Tuesday, 25 May 2021
Monday, 24 May 2021
Majaliwa: Watafiti, Wabunifu Ongezeni Kasi Ya Tafiti
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka watafiti na wabunifu nchini kuongeza kasi ya kufanya tafiti ili nchi iende sambamba na mabadiliko yanayotokea ulimwenguni kote.
Ametoa wito huo leo Mei 24, 2021 wakati wa ufunguzi wa maadhimisho ya sita ya wiki ya utafiti na ubunifu yakiyofanyika katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Jijini Dar es Salaam.
“Mabadiliko haya ya teknolojia yanatokea kwa kasi kubwa ulimwenguni yanachochewa na mwenendo wa maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Hivyo basi, nasi hatunabudi kujipanga vyema ili kuendana na kasi hiyo”.
Amesema kuwa ni lazima watafiti na wabunifu katika sekta zote wachukue hatua za makusudi katika kubuni na kutumia teknolojia zinazoibuka kwa ajili ya kuleta maendeleo endelevu ya viwanda na jamii yetu.
“Wakati tukifanya hayo yote, ni muhimu pia kujitayarisha kutumia kikamilifu matokeo ya tafiti zetu kama fursa au bidhaa adimu ya biashara”
Aliongeza kuwa baada ya tafiti hizo wahakikishe matokeo ya tafiti yanapelekwa kwa umma ili uweze kufaidika na matokeo hayo kwa kupata suluhisho za changamoto mbalimbali zinazoikabili Jamii badala ya kuyafungia makabati.
Aidha, Waziri Mkuu amevitaka vyuo vikuu vyote nchini kuweka utaratibu wa kufanya utafiti na kisha kuonesha matokeo ya tafiti ili kusaidia kuimarisha uhusiano wa karibu baina ya vyuo na soko la ajira.
Kadhalika Waziri Mkuu ametoa wito kwa wenye viwanda kutoa ufadhili wa tafiti na bunifu zinazohusiana na bidhaa zinazozalishwa katika viwanda vyao.
“Tumieni vizuri wataalamu wa vyuo vyetu kwani wanaweza kuleta majibu ya changamoto mbalimbali katika uzalishaji bidhaa, masoko ya bidhaa, mahitaji ya wateja na mambo mengine mengi”
Pia, Waziri Mkuu amekitaka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kutekeleza mpango wa vitengo vya utafiti kwenye mikoa ikiwemo cha mkoa wa Lindi ambako tayari walikwisha pewa eneo.
Naye Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako amesema kuwa Serikali itaendelea kuimarisha tafiti ili taifa liweze kunufaika na teknolojia ya kisasa na kutoa huduma kwa jamii.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
Ntobo Mik 1....Ni Dawa Ya Asili ya Vidonda Vya Tumbo Iliyofanyiwa Utafiti Kwa Miaka Mingi
Ni Dawa ya vidonda vya tumbo iliyofanyiwa utafiti kwa miaka mingi mwanga wa matumaini kwa wanao teseka na Vidonda vya Tumbo.
Huwezi kuzungumzia magonjwa yanayotesa Jamii ya watu wengi Duniani bila kuzungumzia Vidonda vya Tumbo.
Ugonjwa huu husababishwa na aina ya bakteria anayeitwa kwa jina la HP (Helicobacter Palory) mtu hujikuta anateseka na maumivu makali ya Tumbo bila kujuwa kuwa ni vidonda vya tumbo
DALILI ZAKE:
1. Tumbo kuwaka moto
2. Tumbo kujaa gesi au haja kubwa kuwa ngumu
3. Kutokupata choo vizuri
4. Kiungulia cha mara kwa mara
5. Kichwa kuuma
6. Maumivu makali ya tumbo lajuu wengi huuita chembe ya moyo
7. Kukosa hamu ya kula
8. Kizunguzungu
9. Kichefu chefu
Ugonjwa huu ukishamili sana mgonjwa hujikuta anatapika damu au kujisaidia choo chenye mchanganyiko na damu.
Nini suluhisho;
BABU MADUHU MTAALAMU MWENYE UWEZO MKUBWA WA KUTIBU VIDONDA VYA TUMBO
BABU MADUHU ANAPATIKANA MAGOMENI MOROCCO HOTEL KITUO CHA KANISANI
PIGA SIMU NO. 0755 684 297/ +255 652 102 152 (WHATSAPP)
TARURA yaombwa kurekebieha barabara ndani ya hifadhi kurahisisha utalii
Samirah Yusuph.
Bunda. Katibu tawala wa Wilaya ya Bunda Halfan Mtetela ametoa wito kwa wakala wa barabara mjini na vijijini TARURA kufanya marekebisho ya mara kwa mara barabara za ndani ya hifadhi ili kurahisisha shughuli ya utalii.
Wito huo umeutoa jana wakati wananchi wa wilaya ya Bunda walipotembelea hifadhi ya Taifa ya Serengeti upande wa Kilawira na kusisitiza kuwa kila mtu ahamasike kutembelea vivutio vya utalii ikiwemo mbuga za wanyama na hifadhi za taifa.
“Barabara zikiwa hazijatengenezwa vizuri inakuwa changamoto kupitika ni lazima wakala wa barabara vijijini na mjini (TARURA) kuona umuhimu wa kizitengeneza na ikiwezekana kuongeza bajeti ili kusaidia kwenye matengenezo hayo, zitasaidia kuvutia watalii na kufika eneo husika kwa urahisi na kwa wakati,”amesema Mtekela.
Alisema Watanzania wanapaswa kuwa wazalendo kwa kupenda vivutio vyao na kuvitangaza ili kufanya idadi ya watanzania wanaotembelea hifadhi na mbinga za taifa iongezeke.
"Kila mmoja anapaswa kuwa balozi wa kutangaza vivutio kwenye mtandano kupokea watalii kutoka ndani na nje kwani kufanya hivyo kutapelekea kuongeza pato la mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.
Kwa upande wake mkurugenzi wa kampuni ya NCT twende kutalii Albart Chenza alisema katika kuhakikisha watanzania wengi wanatembelea hifadhina vivutio hivyo,kampuni yake kwa kushirikiana na uongozi wa Serengeti wameanzisha mpango wa kutembelea taasisi na wananchi ili kuhamasisha wananchi hao wanatembelea hifadhi hizo
“Hifadhi ya Serengeti imeanzisha mpango unaoitwa mlango kwa mlango…na sisi kampuni yetu tunaunga mkono na kuhamasisha wananchi na mpaka sasa mwamko umeanza kuonekana.
Nae Gilango Nyarunge mfugaji wa kijiji cha Salangwe Bunda ambaye amepata fursa ya kutembelea hifadhi ya Serengeti alisema amejifunza vitu vingi na kuahidi kuhamasisha wenzake kuwa na desturi ya kutembelea hifadhi hizo.
"Watanzania tupo zaidi ya milioni 60 kwa sasa lakini ukiangalia idadi ya watu wanaoingia kwenye hifadhi zetu kuangalia utalii ni wachache kuliko idadi ya watu waliopo nchini hali hii inaonyesha sisi siyo wazalendo ni vyema tupende utalii wa kwetu wa ndani .
mwisho
Waziri Bashungwa Asisitiza Maafisa Habari kutoa Taarifa kwa Umma
Na Shamimu Nyaki,Mbeya
Waziri wa Habari, Itamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Innocent Bashungwa amewaagiza Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano Serikalini kujituma kwa kasi, ari na weledi ambapo amesema atayezembea hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
Mhe.Bashungwa ameyasema hayo Mei 24, 2021 Jijini Mbeya wakati akifungua Kikao kazi cha Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano wa Serikali ambapo amesema kikao hicho kiwe chachu ya kuboresha utendaji pamoja na kufanya tathmini ya utekelezaji wa majukumu ya maafisa hao kwa mwaka 2021 ili kutekeleza kauli ya Baba wa Taifa Mwl. nyerere inayosema " Kujikosoa ni Kujisahihisha"
"Nimeguswa na Kauli Mbiu ya kikao hiki kwa mwaka huu isemayo "Utoaji Taarifa kwa Umma ni Takwa la Kisheria Viongozi wa Umma na Maafisa Habari Tuwajibike, Hivyo
Wizara ninayoisimamia inaendelea kufanya mageuzi makubwa katika kusimamia utoaji wa huduma za habari kwa umma, na hii ni utekelezaji wa Sheria ya Huduma ya Habari ya Mwaka 2016, na Sheria ya Haki ya Kupata Habari ya Mwaka 2016" amesisitiza Mhe. Bashungwa.
Aidha Mhe.Bashungwa ametumia nafasi hiyo kutoa rai kwa Makatibu Wakuu wa Wizara yake na Ofisi ya Rais TAMISEMI kuhakikisha changamoto zote zinazowakabili maafisa hao ikiwemo kutoshirikishwa kwenye ziara za kutembelea miradi mbalimbali inayotokelezwa na Wizara au Taasisi, baadhi ya Maafisa Habari kuwekwa chini ya Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ( TEHAMA) ambapo majukumu yake hayapewi kipaumbele pamoja na kutokuwa na bajeti, vifaa na bajeti ya Inteneti na Simu zinatatuliwa mara moja
Hata hivyo amewasisitiza Viongozi wa Wizara, Taasisi, Halmashauri za Wilaya, Manispaa Miji na Majiji kuhakisha wanatoa ushirikiano kwa maafisa habari ili watekeleze majukumu yao vizuri.
Kwa Upande wake Naibu Waziri Mhe.Pauline Gekul amesema Wizara yake inagusa watu wengi na ni Wizara inayozungumza, hivyo itaendelea kushirikiana kutatua changamoto za maafisa hao
"Natoa rai kwenu kufanya kazi kwa bidii, tuhabarishe umma mambo yote yanayotekelezwa na Serikali, tufanye kwa wakati na kuzingatia weledi na taaluma ya habari, pamoja na kuwa waadilifu" Mhe.Gekul.
Awali, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt.Hassan Abbasi alitumia kikao hicho kushukuru maafisa hao kwa ushirikiano waliompatia wakati akiwa Mkurugenzi Idara ya Habari - MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali na kuwasihi kuendelea kutekeleza majukumu yao vyema.
"Tuendelee kushirikiana katika Cheo kipya cha Katibu Mkuu katika Wizara hii ambayo ni Wizara muhimu katika kugusa umma kwa nyanja ya Burudani na Huzuni kutokana na Sekta zake"amesema Dkt. Abbasi.
Hata hivyo wakati kikao kinaendela Katibu Mkuu alipokea ujumbe kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan kwa maafisa hao
Akisoma ujumbe kwa Maafisa Habari na Uhusiano kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan, Dkt.Abbasi amenukuu
"Naomba muendelee kuhimizana kuhusu umuhimu wa taarifa kwa Umma, yale yasiyo mazuri na yasiyo ya lazima kuwe na namna bora ya kutoa taarifa na msiache kusema mpaka wananchi waanze kulalamika ndiyo watoe taarifa"
Naye Katibu Mkuu TAMISEMI Prof. Riziki Shemdoe alisisitiza maafisa hao Maafisa Habari kutangaza miradi ya Serikali kwa umma.
Huku Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe.Juma Homera akitoa rai kwa Wakurugenzi kutenga bajeti kwa ajili ya Maafisa hao na kuwapatia vifaa mbalimbali wanavyohitaji katika kutekeleza majukumu yao.
Vilevile Mwenyekiti wa Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) Paschal Shelutete akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Maafisa hao amesema kikao hicho ni chachu ya kuendelea kuboresha utendaji wa maafisa hao.
Waziri Wa Maliasili Atangaza Rasmi Operesheni Ya Wavamizi Wa Hifadhi Wilayani Tunduru
Na Happiness Shayo – TUNDURU
Wizara ya Maliasili na Utalii imetangaza operesheni kabambe ya kuwaondoa wafugaji wote waliovamia na kufanya shughuli zao katika hifadhi ya Taifa ya Nyerere na maeneo mengine yaliyotengwa kwa ajili ya utalii na uhifadhi wa wanyama mkoani Ruvuma.
Kauli hiyo imetolewa jana na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro wakati akiongea na wananchi wa vijiji vya Kalulu na Jakika wilayani Tunduru, wakati wa ziara yake ya kusikiliza kero ya wananchi kuhusiana na wanyamapori wanaovamia mashamba na kufanya uharibifu wa mazao wilayani humo.
Alisema, tatizo la wanyama hususani Tembo wanaokula mazao ya wakulima limechangiwa kwa kiasi kikubwa na wafugaji kuingiza mifugo yao kwenye maeneo yasioruhusiwa kisheria jambo linalosababisha wanyama hao kukimbia.
Kwa mujibu wa Dkt. Ndumbaro Serikali imeshatenga maeneo maalum kwa ajili ya shughuli za ufugaji, lakini kutokana na kiburi cha fedha wafugaji wanawatumia baadhi ya wenyeviti na watendaji wa serikali za vijiji wasiokuwa waaminifu kukaidi kupeleka mifugo kwenye maeneo waliyotengewa.
Dkt Ndumbaro amewaonya wenyeviti na watendaji hao kujiepusha na vitendo vya rushwa kwa kupokea fedha na kuruhusu wafugaji kufanya shughuli zao kwenye maeneo ya utalii kwani tabia hiyo ni kukiuka sheria za utumishi wa umma.
Waziri Ndumbaro, amewataka wananchi kuepuka kuishi na kufanya shughuli zao kwenye hifadhi kwani serikali haitahusika kulipa fidia wala kifuta machozi kwa mtu atakayepoteza maisha, kujeruhiwa na kuharibiwa mazao.
Aidha alisema, ili kukabiliana na wanyama wanaovamia mashamba na kuharibu mazao, Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imeanza kutoa mafunzo kwa vijana kwenye vijiji vinavyozungukwa na hifadhi na mapori ya akiba ili kuwajengea uwezo wa kufukuza wanyama pindi wanapofika kwenye makazi ya watu.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Tunduru, Julius Mtatiro alisema, wilaya hiyo ni ya kilimo lakini changamoto kubwa kuvamiwa na wafugaji na mifugo mingi kutoka katika maeneo mengine ya nchi jambo lililosababisha kutokea kwa migogoro kati ya jamii ya wafugaji na wakulima.
Alisema, licha ya serikali ya wilaya kutenga zaidi ya vitalu 200 vya ufugaji, lakini jambo la kusikitisha baadhi ya viongozi wa ngazi za vijiji wanaruhusu wafugaji kupeleka mifugo kwenye maeneo yasioruhusiwa.
Mtatiro ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama alisema, katika kukabiliana na changamoto hiyo serikali ya wilaya inafanya operesheni za mara kwa mara kuwaondoa wavamizi wote wanaofanya shughuli za kibinadamu kwenye hifadhi na maeneo yote yasiyoruhusiwa.
Baadhi ya wananchi wa vijiji hivyo, wameiomba serikali kupitia upya viwango vya fedha vinavyotolewa kwa waathirika wa matukio ya kushambuliwa na wanyama wakali na wanaoharibu mazao kwani havilingani na hasara inayotokea.
Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Wilaya ya Tunduru, Ajili Kalolo alisema, wananchi wanalazimika kuondoa mazao yao mashambani kabla hayajakomaa ili kuepuka kuliwa na wanyama.
Kalolo alisema, kama serikali itaendelea na msimamo wake wa kuwaona wananchi ndiyo wenye makosa kwa kile kinachodaiwa kuvamia kwenye hifadhi basi kuna hatari wilaya hiyo kukumbwa na janga la njaa.
Msanga Rashid mkazi wa kijiji cha Kalulu, ameiomba Wizara ya Maliasili na Utalii kuwasaidia kukabiliana na wanyama wakali na waharibifu wa mazao, badala ya kuwaona wananchi ndiyo wakosaji kwani kama serikali itaendelea na msimamo huo kuna hatari baadhi ya vijiji kutokuwa na watu kwa kuuawa na wanyama.
WAJASIRIAMALI VIJIJI VINAVYOZUNGUKA MGODI WA BULYANHULU WATUA NA BIDHAA 100 MAONESHO YA WAJASIRIAMALI NA WAWEKEZAJI KAHAMA
HAFLA YA MAKABIDHIANO YA MAGARI YA MRADI WA REGROW JIJINI DODOMA
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Allan Kijazi akizungumza katika halfa ya kukabidhi magari 9 kwa taasisi za TAWIRI, Wakala wa Huduma za Misitu (TFS), Bodi ya Utalii (TTB) ,Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC) ,Bonde la Mto Rufiji (RBWB) ,na Timu ya Uratibu kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii kwa lengo la kuimarisha utendaji kazi wa taasisi hizo katika shughuli za mradi wa REGROW. Makabidhiano hayo yalifanyika jijini Dodoma.
Mratibu wa Mradi , Aenea Saanya akizungumza kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu kwenye hafla ya makabidhiano ya magari ya Mradi wa Regrow iliyofanyika jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Allan Kijazi akikata utepe katika hafla ya makabidhiano ya magari ya mradi wa REGROW huku akishuhudiwa na Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Dkt. Ezekiel Mwakalukwa na mwakilishi wa Tawiri, Dkt. Wilfred Mareale.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Allan Kijazi akimkabidhi funguo za gari mwakilishi wa TAWIRI, Dkt. Wilfred Mareale kwenye hafla ya makabidhiano ya magari ya mradi wa REGROW jijini Dodoma.
Relationship Manager, SME – Eastern Zone, Morogoro (Re-advertised) at NMB Bank
This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content
Job Purpose Responsible for growing both Liabilities (Deposits) and Assets from Small and Medium Enterprises (SMEs) for Business banking; advising the department on business strategy, assisting SME Business Bankers /Relationship Officers/Branch Managers in recruiting business customers to ensure SME business growth. Main Responsibilities Actively selling SME deposits, lending and cross selling of other banks products […]
This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details
Spika Ndugai awaapisha Wabunge wapya Muhambwe na Buhigwe
Spika wa Bunge Job Ndugai, leo Jumatatu Mei 24, 2021 amewaapisha wabunge wawili waliochaguliwa hivi karibuni katika majimbo ya Mkoa wa Kigoma.
Wabunge hao ni Dk Florence Samizi wa jimbo la Muhambwe na Kavejuru Felix wa la Buhigwe, wote wakitokea CCM.
Wabunge hao wameapishwa baada ya ushindi waliopata katika uchaguzi mdogo uliofanyika kwa majimbo hayo kuwa wazi kufuatia kifo cha aliyekuwa mbunge wa Muhambwe, Atashasta Nditiye na Dk Philip Mpango wa Buhigwe aliyeteuliwa kuwa Makamu wa Rais.
Data Clerks at COCODA
This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content
JOB VACANCIES ANNOUNCEMENT Community Concern of Orphans and Development Association (COCODA) is a non-governmental organization established in 2000. COCODA’s establishment as its name suggests, resulted from intensifying concern among community members in Njombe over the surging number of orphans, mainly as a consequence to swelling amount of people infected by HIV and dying from AIDS, […]
This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details
Communication Coordinator at Grumeti
This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content
COMMUNICATION COORDINATOR (1) JOB PURPOSE Grumeti Fund Trust (Grumeti Fund) is a non-profit organization created in Tanzania in 2003. The GFT mission is to contribute to the conservation of the Serengeti Ecosystem in partnership with local communities and other stakeholders. Grumeti Fund Trust located in the concessions of Western Corridor of the Serengeti Ecosystem, collaborates with […]
This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details
Moto Mpya Watinga Na Zawadi Kemkem
Sio wengine tena ni wale wale nguli wa simu za Mkononi Tanzania wanakuja na mazawadi kibao kwa wale watakao nunua simu mpya ya Infinix HOT 10T.
Katika uzinduzi wa Promotion ya nunua na ushinde zawadi iliyotambulishwa na Meneja Mauzo wa Infinix Bi. Winifrida Chumi alipokuwa akizungumza katika kipindi cha Sports Arena kinachoruka kupitia Kituo cha redio ya Wasafi FM alitangaza zawadi zitakazotolewa ni Jiko la Gesi, jiko la Umeme pamoja na Air coolers kama zawadi kubwa.
Unaweza kujiuliza ni nini cha ajabu kwenye hii simu? Akielezea sifa za simu hii mpya Bi. Eddah Charles ambae ni Afisa Elimu na Mafunzo wa kampuni ya Infinix amesema simu hii kwanza kabisa ina kamera bora yenye uwezo wa mp48 inayokuwezesha kupata picha zenye rangi halisia ya eneo husika vile vile ina wigo mpaka wa kioo cha ukubwa wa nchi6.82” ambacho ni HD+ (Kioo ng’aavu), na processor G70 yenye speed ya ajabu na kuifanya simu yako kuwa nyepesi wakati wa utumiaji.
Aisee jiunge na wajanja wenzako mjini kwa kujipatia simu yako ya HOT 10T ukatambe na wanao kitaa. Kwa mengi Zaidi tembelea www.infinixmobility.com
au piga nambari ya simu 0744606222.

























