Monday, 24 May 2021

Moto Mpya Watinga Na Zawadi Kemkem

Sio wengine tena ni wale wale nguli wa simu za Mkononi Tanzania wanakuja na mazawadi kibao kwa wale watakao nunua simu mpya ya Infinix HOT 10T. 

Katika uzinduzi wa Promotion ya nunua na ushinde zawadi iliyotambulishwa na Meneja Mauzo wa Infinix Bi. Winifrida Chumi alipokuwa akizungumza katika kipindi cha Sports Arena kinachoruka kupitia Kituo cha redio ya Wasafi FM alitangaza zawadi zitakazotolewa ni Jiko la Gesi, jiko la Umeme pamoja na Air coolers kama zawadi kubwa.

Pia zawadi ndogondogo ni pamoja na Vikombe, Headphones, Wireless Keybords na zingine kibao. Promotion hii ni kuanzia Tarehe 6/5 mpaka Tarehe 25/5 katika maduka yote ya simu.

Unaweza kujiuliza ni nini cha ajabu kwenye hii simu? Akielezea sifa za simu hii mpya Bi. Eddah Charles ambae ni Afisa Elimu na Mafunzo wa kampuni ya Infinix amesema simu hii kwanza kabisa ina kamera bora yenye uwezo wa mp48 inayokuwezesha kupata picha zenye rangi halisia ya eneo husika vile vile ina wigo mpaka wa kioo cha ukubwa wa nchi6.82” ambacho ni HD+ (Kioo ng’aavu), na processor G70 yenye speed ya ajabu na kuifanya simu yako kuwa nyepesi wakati wa utumiaji.

Sifa nyengine ambayo ni ya ziada Infinix HOT 10 T PEEK PROOF inakifanya kioo cha simu yako kuwa cheusi na kumnyima uwezo wa kuona aliyepo pemebni yako hivyo kutohitaji kuweka glass protector ya Privacy.

Aisee jiunge na wajanja wenzako mjini kwa kujipatia simu yako ya HOT 10T ukatambe na wanao kitaa. Kwa mengi Zaidi tembelea www.infinixmobility.com
au piga nambari ya simu 0744606222.

Share:

Technical Director – OVC at Save the Children

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

Save the Children (SC) is seeking an experienced Technical Director – OVC for an anticipated USAID/PEPFAR-funded project providing support to orphans and vulnerable children (OVC) in Tanzania. The Technical Director will be responsible for the technical oversight of the project and is specifically responsible for project implementation of evidence-based, high quality, multi-sectoral interventions to increase […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

Share:

Case managers (3) – Temporary job at COCODA

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

JOB VACANCIES ANNOUNCEMENT Community Concern of Orphans and Development Association (COCODA) is a non-governmental organization established in 2000. COCODA’s establishment as its name suggests, resulted from intensifying concern among community members in Njombe over the surging number of orphans, mainly as a consequence to swelling amount of people infected by HIV and dying from AIDS, […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

Share:

Data Clerks at COCODA

SERIKALI YATOA MAAGIZO KWA WAMILIKI VIWANDA VYA CHUMA NCHINI

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira), Patrobas Katambi, akitazama baadhi ya malighafi katika kiwanda cha Fujian Hexingwang alipofanya ziara katika viwanda hicho kilichopo Mkuranga na viongozi wa OSHA kwa lengo la kufuatilia utekelezaji wa maagizo yaliyotolewa na serikali hivi karibuni kuhusu uboreshaji wa mazingira ya kazi.

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira), Patrobas Katambi, akipitia nyaraka kuhusu masuala ya Usalama na Afya katika kiwanda cha nondo cha Fujian Hexingwang, alipofanya ziara katika kiwanda hicho mwishoni mwa wiki. Wanaomtazama ni Kaimu Mtedaji Mkuu wa OSHA, Khadija Mwenda na Meneja wa Kanda ya Pwani wa OSHA, George Chali.

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira), Patrobas Katambi (wa kwanza kushoto-kwa waliovalia kofia zenye nembo ya OSHA), Kaimu Mtedaji Mkuu wa OSHA, Khadija Mwenda, Meneja wa Kanda ya Pwani wa OSHA, George Chali na Mkaguzi wa Usalama wa Umeme, James Bandoma, wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa kiwanda cha nondo cha Fujian Hexingwang, wakati viongozi hao walipofanya ziara katika kiwanda hicho mwishoni mwa wiki.

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira), Patrobas Katambi, akizungumza na wafanyakazi wa kiwanda cha nondo cha Fujian Hexingwang, wakati kiongozi huyo alipofanya ziara katika kiwanda hicho mwishoni mwa wiki akiwa ameambatana na viongozi wa OSHA.

Na Mwandishi Wetu

Serikali imewaagiza wamiliki wa viwanda vya chuma nchini kukaa kikao cha pamoja kwa ajili ya kujadili na kukubaliana kuhusu teknolojia sahihi ya kuchambua vyuma chakavu ambayo itakuwa na uwezo wa kutambua vitu vyenye milipuko wakati wa kufanya uchakataji wa vyuma hivyo ili kutengeneza bidhaa mbali mbali za chuma.

Agizo hilo limetolewa na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira), Patrobas Katambi, alipofanya ziara katika viwanda vya Fujian Hexingwang na Lodhia Group of Companies vilivyopo Mkuranga kwa lengo la kufuatilia utekelezaji wa maagizo ya kuboresha mazingira ya kazi yaliyotolewa na Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) hivi karibuni.

“Wote wanaofanya bishara zinazohusiana na kuchakata chuma wakae katika kikao cha pamoja watafute teknolojia itakayo tusuaidia kugundua malighafi zenye mlipuko ili kuepuka ajali zinasababishwa na uchambuzi usiofaa wa malighafi ya viwanda hivyo hali ambavyo inasababisha kutokea ajali nyingi ambazo baadhi yake zimekuwa zikigharimu uhai wa Watanzania wenzetu,” amesema Naibu Waziri Katabi.

Kaimu Mtendaji Mkuu wa OSHA, Khadija Mwenda, ambaye aliambatana na Naibu Waziri katika ziara hiyo amesema lengo la ziara hiyo ni kufuatilia maagizo ambayo yalitolewa na OSHA hivi karibuni wakati Taasisi yake ilipokuwa ikichunguza ajali iliyotokea katika kiwanda cha Fujian Hexingwang ambapo ajali hiyo ilisababisha vifo vya wafanyakazi wawili.

Ameleza kuwa pamoja na wamiliki wa kiwanda hicho kupewa maelekezo juu kuboresha mazingira ya ufanyaji kazi baada ya tukio la ajali kutokea na kugharimu maisha ya wafanyakazi lakini bado kiwanda hicho hakijatekeleza kwa kiwango kikubwa.

“Tumekuja kuangalia utelezaji wa maagizo tuliyoyatoa ili tufungue kiwanda hiki kiendelee na shughuli zake lakini bado hawajatekeleza na sababu ya kutotekeleza tumebaini ni kutokana na wenye kiwanda hiki kuwa na uelewa mdogo kuhusiana na mambo tuliyowaelekeza. Hivyo, japokuwa kazi ya kutengeneza mifumo ya Usalama na Afya mahali pa kazi ni wajibu wao lakini tumeamua kwamba tutaleta watalaam wetu ili waweze kuwaongoza kwa karibu kusudi wakamilishe marekebisho hayo muhimu na kisha tuwaruhusu kuendelea na uzalishaji,” ameeleza Kiongozi huyo Mkuu wa OSHA.

Aidha, amesema Taasisi yake kwasasa inafanya ukaguzi wake kisekta kwa kuzingatia hali ya vihatarishi vya kiusalama na afya (risk-based inspections) ambapo wamekwisha fanya katika sekta kadhaa ikiwemo madini, fedha na hifadhi kwa jamii.

“Kwasasa tunaendelea na ukaguzi katika viwanda vya chuma kote nchini. Baada ya kukamilisha ukaguzi huu na kuandaa repoti tutazishirikisha mamlaki nyingine zikiwemo Wizara ya Viwanda na Biashara pamoja ya Uwekezaji ili wanapoandaa sera, sheria na miongozo mbali mbali ya uwekezaji wahakikishe kwamba miongoni mwa matakwa muhimu kwa wawekezaji nchini ni kuwa na mifumo na teknolojia sahihi zinazozingatia afya na usalama wa wafanyakazi,” alisema Mwenda.

Kaimu Mtendaji Mkuu wa OSHA, Khadija Mwenda, ambaye aliambatana na Naibu Waziri katika ziara hiyo amesema maagizo hayo waliyatoa hivi karibuni wakati Taasisi yake ilipokuwa ikichunguza ajali iliyotokea katika kiwanda cha Fujian Hexingwang ambapo ajali hiyo ilisababisha vifo vya wafanyakazi wawili.

Kwa upande wao wafanyakazi wa kiwanda cha Fujian Hexingwang wameeleza kutofurashwa kwao na jinsi ambavyo mwajiri wao anashindwa kuendesha shughuli zake kwa kuzingatia sheria za nchi.

“Haipendezi kuona mwekezaji kama huyu anakiuka sheria na miongozo mbali mbali anayopewa na mamlaka mbali mbali za serikali jambo ambalo linapelekea hata sisi wafanyakazi kukosa haki zetu za msingi ikiwemo kufanya kazi katika mazingira salama,” alieleza Ramadhani Mdimu.

Ziara hiyo ya Naibu Waziri inafanyika kwa lengo la kufuatilia maboresho yaliyofanyika kufuatia uchunguzi wa ajali zilizotokea katika viwanda viwili vya chuma ambazo zinaonekana zimetokea katika namna inayofanana. Aprili 17 na Mei 04 mwaka huu zilirepotiwa ajali katika kiwanda cha PNP Industries Limited kilichopo Mikocheni ambapo wafanyakazi watatu walijeruhiwa vibaya na nyingine ilitokea katika kiwanda cha Fujian Hexingwang cha Mkuranga ambayo ilipelekea vifo vya wafanyakazi wawili.

Share:

NAIBU WAZIRI ULEGA ATAKA MAJIBU YA UKOSEFU WA MALIGHAFI KATIKA VIWANDA VYA KUCHAKATA SAMAKI

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (kulia) akiuliza jambo baada ya kupatiwa ufafanuzi juu ya uchakataji wa minofu ya samaki kutoka kwa mmoja wa viongozi wa kiwanda cha Victoria Perch Limited kilichopo jijini Mwanza, mara baada ya kutembelea kiwanda hicho kufahamu upatikanaji wa malighafi, uzalishaji na masoko. (Picha na Edward Kondela, Afisa Habari – Wizara ya Mifugo na Uvuvi)
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (kushoto) akiangalia makasha mbalimbali yenye minofu ya samaki yakiwa tayari kwa ajili ya kusafirishwa kwenda nje ya nchi, mara baada ya kutembelea kiwanda cha kuchakata minofu ya samaki cha Tanzania Fish Processor kilichopo jijini Mwanza. (Picha na Edward Kondela, Afisa Habari – Wizara ya Mifugo na Uvuvi)
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (Mb) akizungumza na viongozi wa kiwanda cha kuchakata minofu ya samaki cha Tanzania Fish Processor kilichopo jijini Mwanza pamoja na maafisa kutoka wizarani mara baada ya kutembelea kiwanda hicho ili kufahamu upatikanaji wa malighafi kiwandani hapo. (Picha na Edward Kondela, Afisa Habari – Wizara ya Mifugo na Uvuvi)

Na. Edward Kondela

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (Mb) amewaelekeza viongozi wa viwanda vya kuchakata samaki Mkoani Mwanza kukaa na maafisa kutoka katika wizara hiyo kutafuta suluhu ya ukosefu wa malighafi ya kutosha katika viwanda vyao ili viweze kufanya kazi kwa kadri ambavyo vinatarajiwa.

Naibu Waziri Ulega amesema hayo jana (23.05.2021) wakati akihitimisha ziara yake ya kikazi ya siku mbili mkoani humo kwa kutembelea viwanda vya kuchakata minofu ya samaki vya Tanzania Fish Processor na Victoria Perch Limited baada ya kupata malalamiko kutoka kwa baadhi ya viongozi wa viwanda juu ya ukosefu wa malighafi ya samaki aina ya sangara.

Akiwa katika nyakati tofauti kwenye viwanda hivyo naibu waziri huyo ameambiwa na viongozi wa viwanda kuwa upatikanaji wa samaki umeendelea kuathiri shughuli za viwandani na kuongeza gharama za uzalishaji na kuiomba serikali kuangalia namna ya kuwasaidia katika kutafuta suluhu ya upatikanaji wa malighafi hizo.

Akitoa maelezo ya jumla mara baada ya kuzungumza na viongozi wa viwanda Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega amesema ukosefu wa malighafi unadaiwa kupungua viwandani kutokana na vitendo vya uvuvi haramu, biashara ya mabondo na bei ndogo ya samaki wanaonunuliwa katika viwanda hivyo na kuelekeza viongozi wa viwanda na maafisa kutoka wizarani kukaa pamoja na kubaini kiini hasa cha tatizo hilo ili kutafuta suluhu.

“Sisi tunafurahi tukisikia wananchi wanapata, wakati huo tunataka viwanda vipate malighafi yote mawili tunayataka lazima tuwe na nyongeza ya maarifa ili tupate suluhu ya jambo hili tutoke kwa mafanikio wote wafurahi.” Amesema Mhe. Ulega

Ameongeza kuwa uwepo wa viwanda vya kuchakata samaki unalinufaisha taifa kwa kuwa serikali inapata mrabaha wa mazao yanayoenda nje ya nchi ambapo fedha hizo zinatumika katika shughuli mbalimbali zikiwemo za kijamii.

Kuhusu kudhibiti vitendo vya uvuvi haramu amesema wizara imejipanga vyema na kuwataka watu wote wanaojishughulisha na vitendo hivyo kuacha mara moja na kwamba serikali itaongeza juhudi za kupambana na uvuvi haramu na kutaka ushirikiano kutoka kwa kila mdau.

Amefafanua kuwa wizara imepanga utaratibu wa kutambua hatua mbalimbali za upatikanaji wa nyavu za uvuvi tangu kutengenezwa kwake hadi kusambazwa na kumfikia mvuvi ili kudhibiti usambaaji wa nyavu zisizohitajika kisheria hapa nchini.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega amemaliza ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani Mwanza kwa kuonana na baadhi ya wavuvi katika Wilaya ya Sengerema na kuzungumza nao juu ya changamoto mbalimbali zinazowakabili pamoja na kutembelea viwanda vya kuchakata minofu ya samaki Jijini Mwanza ili kujionea upatikanaji wa malighafi ya samaki aina ya sangara.

Share:

Project Manager at North Mara Gold Mine Limited

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

JOB ADVERT – PROJECT MANAGER (01) POSITION DESCRIPTION: North Mara Gold Mine Limited is seeking to recruit one (01) Project Manager for North Mara team. The successful candidates for this role reports to Engineering Manager and the role holder will be involved in initiation, planning, execution, monitoring/control and closure of capital and maintenance-based projects, to […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

Share:

Logistics Assistant G5 (Shipping and Documentation) at WFP

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

ABOUT WFP The United Nations World Food Programme is the world’s largest humanitarian agency fighting hunger worldwide.  The mission of WFP is to help the world achieve Zero Hunger in our lifetimes.  Every day, WFP works worldwide to ensure that no child goes to bed hungry and that the poorest and most vulnerable, particularly women and children, […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

Share:

Call for Evaluation Consultancy at UNFPA

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

Background The UNFPA Tanzania Country Office (CO) is currently implementing its 8th Country Programme (CP) 2016/17-2021/22 with the Government of the United Republic of Tanzania and other partners. The goal of the CP is to achieve universal access to sexual and reproductive health, realize reproductive rights and reduce maternal mortality, to improve the lives of […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

Share:

Advisor Risk and Crisis Communication at GIZ

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

Advisor Risk and Crisis Communication Location: Arusha, Tanzania Job Title: Advisor Risk and Crisis Communication Overview As a federal enterprise, GIZ supports the German Government in achieving its objectives in the field of international cooperation for sustainable development. The Support to Pandemic Preparedness in the EAC Region Project (PanPrep) assists the East Africa Community Secretariat (EAC) in […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

Share:

Sunday, 23 May 2021

Kibiti Pwani JKT Selection Form six 2021

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

The Kibiti National Services JKT, has released names of form six students who have been selected attend the National Services training for the 2021 academic year [majina ya waliochaguliwa jkt 2021 Kibiti Pwani]. JKT has set up a three-month training camp and they should report to the camps as instructed. Kibiti JKT Form six JKT […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

Share:

Wauzaji Na Wasambaji Nyavu Haramu Kikaangoni

 Na. Edward Kondela
Serikali imepanga kuweka utaratibu wa kutambua hatua mbalimbali za upatikanaji wa nyavu za uvuvi tangu kutengenezwa kwake hadi kusambazwa na kumfikia mvuvi ili kudhibiti usambaaji wa nyavu zisizohitajika kisheria hapa nchini.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega amebainisha hayo jana (22.05.2021) wakati akizungumza na baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Kanyala kilichopo Wilaya ya Sengerema Mkoani Mwanza, akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani humo na kubainisha kuwa serikali inataka suala la kuchoma nyavu lipungue au liishe kabisa.

“Tumejipanga vyema sana wavuvi mmekuwa mkipata sintofahamu kubwa unaenda dukani kununua nyavu ya milimita nane (8) ukija nayo huku ikipimwa inaonekana iko chini ya milimita hizo ambapo ni kinyume na sheria na wewe kuchukuliwa hatua, sasa tutapambana na wauzaji na wasambazaji wa nyavu hizo.” Amesema Mhe. Ulega

Ameongeza kuwa ili kuhakikisha nyavu za uvuvi zinakuwa katika viwango vinavyotambulika, wizara itaweka pia utaratibu wa kuwepo kipimo kimoja ambacho kitatambulika nchi nzima kwa kushirikiana na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) ili kumuokoa mvuvi asiendelee kuumizwa kwa kuarifiwa kuwa nyavu zake ziko kinyume na sheria.

Naibu waziri huyo amewapongeza pia wakazi wa Kijiji cha Kanyala kwa kuonesha uelewa mpana juu ya kutotumia zana haramu kwa kushirikiana na serikali jambo ambalo kwa kiasi kikubwa limepunguza shughuli za uvuvi zisizozingatia sheria za nchi.

Kuhusu kuanzishwa kwa vyama vya ushirika vya wavuvi Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega amesema serikali ya awamu ya sita ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa Rais Samia Suluhu Hassan imepanga kuwawezesha wavuvi kupitia vyama hivyo kwa kupata mikopo ili waweze kununua vyombo vya kisasa zaidi vya shughuli za uvuvi.

“Vikundi vya ushirika vinafanya vizuri sana na wengine wamejitengenezea vyombo vya uvuvi, tuweke utaratibu mzuri tusirudi nyuma nimekuja kutazama namna mnavyosonga mbele nataka kurudisha ari ya kufanya vizuri sana, nataka nirudi tena hapa kukabidhi hundi.” Amefafanua Mhe. Ulega

Katika kuhakikisha vyama vya ushirika vya wavuvi vinanufaika na mikopo kupitia taasisi mbalimbali za kifedha ikiwemo Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Naibu Waziri Ulega amevitaka vyama ambavyo tayari vimepatiwa mikopo kufanya marejesho kwa wakati ili viweze kuwa na sifa ya kukopeshwa tena pamoja na kuwezesha vyama vingine kupata mikopo na kukuza sekta ya uvuvi.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Buchosa Mhe. Eric Shigongo akizungumza katika mkutano huo ameipongeza Wizara ya Mifugo na Uvuvi namna inavyohakikisha inasimamia maslahi ya wavuvi na kuiomba kuhakikisha inadhibiti nyavu za uvuvi zisizotakiwa kisheria kabla hazijafika kwa wavuvi, kwa kukagua nyavu kwa watu au makampuni yaliyopewa vibali vya kuingiza nyavu hizo nchini.

Aidha, amesema serikali haiko tayari kukandamiza raia wake wakiwemo wavuvi na kukemea vitendo vya rushwa vinavyofanywa na baadhi ya watendaji wakati wa ukaguzi wa nyavu za uvuvi kwa wavuvi.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Mhe. Emmanuel Kipole amekemea pia vitendo vya rushwa na kuwataka wavuvi wasikubali kutoa rushwa kwa mtendaji yeyote wa serikali kwani kwa kufanya hivyo wanakuwa wanahalalisha kuendelea kuwepo kwa vitendo hivyo.

Amewataka watendaji wanaohusika na ukamataji wa zana za uvuvi zisizotakiwa kisheria kufuata sheria za nchi kwa kuwa vitendo vya rushwa vinabomoa nchi na kusababisha kutokuwepo kwa mahusiano mazuri baina ya watendaji hao na wavuvi.

Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Kanyala wakizungumza katika mkutano wa Naibu Waziri Ulega, wamelalamikia baadhi ya vyama vya ushirika vya wavuvi kukosa mikopo kutoka taasisi mbalimbali za kifedha licha ya kufuata taratibu ambazo zimekuwa zikianishwa na taasisi hizo, jambo ambalo Mhe. Ulega alifanya mazungumzo kwa njia ya simu na Mkurugenzi Mtendaji wa TADB Bw. Japhet Justine katika mkutano huo juu ya jambo hilo ambapo mkurugenzi huyo aliahidi kulifanyia kazi.

Wakazi hao pia wameiomba serikali kutokomeza kabisa uwepo wa nyavu haramu ili waweze kununua nyavu zinazotakiwa kisheria kwa kuwa wamekuwa wakipata hasara kwa kununua nyavu zisizotakiwa kisheria bila kufahamu na hatimaye kukamatwa kwa nyavu hizo na kuchomwa moto jambo ambalo limekuwa likiwarudisha nyuma kimaendeleo.

Akiwa katika Wilaya ya Sengerema, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega akiambatana na Mbunge wa Jimbo la Buchosa Mhe. Eric Shigongo na mkuu wa wilaya hiyo Mhe. Emmanuel Kipole pamoja na viongozi wengine, amefika katika Kijiji cha Zilagula na kukutana na Chama cha Ushirika wa Wavuvi Zilagula na kujionea namna mkopo wa Shilingi Milioni 100.7 waliopatiwa na TADB wanavyoutumia kwa kutengeneza boti za uvuvi, vichanja vya kuanikia dagaa, kujenga eneo la kuhifadhia samaki pamoja na kujulishwa mikakati mbalimbali ambayo chama hicho kitaendelea kufanya kupitia fedha hizo.

Akiongea na wakazi wa Kijiji cha Zilagula Mhe. Ulega amekitaka Chama cha Ushirika wa Wavuvi Zilagula kuwasaidia vijana na kutaka wataalam kufikishwa katika kijiji hicho ili kutoa elimu ya matumizi bora ya fedha za mikopo ili mkopo huo uweze kuwa na tija zaidi kwao na jamii inayowazunguka.

Amekitaka chama hicho kufanya kazi vizuri zaidi ili siku zijazo waweze kununua boti za kisasa zaidi za uvuvi na kuwataka wakazi wa Kijiji cha Zilagula kuunga mkono uwepo wa Chama cha Ushirika wa Wavuvi Zilagula.

Ameongeza kuwa kupitia chama hicho wavuvi wataweza kuuza samaki kwa bei nzuri zaidi badala ya kulanguliwa na watu wachache ambao wamekuwa wakinunua samaki kwa bei ndogo zaidi na wenyewe kwenda kuuza kwa bei kubwa katika masoko mengine.

Share:

TaSUBa Yaagizwa Kuibua Vipaji vya Vijana Mikoani na Kutoa Mafunzo Kwa njia ya Mitandao

 Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Pauline Gekul ameiagiza Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo kuanzisha utaratibu wa mafunzo kwa kutumia mitandao ili kuwafikia vijana wengi  Mikoani ambayo yatasaidia katika kukuza vipaji vya vijana hao.

Naibu Waziri Gekul ameyasema hayo Mei 22, 2021 Wilayani Bagamoyo alipotembelea Taasisi hiyo  ambapo amesema uhitaji wa mafunzo ya kukuza vipaji ni mkubwa kwa maeneo mbalimbali nchini lakini vijana wengi wanashindwa kufika katika Taasisi hiyo kutokana na changamoto ya ukosefu wa fedha.

“Vijana wanahitaji haya mafunzo ila kuna changamoto ya uhaba wa majengo ya mabweni pamoja na gharama za mafunzo, TaSUBa mkienda Mikoani  na kutumia njia ya mitandao mtakuwa mmewafikia vijana ambao kupitia vipaji vyao watajiajiri na kujipatia vipato "amesema Mhe. Gekul.

Kwa upande wake Mkuu wa Taasisi hiyo, Dkt. Herbert Makoye amesema Taasisi hiyo imeanza kutekeleza suala hilo na tayari muitikio ni mkubwa kwa maeneo waliyofika na wataendelea kutekeleza maagizo hayo.

Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo ni moja ya Taasisi kongwe nchini zinazotoa mafunzo yanayosaidia kunoa vipaji mbalimbali vinavyotokana na Sekta za Sanaa pamoja na Utamaduni  ambazo zinachangia kutoa ajira pamoja na kuchangia pato  la Taifa.

Share:

Waziri Bashungwa Awahimiza Wasanii Kukata Bima ya Afya

Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa amehimiza Wasanii nchini kuhakikisha  wanamiliki Bima za Afya ambazo zitawasaidia wanapokua wagonjwa wakati wowote

Mhe. Bashungwa amesema hayo alipomtembelea  Msanii Mkongwe wa Mziki wa Dansi nchini Kikumbi M. Mpango maarufu King Kikii  Nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam  Mei 22, 2021.

"Wizara itaendelea kufuatilia kwa ukaribu matibabu yako na kwasababu daktari wako tuna mawasiliano ya karibu tutakuwa tunajua hali yako inavyoendelea kila siku" alisisitiza Mhe. Bashungwa.

Kwa upande wake Msanii King Kikii amemshukuru Waziri Bashungwa kwa kumtembelea na kumfariji pia amemuomba Waziri amfikishie Salam zake kwa Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kumpongeza kwa kazi  nzuri ya kuliongoza Taifa.

Mzee King Kikii ametumia nafasi hiyo  kuwaasa wanamziki na wasanii  wengine  kuwa na nidhamu katika kazi ili kuendelea kufanya sanaa kwa muda mrefu.

Share:

ANGALIA HAPA MAJINA YA VIJANA WALIOPANGIWA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA JKT 2021 KAMBI MBALIMBALI

TAARIFA KWA UMMA

WITO WA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA JKT MUJIBU WA SHERIA MWAKA 2021

Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), linawaita vijana waliohitimu elimu ya sekondari kidato cha sita kwa mwaka 2021, kutoka shule zote za Tanzania Bara kuhudhuria mafunzo ya JKT kwa mujibu wa Sheria.

Sanjari na wito huo, JKT limewapangia makambi watakayo kwenda kupatiwa mafunzo na wanatakiwa kuripoti makambini kuanzia tarehe 01 hadi 10 June 2021.

Vijana walioitwa wamepangwa katika kambi za JKT Rwamkoma - Mara, JKT Msange - Tabora, JKT Ruvu - Pwani, JKT Mpwapwa, na Makutupora JKT Dodoma, JKT Mafinga - Iringa, JKT Mlale - Ruvuma, JKT Mgambo na JKT Maramba -Tanga, JKT Makuyuni - Arusha, JKT Bulombora, JKT Kanembwa, na JKT Mtabila - Kigoma, JKT Itaka - Songwe, JKT Luwa na JKT Milundikwa - Rukwa, JKT Nachingwea - Lindi na JKT Kibiti- Pwani na Oljoro JKT- Arusha.

Wahitimu wenye ulemavu wa kuonekana kwa macho (Physical disabilities) waripoti katika kambi ya Ruvu JKT iliyopo Mlandizi Mkoani Pwani ambayo ina miundombinu ya kuhudumia watu wa jamii hiyo.

JKT linawataka vijana hao kuripoti wakiwa na vifaa vifuatavyo.

  1. Bukta ya rangi ya ‘Dark Blue’ yenye mpira kiunoni (lastic), iliyo na mfuko mmoja nyuma, urefu unaoishia magotini, isiyo na zipu.
  2. T-shirt ya rangi ya kijani (Green Vest)
  3. Raba za michezo zenye rangi ya kijani au blue.
  4. Shuka mbili za kulalia zenye rangi ya blue bahari.
  5. Soksi ndefu za rangi nyeusi.
  6. Nguo za kuzuia baridi kwa waliopangiwa mikoa yenye baridi.
  7. Track suit ya rangi ya kijani au blue
  8. Nauli ya kwenda makambini na kurudi nyumbani.

Orodha kamili ya majina ya vijana walioitwa, Makambi ya JKT waliyopangiwa na maeneo yaliyopo inapatikana hapo chini.

 BOFYA JINA LA KIKOSI HAPO CHINI  KUANGALIA MAJINA YA VIJANA WA MUJIBU WA SHERIA 2021

 Tafadhali bonyeza jina la kikosi kutafuta jina lako

 BULOMBORA -KIGOMA  RWAMKOMA - MARA  KANEMBWA-KIGOMA
     
 MSANGE - TABORA  MPWAPWA - DODOMA  RUVU - PWANI
     
 MGAMBO - TANGA  MARAMBA - TANGA  MLALE - RUVUMA
     
 MAFINGA - IRINGA  MTABILA - KIGOMA  MAKUYUNI - ARUSHA
     
 ITAKA - SONGWE  LUWA - RUKWA  KIBITI - PWANI
     
 NACHINGWEA - LINDI  MILUNDIKWA - RUKWA  OLJORO - ARUSHA
     
MAKUTUPORA - DODOMA    

Mkuu wa JKT Brigedia Jenerali Rajabu Mabele, Anawakaribisha vijana wote walioitwa ili waweze kujiunga na vijana wenzao katika kujifunza uzalendo, umoja wa kitaifa, stadi za kazi, stadi za maisha na utayari wa kulijenga na kulitumikia Taifa.

Share:

WAUZAJI NA WASAMBAZAJI NYAVU HARAMU KIKAANGONI

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega akizungumza wakati wa mkutano na baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Kanyala kilichopo Wilaya ya Sengerema Mkoani Mwanza,   na kubainisha kuwa serikali imepanga kuweka utaratibu wa kutambua hatua mbalimbali za upatikanaji wa nyavu za uvuvi tangu kutengenezwa kwake hadi kusambazwa na kumfikia mvuvi ili kudhibiti usambaaji wa nyavu zisizohitajika kisheria hapa nchini. (Picha na Edward Kondela, Afisa Habari – Wizara ya Mifugo na Uvuvi)

Mbunge wa Jimbo la Buchosa Mhe. Eric Shigongo, akizungumza wakati wa mkutano wa Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega na baadhi ya wakazi (hawapo pichani) wa Kijiji cha Kanyala kilichopo Wilaya ya Sengerema Mkoani Mwanza, ambapo Mhe. Shigongo amekemea vitendo vya rushwa vinavyofanywa na baadhi ya watendaji katika kudhibiti uvuvi haramu. (Picha na Edward Kondela, Afisa Habari – Wizara ya Mifugo na Uvuvi)
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (kulia) akiteta jambo na Mbunge wa Jimbo la Buchosa Mhe. Eric Shigongo, wakati wa mkutano na baadhi ya wakazi (hawapo pichani) wa Kijiji cha Kanyala kilichopo Wilaya ya Sengerema Mkoani Mwanza. Naibu Waziri Ulega amefika katika Wilaya hiyo kwenye Halmashauri ya Buchosa kwa mwaliko wa Mbunge wa Jimbo la Buchosa Mhe. Shigongo ili kutatua kero mbalimbali za wavuvi. (Picha na Edward Kondela, Afisa Habari – Wizara ya Mifugo na Uvuvi)
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (katikati), Mbunge wa Jimbo la Buchosa Mhe. Eric Shigongo (kulia) na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Sengerema Mhe. Mark Makoye wakiwa kwenye boti kuelekea Kijiji cha Zilagula, ambapo Mhe. Ulega amefanya ziara ya kikazi ya siku moja wilayani humo ili kutatua kero mbalimbali za wavuvi na kuhamasisha ushirika. (Picha na Edward Kondela, Afisa Habari – Wizara ya Mifugo na Uvuvi)
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega akiangalia boti sita za Chama cha Ushirika wa Wavuvi Zilagula zilizotengenezwa kwa ajili ya uvuvi wa dagaa baada ya chama hicho kupokea mkopo wa Shilingi Milioni 100.7 kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB). Naibu Waziri Ulega ameridhishwa na maendeleo ya matumizi ya fedha za mkopo huo wakati akiwa kwenye ziara kikazi ya siku moja wilayani Sengerema. (Picha na Edward Kondela, Afisa Habari – Wizara ya Mifugo na Uvuvi)
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (wa kwanza) akikagua na kupatiwa maelezo juu ya uwekezaji wa vichanja vya kuanikia dagaa kutoka kwa Mwenyekiti wa Chama cha Ushirika wa Wavuvi Zilagula Bw. Joram Yuda (mwenye koti jeusi) baada ya chama hicho kupatiwa mkopo wa Shilingi Milioni 100.7 kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB). (Picha na Edward Kondela, Afisa Habari – Wizara ya Mifugo na Uvuvi)
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (aliyeshika boti)) akikagua na kupatiwa maelezo juu ya matengenezo ya boti tatu kati ya tano alizozikagua kwa ajili ya uvuvi wa samaki aina ya sangara kutoka kwa Mwenyekiti wa Chama cha Ushirika wa Wavuvi Zilagula Bw. Joram Yuda (mwenye suti nyeusi) baada ya chama hicho kupatiwa mkopo wa Shilingi Milioni 100.7 kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB). (Picha na Edward Kondela, Afisa Habari – Wizara ya Mifugo na Uvuvi)

Na. Edward Kondela

Serikali imepanga kuweka utaratibu wa kutambua hatua mbalimbali za upatikanaji wa nyavu za uvuvi tangu kutengenezwa kwake hadi kusambazwa na kumfikia mvuvi ili kudhibiti usambaaji wa nyavu zisizohitajika kisheria hapa nchini.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega amebainisha hayo jana (22.05.2021) wakati akizungumza na baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Kanyala kilichopo Wilaya ya Sengerema Mkoani Mwanza, akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani humo na kubainisha kuwa serikali inataka suala la kuchoma nyavu lipungue au liishe kabisa.

“Tumejipanga vyema sana wavuvi mmekuwa mkipata sintofahamu kubwa unaenda dukani kununua nyavu ya milimita nane (8) ukija nayo huku ikipimwa inaonekana iko chini ya milimita hizo ambapo ni kinyume na sheria na wewe kuchukuliwa hatua, sasa tutapambana na wauzaji na wasambazaji wa nyavu hizo.” Amesema Mhe. Ulega

Ameongeza kuwa ili kuhakikisha nyavu za uvuvi zinakuwa katika viwango vinavyotambulika, wizara itaweka pia utaratibu wa kuwepo kipimo kimoja ambacho kitatambulika nchi nzima kwa kushirikiana na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) ili kumuokoa mvuvi asiendelee kuumizwa kwa kuarifiwa kuwa nyavu zake ziko kinyume na sheria.

Naibu waziri huyo amewapongeza pia wakazi wa Kijiji cha Kanyala kwa kuonesha uelewa mpana juu ya kutotumia zana haramu kwa kushirikiana na serikali jambo ambalo kwa kiasi kikubwa limepunguza shughuli za uvuvi zisizozingatia sheria za nchi.

Kuhusu kuanzishwa kwa vyama vya ushirika vya wavuvi Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega amesema serikali ya awamu ya sita ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa Rais Samia Suluhu Hassan imepanga kuwawezesha wavuvi kupitia vyama hivyo kwa kupata mikopo ili waweze kununua vyombo vya kisasa zaidi vya shughuli za uvuvi.

“Vikundi vya ushirika vinafanya vizuri sana na wengine wamejitengenezea vyombo vya uvuvi, tuweke utaratibu mzuri tusirudi nyuma nimekuja kutazama namna mnavyosonga mbele nataka kurudisha ari ya kufanya vizuri sana, nataka nirudi tena hapa kukabidhi hundi.” Amefafanua Mhe. Ulega

Katika kuhakikisha vyama vya ushirika vya wavuvi vinanufaika na mikopo kupitia taasisi mbalimbali za kifedha ikiwemo Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Naibu Waziri Ulega amevitaka vyama ambavyo tayari vimepatiwa mikopo kufanya marejesho kwa wakati ili viweze kuwa na sifa ya kukopeshwa tena pamoja na kuwezesha vyama vingine kupata mikopo na kukuza sekta ya uvuvi.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Buchosa Mhe. Eric Shigongo akizungumza katika mkutano huo ameipongeza Wizara ya Mifugo na Uvuvi namna inavyohakikisha inasimamia maslahi ya wavuvi na kuiomba kuhakikisha inadhibiti nyavu za uvuvi zisizotakiwa kisheria kabla hazijafika kwa wavuvi, kwa kukagua nyavu kwa watu au makampuni yaliyopewa vibali vya kuingiza nyavu hizo nchini.

Aidha, amesema serikali haiko tayari kukandamiza raia wake wakiwemo wavuvi na kukemea vitendo vya rushwa vinavyofanywa na baadhi ya watendaji wakati wa ukaguzi wa nyavu za uvuvi kwa wavuvi.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Mhe. Emmanuel Kipole amekemea pia vitendo vya rushwa na kuwataka wavuvi wasikubali kutoa rushwa kwa mtendaji yeyote wa serikali kwani kwa kufanya hivyo wanakuwa wanahalalisha kuendelea kuwepo kwa vitendo hivyo.

Amewataka watendaji wanaohusika na ukamataji wa zana za uvuvi zisizotakiwa kisheria kufuata sheria za nchi kwa kuwa vitendo vya rushwa vinabomoa nchi na kusababisha kutokuwepo kwa mahusiano mazuri baina ya watendaji hao na wavuvi.

Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Kanyala wakizungumza katika mkutano wa Naibu Waziri Ulega, wamelalamikia baadhi ya vyama vya ushirika vya wavuvi kukosa mikopo kutoka taasisi mbalimbali za kifedha licha ya kufuata taratibu ambazo zimekuwa zikianishwa na taasisi hizo, jambo ambalo Mhe. Ulega alifanya mazungumzo kwa njia ya simu na Mkurugenzi Mtendaji wa TADB Bw. Japhet Justine katika mkutano huo juu ya jambo hilo ambapo mkurugenzi huyo aliahidi kulifanyia kazi.

Wakazi hao pia wameiomba serikali kutokomeza kabisa uwepo wa nyavu haramu ili waweze kununua nyavu zinazotakiwa kisheria kwa kuwa wamekuwa wakipata hasara kwa kununua nyavu zisizotakiwa kisheria bila kufahamu na hatimaye kukamatwa kwa nyavu hizo na kuchomwa moto jambo ambalo limekuwa likiwarudisha nyuma kimaendeleo.

Akiwa katika Wilaya ya Sengerema, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega akiambatana na Mbunge wa Jimbo la Buchosa Mhe. Eric Shigongo na mkuu wa wilaya hiyo Mhe. Emmanuel Kipole pamoja na viongozi wengine, amefika katika Kijiji cha Zilagula na kukutana na Chama cha Ushirika wa Wavuvi Zilagula na kujionea namna mkopo wa Shilingi Milioni 100.7 waliopatiwa na TADB wanavyoutumia kwa kutengeneza boti za uvuvi, vichanja vya kuanikia dagaa, kujenga eneo la kuhifadhia samaki pamoja na kujulishwa mikakati mbalimbali ambayo chama hicho kitaendelea kufanya kupitia fedha hizo.

Akiongea na wakazi wa Kijiji cha Zilagula Mhe. Ulega amekitaka Chama cha Ushirika wa Wavuvi Zilagula kuwasaidia vijana na kutaka wataalam kufikishwa katika kijiji hicho ili kutoa elimu ya matumizi bora ya fedha za mikopo ili mkopo huo uweze kuwa na tija zaidi kwao na jamii inayowazunguka.

Amekitaka chama hicho kufanya kazi vizuri zaidi ili siku zijazo waweze kununua boti za kisasa zaidi za uvuvi na kuwataka wakazi wa Kijiji cha Zilagula kuunga mkono uwepo wa Chama cha Ushirika wa Wavuvi Zilagula.

Ameongeza kuwa kupitia chama hicho wavuvi wataweza kuuza samaki kwa bei nzuri zaidi badala ya kulanguliwa na watu wachache ambao wamekuwa wakinunua samaki kwa bei ndogo zaidi na wenyewe kwenda kuuza kwa bei kubwa katika masoko mengine.

Share:

Wizara Zatekeleza Maelekezo ya Waziri Mkuu

Na Shamimu Nyaki, Dar es Salaam
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imetekeleza maelekezo yote aliyoyatoa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa Mei 21,2021 wakati akizindua Kongamano la kuenzi mchango wa Tanzania kwenye ukombozi wa Afrika kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam ya kuitaka Wizara ikae na Wizara ya Utumishi na TAMISEMI kutatua changamoto za kimuundo kwenye Sekta za Utamaduni na Michezo.

Katibu Mkuu wa Habari Dkt. Hassan Abbasi ameongoza kikao hicho kilichoshirikisha Makatibu Wakuu wa Wizara za TAMISEMI na Utumishi, kwenye kikao kazi cha Maafisa Utamaduni na Michezo nchi nzima ambapo amesema maelekezo yote yamefanyiwa kazi na kukamilika kilichobaki  ni kuandaa nyaraka ili fanikisha  utekelezaji wa maelekezo hayo.

"Kikao hiki kimejadili na kutekeleza maagizo ya Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa aliyotoa Mei 21,2021 wakati akifungua Kongamano la Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika ikiwemo kufanya marekebisho ya Muundo wa kada za Maafisa Utamaduni na Michezo, na tayari kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI na Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora tumeyafanyia kazi" amesema Dkt.Abbasi.

 Amesema Muundo kama huo unatengenezwa kwenye Sekta ya Sanaa ili taaluma za Sekta hizo zitumike kwa ufanisi.

Aidha Dkt. Abbasi amesema kuwa Sera ya Michezo haina changamoto yoyote na inaendelea kutekelezwa kwa namna inavyoelekeza ikiwemo kuwa na miundombinu ya michezo, kutambua michezo kama taaluma, kuwa na vituo vya kukuza vipaji na mambo mengine yaliyoanishwa katika Sera hiyo.

Naibu Katibu Mkuu Utumishi, Dkt. Francis Michael amefafanua kuwa muundo wa sasa umeboreshwa ambapo mtaalam mwenye fani nyingine ambazo siyo za michezo lakini ana uzoefu kwenye michezo na amepata mafunzo ya michezo anakuwa na nafasi ya kuwa kwenye kada Afisa Michezo.

Dkt.Michael amesema muundo wa awali ulikuwa unashindwa kuitambua kada ya maafisa michezo hivyo kuwafanya wataalam  kushindwa kufanya majukumu yao kwa ufanisi.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI anaeshughulikia Elimu Gerald Mweli amesema kuwa Kitengo cha Utamaduni, Sanaa na Michezo kitatengewa bajeti kwa ajili ya kutekeleza majukumu ya sekta hizo ambapo amesisitiza maafisa hao kutekeleza majukumu yao kwa ufasaha ili waweze kupimwa utendaji wao kwa mujibu wa sheria za utumishi wa umma

Naye, Afisa Utamaduni wa Tabora Tito Lulandala kwa niaba ya maafisa Utamaduni na Michezo ameishukuru Serikali kwa namna ilivyotatua changamoto za Maafisa hao hatua ambayo itaboresha utendaji kazi wao.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive

Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger