Monday, 19 September 2022
Sunday, 18 September 2022
WAANDAAJI WA MAUDHUI YA NDANI WACHAGIZWA KUCHANGAMKIA FURSA ZA TEHAMA KUZALISHA MAUDHUI BORA YA NDANI
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Moses Nnauye (Mb.) akiongoza kikao na Kamati ya Maudhui ya TCRA muda mfupi baada ya kufungua Warsha ya Waandaaji na Watayarishaji wa Maudhui iliyofanyika kwa siku mbili jijini Dar es salaam, ikiratibiwa na TCRA. Picha na: TCRABENKI CRDB YAFANYA TAMASHA MAALUM LA KUTOA ELIMU YA BIMA YA VYOMBO VYA MOTO 'KUWA MSHUA’

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Godwin Gondwe (kulia) akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Maendeleo ya Biashara wa Kampuni ya Bima ya Sanlam, Ernest Selestine (watatu kushoto) wakati akitembelea mabanda katika tamasha la kutoa elimu ya bima kwa vyombo vya moto lililoandaliwa na Benki ya CRDB na kufanyika kwenye viwanja vya Posta, Kijitonyama jijini Dar es salaam. Tamasha hilo liliwaleta pamoja wadau mbalimbali wa vyombo vya moto kama Kampuni za Bima, Mamlaka ya Usimamizi wa Bima (TIRA), Msuluhishi wa Migogoro ya Bima, Jeshi la Polisi, gereji pamoja na maduka ya vifaa mbalimbali za vyombo hivyo. Katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Bima Benki ya CRDB, Moureen Majaliwa.
RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI ...MHANDISI KHATIB APELEKWA TCRA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi kama ifuatavyo:
- Amemteua Bw. Sosthenes Laurent Kewe kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Maendeleo ya Tanzania (TIB). Bw. Kewe ni Mshauri Binafsi wa Uendelezaji wa Sekta Binafsi za Fedha, Dar es Salaam.
2.Amemteua Mhandisi Othman Sharif Khatib kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA). Bw Khatib anachukua nafasi ya Dkt. Jones Kilembe ambaye uteuzi wake umetenguliwa. Bw. Khatib ni Mhandisi Mstaafu (TCRA).
3.Amemteua Dkt. David Nkanda Manyanza kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI). Dkt. Manyanza ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Development Solution Consultancy (T) Limited.
4.Amemteua Bi. Hawa Abdulrahman Ghasia kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Shirika la Masoko Kariakoo. Bi Ghasia ni Mbunge mstaafu.
5.Amemteua Bw. Sylvester Jospeh Kainda kuwa Msajili wa Mahakama ya Rufani. Bw. Kainda ni Naibu Msajili wa Mahakama Kuu, Kanda ya Morogoro.
Uteuzi huu unaanza mara moja.
SIMBA SC YAENDELEZA UBABE KIMATAIFA, YAICHAPA NYASA BIG BULLETS 2-0
SERIKALI YAIPONGEZA BARRICK KWA KUTEKELEZA SERA YA USHIRIKISHAJI WANANCHI KATIKA MNYORORO WA SEKTA YA MADINI (LOCAL CONTENT) KWA VITENDO

Saturday, 17 September 2022
TBS YASHIRIKI VIWANGO SPORTS BONANZA
Watumishi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) wakicheza drafti katika Bonanza la Michezo kwa wafanyakazi wa Shirika hilo lililofanyika leo Septemba 17,2022 katika viwanja vya Chuo cha Ardhi Jijini Dar es Salaam.
Watumishi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) wakicheza bao katika Bonanza la Michezo kwa wafanyakazi wa Shirika hilo lililofanyika leo Septemba 17,2022 katika viwanja vya Chuo cha Ardhi Jijini Dar es Salaam.
Watumishi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) wakicheza mpira wa miguu katika Bonanza la Michezo kwa wafanyakazi wa Shirika hilo lililofanyika leo Septemba 17,2022 katika viwanja vya Chuo cha Ardhi Jijini Dar es Salaam.
Watumishi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) wakicheza Volley ball katika Bonanza la Michezo kwa wafanyakazi wa Shirika hilo lililofanyika leo Septemba 17,2022 katika viwanja vya Chuo cha Ardhi Jijini Dar es Salaam.
Watumishi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) wakicheza mpira wa pete katika Bonanza la Michezo kwa wafanyakazi wa Shirika hilo lililofanyika leo Septemba 17,2022 katika viwanja vya Chuo cha Ardhi Jijini Dar es Salaam.
Watumishi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) wakicheza mchezo wa kuvuta kamba katika Bonanza la Michezo kwa wafanyakazi wa Shirika hilo lililofanyika leo Septemba 17,2022 katika viwanja vya Chuo cha Ardhi Jijini Dar es Salaam.









































