Monday, 26 September 2022

TMEA, TBS KUSHIRIKIANA KUKUZA BIASHARA YA TANZANIA KWENYE MASOKO YA KIMATAIFA

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango (TBS), Dkt.Athuman Ngenya pamoja na Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya TradeMark East Africa (TMEA) Bi.Monica Hangi wakisaini makubaliano ya ufadhili na Taasisi hiyo leo Septemba 26,2022 Jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango (TBS), Dkt.Athuman Ngenya pamoja na Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya TradeMark East Africa (TMEA) Bi.Monica Hangi wakisaini makubaliano ya ufadhili na Taasisi hiyo leo Septemba 26,2022 Jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango (TBS), Dkt.Athuman Ngenya pamoja na Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya TradeMark East Africa (TMEA) Bi.Monica Hangi wakisaini makubaliano ya ufadhili na Taasisi hiyo leo Septemba 26,2022 Jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango (TBS), Dkt.Athuman Ngenya akipeana pongezi na Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya TradeMark East Africa (TMEA) Bi.Monica Hangi mara baada ya kusaini makubaliano ya ufadhili na Taasisi hiyo leo Septemba 26,2022 Jijini Dar es Salaam.Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango (TBS), Dkt.Athuman Ngenya akizungumza katika hafla ya kusaini makubaliano ya ufadhili na Taasisi ya TradeMark East Africa (TMEA) leo Septemba 26,2022 Jijini Dar es Salaam.Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya TradeMark East Africa (TMEA) Bi.Monica Hangi akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya kusaini makubaliano ya ufadhili na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) leo Septemba 26,2022 Jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Upimaji na Ugezi (TBS), Mhandisi Johanes Maganga akifuatilia hafla ya utiaji saini wa makubaliano ya ufadhili na Taasisi ya TradeMark East Africa (TMEA) leo Septemba 26,2022 Jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Udhibiti Ubora (TBS), Bw.Lazaro Msasalaga akifuatilia hafla ya utiaji saini wa makubaliano ya ufadhili na Taasisi ya TradeMark East Africa (TMEA) leo Septemba 26,2022 Jijini Dar es Salaam.Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Dkt.Athuman Ngenya akiwa pamoja na Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya TradeMark East Africa (TMEA) Bi.Monica Hangi wakipata picha ya pamoja na watumishi wa TBS mara baada ya kusaini makubaliano ya ufadhili na Taasisi ya TradeMark East Africa (TMEA) leo Septemba 26,2022 Jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

*******************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Katika kuashiria ubia unaoendelea, Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na TradeMark East Africa (TMEA) leo wametia saini makubaliano ya ufadhili yenye thamani ya TZS 9 bilioni yenye lengo la kuimarisha mifumo inayoongoza maendeleo na utekelezaji wa viwango, mifumo ya usimamizi wa ubora. uwezo wa kupima maabara na ithibati.

Msaada huu unaoendelea kwa TBS unalenga kuongeza ufanisi katika jinsi viwango vinavyotengenezwa na kutekelezwa, na pia kuhakikisha kuwa viwango vilivyotengenezwa vinawezesha biashara.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Septembaa 26,2022 katika Ofisi za TBS, Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Dkt.Athuman Ngenya amesema msaada huo umekuwa muhimu kwa uchumi wa nchi sio tu kupitia otomatiki kwa shughuli zote za uendeshaji ambazo ziliimarisha ufanisi wa utoaji wa huduma kwa jumuiya ya wafanyabiashara lakini pia kwa kukuza upatanishi wa viwango vya kikanda.

"TBS inapenda kuishukuru TMEA kwa juhudi kubwa na msaada mkubwa unaotolewa ili kuongeza ufanisi katika usimamizi na utekelezaji wa viwango vyote viwili, vya hiari na vya lazima (Kanuni za Kiufundi), kwa lengo la kuwezesha biashara'. Amesema Dkt.Ngenya.

Aidha ameahidi kuendelea kutoa ushirikiano wa hali ya juu katika utekelezaji wa miradi inayokuja kwa manufaa ya maendeleo ya uchumi wa nchi.

"Miundombinu ya Viwango na Ubora ina jukumu kubwa kuelekea Kizazi cha Nne cha Viwanda. Kwa hiyo, kusaidia shughuli za Viwango na Ubora wa Miundombinu ni kusaidia hatua kuelekea Kizazi cha Nne cha Viwanda”. Amesema

Nae Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya TradeMark East Africa (TMEA) Bi.Monica Hangi amesema Juhudi hizi za kurahisisha biashara zimewekwa ili kukabiliana na changamoto hizo, sambamba na kupunguza vikwazo vya kibiashara na visivyo vya Ushuru nchini.

Amesema hatua za awali za Mifumo ya Kusaidia iliyolenga kukuza biashara kupitia uboreshaji wa Viwango na mifumo ya SPS nchini Tanzania inasalia kuwa kipaumbele cha TradeMark East Africa.

‘’Wafanyabiashara nchini Tanzania bado wanakabiliwa na changamoto katika kufuata Viwango na hatua za SPS, kwa kiasi kikubwa kutokana na uelewa mdogo na gharama kubwa za kufuata, zinazopunguza uwezo wao katika kutumia masoko ya kikanda na kimataifa kwa mauzo ya nje". Amesema

Pamoja na hayo amesema TBS imekuwa mmoja wa washirika wakuu ambao wameonyesha uwezo wa kutoa matokeo yanayoonekana katika miradi mbalimbali inayoungwa mkono na TMEA. Hivyo ametoa wito wa kuendelea kushirikiana katika kuhakikisha kuwa awamu hii ya mradi pia inaenda kuwa na mafanikio makubwa.
Share:

KIPINI CHA PUANI KILICHOPOTEA MIAKA MITANO CHAKUTWA KWENYE MAPAFU

Joey Lykins (35)

JAMAA huyo wa nchini Marekani kwa jina la Joey Lykins (35) alilala alipoamka akawa hakioni kipini chake cha pua. Alihangaika kukitafuta kwa udi na uvumba bila mafanikio lakini miaka mitano baadaye kimekuja kuonekana katika mapafu yake.


Alianza kukohoa mfululizo huku akipata maumivu makali nyuma ya mgongo ilibidi akimbizwe hospitali ambapo awali daktari alidhani labda ni dalili za pneumonia lakini baada ya kupigwa x-ray picha ikaonesha ana kipini hicho cha pua ambapo alipooneshwa na daktari na kuulizwa kama anakumbukumbu zozote kuhusu kitu kama hicho akashangaa.


Ndipo akakumbuka miaka mitano iliyopita alipopoteza kipini chake baada ya kuamka akawa hakioni licha ya kukitafuta huku na huko.


Kwa bahati kipini hicho hakikupasua mapafu yake na ameweza kufanyiwa sajari kukiondoa ambapo sasa yupo vizuri ingawa hata yeye haamini ilikuwajekuwaje kikaingia mapafuni.

Share:

TBS YAWATAKA WAWEKEZAJI NA WAFANYABIASHARA KUZINGATIA TARATIBU KUEPUKA VIKWAZO VYA KIBIASHARA


*************************

WAFANYABIASHARA wanaokuja kufanya biashara pamoja na kuwekeza nchini, wametakiwa kuzingatia taratibu zilizowekwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) ili kuepuka vikwazo vya kibiashara wanavyoweza kukumbana navyo.

Ushauri huo ulitolewa mwishoni mwa wiki na Afisa Masoko wa TBS, Deborah Haule, wakati akizungumza na washiriki waliotembelea banda la shirika hilo kwenye Maonesho ya Biashara ya Afrika Mashariki yaliyofanyika Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam kuanzia Septemba 22 hadi 24, mwaka huu.

Kwa upande wa wafanyabiashara wa biadhaa ambao walihudhuria maonesho hayo kutoka nchi za Afrika Mashariki, Haule alisema walielimishwa jinsi mashirika ya viwango ya nchi hizo yalivyo na makubaliano ya pamoja, ambapo mfanyabiashara kutoka nchi mojawapo anapopeleka bidhaa yake nchi nyingine ikiwa na alama ya ubora ya shirika la nchi husika, basi bidhaa yake haiwezi kupimwa tena kwa ajili ya kuithibitisha ubora.

Alisema mashirika ya viwango ya nchi hizo za Afrika Mashariki yaliingia makubaliano hayo ili kuwaondolea vikwazo vya kibiashara wafanyabiashara, hivyo ni muhimu kuhakikisha bidhaa zao zina alama ya ubora kutoka mashirika ya nchi husika.

''Hii imelenga kurahisisha ufanyaji biashara katika nchi za Afrika Mashariki,'' alisema Haule.

Kwa upande wa wafanyabiashara ambao wanafanya biashara kutoka nje ya nchi za Afrika Masharik, Haule alisema;

''Kwa wanaoleta bidhaa za chakula na vipodozi cha kwanza wanachotakiwa kufanya ni kusajili bidhaa zao za chakula au vipodozi kupitia tovuti ya TBS, ambapo wakishaingia kwenye mfumo, utawasaidia namna ya kujaza taarifa zao pamoja na kulipia gharama zinazotakiwa.

Baada ya hapo wataleta sampuli tutazipima,''alisema Haule na kuongeza; ''Wakishapatiwa huo usajili, hatua inayofuatia pale wanapoleta mzigo taratibu ambazo TBS tunafanya tuna huduma ambayo inaitwa Pre-Shipment Verification of Conformity (PVoC) ambapo kupitia utaratibu huo mteja anatakiwa akague bidhaa yake kule kwenye nchi ambako zinatoka.

Akikagua kule zinakotoka anapewa cheti kinachoitwa Certificate of Conformity (CoC) . Hiyo CoC ndiyo ataingia nayo nchini tutaihakiki ili kujua kama ni halisi, lakini pia tutakagua mzigo wake na baada ya hapo kama hautakuwa na shida yoyote ataruhusiwa kuuza mzigo wake nchini.''

Kwa upande wa mfanyabiashara ambaye atashindwa kuja na CoC, atatozwa faini ya asilimia 15 ya gharama za mzigo na baada ya hapo TBS itampimia mzigo (bidhaa)

''Bidhaa ikionekana ina shida itabidi airudishe nchi alikoitoa au ateketeze mzigo huo hapa nchini kwa gharama zake mwenyewe.''

Alifafanua kwamba kwa bidhaa nyingine za kawaida aambazo sio za chakula na vipodozi zitafuata taratibu za PVoC, lakini haina haja ya kuzisajili, kwa kuwa zinazosajiliwa ni za chakula na vipodozi.

Kuhusu wafanyabiashara waagizaji wa magari kutoka Japan, Haule alisema kwa sasa hivi shirika limebadilisha utaratibu mtu anatakiwa akague gari lake kutoka Japan, ambako shirika lina wakala wake wa ukaguzi wa magari.

''Kwa hiyo gari linatakiwa lije huku likiwa limeishakaguliwa kutoka Japan, mtu akija kutoka Japan hajakagua atatozwa faini na baadaye gari lake litakaguliwa hapa nchini.

Kwa wale wanaotoa magari nje ya Japan, Haule alisema magari yao yatakaguliwa hapa nchini kwa sababu bado kituo kwa ajili ya kazi hiyo, kipo.
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU SEPTEMBA 26,2022

Magazetini leo Jumatatu September 26 2022













Share:

Sunday, 25 September 2022

MKUTANO WA WADAU KUJADILI MAPITIO YA SERA YA ELIMU NA MITAALA KUFANYIKA KWA SIKU TATU JIJINI DODOMA.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia  Prof Adolf Mkenda.


Na Mathias Canal, WEST-Dodoma.

Serikali imeandaa mkutano maalumu kwa mara nyingine wa wadau wa elimu kutoka maeneo na sekta mbalimbali nchini kote nchini utakaofanyika Jijini hapa kwa lengo la kuboresha elimu nchini .


Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma leo tarehe 25 Septemba 2022 Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe Prof Adolf Mkenda amesema kuwa mkutano huo unatarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 26 hadi 28 Septemba 2022 Jijini Dodoma.


Waziri Mkenda ameeleza lengo la Mkutano huo kuwa ni kujadili Mapitio ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 na Mabadiliko ya Mitaa ya Elimu msingi. 


Amesema kuwa Majadiliano hayo yatatokana na hatua iliyofikiwa na mapitio hayo kupitia kamati maalumu zilizopewa majukumu hayo.


Waziri Mkenda amesema kuwa Mkutano  huo unajumuisha, Wahadhiri, Waajiri, Wadau wa Maendeleo, Taasisi za umma na Binafsi, Taasisi za Dini, Taasisi zinahusika na uendelezaji wa lugha, Wabunge, Wajumbe toka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Taasisi zisizo za Kiserikali, Jumuiya za kitaaluma, na Taasisi za Sayansi na Utafiti.


Katika hatua nyingine, Waziri Prof Mkenda amesema kuwa tarehe 27 Septemba, 2022 serikali itatangaza rasmi majina ya wanafunzi waliopata ufadhili wa SAMIA SCHOLARSHIPS”. 


"Mtakumbuka Wizara yetu ilitoa ahadi kupitia hotuba ya bajeti ya kuanzisha programu mpya ya kutoa ufadhili wa masomo ya elimu ya juu kwa wahitimu bora wa kidato cha sita katika masomo ya sayansi. Hivyo mpaka sasa tuna majina karibu 600 ya wanafunzi ambao wamechaguliwa" Amekaririwa Waziri Mkenda


Kadhalika, Waziri Mkenda ameukumbusha umma kuwa serikali imezindua tuzo za waandishi bunifu zijulikanazo kama Tuzo za Mwalimu Nyerere, hivyo ameendelea kukaribisha Waandishi Bunifu wa Riwaya na Mashairi kuwasilisha maandiko yao ili kuwania tuzo hizo. 


Prof Mkenda amesema kuwa Mwisho wa kupokea Mawasilisho hayo ni  Novemba 30, 2022 ambapo kwa taarifa zaidi kuhusu tuzo hizo na maulizo wanaweza kufuatilia katika akaunti maalumu za mitandao ya kijamii za  tuzo Nyerere au mitandao na tovuti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Taasisi ya Elimu Tanzania-TET kwa anuani ya tuzonyerere@tie.go.tz




Share:

HESLB NA TAASISI 11 ZINAZOTOA MIKOPO ELIMU YA JUU AFRIKA ZAKUTANA KUJADILI UFANISI


**************************

Na Mwandishi Wetu,

Cape Town, Afrika Kusini

25 Septemba, 2022

Taasisi 11 zinazotoa mikopo ya elimu ya juu barani Afrika zinatarajia kuanza mkutano wao wa kimataifa wa siku nne utakaoanza kesho Jumatatu Septemba 25, 2022, Cape Town, Afrika Kusini ambapo Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) ni miongoni mwa taasisi zinazoshiriki mkutano huo unaojadili uzoefu uliopatikana kutokana na janga la ugonjwa wa UVIKO 19.

Akizungumza moja kwa moja kutoka Cape Town, Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Abdul-Razaq Badru amesema mkutano huo umeandaliwa na nchi wanachama 11 ambazo ni Shirikisho la Taasisi za kiserikali zinazotoa Mikopo ya Elimu ya Juu Afrika (AAHEFA) na jumla ya washiriki 150 wakiwemo wakuu wa nchi, wajumbe wa bodi na maafisa waandamizi kutoka nchi wanachama wanatarajia kushiriki mkutano huo.

“Mara ya mwisho tulikutana mwaka 2019, Lusaka Zambia…… yapo masuala mengi yanayojitokeza baada ya mlipuko wa ugonjwa wa UVIKO 19 ambao ulizuia mikutano ya ana kwa ana. Tukiwa kama nchi mwanachama, tumefika katika mkutano huu kwa ajili ya kujifunza kutoka kwa wenzetu na kupata uzoefu wa namna tunavyoweza kusimamia mikopo katika taasisi za elimu ya juu”, Mkurugenzi Badru na kuongeza:

“Kama nchi, ushiriki wetu katika mkutano huu umedhihirisha umuhimu wa kuimarisha utendaji wetu hususani matumizi ya teknolojia. Kwa mwaka huu msafara wetu unaongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Carolyne Nombo na Mwenyekiti wa Bodi, Prof. Hamisi Dihenga” amesema Badru.

Kwa upande wake, Rais wa AAHEFA ambaye pia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Kenya (HELB), Charles Ringera akizungumza kutoka Cape Town amesema mkutano huo wa tatu wa AAHEFA utakuwa na kauli mbiu isemayo: Uendelevu wa Mikopo ya wanafunzi na taasisi za mikopo ya Elimu ya Juu – Je kuna fursa zipi baada ya ugonjwa wa UVIKO 19?

Ringera amesema mkutano huo unatarajiwa kufunguliwa na Waziri wa Elimu ya Juu, Sayansi na Ubunifu wa Afrika Kusini Dkt. Blade Nzimande na utakuwa na jumla ya mada 10 na kutakuwa na maazimio mwisho wa mkutano.

“Kesho tutakuwa na mada kutoka kwa wenzetu wa NSFAS taasisi ya mikopo ya elimu ya Afrika Kusini ikizungumzia kuhusu Sera ya elimu ya juu na itawasilishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Elimu ya Juu na Mafunzo wa NSFAS, Dkt. Nkosinathi Sishi na mada nyingine itawasilishwa na Mwenyekiti wa Mfuko wa Vyuo Vikuu vya Kenya Prof. Karuti Kanyinga”, amesema Ringera.

AAHEFA ni Shirikisho lilioanzishwa mwaka 2008 na Taasisi za Serikali zinazosimamia mikopo ya Elimu ya Juu Barani Afrika lililoanzishwa mahsusi kwa ajili ya kubadilishana ujuzi na uzoefu wa masuala ya usimamizi wa mikopo ya elimu ya juu. Nchi wanachama wa AAHEFA ni Afrika Kusini, Tanzania, Malawi, Botswana, Ghana, Kenya na Lesotho. Nchi nyingine ni Rwanda, Namibia, Uganda na Zambia.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger