Monday, 1 March 2021
Sunday, 28 February 2021
Market Sales Manager at TalentintheCloud International
This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content
Market Sales Manager TalentintheCloud International Zanzibar West, Tanzania The continent’s most successful and fastest growing payments company is looking to add a talented and experienced Market Sales Manager to their team. Since identifying a gap in the African online payments landscape, they have rapidly led the online payments industry into centre stage – turning […]
This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details
Medical Specialist II (Dermatologist) at Muhimbili National Hospital
This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content
POST: MEDICAL SPECIALIST II (DERMATOLOGIST) – 1 POST POST CATEGORY(S) HEALTHCARE AND PHARMACEUTICAL EMPLOYER Muhimbili National Hospital APPLICATION TIMELINE: 2021-02-26 2021-03-11 DUTIES AND RESPONSIBILITIES To provide routine specialized medical services for in-patients and out patients; To supervise ward rounds and advice on appropriate medication; To participate in the training of student doctors in their areas […]
This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details
Tanzia : MFANYABIASHARA MAARUFU JIJINI ARUSHA AFARIKI DUNIA
JOGOO ASHIKILIWA POLISI KWA KUUA MMILIKI WAKE
AWESO ATOA SIKU SABA MKANDARASI KULIPWA DENI LAKE
Na Abby Nkungu, Manyoni
WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso amemwagiza Meneja wa Wakala wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) mkoa wa Singida kumlipa ndani ya siku saba Mkandarasi wa Kampuni ya CMG Construction takriban Sh milioni 700 anazodai kutokana na kujenga tanki la kuhifadhia na kusambaza maji Lusilile wilayani Manyoni lenye ujazo wa lita milioni mbili.
Waziri Aweso alilazimika kutoa agizo hilo baada ya Mbunge wa Manyoni Mashariki, Dk Pius Chaya kudai kuwa wananchi wake zaidi ya 50,000 katika vijiji 11 vilivyopo eneo hilo hawajaanza kunufaika na huduma ya maji ya mradi huo kutokana na Mkandarasi huyo kutolipwa deni lake.
"Lengo la mradi huu lilikuwa kupeleka maji kwenye Kituo cha Afya Kintinku na vijiji vilivyopo eneo hili lakini usambazaji wa maji unasuasua sana japo tanki lipo tayari." alisema Mbunge huyo na kuongeza;
Kituo hiki cha afya kinahudumia wananchi wa tarafa mbili; hivyo ni matamanio yangu huduma hii ya maji ifikishwe hapo mapema ili huduma nyingine za kiafya pia ziweze kufanyika ipasavyo".
Kutokana na hoja hiyo, Waziri Aweso alimuuliza Meneja RUWASA mkoa, Mhandisi Lucas Saidi iwapo ni kweli Mkandarasi huyo anaidai Serikali naye akathibitisha kuwa anadai takriban Sh milioni 700.
"Ndio maana mradi huu unasuasua. Hakikisha ndani ya siku saba Mkandarasi huyu awe amelipwa. Katoe Sh milioni 700 kwenye akaunti yenu umpe ili amalizie kazi wananchi waanze kupata huduma ya maji" aliagiza Waziri Aweso.
Akiwa kijiji cha Kashangu, Itigi Jimbo la Manyoni Magharibi, kwenye ziara yake ya kikazi ya siku moja mkoani Singida kukagua miradi mbalimbali ya maji, Waziri Aweso alielezwa kuwa jumla ya Sh milioni 150 ziliweza kuokolewa katika ujenzi wa mradi huo wa maji.
Meneja wa RUWASA wilaya ya Manyoni, Gabriel Ngongi alimweleza Waziri kuwa mradi huo ingawa ulitengewa jumla ya Sh milioni 350, lakini kwa kutumia wataalam wa ndani na mbinu nyingine mbadala, wameweza kutumia Sh milioni 200 tu; hivyo kuokoa Sh milioni 150.
Waziri Aweso aliipongeza hatua hiyo huku akiahidi kuwa Serikali haitakuwa kikwazo bali itatoa ushirikiano wake wote kwa watumishi wanaojituma kama RUWASA Manyoni.
Aidha, alitoa mwito kwa wananchi wa eneo hilo na popote ilipo miradi ya aina hiyo Nchini kuitunza na kuilinda kwa nguvu zao zote kwa kuwa Serikali inatumia gharama kubwa katika kutekeleza miradi hiyo.
Picha : ASKOFU MACHIMU AZINDUA WIMBO MAALUMU WA TANZANIA YA AMANI WA KWAYA YA DYNAMIC EAGT...AONGOZA MAOMBI DHIDI YA CORONA
Muonekano wa DVD ya wimbo wa Tanzania ya Amani