Sunday, 23 May 2021

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI MEI 23,2021












Share:

Saturday, 22 May 2021

Form Six JKT selections 2021- Form Six waliochaguliwa kujiunga na JKT 2021

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

Form Six JKT selections 2021- Form Six waliochaguliwa kujiunga na JKT 2021 How do I view JKT selection after they have been released ?? JKT National Service selection list will be uploaded online after its official release by JKT, to check your Selection status follow the below lead from:- Go to JKT Official website  Find […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

SIMBA SC YAICHAPA KAIZER CHIEFS 3-0... YANG'OLEWA LIGI YA MABINGWA KWA TABU

Nahodha John Raphael Bocco amefunga mabao mawili Simba SC ikiibuka na ushindi wa 3-0 dhidi ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini katika mchezo wa marudiano wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika jioni ya leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Pamoja na ushindi huo, Simba SC imetolewa baada ya kuchapwa 4-0 katika mchezo wa kwanza Jumamosi iliyopita Jijini Johannesburg, Afrika Kusini.

Bocco alifunga mabao yake dakika za 24 akimalizia pasi ya mshambuliaji Mkongo, Chris Kope Mugalu na dakika ya 56 akimalizia krosi ya kiungo wa kimataifa wa Msumbiji, Luis Jose Miquissone.

Bao la tatu la Simba limefungwa na kiungo Mzambia, Clatous Chota Chama baada ya juhudi zake mwenyewe kabla ya kufumua shuti kali.

Simba SC ingeweza kuondoka na ushindi waliouhitaji kama safu yake ya ushambuliaji ingetumia vyema nafasi zote walizopata.

Wekundu wa Msimbazi Simba walihitaji ushindi wa mabao 5-0 ili kujihakikishia nafasi ya kufuzu hatua ya nusu fainali kwa mara ya kwanza lakini imeshindikana.

Mwaka 1997 klabu ya Simba ili pindua matokeo na kusonga mbele kwenye michuano hii ya vilabu barani Afrika dhidi ya Mufurila Wonders ya Zambia ambapo mchezo wa kwanza Simba ilifungwa bao 4-0 lakini mchezo wa pili walipindua matokeo na kushinda 5-0 na kusonga mbele.

 Via >>Binzubeiry blog

Share:

Rais Samia afanya Uteuzi wa Mabalozi 23



Share:

Rais Samia akutana na Mkurugenzi Mkuu wa TRC, wazungumza kuhusu miradi ya ujenzi wa reli ya kisasa (SGR).



Share:

Serikali Yasisitiza Upatikanaji Wa Taarifa Sahihi Za Uvuvi Mdogo


Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi imesisitiza upatikanaji wa taarifa sahihi za uvuvi mdogo nchini kwa kuangaza taarifa za wavuvi wadogo zilizofichika ili ziweze kutumika kwa mipango ya maendeleo endelevu kwa lengo la kukuza Uchumi.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Uvuvi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye hotuba yake ya ufunguzi wa warsha ya wadau wa sekta ya uvuvi ya kupitia matokeo ya utafiti wa mchango wa Uvuvi mdogo iliyosomwa kwa niaba yake na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti, Mafunzo na Ugani (DRTE) Dkt. Erastus Mosha mjini Morogoro (21.5.2021).

Akisoma hotuba hiyo, Mkurugenzi amewakumbusha wadau kuwa Uvuvi ni sayansi, hivyo usimamizi wa rasilimali hiyo ni muhimu na unahitaji taarifa za kutosha za kitafiti ili kufikia malengo ya kuwa na Uvuvi endelevu nchini.

Alizitaja baadhi ya changamoto zinazoikabili sekta ya Uvuvi kwa muda mrefu kuwa ni kukosekana kwa taarifa sahihi za mavuvi, zana haramu, idadi ya wavuvi, vyombo vya Uvuvi na nyinginezo.

Pia alisema ana matumaini makubwa kuwa matokeo ya utafiti huo wa kuangaza taarifa za uvuvi zilizofichika yatasaidia kuboresha mipango ya sekta ya Uvuvi nchini kuendana na kasi ya maendeleo ya viwanda na kuongeza mchango wa sekta kwenye pato la Taifa kutoka asilimia 1.7 hadi asilimia 3.5 ifikapo mwaka 2025.

Aidha katika hotuba yake mgeni rasmi aliwafahamisha wadau kuwa,mwaka 2016 Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi iliingia makubaliano na Shirika la Kilimo na Chakula (FAO) ili kutekeleza mradi wa kuwezesha utekelezaji wa Mwongozo wa Hiari wa Kuhakikisha Uvuvi Mdogo unakuwa Endelevu katika Muktadha wa Uhakika wa Chakula na Kuondoa umasikini.

Aliongeza kuwa matokeo mazuri yanayoendelea kutokea yanatokana na Mradi wa kutekeleza Mwongozo wa Wavuvi Wadogo (SSF Guidelines),ambapo Wizara kwa mara nyingine tena ilisaini makubaliano ya kutekeleza Mradi huo wa kuimarisha mchango wa Uvuvi Mdogo kwa usalama wa Chakula na Maisha Endelevu.

Kwa upande wake kiongozi wa timu ya utafiti Dkt. Paul Onyango kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam anasema utafiti huo uliofadhiliwa na FAO ulianza Mwaka 2018, na umefanyika kwenye takribani nchi 40 Duniani.

Akigusia matokeo ya utafiti huo, Dkt. Onyango anasema kuwa kuna taarifa nyingi zilizofichika ambazo zinasababisha thamani ya mchango wa uvuvi mdogo kiuchumi kuonekana ndogo sana tofauti na uhalisia wenyewe.

Dkt. Onyango anabainisha mapendekezo ya kukabiliana na changamoto hiyo kuwa ni vyema Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) kuwa na bajeti maalum ya ukusanyaji takwimu za wavuvi wadogo, kuongeza wakusanya takwimu wenye weledi wa kazi hiyo na pia kutoa elimu kwa wavuvi kuhusu umuhimu wa kutoa taarifa sahihi kwa Serikali.

Mvuvi mdogo Bw. Peter Sumuni kutoka ziwa Nyasa akizungumzia sababu ya wao wavuvi kutokutoa takwimu sahihi kwa maafisa Uvuvi wa maeneo yao, anasema kuwa hawana elimu ya kutosha ya umuhimu wa takwimu hizo pia ushirikiano wao na maafisa Uvuvi hauridhishi.

Aidha Bi.Sijali Hemedi kutoka Kilwa ambaye ni mkusanya takwimu ameelezea kuwa changamoto ni uchache wa wakusanyaji wa takwimu pamoja na uwezeshwaji wa rasilimali Fedha kwa ajili ya kazi hiyo.

Ili kufanikisha lengo la kuwa na Uvuvi Endelevu kwa ajili ya kukuza uchumi, Bw. Yusuph Semuguruka kutoka ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anasisitiza ushirikiano kati ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi na TAMISEMI ikiwa ni pamoja na kufuata taratibu za kupeana taarifa katika utekelezaji wa shighuli mbalimbali za sekta ya Uvuvi nchini.


Share:

RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI WA MABALOZI 23...YUMO MLIMBWENDE HOYCE


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa mabalozi 23 akiwemo mlimbwende wa Tanzania mwaka 1999, Hoyce Temu.

Share:

WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA YAWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA BAJETI KWA MWAKA 2021/2022 IMEJIKITA KUFUFUA VIWANDA

 <,

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Prof.Kitila Mkumbo,akizungumza bungeni leo Mei 22,2021 wakati akiwasilisha hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha kwa Mwaka 2021/2022.


Na.Alex Sonna, Dodoma.

Wizara ya Viwanda na Biashara imewasilisha bungeni makadirio ya matumizi kwa Wizara hiyo kwa mwaka 2021-2022 na kueleza kuwa katika makadirio hayo yamelenga katika kupanua wigo wa upatikanaji wa viwanda hasa vya sukuari ili kupunguza uhaba wa sukari ambapo hutokea mara kwa mara.

Akizungumza wakati wa kuwasilisha bajeti hiyo Bungeni leo Mei 22, 2021 Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Prof. Kitila Mkumbo amesema wamejipanga kukabiliana na upungufu wa sukari kwa kuanzisha viwanda vipya na kupanua uwezo wa viwanda vilivyopo kwa sasa.

“Serikali inaendelea kuchukua hatua mbalimbali katika kuongeza uzalishaji wa sukari kwa kupanua na kuongeza uwezo wa viwanda vikubwa vilivyopo, ikiwemo Kiwanda cha Sukari cha Kilombero,pamoja na kuanzisha viwanda vikubwa vipya,

“Sambamba na hatua hizi, katika jitihada za kuongeza uzalishaji wa sukari ili kukidhi mahitaji ya bidhaa hii nchini, Serikali imeelekeza Taasisi ya TEMDO kufanya usanifu na kuanza kutengeneza mitambo midogo kwa lengo la kuwawezesha wajasiriamali wadogo waanze kuchakata miwa ili kupata sukari (Sugar Min –Processing Plant)” amesema Mkumbo.

Amesema kuwa hatua hii itaweza kuongeza uzalishaji wa sukari na kuhakikisha kuwa wakulima wadogo (out growers) wanaweze kuchakata miwa yao bila kuwa tegemezi katika viwanda vikubwa.

Pia amesema watakamilisha taratibu za kuwapata wawekezaji wapya waviwanda vilivyobinafisishwa na baadaye kurudishwa serikalini, kukamilisha kanzidata ya viwanda na biashara nchini, kuimarisha mfumo wa usajili wa makampuni na leseni za biashara kupitia Wakala wa Usajili na Leseni za Biashara (BRELA).

Vipaumbele vingine ni kuimarisha Mfuko wa Taifa wa Kuendeleza wajasiriamali Wadogo(National Entrepreneurship Development Fund-NEDF) kwa kupanua wigo wa mtaji wa mfuko huo, kuratibu na kusimamia uanzishwaji wa maeneo maalum ya kibiashara (trading hubs).

Ameongeza kuwa “Vipaumbe vingine ni kuimarisha na kukuza matumizi ya utafiti na maendeleo, teknolojia na ubunifukatika sekta ya viwanda na biashara, kuendelea kusimamia viwango vya ubora na kubuni viwango vipya kwa ajili ya bidhaa zinazozalishwa na kuingizwa Tanzania kupitia TBS na Wakala wa Vipimo (WMA)” amesema.

Vipaumbele vingine ni kuhamasisha, kuendeleza na kulinda viwanda vya kuzalisha chuma na bidhaa za chuma, kuendeleza na kuhamasisha ujenzi wa viwanda vya ngozi, nguo na mavazi, kuhamasisha, kuendeleza na kulinda viwanda vya kuzalisha chuma na bidhaa za chuma.

Kuweka msukumo na mazingira mazuri kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda vya kuunganisha vifaa vya kielekroniki na magari, kuhamasisha viwanda vinavyozalisha vifaa vya ujenzi.

Pia amebainisha kuwa Serikali imejipanga katika kuhamasisha ujenzi wa viwanda vya kutengeneza betri na umeme wa magari kwa kutumia rasilimali asili za nchi kama vile madini ya Lithium, Vanadium na Titanium, ambayo pia yanapatikana hapa nchi.

Vile vile tutajikita kuweka mazingira wezeshi kisera na kisheria ya kufanya biashara, kujiunga au kuimarisha ushiriki wa Tanzania katika jumuiya za kiuchumi na kimasoko za kikanda kwa ajili ya kupanua fursa za kibiashara kwa bidhaa za Tanzania ambazo zitazalishwa hapa nchini.

Waziri Mkumbo ameongeza kuwa “Pia tutajikita katika kuimarisha upatikanaji wa mitaji kwa wajasiriamali na wafanya biashara wadogo ili wapanue mitaji yao ili kuendesha biashara zao, tutaweka mazingira bora kisera, kisheria na kiutendaji kwa ajili ya kuchochea na kulinda ukuaji wa sekta binafsi kama injini na msingi wa ujenzi wa uchumi wa viwanda na shindani kuweza kushindana na mataifa mengine” amesema.

Ameongeza kuwa “Lengo kuu la ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 ni kuleta mapinduzi ya uchumi kwa maendeleo ya watu, moja ya nyenzo ya kuleta mapinduzi ya uchumi iliyoanishwa katika ilani hiyo ni kujenga Tanzania ya uchumi wa viwanda na kukuza biashara” amesema.

Wizara ya Viwanda na Biashara imeomba kuidhinishiwa jumla ya shilingi Shilingi bilioni, 105,670,459,000, kati ya fedha hizo, Shilingi bilioni, 52,582,573,000, ni za Matumizi ya kawaida na Shilingi bilioni 53,087,886,000, ni za Matumizi ya Maendeleo.

Share:

ACHARANGWA MAPANGA NA KUIBIWA PESA BAADA YA KUUZA NG'OMBE, WANANCHI WACHOMA MOTO NYUMBA ZA WATUHUMIWA

 

Na Dinna Maningo,Tarime 

Mwita Samson maarufu kwa jina la Mswahili mkazi wa kitongoji cha Kihero kijiji cha Kemakorere kata ya Nyarero wilaya ya Tarime mkoa wa Mara amejeruhiwa kwa kukatwa katwa kwa mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake baada ya kuvamiwa nyumbani kwake na vijana watatu na kisha kuchukua fedha zake na kuondoka nazo.

 

Mwenyekiti wa kijiji cha Kemakorere Marwa Chacha Nyabikone amethibitisha kutokea kwa tukio hilo lililotokea muda wa saa nne usiku wa kuamkia leo na kwamba watu wawili waliohusika na tukio hilo walitambuliwa kwa sura na majina na wote walikimbia.

Nyabikone alisema kuwa polisi walifika eneo la tukio nakumchukua Samson na kumpandisha kwenye gari la polisi kumuwahisha hospitali ya wilaya ili kupata huduma zaidi na anaendelea na matibabu.

"Huku kijijini hatuna zahanati,majeruhi alikuwa bado ana ufahamu aliwatambua vijana wawili ambao majina yao tunayahifadhi kwa uchunguzi zaidi ila mmoja ndiyo hakumtambua kwa sura,walimjeruhi kwa kumkata kwa mapanga kiunoni,tumboni,mkononi,kifuani na begani.

Aliongeza "Ilibidi apatiwe huduma ya kwanza kwenye duka moja la dawa wakamshona na kuwekewa bandeji wakati anaendelea kushonwa polisi walifika wakasema ili kumuokoa akapatiwe matibabu hospitali wakamchukua na kuondoka nae na ndugu zake kwa matibabu zaidi,nawashukuru polisi kwa kufika tunaomba wahusika wakamatwe na wawajibishwe kwenye vyombo vya sheria ili iwe fundisho.

"Wananchi walikusanyika pamoja na kufatilia nyayo za miguu hadi nyumbani kwa watuhumiwa ambao wengine walitambuliwa na Samsoni aliyejeruhiwa na wakabomoa nyumba na kuteketeza kwa moto, mimi mtu mmoja sikuweza kuwazuia na nikaogopa hata kwenda kwenye tukio ningefanyiwa kitu kibaya maana walijawa na hasira nilichokifanya nimetoa taarifa polisi",ameongeza.

Mmoja kati ya wananchi wa kijiji hicho ambaye hakutaka jina lake litwaje alisema kitendo cha kuchoma mali siyo cha haki kwani watoto na mke hawana makosa na kitendo hicho kitawakwamisha wanafunzi kutokwenda shule baada ya nguo zao za shule kuteketea kwa moto. 

Mwenyekiti wa kitongoji cha Kihero Paul Emanuel alisema kuwa alipata taarifa muda wa saa nne usiku ya kuvamiwa mwananchi wake nakwamba chanzo cha kuvamiwa ni baada ya yeye kwenda kuuza ng'ombe wake kwenye soko la ng'ombe jana ijumaa, Mei, 21,2021na ilipofika usiku akavamiwa,bado hakijafahamika kiasi halisi cha fedha zilizoibiwa na wanaendelea na ufuatiliaji.

Kutokana na tukio hilo wanakijiji wanaokadiliwa kuwa zaidi ya 200 majira ya saa kumi na moja leo jumamos wakiwa wanapiga yowe waliandamana hadi kwenye nyumba za watuhumiwa wanaodai hukusika na tukio hilo na kisha kubomoa nyumba zao na kuziteketeza kwa moto pamoja na mali zote zilizokuwa ndani ya nyumba hizo.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Polisi Tarime/Rorya William Mkonda amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo tayari mtuhumiwa mmoja anashikiliwa na polisi na wengine wanaendelea kusakwa. 

Mkonda alisema kuwa tayari ametuma askari kwenda eneo la tukio huku akiwataka wananchi kutojichukulia sheria mkononi nakwamba waliohusika kufanya uhalibifu wa mali watakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Share:

Waziri Mkuu Akabidhi Magari 184 Kwa Halmashauri Nchini


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amekabidhi jumla ya magari 184 kwa maafisa elimu wa Halmashauri ikiwa ni mkakati wa Serikali ya awamu ya sita ya kuendelea kuboresha sekta ya elimu nchini.

Hafla hiyo imefanyika jana (Mei 21, 2021) katika viwanja vya Shule ya Sekondari Kibasila, Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika tukio hilo, Waziri Mkuu amezitaka Halmashauri zilizopokea magari zizingatie taratibu za serikali katika matumizi na matengenezo ya magari hayo.

“Magari haya mmekabidhiwa,  maafisa elimu na wakurugenzi wa Halmashauri, tukute gari limepaki kisa limekosa ‘Service’ utakuwa umekosa kazi, lazima tuambizane ukweli, magari haya lazima yafanye kazi kwa zaidi ya miaka mitano hadi sita”

Amesema kuwa magari hayo ni kwa ajili ya kuimarisha shughuli za ufuatiliaji na tathmini kwa Maafisa Elimu, na yametolewa na Serikali ili yasaidie kuharakisha shughuli za utekelezaji wa majukumu katika sekta ya elimu.

Aidha, Waziri Mkuu amewataka Wakuu wa Mikoa na Makatibu tawala wa mikoa kuchukua hatua ikiwa magari hayo yatatumika tofauti na malengo yaliyotarajiwa “hakikisheni magari haya yanakwenda kutekeleza shughuli za elimu kwenye halmashauri zenu na si vinginevyo”

Kadhalika Waziri Mkuu amewaagiza Maafisa elimu na wakurugenzi wa Halmashauri kuhakikisha kila kwenye shule ya Sekondari wanakamilisha ujenzi wa maabara  ili kila shule iweze kupatiwa vifaa vya maabara.

Wakati huohuo, Waziri Mkuu amewataka viongozi waliopo katika Halmashauri nchini kushughulikia kwa nguvu zote tatizo la utoro  lengo ni kuhakikisha kila mtoto anayeanza shule anamaliza.

“Mtoto wa kitanzania kwenda shule sio hiari ni lazima, na tutawachukulia hatua kali wote wanaozuia watoto wao kwenda shule”

Waziri Mkuu pia amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan itaendelea kushirikiana na Washirika wa Maendeleo pamoja na wadau mbalimbali katika kuboresha sekta ya elimu kupitia miradi mbalimbali inayotekelezwa.

Naye, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI Ummy Mwalimu amesema Magari hayo yamenunuliwa na Serikali kupitia Programu ya Lipa Kulingana na Matokeo katika Sekta ya Elimu (EP4R) kwa gharama ya shilingi bilioni 16.4.

Amesema kuwa hii ni awamu ya pili ya ununuzi wa magari baada ya awamu ya kwanza ambayo magari 26 yalinunuliwa kwa ajili ya usimamizi wa elimu katika ngazi ya Mikoa.

 (Mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,


Share:

Kampuni Ya SD Biosensor Ya Korea Yakabidhi Vifaa Vya Maabara Vya Uchuguzi Wa Codiv 19 Kwa Wizara Ya Afya Zanzibar.


Na Miza Kona Maelezo Zanzibar
Makamu wa Kwanza wa Rais Mhe.Othman Masoud Othman ameitaka jamii kufuata miongozo ya afya na kuongeza hamasa ya mapambano ili kujikinga ugonjwa wa Corona nchini.

Makamu wa Kwanza ameyasema huko katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Mjini Zanzibar katika hafla Makabiadhiano ya Vifaa vya haraka vya kupimia Virusi vya Corona, amesema  ni jukumu la kila mtu kuongeza kasi ya mapambano dhidi ya ugonjwa huo .

Amesema Serikali  ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania inachukua jitihada kubwa ya kupambana na ugonjwa Corona nchini, vifaa hivyo vitasaidia kuongeza kasi ya kiwango cha  upimaji wa virusi vya ugonjwa huo katika jamii.

Amefahamisha ugonjwa wa Corona umeathiri kwa kiasi kikubwa duniani hivyo ni vyema kushirikiana wafadhili na wadau mbalimbali katika kujenga miundombinu mizuri ya afya ili kuepukana na maambukizi.

Makamu wa Kwanza amewasisita wafanyakazi wa wizara ya afya kuitumia vyema msaada huo kwa kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Akizungumzia kuhusu hali ya maambukizi nchini Makamu wa kwanza amesema kuwa ugonjwa upo lakini hali sio mbaya hivyo amewasisitiza wananchi kuwa watulivu na kutosikiliza taarifa potofu zinazotolewa katika mitandao ya kijamii ili kuepuka taharuki.

Nae Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto mhe. NassorAhme Mazrui amesema ugonjwa Corona ni tishio duniani  ni vyema jamii kufuata maelekezo yanayotolewa na wataalamu wa afya ili kujikinga na maambukizi

Amefahamisha kuwa vifaa hivyo vya kupimia virusi vya Corona ni vyenye ubora wa hali ya juu ambavyo hutoa majibu ya papo kwa papo vitasaidia kugundua kwa haraka wale wenye kupata maambukizi ya ugonjwa huo.

 Mapema Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Supplier CEO Sunjay  C. Patadia amesema kampuni yake ina uwezo wa kutengeneza dawa na vitendakazi vyevye ubora kimataifa na vifa vipo tayari kwa ajili ya kutoa huduma kwa jamii bila madhara.  

Vifaa hivyo vya haraka vya  kupimia Virusi vya Corona vyenye thamani ya Tsh. Miliono 250 vimetolewa na Kampuni ya SD BIOSENSOR na SUPLIER CEO kutoka Korea.


Share:

Jafo Ateua Wajumbe Kamati Ya Ushauri Kuhusu Elimu Ndani Ya Muungano


1.Mnamo tarehe 17 Mei 2021 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Selemani Saidi Jafo (Mb.) aliteua Wajumbe saba (7) kutoka Tanzania Bara na Zanzibar kwa lengo la kupata ushauri wa kitaalamu kuhusu uboreshaji wa elimu katika Muungano ili sekta zinazohusika na masuala ya elimu za Tanzania Bara na Zanzibar ziweze kushauriwa ipasavyo. 
 
Hata hivyo kutoka na umuhimu wa Kamati tajwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Selemani Saidi Jafo (Mb.) ameongeza wajumbe watatu ili kuongeza ushiriki na upana wa kupata maoni ya pande zote mbili. Kamati hii inaundwa na wajumbe kumi (10), wajumbe watano (5) kutoka Tanzania Bara na wajumbe watano (5) kutoka Zanzibar.

2. Wajumbe walioteuliwa leo ni:-

i. Dkt. Zakia Mohammed Abubakar, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Zanzibar (SUZA)

ii. Prof. Hamed Rashid Hikmany, Mwenyekiti wa Chuo Kikuu cha SUMAIT, Zanzibar na

iii. Prof. Sylvia Temu, Mhadhiri Mwandamizi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

3.    Wajumbe walioteuliwa awali ni:-
 i. Prof. Alexander Boniface Makulilo, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Taaluma, Utafiti na Huduma kwa Umma) -         Mwenyekiti

 ii.Mhe. Najma Murtaza Giga (Mb.), Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Viti Maalumu) Zanzibar – Makamu Mwenyekiti
iii.Bw. Abdulmarik Mollel, Mkurugenzi Mtendaji wa Global Education Link – Katibu
iv.Bw. Khalid Bakari Hamrani, Mkurugenzi wa Uratibu wa Shughuli za Serikali, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi – Mjumbe
v.Dkt. Charles Msonde, Katibu Mtendaji wa NECTA – Mjumbe
vi. Bw. Gerald Mweli, Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – TAMISEMI – Mjumbe
vii.Bw. Said Hamad Shehe, Mkufunzi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Zanzibar (IPA) – Mjumbe

4.Uteuzi huo umefanyika ikiwa ni hatua ya kushughulikia maoni yaliyotolewa na wadau mbalimbali kuhusu tofauti ya ufaulu wa wanafunzi wa Shule za Sekondari za Tanzania Bara na Zanzibar kwa matokeo mbalimbali ya Kidato cha Nne na Sita. Aidha, Wabunge mbalimbali wamekua wakiwasilisha hoja hiyo wakati wa mjadala wa bajeti ya mwaka 2021/22 wa Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira).

5.    Kamati iliyoteuliwa itafanya kazi kwa siku thelathini na tano (35) na kuwasilisha taarifa kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) ili kwa kushirikiana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi waweze kukaa na Mawaziri wanaohusika na masuala ya elimu kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na kuwashauri namna bora ya kuboresha elimu pande zote mbili za Muungano.

Lulu Mussa
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini




Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo May 22



Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI MEI 22,2021










 


Share:

Friday, 21 May 2021

Infinix Hot 10T Yenye Mp48 Kuzinduliwa Mubashara Na Jopo La Wasanii Tanzania.


Kwa mara ya kwanza series ya HOT kutoka kampuni ya simu Infinix kubeba sifa ya toleo la Infinix NOTE na Infinix S. Tulishazoea kuona toleo la HOT likitamba na nguvu ya battery Safari hii inasemekana kukawa na tofauti kubwa kwenye simu iyo inayodhaniwa kuwa ni Infinix HOT 10T.

Si kama vile tulivyozoea inasemekana Infinix HOT 10T kuja na camera kali yenye MP48 na Mediatek Helio G70 processor na pasipo kusahau ujazo wa battery unaosadikika kuwa mAh 5000 au zaidi.

Vijana wengi hasa wanafunzi wameonyesha matarajio mengi na kuamini kupitia HOT 10T basi wataepuka kero ya simu kupata moto wakati wa uchezaji games lakini pia watahifadhi kazi za kujisomea kwa wingi pasipo simu kugoma goma (stuck).
 

Inasemekana simu hii kuzinduliwa kesho majira ya saa 1:00 ambapo tukio zima litakuwa mubashara kupitia @infinixmobiletz. Uzinduzi huu utashareheshwa na japo la wasanii kutoka kwenye Sanaa ya music ambao ni Billnass anaekimbiza na wimbo wa ‘TATIZO’na Frida amani anaekimbiza na wimbo wa Madame President pamoja na wengine wengi.


Tembelea https://www.infinixmobility.com/ kujua mengi kuhusu bidhaa za Infinix.






Share:

Mhandishi Masauni: Serikali Ilitoa Msamaha Kwa Wadaiwa Wa Kodi


Na, Saidina Msangi na Josephine Majura, WFM, Dodoma
Serikali imesema kuwa katika Mwaka wa Fedha 2018/19 ilitoa msamaha kwa wadaiwa wa Kodi (Tax Amnesty) uliohusisha riba na adhabu zinazoambatana na madeni yote yaliyolimbikizwa kwa miaka ya nyuma ili kuongeza makusanyo.

Hayo yameelezwa bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Hamad Yussuf Masauni (Mb), alipokuwa akijibu swali la Mheshimiwa Henry Maganga Nicodemus, Mbunge wa Mbogwe aliyetaka kujua mpango wa Serikali wa kufuta madeni ya muda mrefu kwa wafanyabiashara wa ndani yatokanayo na ukosefu wa elimu juu ya matumizi sahihi ya mashine za EFD wanayodaiwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania.

Mhe. Masauni alisema kuwa msamaha huo ulilenga kusamehe malimbikizo ya nyuma ya riba na adhabu (Interest and Penalties) kwa kiwango cha asilimia 100 kwa wafanyabiashara wote hapa nchini ambao walikuwa na malimbikizo ya madeni hayo ya kodi.

“Msamaha huo ulitolewa kwa kipindi cha miezi sita (6) kilichoanzia tarehe 1 Julai 2018 mpaka tarehe 31 Desemba 2018, kutokana na kusuasua kwa utekelezaji wake, Serikali iliongeza muda wa msamaha huo kwa miezi sita ili wafanyabiashara waliokuwa na madeni hayo wakamilishe malipo husika”alieleza Mhe. Masauni.

Aidha Mhe. Masauni alisema kuwa hatua hiyo ya marekebisho ya Sheria ya Usimamizi wa Kodi SURA 438 ilitarajiwa kuongeza mapato ya Serikali na kukusanya malimbikizo ya madeni ya nyuma ya kodi (Principal Tax) pamoja na kuinua kiwango cha ulipaji kodi kwa hiyari kwa zaidi ya asilimia 10.

Mhe. Masauni aliongeza kuwa licha ya nia nzuri ya Serikali ya kufuta riba na adhabu ili kuwawezesha walipakodi wenye madeni sugu ya kodi kuyalipa kwa awamu ili kurahisisha mwendelezo wa biashara zao wengi wao hawakulipa kodi hizo hata baada ya kuingia mikataba na TRA na hata baada ya Serikali kuongeza muda wa ziada wa kufanya malipo ya kodi husika yaliyotokana na msamaha huo.

Mwisho.


Share:

Waziri Wa Kilimo Afungua Warsha Ya Kitaifa Juu Ya “kutumia Uwekezaji Mkubwa Katika Kilimo Kuleta Maendeleo Shirikishi Tanzania”


Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma
Tanzania inatambua umuhimu wa wakulima wote nchini – yaani wakulima wadogo, wa saizi ya kati na wakubwa - katika mageuzi ya kilimo na kuendeleza mbinu za kisasa na kilimo cha kibiashara chenye tija zaidi na faida kubwa  kwao.

Mkakati wa Sekta ya Kilimo (ASDS I na ASDS II) na Programu ya kuendeleza Kilimo (ASDP I na ASDP II) imelenga kukuza kilimo kwa ushirikiano baina ya Serikali na Sekta binafsi ili kuleta matumizi endelevu ya ardhi na maji, kuendeleza kilimo cha umwagiliaji, huduma za utafiti na ughani, upatikanaji wa mbegu bora na pembejeo, masoko na uchakataji wa mazao ili kuongeza thamani za mauzo ya nje (value addition).

Waziri wa Kilimo Mhe Prof Adolf Mkenda ameyasema hayo Jijini Dodoma tarehe 21 Mei 2021 wakati akifungua warsha ya kitaifa juu ya “kutumia uwekezaji mkubwa katika kilimo kuleta maendeleo shirikishi tanzania” iliyoandaliwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

“Kulingana na sera zetu za kilimo wawekezaji wakubwa wanategemewa sio tu kuzingatia haya katika kilimo chao wenyewe bali pia kusaidia wakulima wadogo – outgrowers na wakulima wengine - kwa kuwakopesha mbegu bora na pembejeo, kutoa elimu, ushauri na huduma za ughani kwa ujumla na kuingia mikataba mizuri ya kununua mazao yao” Amekaririwa Mhe Mkenda

Amesema kuwa Wakulima wakubwa wanategemewa pia kuchangia katika kuongeza thamani ya mazao na uboreshaji wa mnyororo wa thamani, na hivyo kuongeza bei za bidhaa za kilimo tunazouza nje ya nchi.

Amesema kuwa kunapokuwa na wawekezaji wakubwa na wa saizi ya kati ambao wengi wao huchukua maeneo makubwa ya ardhi, mojawapo ya majukumu ya serikali ni kulinda haki za raia na kuhakikisha ardhi yao na maji haviporwi, na pia wanalipwa fidia stahiki na bei nzuri kwa mazao yao.

Waziri Mkenda amesema kuwa Zaidi ya asilimia sabini (70%) ya watanzania wanaishi vijijini ambako wanajishughulisha na kilimo, kilimo huchangia 26%  hivi ya pato la taifa na asili mia thelathini (30%) ya mauzo ya nje (exports). “Lakini kwa miaka mingi tumejitahidi kuinua ubora wa kilimo kwa mafanikio japo si makubwa sana, kutokana na ujuzi mdogo wa wakulima wetu na matumizi hafifu ya sayansi na teknolojia ya kilimo, na hivyo tumeendelea kuwa na tija ndogo sana (low agricultural productivity) na upotevu wa mavuno” Amesema

Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam/Taaluma Prof Bonaventure Rutinwa amesema kuwa Warsha hiyo ni kilele cha Utafiti wa mwaka mmoja uliofanywa na taasisi ya taaluma za maendeleo ya Chuo Kikuu cha dar es salaam kwa kushirikiana na Taasisi ya  Bill&Melinda Gates ikiwa na lengo la namna ya kutumia fursa za uwekezaji mkubwa katika kuchochea maendeleo katika sekta ya kilimo.

Naye, Mkurugenzi wa Taasisi ya Taaluma ya Maendeleo Dkt Ronald Ndesanjo amesema kuwa radi huo wa utafiti ni sehemu ya majukumu ya taasisi hiyo ambapo ulikuwa na malengo makubwa mawili ikiwa ni pamoja na kufahamu kiwango cha ujumuishi katika ngazi ya miradi ya Uwekezaji wa kilimo chini ya Programu ya kuendeleza sekta ya kilimo awamu ya pili (ASDP II).

Pia amesema lengo la pili ilikuwa ni kubuni namna bora ya kubadilisha mabadiliko jumuishi ya kilimo katika ngazi za uwekezaji pamoja na ngazi ya sera.

MWISHO


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger