Monday, 7 March 2022

TGNP YASHIRIKI KONGAMANO LA KITAIFA LA WANAWAKE JIJINI ARUSHA

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Amon Mpanju akifungua Kongamano la Kitaifa la Wanawake lililofanyika leo Jumatatu Machi 7,2022 katika Ukumbi wa AICC Jijini Arusha.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) umeshiriki Kongamano la Kitaifa la Wanawake lililofanyika leo Jumatatu Machi 7,2022 katika Ukumbi wa AICC Jijini Arusha kwa lengo la kuwakutanisha Wanawake na wadau wengine katika kujadili changamoto zinazowakabili Wanawake na Ustawi wao.

Kongamano hilo limeongozwa na kauli mbiu ‘Kizazi cha haki na usawa kwa maendeleo endelevu, Tujitokeze kuhesabiwa’.

Akifungua Kongamano hilo Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Amon Mpanju amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya mapinduzi makubwa ndani ya kipindi cha mwaka mmoja wa uongozi wake kwa kuwezesha wanawake kufikia kizazi cha haki na usawa kwa maendeleo endelevu.

Mpanju amesema katika kipindi cha mwaka mmoja wa uongozi wa Rais Samia kumefanyika mapinduzi makubwa na hatua kubwa imepigwa katika kujenga kizazi cha haki na usawa huku wanawake wakichaguliwa na kuteuliwa kuongoza Idara nyeti katika taifa.

“Wanawake ni nguzo ya maendeleo duniani. Ndani ya mwaka mmoja wa Uongozi wa Rais Samia tumepiga hatua kubwa ndani ya mwaka mmoja, tuna Rais Mwanamke, Spika wa Bunge Mwanamke, Katibu Mkuu wa Bunge mwanamke, tuna Mawaziri wanawake 9 katika Wizara nyeti wanafanya kazi vizuri na maendeleo tunayaona, mambo yanakwenda vizuri”,amesema Mpanju.


Mpanju amewataka wadau na wananchi kwa ujumla kuwa tayari kutoa taarifa za matukio ya ukatili wa kijinsia katika jamii ikiwemo ukeketaji kwa watoto wa kike akiongeza kuwa ni vyema jamii ikapambana na vitendo vya ukatili hasa dhidi ya Wanawake ili kutorudisha nyuma juhudi za Serikali na wadau za kuleta Usawa wa kijinsia.

Amesema jamii inatakiwa kusimama katika kupambana na kupinga Mila hasi za kumnyima mwanamke haki na kumkandamiza katika kupata fursa mbalimbali zinazojitokeza kwenye jamii ili kumuwezesha mwanamke kuwa na uwezo wa kutatua changamoto zinazomkabili.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Amon Mpanju akifungua Kongamano la Kitaifa la Wanawake lililofanyika leo Jumatatu Machi 7,2022 katika Ukumbi wa AICC Jijini Arusha. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Amon Mpanju akifungua Kongamano la Kitaifa la Wanawake lililofanyika leo Jumatatu Machi 7,2022 katika Ukumbi wa AICC Jijini Arusha.
Mkurugenzi wa TGNP Lilian Liundi (kulia) akifuatilia hotuba ya
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Amon Mpanju wakati akifungua Kongamano la Kitaifa la Wanawake lililofanyika leo Jumatatu Machi 7,2022 Jijini Arusha.
Wanachama wa TGNP, Gemma Akilimali (kushoto) na Jovitha Mlay wakiwa kwenye Kongamano la Kitaifa la Wanawake lililofanyika leo Jumatatu Machi 7,2022 Jijini Arusha.
Wanachama wa TGNP, Gemma Akilimali (kushoto) na Jovitha Mlay wakiwa kwenye Kongamano la Kitaifa la Wanawake lililofanyika leo Jumatatu Machi 7,2022 Jijini Arusha.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Amon Mpanju akifungua Kongamano la Kitaifa la Wanawake lililofanyika leo Jumatatu Machi 7,2022 Jijini Arusha.
Wadau wakiwa kwenye Kongamano la Kitaifa la Wanawake lililofanyika leo Jumatatu Machi 7,2022 Jijini Arusha.
Mkurugenzi wa TGNP Lilian Liundi (wa pili kushoto) akiwa kwenye Kongamano la Kitaifa la Wanawake lililofanyika leo Jumatatu Machi 7,2022 Jijini Arusha.
Mwanachama wa TGNP, Gemma Akilimali akiandika dondoo muhimu kwenye Kongamano la Kitaifa la Wanawake lililofanyika leo Jumatatu Machi 7,2022 Jijini Arusha.
Wadau wakiwa kwenye Kongamano la Kitaifa la Wanawake lililofanyika leo Jumatatu Machi 7,2022 Jijini Arusha.
Wadau wakiwa kwenye Kongamano la Kitaifa la Wanawake lililofanyika leo Jumatatu Machi 7,2022 Jijini Arusha.
Wadau wakiwa kwenye Kongamano la Kitaifa la Wanawake lililofanyika leo Jumatatu Machi 7,2022 Jijini Arusha.
Wadau wakiwa kwenye Kongamano la Kitaifa la Wanawake lililofanyika leo Jumatatu Machi 7,2022 Jijini Arusha.
Wadau wakiwa kwenye Kongamano la Kitaifa la Wanawake lililofanyika leo Jumatatu Machi 7,2022 Jijini Arusha.
Wadau wakiwa kwenye Kongamano la Kitaifa la Wanawake lililofanyika leo Jumatatu Machi 7,2022 Jijini Arusha.
Wadau wakiwa kwenye Kongamano la Kitaifa la Wanawake lililofanyika leo Jumatatu Machi 7,2022 Jijini Arusha.
Wadau wakiwa kwenye Kongamano la Kitaifa la Wanawake lililofanyika leo Jumatatu Machi 7,2022 Jijini Arusha.
Wadau wakiwa kwenye Kongamano la Kitaifa la Wanawake lililofanyika leo Jumatatu Machi 7,2022 Jijini Arusha.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Share:

WAFANYAKAZI WANAWAKE WA BARRICK NORTH MARA NA BULYANHULU WAJENGEWA UWEZO MAADHIMISHO SIKU YA WANAWAKE


Wafanyakazi wanawake wa Barrick wakifurahia Siku ya wanawake baada ya kupata mafunzo ya kuwajengea uwezo.
Baadhi ya wafanyakazi wanawake wa Barrick wakikata keki kusheherekea Siku ya Wanawake duniani

****
Katika kuelekea Siku ya wanawake Duniani 2022,Kampuni ya Barrick imeandaa semina ya kuwajengea uwezo wafanyakazi wake wanawake katika migodi ya North Mara na Bulyanhulu. 

Semina hizo zimejikita kuwawezesha kujua haki zao za msingi sambamba na kuwawezesha kujiamini katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku.

Barrick imeweka mkazo kwa kuongeza ajira za Wanawake katika sekta ya madini ambayo kwa jadi ilikuwa inatawaliwa na Wanaume kupitia mpango unaolenga kampeni ya ajira na mipango ya maendeleo kuwawezesha katika ngazi zote za kampuni.

Wafanyakazi wanawake wa Barrick na wadau wake pia waliweza kushiriki katika kongamano la wanawake mkoani Shinyanga, ambalo limeendana na uzinduzi wa jukwaa la uwezeshaji wanawake kiuchumi, ambalo limekutanisha wanawake wa mkoa huo kujadili fursa mbalimbali za kiuchumi na upataji wa haki zao.

Kongamano hilo limefanyika wilayani Kahama, kwa kukutanisha wanawake wote wa Mkoa wa Shinyanga, limeandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema katika kuelekea kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani Machi 8.

Wafanyakazi pia mbali na kujengewa uwezo walipata fursa ya kusherekea kwa kupata burudani kutoka kwa msanii mkongwe wa taarabu nchini Hadija Kopa.
Afisa Mwandamizi wa Mahusiano ya Jamii wa Barrick Bulyanhulu, Zuwena Senkondo, akiongea katika hafla ya Wanawake katika kuelekea kuadhimisha siku ya wanawake duniani
Wafanyakazi wakifurahia siku ya wanawake duniani
ASP Fatma Mtalimbo kutoka dawati la jinsia katika Jeshi la Polisi akiendesha semina kwa wafanyakazi wanawake wa Barrick katika mgodi wa North Mara kuelekea Siku ya Wanawake Duniani. Barrick imebadili mwelekeo wa kijinsia katika sekta ya madini
Mmoja wa wafanyakazi wa barrick Bulyanhulu akichangia mada wakati wa semina hiyo
Baadhi ya wafanyakazi wa Bulyanhulu wakiwa katika picha ya pamoja na msanii nguli wa taarabu nchini Hadija Kopa wakati wa hafla ya kusherekea siku ya wanawake duniani
Share:

MBEWE AZUA GUMZO KUISHI NA WAKE WANNE NYUMBA MOJA





Wa kwanza kushoto ni Mbewe akiwa na wake zake wawili kati ya wanne anaoishi nao nyumba moja
***
Mwanaume mmoja Raia wa Zambia anayefahamika kwa jina la Mbewe ame-make headline kwa kuweza kuishi na wake zake wanne kwenye nyumba moja.

Kupitia Interview yake inayotrend huko Zambia aliyofanya na Mchungaji Jimmy Kay aliulizwa kwamba unawezaje kuwamiliki na kuwatunza wanawake wote?

Mbewe akajibu kwamba "Sitafichua ni nani aliyeniambia haya, lakini mmoja wao alisema mzee wewe ni mzuri, kucheat hakuna maana hasa kuwaridhisha licha ya umri mkubwa".

Aidha wake zake wawili kati ya wanne wamesema wanaridhishwa na Mbewe ni mwanaume wa kweli na hakuna mwanaume mwenye mwanamke mmoja hata akikununulia Mercedes Benz au Mjengo wa kuishi.
Share:

MWANAMKE AKWAMA KWENYE MASHINE YA KUFULIA NGUO



Mwanamke akiwa ndani ya mashine ya kufulia
**

Video imesambaa mitandaoni ikimuonesha mwanamke mmoja akiwa amekwama ndani ya mashine ya kufulia nguo, bila kujulikana aliingia vipi kwenye mashine hivyo.

Katika video hiyo wameonekana maafisa wa polisi wakihangaika kutafuta njia nzuri ya kuweza kumtoa, mwanzo wa video hiyo umeonekana mgongo pekee wa mwanamke huyo, huku viungo vingine kama kichwa, miguu, mikono na tumbo vikiwa ndani ya mashine.
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU MACHI 7,2022








.











Share:

Sunday, 6 March 2022

KAMISHNA WA ARDHI MTWARA AMPELEKEA HATI NYUMBANI MMILIKI WA ARDHI ALIYEPOOZA MIGUU

Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Mtwara Rehema Mwinuka (Kulia) akimkabidhi hati mkazi wa kijiji cha Nanyhanga halmashauri ya wilaya ya Tandahimba mkoani Mtwara Ally Salum Mkulumwile alipompelekea hati nyumbani kwake kufuatia kushindwa kujitokeza kuchukua kutokana na changamoto za ugonjwa mwishoni mwa wiki.

Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Mtwara Rehema Mwinuka (Kulia) akiwa na hati mkazi wa kijiji cha Nanyhanga halmashauri ya wilaya ya Tandahimba mkoani Mtwara Ally Salum Mkulumwile (katikati) pamoja na mke wake mara baada ya kumkabidhi hati yake ya ardhi alipompelekea nyumbani kwake kufuatia kushindwa kujitokeza kuchukua kutokana na changamoto ya ya ugonjwa mwishoni mwa wiki.

************************

Na Munir Shemweta, WANMM

Katika jitihada za Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuongeza kasi ya umilikishaji ardhi nchini, Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Mtwara Rehema Mwinuka amempelekea Hati ya Ardhi mkazi mmoja wa kijiji cha Nanyhanga kilichopo katika halmashauri ya wilaya ya Tandahimba mkoani Mtwara ambaye amepooza miguu.

Hatua hiyo ilimfanya mke wa mmiliki huyo Ally Salum Mkulumwile kutoa shukran za dhati kwa Wizara ya Ardhi kupitia Kamishna wake mkoani Mtwara na kueleza kuwa, uamuzi huo siyo tu unampa faraja mume wake ambaye ni mgonjwa bali unaongeza imani kwa wananchi juu ya utekelezaji wa majukumu ya Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

" Nikushukuru sana Kamishna kwa uamuzi huu mlioamua kutuletea hati hapa nyumbani maana kama unavyomuona mume wangu hawezi hata kutembea na kuongea kwake pia ni shida, asante sana" alisema mke wa Mkulumwile.

Kwa Mujibu wa Rehema aliyempekea hati mteja wake huyo mwishoni mwa wiki, hatua ya ofisi yake kumpelekea hati nyumbani ni moja ya juhudi za ofisi yake kuhakikisha wamiliki wa ardhi wasiokuwa na uwezo wa kuzifuata hati za ardhi kwenye ofisi za ardhi za mkoa kutokana na changamoto za kiafya basi wanafikiwa na kupatiwa hati.

"Hapa ni Tandahimba katika kijiiji cha Nanyhanga nimemletea hati mteja wangu mzee wangu Mkulumwile ambaye amepooza miguu na hakuweza kuja kuchukua hati yake tulipofanya zoezi la kugawa hati katika halmashauri ya Tandahimba" alisema Kamishna Rehema.

Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Mtwara aliongeza kuwa, ofisi yake iligawa jumla ya hati 26 kati ya 50 katika halmashauri hiyo ya Tandahimba na kubainisha kuwa, uelewa mdogo wa wamiliki kuhusu taratibu za kuchukua hati ulichangia wengine kushindwa kuzichukua kutokana na kutuma wawakilishi wasiozingatia taratibu za kumchukulia mmiliki hati.

"Watu wanajitokeza kuchukua hati lakini tatizo uelewa. Kuna wamiliki waliwatuma wawakilishi tukashindwa kuwapa kutokana na kushindwa kutimiza masharti ya kumchukulia mtu hati" alisema Rehema.

Alisema, ofisi yake imekuwa ikifanya zoezi la ugawaji hati mara kwa mara katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Mtwara na kwa sasa jumla ya hati 453 hazikachukuliwa na wamiliki wake mbali na juhudi mbalimbali zinazofanyika kuhakikisha wamiliki hao wanachukua hati.

Hata hivyo, alibainisha kuwa, changamoto kubwa kwa zile hati zisizo chukuliwa ni kuwa, wamiliki wake sio wakazi Mtwara na oifisi yake haina namba zao za simu huku ikidaiwa wengi wao walichukua viwanja wakati wa kipindi cha mradi wa Gesi.
Share:

Saturday, 5 March 2022

MKUU WA MAJESHI AWASAMEHE VIJANA WA JKT 853 WALIOFUKUZWA KAMBINI, AAMURU WARUDI MAKAMBINI



Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo, amewasamehe Vijana wa JKT waliofukuzwa makambini April 12,2021 kutokana na utovu wa nidhamu "JWTZ ina taarifa Kijana mmoja kati ya wale Vijana 854 waliofukuzwa amefariki na walio hai ni 853, imeamuriwa Vijana wote 853 warudi makambini"
Share:

SENETA WA MAREKANI ATAKA PUTIN AUAWE



KUPITIA kituo cha runinga cha Fox News, Seneta wa Marekani, Lindsey Graham amesababisha hasira kwa baadhi ya raia wa Urusi baada ya kuwataka watu wa Urusi kumuua rais wao, Vladimir Putin.

Graham kutoka Chama cha Republican katika Jimbo la South Carolina, amenukuliwa akisema: “Njia pekee ya uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine kuisha ni kwa mtu nchini Urusi kumuua Putin, atakuwa ameifanyia nchi yake na ulimwengu kazi nzuri sana.”

Kauli hiyo imezua hasira na kusababisha balozi wa Urusi nchini Marekani, Anatoly Antonov, kuomba maelezo juu ya matamshi hayo ambayo ameyaita kuwa ni matamshi yasiyokubalika na ya mauudhi.


Mzozo wa Urusi na Marekani bado unaendelea huku asilimia kubwa ya Jeshi la Urusi likiwa tayari limeshaingia nchini Ukraine na linatekeleza mashambulizi katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo.

Zaidi ya raia 2,000 wa Ukraine wameshathibitishwa kupoteza maisha huku watu zaidi ya milioni moja wakikimbia taifa hilo ili kuokoa maisha yao.

Mataifa mbalimbali ya Ulaya na Marekani yamekuwa yakipinga vikali vita hivyo yakisema uvamizi wa Putin nchini Ukraine ni ugaidi huku wakimtaka aondoe jeshi lake nchini humo mara moja. Wakati huo huo Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky yeye ameomba maridhiano ili kumaliza mzozo huo.
Share:

RAIS SAMIA AKUTANA NA MBOWE IKULU.....WAKUBALIANA KUFANYA SIASA ZA KISTAARABU NA KIUNGWANA

 






Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na kuzungumza na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe alipowasili Ikulu Jijini Dar Es salaam leo tarehe 04 March 2022 .

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe alipowasili Ikulu Jijini Dar Es salaam leo tarehe 04 March 2022




Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger