Tuesday, 2 November 2021

Soni Seminary Secondary School

About Soni Seminary Secondary School Soni Seminary Secondary School is a secondary school in Tanzania with The National Examinations Council of Tanzania (NECTA) registration number S0376 – Known as Shule ya Sekondari Soni Seminary Secondary School Soni Seminary is a independent secondary school, this institution is non government owned. This school is flagged as “Operational”. […]

This post Soni Seminary Secondary School has been posted by Udahiliportal Editor 02

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

St. Ann’s Girls Seminary Secondary School

About St. Ann’s Girls Seminary Secondary School St. Ann’s Girls Seminary Secondary School is a secondary school in Tanzania with The National Examinations Council of Tanzania (NECTA) registration number S0260 – Known as Shule ya Sekondari St. Ann’s Girls Seminary Secondary School St. Ann’s Girls Seminary Secondary School Facilities The St. Ann’s Girls Seminary Secondary […]

This post St. Ann’s Girls Seminary Secondary School has been posted by Udahiliportal Editor 02

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

TAKUKURU SHINYANGA YAANIKA MIKAKATI MIKUBWA YA UFUATILIAJI FEDHA ZA MIRADI KUZUIA UPIGAJI


Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga Hussein Mussa akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu taarifa ya kazi zilizotekelezwa na TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga katika kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2021/2022 (Julai – Septemba 2021). Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga Hussein Mussa akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu taarifa ya kazi zilizotekelezwa na TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga katika kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2021/2022 (Julai – Septemba 2021).

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Shinyanga inaendelea kutekeleza Mkakati wake mkubwa wa kufuatilia fedha zilizotumika na zinazotarajiwa kutumika katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo pamoja na kukagua miradi yote inayotekelezwa ili kuhakikisha kuwa miradi hiyo inakuwa na thamani halisi ya fedha zilizotolewa.

Hayo yamesemwa leo Jumanne Novemba 2,2021 na Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga Hussein Mussa wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu taarifa ya kazi zilizotekelezwa na TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga katika kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2021/2022 (Julai – Septemba 2021).

Mussa amesema katika mikakati ya utendaji kazi wa TAKUKURU mkoa wa Shinyanga kwa kipindi cha mwezi Oktoba hadi Disemba 2021 wamejipanga kikamilifu kuendelea kufanya ufuatiliaji wa fedha za miradi na ukaguzi wa miradi ili kuhakikisha miradi inaendana na thamani halisi ya fedha zinazotolewa na Serikali na wadau wa maendeleo.

“Katika kipindi cha mwezi Julai hadi Septemba 2021 tulijikita katika kuzuia rushwa kwenye miradi ya maendeleo inayotekelezwa mkoa mzima wa Shinyanga na miradi iliyopewa fedha za serikali na ufadhili wa wadau wa maendeleo kwa miradi inayotekelezwa katika mwaka wa fedha 2020/2021”,ameeleza.

“Katika ufuatiliaji huo kwa kipindi cha Julai – Septemba 2021 jumla ya miradi 10 yenye thamani ya shilingi 3,795,962,441/= ilitembelewa,ilikaguliwa na kutolewa ushauriwa namna bora ya kuiboresha ili miradi hiyo inakuwa na thamani halisi ya fedha iliyotolewa ili kuhakikisha hakuna ubadhirifu wala ufujaji wa fedha hizo”,ameongeza Mussa.

Amefafanua kuwa katika kipindi hicho cha Julai - Septemba 2021,TAKUKURU Shinyanga imefanya uchambuzi wa kubaini iwapo kuna mianya ya rushwa katika mapato ya stendi ya mabasi Maganzo,ukusanyaji wa ada za maegesho ya vyombo vya usafiri katika Manispaa ya Shinyanga na faini kwa wanaokiuka utaratibu wa maegesho pamoja na uchambuzi wa mfumo wa usimamizi wa mitihani katika vyuo vya kati ambapo Chuo cha Ufundi VET Shinyanga na Kahama vilifanyiwa kazi.

Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa TAKUKURU amesema wamepokea malalamiko 46 ambapo taarifa zinazohusu rushwa zilikuwa 27, kati ya hizo 20 uchunguzi wake unaendelea na malalamiko 7 uchunguzi wake umefungwa kwa kukosa ushahidi.

“Kwa mujibu wa taarifa tulizopokea Idara zilizolalamikiwa ni serikali za mitaa (15),elimu (6), ardhi (4), madini (4), ujenzi (3),afya (2), siasa (2), fedha (2), biashara (2),mahakama (2), kazi (2),maliasili (1) na barabara (1). Kesi zinazoendelea mahakamani ni 21. Kati ya hizo kesi mpya ni 3, kesi 4 ziliamuliwa mahakamani, kesi 2 zilishinda kwa watuhumiwa kutiwa hatiani na kulipa faini”,ameeleza Mussa.

Hata hivyo amesema TAKUKURU Shinyanga imeweka utaratibu wa kusikiliza kero za wananchi siku moja kila mwezi ‘TAKUKURU Inayotembea’ kwa kuwafuata wananchi katika maeneo yao ambapo wananchi wanapatiwa elimu ya kutosha juu ya madhara ya rushwa na namna ya kutoa taarifa za vitendo vya rushwa kwenye ofisi za TAKUKURU.



Share:

JE UMEWAHI KUSIKIA HABARI ZA MWANAMALUNDI?? YULE MSUKUMA MWENYE MIUJIZA?? ....SOMA HAPA


Mwanamalundi ni jina ambalo lilikuwa maarufu sana karne ya 18 na 19 (enzi za mkoloni) maeneo ya kanda ya ziwa; hususani Mwanza na Shinyanga. Habari za huyu mtu zimewahi kuandikwa kwenye kitabu kiitwacho "MWANAMALUNDI: Mtu maarufu katika Historia ya Usukuma". Ni kitabu ambacho kiliingizwa kwenye mtaala wa elimu ya msingi miaka ya 1970-80. Wazee wenzangu watakuwa wanakumbuka. Hivi sasa habari za mtu huyu ni Kama vile zimepotea kabisa.

MWANAMALUNDI NI NANI HASA?

Mwanamalundi ni jina la mtu wa miujiza kutoka kabila la Wasukuma. Matamshi sahihi ya jina hili Ni "Ng'wanamalundi" na sio "Mwanamalundi" kama ambavyo wengi hutamka.

Mwanamalundi alizaliwa kijiji cha Ng'wakwibilinga, wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza mwaka 1892. Baba yake aliitwa Bugomola na mama yake aliitwa Ngolo. Wazazi hawa wawili hawakujaaliwa kupata watoto kwa muda mrefu sana. Uzee uliwakaribia bila hata kupata mtoto. Jambo hili liliwakosesha sana raha, hasa Mzee Bugomola ambae alitamani sana japo apate mrithi wa mali zake. Hali hii ilimfanya Bugomola kuwa mtulivu na mpole muda mwingi katika maisha yake.

Katika jamii ya wasukuma wakati huo, mwanamke asiposhika mimba ndani ya kipindi cha miezi 6 hadi 12 tangu aolewe, ilikuwa ni lazima aende kwa mganga kujua kinachomsumbua. Ni nyakati ambazo hakukuwa na makanisa ya maombezi kama ilivyo leo hii, misikiti ya kuomba dua wala hospitali. Waganga ndio watu pekee waliotatua matatizo mbalimbali ya jamii zao.

Mzee Bugomola na mke wake Ngolo wakaamua kwenda kwa mganga upande wa mashariki ya kijiji walichokuwa wakiishi (Ng'wakwibilinga) ili wapate ufumbuzi wa tatizo lao. Mganga aliwaambia ujio wao hata kabla hawajajieleza wenyewe. Mganga akawatengenezea dawa kisha akawaambia kuwa Ngolo (mama/mke) atashika mimba na atazaa mtoto wa kiume ambae atakuja kuwa mashuhuri siku za hapo baadae lakini kwa bahati mbaya Bugomola (baba/mume) hatoweza kumuona mtoto huyo; yaani Bugomola atafariki kabla mtoto hajazaliwa.

Habari hii ilimfurahisha sana Bugomola pamoja na kwamba aliambiwa atakufa bila kumuona mtoto. Mkewe pia alifurahi kusikia kuwa atashika mimba. Bugomola hakujali kifo chake sababu hata umri wake ulikuwa umeenda kidogo. Furaha yake kubwa ilikuwa ni kumpata mrithi wake. Walirudi nyumbani wakiwa na furaha kubwa. Bugomola hakuweza kuificha furaha yake. Muda mwingi alionekana ni mwenye tabasamu na vicheko vingi tofauti kabisa na vile watu wavyomzoea kumuona.

Baada ya wiki kadhaa Ngolo alishika mimba. Mimba ilipotimiza miezi mitatu tu, Bwana Bugomola aliaga dunia bila hata kuugua. Ngolo ambae alikuwa mjane wakati huo aliilea mimba hiyo hadi ilipofikisha miezi 9.

Siku moja kabla Ngolo hajajifungua mtoto, wingu kubwa lilitanda angani. Mvua kubwa na yenye radi kali ikaanza kunyesha. Mtoto aliyekuwa tumboni akaruka mruko usio wa kawaida na kisha ikaskika sauti ya kitoto kutoka tumboni ikisema, "máyù nibyalage, yaani mama nizae!" Ngolo akashtuka na kuingiwa hofu baada ya kuskia sauti hiyo, hivyo akamuita mama mkwe wake na baadhi ya majirani ili nao waweze kuwa mashahidi wa sauti hiyo. Kwa bahati nzuri sauti ile ikajirudia tena na ghafla uchungu ukamshika Ngolo. Ilikuwa ni mwaka 1892 Ngolo alipojifungua mtoto wa kiume mwenye maajabu tangu akiwa tumboni mwake. Mtoto huyo akaitwa Igulu, yaani Mbingu.

Igulu (Mwanamalundi) alizaliwa akiwa mwenye afya njema kabisa isipokuwa tu miguu yake ilikuwa myembamba na yenye nyayo kubwa tangu alipozaliwa. Kutokana na wembamba wa miguu yake, jamii ikampa jina la utani "Mamilundi" likimaanisha "mamiguu membamba".

Igulu alikuwa ni mtu mwenye aibu sana enzi za utoto wake. Alikuwa akiwakimbia wageni wasimuone na kuuficha uso wake kwa aibu. Pamoja na aibu alizokuwepo nazo, alipenda sana kuzurura mitaani akiwa ameambatana na marafiki zake. Baadhi ya wazazi hawakupendezwa na tabia yake ya uzururaji akiwa ameambatana na watoto wao. Mara kadhaa wazazi wa marafiki wa Igulu walimtamkia Igulu (Mwanamalundi) maneno mabaya kila Igulu (Mwanamalundi) alipotoka kuzurura na watoto wa majirani zake, walimwambia, “Mamirundi galyo lilihumbura bana bise”, ikiwa na maana "mamiguu yake marefu linarubuni watoto wetu”.

Katika ujana wake Igulu, alipenda sana kucheza ngoma aina ya Kahela. Kila aliposhiriki kucheza ngoma hiyo, alipenda sana kuuficha uso wake kwa kitambaa cheusi. Katika mashindano ya kucheza ngoma hiyo, Igulu na marafiki zake walishindwa kuwa washindi. Watu kama Samíke, Ng'wanikinga, Ng'wanilong'ho na Gíndù Nkíma walikuwa si rahisi kuwashinda katika uchezaji wa ngoma. Ni watu ambao walijua kucheza ngoma kwa umahili kuliko Igulu (Mwanamalundi). Mara nyingi matumizi ya uchawi yalihusika katika kuwapa ushindi wa kucheza ngoma hiyo na kukubalika kwa watu mbalimbali.

Kutokukubalika kwa Igulu (Mwanamalundi) na marafiki zake mbele ya jamii hasa katika uchezaji wa ngoma kulipelekea achukue uamuzi wa kwenda kwa mganga. Igulu aliwashawishi vijana wenzie waende kwa mganga atakaewapa dawa ya mvuto kwa watu na kuwa washindi nyakati zote za mashindano ya ngoma. Vijana wenzie walikubali sababu kwa nyakati zile suala la kwenda kwa mganga lilikuwa ni jambo dogo sana.

Safari ya kuelekea mashariki zaidi mwa kijiji chao ikawadia. Mganga alikuwa ni mwanamke, mwenye umri ufaao kuitwa bibi ndani ya kijiji cha Nyaraja, wilaya ya Iramba mkoa wa Singida. Walipokelewa vizuri na mwenyeji wao. Iliwachukua wiki moja bila kuhudumiwa chochote kile, siku ya nane mganga akawaamuru wachukue panga na majembe kuelekea porini ili wakachimbe dawa itakayowasaidia kupendwa na watu.

Wakiwa porini, yule bibi mganga alitafuta vinyonga watatu kwa idadi ya vijana hao wanaotaka dawa kisha akawaambia wachimbe mashimo yenye nusu ya urefu wao. Vijana wakachimba mashimo hayo huku wakiwa na vinyonga vichwani mwao. Walipomaliza kuchimba, bibi mganga akawaambia wafunike mashimo hayo kwa kuni kavu. Vijana hao wakatii maagizo ya bibi mganga na kisha bibi akawatoa vinyonga waliokuwa wameng'ang'ania kwenye vichwa vya vijana hao watatu na kisha akawatia dawa midomoni vinyonga hao na kisha akawaweka juu ya kuni zilizofunika mashimo yale yaliyochimbwa na vijana wale watatu. Mara baada ya kuwaweka vinyonga hao juu ya kuni zile, moto ukawashwa ili kuwachoma vinyonga hao.

Hazikupita dakika kadhaa wakiwa wanashuhudia kuteketea kwa vinyonga hao, ghafla akatokea kifaru katika mazingira ya kutatanisha na akaanza kuwafukuza watu wote, akiwemo yule bibi mganga. Igulu (Mwanamalundi) ilimlazimu apande juu ya mti kujinusuru na madhira hayo. Wale vijana wawili walitimka mbio na hawakurudi tena. Bibi mganga akararuliwa na yule kifaru mpaka akapoteza maisha na kisha kifaru akamjia Igulu (Mwanamalundi) aliekuwa juu ya mti na kuanza kuudhuru ule mti kwa pembe yake. Kifaru hakufanikiwa kuuangusha mti aliopanda Igulu zaidi ya kuubandua magome yake. Kifaru alipochoka akaamua kuondoka na kutokomea kusikojulikana.

Igulu (Mwanamalundi) akashuka juu ya ule mti na kumwendea bibi mganga ambae muda huo alikuwa ni marehemu. Igulu akaubeba mwili wa yule bibi mganga na kuurudisha nyumbani. Akiwa njiani, ule mwili wa bibi mganga uliokuwa mabegani mwake ukaonesha kuwa ni kama vile unavuta pumzi mapafuni. Ghafla yule bibi akapiga chafya na kuamka kisha akamuuliza Igulu (Mwanamalundi), "Bhaja hálí abhayanda abhalaha" akimaanisha kuwa wako wapi vijana waliokuwa hapa? Igulu akamwambia kuwa wale vijana wenzie wamekimbia baada ya kumuona yule kifaru. Bibi mganga ambae muda huu alionekana kuwa ni mzima kabisa na hana majeraha tena akaomba warudi eneo la tukio ili wachukue dawa. Wakiwa njiani kurudi eneo la tukio, yule bibi mganga akamsifia sana Igulu kwa kumuita "Ni mwanaume kamili" aliekuja kweli kutafuta dawa. Bibi akaokota yale magome yaliyobanduliwa na kifaru na kisha kuondoka nayo.

Walipofika nyumbani, yule bibi akaamua kumwambia ukweli Igulu (Mwanamalundi) kuwa yule kifaru ni yeye mwenyewe bibi. Aliamua kujibadili ili kuwapima uwezo wao wa kuvumilia magumu. Kwa kuwa Igulu pekee ndio alionesha yuko imara, bibi yule alimtunuku dawa nzuri zitakazompa mvuto na nguvu katika ngoma zake. Wale vijana wawili walipitiliza hadi kwao bila kurudi tena kwa mganga. Bibi mganga alimpa masharti Igulu baada ya kumpa dawa. Bibi mganga alimzuia Igulu (Mwanamalundi) kumparaza mtu yeyote au kumnyooshea kidole. Iwapo atafanya hivyo basi alieparazwa au kunyooshewa kidole atakufa hapohapo.

Igulu (Mwanamalundi) aliporudi kijijini kwake na kisha kucheza ngoma ya kwanza baada tu ya kurudi kutoka kwa mganga, alishinda. Kuna nyakati Igulu aliamua kucheza ngoma akiwa juu ya jiwe kubwa. Wakati akicheza ngoma hizo, nyazo zake zilionekana juu ya mawe aliyokuwa akitumia kucheza ngoma. Ni alama za nyayo ambazo zipo mpaka leo pale kijiji cha Nyandekwa, wilaya ya Kahama mkoa wa Shinyanga. Ni kama km 10 tu kutoka makao makuu ya wilaya. Kuna nyakati Igulu alitengeneza mashimo ya mchezo wa bao juu ya jiwe kwa kutumia kisigino chake. Ni alama ambazo pia bado zipo kijiji cha Nyandekwa, Kahama-Shinyanga.

Igulu aliposhinda mashindano ya ndani ya kijiji, akaamua kuomba kushindana na wapinzani wakubwa zaidi walioishi kijiji cha Ng'wagala wilaya ya Maswa; yaani akina Samíke, Ng'wanikînga, Ng'wanilog'ho na mwanamke mwenye nguvu za kiganga aitwae Gíndü Nkíma. Hawa watu wanne walikuwa hawana mpinzani katika ngoma lakini Igulu (Mwanamalundi) akajitosa kushindana nao kwa mara nyingine.

Mwanamalundi alipofika kwenye mashindano, akafanya miujiza kwa kujirefusha kama ngongoti asiye na magongo yoyote yale na kisha akaanza kucheza huku akiwa ameficha uso wake kwa kitambaa cheusi kama kawaida yake. Wakati anacheza ngoma akiwa ana urefu wa ngongoti, baadhi ya watu walijaribu kugusa na kuifunua miguu yake ili wajue kulikuwa kuna nini. Wote waliothubutu kuigusa walikufa baada ya muda mfupi. Katika ngoma hiyo, Gíndü Nkíma akatumia nguvu zake za kiganga kumrudisha Igulu (Mwanamalundi) kama alivyokuwa awali; yaani pasipo kurefuka kama ngongoti. Kwa kufanya hivyo, Mwanamalundi alipoteza pambano hilo.

Mwanamalundi akaondoka Maswa na kwenda kijiji cha Nela ambako lilipangwa shindano jingine. Shindano hili Mwanamalundi alishinda. Kwa kuwa katika safari zake zote huambatana na jopo la wapishi wa chakula, ushindi huu ulimkwaza Gíndü Nkíma, mpinzani wake mkubwa ambae aliamua kuloga chakula anachoandaliwa Mwanamalundi ili kisiive hata kikipikwa wiki nzima.

Ni kweli kabisa, wapishi wa Mwanamalundi walilalamika kuhusu chakula kutoiva kabisa kwa muda mrefu na kuni zinakaribia kuisha. Hivyo wapishi wakaomba msaada wa kuni kwa Mwanamalundi. Baada ya wapishi kulalamika, Mwanamalundi akasonta/akanyoosha kidole kwenye pori fulani eneo hilo na kuwaambia wapishi waende wakakate kuni alikonyooshea kidole. Kwa bahati mbaya wakati ananyoosha kidole hicho hakujua kama ndani ya pori hilo kulikuwa kuna mifugo na wachungaji kadhaa ambao wote walikufa na kukauka kama kuni.

Tukio hili la kukausha miti na kuua ng'ombe na wachungaji wake lilimuudhi sana Mtemi Masanja wa III ambae aliamuru askari wake waende kumkamata Mwanamalundi haraka iwezekanavyo ili awajibishwe. Askari wa Mtemi Masanja waliogopa sana kumkamata Mwanamalundi wakihofia kufa. Iliwalazimu kumkamata tu sababu walimuogopa zaidi mtemi kuliko Mwanamalundi.

Kabla Mwanamalundi hajakamatwa, alijua jambo hilo lingetokea. Hivyo akaenda haraka kumuaga mama yake mzazi na kumuachia maagizo. Mwanamalundi alikamua maziwa kiasi fulani kwenye kikombe na kisha akampa mama yake na kumwambia, "Iwapo maziwa haya yataanza kuganda, ujue kuwa nipo katika hali mbaya, iwapo yataganda kabisa, ujue kuwa nimekufa!", Mwanamalundi akachukua shoka isiyo na mpini kisha akaiegamisha ukutani na kumwambia mama yake, "Iwapo nitakamatwa na kupelekwa kuuliwa, shoka hii itakuwa ikipanda ukutani nikiwa napelekwa kuuliwa, tukifika eneo nitakalouliwa, basi hii shoka itapandisha hadi mwisho wa ukuta kuonesha kuwa tumefika mwisho wa safari!" Mama yake alipokea maagizo hayo na haikuchukua muda Mwanamalundi akakamatwa na askari wa Mtemi Masanja.

Mtemi Masanja III aliamua kupeleka shauri hilo kwa watawala wa kizungu (Wajerumani) ili wamchukulie hatua Mwanamalundi. Uchunguzi ukafanyika na Mwanamalundi akaonekana ana hatia ya mauaji ya watu wasio na hatia. Adhabu ya kosa hili ilikuwa ni kunyongwa.

Katika safari hii ya kunyongwa, Mwanamalundi aliambatana na Makongoro Igana ambae alikuwa ni Mtemi wa Ilemela. Mtemi huyu alikuwa ana hatia ya kuwachapa fimbo wajerumani baada ya kupita upande usio sahihi katika njia kadiri ya utaratibu wa utawala wake. Mtemi Makongoro Igana kila alipokuwa akisafiri juu ya punda, mkono wake wa kuume ulikuwa umeshika fimbo ndefu. Fimbo hiyo hutumika kumchapia kila atakaepita upande wa kuume katika safari zake. Kwa bahati mbaya wajerumani hawakujua utaratibu huo wa Mtemi Makongoro. Siku wajerumani walipopishana safarini na Mtemi Makongoro, walipita upande wa kuume wenye fimbo. Mtemi Makongoro akawachapa fimbo wazungu hao kama ilivyo jadi yake. Wazungu hao walishindwa kumvumilia, wakamkamata na kumfungulia mashtaka yaliyoamuru Mtemi anyongwe.

Kaliyaya ni mtu wa pili alieambatana na Mwanamalundi katika safari ya kunyongwa. Huyu Kaliyaya alikuwa ni mtu alieonekana ni mwenye ushawishi mkubwa kwa watu wa jamii yake. Kukubalika kwake kulimfanya apate wafuasi wengi ambao walihofiwa kumpindua mjerumani. Hivyo wajerumani wakaona ni bora wamfungulie mashtaka ili wamnyonge kabla hajawapindua. Kaliyaya alikuwa ni mtu wa kawaida tu ila ni mwenye ushawishi na kipenzi cha watu wengi.

Mtu wa tatu alieambatana na Mwanamalundi katika safari ya kunyongwa ni Mtemi Italange wa Bugando. Mtemi huyu aliingia mgogoro na Wajerumani baada ya kuhodhi eneo kubwa la pwani ya ziwa Victoria na bandari zake kisha akakataa kuwapa Wajerumani. Ili kumnyang'anya utajiri huo, wajerumani wakaamua kumfungulia mashtaka ili wamnyonge.

Zoezi la kunyongwa lilipofika, Mwanamalundi alikuwa ndio mtu wa kwanza kuvishwa kitanzi. Kamba ilipofyatuliwa tu ili kumuua, kamba ikakatika yenyewe. Zoezi la kumuua likaahirishwa, badala ya kunyongwa akabadilishiwa adhabu.

Ikaja zamu ya Mtemi Makongoro Igana. Mtemi alipowekewa tu kitanzi shingoni na kisha kuifyatua kamba hiyo ili kumuua, ghafla kukatokea mfano wa sinema kwenye ukuta. Ni sinema ya kimiujiza iliyoonesha matukio ya kivita miaka ya nyuma. Askari wakageuka kuitazama sinema hiyo. Sinema haikuchukua zaidi ya dakika moja, ikaisha. Walipomgeukia yeye (Mtemi Makongoro Igana) wakaona hana kamba shingoni. Huyu nae akawekwa pembeni na kubadilishiwa adhabu.

Akaja Mtemi Italange. Huyu alipowekewa kitanzi shingoni, nae pia kamba ilifyatuka. Akawekwa pembeni na kubadilishiwa adhabu. Ilipofika zamu ya Bwana Kaliyaya, kitanzi kilipofyatuliwa ili kumnyonga, hakika kitanzi kilimuua. Huyu hakuwa mwenye ulinzi wowote ule kishirikina; yaani alikuwa ni mtu wa kawaida tu.

Ndipo mamlaka za mjerumani zikaamuru askari wawapeleke watu hao watatu Tabora. Wakiwa njiani kuelekea Tabora, walifika Nzega na kuamua kupumzika kidogo chini ya mti mkubwa nje ya Shule ya Sekondari Chama. Askari wakijerumani wakawa wakimuuliza maswali Mwanamalundi kuhusu nguvu zake na kisha wakamuomba afanye muujiza wa mwisho kabla hajafikishwa gerezani. Mwanamalundi akawaambia askari kuwa bado ana uwezo mkubwa, hata huo mti waliopumzikia anaweza kuukausha. Aliongea maneno hayo huku akiupigapiga mti huo. Kabla hajamalizia sentensi yake kuwa anaweza kuukausha, mti ulikauka palepale na majani makavu yakaanza kudondoka. Askari wa kijerumani waliogopa sana tukio hilo.

Walipofika Tabora mjini, Mwanamalundi na wale watemi wawili waliunganishwa na watu wengine wenye makosa ya uhaini na uhujumu uchumi na kisha kupelekwa kisiwa cha Mafia kutumikia kifungo cha miaka mitatu.

Akiwa gerezani, Mwanamalundi aliwekwa chumba kimoja na mtemi Makongoro Igana. Mtemi Makongoro akamuuliza Mwanamalundi, "Hivi huna namna ya kujiokoa mahali hapa?" Mwanamalundi akamjibu kuwa kwa wakati huo hangeweza kujiokoa, ila kuna miujiza ya shoka na maziwa amemuachia mama yake nyumbani. Mtemi akamuuliza, "Una miujiza mingine yoyote?" Mwanamalundi akamwambia Mtemi Makongoro kuwa yeye (Mwanamalundi) anaweza kupanda viazi na mihogo na ikavunwa ndani ya dakika kadhaa tu na ikawa tayari kabisa kwa chakula. Wakiwa kisiwani hapo, wakakubaliana kwenda ng'ambo ya kisiwa (bara) kisha wakachukue mbegu za viazi na mihogo ili washuhudie miujiza hiyo ya kupanda na kuvuna ndani ya dakika kadhaa.

Kwa kuwa nyakati hizo wafungwa wa visiwani walikuwa wakiachwa huru sababu hawataweza kutoroka, Mwanamalundi na Mtemi Makongoro walienda mpaka baharini ndani ya kisiwa hicho. Makongoro akiwa ameshika jiwe na Mwanamalundi akiwa ameshika fimbo. Makongoro aliporusha jiwe umbali mrefu baharini, Mwanamalundi aliyapiga maji kwa fimbo na kisha maji yakajitenga na kuacha njia mpaka pale lilipotua jiwe. Walifanya hivyo mpaka walivyofika bara (mainland). Wakatafuta mbegu za mihogo na viazi na kuonesheana miujiza.

Kila walipokuwa wakitoroka gerezani, waliacha vivuli vyao vilivyoonekana kama watu halisi. Kuna nyakati Mwanamalundi na Mtemi Makongoro walionekana wakiwa Mwanza au Shinyanga na gerezani pia muda huohuo. Jambo hili liliwachanganya sana wajerumani.

Walipomaliza kifungo chao walirudishwa nyumbani kwao kwa ndege. Jamii ya Mwanamalundi ilipoona ndugu yao amerudishwa kwa ndege wakaamua kumpa jina jipya, "Ng'wenhwandege", wakimaanisha "aliyerudishwa kwa ndege". Mwanamalundi anaaminika kuwa ndie msukuma wa kwanza kupanda ndege.

Wakati anarudishwa nyumbani baada ya kumaliza kifungo chake, mama yake alifurahi sana. Mama yake alifurahi kwa sababu maziwa hayakuganda kwa miaka mitatu jambo ambalo lilionesha kuwa huko aliko alikuwa hai. Maziwa yalibaki katika ubora uleule kwa miaka mitatu. Shoka ilianza kuteremka taratibu kwenye ukuta kadiri Mwanamalundi alivyokuwa akikaribia kufika nyumbani. Alivyofika tu, shoka ilikuwa tayari imefika ardhini kuashiri kuwa muda wowote Mwanamalundi atafika hapo. Na ndivyo ilivyokuwa.

Aliporudi mtaani, Mwanamalundi hakuacha asili yake. Aliendelea kucheza ngoma maeneo mbalimbali. Mtemi Masanja ambae ndie aliesababisha Mwanamalundi kunusurika kunyongwa na hatimae kufungwa, aliamua kumfukuza Mwanamalundi katika himaya ya utawala wake. Mwanamaundi akaamua kuhamia kijiji kiitwacho Seke kwa Mtemi Mahizi ambako akiendelea kucheza ngoma na kufanya miujiza yake.

Akiwa Seke wilayani Kishapu ,mkoani Shinyanga; Mwanamalundi alifanya muujiza uliomuongezea heshima kijijini Seke. Wanakijiji cha Seke waliibiwa ng'ombe wengi sana na Wamasai kutoka Tabora. Wanakijiji wakataka kwenda kufuatilia ng'ombe hao usiku huo huo jambo ambalo Mwanamalundi alikataa. Mwanamalundi aliwahakikishia wanakijiji kuwa ng'ombe hao wapo salama na watarudishwa salama tu kesho asubuhi na sio usiku huo. Wanakijiji walikubali kutokana na kumuamini Mwanamalundi.

Usiku wa siku hiyo, Mwanamalundi akatuma nguvu zake zilizowazingira Wamasai na kisha kuwafanya wasinzie na mifugo hiyo. Hata walipofuatwa asubuhi, walikutwa wamelala fofofo. Wanakijiji wakawaua Wamasai hao na kisha wakarudi na mifugo yao. Mwanamalundi akapewa jina jingine ugenini na kuitwa "Kishosha mang'ombe nga Seke", ikimaanisha "Alierudisha ng'ombe za Seke".

Kuna kipindi, Mwanamalundi alivamia pori la Mtemi wa Ng'hung'hu aitwae Chalya ili achimbe mizizi fulani ya dawa. Mtemi Chalya alipata machale kuwa kuna mvamizi katika mapori yake anachimba mizizi ya dawa. Mtemi akaondoka na kuelekea kule ambako machale yalimuelekeza. Ni kweli, akamkuta Mwanamalundi akichimba mizizi ya dawa fulani. Mtemi akamuuliza Mwanamalundi, "ni kwanini umeingia katika utemi wangu bila kunijulisha?" Mwanamalundi akajibu, "Wewe ni mtemi wa watu wote ila mimi ndie mtemi wa miti yote!" Jibu hilo lilimkwaza Mtemi Chalya ambae aliamua kurudi kwenye himaya yake kwa ghadhabu na kuwaamuru askari wake wamkamate Mwanamalundi ili aadhibiwe.

Askari wakiwa wameambatana na Mtemi Chalya walipofika porini eneo alilokuwepo Mwanamalundi, hawakumkuta. Badala yake waliwakuta simba wengi wakiwa wamelala eneo hilo. Ilibidi watimue mbio kujiokoa wenyewe dhidi ya simba hao walioanza kuwafukuza. Walipofika kwenye himaya ya Mtemi wakiwa salama, walimkuta Mwanamalundi amemaliza kula chakula chao na anaondoka. Ilibidi mtemi amuache tu Mwanamalundi aondoke bila kumbughudhi kwa lolote.

Mwanamalundi alifariki mwaka 1936 kwa maradhi ya kawaida na kuzikwa Ididí Jihū huko kijiji cha Seke wilaya Kishapu mkoa wa Shinyanga akiwa ana umri wa miaka 44. Tukio la kifo chake liliitwa "hang'witulo gwa shigela" ikimaanisha "Vita ya kuwakimbia wamasai". Hii ni kwa sababu wakati Mwanamalundi anakata roho, kulitokea kishindo kikubwa kama tetemeko la ardhi. Watu wengi walikimbia ovyo kwa hofu kuwa labda wamasai wamevamia eneo lao ili kuwaua. Baada ya kishindo hicho, giza likaingia ghafla, giza ambalo hata kuku wakaanza kurudi nyumbani, fisi wakaanza kutembea mitaani wakidhani ni usiku. Hata baada ya mazishi yake, kaburi lake lilifuka moshi mwingi sana uliopanda mpaka juu mawinguni na kutengeneza giza la muda mfupi. Mwanamalundi anakumbukwa pia kwa kuweza kutembea hewani bila kukanyaga ardhi, kujibadili na kuwa kiumbe tofauti kama mnyama, ndege, majani, mti au jiwe na uwezo wake wa kutembea juu ya maji au kuwa ndani ya maji kwa muda mrefu. Mwanamalundi ni mmoja tu wa watu mashuhuri katika tawala za Kisukuma. Kuna watu mashuhuri kabla yake kama akina Níndwa, Italange na Sïta. Hawa wote walikuwa ni watu wa miujiza kama alivyokuwa Mwanamalundi.

Makala hii inasimuliwa na Msukuma halisi na mwanahistoria ya Wasukuma Nghwana Ibengwe Shileki Mazege katika kitabu chake kiitwacho "Miujiza ya akina NG'WANA MALUNDI", toleo la kwanza 2015. Huyu Bwana ana vitabu vingi sana kuhusu historia ya wasukuma.

Kwa maswali yoyote kuhusu makala hii unaweza kuwasiliana nae kupitia:

+255 763 379 387
Share:

LIFAHAMU KABILA LA WASUKUMA...AINA ZA WASUKUMA, MILA NA DESTURI ZA WASUKUMA


WATU WENGI WAMEKUWA WAKILIPONDA KABILA LA WASUKUMA LAKINI HUU NDIO UKWELI KUHUSU WASUKUMA NA HII NDIO HISTORIA YAO TAFADHALI JITAHIDI KUISOMA HADI MWISHO ANGALAU UPATE KITU.

Wasukuma limetokana na neno SUKUMA(KASIKAZINI).Hivyo Msukuma ni mtu wa Kasikazini.

Lakini Wasukuma haimaanishi tu watu wa kaskazini bali wanajumuishwa pia watu wa 

1.Mashariki(Bhanakiya:Ntuzu):Mkoa wa Simiyu.

2.Kusini(Wadakama,hawa wanaweza kuwa Shinyanga ama Tabora kutegemeana upo wapi). 

Msukuma wa Mwanza yeye ndio anaona yupo kaskazini hasa kuliko wote kwa hiyo akiwaita watu wa Shinyanga ni wa Kusini(Wadakama) hawezi kuwa amekosea.

Japo ukiwa Shinyanga napo utawasikia watu wa Shinyanga wakisema wao wapo kaskazini hivyo ni wasukuma na kusini yao ndio kuna wadakama(Mkoa wa Tabora ndio upo kusini).

 Inajulikana zaidi kuwa Wenyeji wa Tabora ni Wanyamwezi.Usukumani hakuna kabila la Wanyamwezi bali wanaitwa Wadakama. Japo ukifika Tabora wilaya ya Sikonge na Urambo hasa yenye Wanyamwezi huku wilaya zingine zikiwa kwa kiasi kikubwa zimekaliwa na wasukuma waliotokea Shinyanga na Mwanza miaka mingi iliyopita.

3.Magharibi(Bhanang'weli). Huku utakutana na Wasumva/Wasumbwa. Hawa ndio wanachukua sehemu ya watu wa Magharibi.

Wasumbwa kama ilivyo kwa Wanyamwezi wao wanaonekana kama si sehemu ya Wasukuma lakini ni sehemu ya wasukuma na karibu kila kitu kinafanana kuanzia lugha,mila na desturi na utamaduni wao.

4.Kaskazini(Wasukuma).
Kwa hiyo Wasukuma wamegawanyika katika pande kuu nne za dunia na jina la pande moja ya Kaskazini ndio lililochukua nafasi ya pande zingine zote.

Kabila la wasukuma linapatikana mikoa mitano Mwanza,Geita,Shinyanga,Simiyu na Tabora.

Hii ni mikoa ya Wasukuma. Japo mkoa wa Tabora unajulikana zaidi kama mkoa wa Wanyamwezi na si wasukuma. Japo wanyamwezi asili kabisa ni wachache na wanachukua wilaya ya Sikonge na Mirambo, wilaya zingine zikikaliwa na Wasukuma kuanzia Igunga na Nzega ama mchanganyiko kama Uyui.

hii ni mikoa asili ambayo wasukuma wanatokea.Lakini Wasukuma wengi pia wanapatikana katika mikoa ya Rukwa,Katavi na Morogoro.Ambapo wamehamia huko kwa ajili ya kufata kilimo na malisho ya mifugo.Wasukuma ndio kabila kubwa zaidi nchini Tanzania likifuatiwa na Kabila la Wahaya na baadae Wachagga.

KILIMO NA MIFUGO.
Wasukuma wanafuga kwa wingi ng'ombe,mbuzi na kwa uchache kondoo.

Kwa harakaharaka wasukuma ndio kabila linalofuga ng'ombe wengi zaidi kati ya makabila yanayofuga.mfano sensa ya mwaka 2002 ilionesha kuwa mkoa uliokuwa na ng'ombe wengi zaidi ulikuwa mkoa wa Shinyanga(Shinyanga+Simiyu kwa sasa).

 Kwa kawaida makabila mengine yote ya wafugaji ukiwatoa wasukuma hakuna kabila lingine ambalo linachukua mkoa mzima. hakuna ubishi kuwa ng'ombe wengi zaidi katika nchi yetu wanamilikiwa na jamii ya wasukuma hasa ukizingatia kuwa mbali na Shinyanga kabla ya kugawanywa bado mkoa wa Mwanza(Mwanza na Geita) na Tabora nayo ilikuwa sehemu ya mikoa ambayo wasukuma wanaishi na kufuga.

Wasukuma pia ni wakulima wa mahindi na mpunga.Zao la biashara Usukumani ni pamba lakini hasa katika wilaya moja ya Maswa iliyopo mkoa wa Simiyu.
MILA NA DESTURI.
Kama ilivyo makabila mengine ya Kiafrika wasukuma wana mila zao na tamaduni zao.Mila za wasukuma zimegawanyika sehemu mbili.

1.Mila za koo ama familia.Hizi hazifanani kabisa kati ya koo na koo.
2.Mila za jumuiya. Hizi zinafana na zinajulikana kwa wanajumuiya/wanachama bila kujali ni wasukuma wa Mwanza,Simiyu(Ntuzu),Tabora(Wanyamwezi),Shinyanga ama wamagharibi(bhanang'weli=wasumbwa).
Jumuiya za mila zipo mbili.

(i)Bhakango,hawa wanafanya kitu kinaitwa bhukango. Mila hizi zinahusu wazazi na watoto wa aina:-

kwanza watoto mapacha. Ukizaa watoto mapacha ni mkosi hivyo lazima ufanye bhukango kuondoa mikosi.wa pili ni watoto waliozaliwa wametanguliza miguu(Kashinje/kashindye). 

Mtoto akitanguliza miguu kwa maana ya kuzaliwa kinyumenyume huo ni mkosi na lazima ufanye bhukango.Wazazi wa mtoto ama watoto mapacha hupelekwa kufanyiwa matambiko maeneo kama mtoni na huko wao watakuwa uchi kabisa huku wakifanyiwa hayo matambiko na wanajumuiya wenzao.

Katika matambiko haya matusi yote husemwa na ndio lugha rasmi inayotumika hata kama wakiwa njiani wanarudi.Matusi ya kutaja majina viungo vya siri hutamkwa bila aibu yoyote mwanzo mwisho.

Kwa wasioshuhudia siku ukibahatika kukutana nao barabarani wanatukana matusi makubwamakubwa njia nzima wala usishangae.
Kwa kawaida kama si mwanajumuiya wa Bhukango hata ukizaa mapacha ama kashinje mila hii hufanyi.Labda mpaka upate mikosi ama matatizo na uelekezwe na wataalamu wa mila kuwa hao mapacha ama huyo kashinje ndio tatizo basi utalazimika na wewe kuwa mwanachama/mwanajumuiya.

Ili uwe mwanachama sharti uzae mapacha,kashinje,ama wewe ni pacha,ama waliokutangulia ni mapacha mfano ni Shija ambaye huzaliwa baada ya mapacha naye ana sifa ya kuwa mkango.
(ii)Bhasweji, hili ni kundi la pili la wanamila wa kisukuma.
Kundi hili ndio hushughulika na matambiko ya kila aina iwe ni kuondoa mikosi,neema ,nk

Hapa si lazima uwe mwanachama wa moja kwa moja kufanya matambiko haya. Ukipata mikosi,laana nk na njia pekee ni ya kuondoa mikosi hiyo ni matambiko basi hawa mabwana watakuja kukufanyia hata kama si mwanachama.Ila matambiko na ngoma watacheza na kufanyia kwako.

Chakula chao hawali kitu kingine zaidi nyama. Fanya ufanyavyo nyama isikosekane. Kama unapika ugali mboga ni nyama. Kama wali mboga ni nyama.Na wanatabia huwa hawaondoki na wanaweza kukaa kwako hata mwezi wanatambika tu.Usipopika nyama siku hiyohiyo wanaondoka.

WASUKUMA NA NDOA.
Ndoa za kisukuma zinaruhusu ndoa za mitaala(mke zaidi ya mmoja).

Kwa kawaida wasukuma huoa kwa mahari ya ng'ombe kati ya ng'ombe 7 mpaka 20. hii ni kawaida.lakinia mahali inaweza kuwa ng'ombe 25 mpaka 70 kutegemeana na mazingira ya anaeolewa na muoaji.Lakini kubwa kuliko yote ni uzuri na tabia nzuri ya mwanamke.

Wasukuma huzaa watoto wengi. Kwa wastani watoto kati ya 6 mpaka 8 ama zaidi na hao ni wa mama mmoja.
WASUKUMA NA WANAWAKE WEUPE.
Ni kweli wasukuma wanapenda wanawake weupe ila weupe natural.

Lakini hili la wanawake weupe si la Wasukuma peke yake bali ukweli ni asimilia kubwa ya wanaume wa makabila yote wanapenda wanawake weupe ila wasukuma ndo wanasingiziwa zaidi utazani wengine hawawapendi wanawake weupe.

CHAKULA CHA WASUKUMA.
Ugali wa mahindi,Ugali wa muhogo na mahindi,Wali,Ugali wa mtama(kipindi cha njaa),maziwa,mboga za kisukuma na nyama. Mboga za kisukuma hasa ni mlenda(rangi=kijani:wakati wa masika),Mkalango(rangi=nyeusi:wakati wa kiangazi) na mzubo(rangi=kijani:wakati wa kiangazi).

NGOMA.
Wasukuma wana aina ya ngoma za burudani zaidi ya 15.

USHAMBA WA WASUKUMA.
Kuna mambo mawili hapa.
1.Wasukuma wana watani wao.
Ushamba wa msukuma umejengwa juu ya watani wa msukuma. Ambapo ni kawaida sana kwa makabila watani wa msukuma kumtania msukuma japo utani unaweza kuwa unabeba sehemu ya ukweli kwa anaetaniwa ila haimaanishi ndo wasukuma wote wapo hivyo.Nje ya makabila watani wa msukuma hata makabila mengine yanatania wasukuma hasa kutokana na ukweli kuwa msukuma kwa kiasi kikubwa hanaga tatizo na jamii yoyote ukiacha wamasai waliokuwa wanatuibia ng'ombe zetu enzi na enzi japo hili sasa ni kama halipo.

2.Maisha ya kijijini. Kama ilivyo makabila mengine wasukuma wengi zaidi wanaishi vijijini na maisha ya vijijini yanafanana kwa karibu makabila yote nchini. kama ni uduni wa mavazi na malazi yanafanana na watu wa vijijini katika jamii zingine,Kama ni kutoyafahamu vyema maisha ya mjini basi ni sawa na watu wa vijijini katika makabila mengine hata kwa watani zetu wagogo.kwa hiyo ieleweke kuwa kila kabila lina washamba na wasio washamba kutegemeana na aina ya ushamba na mazingira ya huyo mshamba.

HAKUNA MAUAJI YANAYOLENGA VIKONGWE BALI KUNA MAUAJI YANAYOLENGA WACHAWI NA ALBINO.

Katika jamii ya wasukuma kama ilivyo jamii zingine kuna wachawi.Suala la wachawi limebakia kuwa suala tete toka enzi na enzi.Utamaduni wa toka zamani kuhusu wachawi ni kuwa ukijulikana ni mchawi uliyeshindikana basi utafukuzwa katika utemi(tawala za kitemizamano)huo na kulazimishwa uvuke temi zingine si chini ya tano.

Na ukikaidi unauawa hadharani na jamii kwa kuwa sehemu kubwa hawapendi uchawi na wachawi. Utamaduni huu wa kuwafukuza wachawi walioshindikana ulikuwa ni wa zamani sana na baadhi ya wachawi walilazimika kuishi kwenye mapango kwa kuwa kila sehemu akienda anakataliwa.

Katika mazingira ya sasa mchawi aliyeshindikana kabisa hafukuzwi kama zamani kwa sababu ya mambo ya sheria bali mtu anayerogwa atajaribu kutafuta dawa za kuzuia uchawi na ikishindikana kabisa basi chaguo la mwisho huwa ni mauaji ambapo atalazimika kukodi watu wa kuua(Kama wahalifu wengine wapo watu wamejiajiri katika uhalifu huu wa kufanya mauaji ya kikatiri kwa hawa wanaodhaniwa ni wachawi).Wanaouwawa huuwawa kwa sababu ya uchawi ila imepotoshwa sana kuwa wanaouwawa ni vikongwe wenye macho mekundu.yapo mauaji mengi yametokea ya watu wasio vikongwe kabisa na wala hawana macho mekundu na pia macho mekundi si ishara ya uchawi usukumani ila imepotoshwa sana na ule wimbo wa kusema ana macho mekundu mleteni hapa ale mapanga.

Mauji ya albino ni jambo ambalo halina taarifa za kina hata kwa wasukuma wenyewe tofauti na mauaji ya wachawi ambayo yanaeleweka kabisa katika jamii ya usukumani.Hakuna taarifa za kueleweka kuhusu jambo hili na huenda ni siri iliyobakia kwa watu wachache miaka mingi.Katika usukumani taarifa za biashara ya viungo vya binadamu zimekuwepo toka zamani lakini zikieleza kuwa biashara za viungo kama ngozi zilikuwa zikiiuzwa kongo kwa ajili ya matumizi ya dawa za kichawi huko.Kuna muda hofu ya wachuna ngozi ilikuwapo kubwa miaka ya 90 na ngozi zilizokuwa zinahusishwa na biashara hiyo ni ngozi za binadamu wa kawaida ambaye si albino.

Swala la albino nalo lilipoibuka taarifa nyingi zilikuwa ni zilezile kuwa viuongo hivyo vina soko kubwa katika nchi ya Kongo. Kuna wakati Kongo iliituhumu Tanzania kuwa biashara ya viungo inafanyika nchini kwetu na wanaouwawa Kongo viungo vinaletwa Tanzania huku na Tanzania pia kuna taarifa kuwa soko ni Kongo.Baadae ikaja kudhihirika kupitia vyombo vyetu vya usalama kuwa waganga wa kienyeji ndio wananunua viungo vya albino. Swala hili bado limebakia kuwa na usiri mkubwa na hakuna taarifa za kueleweka ni nini hasa chanzo chake na soko hili liko wapi?

Ukweli uliowazi ni kuwa mauaji yanatekelezwa na watu wachache waliojivika unyama na kujiajiri katika kazi ya kuua ili wapate kipato chao. Na hawa mtandao wao ni mtandao wa kihalifu na si mtandao wa wasukuma Na ndio sababu ikitokea muuaji akajulikana basi anaweza kuuwawa na wanachi wenye hasira kali kwa kuwa hakuna anayependa haya mauaji katika jamii ya usukumani.ukumbuke pia kuwa kanda ya ziwa ndio ina albino wengi zaidi.

UPOLE WA WASUKUMA.
Mwisho kabisa asili ya wasukuma wengi ni wapole,wakarimu na si wachoyo ama wabahiri kama wengi wanvyofikiria pia siyo washamba kama ambavyo wengi wamekuwa wakisambaza picha halisi lakini pia wasukuma huwa na mapenzi ya ukweli akipenda amependa haswa haswa.

Japo haimanishi kuwa hakuna wakali,wachoyo na wabahiri. Nao wapo japo ni wachache sana.

Share:

HAWA NDIYO WANYAMA WANAKUFA MARA TU BAADA YA KUJAMIIANA


Kupata mwenza unayemtaka sio jambo jepesi hata kidogo wanyama wengi hupoteza uhai pale tu wanapokutana na wale wawapendao na wa muhimu kwao.

Mambo ya kustaajabisha kuhusu wanyama ,tumeangalia kwa ukaribu zaidi mpango wa uzalishaji unaofahamika kama Semelparity au kwa jina lingine uzazi wa kujitoa uhai, mara nyingi wanyama wengi huwekeza nguvu zao nyingi kwenye kuzaliana kabla ya kufa.

Mmoja kati ya wanyama wa kipekee ni panya mdogo aina ya antechinus wanaopatikana huko nchini Australia, mnyama huyu mwenye sifa za kujamiana kwa muda wa saa 14, hali hii inapomtokea kinga ya mwili inaanza kudhoofu na hata kupelekea kifo chake.

Pengine unaweza kuita kujitoa mhanga kwa mzazi, Panya hawa aina ya 'Antechinus' hufariki katika mazingira hayo huku wakifahamu kuwa wameacha mbegu na kuzisambaza mbali zaidi.

"Jambo kubwa hapa ni kwamba spishi hizi zinapokutana huzaa watoto wengi zaidi," Amesema Jeyaraney Kathirithamby,Mtaalamu wa entomolojia katika chuo kikuu cha Oxford.

Upindukaji wa vimelea

Kwa mfano, vimelea vyenye kutofautiana mfumo wa Strepsiptera, wanawake huzalisha kati ya mabuu 1,000 hadi 750,000 katika tendo lao moja walilokutana.

Wanyama hawa wana maisha ya kustaajabisha sana, wanyama wa kike huzika miili yao ndani ya mwili wa nyuki aliyekufa akijificha lakini huzingatia kutokuwa na mabawa,macho, miguu au antenna, huko pia uhifadhi vitoto vyake ambavyo huonekana kama peremende.

Sehemu pekee ya mwili wao ambayo hutoka kwenye mfereji wa mwili wa mdudu aliyekufa ndio hupitishia watoto,njia iliyowazi inamuwezesha mwanaume kupandikiza kwa wakike na mabuu kutoka nje. (Uhusiano: "Upendo wenye mahangaiko: Vimelea vya Kiume unavyowakamata wa kike shingoni kwa kutumia uume,")

Nyuki wa kiume wanaoishi kwa saa nane, ambao huruka akiwa na nyuki jike na hujamiana mpaka kifo kinapowatenganisha, Kathirithamby anasema kwamba, Baada ya mabuu kutoka ndani ya mwili wa mwanamke naye pia hufa.

Maajabu mapenzi ya samaki

Samaki huyu ni maarufu sana kwa kutotolesha mayai mengi sana.

Samaki wa kipasifiki hufa tu baada ya kuzaa-spishi wa chinook husifika kwa kutotolesha mayai mpaka 5,000.

Mikunga kutoka Amerika hutoa mayai mpaka milioni 30 kwa wakati muda mmoja, lakini maisha yao ya kuzalishana bado ni kimaajabu, anasema John Casselman, Mhadhiri wa chuo kikuu Ontario huko Canada.

Aina hii ya samaki huchukua miaka 20 kukua, mara nyingi maisha yao wanaenda mpaka ukingoni chini kabisa mwa bahari na hii inawapa maswali wataalamu kwani wameshindwa kufahamu wanavyozaliana, hata hivyo bado wanafanya uchunguzi wa kina zaidi kuona kama wataweza kupata njia zao.

Samaki huyu yuko hatarini zaidi kupotea kwa sababu nyingi zinazochangiwa na uvuvi wa kupita kiasi na ukarabati wa mabwawa makubwa, ndio maana ni vigumu kufahamu siri zao za kupandana.
Buibui anaejitoa

Buibui wa kike, hupata hisia mbaya pale tu wadudu wengine hatari wa kike wanapoamua kula wenzi wao, lakini buibui aina ya Stegodyphus lineatus yeye huamua kufa kwa ajili ya watoto wake wasidhulike.

Baada ya kundi lake la kwanza la mayai kuanguliwa, "mama huchukua jukumu la kuwatafutia chakula buibui wadogo na kisha kuwaacha wamle yeye," Amesema Catherine Scott, Mwanafunzi wa uzamivu katika chuo kikuu cha Toronto.

Buibui wa kiume huwa na tabia ya kujitolea miili yao ili tu waonekane kuwa wao ndi baba halisi wa buibui hao wadogo.

Buibui wa kiume "wana viungo viwili vya kuhamisha manii,ambavyo hufahamika kama pedipalps," ambayo hutumia kuingizia mmoja baada ya nyingine kwenye sehemu ya buibui wa kike' anasema Scott.

Baada ya kufa, "Mwili wa buibui wa kiume unasia katika nyeti za buibui wa kike na hii huwapa shida buibui wengine pale wanapopata matamanio ya kukutana na buibui huyo.

Buibui wa kiume aina ya Argiope hupendelea kukutana na wale walioteyari yeyuka na mwisho hushindwa kuwala. Lakini inapotokea ni buibui mzee , "Atamla baada tu ya kufa ," Anasema Scott.

CHANZO - BBC SWAHILI
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger