Thursday, 27 May 2021

WATOA HUDUMA ZA AFYA, WADAU WATAKIWA KUZINGATIA USAHIHI WA VIPIMO

Meneja wa Kanda Nyanda za juu kusini Bw.Abel Mwakasonda akizungumza na washiriki wa semina ya Umuhimu wa Vipimo katika sekta ya afya iliyofanyika katika ukumbi wa Dk. Shein Jijini Mbeya. Mwakasonda alisema TBS kwa kushirikiana na taasisi zingine zenye dhamana ya kushughulika na vipimo zimejipanga kuhakikisha kila mtoa huduma katika sekta ya afya anapata uwezo wa kutoa huduma kwa kuzingatia vipimo sahihi.

 ****
Watoa huduma katika sekta ya afya na wadau wote kila mmoja kwa nafasi yake wametakiwa kuchukua hatua stahiki kwa pamoja kuhakikisha wanalinda afya za Watanzania kwa kuzingatia upimaji sahihi, kufuata miongozo na viwango vya kitaifa na kimataifa.

Wito huo umetolewa leo Mei 27 2021 na Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya, Mwajabu Nyamkomora, katika semina iliyoandaliwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kwa lengo la kutoa uelewa kwenye masuala ya Sayansi ya Vipimo hususani katika sekta ya afya kwa wadau. 

Semina hiyo ni sehemu ya mwendelezo wa maadhimisho ya Siku ya Vipimo Duniani yaliyofanyika Mei 20, mwaka huu kitaifa mkoani Dodoma, kauli mbiu ikiwa na ujumbe usemao; "Umuhimu wa Vipimo Katika Sekta ya Afya." 

Nyamkomora alisema vipimo ni huduma muhimu sana katika utoaji wa huduma za afya na uzalishaji wa dawa katika viwanda vyetu, kwani Taifa ambalo watu wake hawana afya, haliwezi kuzalisha.

Aliongeza pia ni muhimu watoa huduma za afya, madaktari, wauguzi na watu wa maabara, watoe huduma kwa kuzingatia viwango, miongozo ya Serikali, weledi, kujituma na kufanya kazi kwa bidii na kwa kukumbuka viapo vyao.

"Lakini pia tutambue kuwa uhai na ustawi wa taifa letu upo katika mikono yenu (watumishi wa afya) hivyo wafanye kazi kwa bidii," alisema Nyamkomora.

Mgeni huyo rasmi, Nyamkomora aliwataka watoa huduma katika sekta ya afya kujitathmini kama wanatoa huduma ya vipimo inayokidhi viwango. 

"Tujikague kwa kujiuliza maswali. Je, una elimu, ujuzi na maarifa ya kutosha kutumia vifaa unavyotumia katika upimaji, je, hali ya vifaa unavyovitumia inaruhusu kufanya vipimo? Je, tunafuata ushauri wa kitaalamu kuhusu matumizi, utunzaji, matengenzo ya muda na yale ya baada ya hitilafu kwa vifaa tunavyotumia?" Alihoji, Nyamkomora na kuongeza;

"Mtoa huduma anatakiwa kujiuliza kama kifaa chako kimehakikiwa kwa usahihi wake wa kutoa majibu sahihi?  Je, umefanya ugezi (Calibration) kwenye vifaa vyako? 

Unatumia cheti cha ugezi kutoka kwa aliyekupa huduma hiyo? je,aliyekupa huduma ya ugezi ana weledi wa kazi anayofanya na je mfumo wa kuhakiki majibu yanayotoka ni sahihi?"

Alisema ni muhimu kila mmoja kwa nafasi yake akachukua hatua stahiki ili wote kwa pamoja tuhakikishe wanalinda afya za Watanzania kwa kuzingatia upimaji sahihi, kufuata miongozo na viwango vya kitaifa na kimataifa.

Alisema ni matumaini yake kuwa baada ya semina hiyo kila mmoja kwa nafasi yake atachukua hatua stahiki ili wote kwa pamoja tuhakikishe tunalinda afya za Watanzania.

Kwa upande wa Meneja wa TBS Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Abel Mwakasonda, alisema vifaa vinavyotumika katika uchunguzi wa afya vina mchango mkubwa katika kuhakikisha ugonjwa ambao mtu anaugua.

Aliwataka wamiliki na waendeshaji wa hospitali, maabara za afya, viwanda vya kuzalisha dawa na taasisi zinazosimamia sekta ya afya kutambua kuwa huduma bora za afya zinawezekana tukizingatia ubora wa vipimo vyetu.

Alisema mtoa huduma katika sekta ya afya anapata uwezo wa kutoa huduma kwa kuzingatia vipimo sahihi.

"Vipimo sahihi ni huduma muhimu sana katika utoaji wa huduma bora za afya, nawashauri wamiliki wa viwanda, hospitali, vituo vya afya, maabara za uchunguzi na watoa huduma wote wa sekta ya afya mtumie vipimo sahihi kwa wakati sahihi na kupata huduma ya ugezi wa vifaa (mashine zinazotumika kupimia ama kutunzia sampuli zenu kutoka katika Taasisi zinazofanya vipimo kwa usahihi ili muweze kutoa huduma bora kwa Watanzania," alisema Mwakasonda na kuongeza;

"Vipimo sahihi ni kiwezeshi cha utoaji wa huduma bora na salama. IIi kuenzi siku ya Vipimo Duniani."

Kwa upande wa Mkuu wa maabara ya ugezi Bw. James Mahilla alisema TBS kupitia Maabara ya Vipimo (Metrolojia) ndiyo watunzaji wa Viwango vya Taifa vya Vipimo.
Mkuu wa Maabara ya Ugezi Bw.James Mahilla akizungumza na washiriki  wa semina ya umuhimu wa vipimo katika sekta ya afya iliyofanyika katika ukumbi wa Dk. Shein jijini Mbeya.
Mahilla alisema ili kuenzi siku ya vipimo duniani,TBS imeandaa semina kwa lengo la kutoa uelewa kwenye masuala ya sayansi ya Vipimo hususani katika sekta ya Afya

Kaimu Katibu tawala wa Mkoa wa Mbeya Bi. Mwajabu Nyamkomora akifungua semina ya umuhimu wa vipimo katika sekta ya afya iliyofanyika katika ukumbi wa Dr. Shein jijini Mbeya mapema leo.
Nyamkomora alitoa wito kwa watoa huduma za afya,madaktari,wauguzi na watu wa maabara  kulinda afya za Watanzania kwa kuzingatia upimaji sahihi, kufuata miongozo pamoja na viwango vya kitaifa na kimataifa.
Baadhi ya washiriki wa semina ya Umuhimu wa Vipimo Katika Sekta ya Afya iliyofanyika mapema leo katika ukumbi wa Dr.Shein jijini Mbeya

Share:

MWAKINYO KUMPA ASANTE RAIS SAMIA KWA KUMCHAPA MAYALA


Mabondia wa kigeni na makocha mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja tayari kwa kupambana na wapinzani wao wa Tanzania katika pambano la Rumble in Dar 2 lililoandaliwa na kampuni ya Jackson Group Sports.

***

Bondia Hassan Mwakinyo ameahidi kumpa kipigo kikali mpinzani wake Antonio Mayala kutoka Angola ikiwa asante kwa Rais wa kwanza mwanamke wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan.

Mwakinyo ambaye atawania mkanda wa Afrika (ABU) wa uzito wa Super welter atapanda ulingoni kesho kwenye ukumbi wa Next Door Arena, Masaki katika pambano lililoandaliwa na kampuni ya Jackson Group Sports.

Alisema kuwa amejiandaa vyema na kwa vile atakuwa anapigana kwa mara ya kwanza chini ya uongozi wa Rais Samia, hatofanya makosa zaidi ya kushinda katika raundi za mwanzoni tu katika pambano hilo lililodhaminiwa na KCB Bank, Plus TV, Multichoice Tanzania, Tanzania Tourism Board, Onomo Hotel, Precision Air, Prestine Logistics, Urban Soul na washirika wa kimataifa Global Boxing Stars na Epic Sports Entertainment.

“Nitakuwa napigana kwa mara ya kwanza chini ya Rais Mama Samia Suluhu Hassan. Sitamwangusha Rais na watanzania kwa ujumla, nawaomba mashabiki kufika kwa wingi ili kunipa sapoti,” alisema Mwakinyo.

Wakati Mwakinyo anasema haya, mpinzani wake Mayala amesema kuwa pamoja na kupata taarifa za muda mfupi, amejiandaa vyema ili kuonyesha kuwa yeye ni bondia wa ngumi za kulipwa.

“Nimekuja kwa ajili ya kushinda na si kupoteza, nilikuwa nafanya mazoezi kwa sababu ngumi ni kazi yangu na siwezi kuruhusu Mwakinyo kushinda na kuchukua mkanda wa Afrika,” alisema Mayala.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Jackson Group Sports, Kelvin Twissa amesema kuwa mbali ya pambano hilo, pia bondia Daniel Matefu atazichapa na bondoa kutoka Bulgaria Pencho Tsvetkov huku bondia wa kike Leila Yazidu atazichapa na bondia wa Bulgarian Joana Nwamerue.

Pia bondia Hamisi Palasungulu atazichapa na bondia wa Congo Brazzaville Ardi Ndembo huku Imani Daudi Kawaya akionyeshana kazi na bondia kutoka Afrika Kusini Chris Thompson.

Pambano lingine la ABU litakuwa kati ya bondia Shabani Jongo chini ya Mnigeria Olanrewaju Durodora ambao watawania uzito wa juu na nyota mwingine Ibrahim Class atazipiga na bondia wa Afrika Kusini, Sibusiso Zingange.
Share:

TIC Kuimarisha Mifumo Ya Uwekezaji Nchini


Na Beatrice Sanga, MAELEZO.
Kituo cha Uwekezaji Tanzania-TIC kimeanza kufanya maboresho ya huduma za uwekezaji  kwa kuunganisha mifumo ya kielektroniki kwa taasisi na idara 11 za Serikali zinazotoa huduma za mfumo wa mahala pamoja lengo likiwa ni kurahisisha utoaji wa vibali na leseni za uwekezaji kwa kuunganisha mifumo hiyo ili kuwa na dirisha moja la uwekezaji nchini.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Dkt. Maduhu Kazi amesema maboresho hayo yatasaidia kuongeza ufanisi katika kutoa huduma za wawekezaji na kuimarisha utendaji kazi wa kituo hicho ikiwa ni agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alilolitoa Aprili, 2021 wakati akiwaapisha makatibu wakuu wa Wizara.

Dkt Maduhu amefanya kikao cha pamoja na  wakuu wa Taasisi na Idara za Serikali 11 zinazotoa huduma kwenye Kituo cha huduma kwa wawekezaji cha mahali pamoja (One Stop Facilitaion Centre) na kubainisha kuwa mchakato wa maboresho hayo unaendelea kufanyiwa kazi.

“Kama mnavyofahamu, Mheshimiwa Rais alitoa maelekezo ya namna ya kuboresha huduma za uwekezaji, kikao hiki ni muendelezo wa utekelezaji wa majukumu hayo, tulishaanza kuyafanyia kazi, na sasa tunaendelea, lengo ni kutoa huduma bora zaidi za uwekezaji” amesema Dkt. Maduhu.

Katika kikao hicho, Dkt. Maduhu amepokea taarifa ya hatua ambazo zimechukuliwa kwa kila Taasisi na Idara husika zikiwepo kila taasisi kufungua mfumo wa kielektroniki kwa ajili ya utoaji vibali na leseni mbalimbali, kuunganisha mifumo hiyo ili kuwa na dirisha moja la huduma kwa wawekezaji nchini na taasisi husika kukamilisha hatua zote ikiwepo kuchambua na kutoa maamuzi kwa maombi husika ya wawekezaji.

Maboresho haya yanaelezwa kuwa yatawawezesha wawekezaji wanaowekeza nchini kupata huduma kwa muda mfupi na kwa kutumia gharama ndogo.

Baadhi ya Taasisi zilizoshiriki katika kikao hicho ni pamoja na Uhamiaji, Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA), Mamlaka ya Chakula na Dawa (TMDA), Mamlaka ya Mapato Tanzani (TRA), Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira  (NEMC), Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Shirika la Viwango Tanzania (TBS) naOfisi ya Waziri Mkuu (Kazi).


Share:

“Kujikosoa Ni Kujisahihisha” Bashungwa


Na Judith Mhina Maelezo
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa, amesema kujikosoa ni kujisahihisha maneno aliyoyanukuu kutoka kwa muasisi wa Taifa la Tanzania Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Maneno hayo ameyatamka wakati wa ufunguzi wa Kikao Kazi cha 14 cha mwaka huu kwa Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano Serikalini kilichofanyika katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Tekinolojia Mbeya (MUST) hivi karibuni.

Waziri Bashungwa amenukuu maneno hayo kutokana na hali halisi ya Maafisa Habari wa Serikali hapa nchini ambao wana wajibu wa kujikosoa na  kujirekebisha  katika kutimiza majukumu yao kama kaulimbiu ya Kikao Kazi hicho inavyosema, “Taarifa kwa Umma ni Takwa la Kisheria, Viongozi wa Umma na Maafisa Habari Tuwajibike.”

Aliongeza kuwa, ili kutimiza takwa hilo  wote kwa pamoja wana wajibu wa kuhakikisha  wanasimamia kama viongozi ili walengwa ambao ni Mafisa Habari wa Serikali  watangaze na kusemea kazi zote za Serikali ikiwemo miradi ya kimkakati, Sheria, Kanuni na Miongozo mbalimbali kwa ustawi wa wananchi na maendeleo ya Taifa kwa ujumla.

“Tuna taarifa kuwa baadhi ya  Maafisa Habari walioko  katika utumishi wa Umma ni watu ambao hawataki kujituma na kuwa wabunifu  ingawa wanawezeshwa kwa kupewa vifaa vya kazi  na kushirikishwa ndani ya  menejimenti husika, pamoja na kushirikishwa katika  ziara zote  lakini hawatimizi wajibu wao.” alisema Waziri Bashungwa.

Aidha, katika dhana nzima ya kujikosoa na kujisahihisha kama alivyosema Mwalimu Nyerere, upo wajibu  wa kukitendea haki Kikao Kazi  hicho, ambacho ni cha siku tano kuanzia Mei 24-28, 2021 ili kuwa  chachu ya kuleta mageuzi makubwa katika kuhakikisha  Maafisa Habari wanaisemea na kuitangaza Serikali ili Umma wa Tanzania wajue kile ambacho Serikali yao  inafanya.

Katika suala zima la wajibu wa mwajiri, Maafisa Habari wengi wapo Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali ya Mitaa (TAMISEMI), Wakala wa Serikali, Taasisi za Umma na Wizara. Kuna changamoto kadhaa zinazowakabili maafisa hao kama vile kuwa chini ya mtumishi wa Kitengo cha TEHAMA, au kuonekana kama mpiga picha tu wakati wa matukio mbalimbali na kutoshirikishwa katika maamuzi ya Menejimenti husika.

Amesema kuwa Sheria ya Huduma za Habari namba 12 ya mwaka 2016 na kanuni zake za Mwaka 2017 pamoja na Sheria ya Haki ya kupata Taarifa Na. 06 ya mwaka 2016 ndivyo vinavyomfanya Afisa Habari kutambulika na kutimiza wajibu wake. Sheria hizi zinajenga taaluma ya Habari na kuifanya kutambulika rasmi.

Waziri Bashungwa amebainisha changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika Halmashauri za Wilaya, Miji, Manispaa na Majiji, zikiwepo za Maafisa Habari kuchanganywa na Watumishi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ambao wakati mwingine huweza kukorofisha mawasiliano ya kimtandao na hivyo kukwamisha kazi za maafisa habari.

Kuhusu suala la kutokuwa na vitendea kazi pamoja na kupewa majukumu ambayo si yao na kushirikishwa tu pale yanapotokea matukio Waziri Bashungwa alitoa maelekezo kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais (TAMISEMI) kuangalia suala hilo na kuona umuhimu wa kuwashirikisha maafisa Habari katika vikao vya maamuzi  ili kuwa na uelewa mpana utakaowasaidia kutangaza na kusemea kazi nzuri zinazofanywa na Serikali.

Kuokana na changamoto mbalimbali zilizoainishwa na Waziri Bashungwa, Idara ya Habari (MAELEZO) ilipata fursa ya kufanya mahojiano na baadhi ya  Maafisa Habari Grace Gwemagobe wa Mkoa wa Songwe ambaye alisema “Maafisa Habari walio wengi katika Mikoa na Halmashauri mbalimbali nchini wana changamoto ya utendaji wa kazi, kwa kuwa inategemea kiongozi anayemkuta katika sehemu husika ana utashi gani juu ya kada ya Afisa Habari. Aidha, mara nyingi inakuwa  kama ni hisani, au  kujuana na kiongozi wako badala ya kusimama kwenye mfumo halisi ulivyo wa kiutumishi  au kulingana na taratibu za kusimamia utumishi wa umma.

Gwemagobe  ameongeza kuwa yeye yupo chini ya  Idara ya Utawala na Rasilimali watu  ambapo kiongozi wake ni Katibu Tawala Msaidizi sehemu ya Utawala na Rasilimali watu, na Maafisa Habari wengi hawajui  miongozo ya uendeshaji  (PMG)  katika Sekretarieti ya Mkoa. Hatua hiyo inasababisha Maafisa Habari wengi wa Mkoa kuishia kuwa Katibu  wa  Wakuu wa Mikoa  badala ya kufanya kazi za Afisa Habari kama ilivyoelekezwa  katika taratibu za utumishi wa umma.

Naye Afisa Habari wa Halmashauri ya Mji wa Mufindi Ndimiyake Mwakapiso amesema “ Ofisi za Serikali ni za umma  kwa hiyo  kama Mkuu wa Kitengo au idara ni Afisa Habari au  Mtumishi wa TEHAMA haina tatizo lolote kwani tunafanya kazi kwa kushirikiana  na  mambo yanaenda tu”.

Mwakapiso pia ameongeza kuwa  kuna baadhi ya Halmashauri Maafisa Habari ndio wakuu  wa vitengo na wanawasimamia watumishi wa TEHAMA, kwa nia njema tu na kusisitiza kuwa wanafanya bila tatizo lolote.

Naye Afisa Habari ambaye hakutaka jina lake litajwa amesema “Mimi binafsi katika ofisi yangu sina vitendea kazi wala hakuna kitengo cha habari tunawekwa mahala popote kiongozi wetu anapodhani tunaweza kuwa hapo. Pia  hatuna bajeti ya kitengo, vilevile mara nyingi wakuu wa idara wenye miradi mbalimbali hawatushirikishi kwa kuhofia tukienda kwenye miradi tutadai kulipwa fedha na wao hawako tayari kulipa posho ya Afisa Habari badala ya yeye na wahusika katika ofisi yake”.



Share:

Majaliwa: Tutaendelea Kusimamia Bei Nzuri Ya Mazao


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan itaendelea kusimamia bei nzuri ya mazao kwa wakulima nchini.

Ametoa kauli hiyo leo (Alhamisi, Mei 27, 2021) wakati akijibu swali la Mbunge wa Kyerwa Innocent Bilakwate katika kipindi cha Maswali ya Papi kwa Papo kwa Waziri Mkuu Bungeni jijini Dodoma.

Mbunge huyo alitaka kufahamu mpango wa Serikali wa kuhakikisha zao la Kahawa linakuwa na soko la uhakika.

"Kahawa ni miongoni mwa mazao ya kimkakati ambayo yanalimwa na jamii pana hivyo Serikali itaendelea kusimamia ushirika, masoko ili wakulima waweze kulipwa kwa wakati".

Aidha, Waziri Mkuu amesema kuwa pamoja na kutafuta changamoto ya  masoko, pia Serikali imeendelea kutekeleza mkakati wa uanzishwaji wa viwanda ndani ya nchi ili zao la kahawa liweze kuongezewa thamani na kuwa na masoko ya uhakika.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu amesema kuwa Serikali itaendelea kuweka mikakati ya kuhakikisha inawalinda raia na mali zake ili wanaendesha kazi zao kwa amani na utulivu.

"Hata Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kupitia hotuba yake moja ya kitaifa, amewaonya wote wanaofikiria huu ni wakati wa kufanya maovu nchini na amewataka wote wanaofikiria kufanya hivyo waache mara moja, haya pia ni maagizo kwa vyombo vya ulinzi na usalama kuwachukulia hatua wote wanaosababisha madhara ya usalama kwa watanzania"

Pia, Waziri Mkuu ametoa wito kwa watanzania kushiriki katika suala la ulinzi na usalama kwa kutoa taarifa kila wanapoona kuna dalili za uvunjifu wa amani katika maeneo yao ili majeshi yaweze kufanya kazi iliyokusudiwa.

Waziri Mkuu ameyasema hayo wakati akijibu Swali la Mbunge wa Makete, Festo Sanga aliyetaka kujua  kuhusu mkakati wa Serikali katika kuthibiti vitendo vya uhalifu nchini ikiwemo ujambazi.

Kadhalika, Waziri Mkuu amesema kuwa mkakati wa ujenzi wa viwanda nchini umelenga kuhakikisha nchi inapunguza changamoto ya ajira kwa Watanzania wa ngazi zote za elimu kwa sababu kwenye viwanda kuna kazi nyingi kwa watu wa kada zote.

Ameongeza kuwa Serikali itaendelea kuimarisha vyuo vya ufundi stadi ili kuwawezesha Watanzania kupata ujuzi wa kujiajiri.  "Katika miaka mitatu iliyopita tumeweza kukusanya vijana zaidi ya 35,000 tukawapeleka kwenye sekta mbalimbali".

Akijibu swali la Mbunge wa Nkasi, Aida Kenani aliyetaka kufahamu kuhusu  mkakati wa Serikali wa  kutoa huduma za magonjwa ya kisukari kuanzia ngazi ya wilaya hadi kata, Waziri Mkuu amesema kuwa kwa sasa huduma za ugonjwa wa kisukari zinatolewa mpaka ngazi ya zahanati kama sera ya afya inavyoelekeza.

"Halmashauri zote ambazo ndizo zinasimamia Zahanati hakikisheni mnaagiza dawa za kisukari na ziende kwenye zahanati na vituo vya afya ili Watanzania wapate huduma hiyo bila ya usumbufu wa  kusafiri"

 Wakati huohuo Waziri Mkuu amesema kuwa Serikali imejipanga kupambana na majanga mbalimbali ili shughuli za watanzania ziwende kwenda vizuri “tumeendelea kukiimarisha kitengo cha maafa ili kukabiliana na majanga kwa kuweka vifaa, kuwa na wataalamu pamoja kupeleka elimu kwa wananchi kushughulikia majanga pindi tu yanapotokea”

MWISHO.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU



Share:

Wazee Wamshukuru Rais Samia Kwa Huduma Bora Zaafya


Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Wazee wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kusimamia na kuboresha huduma ya matibabu kwa Wazee katika Hospitali mbalimbali nchini.

Shukrani hizo zimetolewa kwa nyakati tofauti na wazee wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, anayeshughulikia Maendeleo ya Jamii, Mwanaidi Ali Khamis katika hospitali ya Benjamin Mkapa iliyopo jijini Dodoma kujionea utekelezaji wa maelekezo yaliyotolewa juu ya kuboresha huduma za matibabu kwa wazee.

Mzee Anthony Mwakyusa aliyekutwa dirisha la dawa amesema kwa hivi sasa naona huduma zimekuwa nzuri zaidi hasa kwa sisi wazee wanahudumiwa harakaharaka na Madktari wanasikiliza shida zao na wanawahudumia vizuri sana.

Ameongeza kuwa wanawashukuru sana kwakwa viongozi wa kitaifa kufuatilia jinsi wazee wanavyohudumiwa kiukweli huduma zimekuwa bora sana.

Kwa upande Mzee Hassan Kijuu amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwaona wazee kuwa ni kundi maalum na linalohitaji kuangaliwa zaidia katika kupatiwa huduma mabaliambali hasa huduma za afya.

“Nimefika kwenye foleni na namba yangu ilikuwa mbali sana lakini alikuja binti simjui, hanijui akaniomba karatasi zangu mara nimepelekwa huku, mara nimepelekwa kule na sasa nimemaliza, tunawashkuru sana.” alisema Mzee Kijuu


Akizungumza wakati wa ziara hiyo Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, anayeshughulikia Maendeleo ya Jamii, Mwanaidi Ali Khamis ameipongeza Hospitali ya Benjamin Mkapa kwa huduma bora kwa wazee na kuwapongeza madakatari na Maafisa Ustawi wa Jamii kwa huduma zao nzuri wanazotoa kwawazee hao.

“Niwashukuru madaktari wa Hospitali hiyo pamoja na Maafisa Ustawi wa Jamii kwa kuwaangalia vyema wazee hao na naviagiza vituo vyote vya kutolewqa huduma za afya pamoja na Hospitali zote nchini kuendelea kutekeleza agizo hili” alisema Naibu Waziri Mwanaidi

Aidha Naibu Waziri Mwanaidi amewahakikishia wazee kuendelea kuoata huduma bira na kwa wakati na kuwaomba waendelee kuishauri Serikali pale panapokuwa na mapungufu ili waendelee kuboresha huduma mbalimbali katika kutoa huduma bora za afya.

Pia Naibu Waziri Mwanaidi amipongeza Hospitali ya Benjamini Mkapa hospitali hiyo kwa ubunifu wake wa kutenga eneo la kupumzikia wazee likiwa na viburudisho mbalimbali kama chai na kahawa pamoja na runinga na kuzitaka hospitali zingine kuiga ubunifu huo wa kuboresha zaidi ya kutoa huduma kwa wazee.

“Wazee ni tunu katika nchi yetu. Wameijenga nchi yetu katika vipindi tofauti na sisi kama wizara tutahakikisha wanapata huduma bora zaidi za matibabu. Nimefurahishwa sana na namna madaktari pamoja na maafisa ustawi wa jamii wanavyowahudumia wazee katika hospitali hii.” Alisema Naibu Waziri Mwanaidi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa, Dkt. Alphonce Chandika amesema Hospitali yake imepokea maelekezo hayo na wameshaanza kuyatekeleza na wamejipanga kuwahudumia wazee wa rika tofauti wakiwemo wenye uoni hafifu na hivyo waratibu wa wazee huwafuata wazee mara wafikapo hospitalini na kuwaongoza kwenye kupata huduma.

“Kila eneo la kutolea huduma tumeweka mtumishi ambaye atashughulikia huduma za wazee na kuhakikisha wanapata matibabu kwa wakati, lakini pia kuhakikisha kama anatakiwa kwenda sehemu nyingine kupata huduma kama maabara, huyo mtumishi atatakiwa kuhakikisha anamfikisha mzee sehemu husika ya huduma,” alifafanua Dkt. Chandika.

Mnamo tarehe 7 Mei, mwaka huu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati akiongea na wazee wa Mkoa wa Dar es salaam aliahidi kuboresha tiba kwa wazee kwani tiba ni haki yao ya msingi katika daraja lolote lile watakalokua wanaugua kuanzia vituo vya afya, Zahanati hata hospitali za Taifa.

MWISHO



Share:

Ridhiwani: “Kikwete ni mzima wa afya, hana tatizo”


Ridhiwani Kikwete,  mtoto wa rais mstaafu Jakaya Kikwete amesema baba yake ni mzima wa afya.

Ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Mei 27, 2021 kupitia ukurasa wake katika mtandao wa kijamii wa Instagram,  akijibu madai yaliyoanza kusambaa mitandaoni tangu jana kuhusu kiongozi huyo mstaafu.

Katika ujumbe wake huo,  Ridhiwani amesema, "baada ya kupokea simu na jumbe mbalimbali nimeona nitumie nafasi hii kuweka kumbukizi sawa. Mzee wetu na Mzazi wetu Dk Kikwete yupo salama wa afya nyingi sana. Hana tatizo lolote kiafya na anaendelea na majukumu yake. Taarifa za aina yeyote ni za kipuuzi na za kupuuzwa.”


Share:

Wizara Ya Afya Kuja Na Mfumo Wa Ufuatiliaji Wa Wajawazito Nchi Nzima


Na – WAMJW, Dodoma
Wizara ya Afya inatarajia kuja na mfumo wa ufuatiliaji wa taarifa za wajawazito wote toka wanapofika kliniki kwa mara ya kwanza hadi baada ya siku 42 za kujifungua.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima leo alipokutana na wataalam wa afya katika kikaokazi cha maandalizi ya utengenezaji wa mfumo huo.

“Nataka muwe mnafuatilia taarifa za wajawazito na kujua maendeleo yao toka wanapofika kituoni siku ya kwanza mpaka baada ya kujifungua kwa data za kila siku na kujua kwa namna gani wajawazito au mama baada ya kujifungua ameweza kupata huduma zetu na muweze kuchukua hatua pale mnapoona changamoto” amesema Dkt. Dorothy Gwajima.

Waziri Gwajima amesema kuwa ili kuweza kuwa na mfumo wenye ufanisi ni lazima tusisitize matumizi sahihi ya takwimu na kuwataka wataalam wa afya katika kazi zao kuhakikisha wanachukua takwimu zote zinazohitajika kwa ajili ya matuzimu katika mfumo huo.

Waziri Dorothy Gwajima amesema kuwa Serikali katika kupambana na vifo vya wajawazito imefanya mambo mengi ikiwemo kuanzisha Kampeni maalum ya Jiongenze Tuwavushe Salama iliyoanzishwa na aliyekuwa Makamu wa Rais na sasa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan yenye lengo la kupunguza na kudhibiti vifo vitokanavyo na uzazi.

“Serikali imejenga vituo vingi vya huduma ngazi zote na mwamko wa wajawazito wanaojitokeza kuhudhuria kliniki umekuwa mkubwa” amesema Dkt. Dorothy Gwajima na kuongezea kuwa bado elimu inahitajika kutolewa kwa ili wajawazito wafike katika vituo vya kutolea huduma za afya na kuanza kliniki mapema.

“Sasa hivi mwitikio umeongezeka, wajawazito wanajitokeza na kujifungua katika vituo vya kutolea huduma kati yao wengine wanafariki, lakini tukijadili kujua kwanini amefariki na tukifuatilia wakati alipokuwa kliniki tunagundua hatukumfuatilia vizuri, hiki ndio kitu tunachoimarisha ili ufuatiliaji uwe imara” amefafanua Dkt. Dorothy Gwajima.

Waziri Gwajima amesema kuwa katika kuimarisha mfumo wa usimamizi na ufuatiliaji wa taarifa za wajawazito, wanatarajia kuimarisha ufuatiliaji wa mteja mmoja mmoja toka anapopata ujauzito, muda wa kuanza kliniki, kujifungua mpaka baada ya siku 42.

Naye Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Aifello Sichwale amesema kuwa kwa kupitia kanzidata wanazochukua kutoka kwenye taarifa za wajawazito zinawasadia kujua bidhaa gani za dawa zinazihitajika kumhudumia mjamzito, miundombinu ipi wanahitaji, inaonyesha uwajibikaji wa watumishi wa afya kwa ujumla wao na mmoja mmoja, pamoja na kutuonyesha kama miongozi iliyopo inatija katika kusaidia kutoa huduma bora kwa wajawazito.

“Hakuna njia nyingine ambayo tutaitumia kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi zaidi ya kuimarisha ufuatiliaji na usimamizi wa mama mmoja mmoja kama kanzidata hii inavyotaka” Amesema Dkt. Sichwale


Share:

WATAALAMU WA UREMBO 'KAHAMA GLAMOUR BEAUTY SALON' WASHIRIKI MAONESHO KAHAMA

Share:

RC SENGATI ATUA KWA KISHINDO SHINYANGA...ATIA NIA YA KUIMARISHA UKUSANYAJI MAPATO, KUDHIBITI WIZI FEDHA ZA UMMA


Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dk. Philemon Sengati akizungumza na viongozi mbalimbali wakati akikaribishwa na kukabidhiwa rasmi ofisi, leo mjini Shinyanga

Na Damian Masyenene, SHINYANGA
MKUU mpya wa Mkoa wa Shinyanga, Dk. Philemon Sengati amepokelewa na kukabidhiwa rasmi ofisi na aliyekuwa Mkuu wa mkoa huo, Zainab Telack ambaye amehamishiwa mkoa wa Lindi, huku akiweka wazi nia yake ya kuimarisha ukusanyaji mapato, kudhibiti matumizi yasiyo sahihi ya fedha za umma na kuhimiza usikilizaji kero za wananchi na kufika maeneo ya miradi kujiridhisha na kinachotekelezwa.

Hafla hiyo ya makabidhiano imefanyika leo Mei 26, 2021 mjini Shinyanga katika ukumbi wa mkuu wa mkoa na kuhudhuriwa na wakuu wa wilaya, wakurugenzi wa halmashauri, mameya na wenyeviti wa halmashauri, wakuu wa taasisi na mashirika ya umma, wawakilishi wa vyama vya siasa, viongozi wa dini, makundi maalum yakiwemo ya wenye ulemavu, wawkilishi taasisi binafsi na asasi za kiraia, viongozi wa taasisi za fedha, watendaji mbalimbali wa serikali, kamati za amani, kamati ya ulinzi na usalama na waandishi wa habari.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa rasmi ofisi, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dk. Philemon Sengati amempongeza Zainab Telack kwa kazi kubwa aliyofanya na kuacha alama ya kukumbukwa ikiwemo kusimamia usalama, ukusanyaji mapato, usimamizi mzuri wa rasilimali, hivyo kumfanya kuwa kiongozi hodari na mchapa kazi.

Dk. Amesema kuwa anaufahamu mkoa wa Shinyanga kwani amewahi kufanya kazi mbalimbali akiwa na mashirika binafsi kwa mwaka mmoja, hivyo yuko imara na wala hatoyumbishwa na mtu yeyote, huku akiweka wazi kuwa ana misimamo ambayo imejikita kusimamia haki, ukweli na maslahi mapana ya wananchi walio wanyonge ili kujenga uchumi endelevu.

“Naifahamu Shinyanga ni nyumbani kuna baadhi ya vitu navifahamu kabla sijafika hapa, nimewahi kufanya kazi hapa. Ni muumini wa diplomsia na hoja jenzi zisizokinzana na imani za dini, muumini wa utawala bora, ukweli, ubunifu na ninapenda kazi kweli kweli. Watu wabunifu, wanaojituma na wanaopenda kazi kwangu ni marafiki,” amesisitiza.

RC Sengati ambaye alikuwa mhadhiri wa chou kikuu cha Dodoma (UDOM) kwa miaka 10 kisha kuwa Mkuu wa Wilaya ya Magu kwa miezi 18 na Mkuu wa mkoa wa Tabora kwa miezi 10 kabla ya kuhamishiwa Shinyanga, ametaja vipaumbele vyake kuwa ni kuona mahusiano makubwa ya utajiri wa mkoa huo yakitafasiriwa kwa maisha bora ya wananchi wa Shinyanga, kwa kuimarisha miundombinu na huduma za kijamii.

“Kipaumbele namba moja nitaimarisha zaidi masuala ya usalama kwa kuhakikisha vitendo vinavyotishia usalama vinakomeshwa, namimi nitafuatilia kwa sababu ninataka usalama wa kweli ndani ya mkoa wa Shinyanga, ninataka watu wafanye kazi saa 24 bila hofu. Tunataka vibaka, wezi na majambazi waishe. Na yeyote atakayenikwamisha kwa hili ama zake ama zangu,” amefafanua.

Ametaja vipaumbele vingine kuwa ni Mapato, ambapo atahakikisha mapato yanayopaswa kukusanywa yakusanywe ipasavyo, vyanzo vya mapato vitunzwe na kubuni vyanzo vipya na kila mmoja aonyeshe uadilifu, nidhamu na uzalendo, vilevile amesisitiza kuwa usimamizi matumizi ya fedha za umma nao ni kipaumbele chake huku akijipambanua kuwa yeye ni mpinga rushwa na wizi namba moja, hivyo anajiamini atasimamia jambo hilo ipasavyo.

“Nielekeze wakuu wa wilaya, jicho lenu nyoyo zenu ziwe kuzisimamia halmashauri katika masuala ya mapato na matumizi ili kusiwe na mianya ya rushwa, kashfa na hati chafu. Tushirikiane na tupendane tukitetea maslahi mapana ya wana Shinyanga na Tanzania, yeyote atakayejaribu kunigombanisha na watendaji wenzangu huyo atakuwa adui yangu namba moja.

“Kipaumbele kingine ni kuboresha huduma za jamii kwa kuboresha miundombinu, afya, elimu, maji na kusimamia upelekaji wa huduma za jamii. Hapa nielekeze watumishi tuwe tunatoka maofisini. Nitafuatilia hatua kwa hatua kuhakikisha miradi inatekelezwa kwa wakati, ubora na thamani ya fedha inaonekana. Kwa wanaofuatilia mimi ni mtu wa porini (field),” ameelekeza.

Katika hatua nyingine, Dk. Sengati amewataka watumishi na watendaji wa serikali mkoani humo kuhakikisha wanashughulikia kero za wananchi kwa kuwatembelea na kushughulikia shida zao na kujiridhisha na miradi inayotekelezwa.

“Niseme tu kwamba sitegemei kupata hati chafu katika mkoa wangu wakati wote nitakaokuwa hapa, ikitokea hivyo nitachukulia kwamba watumishi hawatoshi na taratibu za kiutendaji na kinidhamu zitachukuliwa kuhakikisha watendaji wazembe wanaoondoka,” amesisitiza RC Sengati.

Vilevile, Dk. Sengati katika kuhakikisha kuwa wanayaenzi na kuendeleza mazuri yaliyofanyika pamoja na kuleta maendeleo endelevu katika mkoa huo, amekuja na salamu mpya ya mkoa wa Shinyanga isemayo ‘Shinyanga, Kazi iendelee kwa maendeleo endelevu’, huku akiomba ushirikiano kwa wadau na makundi yote katika jamii kuhakikisha mkoa huo unaendelea kusonga mbele.

“Shinyanga ni mkoa wa kimkakati kiuchumi ndani ya taifa la Tanzania kwa sababu uko njia panda kuelekea mataifa ya jirani, mkoa unao rasilimali nyingi ikiwemo mifugo inayokadiriwa kufika milioni tano. Nitahakikisha naendelea kusimamia sifa hiyo ya mkoa wetu kuhakikisha tunaendelea kuchangia kwenye pato la taifa,” amesema.

Akizungumza wakati akimkaribisha mkuu mpya wa mkoa na kuwaaga watendaji wa mkoa huo, aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack amewashukuru wana Shinyanga kwa ushirikiano mkubwa waliompa akiwa kiongozi wao kwa miaka mitano na miezi mitatu, huku akikumbuka namna alivyofanikisha uwekaji wat aa za barabarani na uanzishaji wa viwanda Zaidi ya 700 katika mkoa huo.

Telack ameeleza kuwa wakati anafika Shinyanga alikuta mambo yakiwa magumu mkoa huo ukiwa umegubikwa na mauaji ya vikongwe, ramli chonganishi, mimba kwa wanafunzi na ndoa za utotoni, lakini sasa vimepungua kwa kiasi kikubwa kutokana na ushirikiano mkubwa kutoka kwa viongozi wa dini,ambapo amemuomba Mkuu mpya wa mkoa kuendeleza ushirikiano huo mkubwa na viongozi hao wa dini.

“Nilipofika hapa niliona mambo ni magumu (mambo fulani mengi), hatuwezi kuachia mkoa unaongozwa na wachawi wakati sisi tupo. Hivyo niliwakabidhi viongozi wa dini wametusaidia sana hata kumaliza mauaji ya Wazee na kutusaidia kufikisha ujumbe kwenye nyumba za ibada hasa masuala ya chanjo.

“Mkuu wa mkoa umekuja kwenye mkoa ambao uko salama, muhimu ni ushirikiano ili muweze kufika, kubwa kuliko mengine ni ushirikiano, hakuna siri ya mafanikio bila ushirikiano, nashukuru kwa ushirikiano mlionipa.

“Watu walidhani Shinyanga ni kisiwa na wengine walioona ni kama mkoa wa mateso, lakini tumeufungua kutoka kwenye boksi, watu wameufahamu na sasa watu wakihamishiwa hapa hawanung'uniki. Tumefanya kazi kubwa sana kuutangaza mkoa wetu,” ameeleza.

Kwa upande wake Mwenyekiti Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga, Mabala Mlolwa amempongeza Zainab Telack kwa kazi kubwa aliyoifanya mkoani humo na kumtakia kheri, huku akimuomba kuyaendeleza yale mazuri katika kituo chake kipya cha kazi.

Mlolwa ameahidi kumpa ushirikiano wa kutosha Dk. Sengati ili kufanikisha mipango mizuri ya maendeleo, huku akimuomba kuongeza ubunifu mwingine kwenye kutekeleza miradi na mipango iliyopo kwenye ilani ya chama hicho

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Amani Mkoa wa Shinyanga, Shekhe Khamis Balilusa, ameeleza kuwa wakati Telack anafika mkoani humo, kwa imani na tamaduni za wenyeji wa mkoa huo wa walimuweka kwenye matazamio kama ataweza kazi, lakini alidhihirisha namna gani alivyo kiongozi shupavu.

Mwenyekiti wa Kamati ya Wazee mkoani humo, Faustine Sengerema amemzungumzia Zainab Telack na kueleza kuwa ni kiongozi shirikishi kwa wakati wote aliwashirikisha wazee kwenye mambo mbalimbali ya maendeleo.
Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela (kushoto) akimkaribisha katika ofisi za mkoa huo, Mkuu mpya wa Mkoa wa Shinyanga, Dk. Philemon Sengati (kulia) baada ya kuwasili leo akitokea Tabora
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dk. Philemon Sengati akisalimiana na baadhi ya viongozi wa dini alipowasili leo katika ofisi za mkuu wa mkoa huo
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dk. Philemon Sengati akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Mabala Mlolwa (wa tatu kushoto)
RC Dk. Sengati akisalimiana na kuteta na baadhi ya watendaji wa ofisi ya mkoa wa Shinyanga alipowasili leo
Dk. Sengati akisalimiana na kuteta na baadhi ya wakurugenzi wa halmashauri zilizopo katika mkoa huo, leo wakati wakimpokea
Afisa Rasilimali watu ofisi ya mkuu wa mkoa Shinyanga, Neema Rwegushora (kushoto) akimkabidhi ua kumkaribisha katika ofisi hizo, mkuu wa mkoa huo, Dk. Philemon Sengati
Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela akizungumza katika hafla hiyo
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack (kushoto) na Mkuu mpya wa mkoa huo, Dk. Philemon Sengati wakiomba wakati wa kufungua hafla hiyo ya makabidhiano
Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Zainab Telack ambaye alikuwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga akizungumza katika hafla hiyo baada ya kukabidhi ofisi kwa Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Dk.Philemon Sengati
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dk. Philemon Sengati (wa pili kulia) akibadilishana hati ya makabidhiano na aliyekuwa mkuu wa mkoa huo, Zainab Telack katika hafla ya kukabidhiana ofisi
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack (kushoto) akimpongeza mkuu wa mkoa huo, Dk. Philemon Sengati (kulia) baada ya kumkabidhi rasmi ofisi hiyo
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Mabala Mlolwa akizungumza katika hafla hiyo
Mwenyekiti wa Kamati ya Amani ya mkoa huo, Shekhe Khamis Balilusa akizungumza na kutoa neno la shukrani kwa niaba ya viongozi wa dini
Mkuu wa wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Talaba (kushoto) akiteta jambo na Mkuu wa wilaya ya Kahama, Anamringi Macha (kulia) wakati wa hafla ya kumkaribisha mkuu mpya wa mkoa wa Shinyanga
Mwenyekiti wa Shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu (SHIVYAWATA) mkoa wa Shinyanga, Richard Mpongo (wa pili kushoto) akimsalimia na kumpongeza Mkuu mpya wa mkoa wa Shinyanga, Dk. Philemon Sengati (wa tatu)




Baadhi ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa huo wakiwa kwenye hafla ya kumkaribisha mkuu wa mkoa
Baadhi ya wawakilishi wa taasisi binafsi na asasi za kiraia wakiwa kwenye hafla hiyo
Baadhi ya wawakilishi wa taasisi mbalimbali wakiwa kwenye hafla hiyo
Washiriki wa hafla hiyo wakifuatilia makabidhiano hayo
Baadhi ya wawakilishi wa migodi, viwanda na TCCIA wakiwa ni sehemu ya hafla hiyo
Hafla ikiendelea
Baadhi ya wawakilishi wa taasisi za fedha wakiwa ni sehemu ya hafla hiyo
Hafla ikiendelea
Baadhi ya wawakilishi wa vyama vya siasa wakiwa ni sehemu ya hafla hiyo
Wawakilishi wa makundi maalum wakifuatilia hafla hiyo
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, ACP Debora Magiligimba akiteta jambo na baadhi ya wawakilishi wa taasisi za kifedha mkoani humo
Picha ya pamoja na wakuu wa wilaya
Picha ya pamoja na viongozi wa dini
Picha ya pamoja na wawakilishi wa taasisi zisizo za kiserikali
Picha ya pamoja na viongozi wa CCM
Picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama
Picha ya pamoja na wawakilishi wa taasisi za fedha
Picha ya pamoja na wawakilishi wa vyama vya siasa
Picha ya pamoja na wawakilishi wa makundi maalum na wajasiriamali




Picha zote na Shinyanga Press Club Blog
Share:

Consultant at PSI

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

ADVERTISEMENT FOR MANAGEMENT INFORMATION SYSTEM CONSULTANCY SERVICES With over 45years of experience, working in over 60 countries, Population Service International (PSI) is the world’s leading non-profit social marketing organization. PSI is reimagining health care, by putting the consumer at the center, and wherever possible – bringing care to the front door. We are working to […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger