Sunday, 31 January 2021
TADB YAWEZESHA WAFUGAJI KUPATA NG'OMBE WA KISASA WA MAZIWA
Sehemu ya wafugaji wakimsikiliza Meneja wa Kanda ya Mashariki wa Benki ya Kilimo (TADB) Jeremiah Mhada akizungumza wakati wa halfa hiyo
BENKI ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imekwisha toa mikopo yenye thamani ya Shilingi billioni 11.80 ili kuwezesha mnyororo wa thamani wa sekta ya maziwa kote nchini.
Pia imewezesha wafugaji Mkoani Tanga kupata mbegu ya ng’ombe bora wa kisasa wa maziwa wakiwemo wafugaji 114 kupitia vyama vya msingi 5 kupata mikopo ya ng’ombe wa kisasa wenye thamani ya Zaidi ya Tsh 396m.
Akizungumza katika hafla iliyoandaliwa na shirika la kimataifa la Heifer,Meneja wa Kanda ya Mashariki wa Benki ya Kilimo (TADB) Jeremiah Mhada alieleza umuhimu wa ushirikiano wa wadau muhimu katika sekta ya mifugo ili kuongeza tija nakuleta mapinduzi ya kweli katika sekta ya maziwa nchini.
Alisema kupitia mkopo huu, TADB imeweza kuwajengea wafugaji hao mabanda ya kutunzia ng’ombe 25 na kupata mitamba ya kisasa ili wanufaike na ufugajiwa ng’ombe wa maziwa ikiwemo kupatiwa mikopo naafuaa itakayowawezesha kupata mbegu bora za ng'ombe wa maziwa.
“TADB ili kuhakikisha wafugaji wananufaika na sekta hii ya maziwa tuliingia katika ushirikiano na shirika la kimataifa la Heifer International kuhakikisha wafugaji wetu wanajengewa uwezo wa namna bora ya ufugaji wa ng’ombe wa maziwa lakini pia kujiunga katika vikundi ili kuweza kupata mikopo kwa urahisi.”Alisema
TADB imewezesha vyama vya msingivya UWAMWA, CHAWAMU, UWAKO, UWAMKI na UWADAKI kuweza kupata jumla ya ng’ombe wa kisasa 156 kwa wafugaji 121 ikiwemo wanawake 39 pamoja na kuwawezesha kupata mkopo huo wafugaji hao tayari wana soko la kuuza maziwa yao.
"Kwa hapa Tanga wataweza kuuza kwa kampuni ya Tanga Fresh ambayo nayo TADB imekwisha iwezesha katika kumudu kuweza kununua maziwa kutoka kwa wafugaji hawa wadogowadogo.” Alisisitiza Mhada.
Kabla ya kufanya makabidhiano hayo,TADB kwakushirikiananaShirika la kimataifa la Heifer International waliendesha mafunzo kwa viongozi wa vyama vya ushirika 26 ambao walijengewa uwezo kwenye namna ya usimamizi bora wa biashara, usimamizi wa fedha, utunzaji wa kumbukumbu, utunzajiwa kumbukumbu na uongozi bora.
“Ufugaji ili uwe na tija nilazima wafugaji wajengewe uwezo na ni muhimu kufahamu namna ya kusimamia fedha, utunzaji wa kumbukumbu,uongozi bora na masuala mengine ya usimamizi wa biashara kwa kuwa na uwezo huu, mfugaji anaweza kuona namna anavyonufaika na mkopo na hata kuweza kufahamu kipato chake.”Aliongezea Mhada.
Alisema Wafugaji wadogo kupitia TADB wanaendelea kunufaika na fursa zilizopo kupitia benki ya kilimo na pia kupitia ushirikiano huo wa TADB nashirika la kimataifa la Heifer.
Serikali imeainisha sekta ya maziwa kama moja ya sekta muhimu katika kuchochea uwekezaji katika viwanda jambo ambalo TADB inawawezesha wawekezaji kama kampuni za Tanga Fresh, Kahama Fresh, Njombe Milk na viwanda vingine katika maeneo mbalimbali nchini.
Aliongeza kwamba kupitia uwekezaji katika mnyororo wa thamani wa sekta ya kilimo, pia kama Taifa wanaweza kujihakikishia upatikanaji na usalama wachakula,lishe bora na kipato kwa wafugajina pia kuongezapato la Taifa.
Mhada alisema sekta ya maziwa nchini inachangia asilimia 1.2% yapato la Taifa huku akieleza ili kuhakikisha wanaongeza kipato kwa wafugaji wadogo wadogo ambao kupitia shughuli hizi za ufugaji huchangia pato la Taifa.
Alisema wamewezesha kupata mitamba ya kisasa na kuwaunganisha na masoko ili kuongeza thamani na kuchochea ongezauzalishaji wa mazi wa nchini.
Saturday, 30 January 2021
WAZIRI MWAMBE AKUTANA NA WAZALISHAJI WA SUKARI NCHINI JIJINI DODOMA
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Geoffrey Mwambe,akizungumza na Mtendaji Mkuu na Meneja wa kiwanda cha Dangote nchini Tanzania Bw.Abdullahi Baba aliyemtembelea ofisini kwake leo Januari 29,2021 jijini Dodoma
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Geoffrey Mwambe,akimsikiliza Mtendaji Mkuu na Meneja wa kiwanda cha Dangote nchini Tanzania Bw.Abdullahi Baba wakati wa mazungumzo ofisini kwake leo Januari 29,2021 jijini Dodoma
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Geoffrey Mwambe,akiwa katika picha ya pamoja na Mtendaji Mkuu na Meneja wa kiwanda cha Dangote nchini Tanzania Bw.Abdullahi Baba mara baada ya mazungumzo ofisini kwake leo Januari 29,2021 jijini Dodoma
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Geoffrey Mwambe,akizungumza na wazalishaji wa Sukari nchini na kusikiliza changamoto zao ili kuzitatua na kuongeza uzalishaji wa Sukari leo Januari 29,2021 jijini Dodoma
Baadhi ya wazalisha wa Sukari Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Geoffrey Mwambe,wakati wa kikao cha wazalishaji wa Sukari nchini ambapo amesikiliza changamoto zao na kuahidi kuzitatua na kuongeza uzalishaji wa Sukari leo Januari 29,2021 jijini Dodoma
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Geoffrey Mwambe,akisisitiza jambo zaidi wakati wa kikao na wazalishaji wa Sukari nchini pamoja na kusikiliza changamoto zao ili kuzitatua na kuongeza uzalishaji wa Sukari leo Januari 29,2021 jijini Dodoma
Afisa Mtendaji Mkuu Utawala TPC Bw.Jaffari Ally akielezea jambo kwa Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Geoffrey Mwambe(hayupo pichani) wakati wa kikao cha wazalishaji wa Sukari nchini ambapo amesikiliza changamoto zao ili kuzitatua na kuongeza uzalishaji wa Sukari leo Januari 29,2021 jijini Dodoma
Mkurugenzi Mkuu Bodi ya Sukari Tanzania Prof.Kenneth Bengesi,akizungumza kwenye kikao cha wazalishaji wa Sukari nchini ambapo Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Geoffrey Mwambe ameahidi kuzitatua changamoto hizo ili kuzitatua na kuongeza uzalishaji wa Sukari leo Januari 29,2021 jijini Dodoma
Na.Alex Sonna,Dodoma
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Geoffrey Mwambe,amekutana na wazalishaji wa Sukari nchini na kusikiliza changamoto zao ili kuzitatua na kuongeza uzalishaji na kuhakikisha Sukari inapatikana kwa urahisi wakati wote nchini.
Akizungumza na na wazalishaji hao leo Janauari 29,2021 jijini Dodoma Mhe.Mwambe amesema kuwa Serikali inalenga kuongeza uzalishaji wenye tija kwa kutumia teknlojia na miundombinu ya kisasa ya umwangiliaji.
”Leo nimekutana na nyie kwa leongo la kujifunza na kujua changamoto mlizonazo katika uzalishaji wa sukari nchini na waahidi tutazifanyia kazi”amesema Mhe.Mwambe.
Hata hivyo Mhe.Mwambe amewatoa wasiwasi wazalishaji hao kuwa Serikali itashughulikia changamoto hizo ili kuleta maendeleo na kuongeza uzalishaji zaidi nchini .
Awali Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Geoffrey Mwambe,amekutana na kufanya mazungumzo na Mtendaji Mkuu na Meneja wa kiwanda cha Dangote nchini Tanzania Bw.Abdullahi Baba.
WAFUGAJI NCHINI WATAKIWA KUFUGA KISASA
wakati wa hafla ya kukabidhi malori na vifaa vya maziwa kutoka shirika la Heifer International kupitia mradi wa usindikaji maziwa Tanzania (TMPP) iliyofanyika katika kiwanda cha Tanga Fresh kilichopo Jijini Tanga kushoto aliyekaa ni Meneja wa Kanda ya Mashariki Benki ya Maendeleo ya kilimo TADB Jeremiah Mhada Mkurugenzi wa mradi wa usindikaji wa maziwa Tanzania kutoka shirika la Helfer Mark Tsoxoakizungumza wakati wa halfa hiyo
Meneja wa Kanda ya Mashariki Benki ya Maendeleo ya kilimo TADB Jeremiah Mhada akieleza jambo wakati wa halfa hiyo
Kaimu Msajili bodi ya maziwa Noely Byamunguakizungumza wakati wa halfa hiyo
Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki kushoto akikata utepe wakati wa hafla ya kukabidhi malori na vifaa vya maziwa kutoka shirika la Heifer International kupitia mradi wa usindikaji maziwa Tanzania (TMPP) iliyofanyika katika kiwanda cha Tanga Fresh kilichopo Jijini Tanga kulia ni Mkurugenzi wa mradi wa usindikaji wa maziwa Tanzania kutoka shirika la Helfer Mark Tsoxo
Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki kushoto akimshukuru Mkurugenzi wa mradi wa usindikaji wa maziwa Tanzania kutoka shirika la Helfer Mark Tsoxo mara baada ya makabidhiano hayo kulia anayeshuhudia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa ambaye pia alimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Tanga katika halfa hiyo
Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki akiwasha moja ya magari hayo
RAIS MAGUFULI AZINDUA MRADI WA MAJI TABORA NA UJENZI WA JENGO LA WAGONJWA WA HUDUMA YA DHARURA HOSPITALI YA KITETE
RAIS MAGUFULI AZINDUA MRADI WA MAJI ISAKA- KAGONGWA ...AMPONGEZA AWESO KUFUKUZA WAKANDARASI FEKI
AGIZO LA WAZIRI NDAKI LATEKELEZWA... WATATU MBARONI
Na. Edward Kondela
Jeshi la polisi Mkoa wa Arusha kwa kushirikiana na Wizara ya Mifugo na Uvuvi pamoja na vyombo vingine vya ulinzi na usalama tarehe 27.01.2021 limewakamata watuhumiwa watatu kwa tuhuma za wizi na utoroshaji wa mifugo maeneo ya mipakani.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa mwishoni mwa wiki na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi Salum Hamduni amesema jeshi hilo limewakamata watuhumiwa hao katika tarafa ya Loliondo, Wilaya ya Ngorongoro mkoani humo kufuatia agizo alilolitoa Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki Jumatano iliyopita la kukamatwa kwa watuhumiwa 67 wa utoroshaji wa mifugo na mazao yake.
Kamanda Hamduni amesema kukamatwa kwa watuhumiwa hao watatu kunatokana na baada ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kutangaza operesheni ya kudhibiti wizi na utororshaji wa mifugo maeneo ya mipakani ambapo zilipatikana taarifa za uwepo wa watu wanaojihusisha na wizi na utoroshaji wa mifugo katika Wilaya ya Ngorongoro.
Ameongeza kuwa upelelezi bado unaendelea kuhusiana na tukio hilo, mara utakapokamilika jalada litapelekwa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria.
Ametoa wito kwa wananchi kuepuka usumbufu kwa kuhakikisha wanafuata sheria za biashara ya usafirishaji wa mifugo kwani wasipofanya hivyo watakamatwa na kuchukuliwa hatua kali za kisheria.
Jumatano ya wiki iliyopita Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki akiwa katika ofisi za wizara hiyo zilizopo katika mji wa serikali Mtumba jijini Dodoma wakati akiwasilishiwa ripoti ya uchunguzi, kuhusu utoroshaji wa mifugo mipakani aliliagiza Jeshi la Polisi nchini Kikosi cha Kuzuia Wizi wa Mifugo kuwakamata mara moja watuhumiwa 67 wa utoroshaji wa mifugo na mazao yake kwenda nchi za jirani.
Katika ripoti ya uchunguzi, kuhusu utoroshaji wa mifugo mipakani, iliyowasilishwa na Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi Julius Mjengi kwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki imeeleza kuwa kabla ya tarehe 7 Novemba, 2020, mifugo iliyokuwa inatoka kwenye minada ya awali ya Handeni na Kilindi kuelekea nchini Kenya kupitia mpaka wa Horohoro haikuwa inafuata taratibu za forodha kama shehena nyingine.
Aliongeza kuwa takwimu za daftari la mifugo katika mpaka wa Horohoro zinaonyesha idadi ya mifugo iliyopitishwa kuelekea nchini Kenya kwa kipindi cha miaka 17 kutoka mwaka 2003 hadi Novemba, 2020 ilikuwa ni ng’ombe 24,980 na Mbuzi na Kondoo 9,368 (sawa na wastani wa Ng’ombe 122 na Mbuzi/Kondoo 46 kwa mwezi).
Taarifa hiyo ilibainisha pia baada ya uchunguzi, ilionekana kuwa kati ya tarehe 7 Novemba, 2020 hadi tarehe 9 Desemba, 2020 (kipindi cha mwezi mmoja tu) jumla ya Ng’ombe 1,096 na Mbuzi na Kondoo 1,044 walipitishwa katika kituo cha Forodha kuelekea nchini Kenya, ambapo huo ni wastani wa idadi ya mifugo iliyopita mpakani ndani ya mwezi mmoja ukilinganisha na siku za nyuma.
Taarifa imebaini pia viashiria vya udanganyifu wa kurekodi idadi sahihi ya mifugo inayokaguliwa kwenda Kenya hususan katika mpaka wa Hororohoro – Tanga.
Mwisho.
Imetolewa: Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Mifugo na Uvuvi
30.01.2021