Tuesday, 18 May 2021

Wash Technical Assistant-Sanitation at Norwegian Refugee Council

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

Job Description All NRC employees are expected to work in accordance with the organization’s core values: dedication, innovation, inclusivity and accountability. These attitudes and believes shall guide our actions and relationships. Job Description Adhere to NRC policies, tools, handbooks and guidelines Assist with the implementation of the support function portfolio according to plan of action […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

HSEQ Officer – Network at Total

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

Job Description Closely follow-up the ICC program, to ensure compliance to ICC requirements, this includes conducting HSE prequalification for all contractors prior to being included in the list of approved contractors for works and arranging for ICC audit. Conducting site supervision of high risk works, this includes inspection and conformance review of the contractor. Organize […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

Education Program Coordinator 3 (School and Community Inclusive Education Coordinator) at RTI International

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

Position Summary RTI International is the prime implementor of the USAID Jifunze Uelewe activity focused on sustainably improving literacy and numeracy outcomes of “all learners” from pre-primary through Standard 4 in five regions of Tanzania. For the purpose of this program, “all learners” includes, but is not limited to, marginalized and vulnerable girls and boys, learners with disabilities, minority and linguistic minority groups, […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

Live: Rais Samia Anafungua Kiwanda cha Ushonaji cha Polisi

 Live: Rais Samia Anafungua Kiwanda cha Ushonaji cha Polisi



Share:

Mambo 19 Yaliyopendekezwa na Kamati ya Corona


Kamati ya kitaalamu iliyoundwa kufanya tathmini ya hali ya ugonjwa wa corona nchini, imetoa mapendekezo 19 ikiwamo matumizi huru ya chanjo ya ugonjwa huo, ili kutoa fursa ya kinga kwa makundi maalumu kama wazee, wenye magonjwa sugu na wahudumu wa afya.


Kamati hiyo pia imebaini kuwa chanjo hizo zina ufanisi na usalama unaokubalika kisayansi na kwamba kabla ya kutolewa kwa makundi hayo kwanza zifanyiwe uchunguzi.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Prof. Said Aboud, akikabidhi ripoti ya kamati hiyo jana kwa Rais Samia Suluhu Hassan, Ikulu, jijini Dar es Salaam, alisema chanjo zilizoorodheshwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) ziruhusiwe kwa makundi maalumu.

Profesa Aboud alisema: “Pamoja na mapendekezo haya, Kamati Huru ya Kitaifa ya Ushauri wa Chanjo (NITAG) na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), ziendelee kushirikishwa katika kutoa ushauri na kudhibiti chanjo hizo.”

Aliongeza: “Watu walio na hatari ya kupata maambukizi ya virusi vya ugonjwa wa corona wapewe fursa ya kupatiwa chanjo hiyo.”

Rais Samia alitangaza kuunda kamati hiyo Aprili 6, mwaka huu ikiwa ni wiki chache baada ya kuapishwa, huku msisitizo mkubwa ukiwa katika kupambana na ugonjwa huo kwa njia za kisayansi.

Prof. Aboud alisema kamati hiyo ilifanyia kazi hadidu za rejea 12, zilizohusu maeneo mbalimbali ya tathmini ya mwenendo wa ugonjwa pamoja na afua za udhibiti ikiwamo chanjo hapa nchini, kikanda na kimataifa.

“Tangu kuingia kwa ugonjwa wa corona nchini Machi mwaka jana, Tanzania imekumbwa na mawimbi mawili makubwa. Na hivi sasa kutokana na mwenendo wa ugonjwa katika mataifa mengine duniani kuna tishio la kutokea kwa wimbi la tatu hapa nchini,” alisema Prof. Aboud.

Alibainisha kwamba baada ya uchambuzi uliofanywa na kamati, mapendekezo kwa serikali ni kuihuisha mipango ya dharura katika ngazi zote, kwa ajili ya kukabiliana na majanga ikiwamo ugonjwa wa corona.

Prof. Aboud alibainisha kwamba, kamati imependekeza serikali itoe taarifa juu ya uwapo wa ugonjwa huo, ichukue hatua madhubuti kuimarisha hatua zote za afua za kinga ili kuepusha wimbi la tatu la ugonjwa huo.

Alisema pendekezo lingine ni wataalamu wa afya watimize wajibu wao kitaalamu, kwa kuzingatia weledi, miiko na maadili katika kuelimisha, kukinga na kutibu ugonjwa huo nchini.

Lingine ni Tanzania ishiriki ipasavyo katika maamuzi na itekeleze maazimio ya kikanda na kimataifa, iliyoridhia katika Jumuiya za Afrika Mashariki (EAC), Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), Umoja wa Afrika (AU) pamoja na Shirika la Afya Duniani (WHO).

kuhusu matumizi ya chanjo, Prof. Aboud alisema kamati inashauri kwamba serikali kutumia vyombo vyake na kuendelea kuchukua hatua kuelekea kuruhusu matumizi huru ya chanjo.

“Kipaumbele cha utoaji wa chanjo dhidi ya corona nchini kwa kuanzia kiwe katika makundi muhimu, wahudumu katika vituo vya kutolea huduma za afya na watumishi walio katika mstari wa mbele wa utoaji wa huduma, mathalani watumishi sekta ya utalii, hoteli, mipakani, viongozi wa dini na mahujaji.

“Wazee na watu wazima kuanzia umri wa miaka zaidi ya 50, wenye maradhi sugu, kisukari, shinikizo la damu, maradhi ya mfumo wa upumuaji, magonjwa ya figo,” alisema Prof. Aboud.

Pia Prof. Aboud alisema kamati pia inapendekeza chanjo hiyo ipewe kipaumbele kwa watumishi wa vyombo vya ulinzi na usalama, wasafiri wanaokwenda nje ya nchi.

Alisema hivi sasa ufanyike uhamasishaji na maandalizi ya upokeaji, utunzaji, usafirishaji na utoaji wa chanjo nchini na wananchi kuwa huru kuamua kuchanja ama la.

“Serikali iratibu upatikanaji wa chanjo kwa watumishi wa taasisi za kimataifa walioko nchini, ijiunge na ‘COVAX Facility’ kwa kuwasilisha andiko la kupatiwa chanjo, kwa kutumia fursa inayotolewa na GAVI.”

“Serikali itumie fursa zilizopo wakati huu wa corona kuanza mchakato wa uanzishaji wa viwanda vya kutengeneza chanjo, iimarishe huduma za uchunguzi kwa kuijengea uwezo Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii na maabara nyingine ili kupanua wigo wa upimaji wa ugonjwa,” alisema Prof. Aboud.

Prof. Aboud alisema kamati inapendekeza serikali kujenga uwezo wa ndani wa utambuzi wa virusi anuai vinavyosababisha ugonjwa wa corona na magonjwa mengine ya kuambukiza.

Alisema serikali pia itoe takwimu sahihi za ugonjwa wa corona kwa umma na WHO, ili wananchi wapate taarifa sahihi kutoka mamlaka za serikali na kuheshimu makubaliano na kanuni ambazo nchi iliridhia.

Mwenyekiti huyo alisema kamati inapendekeza kuwa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kukamilisha mwongozo mpya wa matibabu ya ugonjwa huo.

“Serikali iendelee kuhakikisha kuwa matumizi ya tiba asili na tiba mbadala katika mfumo rasmi wa tiba za kisasa yanazingatia misingi ya kisayansi.

“Na serikali iendelee kutoa fursa na kuwawezesha wanasayansi kufanya utafiti kwa kufuata miiko, maadili na taratibu zilizowekwa ili kuimarisha kinga, tiba, uchunguzi wa ugonjwa wa corona na athari zake katika jamii nchini,” alisema Prof. Aboud.

Pia alisema kamati inapendekeza serikali kuendelea kuzingatia mazingira ya Kitanzania katika udhibiti wa corona katika kuamua kuweka au kutokuweka shuruti ya kujifungia na kuwa na ubunifu, ili kuruhusu ukuaji wa uchumi na kuimarisha sekta zinazochangia katika uchumi.


Share:

Serikali Mbioni Kutunga Sheria Ya Kulinda Taarifa Binafsi


Na Prisca Ulomi, WMTH
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt Faustine Ndugulile amesema kuwa Wizara yake iko mbioni kupeleka Bungeni muswada utakaowezesha kutungwa kwa Sheria ya Kulinda Taarifa Binafsi iili kulinda faragha na taarifa za mwananchi

Dkt. Ndugulile ameyasema hayo kwenye ukumbi wa Bunge, Dodoma wakati akijibu mijadala mbalimbali iliyotolewa na Wabunge kwenye semina iliyotolewa kwao kuhusu huduma za mawasiliano na intaneti ili waweze kufahamu namna Wizara inavyotekeleza majukumu yake kwa kushirikiana na taasisi zilizo chini yake

Ameongeza kuwa Wizara inaandaa sheria hiyo ili kulinda faragha na taarifa binafsi za wananchi katika hatua ya ukusanyaji wa taarifa, usafirishaji, matumizi na utunzaji wa taarifa hizo kwa kuwa taasisi mbalimbali zinatumia taarifa husika hivyo amewataka Wabunge kuwa tayari pindi pendekezo la muswada litakapowasilishwa Bungeni ili sheria hiyo iweze kutungwa kwa maslahi mapana ya taifa
 
“Hivi sasa ujambazi umehama kutoka silaha za mkononi na kuhamia mtandaoni, Serikali itaendelea kuelimisha wananchi, kuboresha mifumo na teknolojia ili nchi iwe mbele zaidi katika kudhibiti uhalifu mtandaoni,” amesisitiza Dkt. Ndugulile

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Seleman Kakoso ameishauri Serikali iongezee fedha za kuuwezesha Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) kutoa ruzuku ya kutosha kwa kampuni za simu ili mawasiliano yafike kwa wananchi wote ikiwemo kuongeza usikivu wa redio kwenye maeneo ya mipakani

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Akson aliipongeza Wizara kwa kuleta semina hiyo kwa Wabunge na anatamani katika kipindi kifupi Wabunge wasizungumzie changamoto ya mawasiliano katika maeneo yao kwa kuwa mawasiliano ni huduma ya msingi kama ilivyo maji, barabara

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dkt. Jabir Kuwe amesema kuwa nchi inaelekea kutumia huduma ya 5G na majaribio yatafanyika ili kuhakikisha kasi ya teknolojia inayotakiwa inapatikana ili kuongeza huduma ya mawasiliano ya data nchini


Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari




Share:

Waziri Jafo Ateua Kamati Ya Ushauri Wa Elimu Katika Muungano


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Selemani Saidi Jafo ameteua wajumbe saba wa Kamati itakayofanya kazi ya kutoa ushauri wa kitaalamu kuhusu uboreshaji wa elimu katika Muungano.

Akizungumza na waandishi wa habari visiwani Zanzibar Jafo alisema uteuzi huo umefanyika ikiwa ni hatua ya kushughulikia maoni yaliyotolewa na wadau mbalimbali kuhusu tofauti ya ufaulu wa wanafunzi wa Shule za Sekondari za Tanzania Bara na Zanzibar kwa matokeo mbalimbali ya Kidato cha Nne na Sita.

Pamoja na maoni hayo alisema pia wabunge mbalimbali wamekuwa wakiwasilisha hoja hiyo wakati wa mjadala wa bajeti ya mwaka 2021/22 wa Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira).

Jafo ameipa kamati hiyo siku 35 kukamilisha kazi ya kushughulikia maoni hayo na kuwasilisha taarifa kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) ili kwa kushirikiana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi waweze kukaa na mawaziri wanaohusika na masuala ya elimu kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na kuwashauri namna bora ya kuboresha elimu pande zote mbili za Muungano.

“Kamati niliyoiteuwa itafanya kazi kwa kipindi kisichozidi siku 35 nami kwa haraka nikutane na wenzangu wanaohusika na sekta ya elimu kwa lengo la kuboresha hata yake maandalizi ya vijana wa kidato cha nne na sita ili tuweze kuwapa ushauri kutoka timu ya wataalamu wetu nini inasema katika kuboresha hili,” alisema.

Aidha Waziri jafo aliwataja wajumbe walioteuliwa kuwa ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Taaluma, Utafiti na Huduma

kwa Umma), Prof. Alexander Boniface Makulilo ambaye atakuwa Mwenyekiti     na Makamu wake ni Mbunge wa Viti Maalumu kutoka Zanzibar Mhe. Najma Murtaza Giga ambaye atakuwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo.

Wajumbe watakaounda kamati ni mdau wa elimu sekta binafsi Abdulmarik Mollel, Mkurugenzi wa Uratibu wa Shughuli za Serikali, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi, Khalid Bakari Hamrani, Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA), Dkt. Charles Msonde, Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Gerald Mweli na Mkufunzi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Zanzibar (IPA), Said Hamad Shehe.


Share:

MTANGAZAJI MAARUFU WA TV AFARIKI DUNIA BAADA YA KUJIFUNGUA

Mtangazaji maarufu wa televisheni ya NBS nchini Uganda Sheilah Nakabuye alifariki dunia saa chache baada ya kujifungua mtoto wa kike.

Sekta ya utangazaji nchini Uganda inaomboleza kufuatia kifo cha mmoja wa waandishi wa Habari Sheila Nakabuye kilichotokea Jumatatu, Mei 17, 2021. 

Kifo cha Sheila ambaye alikuwa na umri wa miaka 32, kimejiri siku moja baada ya kujifungua mtoto wa kike, aliripotiwa kupoteza fahamu pindi alipofanyiwa upasuaji. 

Kulingana na ripoti ya daktari katika kliniki ya Cedus, marehemu alipatikana na matatizo ya uvimbe kwenye mishipa ya ubongo. 

Mamake alisema bintiye alipoteza fahamu na alipokimbizwa katika hospitali ya rufaa ya Mbarara, alikata roho saa chache baada kuhudumiwa na madaktari.

 " Kama hali hiyo ingeshughulikiwa kwa wakati ufaao ama kwa dharura, nadhani binti yangu hangepoteza maisha yake, ripoti ya daktari inasema aliangamizwa na uvimbe kwenye mishipa ya ubongo," Mamaake Sheila alisema.

 Mtangazaji mwenzake Ambrose Muhumuza alisema kabla ya kulemewa, Sheila alijaribu kula vitafunio lakini alitapika na alionekeana mdhaifu sana. 

Kwa mujibu wa taarifa za Daily Monitor, babaake marehemu Mzee Matovu alizirai na kukimbizwa hospitalini baada ya kupokea habari za kifo cha bintiye.

 Viongozi wa tabaka mbali mbali, marafiki na watangazaji wenzake wameomboleza kifo chake kupitia mitandao ya kijamii. 

Sheilah tayari amezikwa kulingana na desturi ya dini ya kiislamu eneo la Kabasanda wilaya ya Butambala. 

Share:

TBS YAWATAKA WATUMIAJI WA VIPIMO VYA AFYA KUVIHAKIKI UBORA

Afisa vipimo Mwandamizi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Bw.Ramadhan Mfaume(Kushoto) akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam kuelekea Siku ya Vipimo Duniani yenye kauli mbiu "VIPIMO KATIKA SEKTA YA AFYA". Mkuu wa Maabara ya Vipimo (TBS), Bw.Joseph Mahila (Kulia) akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam kuelekea Siku ya Vipimo Duniani yenye kauli mbiu "VIPIMO KATIKA SEKTA YA AFYA".

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

******************************

NA EMMANUEL MBATILO

Kuelekea Siku ya Vipimo Duniani Mei 20,Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limewataka watumiaji wa Vipimo katika sekta ya afya nchini kuhakikisha vipimo hivyo vimepitishwa na Shirika hilo kabla havijatumika.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam Afisa Vipimo Mwandamizi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Bw.Ramadhan Mkumba amesema wamekuwa wakikutana na Changamoto kubwa ya watumiaji wa Vipimo kutokuwa na uwelewa wa kufanya uhakiki wa vifaa vyao ili kuboresha huduma wanazozitoa kwenye sekta za afya.

"Vipimo vinavyotumika katika sekta ya afya ni muhimu vikahakikiwa na kujulikana ubora wao kwa kufanya hivi itakuwa inalinda afya ya wagonjwa kwasababu daktari anaweza kufanya maamuzi kupitia vipimo vinavyotoka maabara vikiwa vipimo sio sahihi vinaweza kupelekea kumpatia madhara mgonjwa". Amesema Bw.Mfaume.

Aidha Bw.Mfaume amesema kuwa dhumuni la kauli mbiu ya mwaka huu ni kuleta uelewa katika jamii jinsi gani vipimo kwenye sekta ya afya vina umuhimu kama tunavyotambua vipimo katika sekta ya afya vinatumika kugundua, kutambua na kutibu magonjwa.

Kwa upande wake Mkuu wa Maabara ya vipimo (TBS), Bw.Joseph Mahila amesema katika maadhimisho ya Siku ya Vipimo kwa mwaka huu watajikita zaidi katika sekta ya afya hasa kutokana na kauli mbiu ya mwaka huu "VIPIMO KATIKA SEKTA YA AFYA".

Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE MEI 18,2021

























Share:

Monday, 17 May 2021

BOYFRIEND WANGU ANATAKA KUMUOA MTOTO WA DADA YANGU...HIVI NDIVYO N NIMESIMAMISHA MAHUSIANO YAO

 Utanishangaa na kujiuliza maswali mengi sana kichwani mwako ila hata mimi naandika ujumbe huu moyo wangu ukiwa umejaa dhiki na machozi makubwa kuona mtoto wa dada yangu namkosesha mtu ambaye alikuwa anaona ndo chaguo la moyo wake.

 Mimi naitwa Rahima mkazi wa Kigamboni Dar es salaam ,umri wa miaka 28. Nikiwa na miaka 17 nasoma kidato cha kwanza niliingia katika mahusiano na Jamary. Jamary alikuwa wanafunzi mwenzangu hapo shuleni hivyo tulikuwa tunaonana mara kwa mara kwa hiyo mahusiano yetu yalikuwa mazuri sana japo yalikuwa ni mausiano ya siri. 

Baada ya semister ya kwanza wazazi wangu waliniamisha kutoka shule ya serikari kwenda shule ya binafsi. Mimi kuhamishwa shule hakuharibu mahusiano yetu japo tulikuwa tunakutana kipindi cha likizo kwa sababu wote tulikuwa tunatoka mtaa mmoja, na baada ya miaka minne wote tumaliza masomo ya secondary na kuwa mtaani. 

Tukiwa mtaani tunasubiri matokeo yetu tulipata nafasi ya kutosha kukaa wote. Ukweli sijawai na sijui kama itatokea tena raha na mapenzi niliyoyapata kutoka kwa Jamary muda huo.
Ni mapenzi ambayo hayana mfano na siwezi kulinganisha na mahusiano yoyote yale maana ilikuwa raha kwa raha.

Kulingana na mapenzi tuliyokuwa nayo tulikubaliana kuwa baada ya masomo tutaoana. Miezi kadhaa kupita tulipata matokeo yetu na wote tulikuwa na sifa za kujiunga masomo ya high school.

 Mimi nilichaguliwa kujiunga na Tabora-Girls na Jamary alichaguliwa kujiunga Morogoro high school. Kabla hatujawasili shuleni tulihakikisha kila moja aliweza washawishi wazazi wake ili tuweze kuwa na siku moja ya kasafiri na ikawa hivyo,tulitafuta hotel Morogoro na kukaa wote kwa kipindi cha siku saba.

Turitumia huo muda kuwekeana ahadi mbalimbali miongoni mwa ahadi zetu ni kuwa baada ya masomo tutaoana. Masomo kwa sisi wote yalikuwa mazuri na mahusiano yetu hayakuwa na doa hata moja na hatimaye tukamaliza masomo ya high school tena tukarudi mtaani japo tulikuwa tunatembeleana na kukutana tukiwa bado tunasoma.

Tuliporudi nyumbani mchezo ukawa ule ule tena mtamu zaidi.Baadhi ya marafiki zetu waliweza fahamu juu ya mahusiano yetu. Bado Mungu akatuwekea mkono wake tukafaulu kujinga masomo ya Chuo Kikuu.

Mimi nilichaguliwa kwenda chuo cha Makumira-Arusha na yeye alichaguliwa kwenda Udom- Dodoma. Mambo yalibadilika haswa tupofika mwaka wa tatu,Jamary alianza kutonijali hata kunipigia simu na baada ya kuhitimu nikapata habari kuwa January anataka kumuoa mtoto wa dada yangu ambaye anasomea Udom.

Mwanzo nilipopata habari sikuamini ila Jamary mwenyewe akanitamkia kwa mdomo wake. Maelekezo yake alisema kuwa mimi nimekuwa sana hivyo hatuwezi kuwa mme na mke.

Na baada ya miezi sita nilipata taarifa ya mwezi na tarehe ambayo Jamary anafunga ndoa.Nilijiuliza mbona kanitumia kwa muda mrefu leo hii hanitaki. Je nitawezaje kusimama siku ya Harusi Jamary anamchukua mtoto wa dada na mimi kuwa Mamakwe wake.

Katika ongea ongea na marafiki zangu ndipo rafiki yangu Faima akaniambia kuwa kuna Dr mashuhuri yupo Kenya anaweza simamisha hiyo ndoa usiwepo. 

Faima alinipatia namba ya simu ambayo ni +254 769404965 nikawasiliana na Dr. Kiwanga kisha nikamwambia kuwa sina uwezo wa kufika Kenya ila nahitaji usaidizi wa haraka maana nilikuwa najiuliza aibu nitaiweka wapi na je mtoto wa dada yangu na dada yangu siku wakifahamu kuwa nilishawahi kupendana na Jamary picha gani itatokea.

Dr. Kiwanga aliniambia kuwa atanisaidia na separation spells ndani ya masaa 48. Hata masaa 24 hayakupita nilipata habari kuwa Jamary amesema hawezi kuoa mwanamke wa kabila moja hivyo atamuoa mtoto wa dada yangu.

Miaka 2 kupita Jamary alioa mwanamke kutoka Tanga na mimi kwa sasa nina mme na watoto 2. Pia nilihakisha mtoto wa dada yangu anapata mwanaume naye yupo na familia yake.

Asante Kiwangadoctors kunisaidia kuficha aibu ambayo ingenikuta endapo wangeoana. Tembelea website yao www.kiwangadoctors.com kwa kupata taarifa zinazowahusu Kiwanga doctors,maana wanatibu magonjwa sugu kama Pressure, Sukari na Nguvu za kiume pia Kiwanga doctors wanasafisha nyota,kupata ujauzito,kupata mme au mke kwa waliokosa mda mrefu, mtu kuacha kutumia pombe.Unaweza kuwapata kwa namba +254 769404965 au barua pepe hii kiwangadoctors@gmail.com.


Share:

MAJIMAMA YAOA WANAFUNZI BUKOBA

Baadhi ya wanawake katika Kata ya Kashai Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera, wamelalamikiwa kuwaoa wanafunzi wa kiume wa Shule za Sekondari Ihungo na Kahororo zote za Manispaa ya Bukoba Mkoani humo.


Katika mkutano wa hadhara ulioitishwa na diwani wa kata hiyo Ramadhan Kambuga amesema kuwa suala hilo limekuwa kubwa na kuliomba jeshi la polisi kuanza msako wa kuwasaka wanafunzi hao na wake zao.

Amesema kuwa ni aibu mama mtu mzima kumuoa mtoto wa mwanamke mwenzake kwa kumlaghai na maneno yasiyo ya kawaida.

Akizungumza katika mkutano huo, mwakilishi wa mkuu wa shule ya Ihungo Mwl. Fraxon Msawile na wa Kahororo wamesema kuwa hali ya vijana ni mbaya na kuwaomba wananchi kuachana nao.

Wamesema kuwa vijana wengine hutoroka shule na kukimbilia kwa wanawake hao na wakati mwingine huvuta bangi..

Share:

SERIKALI YASEMA IPO TAYARI KUKUTANA NA MANABII WANAODAI KUFUFUA WAFU



Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi imesema kuwa ipo tayari kukutana na manabii wanaodai kuweza kufufua wafu ili iweze kuwaelimisha na kuwaelekeza kuwa mwenye uwezo wa kuchukua na kurejesha ni Mungu pekee.

Kauli hiyo imetolewa hii leo Mei 17, 2021, Bungeni Dodoma, na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Hamza Chilo, wakati akijibu swali la Mbunge wa Mtambwe kupitia Chama cha ACT-Wazalendo Khalifa Mohamed Issa, aliyehoji umuhimu wa serikali kukutana na wale manabii wanaodai kuweza kufufua wafu ili waweze kuwafufua wapendwa wao.
Share:

RAIS SAMIA APOKEA RIPOTI MAALUMU YA TATHMINI YA COVID - 19.... "CHANJO YA CORONA ITOLEWE"


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akipokea Ripoti ya Kamati Maalum aliyoiunda kwa ajili ya kufanya tathmini ya Ugonjwa wa Corona COVID -19 nchini kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo Profesa Said Aboud Ikulu Jijini Dar es Salaam leo tarehe 17 Mei, 2021.

Akizungumza wakati wa kukabidhi ripoti hiyo, mwenyekiti wa Kamati hiyo, Prof. Said Aboud amesema;

 

“Tangu kuingia kwa Covid 19 Tanzania March 2020, Tanzania imekumbwa na mawimbi mawili makubwa na sasa kutokana na mwenendo wa ugonjwa huo katika Mataifa mengine Duniani, kuna tishio la kutokea wimbi la tatu nchini.

 

“Chanzo ya COVID-19 itolewe kwa vipaumbele kwa kuanzia kwa wahudumu wa afya, watumishi wa umma, viongozi wa dini na mahujaji, wazee, wenye maradhi sugu, watumishi wa vyombo vya ulinzi na usalama na wasafiri wanaokwenda nje ya nchi.

 

“Kamati inaishauri serikali kwa kutumia vyombo vyake iendelee na hatua kuelekea kuruhusu matumizi huru ya chanjo dhidi ya COVID-19 kwa kutumia chanjo zilizoorodheshwa na WHO ili kuwapa fursa ya kinga wananchi wake.

 

“Kamati imebaini kuwa mwamko wa kudhibiti wimbi la kwanza la Corona ulikuwa mkubwa ukilinganisha na wimbi la pili, Kamati imeshauri kuimarisha kasi kudhibiti tishio la wimbi la tatu.

 

“Baada ya uchambuzi wa kina Kamati imependekeza Serikali itoe taarifa juu ya uwepo wa ugonjwa wa Covid 19 na ichukue hatua madhubuti kuimarisha hatua zote za kinga katika ngazi zote ili kuepusha wimbi la tatu la ugonjwa huo.

 

“Tanzania ishiriki ipasavyo katika maamuzi na itekeleze maazimio ya Kikanda na Kimataifa iliyoridhia katika Jumuiya za Afrika Mashariki, SADC, AU na WHO,” amesema Prof. Said Aboud.

Share:

Waziri Mwigulu Nchemba Atoa Maagizo kwa Msajili wa Hazina


Na Mwandishi Maalumu, Arusha
WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba amemuelekeza Msajili wa Hazina kufanya tathmini ya utendaji na ufanisi wa Taasisi na Mashirika ya Umma ili aje na ushauri mzuri kwa Serikali ikiwemo kupendekeza kufutwa na kuunganishwa kwa baadhi ya taasisi au kuanzishwa kwa taasisi mpya kama kutakuwa na ulazima huo. 


“Hii itasaidia serikali kubaki na taasisi na mashirika yenye kuleta tija badala ya kuwa mzigo kwa serikali,” ameeleza.


Aidha, amesema hatakubali kuona taasisi, mashirika ya umma na wakala za serikali zinashindwa kuwasilisha hesabu zake kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) mwaka huu, huku akianisha maeneo 10 ambayo wanatakiwa kuyawekea msisitizo na kuimarisha mifumo ya utendaji na uwajibikaji wa taasisi ili zitoe huduma sahihi na endelevu.


Dk Mwigulu aliyasema hayo jana jijini hapa wakati akifungua mafunzo ya mikataba ya utendaji kazi ya Ofisi ya Msajili wa Hazina na bodi za taasisi, mashirika ya umma na wakala za serikali yanayofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC).


Katika hotuba yake iliyosomwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dk Khatibu Kazungu, Dk Mwigulu alisema serikali imefanya uwekezaji wa takriban Sh trilioni 65 kwenye taasisi na mashirika yapatayo 237 kwa lengo la kutoa huduma mbalimbali za kijamii, kiuchumi na kusaidia katika kuchangia Pato la Taifa. 


“Ni vyema mkafahamu kwamba taasisi na mashirika haya yanatumia kiasi kikubwa cha fedha za umma kwa njia ya mitaji, mishahara na matumizi mengineyo. Kwa misingi hiyo ni matarajio ya Serikali ya Awamu ya Sita, chini ya Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ni kwamba, taasisi na mashirika haya yatasimamiwa ipasavyo ili yaweze kutoa huduma sahihi na endelevu,” alisema Dk Mwigulu.


Aliongeza kuwa pamoja na jitihada zinachokuliwa na serikali, bado kuna maeneo 10 ambayo ni muhimu kuweka msisitizo wa kuimarisha mifumo ya utendaji kazi na uwajibikaji wa taasisi hizo.


Aliyataja kuwa ni baadhi ya taasisi bado zinachelewa kuwasilisha hesabu za taasisi kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa ajili ya ukaguzi. “Katika mwaka huu wa fedha na miaka ijayo sitapenda kusikia tena taasisi yoyote ya umma kwamba imeshindwa au kuchelewa kuwasilisha hesabu kwa wakati,” alieleza.
 
“Aidha, taarifa hizo (za utekelezaji za robo mwaka na mwaka) zinazowasilishwa kwa Msajili wa Hazina ni lazima zipitiwe na kumilikiwa na uongozi wa taasisi,” alibainisha na kumuagiza Msajili wa Hazina kuchukua hatua stahiki kwa watakaoshindwa kutekeleza hilo.


Jingine ni kuagiza taasisi na mashirika yote kuhakikisha matumizi yao yanazingatia Mwongozo wa Bajeti wa Mwaka 2021/22 na kanuni zake zinafuatwa ipasavyo katika utekelezaji wa bajeti.


“Na kwa taasisi na mashirika ambayo hazikuzingatia mwongozo wa bajeti hususan kwa fedha za maendeleo, nakuagiza Msajili wa Hazina kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha na Mipango mzichambue upya na kusitisha miradi yote itakayoshindwa kukidhi matakwa ya mwongozo wa Bajeti kwa mwaka 2021/22,” aliagiza.


Aidha, alisema maombi ya fedha au idhini ya mikopo kwa taasisi na mashirika ya umma yote yapitishwe kwa Msajili wa Hazina kufanyiwa uchambuzi wa maandiko husika kabla ya kuwasilishwa Hazina ili kukidhi matakwa ya Sheria ya Misaada, dhamana na mikopo ya mwaka 1974 kama ilivyorekebishwa 2017. 


Dk Mwigulu alisema hatua hii inalenga kuiwezesha kuwa na kumbukumbu sahihi na udhibiti wa mikopo na matumizi ya fedha kwenye miradi ya maendeleo kwa taasisi na mashirika ya umma.


“Taasisi ziwasilishe michango kwa wakati na kiasi kinachohitajika kwa mujibu wa Sheria ya Msajili wa Hazina na Fedha. Ili kuhakikisha maduhuli na michango inakusanywa ipasavyo na kwa wakati, nakuagize Msajili wa Hazina kuhakikisha makusanyo ya maduhuli ya taasisi zote pamoja na michango yote ya asilimia 15 inakusanywa kwa njia ya kielektroniki,” alibainisha eneo jingine Dk Mwigulu linalopaswa kusimamiwa.


Alisisitiza taasisi kutumia Mfumo wa Mipango na Bajeti (PLANREP), Mfumo wa Kihasibu wa Serikali (MUSE) na Mfumo wa Taarifa za Kimenejimenti na Bodi wa Msajili wa Hazina (OTRMIS) pamoja na mingine yote kama itakavyoelekezwa ili kuimarisha udhibiti wa matumizi ya fedha na utekelezaji wa mipango ya taasisi.


Alisema matumizi ya bodi za wakurugenzi za taasisi yafuate miongozo iliyotolewa na serikali kupitia Ofisi ya Msajili wa Hazina. Aliagiza vitengo vya ukaguzi vya taasisi vidhibiti matumizi ambayo ni kinyume cha miongozo hiyo. 


Pia kwa taasisi za umma ambazo sehemu ya mapato zinakusanya zenyewe, alisema zinapaswa kupunguza utegemezi toka serikali. 


“Bado kuna taasisi nyingi hata matumizi ya kawaida bado zinategemea zilitewe na serikali. Nawakumbusha tena katika hili, zitumieni fursa mlizonazo kuongeza na kukusanya mapato. Kuweni wabunifu kwa kutumia fursa mlizonazo ili kujiongezea mapato. Badilikeni na kuachana na tabia ya kufanya kazi kwa mazoea,” alisema Dk Mwigulu na kuongeza kuwa anatarajia eneo hilo lichangie angalau asilimia 10 ya bajeti za taasisi.


Aidha, aliagiza taasisi ziwe na mipango madhubuti ya kujenga uwezo wa watumishi wa vitengo vya Ukaguzi wa Ndani ili wawe na uelewa mzuri kuhusu majukumu yote ya taasisi pamoja na mifumo mbalimbali inayotumika katika utendaji kazi ili kuviwezesha kuleta tija katika kutekeleza majukumu yake ya ushauri na udhibiti mahala pao pa kazi.


“Mwisho kabisa nikuagize Msajili wa Hazina, nenda kafanye tathmini ya utendaji na ufanisi wa taasisi na mashirika ya umma ili uje na ushauri mzuri kwa serikali ikiwemo kupendekeza kufutwa na kuunganishwa kwa baadhi ya taasisi kama au kuanzishwa kwa taasisi mpya kama kutakuwa na ulazima huo. Hii itasaidia serikali kubaki na taasisi na mashirika yenye kuleta tija badala ya kuwa mzigo kwa serikali,” alieleza Dk Mwigulu.


Alisema ni matarajio yake kuwa masuala hayao yatafanyiwa kazi na taasisi zote na kuhakikisha mapungufu hayo hayajirudii katika taasisi, huku akiagiza kuwa kuanzia mwaka 2022/23 matokeo ya tathmini ya mikataba ni vizuri yawekwe wazi ikionesha taasisi itayofanya vizuri zaidi hadi ile itakayofanya vibaya.  


Awali, Msajili wa Hazina, Athumani Mbuttuka alisema mafunzo hayo yanahusisha washiriki 711 kutoka taasisi, mashirika ya umma na wakala za serikali 237 yaliyoko chini ya Ofisi ya Msajili wa Hazina. 


Mbuttuka alisema katika mwaka huu wa fedha (2020/21), ofisi yake imesaini Mikataba ya Utendaji Kazi na taasisi na mashirika ya umma 230 kati ya taasisi na mashirika ya umma 237 sawa na asilimia 97 ya taasisi zote 237 ambazo zimekeleza matakwa ya kisheria ukilinganisha na mikataba 13 iliyosainiwa mwaka 2014/15.



Share:

IGP Sirro Amvalisha Cheo Cha Ukamishna, Salum Hamduni kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan


 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amemtaka kamishna Salum Hamdun kutimiza wajibu wake kwa mujibu wa kiapo chake na kuhakikisha anasimamia sheria na taratibu za nchi ikiwa pamoja na kuwatendea haki wananchi atakaowahudumia.

IGP Sirro amesema hayo wakati akimvalisha Cheo cha Ukamishna wa Polisi CP Salum Hamdun kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan baada ya Mhe. Rais kumpandisha cheo hicho.

Hata hivyo, IGP Sirro wakati akimvalisha cheo cha Ukamishna pia alimkabidhi Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na kitabu cha muongozo kinachoongoza Jeshi hilo.

Naye Kamishna mteule CP Salum Hamduni amesema kuwa, ataendelea kutenda kazi zake kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizopo na kwamba atahakikisha anawatendea haki Watanzania kwa kulinda usalama wao na mali zao.

Kwa upande wake Kamishna wa Kamisheni ya Ushirikishwaji wa Jamii CP Dkt. Mussa Ali Mussa amesema kuwa, Jeshi la Polisi litaendelea kufanya kazi kwa weledi na kwa uaminifu ili kuhakikisha Jeshi linaendelea kujijengea heshima kwa wananchi.

Awali kabla ya kupandishwa cheo hicho na Mhe. Rais, Kamishna Salum Hamdun alikuwa Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalum ya Dar es salaam akiwa na Cheo cha Kamishna Msaidizi wa Polisi.


Share:

FAMILIA YATAKA KUJUA ALIPO MUUZAJI WA COMPUTER DENNIS ALIYEPOTEA KWA SIKU 48

Fundi Computer & CCTV Camera na Muuzaji wa  Computer Dennis Richard Katangwa (aliyepotea/hajulikani alipo)
Dada wa Dennis Richard Katangwa Bi. Winfrida Kalubale (kulia) na Baba Mzazi wa Dennis Bwana Richard Katangwa wakizungumza na Waandishi wa Habari leo Jumatatu Mei 17,2021 katika ofisi ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club - SPC)
Dada wa Dennis Richard Katangwa Bi. Winfrida Kalubale (kulia) na Baba Mzazi wa Dennis Bwana Richard Katangwa wakizungumza na Waandishi wa Habari leo Jumatatu Mei 17,2021 katika ofisi ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club - SPC)
Fundi Computer & CCTV Camera na Muuzaji wa  Computer Dennis Richard Katangwa (aliyepotea/hajulikani alipo)
Ofisi ya Fundi Computer & CCTV Camera na Muuzaji wa  Computer Dennis Richard Katangwa (aliyepotea/hajulikani alipo)
Fundi Computer & CCTV Camera na Muuzaji wa  Computer Dennis Richard Katangwa (aliyepotea/hajulikani alipo) akiwa ofisini kwake

Fundi Computer &CCTV Camera na Muuzaji wa  Computer Dennis Richard Katangwa (aliyepotea/hajulikani alipo) akiwa kwenye gari lake aina ya Vitiz lenye namba za usajili DFY 863


Na Shinyanga Press Club Blog

FAMILIA ya kijana Dennis Richard Katambwa (31) mkazi wa Bushushu wilaya ya Shinyanga mkoani Shinyanga imeiomba Serikali kuingilia kati ili kujua hatma ya mtoto wao  huyo aliyepotea tangu Machi 31, mwaka huu katika mazingira ya kutatanisha.

Kijana huyo ambaye ni fundi maarufu wa Kompyuta mjini Shinyanga lakini pia anajihusisha na kufunga kamera za CCTV pamoja na kuuza kompyuta na vifaa vyake, alipotea Machi 31, mwaka huu akiwa na gari lake na hajaonekana hadi sasa licha ya jitihada za familia hiyo kumtafuta kwa kushirikiana na vyombo vya usalama.

Hata hivyo, Mapema mwezi huu inaelezwa kuwa Gari la kijana huyo lenye namba za usajili DFI 863 VITZ rangi ya blue bahari lilipatikana  katika kijiji cha Natta wilayani Nzega likiwa limetelekezwa ambapo ndugu wa kijana huyo walipigiwa simu Mei 5,2021 kuhusu kuonekana kwa gari hilo.

Akizungumza leo Mei 17,2021 na Waandishi wa Habari katika ofisi za Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club - SPC), Dada wa Dennis, Winfrida Kalubale akiwa ameambatana na baba mzazi wa kijana huyo, Richard Katangwa amesema kuwa siku ya Machi 31, 2021 ndugu yao akiwa kwenye mazingira yake ya kazi asubuhi alienda kupokea mzigo wa Computer eneo la washusha mizigo mbalimbali kutoka Dar es Salaam (Shy elimu) mtaa wa Makongoro mjini Shinyanga na kuufikisha ofisini na kumwambia kijana anayemsaidia kuuza dukani aupange mzigo huo, kisha yeye akaondoka na flash akasema anarudi.

Lakini baada ya takribani dakika 45 gari lake lilirudi na watu wawili mwanamke na mwanaume ambao hawakushuka kutoka kwenye gari, wakafika karibu na ofisi kisha Dennis akampigia kijana wake awapatie laptop na Sh. 10,000.

“Kijana akawapelekea kwenye gari wakashusha kioo wakachukua. Kazi zikaendelea lakini baadae wateja wakiwa wanakuja wanalalamika hawampati Dennis na simu hapokei, ilipofika jioni kijana akawa na mashaka kwamba kwanini boss wake hapokei simu, ikabidi aende nyumbani kuangalia akakuta Jirani nae analalamika kwamba wanampigia simu hawampati maana kaacha bomba chumbani linamwaga maji.

“Asubuhi simu ikawa inapigwa inaita tu lakini haipokelewi na sms hazijibiwi. Rafiki yake mmoja akaona simu yake iko mtandaoni (online) akamtumia sms kwamba mbona unatafutwa hupatikani baadae ile simu ikapotea hewani,” ameeleza Winfrida.

Akisimulia kwa masikitiko, Winfrida aliendelea kwa kueleza kuwa jitihada za kumtafuta ziliendelea na baadhi ya ndugu walikuja ndipo wakapata wazo la kwenda kuvunja mlango wa nyumbani kwake, ambako waliingia ndani lakini wakakuta kila kitu kiko sawa ndani ya nyumba.

"Tukaendelea na juhudi za kumtafuta, simu ikawa hewani mara inapotea, baada ya masaa 24 tukaenda polisi ambao mpaka leo wanaendelea kufuatilia. Leo ni siku ya 48 hajaonekana na hatujui alipo, tunaomba serikali iingilie kati ili tujue kijana wetu yuko wapi", amesimulia.

Wakiwa bado wako njia panda na huzuni kubwa, Jumatano ya Aprili 4, mwaka huu walipokea simu na kuelezwa kuwa gari la ndugu yao aliyepotea limeonekana wilayani Nzega mkoa wa Tabora  ndipo walipofanya juhudi za kufuatilia kujiridhisha na kubaini kuwa ndilo gari lenyewe wakawasiliana na Jeshi la Polisi Nzega ambapo ulipofanyika utaratibu wa kulirudisha Shinyanga na mpaka sasa lipo katika kituo cha Polisi Shinyanga.

Amesema tayari familia hiyo imetoa polisi taarifa ya kupotelewa ndugu yao na kuandikiwa RB namba SHY/RB/1385/2021 ambayo walipewa Aprili Mosi, mwaka huu.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger