Saturday, 4 December 2021

RC SOPHIA MJEMA AZINDUA RASMI KAMPENI YA UPANDAJI MITI YA 'PENDEZESHA TANZANIA' INAYOENDESHWA NA BENKI YA CRDB

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema  akiandaa mti kabla ya kuupanda wakati akizindua rasmi Kampeni ya Upandaji miti kupitia Programu ya Pendezesha Tanzania inayoendeshwa na Benki ya CRDB  ili kuhamasisha upandaji miti na utunzaji wa mazingira nchini.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema  amezindua rasmi Kampeni ya Upandaji miti kupitia Programu ya Pendezesha Tanzania inayoendeshwa na Benki ya CRDB inayolenga kuhamasisha upandaji miti na utunzaji wa mazingira nchini.

Uzinduzi huo umefanyika leo Jumamosi Desemba 4,2021 katika Viwanja vya Maonesho ya Biashara na Madini wa Butulwa maarufu viwanja vya Zainab Telack uliopo kata ya Old Shinyanga katika Manispaa ya Shinyanga ambapo pia wananchi wamepatiwa miti bure kwa ajili ya kwenda kupanda kwenye maeneo yao.

Mkuu huyo wa mkoa ameipongeza Benki ya CRDB kwa kuunga mkono juhudi za Serikali za kupambana na mabadiliko ya tabia ya nchi kwa kuja na Programu ya Pendezesha Tanzania kwa kuhamasisha upandaji wa miti na utunzaji mazingira nchini kupitia kanda zake 7 za Kibenki.

“Kwa upande wa Kanda ya Magharibi mkoa wetu wa Shinyanga umebahatika kuwa chaguo la Benki ya CRDB kuendesha Programu hii kupitia kwenye viwanja vyetu vya maonesho ya Biashara na Madini vya Zainab Telack. Hadi leo katika viwanja hivi Benki ya CRDB wamekwisha panda takribani miti 1,000 na leo imekusudiwa kupandwa miti 900 ili kufikisha adhima yao ya kupanda miti 2,000. Naomba tuwapongeze”,amesema Mhe. Mjema.

“Napenda kuwashukuru Benki ya CRDB kwa kuendesha Programu hii ya Kizalendo . Pia nawashukuru wadau wote mliojitokeza katika zoezi hili la upandaji miti. Napenda kuzihamasisha taasisi zote zilizopo mkoani Shinyanga kwa kuiga na kuunga mkono juhudi hizi ambazo wenzetu Benki ya CRDB wamezionesha kwa Programu yao ya PendezeshaTanzania kwa kupanda miti na kuhamasisha utunzaji mazingira”,ameongeza Mjema.

Mkuu huyo wa mkoa amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa juhudi zake za utunzaji mazingira na uwekaji wa mikakati ya kupambana na mabadiliko ya tabia ya nchi zilizopelekea kupata fedha za Mfuko wa Utunzaji Mazingira (GCF).

Mjema amesema Mkoa wa Shinyanga umejipanga kupanda miti Milioni 9 na sasa miti milioni 5 imepatikana tayari kwa kuanza kupandwa huku akiagiza Wakuu wa wilaya na Wakurugenzi wa halmashauri zote za wilaya Mkoa wa Shinyanga kuhakikisha wanasimamia upandaji miti na miti iliyopandwa.

Amefafanua kuwa dunia kwa ujumla inakabiliwa na changamoto ya mabadiliko ya tabia ya nchi yanayochangiwa shughuli za kibinadamu hususani ukataji miti na ukuaji wa viwanda ambao unasababisha ongezeko la gesi ukaa hali inayosababisha ukosefu wa mvua za kutosha na zisizotabilika na ongezeko la joto na kuyeyuka kwa barafu katika Mlima Kilimanjaro.

“Kwa ujumla hali siyo nzuri, sisi sote ni mashahidi siku hizi hata msimu wa mvua haueleweki hivyo kusababisha mavuno hafifu, ukosefu wa maji ya uhakika. Mwarobaini wa haya ni sisi kuamua kwa dhati kutunza mazingira hasa kwenye vyanzo vya maji kwa kupanda miti na kuachana na ukataji miti ovyo kwa faida yetu pamoja na vizazi vijavyo”
,ameeleza.

“Wananchi wa Shinyanga tuhakikishe katika makazi yetu tunatunza mazingira na kupanda miti hususani miti ya matunda,vivuli na mbao ili kuifanya dunia iwe sehemu salama ya kuishi”,amesema.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko amesema tayari wilaya ya Shinyanga inaendelea na Kampeni ya Upandaji miti ya ‘Shinyanga ya Mikwaju na Miembe’ hivyo kuishukuru Benki ya CRDB kwa kuunga mkono juhudi za serikali katika upandaji miti na utunzaji mazingira.

Naye Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Saidi Pamui wamesema wameanza Programu ya Pendezesha Tanzania kwa ajili ya kuhamasisha wananchi kupanda miti na kutunza mazingira ili kuunga mkono juhudi za serikali katika mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi.

Amesema lengo la Benki ya CRDB ni kupanda miti 2,000 katika viwanja vya maonesho ya Biashara na Madini vya Zainab Telack na tayari walishapanda miti 1,100 na leo wamepanda miti 900 kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema.

“Sisi Benki ya CRDB ni Mabalozi wazuri wa upandaji miti na utunzaji mazingira hivyo tumeanzisha Programu ya Pendezesha Tanzania ili kuonesha mfano kwa wananchi wawe na mwamko wa kupanda miti na kutunza mazingira. Tunawashukuru wadau wote ambao leo mmeungana nasi kushiriki zoezi hili la upandaji miti”,amesema Pamui.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema (katikati) akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali akiwasili katika Viwanja vya Maonesho ya Biashara na Madini wa Butulwa maarufu viwanja vya Zainab Telack uliopo kata ya Old Shinyanga kwa ajili ya kuzindua rasmi Kampeni ya Upandaji miti kupitia Programu ya Pendezesha Tanzania inayoendeshwa na Benki ya CRDB  ili kuhamasisha upandaji miti na utunzaji wa mazingira nchini. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Maandishi yakisomeka 'Pendezesha Tanzania: Karibu Uwanja wa Maonesho Butulwa Shinyanga, CRDB yaliyopo katika Viwanja vya Maonesho ya Biashara na Madini wa Butulwa maarufu viwanja vya Zainab Telack uliopo kata ya Old Shinyanga katika Manispaa ya Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema (katikati) akizungumza wakati akizindua rasmi Kampeni ya Upandaji miti kupitia Programu ya Pendezesha Tanzania inayoendeshwa na Benki ya CRDB  ili kuhamasisha upandaji miti na utunzaji wa mazingira nchini. Kulia ni Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Saidi Pamui. Kushoto ni Kaimu Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Erenestina Richard

Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Saidi Pamui (kulia) akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa Kampeni ya Upandaji miti kupitia Programu ya Pendezesha Tanzania inayoendeshwa na Benki ya CRDB  ili kuhamasisha upandaji miti na utunzaji wa mazingira nchini. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema.

Mkuu w wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa Kampeni ya Upandaji miti kupitia Programu ya Pendezesha Tanzania inayoendeshwa na Benki ya CRDB  ili kuhamasisha upandaji miti na utunzaji wa mazingira nchini. Kushoto  ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema, Kulia ni Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Saidi Pamui.
Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga (kushoto) akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa Kampeni ya Upandaji miti kupitia Programu ya Pendezesha Tanzania inayoendeshwa na Benki ya CRDB  ili kuhamasisha upandaji miti na utunzaji wa mazingira nchini. 

Afisa Maliasili Mhifadhi Manispaa ya Shinyanga, Ezra Manjerenga (kulia) akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa Kampeni ya Upandaji miti kupitia Programu ya Pendezesha Tanzania inayoendeshwa na Benki ya CRDB  ili kuhamasisha upandaji miti na utunzaji wa mazingira nchini. 
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema  akiandaa mti kabla ya kuupanda wakati akizindua rasmi Kampeni ya Upandaji miti kupitia Programu ya Pendezesha Tanzania inayoendeshwa na Benki ya CRDB  ili kuhamasisha upandaji miti na utunzaji wa mazingira nchini.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema  akipanda mti wakati akizindua rasmi Kampeni ya Upandaji miti kupitia Programu ya Pendezesha Tanzania inayoendeshwa na Benki ya CRDB  ili kuhamasisha upandaji miti na utunzaji wa mazingira nchini.

Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Said Pamui akijiandaa kupanda mti wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Upandaji miti kupitia Programu ya Pendezesha Tanzania inayoendeshwa na Benki ya CRDB  ili kuhamasisha upandaji miti na utunzaji wa mazingira nchini.
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Said Pamui akimwagilizia maji mti aliopanda wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Upandaji miti kupitia Programu ya Pendezesha Tanzania inayoendeshwa na Benki ya CRDB  ili kuhamasisha upandaji miti na utunzaji wa mazingira nchini.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga, Zuwena Omary akipanda mti wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Upandaji miti kupitia Programu ya Pendezesha Tanzania inayoendeshwa na Benki ya CRDB  ili kuhamasisha upandaji miti na utunzaji wa mazingira nchini.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko akipanda mti wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Upandaji miti kupitia Programu ya Pendezesha Tanzania inayoendeshwa na Benki ya CRDB  ili kuhamasisha upandaji miti na utunzaji wa mazingira nchini.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko akimwagilizia maji mti aliopanda wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Upandaji miti kupitia Programu ya Pendezesha Tanzania inayoendeshwa na Benki ya CRDB  ili kuhamasisha upandaji miti na utunzaji wa mazingira nchini.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP George Kyando akipanda mti wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Upandaji miti kupitia Programu ya Pendezesha Tanzania inayoendeshwa na Benki ya CRDB  ili kuhamasisha upandaji miti na utunzaji wa mazingira nchini.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, Jomaary Satura akipanda mti wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Upandaji miti kupitia Programu ya Pendezesha Tanzania inayoendeshwa na Benki ya CRDB  ili kuhamasisha upandaji miti na utunzaji wa mazingira nchini.
Kaimu Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Erenestina Richard akipanda mti wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Upandaji miti kupitia Programu ya Pendezesha Tanzania inayoendeshwa na Benki ya CRDB  ili kuhamasisha upandaji miti na utunzaji wa mazingira nchini.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Ramadhani Elias Masumbuko akipanda mti wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Upandaji miti kupitia Programu ya Pendezesha Tanzania inayoendeshwa na Benki ya CRDB  ili kuhamasisha upandaji miti na utunzaji wa mazingira nchini.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, Nice Munissy akipanda mti wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Upandaji miti kupitia Programu ya Pendezesha Tanzania inayoendeshwa na Benki ya CRDB  ili kuhamasisha upandaji miti na utunzaji wa mazingira nchini.
Mfanyabiashara Maarufu Gilitu Makula akipanda mti wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Upandaji miti kupitia Programu ya Pendezesha Tanzania inayoendeshwa na Benki ya CRDB  ili kuhamasisha upandaji miti na utunzaji wa mazingira nchini.
Meneja Biashara wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Jumanne Wagana akimwagilizia maji mti aliopanda wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Upandaji miti kupitia Programu ya Pendezesha Tanzania inayoendeshwa na Benki ya CRDB  ili kuhamasisha upandaji miti na utunzaji wa mazingira nchini.
Mkuu wa Magereza Mkoa wa Shinyanga akipanda mti wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Upandaji miti kupitia Programu ya Pendezesha Tanzania inayoendeshwa na Benki ya CRDB  ili kuhamasisha upandaji miti na utunzaji wa mazingira nchini.
Mwenyekiti wa Kamati ya Amani Mkoa wa Shinyanga Sheikh Hamis Balilusa akipanda mti wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Upandaji miti kupitia Programu ya Pendezesha Tanzania inayoendeshwa na Benki ya CRDB  ili kuhamasisha upandaji miti na utunzaji wa mazingira nchini.
Zoezi la upandaji miti likiendelea wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Upandaji miti kupitia Programu ya Pendezesha Tanzania inayoendeshwa na Benki ya CRDB  ili kuhamasisha upandaji miti na utunzaji wa mazingira nchini.

Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Saidi Pamui akiwashukuru wadau mbalimbali waliojitokeza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Upandaji miti kupitia Programu ya Pendezesha Tanzania inayoendeshwa na Benki ya CRDB  ili kuhamasisha upandaji miti na utunzaji wa mazingira nchini.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile akitoa elimu  ya UVIKO 19 na kuwahamasisha wananchi kujitokeza kupata chanjo dhidi ya UVIKO 19 pamoja na kuchukua tahadhari dhidi ya UVIKO 19  kwa wananchi waliojitokeza kwenye uzinduzi wa Kampeni ya Upandaji miti kupitia Programu ya Pendezesha Tanzania inayoendeshwa na Benki ya CRDB  ili kuhamasisha upandaji miti na utunzaji wa mazingira nchini.
Mkazi wa Old Shinyanga akiwa amebeba miti iliyotolewa bure kwa wananchi wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Upandaji miti kupitia Programu ya Pendezesha Tanzania inayoendeshwa na Benki ya CRDB  ili kuhamasisha upandaji miti na utunzaji wa mazingira nchini.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema (katikati aliyevaa kofia) akipiga picha na wadau mbalimbali waliojitokeza wakati wa uzinduzi rasmi wa Kampeni ya Upandaji miti kupitia Programu ya Pendezesha Tanzania inayoendeshwa na Benki ya CRDB  ili kuhamasisha upandaji miti na utunzaji wa mazingira nchini.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema (katikati) akipiga picha na wadau mbalimbali waliojitokeza wakati wa uzinduzi rasmi wa Kampeni ya Upandaji miti kupitia Programu ya Pendezesha Tanzania inayoendeshwa na Benki ya CRDB  ili kuhamasisha upandaji miti na utunzaji wa mazingira nchini.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema (wa tatu kulia) akipiga picha ya kumbukumbu na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko (kulia) akifuatiwa na Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga , Zuwena Omary. Wengine ni Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga, Luther Mneney  (kushoto) akifuatiwa na Meneja Biashara Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana na Meneja wa Benki ya CRDB Kanda yaa Magharibi, Saidi Pamui baada ya uzinduzi rasmi wa Kampeni ya Upandaji miti kupitia Programu ya Pendezesha Tanzania inayoendeshwa na Benki ya CRDB  ili kuhamasisha upandaji miti na utunzaji wa mazingira nchini.
Muonekano wa sehemu ya Viwanja vya Maonesho ya Biashara na Madini wa Butulwa maarufu viwanja vya Zainab Telack uliopo kata ya Old Shinyanga 
Muonekano wa sehemu ya Viwanja vya Maonesho ya Biashara na Madini wa Butulwa maarufu viwanja vya Zainab Telack uliopo kata ya Old Shinyanga .

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Share:

PAKUA APP MPYA YA MALUNDE 1 BLOG....IMEBORESHWA ZAIDI KUKUPA RAHA YA HABARI NA MATUKIO BURE KWENYE SIMU YAKO

Toleo Jipya Kabisa la App ya Malunde 1 blog, Kama unayo kwenye simu Pakua Upya mtu wangu...  Bofya mara Moja <<Hapa>>

Habari Njema Wasomaji wa Malunde 1 blog !! Ili kuwa wa Kwanza kupata habari na matukio  ya ukweli na uhakika kwa wakati yanayojiri Tanzania na dunia kwa ujumla tunakushauri kupakua/ kudownload Aplikesheni ya Malunde 1 blog

Usikubali kupitwa na habari na Matukio yanayotokea… Pakua leo App ya Malunde 1 blog

Tembea na dunia kiganjani mwako kiulaini kabisa.

Pakua App mpya ya Malunde 1 blog imeboreshwa zaidi ili kukidhi mahitaji ya wasomaji wetu. 

Ni rahisi sana : Ingia Play store kisha Andika Malunde 1 blog halafu bonyeza Install

https://bit.ly/2Qb7qyF

Usikubali kukosa habari kizembe..Pakua app yetu Mpya ya Malunde1 blog Sasa

Toleo Jipya Kabisa la App ya Malunde 1 blog, Kama unayo kwenye simu Pakua Upya mtu wangu...  Bofya mara Moja <<Hapa>>

Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI DESEMBA 4,2021

Magazetini leo Jumamosi December 4,2021

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive

Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger