Monday, 1 August 2022

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE AGOSTI 2,2022













Share:

WASIOJULIKANA WAMUUA MUUZA DUKA BAADA YA KUNUNUA PIPI NA SODA SHINYANGA

Picha haihusiani na habari hapa chini

Mwanamke aliyetambulika kwa jina la Kabula Ngasa mwenye umri wa miaka 60, mkazi wa kijiji cha Nyida Kata ya Nyida katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga , ameuawa na watu wasiojulikana kwa kukatwa panga sehemu mbalimbali za mwili wake.

Mwenyekiti wa kijiji cha Nyida Kidoto Maganga ameiambia Redio Faraja kuwa, tukio hilo limetokea majira ya saa tatu usiku wa kuamkia leo Jumatatu Agosti 1,2022, wakati Marehemu akiwa nyumbani kwake katika kijiji hicho.

Taarifa zaidi zinabainisha kuwa, watu waliofanya mauaji hayo walikuwa ni wawili ambao walifika nyumbani kwa Marehemu mapema na kujifanya wateja katika kibanda chake cha bidhaa ndogo ndogo kilichopo hatua chache kutoka kwenye nyumba yake ambapo mwanzoni waliagiza Pipi na baadaye Soda na kuhudumiwa.

Baada ya dakika chache kupita walimtuma mjukuu wake anayesoma darasa la nne aliyekuwa naye kibandani kuwafuatia maji ya kunywa ndani, ambapo baada ya kurudi na maji walimpiga kwa ubapa wa panga hali iliyosababisha aanguke chini.

Alipoamka alikimbia kwa Mama yake ambaye anaishi jirani na kumweleza kinachoendelea, lakini inaelezwa kuwa Mama wa mtoto huyo aliogopa kutoka nje kwa vile Mume wake hakuwepo na hivyo watu hao wakatumia mwanya huo kumshambulia marehemu kwa Panga sehemu mbalimbali za mwili wake mpaka alipofariki dunia.

Diwani wa kata ya Nyida Selemani Seregeti , amethibitisha kutokea kwa mauaji hayo huku kamanda wa Polisi wa mkoa wa Shinyanga George Kyando akibanisha kuwa,bado hajapata taarifa za tukio hilo kwa sababu yuko nje ya ofisi kikazi.

CHANZO - RADIO FARAJA BLOG

Share:

NYUKI WAVAMIA SHULE, WAJERUHI WALIMU NA WANAFUNZI


Picha haihusiani na habari hapa chini

KUNDI la nyuki ambalo halikujulikana limetokea wapi limezua taharuki baada ya kuvamia Shule ya Msingi ya Kamena Wilaya ya Liwale mkoani Lindi na kujeruhi walimu na wanafunzi.

Taarifa kutoka wilayani humo na kuthibitishwa na mmoja wa walimu wa shule hiyo, Rehema Mwaitenda, zinaeleza tukio hilo lilitokea saa nane mchana, Julai 26, mwaka huu.

Mwaitenda alisema siku ya tukio, yeye na walimu wenzake wakiwa wanaendelea na majukumu yao ya kikazi, kundi hilo la nyuki lilivamia shuleni hapo na kuwashambulia walimu na wanafunzi.


Alisema katika uvamizi huo, wanafunzi wanane pamoja na walimu wawili walikimbizwa Hospitali ya Wilaya mjini Liwale na kupatiwa matibabu baada ya kung’atwa na nyuki hao.

Chanzo - Nipashe
Share:

MWENGE WA UHURU WAMULIKA MRADI WA MAJI NYAMILANGANO UNAOTEKELEZWA NA RUWASA KAHAMA


Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Sahili Nyanzabara Geraruma, akikata Utepe kwenye Mradi wa Majisafi na salama wa Nyamilangano Halmashauri ya Ushetu ambao unatekelezwa na RUWASA.

Na Marco Maduhu, USHETU

KIONGOZI wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Sahili Nyanzabara Geraruma, ameweka jiwe la Msingi katika Mradi wa Majisafi na salama Katika kijji cha Ididi Kata ya Nyamilangano Ushetu wilayani Kahama ambao utaondoa adha ya ukosefu wa maji kwa wananchi.



Mradi huo wa Maji umewekewa Jiwe hilo la Msingi Julai 31,2022 na Mwenge wa Uhuru, huku wananchi wakionyesha furaha ya kupata mradi huo wa Majisafi na salama, ambao unatekelezwa na Wakala wa Majisafi na usafi wa Mazingira vijijini (RUWASA) wenye thamani ya Sh.milioni 350.

Akizugumza wakati wa uwekaji wa jiwe hilo la Msingi Kiongozi huyo wa Mwenge wa Uhuru Kitaifa Sahili Nyanzabara Geraruma, amesema mradi huo wa Maji una manufaa makubwa kwa wananchi, kuwaondolea adha ya ukosefu wa Maji na kuagiza ukamilishwe kwa wakati.

"Mradi huu wa maji ni mzuri tumeukagua ila naagiza ukamilishwe kwa wakati, ili wananchi wapate huduma ya Maji haraka na kutekeleza dhamira ya Rais wetu Samia Suluhu Hassan ya kumtua ndoo kichwani Mwanamke," amesema Geraruma.

Naye Meneja Wakala wa Majisafi na usafi wa Mazingira RUWASA wilayani Kahama Magili Maduhu, amesema mradi huo wa Maji ni wa Kisima kirefu na utekelezaji wake kwa sasa ni asilimia 85 na unatarajiwa kukamilika mwaka huu na utanufaisha wananchi 5,296.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Ushetu Emmanuel Cherehani, amesema mradi huo wa maji ni mkombozi mkubwa kwa wananchi wa wananchi wa Nyamilangano na vijiji jirani na kuwataka wananchi wautunze mradi huo.

Pia amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan katika mwaka wa fedha (2022-2023) ametoa kiasi cha fedha Sh.bilioni 1.8 kwa ajili ya kukamilisha miradi yote ya Maji ambayo ipo Halmashauri ya Ushetu.

Nao baadhi ya wananchi wa Nyamilangano akiwamo Sophia Boniphace ,wameishukuru Serikali kwa kutekeleza mradi huo wa Majisafi na salama ambao umewaondolea changamoto pia ya Mgogoro ya kifamilia sababu ya kufuata Maji umbali mrefu.

Aidha, Mwenge huo wa Uhuru leo umekabidhiwa mkoani Tabora.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Sahili Nyanzabara Geraruma akizungumza wakati akiweka jiwe la Msingi kwenye Mradi wa Maji wa Nyamilangano Halmashauri ya Ushetu ambao umetekelezwa na RUWASA.
Mbunge wa Jimbo la Ushetu Emmanuel Cherehani akizungumza kwenye mradi huo wa Maji.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Festo Kiswaga, akizungumza kwenye mradi huo wa Maji.
Meneja wa RUWASA wilayani Kahama Mhandisi Magili Maduhu, akitoa taarifa ya utekelezaji wa Mradi huo wa Maji.
Meneja wa RUWASA Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Juliety Payovela, akitetea jambo na mmoja wa wakimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Sahili Nyanzabara Geraruma, akiweka jiwe la Msingi kwenye Mradi wa Maji wa Nyamilangano Halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama ambao unatekelezwa na RUWASA.
Tenki la kuhifadhia Maji kwenye Mradi wa Maji wa Nyamilangano Halmshauri ya Ushetu.

Mwenge wa Uhuru ukiwa kwenye Mradi wa Maji wa Nyamilangano Halmashauri ya Ushetu.

Share:

MAFURIKO YAUA WATU 10

Watu kumi wamepoteza maisha nchini Uganda kufuatia mafuriko makubwa mashariki kwa taifa hilo la ukanda wa Afrika Mashariki, shirika la Msalaba Mwekundu lilisema Jumapili.

Mvua kubwa ilisababisha mito kufurika na maji kusambaa hadi katika maboma ya watu na barabara huku Red Cross ikielezea uwezekano wa idadi ya maafa kuongezeka.

 Waliofariki ni waathiriwa wa mvua kubwa iliyohushudiwa usiku wa Jumamosi katika wilaya za Kapchorwa na Mbale. Video zinaonyesha wakaazi waliojawa na hofu wakikimbilia usalama wao huku viwango vya maji vikiongezeka katika kijiji kimoja na kuangusha nyumba na migomba ya ndizi.

Kwa mujibu wa kamishna wa Mbale Ahamada Waashaki, mwanajeshi ni mmoja wa watu waliongamizwa na mafuriko hayo. 

"Watu wengi hawajulikani waliko na wanahofiwa kuaga dunia. Kuna uharibifu mkubwa. Barabara zimezibwa, nyumba kumezwa kwa sababu ya mvua kubwa iliyoanza usiku wa jana (Jumamosi) hadi asubuhi hii (Jumapili)," Ahamada Waashaki aliambia shirika la habari la AFP.

 Waziri Mkuu Robinah Nabbanja alitembelea Mbale, eneo ambalo linapatikana takriban kilomita 300 mashariki mwa jiji kuu la Kampala.

 "Polisi na wanajeshi wa majini watafika kusaidia katika uokoaji na kutafta miili ya walioaga dunia tunapotoa msaada kwa wale walioathirika," ofisi ya waziri mkuu ilisema. 

AFP inaripoti kuwa wanahabari wawili waliiambia kuwa waliona miili ikielea katika maji hayo yaliyojaa matope kabla ya kuopolewa na polisi. Magari kadhaa pia yalisombwa pamoja na vitu vya nyumbani wakaazi wakikimbilia maeneo ya juu kwa usalama wao.
Share:

MFUNGWA ATOROKA POLISI UCHI AKIOGA

Polisi jijini Nairobi wanamsaka mfungwa mwenye umri wa miaka 19, ambaye alitoroka katika Kituo cha Polisi cha Viwandani.

Katika kisa hicho cha Jumatano, Julai 27, Erickson Khata aliomba ruhusa ya kuoga na afisa aliyekuwa kwenye zamu alimsindikiza kuchota maji na kuoga.

Hata hivyo, Khata alitumia fursa hiyo kutoroka baada ya afisa aliyekuwa amemsimamia kujinafasi ili kumpa faragha. DCI inasema kuwa mfungwa huyo alitoroka akiwa amevalia suruali ya ndani pekee yake, na kuacha nyuma nguo zake zote.

"Afisa huyo alishuku kuwa kila kitu kilikuwa si sawa baada ya mtungi wa maji ya kumwagika kusimama ghafla, na kufuatiwa na kimya cha kishindo. Alipokwenda kuangalia, alikumbana na beseni la maji yaliyopakwa nusu, kipande cha sabuni na nguo za mfungwa, bila mfungwa kuonekana,” wapelelezi walieleza.

Khata alikuwa amezuiliwa katika gereza la mgao wa ulinzi wa juu jijini Nairobi baada ya kulalamika kuwa yeye ni mtoto mdogo.

Ni hadi alipopelekwa katika Hospitali ya Mbagathi, mnamo Julai 26, ambapo vipimo vilifanywa na kuthibitishwa umri wake ulikuwa wa miaka 19. 

Kesi hiyo ilitakiwa kutajwa mahakamani siku aliyotoweka bila kujulikana aliko.
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU AGOSTI 1,2022

Magazetini leo Jumatatu August 1 2022





















Share:

HAULE AONGEZA JOTO LA UCHAGUZI JUMUIYA YA WAZAZI

Share:

Sunday, 31 July 2022

UTEUZI: RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI WA MKUU WA MKOA WA MARA

 


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger