Tuesday, 25 May 2021

TAGCO CHAMPA TUZO DKT ABBASI KWA KUTAMBUA MCHANGO WAKE

 

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi, akitunukiwa Tuzo ya Shukrani kutoka kwa viongozi na wanachama wa Chama cha Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano Serikalini (TAGCO) kwa mchango wake aliotukuka kwenye kuleta mageuzi katika sekta ya habari nchini.



a.Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi (katikati) akiongoza kikao kazi cha Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano Serikalini Jijini Mbeya, kushoto ni Naibu wake Dkt. Ally Possi, kulia ni Katibu Mkuu -TAMISEMI Prof. Riziki Shemdoe

Na John Mapepele, Mbeya

 

Katibu Mkuu wa Habari wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbasi ametunukiwa tuzo na Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano wa Serikali (TAGCO) kwa kutambua mchango na mageuzi makubwa aliyoyafanya kwenye Sekta ya Habari hapa nchini.

Akikabidhi tuzo hiyo kwa Dkt. Hassan Abbasi, Mwenyekiti wa TAGCO, Paschal Shelutete wakati wa kikao cha 16 cha TAGCO kilichofanyika Jijini Mbeya Mei 24,2021 amesema Dkt. Abbasi ametoa mchango mkubwa akiwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari- MAELEZO na Mkuu wa Serikali tofauti na hapo awali.

“Ni katika kipindi hiki ambapo miradi ya kimkakati ya Serikali ilisemewa vizuri zaidi na kufahamika na watu wengi hivyo kuwafanya wananchi kuipenda Serikali yao” Amefafanua Shelutete.

Ameongeza kwamba Dkt. Abbasi amefanikiwa kusimamia tasnia ya Habari na uboresha mahusiano ya kikazi miongoni mwa wadau wote wa Sekta ya Habari.

kwa upande wake Dkt. Abbasi amewashukuru Waandishi kwa kumpa tuzo hiyo na kuahidi kuendelea kuwapa ushirikiano ili waweze kuendelea kutekeleza majukumu wao kikamilifu kwa nafasi yake ya sasa ya Katibu Mkuu. Wizara ya Habari, Utamadunim Sanaa na Michezo.

“Tuendelee kushirikiana katika cheo hiki kipya cha Katibu Mkuu katika Wizara yetu ambayo ni Wizara muhimu inayogusa umma kwa nyanja ya burudani na huzuni kutokana na Sekta zake” Ameongeza Dkt. Abbasi.

Amewataka Waandishi  kuzingatia weledi wakati wote wa undaji wao wa kazi ambapo amesisitiza kwamba Serikali inatambua mchango wa waandishi na kwamba  itaendelea  kuhakikisha sekta inaboreka  na kuchangia kwenye  uchumi wa Taifa.

Aidha amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kumwamini na kumrejesha  tena kwenye nafasi ya Katibu Mkuu  na kuahidi kufanya kazi kwa weledi na  bidi ili kutekelea Ilani ya Chama cha Mapinduzi na maelekezo ya Mheshimiwa Rais Samia.

Kikao hiki kimefunguliwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Innocent Bashungwa kimehudhuriwa na Naibu wa Wizara hiyo, Katibu Mkuu -TAMISEMI Prof. Riziki Shemdoe ambaye ametoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali ya kiutumishi kwa maafisa Habari kutoka halmashauri zote nchini,na viongozi mbalimbali wa Serikali na Maafisa Habari, Mawasiliano  na Uhusiano wa Serikali zaidi ya 270.


Share:

WAZIRI KALEMANI AAGIZA WAKANDARASI KUANZA UTEKELEZAJI WA MRADI WA KUMALIZIA VIJIJI VISIVYO NA UMEME

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akizungumza na Wakandarasi kutoka Kampuni 34 ambao wanatekeleza Mradi wa usambazaji umeme Vijijini wa Awamu ya Tatu, mzunguko wa Pili (hawapo pichani) kilichofanyika leo Mei 25,2021 jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato akizungumza wakati wa kikao na Wakandarasi kutoka Kampuni 34 ambao wanatekeleza Mradi wa usambazaji umeme Vijijini wa Awamu ya Tatu, mzunguko wa Pili (hawapo pichani) kilichofanyika leo Mei 25,2021 jijini Dodoma.

Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini REA, Mhandisi Amos Maganga akizungumzawakati wa kikao cha Waziri wa Nishati Dkt.Medard Kalemani na Wakandarasi kutoka Kampuni 34 ambao wanatekeleza Mradi wa usambazaji umeme Vijijini wa Awamu ya Tatu, mzunguko wa Pili (hawapo pichani) kilichofanyika leo Mei 25,2021 jijini Dodoma.

Baadhi ya Wasimamizi wa Miradi ya usambazaji umeme vijijini kutoka Wizara ya Nishati, watendaji wa REA, TANESCO na wakandarasi wa mradi wa usambazaji umeme vijijini wa Awamu ya Tatu mzunguko wa Pili wakimsikiliza Waziri wa Nishati, Dkt.Medard Kalemani (hayupo pichani) kilichofanyika leo Mei 25,2021 jijini Dodoma.wa mwisho kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Jones Olotu.

Baadhi ya Mameneja wa TANESCO kutoka sehemu mbalimbali nchini pamoja na Wakandarasi wa mradi wa usambazaji umeme vijijini wa Awamu ya Tatu, mzunguko wa Pili wakimsikiliza Waziri wa Nishati, Dkt.Medard Kalemani (hayupo pichani) wakati alipofanya kikao na wakandarasi hao jijini Dodoma.


Na.Alex Sonna,Dodoma

WAZIRI wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amewaagiza wakandarasi walioshinda zabuni ya kutekeleza Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili kuripoti kwa viongozi wa wilaya ambako wanatekeleza miradi ya kusambaza umeme vijijini pamoja na kuanza utekelezaji wa Mradi huo mara moja.

Dkt. Kalemani alitoa agizo hilo leo Mei 25,2021 jijini Dodoma wakati wa kikao kazi kati ya Wizara ya Nishati, Wakala wa Nishati Vijijini (REA), TANESCO na wakandarasi amesema kuwa Kuna faida nyingi za kuripoti katika ofisi za wilaya na vijiji ikiwa ni pamoja na kupata uhakika wa usalama wa rasilimali watu na vifaa vya mradi. Madhara ya kutoripoti ni makubwa zaidi”

“Baada ya mkutano huu msambae katika maeneo yenu ya kazi mara moja..niwaombe sana muende site muanze kuchapa kazi” alisema na kuwataka wahakikishe wanaunganisha umeme kwenye vijiji vyote nchini ambavyo havina huduma ya umeme ndani ya miezi 18 kuanzia sasa.

Amesema kuwa wakandarasi watekeleze miradi kwa kushirikisha viongozi na wananchi ili kujenga mahusiano mazuri na watoe kipaumbele kwa kutoa ajira hasa kazi za vibarua kwa vijana wa vijijini ambako miradi ya kusambaza umeme inatekelezwa.

Dkt. Kalemani amewataka wakandarasi kuwaunganishia umeme wananchi ndani ya siku 14 baada ya kufanya malipo ya kuunganishiwa umeme na wasibague nyumba za tembe, vibanda vya biashara pamoja na maeneo ya mazizi ya mifugo kwa wananchi watakaohitaji huduma hiyo.

Aidha Dkt.Kalemani ametoa onyo kwa wakandarasi na mafundi wanaoweka mifumo ya nyaya ndani ya nyumba ‘wiring’ ambao sio waaminifu kuacha tabia hiyo mara moja ya kuwatapeli wananchi na kuwataka REA na TANESCO kuhakikisha kero hiyo haitokei tena katika miradi ya kusambaza umeme vijijini.

Miongoni mwa mambo ambayo Waziri amewasisitizia wakandarasi kuyazingatia ni pamoja na kununua vifaa bora vinavyotengenezwa na viwanda vya ndani ya nchi na amewataka wenye viwanda kutengeneza vifaa vyenye ubora na kwa wingi ili kukidhi mahitaji ya miradi ya kusambaza umeme vijijini.

Amesema kutokana na mradi huo kutohusisha ulipaji fidia kwa wananchi ambao sehemu ya maeneo yao itatumika kupitishia miundombinu ya umeme, wakandarasi wanapaswa kutumia busara wakati wa ujenzi wa miundombinu hiyo. “Mwananchi ana kiwanja chake kidogo, lakini nguzo inatakiwa kuwekwa katika eneo hilo. 

Utakuta badala ya nguzo kuwekwa mahali ambapo ataweza kuendelea na shughuli nyingine katika eneo hilo, mkandarasi anasimika nguzo katikati ya eneo…naomba mkatumie busara mkapitishe miundombinu ya umeme pasipo kuathiri matumizi eneo la mwananchi,” amefafanua.

Hata hivyo, Dkt. Kalemani amesema ili kupunguza hujuma za vifaa na miundombinu, wakandarasi wanapaswa kuajiri vibarua ambao ni waaminifu na wawe wa kwanza kulinda vifaa vyao na aliwataka wananchi kuacha kuhujumu miundombinu ya kusambaza umeme vijijini.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Nishati, Stephen Byabato ameahidi kuhakikisha mradi huo unatekelezwa kwa wakati huku akiwataka wasimamizi wa mradi kuwa vikao kazi na wakandarasi katika maeneo ya miradi na kuandaa ripoti za vikao hivyo ambazo zitatumika kwa ajili ya maelekezo ikiwa ni pamoja na kuboresha utekelezaji wa Mradi.

 "Tutajikita zaidi kusimamia mikataba yenu, kuna wengine hamzingatii masharti ya mikataba yenu lazima tukumbushane” amesema. 

 

Naye Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Amos Maganga amewahakikishia wakandarasi kuwa Serikali inafuatilia malalamiko ya hujuma ya miundombinu na vifaa katika baadhi ya maeneo na kuwashauri wawashirikishe viongozi wa vijiji katika ulinzi wa vifaa.

Share:

Wimbo Mpya: Tundaman Ft. Mo Dewji – True love

 Wimbo Mpya: Tundaman Ft. Mo Dewji – True love



Share:

Mkuu wa Mkoa wa Dar , Amos Makalla awataka majambazi Dar kusalimisha silaha

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam , Amos Makalla amewataka majambazi na wahalifu kujisalimisha Polisi na kukabidhi silaha zao huku akitangaza operesheni ya kuwasaka popote walipo.

Makalla amesema hayo baada ya kikao na Makamanda wa Polisi huku akirejea matukio yaliyotokea hivi karibuni likiwemo la Mbezi ambapo Jimmy Kibiti aliuawa kwa kupigwa risasi wakati akitoka benki na kuporwa Sh4 milioni na la jana la mfanyabiashara kujeruhiwa kwa risasi eneo la Mabibo.


“Nataka Dar es Salaam iwe mahali salama. Tunawaonya waache mara moja, matukio hayo mawili waliyoyafanya yanatosha. Hawa wanabip sisi tuna bando la kutosha. Tunawaonyesha shoo kwa shoo kwamba polisi wapo, watakuwa fundisho kwa wengine.

"Wasijaribu njiti kama zimejaa kwa kutingisha kiberiti. Niseme tu wasalimishe silaha, kamanda Wambura (Camillius) sikufundishi kazi ila nakwambia wanyang'anye, najua wapo watakaotoa kwa hiari na wale mtakaowakuta nazo wanyang'anyeni," amesema.

Katika mkutano na wanahabari, Wambura ametoa onyo kwa wahalifu akiwataka kuacha mara moja, “wasijaribu kupima kina cha maji kwa miguu yao kwani ni mifupi. Tunawaonya wale wote wanaotaka kucheza na jeshi la polisi, wajitathmini kwanza. Wale wote wanaotaka kushindana na Serikali wakae chonjo saa mbaya, wasijaribu kupima kina cha maji na miguu yao mifupi, wajitathmini kwanza.”

Alieleza kuwa polisi wamekamata bunduki aina ya Short Gun Pump, watuhumiwa 20, magari manne pamoja na pikipiki moja.


Share:

SALOME WIG POINT TZ WANOGESHA MAONESHO YA WAJASIRIAMALI NA WAWEKEZAJI KAHAMA....TAZAMA BIDHAA ZAO HAPA

Kampuni ya Salome Wig Point Tz wanaojihusisha na utengenezaji wa Wig aina zote, kusuka mitindo yote ya nywele,kukodisha magari na kupamba maharusi inashiriki katika Maonesho ya Wajasiriamali na Wawekezaji Kahama yaliyoandaliwa na Taasisi ya GS1 Tanzania kupitia Kituo cha Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Kahama.

Akizungumza na Malunde 1 blog leo Jumanne Mei 25,2021 Mkurugenzi wa Kampuni ya Salome Wig Point Tz, Bi. Salome Mvanga amesema wanashiriki maonesho hayo ili kuonesha na kuuza bidhaa mbalimbali wanazotengeneza.

"Salome Wig Point Tz tunapatikana  Mkabala na Gaprena Hotel Mjini Kahama na Kariakoo Jengo la JAH Plaza jijini Dar es salaam.

Tunatengeneza ma wig,  tunauza vipodozi, ma wig aina zote kwa bei ya jumla na reja reja, tunatengeneza nywele natural, vibanio vya nywele, tunafanya make up, tunasuka nywele aina zote.  Karibuni kwa huduma zote za urembo na ushauri. Mawasiliano yetu ni 0763278182",amesema Salome.

Maonesho ya Wajasiriamali na Wawekezaji Kahama yameanza Jumatatu Mei 24,2021 yakitarajiwa kufikia tamati Mei 30,2021 katika viwanja vya Kituo cha Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kilichopo Nyihogo Mjini Kahama yanaongozwa na kauli mbiu ya ‘Nunua bidhaa za Kitanzania kuza uchumi wa nchi’ yakiwapa Wajasiriamali fursa ya kuonesha na kuuza bidhaa zao.
Mfanyakazi wa Kampuni ya Salome Wig Point Tz, Bi. Magreth Paschal akionesha bidhaa mbalimbali wanazotengeneza na kuuza kwenye Maonesho ya Wajasirimali na Wawekezaji Kahama leo Jumanne Mei 25,2021 . Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Wafanyakazi wanKampuni ya Salome Wig Point Tz, Bi. Magreth Paschal na Elvira Richard (kushoto) wakionesha bidhaa mbalimbali wanazotengeneza na kuuza kwenye Maonesho ya Wajasirimali na Wawekezaji Kahama leo Jumanne Mei 25,2021 
Wafanyakazi wa Kampuni ya Salome Wig Point Tz, Bi. Magreth Paschal na Elvira Richard  (kushoto) wakionesha bidhaa mbalimbali wanazotengeneza na kuuza kwenye Maonesho ya Wajasirimali na Wawekezaji Kahama leo Jumanne Mei 25,2021 
Wafanyakazi wa Kampuni ya Salome Wig Point Tz, Bi. Magreth Paschal na Elvira Richars (kushoto) wakionesha bidhaa mbalimbali wanazotengeneza na kuuza kwenye Maonesho ya Wajasirimali na Wawekezaji Kahama leo Jumanne Mei 25,2021 

Share:

BRI COLLECTION & ASILIA AFRICAN CRAFT WASHIRIKI MAONESHO YA WAJASIRIAMALI NA WAWEKEZAJI KAHAMA

Kampuni ya Bri Collection inayojihusisha na uuzaji nguo na Kampuni ya uuzaji wa viatu vya ubunifu za uzi na ngozi na asali inayojulikana kwa jina Asilia African Craft wanashiriki Maonesho ya Wajasiriamali na Wawekezaji Kahama yaliyoandaliwa na Taasisi ya GS1 Tanzania kupitia Kituo cha Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Kahama ili kuonesha na kuuza bidhaa zao.

Bri Collection na Asilia African Craft ni Wajasiriamali kutoka Jijini Dar es salaam wanapatikana Mwenge, wanauza bidhaa mbalimbali ikiwemo  nguo  za pamba, tisheti na Vest pamoja na asali mbichi na viatu vya ubunifu za uzi na ngozi ambazo wametengeneza wao wenyewe. Mawasiliano yao ni 0718903197 (Bri Collection) au 0719365727 (Asilia African Craft).

Maonesho ya Wajasiriamali na Wawekezaji Kahama yameanza Jumatatu Mei 24,2021 yakitarajiwa kufikia tamati Mei 30,2021 katika viwanja vya Kituo cha Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kilichopo Nyihogo Mjini Kahama yanaongozwa na kauli mbiu ya ‘Nunua bidhaa za Kitanzania kuza uchumi wa nchi’ yakiwapa Wajasiriamali fursa ya kuonesha na kuuza bidhaa zao.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Bri Collection inayojihusisha na uuzaji nguo Bi. Brihanna Emmanuel na Mkurugenzi wa Kampuni ya uuzaji wa viatu vya ubunifu za uzi na ngozi na asali inayojulikana kwa jina Asilia African Craft,  Reginald Saria (kulia) wakionesha bidhaa mbalimbali kwenye Maonesho ya Wajasiriamali na Wawekezaji Kahama leo Jumanne Mei 25,2021. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkurugenzi wa Kampuni ya Bri Collection inayojihusisha na uuzaji nguo Bi. Brihanna Emmanuel (kushoto) na Mkurugenzi wa Kampuni ya uuzaji wa viatu vya ubunifu za uzi na ngozi na asali inayojulikana kwa jina Asilia African Craft,  Reginald Saria wakionesha bidhaa mbalimbali kwenye Maonesho ya Wajasiriamali na Wawekezaji Kahama leo Jumanne Mei 25,2021. 
 Mkurugenzi wa Kampuni ya uuzaji wa viatu vya ubunifu za uzi na ngozi na asali inayojulikana kwa jina Asilia African Craft,  Reginald Saria akionesha asali kwenye Maonesho ya Wajasiriamali na Wawekezaji Kahama leo Jumanne Mei 25,2021. 
Mkurugenzi wa Kampuni ya Bri Collection inayojihusisha na uuzaji nguo Bi. Brihanna Emmanuel akionesha nguo anazouza kwenye Maonesho ya Wajasiriamali na Wawekezaji Kahama leo Jumanne Mei 25,2021. 
Mkurugenzi wa Kampuni ya Bri Collection inayojihusisha na uuzaji nguo Bi. Brihanna Emmanuel akionesha viatu kwenye Maonesho ya Wajasiriamali na Wawekezaji Kahama leo Jumanne Mei 25,2021. 
Mkurugenzi wa Kampuni ya Bri Collection inayojihusisha na uuzaji nguo Bi. Brihanna Emmanuel bidhaa za utamaduni kwenye Maonesho ya Wajasiriamali na Wawekezaji Kahama leo Jumanne Mei 25,2021. 
Mkurugenzi wa Kampuni ya Bri Collection inayojihusisha na uuzaji nguo Bi. Brihanna Emmanuel bidhaa za utamaduni kwenye Maonesho ya Wajasiriamali na Wawekezaji Kahama leo Jumanne Mei 25,2021. 
Share:

MV- Mwanza Kuweka Msingi Imara Wa Biashara Ukanda Wa Ziwa Victoria, Kenya Na Uganda.


Na.Paschal Dotto-MAELEZO
Serikali inaendelea na utekeleza wa miradi mingi ya kuimarisha miundombinu katika sekta mbalimbali ikiwemo mradi ya umeme (JNHPP-Julius Nyerere Hydropower project) kwa gharama ya TZS Trilioni 6.5, Ujenzi wa Reli ya Kisasa SGR kwa gharama ya shilingi trilioni 7 na miradi mingine ambayo itaweka mazingira wezeshi kwa wananchi kufanya biashara na uwekezaji.

Mnamo Desemba 8, 2019, Rais wa  Awamu ya Tano  Hayati,  Dkt. John Magufuli alizindua ujenzi wa mradi mwingine mkubwa wa ujenzi wa meli kubwa ya abiria na mizigo, ukarabati wa meli na ujenzi wa chelezo  katika lango la biashara na kiuchumi kanda za ziwa  ambao utekelezaji wake unaendelea vizuri ambapo hadi kukamilika kwake utagharimu zaidi ya shilingi  bilioni 153.

Meli ya “MV Mwanza Hapa Kazi” itakayogharimu shilingi bilioni 89,  ni mradi wa ujenzi ambao unatekelezwa na kampuni ya ujenzi ya GAS ENTEC wakishirikiana na KANG NAM kutoka Korea Kusini pamoja na SUMA JKT kutoka Tanzania. Meli hii itakuwa mbadala wa meli ya MV Bukoba ambayo miaka 25 iliyopita ilizama na kupoteza maisha ya Watanzania wengi. Katika kampeni za Uchaguzi Mkuu wa 2015 Rais wa Awamu ya Tano, Hayati, Dkt John Pombe Magufuli aliwaahidi wananchi wa kanda ya ziwa kuwa atajenga meli kubwa kuwaenzi waliokufa kwenye ajali hiyo lakini pia  kuimarisha usafirishaji upande huo wa Tanzania kwani kuna fursa nyingi za biashara, anaeleza Meneja Mradi Mhandisi,  Vitus Mapunda.

Katika moja ya Hotuba zake akiwa ziarani Jijini Mwanza 2019,  Hayati Magufuli alisema  “Ni miaka 23, Baada ya kuzama meli ya MV Bukoba mwaka 1996, miaka mingi imepita, lakini pia kuharibika kwa meli ya mizigo kumekuwa na tatizo kubwa katika  sekta ya usafarishaji kwa wananchi wanaioshi kuzunguka ziwa Victoria na hivyo kuathiri shughuli za uchumi na uzalishaji kanda ya ziwa”.

 Serikali ya Awamu ya Sita Chini ya Jemedari, Samia Suluhu Hassan, inaendelea na  utekelezaji wa mradi huo mkubwa ambao uliambatana na miradi mingine kama vile ukarabati wa meli ya Mv Victoria uliogharimu shilingi bilioni 22.7, Mv Butiama bilioni 4.9, ambapo ujenzi wake ulitekelezwa na Kampuni ya Ujenzi ya KTMI kutoka Korea Kusini huku ujenzi wa chelezo uliogharimu shilingi Bilioni 36.4, ukitekelezwa na Stx Engine ikishirikina na SAE Kyong kutoka Korea Kusini. Kati ya miradi hiyo, ujenzi wa chelezo na ukarabati wa meli mbili umekamilika na ujenzi wa meli mpya ya MV Mwanza Hapa Kazi Tu ukiwa  umefikia asilimia zaidi ya 50, na  miradi yote hii itagharimu shilingi  bilioni 153.7, baada ya kukamilika na miradi yote hii inatekelezwa kwa  pesa za Watanzania.

MV Mwanza Hapa Kazi tu, itakuwa na uwezo wa kubeba abiria 1,200, mizigo tani 400, magari makubwa 3 na magari madogo 20, huku ikiwa na urefu wa mita 92, ambapo MV. Victoria ikibeba abiria 1,200, mizigo tani 200 na MV. Butiama ikibeba abiria 200 na mizigo tani 100. Meli zote tatu zitakuwa na uwezo wa kubeba abiria 2,600 na tani 700 za mizigo, kwa wakati mmoja na hivyo  kupunguza adha ya usafiri na usafirishaji kwa abiria na mizigo katika ukanda huo.

“Ni wazi kuwa utekelezaji  wa miradi hii utakaogharimu shilingi bilioni 153 utasaidia sana kutatua tatizo la usafirishaji kwa wananchi wanaoishi ziwa Victoria, siyo tu hapa nchini bali hata kwa jirani zetu Kenya na Uganda kwa hiyo ni miradi ambayo ina manufaa kwa uchumi wetu”, Hayati, Dkt. John Magufuli.

 Aidha, Serikali ya Awamu ya Sita inaeleza kuwa ujenzi wa mradi huo mkubwa  MV Mwanza Hapa Kazi Tu, utafungua ukanda huo kibiashara na kusaidia kukuza pato la taifa, kama ilivyokuwa kwa Serikali ya Awamu ya Tano Serikali ya sasa imejitabanaisha kuendelea kufanya mabadiliko makubwa kwa kuleta miradi wezeshi kwa wananchi bila kutegemea misaada yenye masharti lukuki.

Sekta hii ya usafirishaji kwa njia ya maji imekuwa muhimu sana na Serikali kupitia Mamlaka ya  Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) pamoja na Shirika la Huduma za Meli Tanzania (MSCL) wamekuwa na usimamizi madhubuti ili kukuza sekta hiyo kwani ni nyenzo kubwa katika uchumi.

Kampuni ya Huduma za meli iliyoanzishwa na  Hayati Baba wa taifa Mwl. Julius Nyerere kwa sasa inafanya kazi kubwa baada ya  Hayati, Dkt. Magufuli kuingia madarakani na kuiongezea nguvu kifedha na kiutendaji. Kijiti hicho kwa sasa kipo kwa Rais Samia Suluhu Hassan, kwani hapo mwanzo ilikuwa na meli 14 ikiwemo meli ya utalii lakini ilikuja kuanguka kutokana uongozi mbovu, vitendo vya wizi na ubadhilifu wa mali za umma na kufanya meli zote 14 kufa na  kubaki na moja tu.

TPA imekuwa ikiendelea na upanuzi  na ujenzi wa Bandari mbalimbali nchini zikiwemo bandari ya Dar es Salaam, Mtwara, Tanga, Mwanza pamoja na bandari zake ndogondogo za Kemondo, Bukoba, Kwemukwikwi na Nyamirembe kwa upande wa kanda ya ziwa, na Bandari ya Kigoma.

Mhandisi Mapunda anaeleza kuwa Ujenzi wa Meli mpya “Mv Mwanza Hapa Kazi Tu” umefikia asilimia 53 tofauti na sasa ujenzi unaendelea vyema ili kuwawezesha wafanyabiashara wa ukanda huo kuwa na nafuu ya usafiri na usafirishaji  mizigo baada ya mradi huo kukamilika.

Utekelezaji wa miradi hiyo umeweza kutoa fursa nyingi kwa wananchi wa mkoa wa Mwanza ikiwemo ajira kwani mpaka sasa kuna ajira zaidi ya 1,000 na bado zinaongezeka kwa kadri siku zinavyosonga mbele katika utekelezaji wa miradi hiyo mikubwa kwa kanda ya ziwa.

Ujenzi wa Meli hii Kubwa ni utekelezaji wa ahadi na kufanya maono ya Baba wa Taifa Mwl.Julius Nyerere aliyetaka kuwepo na meli kubwa kwa ukanda huo wa kiuchumi wa Tanzania, na alijenga MV Bukoba iliyokuja kuzama mwaka 1996 na kuleta ugumu wa sekta ya usafirishaji kutumia Ziwa Victoria na sasa Serikali inayaishi maono ya Hayati Baba wa Taifa Julius Nyerere,  baada ya kujenga MV Mwanza Hapa Kazi Tu.

Mwisho





Share:

Finance Manager at Plan International

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

Location: Geita, Tanzania Company: Plan International The Organisation Plan International is an independent development and humanitarian organisation that advances children’s rights and equality for girls. We believe in the power and potential of every child. But this is often suppressed by poverty, violence, exclusion and discrimination. And it’s girls who are most affected. Working together with children, […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

Mwili wafukuliwa kaburini, wakatwa kichwa na Viungo Vingine


Mkuu wa wilaya ya Gairo mkoani Morogoro, Siriel Mchembe ameagiza kutafutwa na kukamatwa kwa watu wanaotuhumiwa kunyofoa viungo vya mwili vya marehemu Rehema Michael Mei 24, mwaka huu.

Mchembe ametoa agizo hilo kwa jeshi la polisi wilayani humo, baada ya kubaini kuwa kaburi ulimozikwa mwili wa Rehema limefukuliwa na watu wasiojulikana, na kunyofolewa viungo kikiwemo kichwa, sehemu za siri, moyo na mapafu na kisha kutokomea navyo kusikojulikana.

Rehema alifariki dunia Mei 22 kwa ajali ya gari na kuzikwa katika kijiji cha Nguyami wilayani Gairo Mei 23 mkoani Morogoro.

Mchembe amefika kwenye kaburi hilo akiwa ameongozana na Kamanda wa polisi wa wilaya ya Gairo na Mganga Mkuu wa wilaya hiyo.


Share:

Azam Media ,TFF na Bodi ya Ligi (TPLB) Wasaini Mkataba wa Bilioni 225.6 kuonesha matangazo ya mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara


Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Bodi ya Ligi (TPLB) na Azam Media Limited kwa pamoja wameingia makubaliano ya kuonesha matangazo ya mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara kwa muda wa miaka 10.

Pande hizo zimesaini makubaliano ya mkataba huo hii leo Mei 24, 2021 jijini Dar es salaam.

Thamani ya mkataba huu ni kwa ajili ya maendeleo ya Ligi Kuu Tanzania Bara na kwa kutambua hilo, fedha ambayo imewekezwa katika mkataba huu, asilimia 67 itakwenda moja kwa moja kwa timu ambazo zinashiriki ligi hiyo.

Kwa ufafanuzi zaidi ni kuwa kwa msimu ujao yaani 2021/2022, Azam Media Limited itatoa Shilingi bilioni 12, huku timu zinazoshiriki katika Ligi Kuu Tanzania Bara zikipata Shilingi bilioni nane, mgao mwingine utakwenda kwa maendeleo ya soka, TFF na Bodi ya Ligi Kuu (TPLB).

Fedha hizo zitaendelea kuongezeka kwa kila msimu na msimu wa mwisho wa mkataba yaani 2030/2031, Azam itatoa Shilingi bilioni 28 na wakati huo timu zote kwa ujumla zitapata takribani Shilingi bilioni 19.

Lakini pia kiwango ambacho kitatolewa msimu ujao kitaongezeka zaidi ya mara mbili mpaka itakapofika msimu wa mwisho wa mkataba. Na kila nafasi ambayo timu imemaliza katika Ligi Kuu Tanzania Bara itakuwa na bonasi ambayo itatolewa kulingana na nafasi ya timu kwenye msimamo wa ligi.

Kwa misimu mitatu ijayo yaani 2021/22 mpaka 2023/24, bingwa wa Tanzania Bara atakuwa akipata Shilingi milioni 500 kwa msimu. Mshindi wa pili Shilingi milioni 250, mshindi wa tatu Shilingi milioni 225 na mshindi wa nne Shilingi milioni 200.

Fedha hizo zitakuwa zikiongezeka kila msimu na ndio maana msimu wa 2028/29 mpaka 2030/31 bingwa atakuwa akipata Shilingi milioni 700 kwa msimu. Mshindi wa pili Shilingi milioni 325, mshindi wa tatu Shilingi milioni 275 na mshindi wa nne Shilingi milioni 250.



Share:

Illustrator (Re-Advertisement) at International Rescue Committee

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

Requisition ID: req12479 Job Title: Re-Advertisement: Illustrator Sector: Education Employment Category: Fixed Term Employment Type: Full-Time Open to Expatriates: No Location: Kasulu, Tanzania Job Description   The International Rescue Committee (IRC) helps people whose lives and livelihoods are shattered by conflict and disaster to survive, recover, and gain control of their future. Founded in 1933 at the request of Albert Einstein, the […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

Technical Lead Gender transformative programming and Influencing at Plan International

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

Location: Geita, Tanzania Company: Plan International The Organisation Plan International is an independent development and humanitarian organisation that advances children’s rights and equality for girls. We believe in the power and potential of every child. But this is often suppressed by poverty, violence, exclusion and discrimination. And it’s girls who are most affected. Working together with children, […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

Wizara Yatangaza Operesheni Komesha Uhalifu Nchi Nzima, IGP Sirro Kuongoza Ma RPC Katika Operesheni Hiyo


 Na Abubakari Akida ,Dodoma
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imetangaza Operesheni Maalumu lengo ni kukomesha uhalifu ambao umeanza kurejea taratibu baada ya muda mrefu nchi kuwa katika hali ya amani na usalama.

Akizungumza  mbele ya Mkutano wa Waandishi wa Habari jijini Dodoma, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,George Simbachawene amesema kwa tathmini uhalifu umepungua sana nchini ila baadhi ya matukio machache yanayotokea yamekua yanapata muhamko mkubwa kutokana na njia za upashanaji habari kubadilika hivi sasa.

“Sisi kama Wizara kupitia Jeshi la Polisi tumejipanga,leo nimekaa kikao na IGP Sirro pamoja na Makamishna wake wote tumejadiliana kuimarisha hali ya ulinzi na usalama kwa wananchi wetu na sasa tunakuja na Operesheni ya Nguvu katika mikoa yote lakini la pili tunasisitiza ulinzi shirikishi maana Watanzania ni wengi ukizingatia idadi ya askari wetu,tunawaomba wenzetu wa TAMISEMI kupitia Kamati za Ulinzi zinazoongozwa na Wakuu wa Mikoa na Wilaya hadi kushuka ngazi ya chini tushirikiane ili kuweza kurudisha dhana ile ya ulinzi shirikishi ambayo ilisaidia sana kukomesha uhalifu” alisema Simbachawene

Akizungumzia tukio la mauaji ya mtoto anaekadiriwa kuwa na umri wa miaka 5 hadi 6 ambae mwili wake uliokotwa karibu na dimbwi la maji katika Kitongoji cha Usadala,Kijiji cha Utemini,kata ya Ndono,wilaya ya Uyui,mkoa wa Tabora, Waziri Simbachawene amesema upelelezi wa awali unaonyesha kama alitupwa huku mwili ukiwa umearibika sana huku akiweka wazi uchunguzi wa jeshi la polisi unaendelea wakishirikiana na Mkemia Mkuu wa Serikali kubaini vinasaba vya mwili wa mtoto huyo kama alikuwa albino au la.

“Nimesikia baadhi ya taasisi za haki za binadamu wakinitaka niseme, nitoe kauli lakini nasema hapana maana upelelezi wa polisi una taratibu zake na tunaendelea kupeleleza kitaalamu juu ya tukio hilo, tunaomba watuamini ili tuache tufanye kazi kitaalamu” alisema Simbachawene

Akizungumza katika Mkutano huo Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini,Simon Sirro amewataka wahalifu kuacha matendo ya hovyo mara moja huku akiweka nguvu ya jeshi katika kupambana na wahalifu.

“Ukitaka kuishi maisha mazuri na marefu acha uhalifu lakini kitendo cha kuendelea kufanya uhalifu ni kuichokoza serikali na niwaambie serikali ni ile ile,IGP ni yuleyule na Rais ni yule yule na ana madaraka ni yaleyale,watu watii sheria bila shuruti kuna watu wametoka gerezani wamerudia matendo yale yale waache hayo matukio kama wanapenda Watoto wao na familia zao” alisema IGP Sirro


Share:

Ujenzi Wa Bomba La Mafuta Ni Kielelezo Cha Ushirikiano Kati Ya Tanzania Na Uganda


 Na. Beatrice Sanga -Maelezo
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania mhe. Samia Hassan Suluhu amesema kuwa ujenzi wa bomba la mafuta utakuza na kuimarisha ushirikiano kati ya nchi za Tanzania na uganda

Akihutubia katika hafla ya utiaji saini mkataba hodhi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi la Afrika Mashariki litakalo jengwa kuanzia Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga nchini Tanzania kati ya Serikali ya Tanzania na kampuni ya mafuta ya ghafi ya Afrika Mashariki (EACOP)  Mhe. Samia alionesha imani kuwa mradi huo utachochea juhudi za pamoja za utafutaji mafuta na gesi katika nchi za ukanda huu zikiwemo Tanzania, DRC, Burundi na Sudan Kusini na pia utawavutia wawekezaji wengi zaidi kuja kuwekeza Tanzania na nchi nyingine katika ukanda huu.

“Ujenzi wa bomba hilo utachochea utafutaji wa mafuta wa pamoja katika eneo la afrika mashariki na unatarajiwa kukuza sekta ya utalii, kilimo biashara na usafirishaji na utafiti wa rasilimali mafuta kwa nchi nyingine za Afrika”,alisema Mhe.Samia.

Kwa upande wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni  amesema moja ya changamoto kubwa alizoziona katika safari yake ya kupigania ukombozi na maendeleo ya Afrika ni kukosekana kwa mwelekeo lakini kuanza kwa mradi huu ni uthibitisho kuwa sasa mwelekeo unaonekana.

Ni miaka takribani mitatu sasa imepita tangu kuwekwa kwa jiwe la ujenzi wa bomba hilo lenye urefu wa jumla ya kilometa 1,443 zikiwemo 1,115 zitakazojengwa ndani ya ardhi ya Tanzania. Mradi huo utagharimu Dola za Marekani bilioni 3.55/- na unatarajiwa kusafirisha mapipa laki 2 ya mafuta kwa siku na wakati wa ujenzi ajira kati ya 6,000 mpaka 10,000 zitazalishwa.

Kwa sasa Serikali za Uganda na Tanzania pamoja na kampuni ya mafuta ya Total ya Ufaransa na Sinoc ya China kwa kushirikiana na mashirika yanayohusika uzalishaji mafuta ya Tanzania na Uganda, zimeshasaini mikataba na ujenzi utaanza mara moja.

Katika mikataba hiyo nchi za Tanzania na Uganda kila moja inamiliki asilimia 15 ya hisa zote za kampuni hiyo, na kutokana na umiliki huo Tanzania itapata asilimia 60 ya mapato na Uganda itapata asilimia 40 zitakazotokana na mapato ya Dola za Marekani Milioni 290 zinazotarajiwa katika kipindi cha miaka 25 ya uhai wa mradi huo. Tanzania itapata mapato ya Dola za Marekani milioni 73, fedha za kigeni zitaongezeka kwa asilimia 53 na ajira zaidi ya 10,000 katika mikoa 8, Wilaya 24, Kata 134, vijiji 257, na vitongoji 527 ambako bomba litapita.

Ujenzi wa mradi huo ni kielelezo tosha cha ushirikiano wa Tanzania na Uganda kwani taarifa zinaeleza kuwa mradi huo ulipaswa kujengwa kupitia bandari ya Lamu nchini Kenya.

Hata hivyo, viongozi wa Tanzania na Uganda wanaamini kwamba utulivu wa kisiasa, usalama na uzoefu wa kuendesha miradi ya kusafirishaji mafuta ndiyo sababu iliyofanya mradi huu kujengwa nchini Tanzania

Aidha, Tanzania ina uzoefu wa muda mrefu katika utekelezaji, ujenzi, uendeshaji na uhudumiaji wa Bomba la Mafuta la Tanzania na Zambia (TAZAMA) lililojengwa mwaka 1968, likitoka Dar es Salaam mpaka Ndola Zambia.

Bomba la TAZAMA lina kipenyo cha inchi 8 mpaka 12 na urefu wa kilometa 1,710, kati ya hizo kilometa 860 zipo kwenye ardhi ya Tanzania na limekuwa likipitisha mafuta tani milioni 1.1 kwa mwaka.

Tanzania pia ina sifa ya uzoefu wa ujenzi, uendeshaji na uhudumiaji wa bomba la gesi kutoka Songo Songo mpaka Dar es Salaam, lenye kipenyo cha nchi 12 na urefu wa kilometa 25 kutoka kisiwa cha Songo Songo mpaka Somangafungu.

Pia kuna bomba lingine la urefu wa kilometa 207 na kipenyo cha inchi 16, kutoka Somangafungu mpaka Ubungo Dar es Salaam, mbali na bomba kubwa la gesi kutoka Mtwara mpaka Kinyerezi Dar es Salaam lenye zaidi ya kilometa 490.

Aidha, kuna bomba la gesi linalotoka Mnazi Bay kwenda Mtwara, lenye urefu wa kilometa 27 na kipenyo cha inchi 8, ambalo limeanza kutumika tangu 2006. Haya yote yanatajwa kusababisha mradi huu kujengwa katika ardhi ya Tanzania.

Hatua hizi zote zinadhihirisha ushirikiano wa kibiashara uliopo kati ya Tanzania na Uganda na nchi zingine za jirani katika kujenga uchumi  kwa nchi zote.


Share:

Rais wa Mali na Waziri Mkuu washikiliwa na jeshi


Maafisa wa kijeshi wa Mali waliokasirishwa na mabadiliko ya baraza la mawaziri wanamshikilia rais na waziri mkuu katika kambi ya jeshi, hatua inayolaaniwa vikali na jumuiya ya kimataifa na kutaka waachiliwe huru.


Taarifa ya pamoja iliyotolewa na Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS, Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika, Umoja wa Ulaya, Marekani na Uingereza imetoa wito wa kuachiliwa huru mara moja kwa Rais Bah N'Daw na Waziri Mkuu Moctar Ouane, ambao wameshikiliwa katika kambi ya kijeshi.

Kukamatwa kwao viongozi hao wanaongoza serikali ya mpito ambayo iliundwa kufuatia mapinduzi ya kijeshi mnamo mwezi Agosti, kumeongeza hofu ya kutokea mapinduzi mengine. Viongozi hao walikamatwa baada ya kufanya mabadiliko ya baraza la mawaziri mapema jana ili kutuliza ukosoaji mkubwa uliokuwa ukiikabili serikali yao ya mpito.

Aidha Umoja wa Ulaya umesema uko tayari kuzingatia kuwachukulia hatua viongozi wa kisiasa na kijeshi ambao wanazuia kufanyika mabadiliko nchini Mali.

"Tunalaani kilichotokea Mali katika masaa machache yaliyopita, utekaji nyara wa Rais na Waziri Mkuu, na tunaunga mkono ujumbe uliotumwa na SADC na Umoja wa Afrika," amesema Charles Michel, Rais wa Baraza la Ulaya.

Michel amesema kwa pamoja wanatoa  wito wa kurudishwa kwa serikali ya mpito, na kwamba klichotokea ni kitu kikubwa na wako tayari kuzingatia kuchukua hatua zinazohitajika.

 Credit:DW



Share:

MBUNGE NEEMA LUGANGIRA AITAKA WIZARA YA KILIMO IJIKITE KATIKA PATO LA MKULIMA NA SIO BEI YA MKULIMA

 

Mbunge wa Viti Maalumu kupitia Asasi za Kiraia Tanzania Bara (NGOs) Neema Lugangira akisisitiza jambo akichangia bajeti ya Wizara ya Kilimo Bungeni Jijini Dodoma



Mbunge wa Viti Maalumu kupitia Asasi za Kiraia Tanzania Bara (NGOs) Neema Lugangira akisisitiza jambo akichangia bajeti ya Wizara ya Kilimo Bungeni Jijini Dodoma

NA MWANDISHI WETU, DODOMA

Mbunge wa Viti Maalumu kupitia Asasi za Kiraia Tanzania Bara (NGOs) Neema Lugangira ameitaka Wizara ya Kilimo iache kuimba wimbo wa Bei ya Mkulima badala yake watoke huko waende kwenye Pato la Mkulima ili kuongeza tija kubwa kwenye sekta hiyo.


Aliyasema hayo leo Bungeni Jijini Dodoma wakati akichangia Bajeti ya Wizara ya Kilimo ambapo Mbunge Neema alisema kwa kipindi kirefu Wizarani wamekuwa wakiongelea tu Bei ya Mkulima lakini wakati umefika sasa waongelee Pato la Mkulima kwa sababu wanapoongelea Pato la Mkulima lina faida mbili ya kwanza ni bei na ya pili ni wingi na ubora yaani kimahesabu Pato la Mkulima lina Variables mbili = Price/Bei x (Quantity/Wingi + Quality/Ubora). 

Alisema kwamba Wizara ya Kilimo wamekuwa wakiweka jitihada kwenye Bei ya Mkulima na sasa ameishauri Wizara ikumbuke hii Variable ya ya pili ya Q ambayo ni Quanity/Wingi na Quality/Ubora.

Mbunge Neema aliendelea kwa kusema kwamba kwa sababu Wabunge wengi wameongelea tija yetu ya kwenye kilimo anapenda kutoa mifano miwili: Kwa wenzetu wa Zambia wanauza kilo moja ya mahindi wanauza TZS. 250 mpaka 300 na wakiuza kwa bei hiyo wanarudisha gharama zao yaani wamefikia break-even point lakini kwetu sisi Tanzania ili kufikia kiwango cha break-even lazima tuuze kilo moja ya mahindi TZS.500 .

“Hivyo hivyo hata kwenye Pamba kwa nchi ambazo tunashindana nazo India, Brazili, China , Egypt wao wanazalisha eka moja kilo 1,000 hadi 1,250 na wao wakiingia sokoni wanaweza kuuza kwa bei ya TZS..500 kwa kilo na kwa kiwango hiko wamekuwa wamefikia kiwango cha break-even lakini sisi kwa sababu tija yetu ni ndogo tunazalisha eka hiyo hiyo moja kilo 250 hivyo hatuwezi kuuza kwa bei ya TZS 500 yaani mpaka ifike angalau TZS 1000” Alisema

Mbunge huyo alipendekeza kwamba ifika wakati Wizara ya Kilimo ianze kuongelea Pato la Mkulima na sio Bei ya Mkulima kwani kufanya hivyo wataweza kuongeza tija ambayo itaongeza mchango wa Sekta ya Kilimo kwenye Pato la Taifa kwa sababu wamekuwa wakisema asilimia 65 ya watanzania wapo kwenye Kilimo lakini bado Sekta ya Kilimo inachangia asilimia 27 tu kwenye Pato la Taifa. 

Mbunge Lugangira alisisitiza kwamba kama Wizara itaendelea na Wimbo wa Bei ya Mkulima basi itakuwa inaendelea kufidia upungufu wetu wa tija kupitia Bei ya Mkulima jambo ambalo sio sahihi kwahiyo ni lazima sasa Wizara ya Kilimo ijikite katika Pato la Mkulima.

Hata hivyo pia Mbunge Lugangira aliishauri Wizara ya Kilimo ipitie upya Vituo vya Rasilimali ya Kilimo Ngazi ya Kata “Ward Agriculture Resource Centres” ione kama Vituo vinatumika kadiri ambavyo ilitakiwa na kama kuna  changamoto virudishwe kuwa chini ya Wizara ya Kilimo ili viweze kuchangia katika kukuza tija kubwa ya kilimo kama ilivyokusudiwa.

Kutokana na kwamba Vituo hivyo vilikuwepo kwa miaka mingi na Halmashauri zimekuwa hazitengi Bajeti ya Huduma ya Ugani jambo ambalo ni changamoto kubwa katika uendelezaji wa kada hiyo muhimu kwa maendeleo ya kilimo nchini.

“Kwanza nakushukuru sana Mh Spika kwa kunipa nafasi ya kuchangia kwenye Bajeti ya Wizara ya Kilimo na naomba nianza kwa kusema naunga mkono Hoja. Sera ya Kilimo hapa nchini inasema Mgani mmoja Kijiji kimoja kama tunavyofahamu kuna Vijiji takribani elfu 12000 na tuna Wagani elfu 7000 kwa sasa nchini hivyo tuna upungfu Wagani elfu  5000” Alisema

“Lakini pia napenda kuipongeza Serikali kupitia Wizara ya Kilimo hususani Waziri Profesa Adolf Mkenda na Naibu Waziri wake Hussein Bashe kwa jitihada kubwa walizoweka kuleta Mageuzi kwenye Huduma za Ugani ikiwemo kutenga Bajeti kwa ajili ya kuwanulilia Maafisa Ugani vitendea kazi kama pikipiki, nawapongeza sana lakini bado kuna changamoto ambayo mimi ninaiona na kwamba bado Wizara ya Kilimo inategemea Afisa Ugani huyo awe mtaalamu kwa kila kitu ajue mazao yote, mbolea, wadudu,masuala ya madawa, fangazi, ukungu na nk jambo ambalo sio rahisi” Alisema

Mbunge Neema Lugangira alisema Serikali iliamua kuanzisha Vituo vya Rasilimali ya Kilimo Ngazi ya Kata ili viweze kuwa na tija kubwa kwenye kilimo na kama sikosei vituo hivyo vilianzishwa kwenye Kata 200 hapa nchini na pamoja na kuanzishwa Serikali iliweka wataalamu kwenye vituo hivyo, vitendea kazi kama kompyuta, Jenereta, screen za kufundishia nk,

“Katika hili niwapongeze Wizara ya Kilimo maana nimeskia kupitia Hotuba ya Waziri wa Kilimo Profesa Adolf Mkenda kwamba wanakwenda kufufua Vituo hivyo lakini ningependa kushauri lazima Wizara ihakikishe Vituo hivyo viweze kufanya kazi ambayo imekusudiwa kwa sababu hivi sasa Vituo hivyo vipo chini ya Halmashauri kwenye Halmashauri nyingi vituo hivyo havifanyi kazi iliyokusudiwa ya kuendeleza kilimo kwa mfano Kituo kilichopo Chamwino badala ya kufanya kazi ya kuendeleza kilimo inatumika na TARURA" Alisema.

Alisema pia hawawezi kuendeleza Kilimo wakati hizo Halmashauri ambazo karibia asilimia 70 ya Mapato yake ya Ndani yanatokana na Kilimo lakini Utengaji wa Bajeti ya Huduma ya Ugani hawatengi na kwakuwa suala hili linahusu Ofisi ya Rais TAMISEMI na Waziri yupo Bungeni anaskia  pengine atawaambia wanapanga vipi kuhakikisha hizo Halmashauri zinatenga Bajeti ya Huduma ya Ugani.

“Na mimi naamini lengo zima la kuanzishwa Vituo hivyo ilikuwa ni kuhakikisha wanaimarisha Huduma ya Ugani na wakifanya hivyo wataweza kuongeza tija na muhimu zaidi kuongeza Pato la Mkulima.

Mbunge Lugangira alimaliza kwa kusisitiza: "Kwa muda mrefu tumekuwa tukiongelea Bei la Mkulima na kabla sijaingia hapa Bungeni nilikuwa nafanya kazi kwenye Shirika ambalo lipo chini ya Wizara ya kilimo la SAGCOT (Southern Agricultural Growth Corridor of Tanzania) kama Mkurugenzi wa Idara ya Sera na nimefurahi nimemuona bosi wangu Mr. Geoffrey Kirenga yupo kwenye Ukumbi wa Bunge kwa hiyo naendelea kusisitiza Wizara ya Kilimo iache Wimbo wa Bei ya Mkulima na ijikite katika Pato la Mkulima” Alisema
Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo May 25



Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger