.

"Tutaendelea kushirikiana na vyombo vya serikali kufuatilia bidhaa ambazo zimeingia sokoni kinyume na sheria na kuchukua hatua stahiki za kisheria na nitoe wito kwa wafanyabiashara wote nchini kuzingatia uaminifu na matumizi mazuri ya fursa zinazotolewa na serikali za kuweka mazingira wezeshi ya biashara ikiwemo hii fursa ya kutoa kibali cha masharti maalumu ya kutoa mzigo bandarini ili bandari yetu iendelee kuwa na ufanisi unaotakiwa na pasiwe na msongamano ili biashara nyingine ziwezee kufanyika". Amesema
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger