Tuesday, 22 March 2022

Picha : DC MKUDE AKAGUA UJENZI WA MIRADI YA MAJI KISHAPU KILELE WIKI YA MAJI...ATAKA RUWASA IONGEZE KASI, WANANCHI WATUMIE MAJI SAFI NA SALAMA


Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude (kushoto) akizungumza katika eneo panapojengwa mnara wa tanki na tanki ya kuhifadhia maji kwenye Mradi ya maji ya bomba katika kijiji cha Bupigi – Butungwa.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude amewataka wananchi kutunza vyanzo vya maji, kutunza miundombinu ya maji pamoja na kutumia maji safi na salama kwani serikali imetumia gharama kubwa kuwafikishia huduma ya maji.

Mkude ameyasema hay oleo Jumanne Machi 22,2022 wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Maji ambayo katika Wilaya ya Kishapu yamefanyika katika Kijiji cha Bubiki kata ya Bubiki.

“Tunapoadhimisha wiki ya maji ni vyema tukakumbushana sheria, taratibu na kanuni zinazosimamia masuala ya maji kama vile kutofanya shughuli za kibinadamu ndani ya mita 60 kutoka katika chanzo cha maji,kutokuharibu mazingira kwa kukata miti hovyo na kuchoma moto misitu,kutunza miundo mbinu ya maji tukitambua kuwa serikali inatumia gharama kubwa kufikisha huduma ya maji kwa wananchi”,amesema Mkude.

“Kauli mbiu ya Wiki ya Maji mwaka huu ni ‘Maji chini ya ardhi hazina isiyoonekana kwa maendeleo endelevu’,hii ina maana kubwa sana kwamba kutunza,kuhifadhi na kulinda vyanzo vya maji yakiwemo yanayopatikana chini ya ardhi, kutunza uoto wa asili na kupanda miti rafiki na vyanzo vya maji”, ameeleza Mkude.

Mkuu huyo wa wilaya amesema Serikali inaendelea na jitihada za kufikisha maji katika maeneo ya vijijini ambako kuna asilimia 80 ya wakazi kwa kufanya tafiti ya vyanzo vya maji na kujenga miundombinu hivyo kutoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano kwa wataalamu wa maji wanapofika kwenye maeneo yao ikiwa ni pamoja na kulinda vifaa na rasilimali zinazoletwa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi.

“Serikali inaendelea na jitihada kuhakikisha huduma ya maji safi na salama inapatikana Mijini na Vijijini ambapo RUWASA Kishapu kwa sasa inawafikia wananchi kwa asilimia 56.5 kutoka 42.3% mwaka 2015”,amesema Mkude.

Mkude ametumia fursa hiyo kuipongeza RUWASA kwa kuendelea kutekeleza vizuri miradi ya maji huku akiwataka Wakandarasi kuongeza kasi ya kutekeleza miradi ya maji inayoendelea kujengwa ukiwemo wa kata ya Bubiki katika vijiji vya Mwamishoni na Nyasamba, Miradi ya maji Bubiki Bupigi – Butungwa.

Kwa upande wake Kaimu Meneja wa RUWASA wilaya ya Kishapu , John Lugembe amesema wanatekeleza ujenzi wa miradi ya maji katika maeneo mbalimbali ikiwemo kata ya Bubiki katika vijiji vya Mwamishoni na Nyasamba, Miradi ya maji Bubiki Bupigi – Butungwa, Miradi ya maji Igaga – Isagala hadi Lagana na michakato inaendelea kwa ofisi ya RUWASA kuainisha maeneo mengi zaidi ili kufikia lengo la wananchi vijijini kupata maji safi na salama.

Amesema lengo la miradi hiyo ya maji ni kutoa huduma ya maji safi na salama kwa wananchi ili kuboresha hali ya maisha na kuongeza upatikanaji wa maji safi na salama pamoja na kumtua mama ndoo kichwani kwa kumpunguzia umbali wa kwenda kutafuta mmaji na badala yake kumuongezea muda wa kufanya shughuli zingine za maendeleo ili kujiimarisha kiuchumi na kijamii.

Akitoa taarifa ya hali ya huduma ya maji vijijini na utekelezaji wa miradi ya maji, Afisa Maendeleo ya Jamii RUWASA Kishapu, Winfrida Emmanuel amesema katika kuhakikisha wananchi wa wilaya ya Kishapu wanapata huduma ya maji safi na salama na yenye kutosheleza katika maeneo ya vijijini na Miji Midogo ya wilaya, wamejikita katika ukarabati wa visima na miradi ya maji yenye kuleta matokeo ya haraka kuongeza upatikanaji wa maji.

“Ujenzi/upanuzi/ukarabati/uboreshaji wa miradi ya maji kwa sasa unatekelezwa kupitia fedha za Programu ya PV4, PbR, NWF na UVIKO – 19 ambapo utekelezaji wake unafanywa na Wakandarasi wajenzi na Watalaamu wa RUWASA”,amesema Emmanuel.

Amesema katika wilaya ya Kishapu kuna jumla ya miradi ya maji ya bomba 19, bwawa moja, visima vifupi 158, visima virefu 13 na matenki ya kuvuna maji ya mvua 173 iliyokwisha kamilika na inahudumia vijijin 69 kati ya vijiji 125 vilivyopo katika wilaya ya Kishapu inayokadiriwa kuwa na wakazi 350,503 (Projection 2021).

Diwani wa kata ya Bubiki Mhe. James Kasomi pamoja na wakazi wa Bubiki wameishukuru serikali kwa kuwapatia huduma ya maji safi na salama kwani hapo awali walikuwa wanatumia muda mwingi kufuata huduma ya maji kwenye mabwawa.

Kabla ya kuzungumza na wakazi wa kata ya Bubiki katika mkutano wa hadhara, Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude ametembelea na kukagua ujenzi wa Miradi ya maji ya bomba katika kijiji cha Bupigi – Butungwa na kata ya Bubiki katika vijiji vya Mwamishoni na Nyasamba na kujionea kazi ya kufyatua tofali,kujenga minara ya matanki na matanki ya kuhifadhia maji ikiendelea chini ya usimamizi wa RUWASA.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude (kushoto) akikagua ubora wa matofali leo Jumanne Machi 22,2022  kwenye Mradi wa maji ya bomba katika kijiji cha Bupigi – Butungwa ambapo kazi ya kufyatua tofali,kujenga mnara wa tanki na tanki ya kuhifadhia maji inaendelea kutekelezwa na Mkandarasi Bent Company Limited chini ya usimamizi wa RUWASA wilaya ya Kishapu. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kaimu Meneja wa RUWASA wilaya ya Kishapu , John Lugembe ( wa pili kulia) akimwelezea Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude kuhusu ujenzi wa Mradi wa maji ya bomba katika kijiji cha Bupigi – Butungwa kata ya Bupigi wilayani Kishapu.
 Fundi akitoa tofali ndani ya maji baada ya kuwekwa siku 7 kwa ajili ya ujenzi wa Mradi wa maji ya bomba katika kijiji cha Bupigi – Butungwa kata ya Bupigi wilayani Kishapu.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude (kushoto) akizungumza katika eneo panapojengwa mnara wa tanki na tanki ya kuhifadhia maji kwenye Mradi wa maji ya bomba katika kijiji cha Bupigi – Butungwa 
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude (kushoto) akizungumza katika eneo panapojengwa mnara wa tanki na tanki ya kuhifadhia maji kwenye Mradi ya maji ya bomba katika kijiji cha Bupigi – Butungwa 
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude (kushoto) akizungumza katika eneo panapojengwa mnara wa tanki na tanki ya kuhifadhia maji kwenye Mradi wa maji ya bomba katika kijiji cha Bupigi – Butungwa.
Kaimu Meneja wa RUWASA wilaya ya Kishapu , John Lugembe ( kushoto) akimwelezea Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude (kulia) kuhusu ujenzi wa Mradi wa maji ya bomba wa kata ya Bubiki katika vijiji vya Mwamishoni na Nyasamba ambapo kazi ya kufyatua tofali,kujenga mnara wa tanki na tanki ya kuhifadhia maji unaendelea chini ya usimamizi wa RUWASA.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude (katikati) akizungumza katika eneo ambapo matofali kwa ajili ya Mradi wa maji ya bomba wa kata ya Bubiki katika vijiji vya Mwamishoni na Nyasamba  yanafyatuliwa.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude (kushoto mwenye suti ya bluu) akizungumza katika eneo ambapo ujenzi wa mnara wa tanki na tanki la kuhifadhia maji kwenye Mradi wa maji ya bomba wa kata ya Bubiki katika vijiji vya Mwamishoni na Nyasamba  unaendelea.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude (kushoto mwenye suti ya bluu) akizungumza katika eneo ambapo ujenzi wa mnara wa tanki na tanki la kuhifadhia maji kwenye Mradi wa maji ya bomba wa kata ya Bubiki katika vijiji vya Mwamishoni na Nyasamba  unaendelea.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude (kulia) akifungua bomba la maji katika moja ya magati ya mradi wa maji uliopo katika kijiji cha Bubiki kata ya Bubiki wilayani Kishapu.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude (kulia) akimtua kichwani ndoo ya maji mmoja  wa wanawake katika kijiji cha Bubiki kata ya Bubiki wilayani Kishapu.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude (kulia) akimtua kichwani ndoo ya maji mmoja  wa wanawake katika kijiji cha Bubiki kata ya Bubiki wilayani Kishapu.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude akizungumza kwenye Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Maji ambayo katika Wilaya ya Kishapu yamefanyika leo Jumanne Machi 22,2022 katika Kijiji cha Bubiki kata ya Bubiki.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude akizungumza kwenye Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Maji ambayo katika Wilaya ya Kishapu yamefanyika katika Kijiji cha Bubiki kata ya Bubiki.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude akizungumza kwenye Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Maji ambayo katika Wilaya ya Kishapu yamefanyika katika Kijiji cha Bubiki kata ya Bubiki.
Wakazi wa Bubiki wakimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude kwenye Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Maji ambayo katika Wilaya ya Kishapu yamefanyika katika Kijiji cha Bubiki kata ya Bubiki.
Katibu Tawala Wilaya ya Kishapu Mhe. Shadrack Kengese akizungumza kwenye Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Maji ambayo katika Wilaya ya Kishapu yamefanyika katika Kijiji cha Bubiki kata ya Bubiki.
Afisa Maendeleo ya Jamii RUWASA wilaya ya Kishapu, Neema Mwaifuge akizungumza kwenye Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Maji ambayo katika Wilaya ya Kishapu yamefanyika katika Kijiji cha Bubiki kata ya Bubiki.
 Afisa Maendeleo ya Jamii RUWASA Kishapu, Winfrida Emmanuel akisoma taarifa ya hali ya huduma ya maji vijijini na utekelezaji wa miradi ya maji kwenye Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Maji ambayo katika Wilaya ya Kishapu yamefanyika katika Kijiji cha Bubiki kata ya Bubiki. Kushoto ni Afisa Maendeleo ya Jamii RUWASA wilaya ya Kishapu, Neema Mwaifuge
 Afisa Maendeleo ya Jamii RUWASA Kishapu, Winfrida Emmanuel akisoma taarifa ya hali ya huduma ya maji vijijini na utekelezaji wa miradi ya maji kwenye Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Maji ambayo katika Wilaya ya Kishapu yamefanyika katika Kijiji cha Bubiki kata ya Bubiki. Kushoto ni Afisa Maendeleo ya Jamii RUWASA wilaya ya Kishapu, Neema Mwaifuge.
Diwani wa kata ya Bubiki Mhe. James Kasomi  akizungumza kwenye Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Maji ambayo katika Wilaya ya Kishapu yamefanyika katika Kijiji cha Bubiki kata ya Bubiki.
 Mwenyekiti wa kijiji cha Bubiki kata ya Bubiki Mhe. William Singu akizungumza kwenye Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Maji ambayo katika Wilaya ya Kishapu yamefanyika katika Kijiji cha Bubiki kata ya Bubiki.
Akina mama wakazi wa Bubiki wakiishukuru serikali kwa kuwaletea huduma ya maji safi na salama kwenye Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Maji ambayo katika Wilaya ya Kishapu yamefanyika katika Kijiji cha Bubiki kata ya Bubiki.
Wananchi wakiwa kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Maji  katika Kijiji cha Bubiki kata ya Bubiki wilayani Kishapu.
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Maji  katika Kijiji cha Bubiki kata ya Bubiki wilayani Kishapu.

Wananchi wakiwa kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Maji  katika Kijiji cha Bubiki kata ya Bubiki wilayani Kishapu.

Wananchi wakiwa kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Maji  katika Kijiji cha Bubiki kata ya Bubiki wilayani Kishapu.
Wafanyakazi wa RUWASA wakiwa kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Maji  katika Kijiji cha Bubiki kata ya Bubiki wilayani Kishapu.
Wafanyakazi wa RUWASA Kishapu na viongozi mbalimbali wa Bubiki wakiwa kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Maji  katika Kijiji cha Bubiki kata ya Bubiki wilayani Kishapu.
Wananchi wakiwa kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Maji  katika Kijiji cha Bubiki kata ya Bubiki wilayani Kishapu.
Wananchi wakiwa kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Maji  katika Kijiji cha Bubiki kata ya Bubiki wilayani Kishapu.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Share:

WATENDAJI WALIOIBA SUMU KIKAANGONI

 

Dawa zilizokamatwa kwa wakala wa duka la pembejeo Iparamasa.

Balozi wa zao la pamba Aggrey Mwanri akitoa maelekezo kwa wakulima Iparamasa 

Na Daniel Limbe, Chato

SERIKALI imetoa siku saba kurejeshwa sumu za wakulima wa zao la pamba zinazodaiwa kuibwa na baadhi ya watendaji wa vyama vya ushirika wa mazao (Amcos) wilayani Chato mkoani Geita.


Hatua hiyo inafuatia kukamatwa chupa 104 za sumu aina ya ekapaki kwenye duka la wakala wa uuzaji wa pembejeo za kilimo kwenye kata ya Iparamasa wilayani humo,hali inayodaiwa kudhoofisha jitihada za serikali kuinua uchumi kwa wakulima.


Kauli hiyo imetolewa leo na Balozi mteule wa zao la pamba nchini, Aggrey Mwanri, wakati akikagua na kuzungumza na wakulima wa zao hilo kwa lengo la kuendelea kuhamasisha kilimo chenye kuzingatia kanuni bora kwa manufaa ya kaya na taifa kwa ujumla.


Hata hivyo balozi huyo, ameagiza kukamatwa na kufikishwa mahakamani, Katibu wa chama cha ushirika wa mazao kata ya Iparamasa (hakumtaja jina) kutokana na tuhuma za kuiba sumu zilizotolewa na serikali kwaajili ya kuwagawia wakulima ili kutokomeza wadudu washambuliao zao la pamba.


Amesema serikali kupitia bodi ya pamba nchini (TCB) iliwakasimisha viongozi wa Amcos jukumu la kuwagawia sumu hizo wakulima ili kurahisha huduma, lakini katika hali isiyokuwa ya kawaida baadhi ya viongozi hao wamekuwa wakiwauzia wafugaji wa ng'ombe kwaajili ya kuogesha mifugo yao kinyume na kusudio la serikali.


Kutokana na hali hiyo, akalazimika kuagiza kurejeshwa kwa sumu zote zilizotolewa kinyume cha utaratibu ndani ya siku 7 na kwamba iwapo kuna mtu yoyote ambaye aliuziwa sumu hizo wakati siyo mkulima wa zao la pamba anatakiwa kujisalimisha kabla hatua kali za kisheria hazijachukuliwa.


Mwanri,amedai serikali haitomfumbia macho mtu yoyote mwenye nia ovu ya kudhoofisha jitihada kubwa za serikali zilizolenga kufufua zao la pamba nchini, kutokana na zao hilo kutoa ajira nyingi kwa vijana.


Kwa upande wake mwakilishi wa Bodi ya pamba Wilayani Chato,Samwel Mdidi, amesema kwa kipindi cha msimu wa kilimo 2022/23 serikali kupitia bodi ya pamba nchini inatarajia kukusanya tani 35,000 za pamba ghafi kutoka kwa wakulima.

Share:

WANANCHI GABIMORI WAPATA HUDUMA YA MAJI BAADA YA KUIKOSA KWA MIEZI 9





Tenki la Maji mradi wa maji Gabimori

Na Dinna Maningo,Rorya.

NI miezi tisa imepita tangu wananchi wa kijiji cha Gabimori kata ya Kyangasaka wilaya ya Rorya mkoa wa Mara kukosa huduma ya maji ya bomba baada ya mashine ya kusukuma maji kutoka kwenye chanzo cha maji kuharibika  hali iliyowalazimu kutembea umbali wa km 3- 5 kufuata maji Ziwa Victoria.

Wakizungumza na Waandishi wa Habari waliotemblea mradi wa maji wa Gabimori ,Mwenyekiti wa mradi wa maji katika kijiji hicho Said Mabele alisema kuwa mradi wa maji ulikamilika 2017 na kutoa maji  lakini Februari,2021 ulistisha hudumalakini kwa sasa mradi huo umeboreshwa na kutoa huduma ya maji.

"Mradi uliharibika inveta ilisheki kule kwenye chanzo cha maji,betri ilikuwa inaharibika kila mara ilibidi watu wakachote maji ziwani umbali wa km3-5 kutegemea na umbali anakoishi,tukawajulisha RUWASA wakatutengenezea mfumo mzuri mashine inasukumwa kutumia Sola(Nishati ya jua) sasa hivi maji yanapatikana muda wote,sisi tunatengeneza matengenezo yale madogomadogo yale makubwa RUWASA ndiyo wanayashughulikia.


"Kata ina vijiji viwili cha Kyangasaka na Gabimori mradi unahudumia zaidi ya kaya 600,ndoo moja ya maji ni sh.50 hadi sasa tuna fedha kwenye akaunti sh.499,000,fedha hizo ni kwa ajili ya kuzitumia  kwenye matengenezo pindi kunapotokea tatizo kama mabomba kupasuka, bila wananchi kuchota maji hatutapata fedha za matengenezo,tunaomba na vitongoji ambavyo havijafikiwa na maji navyo vipate maji yasambazwe kwakuwa mashine ipo haina tatizo ",alisema Said.


Fundi mradi Nyabimori Marwa Matare alisema”kuna changamoto ya vifaa vya mradi kuharibika ukiweka vifaa umbali wa mita moja ni sh.75,000 na gharama uongezeka kadri ya umbali ulivyo, mabomba yanapasuka mara kwa mara tunaendesha mradi kwa kutumia sola mvua ikinyesha maji yanakuwa ya kusuasua ,sola zipo 44 kila sola moja ina watsi 260 mashine inayosukuma maji kwenda kwenye tenki ni ya kisasa.

"Awali ilisukumwa kwa inveta na betri viliharibika tukabadilishiwa mfumo wa jua unaoingiza moto moja kwa moja kwenye mashine kwenye chanzo cha maji kinachopeleka maji kwenye tenki kubwa  lililopo senta ya Gabimori km5 kutoka ziwani", alisema Marwa.

Diwani wa kata ya Kyangasaka Zuberi Mhamed alisema "Mradi ulisimama kutoa maji mwezi February 2021 kwasababu ya inveta kutozalisha moto tukawaambia RUWASA wakabadilisha mfumo sasa hivi  tunapata maji ya kutosha tunaishukuru RUWASA kwa kutatua changamoto ya maji.


Mhamed alisema kuwa awali kabla ya kupata maji safi na salama wananchi walitumia maji yasiyo salama hali iliyosababisha baadhi yao kuugua kichocho nakwamba bado vitongoji vya Nyansagaro na Buhare havijapata huduma ya maji alisema vitongoji vyote vikipata maji maradhi ya kichocho kijijini hapo yatakwisha.


Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA)Wilaya ya Rorya James Kishinhi alisema kuwa serikali imetoa fedha Bilioni 3.3 kutekeleza miradi ya maji 9 katika wilaya hiyo ambayo itakamilika ifikapo juni,30,2022.

Share:

HII NDIO SABABU KUU NIMEFANIKIWA KWA MAISHA KULIKO MARAFIKI WANGU

 

Kwa Muda mfupi tu biashara zangu za kuuza nguo zimenoga sababu ya kuwa mjanja wa maisha. Wengine hawafahamu mimi nilifanya nini ndiyo nikawa tajiri hivyo. 

Kwa majina naitwa Abdalla mkaazi wa Kongowea Mombasani na nimekuwa na matatizo ya pesa kwani umaskini ni kama ulipiga hodi kwangu na nikaitika. Niliteseka kwa muda mrefu lakini ya Mungu ni Mengi. 

Mimi kwa kweli napenda kusoma mitandao na baada ya kuhangaika kwa muda mrefu baadaye nilipata nambari ya simu ya Dakatari mmoja anayeitwa Kiwanga na nikainakiri kwa kijitabu changu.

 Jambo lililonifanya nikainakiri ni kwa sababu niliona kazi yao nzuri ambao walikuwa wamewafanyia wateja wao kupitia wavuti yaani website yao.

 Ilinichukua siku tatu tu baada ya kuwatembelea Kiwanga na hela zikaanza kuingia kwangu kama mfereji. Chochote nilichojaribu kufanya kilifaulu kwa haraka hadi wa leo.

 Kiwanga Doctors wana uwezo mkubwa wa kuimarisha nyota yako ya biashara yoyote ile unayofanya na kwa muda mchache ukaaza kupata wateja wengi kwa siku. Wengi ambao wametafuta usaidizi wao wanasema kuwa wamefanikiwa pakubwa kimairisha maisha yao ya biashara. Kiwanga wanatekeleza Money Spells ama Wealth Spells na utaona mwangaza kwa muda mfupi mno.

 Usiwahi kujali na kusafiri au gharama za kusafiri hadi ofisi zao, wewe piga simu tu na utapata kusaidiwa unavyotaka. 

Kwa biashara, masomo, kuongezwa cheo, magonjwa sugu na kadhalika, tafadhali wasiliana na Kiwanga Doctors na hautajuta. Pia wanatatua shida nyingi kama Kupata mpenzi, kurudisha mpenzi, kuongezewa mamlaka kazini, kuleta furaha na amani katika familia nk. Kiwanga vile vile wanatibu magonjwa sugu kama Kisukari, Pressure kwa kutumia miti shamba na mengineyo. Wasiliana na Kiwanga Doctors kwa nambari +254 769404965 kwa ajili ya kupata huduma. Pia unaweza pitia mtandao huu www.kiwangdoctors.com au kwa barua pepe yaani Email: kiwangadoctors@gmail.com.

Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE MACHI 22,2022



Magazetini leo Jumanne March 22 2022


Share:

Monday, 21 March 2022

FARU RAJABU MTOTO WA FARU JOHN AFARIKI


Faru Rajabu enzi akiwa hai


Faru Rabaju amefariki usiku wa kuamkia leo Machi 21, 2022 akiwa na miaka 43. Faru Rajabu ni mtoto wa Faru John ambaye naye alifariki mwaka 2015.

Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) limetoa taarifa.

Share:

BALOZI WA UINGEREZA AITEMBELEA KLABU YA WAANDISHI WA HABARI YA MKOA WA MWANZA -MPC

Balozi ya Uingereza nchini Tanzania Bwana David Concar amefanya ziara kwenye ofisi ya Klabu ya Waandishi wa Habari ya Mkoa wa Mwanza (MPC) na kufanya mazungumzo mafupi juu ya hali ya utendaji kazi wa vyombo vya habari nchini.


Balozi Concar aliwasili kwenye ofisi za MPC na kupokelewa na Mwenyekiti wa MPC bwana Edwin Soko na kisha kupewa kwa ufupi historia na majukumu ya MPC.

Pia balozi alifanya mkutano na waandishi wa habari na kuzungumzia masuala mbalimbali ikiwemo kuimarika kwa uhuru wa vyombo vya habari ndani ya mwaka mmoja.

"Ni vyema MPC kwenye mpango kazi wake ikaongeza jukumu la kuripoti habari zinazowahusu usawa wa kijinsia na haki za wanawake na watoto", alisema Balozi Concar.

Juu ya mzozo wa Ukraine balozi alieleza kuwa, nchi yake inajikita zaidi kwenye kutoa misaada ya kibinadamu na inaamini kuwa, uvamizi wa Russia Ukraine haukuwa wa haki na ndiyo maana mataifa mengi yanapaza sauti na kumtaka Rais Putin kusitisha vita hivyo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa MPC bwana Edwin Soko alimshukuru Balozi kwa ziara yake hiyo na kusisitiza kuwa bado kuna uhitaji wa serikali ya Uongereza kuwa na programu maalumu za kuwajengea uwezo wa waandishi wa habari wa Tanzania.

"Kwa mwaka mmoja wa utawala wa Rais Samia kumekuwa na uimarikaji wa uhuru wa vyombo vya habari", alisema Soko.

Hii ni ziara ya pili kubwa ya mabalozi kuitembelea MPC ikiwa ziara ya kwanza ilikuwa Mwezi Disemba 2021, ambapo Balozi wa Marekani Bwana Donald Wright aliitembelea MPC na kufanya mazungumzo na viongozi na pia mkutano na wanachama wa MPC.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger