Tuesday, 8 June 2021

DKT. MAHENGE AWATAKA WATUMISHI KUSHIRIKIANA ,WANA CCM KUVUNJA MAKUNDI


Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge akiongea na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama katika ziara yake ya kikazi ya kukagua miradi ya maendeleo.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge (kushoto) akimkabidhi Mkuu wa wilaya wa Mkalama Mhandisi Jackson Masaka funguo ya gari la kubebea wagonjwa  katika Zahanati ya Wilaya ya Mkalama.
Wananchi wa kata ya Mwangeza  Kijiji Cha Hilamoto  walivyompokea Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge kwa zawadi ya Mbuzi.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge (kulia) akisikiliza maelezo wakati akikagua jengo la wodi ya wazazi katika Zahanati ya Wilaya ya Mkalama.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi ( CCM) Wilaya ya Mkalama  Lameck Itungi  akichangia jambo 
Mwenyekiti wa Halmashauri  ya Mkalama James Mkwega  akiomba jambo kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge


Na Edina Alex, Singida

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge amewataka watumishi wa umma kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuongeza ukusanyani wa mapato ya ndani.

Hayo yamejiri wakati alipokutana na kuongea na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Makalama kwenye ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo.

"Kama hukufanya vizuri wakati wa mtangulizi wangu sasa anza na Mahenge kwa kufanya kazi kwa bidii tusikate tamaa", alisema Mahenge.

Alisisitiza kuwa suala la ukusanyaji wa mapato ya ndani sio la mzaha na linamhusu kila mtu katika Mkoa wa Singida.

Aidha aliwataka watumishi na Chama Cha Mapinduzi ( CCM) kuvunja makundi yao na kuleta mabadiliko na kuendana na kasi ya Rais wa awamu ya sita Mhe. Samia Hassan Suluhu.

Akitoa taarifa ya maendeleo ya Wilaya,  Mkuu wa wilaya wa Mkalama Mhandisi Jackson Masaka alisema Wakazi wa Mkalama wanakabiliwa na changamoto ya pembejeo ambayo iko juu hasa katika mbegu bora ya alizeti chotara ya Hysun 33 ambayo huuzwa kwa sh. 35,000 kwa kilo moja.

Aidha Masaka alisema Wilaya ya Mkalama ina changamoto ya maafisa ugani ,Magari na pikipiki na wakulima kutotumia vizuri mvua kidogo inayonyesha katika Wilaya hiyo.

Share:

Monday, 7 June 2021

BENKI YA MAENDELEO TIB YANG'AA KWENYE MAONESHO YA BIASHARA TANGA





Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga, Pili Hassani Mnyima akimkabidhi Cheti Afisa Mwandamizi wa Miradi kutoka Benki ya Maendeleo TIB, Sonia Mlaki (kushoto) baada ya Benki hiyo kushika nafasi ya kwanza katika kipengele cha Benki zenye huduma zenye tija za maendeleo ya nchi kwa ujumla wake tofauti na benki  zingine zilizoshiriki maonyesho hayo ya biashara ya 8 yaliyofanyika kitaifa mkoani Tanga. TIB Development Bank pia imeshika nafasi ya tatu katika kipengele cha huduma za bima. 
Afisa Mwandamizi wa Miradi kutoka Benki ya Maendeleo TIB, Sonia Mlaki  akionesha cheti
Afisa Msimamizi wa miradi kutoka Benki ya Maendeleo TIB Sonia Mlaki akiwa na Afisa Mwandamizi Idara ya Masoko na Mahusiano Carlos Nathaniel Ntangeki kwenye Maonyesho ya biashara ya 8 ambayo kitaifa yamefanyika mkoani Tanga.
Share:

BENKI YA CRDB, NHIF & KACU WATIA SAINI YA MAKUBALIANO YA BIMA ZA AFYA KWA WAKULIMA


Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika Kahama (KACU) , Emmanuel Cherehani (kushoto) Mkurugenzi Mkuu wa Biashara Benki ya CRDB, Dkt.  Joseph Witts (katikati) na Kaimu Mkurugenzi wa Huduma kwa Wanachama Mfuko wa Taifa Bima ya afya NHIF Hipoliti Lelo wakionesha nyaraka baada ya kutia saini Makubaliano ya Bima ya Afya kwa wakulima baina ya benki ya CRDB, NHIF na KACU
***
 Na Kadama Malunde na Mavala - Kahama
Mkuu wa Wilaya Kahama Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha ameshuhudia utiaji saini wa makubaliano ya Bima ya afya kwa wakulima baina ya benki ya CRDB,NHIF na Chama Kikuu Cha Ushirika Kahama (KACU)

Akizungumza wakati wa utiaji saini huo leo Jumatatu Juni 7,2021 Mkurugenzi Mkuu wa Biashara Benki ya CRDB Dkt. Joseph Witts amesema Benki ya CRDB imeamua kuwashika mkono wakulima kwa kuwalipia gharama zote zinazohusu huduma za afya na mkulima atalipia pindi atakapovuna mazao yake.

"Kupitia Mpango huu unaolenga kurahisha huduma za bima ya afya kwa wakulima, baada ya mavuno mkulima atarejesha malipo hayo bila riba yoyote baada ya kuuza mazao yao ambapo tunaanza kuwapatia bima ya afya Wakulima 590 wa tumbaku na wakulima 6800 wa pamba, jumla wakulima 7390", amesema Dkt.Witts.

"Mkulima akiwa anadunduliza anaweka kidogo kidogo katika benki yetu ya CRDB fedha zitakaa vile vile bila makato hata ya shilingi moja", ameongeza Dkt. Witts.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Huduma kwa wanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya afya NHIF Bw. Hipoliti Lelo amesema licha ya NHIF kuwa na jukumu la kuwafuata wanachama kukusanya michango na kuwapa matibabu wameamua kuwarahisishia wateja wao kwa kuwapa njia rahisi ya kulipa michango yao akibainisha kuwa ukiwa na Bima itagharamia matibabu ya familia nzima.

Kaimu Mrajisi wa Mkoa wa Shinyanga Hilda Boniface amewapongeza benki ya CRDB na NHIF kwa huduma hiyo huku akisisitiza kuwa kumekuwa na changamoto za wakulima wa tumbaku katika ulipaji wa mikopo kwa kuwa NHIF baada ya kutoa huduma isije ikawa kilio kwa Benki ya CRDB.

"Tuweke mikakati mizuri namna mikopo itavyolipwa ili isije ikawa mzigo kwa Benki ya CRDB", amesema Hilda.

Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika Kahama (KACU) Emmanuel Cherehani ameeleza kufurahishwa na hatua zilizochukuliwa na Benki ya CRDB na NHIF katika kusaidia wakulima na kuahidi kuwa atatoa ushirikiano wa hali ya juu ili kufanikisha adhma ya mkulima kupata matibabu na kulipa malipo taratibu na bila shida yoyote.

"Wakulima wote watakaokuwa wameandikishwa kwenye mfuko huu tuhakikishe wana uwezo mzuri wenye kilimo kikubwa na kidogo ili tuwavute wengi" ,amesema Cherehani.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya Kahama Mhe. Anamringi Macha amesema moja ya changamoto kubwa katika wilaya ya Kahama ni hamasa na uelewa wa wananchi kujiunga na bima ya Afya akibainisha kuwa kama mkuu wa wilaya amekuwa akipiga kampeni kubwa ili kuhakikisha wananchi wanajiunga na bima ya afya kitu ambacho ni kizuri na kinapunguza gharama za matibabu pindi wana familia wanapoumwa.

Licha ya kuwapongeza CRDB,NHIF na KACU amewaomba waendelee kutoa hamasa kwa wananchi wajiunge na huduma za afya.

"Kwa mazingira ya sasa magonjwa ni mengi na gharama za matibabu ni kubwa kwa hiyo suala la kuwa na Bima ni muhimu sana. Naomba viongozi tuendelee kuhamasisha wananchi kujiunga na bima ya afya kwani wapo baadhi ya viongozi wamekuwa wakipotosha kuhusu huduma za afya kitu ambacho kinapelekea wananchi kutokuwa na maamuzi sahihi," amesema Macha.
Mkurugenzi Mkuu wa Biashara Benki ya CRDB, Dkt.  Joseph Witts akitia saini Makubaliano ya Bima ya Afya kwa wakulima baina ya benki ya CRDB,NHIF na KACU uliofanyika leo Jumatatu Juni 7,2021 Mjini Kahama
Mkurugenzi Mkuu wa Biashara Benki ya CRDB, Dkt.  Joseph Witts  (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi wa Huduma kwa Wanachama Mfuko wa Taifa Bima ya afya NHIF Hipoliti Lelo  wakitia saini Makubaliano ya Bima ya Afya kwa wakulima baina ya benki ya CRDB,NHIF na KACU
Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika Kahama (KACU), Emmanuel Cherehani akitia saini Makubaliano ya Bima ya Afya kwa wakulima baina ya benki ya CRDB, NHIF na KACU . Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Kahama, Mhe. Anamringi Macha akishuhudia utiaji saini
Mkurugenzi Mkuu wa Biashara Benki ya CRDB, Dkt.  Joseph Witts akibadilisha nyaraka na Kaimu Mkurugenzi wa Huduma kwa Wanachama Mfuko wa Taifa Bima ya afya NHIF Hipoliti Lelo wakati wa kutia saini Makubaliano ya Bima ya Afya kwa wakulima baina ya benki ya CRDB, NHIF na KACU
Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika Kahama (KACU) , Emmanuel Cherehani (kushoto) akibadilishana nyaraka na Mkurugenzi mkuu wa biashara Benki ya CRDB, Dkt.  Joseph Witts wakati wa kutia saini Makubaliano ya Bima ya Afya kwa wakulima baina ya benki ya CRDB, NHIF na KACU
Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika Kahama (KACU) Bwana Emmanuel Cherehani (kushoto) akibadilishana nyaraka na Kaimu Mkurugenzi wa Huduma kwa Wanachama Mfuko wa Taifa Bima ya afya NHIF Hipoliti Lelo wakati wa kutia saini Makubaliano ya Bima ya Afya kwa wakulima baina ya benki ya CRDB, NHIF na KACU
Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika Kahama (KACU) , Emmanuel Cherehani (kushoto) Mkurugenzi Mkuu wa Biashara Benki ya CRDB, Dkt.  Joseph Witts  (katikati) na Kaimu Mkurugenzi wa Huduma kwa Wanachama Mfuko wa Taifa Bima ya afya NHIF Hipoliti Lelo wakionesha nyaraka baada ya kutia saini Makubaliano ya Bima ya Afya kwa wakulima baina ya benki ya CRDB, NHIF na KACU 
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha akizungumza wakati wa utiaji saini Makubaliano ya Bima ya Afya kwa wakulima baina ya benki ya CRDB, NHIF na KACU
Kaimu Mrajisi mkoa wa Shinyanga Hilda Boniface akizungumza wakati wa utiaji saini Makubaliano ya Bima ya Afya kwa wakulima baina ya benki ya CRDB, NHIF na KACU
Mkurugenzi mkuu wa biashara Benki ya CRDB, Dkt.  Joseph Witts  akizungumza wakati wa utiaji saini Makubaliano ya Bima ya Afya kwa wakulima baina ya benki ya CRDB, NHIF na KACU
Kaimu Mkurugenzi wa Huduma kwa Wanachama Mfuko wa Taifa Bima ya afya NHIF Hipoliti Lelo akielezea umuhimu wa bima ya afya wakati wa utiaji saini Makubaliano ya Bima ya Afya kwa wakulima baina ya benki ya CRDB, NHIF na KACU
Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika Kahama (KACU) Bwana Emmanuel Cherehani akizungumza wakati wa utiaji saini Makubaliano ya Bima ya Afya kwa wakulima baina ya benki ya CRDB, NHIF na KACU
Mkuu wa Wilaya Kahama, Mhe. Anamringi Macha (katikati) akiwa na viongozi wa Benki ya CRDB,NHIF na KACU katika hafla ya utiaji saini makubalinao ya Bima ya afya kwa wakulima kati ya benki ya CRDB,NHIF na KACU
Mkuu wa Wilaya Kahama, Mhe. Anamringi Macha ,viongozi wa Benki ya CRDB,NHIF na KACU pamoja na wadau wa kilimo wakipiga picha ya kumbukumbu
Mkuu wa Wilaya Kahama, Mhe. Anamringi Macha ,viongozi wa Benki ya CRDB,NHIF na KACU pamoja na wadau wa kilimo wakipiga picha ya kumbukumbu
Mkuu wa Wilaya Kahama, Mhe. Anamringi Macha ,viongozi wa Benki ya CRDB,NHIF na KACU pamoja na wadau wa kilimo wakipiga picha ya kumbukumbu


Share:

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Kufungua Dirisha La Maombi Ya Mikopo Julai Mosi Mwaka Huu


BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetangaza kuwa dirisha la maombi ya mikopo kwa wanafunzi wa Elimu ya juu kwa mwaka 2021/2022 linatarajia kufunguliwa Julai Mosi mwaka huu.

Akizungumza katika hafla ya utiaji saini wa hati ya makubaliano baina ya HESLB na Wakala wa Usajili, Ufuilisi na Udhamini (RITA) iliyofanyika leo Jumatatu (Juni, 7, 2021), Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Abdul-Razaq Badru alisema kabla ya kufunguliwa kwa dirisha la maombi HESLB, itatoa mwongozo wa uombaji mikopo unaotarajiwa kutolewa Juni 25 mwaka huu.

Aidha Badru alisema ofisi yake imekamilisha maandalizi yote kwa ajili ya msimu mpya wa masomo wa mwaka 2021/2021 na kuwataka wanafunzi wahitaji kutumia muda uliopo kwa ajili ya kukamilisha taratibu mbalimbali za uombaji mikopo.

“Tunawasihi wanafunzi kusoma kwa makini mwongozo wa uombaji mikopo utakaopatikana katika tovuti yetu (www.heslb.go.tz) ambao utachapishwa katika lugha ya kiingereza na Kiswahili, kabla ya kufungua dirisha la maombi mwanafunzi anapaswa kusoma mwongozo huu” alisema Badru.

Kuhusu bajeti ya mikopo, Badru alisema katika mwaka wa masomo 2021/2022 Serikali imetenga kiasi cha TZS 500 Bilioni kwa ajili ya mikopo ya elimu ya juu inayotarajia kunufaisha jumla ya wanafunzi 160,000.

Akifafanua kuhusu hali ya utoaji mikopo kwa mwaka wa masomo 2020/2021, Badru alisema hadi kufikia Juni mwaka huu jumla ya wanafunzi 149,472 wamepangiwa mikopo yenye thamani ya TZS 464 Bilioni, Kati yao, wanafunzi 55,337 ni wa mwaka wa kwanza na wengine 94,135 wanaoendelea na masomo.

Kwa upande wa urejeshaji mikopo, Badru alisema hadi kufikia mwezi Mei mwaka huu, HESLB ilikusanya kiasi cha TZS 168 Bilioni, ambayo ni sawa na 88.4% ya lengo la kukusanya TZS 190 Bilioni katika mwaka wa fedha 2020/2021.

Kwa upande wake, Kaimu Afisa Mtendaji wa RITA, Emmy Hudson alisema Ofisi imekamilisha hatua mbalimbali za kuwawezesha wanafunzi wahitaji ikiwemo kutoa mwongozo wa uhakiki wa vya kuzaliwa ambavyo ni moja ya nyaraka muhimu zinazohitaji wakati wa kuomba mikopo.

Aliongeza kuwa hadi sasa RITA imepokea jumla ya maombi 13,938 ya uhakiki wa vyeti vya kuzaliwa, ambapo kati yao maombi 7334 tayari yamehakikiwa, hivyo kuwataka wazazi na wanafunzi kutumia muda uliopo kwa ajili ya kukamilisha uhakiki wa nyaraka hizo.

Aidha Emmy alisema RITA itafanyia kazi maelekezo yote yaliyotolewa na kuimarisha ushirikiano na HESLB ikiwemo kuimarisha mifumo ya Tehama inayolenga kuondoa changamoto mbalimbali zinazowakabili wanafunzi wakati wa uombaji mikopo ya elimu ya juu.

MWISHO


Share:

Ufunguzi Wa Umitashumta Na Umisseta 2021- Mtwara


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa, Kassim Majaliwa Majaliwa kesho Juni 8, 2021 anatarajia kufungua Mashindano ya Michezo na Taaluma kwa Shule za Msingi (UMITASHUMTA) na Sekondari (UMISSETA) kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.

Mashindano haya yanajumuisha mikoa yote kutoka Tanzania Bara na Visiwani ambapo yatafanyika kwenye viwanja vya Nangwanda Sijaona, Chuo cha Walimu Mtwara (TTC kawaida) Chuo cha Walimu Ufundi maarufu kama Mwasandube, na viwanja vya Shule ya Sekondari ya Ufundi Mtwara ambapo yanaanza kesho Juni 08, 2021 na kumalizika Julai 03, 2021. Mashindano yameandaliwa na Wizara tatu zinazohusika na Elimu, Habari na TAMISEMI chini ya Kamati ya Uratibu ya Kitaifa ya Makatibu Wakuu wa Wizara hizo.

Michezo itakayoshindaniwa kwa upande wa UMITASHUMTA ni mpira wa miguu kwa wasichana na wavulana, mpira wa miguu maalum kwa wavulana (wenye ulemavu wa kusikia) mpira wa pete, mpira wa goli kwa wasichana na wavulana wasioona na wenye uoni hafifu, mpira wa wavu kwa wasichana na wavulana, mpira wa mikono kwa wasichana na wavulana, mpira wa meza kwa wasichana na wavulana, riadha jumuishi, kwaya na ngoma.

Kwa upande wa UMISSETA michezo itakayochezwa ni yote ya UMITASHUMTA pamoja na mchezo wa mpira wa kikapu kwa wasichana na wavulana isipokuwa mchezo wa mpira wa goli, aidha kutakuwa na mashindano ya usafi katika mazingira wanayoishi. Mashindano yatapambwa na wasanii wa kizazi kipya kama Ibrah kutoka Konde Gang, Beka Flavour, Dulla Makabila, Linah Sanga na Peter Msechu na kwa upande wa taarabu Mzee Yussuf pia atakuwepo ili kutoa hamasa na burudani. Pia vyama vya michezo, mashirikisho na vilabu vya michezo mbalimbali vimealikwa kuja kuangalia vipaji mbalimbali.


Share:

Balozi Mulamula Akutana Na Kufanya Mazungumzo Na Mkurugenzi Mtendaji Wa Benki Ya Dunia Kanda Ya Afrika


 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika kundi la kwanza Dkt. Taufila Nyamadzabo ofisini kwake jijini Dodoma.

Waziri Mulamula amesema mazungumzo yake na Dkt. Taufila ambaye pia alikuwa anajitambulisha yamelenga kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Benki ya Dunia na Tanzania ili kuimarisha mahusiano hayo na hivyo kunufaika na miradi ya maendeleo.

Akiongelea uhusiano baina ya Tanzania na Benki ya Dunia Mhe. Balozi Mulamula amesema Tanzania imejipanga kuhakikisha mahusiano kati ya Tanzania na Benki hiyo yanaimarika na kuendeleza uwezo wa Watanzania wanaosimamia miradi ya maendeleo inayofadhiliwa na Benki ya Dunia ikiwa ni pamoja na kuendeleza sekta binafsi na kuifanya kuwa imara.

“leo hapa tumejadiliana juu ya mahusiano yetu, kuangalia namna ya kuyaboresha ili kunufaika na miradi  ya maendeleo inayofadhiliwa na Benki hiyo, kuwajengea uwezo watu wetu wanaosimamia utekelezaji wa miradi hiyo na uimarishaji wa Sekta binafsi ili kuwa imara na hivyo kufikia maendeleo ya kweli,” alisema Balozi Mulamula

Akiongelea kuhusu mipango ya Serikali ya kuimarisha Sekta Binafsi Mhe Waziri Mulamula amemuhakikishia Dkt. Taufilo nia na mtizamo wa Serikali wa kuweka mazingira mazuri ya kufanya biashara na kuwekeza nchini ikiwa ni pamoja na kushirikiana na sekta binafsi hasa ikizingatiwa kuwa Benki ya Dunia inachukulia sekta binafsi kama chachu ya maendeleo na hivyo kuwa na miradi ya kusaidia ukuzaji wa Sekta binafsi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji huyowa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika kundi la kwanza Dkt. Taufila Nyamadzabo amesema miongoi mwa mambo waliyojadili leo ni pamoja na umuhimu wa kuhusisha sekta binafsi na kuiendeleza.

Amesema miongoni mwa vipaumbele vya Benki ya Dunia kwa sasa ni kuimarisha Sekta binafsi na kuifanya kuwa imara hasa katika maeneo ya biashara na uwekezaji pamoja na kuimarisha miundombinu ya usafirishaji, na ukuzaji wa teknolojia ya habari na mawasiliano ili kuiwezesha duniani kuendelea kufanya shughuli zake hasa katika kipindi hiki cha changamoto ya ugonjwa wa Covid 19.

Amesema wamekubaliana kuendelea kushirikiana na kuimarisha mahusiano kati ya Tanzania na Benki hiyo na hivyo kuiwezesha Tanzania kunufaika na miradi ya maendeleo inayosimamiwa na benki hiyo.


Share:

WAFANYAKAZI WA MGODI WA BUZWAGI WAADHIMISHA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI KWA KUPANDA MITI YA MATUNDA


Wafanyakazi wa mgodi  wa Barrick wa Buzwagi wameadhimisha Siku ya Mazingira Duniani mwaka 2021 kwa kupanda miti ya maembe katika eneo  la mgodi huo uliopo wilayani Kahama mkoani Shinyanga
Wafanyakazi wa Barrick Buzwagi wakishiriki kupanda miti na kumwagilia miche waliyopanda
Wafanyakazi wa Barrick Buzwagi wakishiriki kupanda miti na kumwagilia miche waliyopanda
Wafanyakazi wa Barrick Buzwagi wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumaliza zoezi la kupanda miti kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani

Share:

WATUMISHI WA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII WAFANYA ZIARA KATIKA MASHAMBA YA WAZIRI MKUU MSTAAFU, MIZENGO PINDA

Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Lusius Mwenda akizungumza na baadhi ya watumishi wa Wizara ya Maliasili na utalii kuhusu utaratibu wa ziara ya mafunzo iliyofanyika jana kwenye mashamba ya Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Mizengo Pinda (hayupo pichani) yaliyoko Zinje (Zuzu) nje kidogo ya jiji la Dodoma.
Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Mizengo Pinda (katikati) akitoa maelezo kuhusu chakula cha samaki kwa Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Allan Kijazi (kulia) na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Ludovick Nduhiye (kushoto) wakati wa ziara ya mafunzo ya watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii iliyofanyika jana katika mashamba yake yaliyoko Zinje (Zuzu) nje kidogo ya jiji la Dodoma.
Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Mizengo Pinda (katikati) akionyesha moja ya bwawa la samaki kwa watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii waliotembelea mashamba yake yaliyopo Zinje (Zuzu) nje kidogo ya jiji la Dodoma jana. Kushoto kwake ni Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Allan Kijazi (kulia) na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Ludovick Nduhiye (kulia kwake) wakifuatilia.
Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Mizengo Pinda (katikati) akitoa maelezo kuhusu shamba la zabibu kwa watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii (hawapo pichani) waliotembelea mashamba yake yaliyopo Zinje (Zuzu) nje kidogo ya jiji la Dodoma jana. Kulia ni Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Allan Kijazi (kulia) na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Ludovick Nduhiye (kushoto).
Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Mizengo Pinda (kulia) akitoa maelezo kuhusu kilimo cha Green House kwa Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Allan Kijazi (kushoto) na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Ludovick Nduhiye (katikati) wakati wa ziara ya mafunzo kwa vitendo ya watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii waliotembelea mashamba yake yaliyopo Zinje (Zuzu) nje kidogo ya jiji la Dodoma jana.
Share:

MKUU WA MKOA WA SHINYANGA DR. SENGATI, RAS MPYA BALOZI DR. BATILDA WAKUTANA NA WAANDISHI WA HABARI

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Philemon Sengati na Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Buriani leo Jumatatu Juni 7,2021 wamekutana na Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga kwa ajili kujadili masuala mbalimbali ya maendeleo ya mkoa wa Shinyanga ikiwa ni siku chache zimepita baada ya kuteuliwa kisha kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu kutekeleza majukumu yao mkoani Shinyanga.  Picha na Kadama Malunde & Frank Mshana
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Dkt. Philemon Sengati akizungumza na Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga leo Jumatatu Juni 7,2021
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Dkt. Philemon Sengati akizungumza na Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga leo Jumatatu Juni 7,2021
 Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Dkt. Balozi Batilda Salha Buriani akizungumza na Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga leo Jumatatu Juni 7,2021
Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Dkt. Balozi Batilda Salha Buriani akizungumza na Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga leo Jumatatu Juni 7,2021
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Dkt. Philemon Sengati akizungumza na Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga leo Jumatatu Juni 7,2021
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Dkt. Philemon Sengati akizungumza na Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga leo Jumatatu Juni 7,2021
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Dkt. Philemon Sengati akizungumza na Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga leo Jumatatu Juni 7,2021
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Dkt. Philemon Sengati akizungumza na Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga leo Jumatatu Juni 7,2021
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Dkt. Philemon Sengati (mwenye suti ya Bluu katikati) akipiga picha ya pamoja na Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Dkt. Philemon Sengati (mwenye suti ya Bluu katikati) akipiga picha ya pamoja na Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Dkt. Philemon Sengati (mwenye suti ya Bluu katikati) akipiga picha ya pamoja na Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga. Picha na Kadama Malunde & Frank Mshana
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger