Sunday, 25 September 2022

DKT MPANGO ATAKA VIONGOZI WA DINI KUFUNDISHA MAADILI MEMA KWA VIJANA

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Dkt Angeline Mabula akizungumza katika Jubilee ya miaka 25 ya Kanisa Katoliki Parokia ya Bikira Maria Mpalizwa Mbinguni Kibiti na sherehe za kutaburuku kanisa na Altare iliyofanyika Kibiti mkoani Pwani ambapo alimuwakilisha Makamu wa Rais Dkt Phillip Mpango tarehe 25 Septemba 2022.Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Angeline Mabula akimsalimia Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam Jude Thaddaeus Ruwa’ichi wakati wa Jubilee ya miaka 25 ya Kanisa Katoliki Parokia ya Bikira Maria Mpalizwa Mbinguni Kibiti na sherehe za kutaburuku kanisa na Altare iliyofanyika Kibiti mkoani Pwani ambapo alimuwakilisha Makamu wa Rais Dkt Phillip Mpango tarehe 25 Septemba 2022.Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akivishwa Skafu na Skauti wakati wa Jubilee ya miaka 25 ya Kanisa Katoliki Parokia ya Bikira Maria Mpalizwa Mbinguni Kibiti na sherehe za kutaburuku kanisa na Altare iliyofanyika Kibiti mkoani Pwani ambapo alimuwakilisha Makamu wa Rais Dkt Phillip Mpango tarehe 25 Septemba 2022.Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Angeline Mabula akimkabidhi Risiti ya Benki ikiwa ni Mchango wa Makamu wa Rais Dkt Phillip Mpango alioutoa kwa ajili ya maendeleo ya ujenzi wa Kanisa Katoliki Parokia ya Bikira Maria Mpalizwa Mbinguni Kibiti kwa Pande Christian Lupindu tarehe 25 Septemba 2022.

Sehemu ya washiriki katika Jubilee ya miaka 25 ya Kanisa Katoliki Parokia ya Bikira Maria Mpalizwa Mbinguni Kibiti na sherehe za kutaburuku kanisa na Altare iliyofanyika Kibiti mkoani Pwani tarehe 25 Septemba 2022.


Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam Jude Thaddaeus Ruwa’ichi katika ibada ya kutabaruku Kanisa Katoliki Parokia ya Bikira Maria Mpalizwa Mbinguni Kibiti iliyofanyika Kibiti mkoani Pwani tarehe 25 Septemba 2022. Kulia ni Padre wa Kanisa hilo Christian Goya Lupindu.(PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)

***********************

Na Munir Shemweta WANMM KIBITI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Phillip Mpango amewataka viongozi wa dini nchini kuwafundisha na kulea vijana katika maadili mema pamoja na kuthamini kufanya kazi kihalali.

Dkt Mpango alisema hayo tarehe 25 Septemba 2022 katika hotuba yake iliyosomwa kwa niaba na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula katika Jubilee ya miaka 25 ya Kanisa Katoliki Parokia ya Bikira Maria Mpalizwa Mbinguni Kibiti na sherehe za kutaburuku kanisa na Altare iliyofanyika Kibiti mkoani Pwani.

Alisema, katika nyakati hizi ni ukweli ulio wazi kuwa kuna mmomonyoko wa maadili katoka jamii, vitendo viovu na mambo yasiyompendeza mungu kuzidi kuongezeka mambo aliyoyaeleza kuwa siku za nyuma yalikuwa nadra sana kutokea au kusikika na hivi sasa yanakuwa habari za kila siku na wakati mwingine huonekani ni kawaida.

Kwa mujibu wa Dkt Mpango, kushuka kwa maadili ni jambo lenye athari mbaya kwa jamii na taifa kwa ujumla hivyo kunachangia kurudisha nyuma juhudi za kujiletea maendeleo nchini na kufanya kazi ya kuondoa umasikini kuwa ngumu.

Kupitia hotuba ya Makamu wa Rais, Dkt Mabula alisema, anaamini watu pamoja na viongozi wa serikali na wa vyama vya siasa wakishika mafundisho ya dini pamoja na kuwa na hofu ya mungu maovu mengi yatapungua na nchi kuongozwa vizuri.

Kufuatia hali hiyo, aliomba kwa niaba ya serikali viongozi wa dini wasaidie kulea taifa kimaadili na kuweka mkazo zaidi kwa vijana kwa kuwa wao ni wahanga wakuu wa maovu yanayotendeka na pia ni viongozi wa kesho.

"Tukiwaandaa vyema vijana wetu mustakabali wa taifa letu na watu wake utakuwa kwenye mikono salama na tukishindwa leo tutalia na kusaga meno kesho, uhai wa taifa letu utakuwa mashakani " alisema Dkt Mpango.

Kupitia hotuba hiyo Dkt Mpango pia alisisitiza suala la usafi na utunzaji mazingira ambapo aliwaomba viongozi wa kanisa katoliki na madhehebu mengine ya dini kupaza sauti kuhamasisha , ulinzi na uhifadhi wa mazingira katika nchi.

" Katika dini zetu Mwenyezi Mungu alitupatia dunia nzuri na akatuamuru tuitunze, niwaombe ninyi mlio mawakala wa mwenyezi mungu hapa duniani muwaongoze waumini na kuwahimiza kuitunza ekolojia ya nchi yetu nzuri kwa kutunza misitu na vyanzo vya maji , kupanda miti na kufanya usafi wa mazingira wakati wote" alisema Dkt Mpamgo.

Kuhusu mimba na ndoa za utotoni, Dkt Mpango aliwaomba viongozi wa dini kukemea mimba na ndoa za utotoni kwa kuwa ni kinyume cha sheria na maadili ambapo alieleza kuwa suala hilo linawanyima fursa watoto wa kike kusoma na kufikia malengo sambamba na kusababisha matatizo ya fistula kwa watoto wa kike na kusisitiza watoto wa kike waachwe wasome ili waweze kufikisha malengo yao.

Kwa upande wake Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam Jude Thaddaeus Ruwa’ichi aliwapongeza wana Kibiti kwa kuwa na kanisa lililokamilika na kuwashukuru wote walioshirikiana katika ujenzi wa kanisa hilo.

Alisema, ujenzi wa kanisa hilo umechukua muda wa miaka 11 na kueleza kuwa, muda huo umekuwa muda wa kukomaa na kuwataka wana kibiti kuonesha ukamavu na kumpongeza Padri wa Kanisa Katoliki Parokia ya Bikira Maria Mpalizwa Mbinguni Kibiti Christian Goya Lupindu kwa kujituma.
Share:

KAMATI YA TAIFA YA UONGOZI YA TASAF YATAKIWA KUZITEMBELEA KAYA MASIKINI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Taifa ya Uongozi ya TASAF pamoja na watendaji wa TASAF, wakati wa uzinduzi wa kamati hiyo uliofanyika jijini Dodoma.

Wajumbe wa Kamati ya Taifa ya Uongozi ya TASAF na baadhi ya watendaji wa TASAF wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao wakati wa uzinduzi wa kamati hiyo uliofanyika jijini Dodoma.


Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Uongozi ya TASAF, Bw. Peter Ilomo akizungumza kabla ya kumkaribisha Mhe. Jenista Mhagama kuzungumza na wajumbe wa kamati na watendaji wa TASAF wakati wa uzinduzi wa kamati hiyo uliofanyika jijini Dodoma.


Mwenyekiti aliyemaliza muda wake kuiongoza Kamati ya Taifa ya Uongozi ya TASAF, Dkt. Moses Kusiluka akitoa neno la shukrani kwa Mhe. Jenista Mhagama na watendaji wa TASAF, wakati wa hafla ya uzinduzi wa kamati mpya iliyoteuliwa hivi karibuni iliyofanyika jijini Dodoma.


Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Bw. Ladislaus Mwamanga akitoa taarifa ya utekelezaji na majukumu ya taasisi yake kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kamati ya Taifa ya Uongozi ya TASAF uliofanyika jijini Dodoma.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akimkabidhi tuzo Mwenyekiti aliyemaliza muda wake kuiongoza Kamati ya Taifa ya Uongozi ya TASAF, Dkt. Moses Kusiluka ya kutambua mchango aliotuoa wakati wa uongozi wake. Wakwanza kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Bw. Ladislaus Mwamanga.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akisikiliza taarifa ya utekelezaji wa mjaukumu ya TASAF, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kamati ya Taifa ya Uongozi ya TASAF iliyofanyika jijini Dodoma.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Taifa ya Uongozi ya TASAF, mara baada ya kuizindua kamati hiyo jijini Dodoma.

************************

Na. Veronica E. Mwafisi-Dodoma

Tarehe 25 Septemba, 2022

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama ameitaka Kamati ya Taifa ya Uongozi ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kuwa na utamaduni wa kuwatembelea walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini, unaoratibiwa na TASAF ili kubaini na kuzitafutia ufumbuzi changamoto zinazoweza kukwamisha utekelezaji wa mpango huo ambao Serikali inautekeleza kwa lengo la kuboresha maisha ya kaya maskini nchini.

Mhe. Jenista ametoa maelekezo hayo jijini Dodoma, wakati akizindua Kamati ya Taifa ya Uongozi ya TASAF iliyoteuliwa hivi karibuni mara baada ya kamati iliyopita kumaliza muda wake kiutendaji.

Waziri Jenista amewahimiza wajumbe wa kamati hiyo, kuhakikisha wanakwenda kuzungumza na viongozi, waratibu na walengwa katika maeneo yote ambayo Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unatekelezwa, ili kufikia lengo la Serikali la kuzikwamua kaya maskini kutoka katika lindi la umaskini.

“Mhe. Mwenyekiti na wajumbe wa kamati hii, tembeleeni maeneo ambayo mpango wa TASAF unatekelezwa ili mjiridhishe namna ambavyo unawafikia walengwa na kuwanufaisha,” Mhe. Jenista amesisitiza.

Mhe. Jenista ameongeza kuwa, wajumbe wa kamati wakitembelea maeneo ambayo mpango wa TASAF unatekelezwa, watapata fursa ya kujionea namna walengwa walivyonufaika, ikiwa ni pamoja na kutatua changamoto ambazo walengwa hao wa TASAF wanakabiliana nazo.

Akizungumzia azma ya Serikali ya Awamu ya Sita ya kuzikwamua kaya maskini, Mhe. Jenista amesema kuwa Serikali chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan haitomuacha mtu nyuma katika kufikia malengo ya maendeleo kama yalivyoainishwa katika dira ya maendeleo (Vision 2025), na ndio maana imejipanga vema katika kuhakikisha inaboresha maisha ya kaya zote maskini kwenye vijiji, mitaa na shehia.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Bw. Peter Ilomo amemhakikishia, Mhe. Jenista kuwa yeye pamoja na kamati yake watayafanyia kazi maelekezo yote ambayo ameyatoa ili kutimiza lengo la serikali la kuboresha maisha ya kaya maskini.

Naye, Mwenyekiti aliyemaliza muda wake, Dkt. Moses Kusiluka amesema, ataendelea kushirikiana na TASAF ili kuhakikisha inatimiza lengo lake la kuboresha maisha ya wananchi ambao wanaishi katika familia zenye hali duni kiuchumi.

Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya taasisi yake, Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Bw. Ladislaus Mwamanga amesema, TASAF imekuwa na mafanikio makubwa katika kuboresha maisha ya kaya maskini ikiwa ni pamoja na kujenga rasilimaliwatu ya kutosha kwa kuwawezesha kielimu wanafunzi wanaotoka kwenye kaya maskini kutoka hatua moja kwenda nyingine.

“Mwaka jana, TASAF kwa kushirikiana na bodi ya mikopo tumewawezesha wanafunzi 1200 kujiunga na elimu ya juu katika vyuo vikuu mbalimbali nchini, na mwaka huu mchakato bado unaendelea lakini tunatarajia kuwawezesha wengi zaidi kwani walioomba wako zaidi ya 3000,” Bw. Mwamanga amefafanua.

Kamati ya Taifa ya Uongozi ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kwa sasa inaundwa na Mwenyekiti Bw. Peter Ilomo, pamoja na wajumbe wengine ambao ni Balozi Zuhura Bundala, Bw. Richard Shilamba, Dkt. Charles Mwamwaja, Dkt. Ruth Lugwisha, Dkt. Naftali Ng’ondi, Bw. Ali Salim Matta, Mhandisi Rogatus Mativila na Dkt. Grace Magembe.


Share:

BONDIA MTANZANIA TWAHA KIDUKU ASHINDA UBINGWA UBO INTERCONTINENTAL



BONDIA Mtanzania Twaha Kiduku ameshinda ubingwa wa UBO Intercontinental baada ya kumtwanga mpinzani wake Abdo Khaled, raia wa Misri, katika pambano la raundi 10 lilifanyika mkoani Mtwara.


Twaha Kiduku ameshinda kwa pointi za majaji wote watatu na kuendelea kuwa na mikanda yote miwili ya UBO waliokuwa wakiipigania.
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI SEPTEMBA 25,2022

Magazetini leo Jumapili September 25,20222








Share:

Saturday, 24 September 2022

WANAFUNZI WANNE WATEKETEA KWA MOTO MWADUI SHINYANGA


Watoto wanne wa familia moja, wamefariki dunia baada ya nyumba walimokuwa wamelala kuteketea kwa moto.

Tukio hilo limetokea majira ya saa 6:30 usiku wa kuamkia leo Jumamosi Septemba 24,2022 katika makazi ya watu yaliyopo ndani ya eneo la mgodi wa Mwadui,wilayani Kishapu mkoani Shinyanga.

Watoto waliopoteza maisha kutokana na tukio hilo, ni Cecilia Richard mwenye umri wa miaka 14, aliyekuwa akisoma darasa la saba katika shule ya msingi Mwadui (C) Clarence Richard mwenye umri wa miaka 6, aliyekuwa akisoma darasa la kwanza katika shule ya msingi Mwadui (A) Thadeo Richard mwenye umri wa miaka 3 na Aisha Ashraf mwenye umri wa miaka 6 aliyekuwa akisoma darasa la kwanza katika shule ya msingi Mwadui (C).

Chanzo cha moto huo kinatajwa kuwa ni dawa ya mbu waliyokuwa wamewasha watoto hao, muda mfupi kabla ya kulala.

Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Shiyanga Jackson Mwakagonda, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Chanzo - Radio Faraja fm

Share:

WATUHUMIWA 15 WADAKWA MAUAJI YA WAFUGAJI TUNDURU


Mifugo iliyokamatwa na kikosi maalum cha Jeshi la Polisi

JESHI la Polisi kupitia kikosi cha kupambana na kuzuia wizi wa mifugo Nchini limesema linawashikilia watuhumiwa 15 waliohusika katika tukio la mauaji ya wafugaji katika kijiji cha Mbatamila Wilaya ya Tunduru Mkoa wa Ruvuma.


Hayo yamesemwa leo Septemba 24 2022 na Kamanda wa Polisi kikosi cha kuzuia wizi wa mifugo na migogoro ya wakulima na wafugaji nchini Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP SIMON PASUA alipofika Kijiji cha Mbatamila wilaya Tunduru Mkoa wa Ruvuma ambapo amebainisha kuwa Jeshi hilo linawashikilia watuhumiwa kumi na tano (15) kwa kosa la mauaji ya vijana wanne wa familia moja katika Kijiji cha mbatamila nakusema kuwa wale wote waliofanya mauaji hayo hawako salama nakuwataka wajisalimishe Jeshi la Polisi.


Aidha amewataka wakulima na wafugaji kutojichukulia sheria mkononi na badala yake wafuate misingi ya sheria na taratibu katika kutatua Changamoto zilizopo.

Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Simon Pasua akiongea na Wananchi wa Tunduru-Ruvuma

Sambamba na hilo amewapa Pole wananchi waliopoteza ndugu zao ambapo kamanda Pasua amesema Jeshi hilo linaendelea kuwatafuta watuhumiwa wote walio baki ili wafikiahwe katika vyombo sheria kujibu tuhuma zinazowakabili.



Pia kamanda Pasua amesema kuwa Jeshi hilo limefanikiwa kukamata mifugo 159 iliyokuwa imeibiwa katika Kijiji cha Mbatamila Wilaya ya Tunduru Mkoa wa Ruvuma ambapo amesema Jeshi hilo linaendelea kushrikiana na wafugaji na wakulima katika kupambana nauhalifu wowote ule.
Kwa upande wake katibu wa chama cha wafugaji Nchini Bi. Prisca Kaponda amesema wao kama chama cha wafugaji kitaendelea kutoa elimu kwa wafugaji juu ya matumizi bora ya ardhi ili kumaliza migogoro ya wakuliama nawafugaji hapa nchini.



Nao baadhi ya wahanga wa tukio hilo wamelishukuru Jeshi la Polisi kwa jitihada walizo chukua za kuwakamata watuhumiwa wa matukio ya mauaji na kukamata mifugo ilikuwa imeibiwa katika Kijiji cha mbatamila Wilaya ya Tunduru Mkoa wa Ruvuma na kuliomba Jeshi hilo kuweka nguvu kubwa ili kupata mifugo ambayo haijapatikana.

Share:

SEKTA BINAFSI ZAKARIBISHWA KUWEKEZA KWENYE KILIMO CHA MAUA MKOANI NJOMBE

Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 24,2022 kuelekea uzinduzi wa mkakati wa utangazaji wa Utalii katika mikoa ya Kusini ambao utafanyika Septemba 26,2022 mkoani Njombe.  Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe.Anthony Mtaka akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 24,2022 kuelekea uzinduzi wa mkakati wa utangazaji wa Utalii katika mikoa ya Kusini ambao utafanyika Septemba 26,2022 mkoani NjombeKaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB),Bw.Felix John akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 24,2022 kuelekea uzinduzi wa mkakati wa utangazaji wa Utalii katika mikoa ya Kusini ambao utafanyika Septemba 26,2022 mkoani Njombe

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

***************************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

BODI ya Utalii Tanzania (TTB) imepanga kuzindua mkakati wa utangazaji wa Utalii katika mikoa ya Kusini kwani kumekuwa na vivutio vingi ikiwemo hifadhi ya Taifa ya Kitulo ambayo nimaalufu duniani kwa maua.

Jambo hilo linatarajia kufanyika Septemba 26,2022 ambapo wataanza Septemba 25 kwa maonesho katika ukumbi wa Njombe Mji na siku ya tarehe 26 watayahitimisha kwa uzinduzi wa mkakati wa utangazaji wa utalii.

Ameyasema hayo leo Septemba 23,2022 Jijini Dar es Salaam,Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB),Bw.Felix John wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelekea uzinduzi wa mkakati wa utangazaji wa Utalii katika mikoa ya Kusini ambao utafanyika Septemba 26,2022 mkoani Njombe

Amesema mkakati huo ni sehemu ya utekelezaji wa malengo mahususi ya Tanzania the Royal Tour ambalo lakwanza lilikuwa ni kutangaza vivutio vyakipekee vya utalii wa nchi yetu na kuvutia wawekezaji kuwekeza katika sekta mbalimbali za uchumi wa nchi yetu.

"Njombe kuna fursa kama ilivyo maeneo mengine ya nchi na ndo maana tumeamua sasa kuffanya huu uzinduzi kule Njombe na sio Kusini mwa Tanzania kama ilivyozoeleka". Amesema Bw.Felix.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe.Anthony Mtaka amesema mkoa huo utafanya kazi kwa ukaribu na TTB na kuwaomba waweze kuwaambiia wananchi kuwa Njombe inazo fursa nyingi kwenye eneo la utalii kama vile hiffadhi ya kitulo ambayo ni maarufu na maalumu kwa maua ambayo hayapatikana kwa wingi katika ameneo mengine duniani.

Aidha amewakaribisha watanzania ambao watatakiwa kuwekeza katika sekta ya Utalii kwenye mkoa huo kwenye mahoteli au kuwekeza kenye kilimo cha maua ya kibiashara.

"Niwakaribisha sekta binafsi ambao watahitaji kufanya kilimo cha maua kama ambavyo kilimo hiki cha maua yakibiashara inafanyika Moshi na Arusha, niwakaribishe Njombe fursa hiyo ipo". Amesema Mhe.Mtaka

Share:

WAHAMIAJI 34 WAFARIKI KWENYE MAJI BAADA YA BOTI KUZAMA


Boti ikiwa imebeba wahamiaji haramu

***
TAKRIBANI watu 34 wamefariki dunia baada ya boti iliyobeba wahamiaji haramu kuzama karibu na Syria huku ikiwa bado haijajulikana siku ambayo boti hiyo ilizama.


Taarifa hiyo imetolewa Septemba 22, 2022 na Shirika la Habari la Serikali la nchi hiyo na kueleza kuwa boti hiyo ilitoka na wahamiaji hao nchini Lebanon, Palestina na ilipokaribia na Syria ikazima.

Kwa upande wa Shirika la haki za binadamu la Syria linalofuatilia vita nchini humo limeripoti kwamba takribani wahamiaji 36 wakifariki dunia katika Bahari ya Mediterania baada ya boti hiyo iliyowabeba wahamiaji haramu iliyokuwa ikielekea Ulaya kuzama.
Wahamiaji haramu wengi wamekuwa wakifariki kila mwaka kutokana na kuzama ndani ya maji katika bahati ya Mediterania

Tukio jingine lilitokea nchini humo ni la zaidi ya watu 1800 kupoteza maisha yao wakati wakijaribu kuvuka bahari hiyo kwa ajili ya kwenda barani ulaya.


Matukio kama haya yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara nchini humo ambapo mwaka 2013 wahamiaji haramu 254 waliokuwa wakitoka Syria kwenda Misri waliokolewa baada ya kuzama kwenye maji.
Wahamiaji wengi haramu wamekuwa wakiokolewa katika bahari ya Mediterania

Maelfu ya wahamiaji haramu wameripotiwa kuhama barani Afrika na pia Mashariki ya Kati na kuhamia barani Ulaya kila mwaka.


Wahamiaji wengi wanatumia mashua ndogo na kufunga safari ya kuelekea Bara la Ulaya kwa kupitia bahari ya Mediterania.


Imeandaliwa na Sanifa Khalifa kwa msaada wa mtandao
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI SEPTEMBA 24,2022




















Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger