Na Jonas Kamaleki, Dodoma
Serikali imetoa shilingi bilioni 49.5 kuimarisha Shirika la Posta na hadi sasa vituo viwili vinavyotoa huduma za pamoja vimeshaanzishwa Dar es Salaam na Dodoma, kwa awamu hii ya kwanza mikoa 10 itafikiwa ikiwemo vituo 2 Pemba na Unguja, Awamu ya pili itafikia vituo (Mikoa) 17 na lengo ni kuwa ifikapo mwaka 2025 mikoa na wilaya zote za Tanzania ziwe na vituo hivi.
Wiki hii Serikali imefanya uzinduzi wa vituo vya huduma za pamoja katika Shirika la Posta. Uzinduzi huu umefanyika Jijini Dar es Salaam na umefanywa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa.
Hayo yamesemwa leo jijini Dodoma na Mkurugenzi wa Idara ya Habari- MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson msigwa alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari.
“Ningependa kufafanua kidogo kuhusu hizi huduma za pamoja, ni kwamba Serikali imeamua kulifanyia mageuzi makubwa ya kimfumo, kiundeshaji na kiteknolojia Shirika letu Posta ambalo katika miaka ya karibuni lilikuwa hoi biin taabani”, alisema Msigwa.
Moja ya mageuzi hayo makubwa ni kuanzishwa kwa vituo vya huduma pamoja kumwezesha mwananchi kupata huduma mbalimbali za Serikali na zisizo za Serikali katika kituo kimoja. Serikali inataka kupitia vituo hivyo vya huduma pamoja mwananchi akienda pale apate huduma za vitambulisho vya Taifa (NIDA), Huduma za Bima ya Afya, Huduma za Usajili wa Vizazi na Vifo, usajili wa biashara, huduma za kibenki, Huduma za TRA, hifadhi ya jamii na huduma za kusafirisha vifurushi katika kituo kimoja.
Serikali imefanya utafiti na kubaini kuwa kutokana na huduma hizo kutolewa na kila taasisi pekee kivyake, ilikuwa inasababisha usumbufu mkubwa, upotevu mkubwa wa muda na gharama kubwa za watu kufuata huduma. Utafiti umeonesha watu walitumia hadi wiki 4 kupata huduma ambazo sasa zitapatikana katika kituo kimoja kwa muda kati ya dakika chache hadi siku 3.
Aidha, Msigwa amesema kuwa sambamba na hili Serikali inataka Posta iwe shirika linaloendeshwa kisasa. Ukienda kwenye hivi vituo utaona huduma zinatolewa katika madirisha mengi, yaani kila taasisi ina dirisha lake na inatumia mifumo yake. Malengo ya baadaye ni kuwa huduma zile zote zipatikane katika dirisha moja na hiyo itawezekana baada ya mifumo ya kidigitali kuunganishwa.
Lakini huduma zenyewe za Posta zinaboreshwa zaidi ili kwenda kisasa na kidigitali zaidi. Posta hii inakwenda kuwa chombo cha usafirishaji cha kitaifa na kimataifa kama ilivyo vyombo vya mataifa mengine kama DHL, TNT, Royal Cargo n.k, Shirika la Posta linakwenda kuwa Wakala wa mabenki, Bima na taasisi nyingine zinazotoa huduma kwa wananchi, Shirika la Posta tayari limeanzisha Duka Mtandao (www.postashoptz.post) kama ilivyo maduka mtandao ya Alibaba, Amazon, E-bay n.k, na pia Posta inapelekwa kiganjani kwamba sasa Mtanzania na mtu yeyote duniani anaweza kupata huduma za posta kupitia simu ya mkononi. Na Posta ipo kwenye mfumo wa Posta wa Kimataifa na ipo kwa lugha zaidi ya 20.
Ndio Maana unamuona Kaimu Postamasta Mkuu Bw. Macrice Mbodo anatamba kuwa Posta hii sasa sio Posta ya barua tu, bali ni Posta ya Kidigitali. Tayari Serikali imeshatoa shilingi bilioni 3.9 kwa ajili ya kuiwezesha Posta kuimarisha huduma zake za usafirishaji wa vifurushi vya wananchi, aliongeza Msigwa.
“Fursa za kufanikisha jambo hili zipo, Shirika letu la Posta lina ofisi zaidi ya 300 nchi nzima, ni mwanachama wa Umoja wa Posta Afrika na Duniani. Makao Makuu ya Posta Afrika yapo hapa Tanzania pale jijini Arusha. Lakini pia ni washiriki wa Mkutano wa Mawaziri wa Mawasiliano Duniani (hawa ndio Katibu Mkuu wa Posta Duniani na wanatunga sera za Posta), ni wajumbe wa Baraza la Utawala la Posta Duniani ambalo lina wajumbe 40 (hawa ndio wanasimamia utekelezaji wa Sera na Mikakati kutoka kwa Mawaziri) na ni wajumbe wa Baraza la uendeshaji la Posta Duniani (hili ndilo linaendesha shughuli za kila siku za Posta duniani, na zaidi tunaongoza kamati ya biashara mtandao {e-commerce} ya baraza la uendeshaji)”, alifafanua Msigwa.
Mwisho
Sunday, 12 September 2021
Serikali Yatoa Sh. bilioni 49.5 kuimarisha Shirika la Posta
RAIS SAMIA KUZINDUA MKAKATI WA UELIMISHAJI, UHAMASISHAJI MASUALA YA SENSA

WATU 50 WANAODHANIWA KULA CHAKULA CHENYE SUMU SINGIDA WARUHUSIWA KURUDI NYUMBANI
Na Dotto Mwaibale, Singida
WATU 50 waliokuwa wamelazwa Hospitali ya Mkoa wa Singida wakipatiwa matibabu baada ya kunusurika kufa baada ya kula chakula kinachodhaniwa kuwa na sumu wameruhusiwa kurudi nyumbani baada ya afya zao kuhimarika.
Akizungumza mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt.Binilith Mahenge alipowatembelea wananchi hao jana Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Banuba Deogratius alisema juzi walipokea juzi jumla ya wagonjwa 50, Wanawake 34 na Wanaume 16 ambapo hali hadi jana hali zao zilikuwa zikiendelea vizuri na baadhi yao wameanza kuwaruhusu kurudi nyumbani kuendelea na majukumu yao ya ujenzi wa Taifa.
Banuba alisema wakazi hao wa Kata ya Unyambwa Kijiji cha Kisasida katika Manispaa ya Singida mkoani hapa walifikishwa hospitalini hapo baada ya hali zao kuwa mbaya kutokana na kula chakula kilichoandaliwa katika shughuli za ufunguzi wa Madrasa moja Katika kijiji hicho.
Akipokea taarifa hiyo Mkuu wa Mkoa Singida Dkt Bilinith Mahenge aliwapongeza madaktari wa Hospitali hiyo kwa jitihada walizozifanya za kuhakikisha wananusuru maisha ya wananchi hao ambapo kwa sasa hali zao zinaendelea vizuri na kuipongeza Serikali kwa kuweka miundombinu mizuri ya huduma katika sekta ya afya.
Alitoa wito kwa viongozi wa Serikali na Dini kuwajibika kikamilifu katika kutoa elimu ya namna ya kuandaa chakula pamoja na kusimamia inapotokea sherehe mbalimbali kwenye maeneo yao ili kuepuka madhara ya namna hiyo yasije kutokea tena.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida Kamishna Msaidizi (ASP) Stella Mutabihirwa alisema wanawashikilia watu saba kuhusika na tukio hilo.
" Tuna walishiriki watu saba ambao waliandaa chakula hicho na uchunguzi ukikamilika tutatoa taarifa kamili kwa sasa tayari tumechukua mabaki ya chakula hicho kwa ajili ya kuyachunguza," alisema Mutabihirwa.
Alisema katika tukio hilo mtoto mmoja mwenye umri wa miaka (7) aliye mtaja kwa jina la Fahad Masoud alifariki dunia kabla ya kufikishwa hospitali kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
Watumishi Wa TRA , Wadau Wa Kodi Waelimishwa Mabadiliko Ya Sheria Za Kodi
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inaendelea kutoa elimu ya mabadiliko ya sheria za kodi ya mwaka 2021 kwa watumishi wa mamlaka hiyo, wadau na walipakodi katika mikoa mbalimbali hapa nchini.
Akizungumza na watumishi, wadau na walipakodi hao katika mikoa ya Simiyu na Mara, Afisa Msimamizi wa Kodi kutoka TRA Makao Makuu Dar es Salaam Bw. Zakeo Kowero alisema kwamba, lengo la kutoa elimu hiyo ni kuwa na uelewa mmoja kwa watumishi wa TRA na kwa upande wa walipakodi na wadau ni kuwafahamisha mabadiliko yaliyotokea ili kuongeza uhiari wa ulipaji kodi.
“Tumeamua kuzunguka kutoa elimu hii ya mabadiliko ya sheria za kodi yaliyofanywa na Serikali katika mwaka wa fedha 2021/22 ili kuhakikisha watumishi tunakuwa na lugha moja wakati tunapowahudumia wateja wetu na kwa upande wa wadau na walipakodi ni kuwafahamisha kuhusu mabadiliko yaliyotokea,” alisema Kowero.
Kati ya mabadiliko yaliyotokea ni pamoja na kuongeza idadi ya waajiriwa kwenye Kodi ya Kuendeleza Mafunzo ya Ufundi Stadi (SDL) kutoka wafanyakazi wanne hadi kumi lakini uwasilishaji wa ritani utaendelea kama kawaida bila kujali idadi ya watumishi.
Eneo lingine lililofanyiwa mabadiliko katika kodi hii ya uendelezaji mafunzo ya ufundi stadi ni la taasisi za kidini ambapo zimesamehewa kulipa kodi kwenye huduma za afya ya umma.
“Lengo la kuongeza idadi ya waajiriwa ni kuwapunguzia mzigo waajiri wadogo ili kukuza mitaji yao na dhumuni la kutoa msamaha kwenye taasisi za dini ni kuzipa unafuu katika kutoa huduma kwa jamii,” alibainisha Kowero.
Akizungumzia mabadiliko yaliyofanyika katika Kodi ya Majengo alisema kwamba, viwango vimeongezeka kwenye nyumba za kawaida katika Majiji, Manispaa na Halmashauri za Miji kutoka shilingi 10,000 hadi shilingi 12,000 kwa mwaka.
Kwa upande wa kila sakafu ya nyumba za ghorofa katika majiji, manispaa, halmashauri za miji, kodi imeongezeka kutoka shilingi 50,000 hadi shilingi 60,000 kwa mwaka na kwa nyumba za ghorofa zilizoko katika halmashauri za wilaya, kodi imeongezeka kutoka shilingi 20,000 hadi shilingi 60,000 kwa jengo zima kwa mwaka.
“Hata hivyo, Serikali imebadilisha njia ya utozaji kodi hii ambapo kwa sasa kodi ya majengo inalipwa kupitia njia ya ununuzi wa umeme wa LUKU kwa kukata shilingi 1,000 kwa mwezi kwa nyumba za kawaida na shilingi 5,000 kwa mwezi kwa nyumba za ghorofa,” alieleza Kowero.
Kwenye Sheria ya Usajili wa Vyombo vya Moto, Serikali imepunguza kodi ya usajili wa namba binafsi kutoka shilingi 10,000,000 hadi shilingi 5,000,000 na usajili huo utadumu kwa miaka mitatu. Lengo la mabadiliko hayo ni kuwavutia watu kusajili vyombo vyao vya moto na hivyo kuongeza mapato ya serikali.
Mabadiliko mengine yamefanyika kwenye sheria ya Ushuru wa Stempu kwa mfano, ushuru wa stempu katika nyaraka mbalimbali umeongezeka kutoka shilingi 500 hadi shilingi 2000.
Naye, Danieli Singiri mmoja wa viongozi wa Vyama vya Msingi vya Ushirika wa mkoani Simiyu waliohuduria semina ya mabadiliko ya sheria mkoani humo, alisema amefurahishwa na elimu hiyo na ameiomba serikali kuangalia kifungu kipya cha kodi ya zuio ya asilimia mbili iliyowekwa kwenye mazao ya kilimo kwani kitawaumiza wakulima.
“Tumefurahi kwa kutupatia elimu hii muhimu lakini tunaiomba serikali iangalie kodi ya zuio ya asilimia mbili kwenye mazao ya kilimo kwani itawadidimiza wakulima kwasababu watapokea fedha pungufu japokuwa lengo la kodi hii ni zuri na imelenga kuongeza mapato ya serikali hata hivyo nashauri itafutwe njia nyingine tofauti na hii,” alisema Singiri.
Elimu ya mabadiliko ya sheria za kodi imekwishatolewa katika mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma, Singida, Tabora, Kigoma, Manyara, Arusha, Kilimanjaro na Tanga. Kwa sasa elimu hiyo inaendelea kutolewa katika mikoa ya Simiyu, Mara, Mwanza, Mbeya, Songwe, Rukwa na Katavi.
Mwisho.
MGEJA AWAPONGEZA MACHIFU KUMSIMIKA RAIS SAMIA 'KUWA CHIFU MKUU WA MACHIFU TANZANIA

BETWAY YAZINDUA KITUO CHA KUSHUHUDIA MICHEZO TANZANIA
Kampuni ya kimataifa ya michezo ya kubashiri, Betway imechukua hatua kubwa katika kuongeza thamani kwenye sekta ya michezo nchini Tanzania. Betway imezindua kituo cha kisasa cha kushuhudia michezo na kubashiri kistaarabu ‘Betway Sports Experience Center.’
Kituo hicho cha kipekee na cha aina yake ni sehemu itakayowakutanisha wapenzi wa michezo kushuhudia michezo mbalimbali na kufanya ubashiri katika mazingira ya kuvutia.
Kituo hiki ambacho kimepewa jina la Dimba la Betway kitakuwa pia ni kituo cha elimu kuhusu michezo na namna ya kubashiri kistaarabu. Kituo hicho kipo ndani ya ofisi za Betway zilizopo Mbezi Beach, Dar es salaam.
Eneo hili la Betway limewekewa vifaa vya kisasa ikiwemo simu janja na kompyuta maalumu kwa ajili ya wateja kujisajili na kufanya ubashiri wa michezo inayoendelea mubashara.
Kituo hicho kimefungwa skrini maalumu za runinga zinazoonesha michezo mubashara inayochezwa kwa wakati huo na kutoa nafasi kwa wateja kufuatilia matokeo ya mechi hizo. Pia, kituo hicho kinatoa nafasi kwa wateja kucheza michezo ya kasino na michezo mingine ya ubashiri.
Ndani ya dimba la Betway mashabiki wa michezo watapata nafasi ya kukutana na kuwasiliana moja kwa moja na timu ya Betway kwa uhuru na katika mazingira mazuri zaidi.
Pia, kituo hiki kinatoa nafasi ya wateja kuuliza maswali, kusajili akaunti mpya, na kufanya ubashiri kwa kutumia simu na kompyuta zilizopo ndani ya kituo.
Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi, Meneja Uendeshaji wa Betway Tanzania, Jimmy Masaoe alisema kuwa uzinduzi wa kituo hicho cha ni sehemu ya juhudi za kampuni hiyo kuongeza thamani katika sekta ya michezo nchini.
"Sisi (Betway) tuna furaha kubwa kuzindua kituo hiki cha kipekee na muhimu kwa mashabiki wa michezo nchini Tanzania kuweza kukutana na kufurahia kwa pamoja na kwenye mazingira ya kuvutia.
Hii ni sehemu ya ahadi yetu - kuongeza thamani katika michezo ya kubashiri na sekta ya michezo kwa ujumla kwa sababu kituo hiki kitakuwa kama kitovu cha michezo ambapo mashabiki wataweza kukutana, kutazama michezo, na kufanya ubashiri wao kwa njia bora ambayo haijawahi kutokea hapo awali," alisema.
Akizungumza na wadau wa michezo pamoja na wanahabari waliohudhuria tukio la uzinduzi, Jimmy alisema kuwa Betway inafanya kazi kutimiza ahadi zake za kukuza maendeleo ya michezo nchini Tanzania kama ilivyoahidi wakati ikiingia nchini na kuwahakikishia wote kuwa Kampuni hiyo itaweza kuwaongoza wateja wake katika kuiishi na kuitimiza kauli mbiu ya "Bashiri Kistaarabu" kwa kuwaonyesha wateja wake kwa vitendo.
"Sisi Betway tunajivunia kuhamasisha wateja wetu wote kubashiri kistaarabu. Tutatumia kituo hiki kama kituo cha kuelimisha mashabiki wa michezo nchini Tanzania kuhakikisha wanaielewa na kuikubali dhana ya kubashiri kistaarabu. Tunawakaribisha mashabiki wa michezo kufika katika kituo hiki kujionea na kufurahia maana halisi ya michezo,'' aliongeza.
Kama sehemu ya hafla ya uzinduzi, wahudhuriaji walifurahia uchambuzi wa moja kwa moja wa michezo ya Ligi Kuu ya Uingereza iliyochezwa siku ya Jumamosi.
Uchambuzi kutoka kwa wachambuzi maarufu wa michezo nchini Tanzania, Maulid Kitenge, na Edo Kumwembe uliwavutia mashabiki wadau waliohudhuria hafla hiyo.
Wahudhuriaji pia walishiriki katika mashindano ya michezo kama vile utabiri wa matokeo na wafungaji wa mabao, na kuweza kujipatia zawadi mbalimbali kutoka Betway.
Michael Valentine, aliyejitambulisha kuwa ni shabiki wa timu ya Manchester United alikuwa ni moja ya waliohudhuria katika hafla hii na kueleza kuwa alijionea utofauti mkubwa katika kituo hicho cha Betway. Michael pia ameunga mkono hatua ya kampuni ya Betway kuwekeza nchini Tanzania na kuitaka iendelee kutoa huduma za kipekee.
“Mimi ni shabiki mkubwa wa michezo, kwa muda mwingi nimekuwa nikiwaona Betway kwenye vyombo vya habari kupitia timu za ligi kuu ya Uingereza zinazofadhiliwa na Betway, na furaha kuona wamekuja nyumbani Tanzania,” alisema.
Pia, aliongeza kwa kusema “sijawahi kuona kituo kama hiki nchini, kituo hiki ni cha kwanza hapa Tanzania na natumaini kitachochea uwekezaji mkubwa zaidi kwenye sekta ya michezo, na mashabiki watafurahia sana Betway kuanzisha shughuli zake nchini”.
Kituo hiki cha Betway kitakuwa kikifunguliwa katika siku zote 7 za wiki kuanzia asubuhi saa 3:00 hadi 5:00 usiku.
JAMAA ADAIWA KUWAUA WATOTO WAKE BAADA YA KUGOMBANA NA MKEWE

TAMBUA DALILI ZA KUISHIWA NGUVU ZA KIUME NA TIBA YAKE
WATUMISHI WA TRA, WADAU WA KODI WAELIMISHWA MABADILIKO YA SHERIA ZA KODI





WAZIRI BITEKO: MICHEZO NI AFYA TUSHIRIKIANE KWA PAMOJA
Waziri Biteko akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa Bonanza kutoka Wizara na Tume ya Madini katika Bonanza hilo lililofanyika Septemba 11, 2021 katika viwanja vya Kilimani jijini Dodoma.
IMEELEZWA kuwa, michezo inaleta afya, akili , urafiki na kuwaweka pamoja Wafanyakazi wa Wizara pamoja na Taasisi zake.
Hayo yamebainisha leo Septemba 11, 2021 na Waziri wa Madini, Doto Biteko wakati wa ufunguzi wa Bonanza ya Wizara ya Madini na Tume ya Madini lililofanyika katika Viwanja vya Kilimani, Jijini Dodoma.
“Nawapongeza Wafanyakazi wote kwa kujitokeza kwa wingi kushiriki katika michezo mbalimbali , tuendelee kufanya mazoezi ili tuweze kupata nguvu ya kuendelea kufanya kazi ya kulinda rasilimali zetu na kukuza Uchumi wa Nchi,” amesema Waziri Biteko.
“Nimechezesha vizuri mechi ya mpira wa miguu kama refa bila upendeleo wowote , niendele kuwapongeza wachezaji kwa kuwa mahiri na kucheza vizuri,” ameongeza Waziri Biteko.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof. Idris Kikula amewapongeza washiriki wa Bonanza na kuwataka waendelee kufanya mazoezi mara kwa mara maana michezo ni furaha.
Naye, Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Mhandisi Yahya Samamba amesema Mhe. Rais Mama Samia Suluhu Hassan, anawasisitiza watu wafanyemazoezi kwa kuwa ni moja kati ya kinga ya kuufanya mwili kuwa imara ili kukabiliana na magonjwa mbalimbali.
“Msisitizo kutoka kwa Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa ni kwamba Wizara na Taasisi zote za Serikali zifanye mazoezi kwa pamoja, na mazoezi hayo ni maandalizi ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) ambayo yamerudishwa na Serikali,”amesema Mhandisi Samamba ”.
Kwa upande wake, Kamishna wa Tume ya Madini, Janet Ruben amesema kuwa watu wapo ofisini lakin ukija kwenye mazoezi wapo, rai yangu tusiache mazoezi tushirikiane na kuwa pamoja Wizara na Tume ya Madini.
RAIS MWINYI ATUMA SALAMU ZA POLE KUFUATIA KIFO CHA JAJI WA MAHAKAMA KUU ZANZIBARI HAJI OMARI HAJI
Saturday, 11 September 2021
WAPENZI WAKUTWA WAMEFARIKI WAKIDAIWA KUNYWA JUISI YA SUMU

MO DEWJI: HANS POPE ALIKUWA NA WEMA WA KIPEKEE

























