Tuesday, 10 November 2020

MWALIMU AKAMATWA KWA KUMBAKA CHOONI MWANAFUNZI WAKE WA DARASA LA TANO











Kamanda wa Polisi, mkoa wa Morogoro, SACP Wilbroad Mutafungwa.

Jeshi la Polisi mkoani Morogoro, linamshikilia mwalimu wa taaluma katika Shule ya Msingi Montfort, Eneza Andarson, 27, kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi wake wa darasa la tano mwenye umri wa miaka 10, kwa nyakati tofauti.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro, SACP Wilbroad Mutafungwa, amesema kuwa mtuhumiwa huyo amekuwa akifanya kitendo hicho cha unyanyasaji kwa mwanafunzi huyo mara kwa mara katika maeneo mbalimbali shuleni hapo, ikiwemo ofisini na hata kumfuata chooni.

"Mwanafunzi huyo ni mkazi wa Kihonda baada ya kumhoji alikubali kufanyiwa vitendo hivyo na mwalimu wake na aliweza kusimulia namna ambavyo alikuwa anafanyiwa vitendo hivyo vya kikatili, wakati mwingine alikuwa anafanyiwa chooni na hata ofisini", ameeleza Kamanda Mutafungwa.

Aidha Kamanda Mutafungwa, amewashauri wazazi kuhakikisha wanafuatilia mienendo ya watoto wao , ikiwemo kuwakagua ili kujihakikisha kama hakuna vitendo vya ukatili wanavyofanyiwa.

CHANZO- EATV
Share:

TAASISI ZA JAMII FORUMS NA DORIS MOLLEL FOUNDATION ZASHIRIKIANA KUTOA ELIMU KUHUSU MTOTO NJITI


Mkurugenzi na Muasisi wa Doris Mollel Foundation Bi.Doris Mollel na Mkurugenzi Mtendaji wa asasi ya kiraia ya Jamii Forums na Waratibu wa mtandao wa JamiiForums Bw. Maxence Melo wakikabidhiana mikataba ya makubaliano ya kushirikiana katika utoaji elimu kwa jamii kuhusu mtoto njiti kupitia mitandao ya kijamii.
Mkurugenzi na Muasisi wa Doris Mollel Foundation Bi.Doris Mollel na Mkurugenzi Mtendaji wa asasi ya kiraia ya Jamii Forums na Waratibu wa mtandao wa Jamii forums Bw. Maxence Melo wakisaini makubaliano ya kushirikiana katika utoaji elimu kwa jamii kuhusu mtoto njiti kupitia mitandao ya kijamii.
Daktari bingwa wa magojwa ya watoto wachanga Dkt. Augustine Massawe akizungumza katika hafla ya makubaliano ya kushirikiana katika utoaji elimu kwa jamii kuhusu elimu ya mtoto njiti kupitia mitandao ya kijamii.
Mkurugenzi Mtendaji wa asasi ya kiraia ya Jamii Forum na Waratibu wa mtandao wa Jamii forums Bw.Maxence Melo akizungumza katika hafla ya makubaliano na Taasisi ya Doris Mollel Foundation kuhusu utoaji elimu kwa jamii kuhusu mtoto njiti kupitia mitandao ya kijamii.Mkurugenzi na Muasisi wa Doris Mollel Foundation Bi.Doris Mollel akizungumza katika hafla ya makubaliano kati ya taasisi hiyo na Jamii Forums kutioa elimu ya Mtoto Njiti katika jamii kupitia mitandao ya kijamii.

(PICHA NA EMMANUEL MBATILO)

*************************************

NA EMMANUEL MBATILO
Taasisi ya Kiraia ya Jamii Forums pamoja na Taasisi ya Doris Mollel Foundation wameingia mkataba wa makubaliano wa kupeleka ujumbe sahihi kwa wananchi kuhusiana na watoto wanaoizaliwa kabla ya wakati (njiti).

Akizungumza katika hafla hiyo Mkurugenzi na Mhasisi wa Doris Mollel Foundation Bi.Doris Mollel amesema wao kama taasisi wanafanya kazi kushirikiana na Wizara ya Afya na tayari taarifa sahihi ambazo wanazipeleka katika jamii zimeshapitishwa na kitengo cha elimu ya afya kupitia Wizara ya Afya.

“Tunaamini kupitia Jamii Forums tunaweza kuwafikia watu wengi wanaotumia mitandao ya kijamii na pia sisi ambao ni vijana tunaweza kuwasaidia watoto ambao wanazaliwa kabla ya wakati kwasababu kila mama anaweza kujifungua kabla ya wakati”. Amesema Bi.Doris Mollel.

Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa asasi ya kiraia ya Jamii Forums na Waratibu wa mtandao wa Jamii forum Bw.Maxence Melo amesema Jamii Forums inauhakika wa kuwafikia wananchi wasiopungua Milioni 10 hivyo kuingia makubaliano na taasisi ya Doris Mollel Foundation wanaamini watawafikia wananchi wengi na kuelewa kuhusu mtoto kuzaliwa kabla ya wakati (Njiti).

“Mtoto Njiti ilikuwa haifahamiki sana ila kupitia Dorine Molle Foundation imejitahidi kuhakikisha kwamba elimu ya Mtoto njiti inawafikia wengi na sisi tukaona kwamba kwa namna ya kipekee tumeona tuwape ushirikiano hasa kwa mwezi huu wa Mwezi 11 na si kwa muda mfupi bali kwa muda wa takribani mwaka mmoja na kuhakikisha jamii inapata elimu ya kutosha kuhusu chanzo sahihi na taarifa sahihi”. Amesema Bw.Melo.

Nae Daktari bingwa wa magojwa ya watoto wachanga Dkt. Augustine Massawe ameshuhudia Asasi mbili za kiraia ya Doris Mollel Foundation pamoja na Jamii Forums wakisaini makubaliano ya ushirikiano wenye lengo la kupaza sauti kwa jamii kufahamu kuhusiana na watoto wanaozaliwa kabla ya wakati yaani watoto njiti katika hafla iliyofanyika jijini Dar es salaam .

Aidha Dkt. Massawe amesema kuwa umri mdogo wa kubeba ujauzito na hali duni ya lishe kwa watanzania ni moja ya sababu ya watoto kuzaliwa njiti ambapo inakisiwa kila watoto kumi wanaozaliwa mmoja anakuwa amezaliwa kabla ya muda.
Share:

LIVE: Kiapo Cha Uaminifu Kwa Wabunge Wateule | Kikao Cha Kwanza Cha Bunge La 12

 LIVE: Kiapo Cha Uaminifu Kwa Wabunge Wateule | Kikao Cha Kwanza Cha Bunge La 12



Share:

Serikali kuwachukulia hatua kali wanaopandisha bei ya saruji


Serikali imesema itawachukulia hatua kali za kisheria, ikiwemo kuwanyang’anya leseni wale wote watakaobainika kuuza saruji kwa bei ya juu.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigella, mara baada ya kutembelea viwanda vya Saruji vilivyopo jijini Tanga na kukuta uzalishaji ukiendelea.

Amesema bei ya kiwandani ni kati ya shilingi elfu kumi na mia sita (10,600) kwa mkoa wa Tanga na nje ya mkoa ni shilingi elfu kumi na moja na mia sita (11,600) kwa mfuko moja.

Aidha amesema kutokana na kutokuwepo kwa ongezeko la bei kutoka viwandani ya bei ya saruji itabaki kama ilivyokua awali na si vinginevyo


Share:

Wizara Ya Afya Imejipanga Kutoa Elimu Ya Bima Ya Afya Kwa Wote


Na. Catherine Sungura, WAMJW- Dar es salaam
Katika kuelekea kwenye bima ya afya kwa wote, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imejipanga kutoa elimu kwa jamii ili wananchi waweze kuelewa umuhimu wa kuwa na bima kuliko kusubiri hadi pale watakapougua.

Hayo yamesemwa leo na Prof. Mabula Mchembe, Katibu Mkuu Wizara ya Afya wakati wa siku ya pili ya kongamano la kitaifa la kisayansi la magonjwa yasiambukiza linaloendelea jijini hapa.

Prof. Mchembe amesema hivi sasa huduma za afya kuazia ngazi ya zahanati hadi hospitali za taifa huduma za afya kwenye miundo mbinu,vifaa na vifaa tiba zimeboreshwa hivyo kwa kuwa na bima ya afya kwa wote itasaidia kupata huduma nzuri zaidi.

“Serikali kupitia Wizara ya Afya hivi sasa inatoa huduma za afya bila malipo kwa watoto chini ya miaka mitano,wazee na wale wenye saratani katika huduma za matibabu, dawa na huduma zingine,hivyo tunahitaji kuboresha zaidi vituo vyetu vya afya ,vifaa pamoja na watumishi ili kuweza kutoa huduma bora zaidi”.

Hata hivyo Katibu Mkuu huyo amewataka wale wenye bima ya afya ya NHIF waweze kujenga mazoea ya kulipa kidogo kidogo kila mwezi ili inapofika mwisho wa mwaka wawe wamekamilisha na hivyo itasaidia kutokwama kwa malipo ya awamu nyingine pale kadi inapomaliza muda wake.

Kwa upande wa magonjwa yasiyoambukiza amesema kuwa wizara pamoja na taasisi zake zote zinahusika katika kuzuia na kukinga mangonjwa yasiyoambukiza, hivyo amesisitza wananchi kuwa waangalifu kwenye vyakula pamoja na kuacha matumizi holela ya dawa.

“Watu wengine wanatumia dawa holela na ambazo zimeisha muda wake au kwa kutoandikiwa na wataalam,tuhakikishe tunatumia dawa zenye ubora kwani kila dawa ina madhara yake hivyo dawa zitumike kufuatana na malengo tarajiwa. Sisi kama wizara tutatumia wataalam wetu kuwaelimisha wananchi matumizi sahihi ya dawa.

Naye Mkurugenzi wa huduma za matibabu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Dkt. David Mwenesano amesema Mfuko umejipanga kuwafikia wananchi wote kwa makundi yao pale walipo hivyo wana aina mbalimbali ya bima ya afya kwa wafanyakazi wa sekta rasmi na zisizo rasmi pamoja na mwananchi mmoja mmoja.

Amesema hivi sasa wanavyo vifurushi vya aina mbalimbali kulingana na hali ya wananchi na kila kifurushi mchangiaji anapata huduma zote zikiwemo matibabu na dawa”Mfano kuna makundi mbalimbali yameingia kama bodaboda,machinga hata wakulima na wavuvi lakini hata kama huna kikundi unaweza kuingia kupitia kifurushi cha najali,wekeza au timiza kwani viwango vya michango ni nafuu sana”.

Wakati huo huo Mkurugenzi wa idara ya tiba kutoka wizara ya afya Dkt. Grace Maghembe amesema kuwa suala ya watu kutokufanya mazoezi au kutojishughulisha mwili ni moja la tatizo la ongezeko la magonjwa yasiyoambukiza

Amewata wananchi wabadilishe mtindo wa maisha kwa kutokula vyakula vya wanga kwa kula kiasi wanachoweza kukitumia kwani ni kisibabishi cha mafuta ambayo yanakwenda kwenye mishipa ya moyo na kusababisha matatizo ya moyo na shinikizo la damu”turudi kwenye kula vyakula vyetu vya asili ikiwemo matunda na mboga mboga

Hata hivyo ameshauri wananchi kujenga tabia ya kwenda kupima afya zao walau mara mbili kwa mwaka kwani wagonjwa wengi wanaenda kwenye vituo vya kutolea huduma pale ugonjwa unapokuwa hatua nyingine ambayo inakua ngumu kutibika


Share:

Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi Apangua Hoja za Wapinzani


 MSEMAJI Mkuu wa Serikali ya Tanzania, Dkt. Hassan Abbasi ameliambia Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) kuwa Watanzania wamemaliza uchaguzi na sasa wanaendelea na michakato ya kidemokrasia, kisheria na kikatiba ya kujenga taasisi za nchi ili kazi iendelee na kamwe hawapotezi muda na kile alichokiita “maigizo” ya baadhi ya viongozi wa upinzani hasa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

“Hivi ninavyoongea na wewe mchakato unaofuata ni bunge kuanza, watachagua spika, watapelekewa jina la waziri mkuu kumthibitisha na kisha rais atazindua bunge, hao walioshindwa uchaguzi na kuanza tuhuma ni maigizo yao ambayo tumeyazoea kila mara wanaposhindwa,” amesema.

Akijibu  madai ya baadhi ya viongozi wa Chadema kuhofia usalama wao na hata kujaribu kuomba hifadhi ya ukimbizi nje ya nchi  Abbasi alishangazwa na madai hayo na kuhoji wametishiwa usalama wao na nani, wapi na lini?

“Mkataba wa Kimataifa wa Mwaka 1951 unaohusu Haki na Hadhi za Wakimbizi kwa mfano unaainisha bayana taratibu za kuwa mkimbizi, huwezi kuamka asubuhi tu ukajitangaza wewe ni mkimbizi au una kesi ya jinai ukataka kukimbia nchi kisa kudai ukimbizi.

“Mtu anaibuka anadai ametishiwa maisha lakini juzi tu katoka kushiriki kampeni siku 60 na amelindwa salama kabisa leo kashindwa anakwambia anahofia maisha. Mkimbizi gani anavuka mpaka mbele kaandaliwa gari ya kumchukua? Haya ni maigizo,” alisema.

Amesisitiza kuwa Serikali ya Tanzania itaendelea kuenzi misingi ya amani na kuwataka Watanzania kuendelea kuchapa kazi, anayehofu usalama wake atoe taarifa kwenye vyombo vya dola 

==>>Msikilize hapo chini



Share:

Ndugai: Niko Tayari Kuliongoza Bunge Kwa Haki Na Usawa Bila Ubaguzi


Na Beatrice Sanga, MAELEZO
MBUNGE wa jimbo la Kongwa ambaye alikuwa mgombea pekee wa nafasi ya Spika katika Bunge la 12 la Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amechuguliwa kuwa Spika wa Bunge hilo kupitia kura zilizopigwa na wabunge waliohudhuria kikao cha kwanza cha bunge hilo baada ya uchaguzi mkuu uliofanyika leo Oktoba 28,2020 kilichofanyika  katika ukumbi wa Bunge Jijini Dodoma.

Ndugai amepigiwa kura na wabunge 345 na kupata asilimia 99.7 za kura zote zilizopigwa ambazo zimemuwezesha kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa muhula wa pili.

Akizungumza mara baada kuchaguliwa, Ndugai amewapongeza wabunge wote walioaminiwa na kupewa nafasi na wananchi  ili waweze kuwasemea changamoto zao na kuwataka wafanye kazi kwa bidii na kuwaletea maendeleo Watanzania waliowapa nafasi kwa kuwa wamewaamini na ndiyo maana wakawatuma ili waweze kuletewa maendeleo kupitia wao pamoja na kushikriki vyema katika utungaji wa sheria.

 “Ni heshima kubwa sana, matarajio ya wananchi wenu ni makubwa sana kwa kila mmoja wetu, tunao wajibu  mkubwa mbele yetu wa kuhakikisha kwamba hatuangushi matumaini ya wananchi. Watanzania hawa waliotuamini tuwe  wawakilishi wao katika nyumba hii tukufu na nina amini kila mmoja hatasahau hata mara moja jukumu la msingi la uwakilishi na kutunga sheria zilizo bora.” Amesema Ndugai

Aidha, ameongeza kuwa kazi za Bunge lazima zionekane na wananchi wanatakiwa kupewa taarifa ya nini kinachoendelea bungeni na ameviomba vyombo vya habari kuwa mstari wa mbele kutoa kazi za bunge ili ziweze kuwafikia wananchi kwa haraka zaidi ili waweze kujua mambo ambayo viongozi wao wanawasemea Bungeni

 Spika Ndugai amesema kuwa yuko tayali kuliongoza Bunge hilo  kwa haki na usawa  bila ubaguzi na atakuwa mstari wa mbele kutatua matatizo ya wabunge  na kuhakikisha anashughulikia  kwa ukaribu mambo yote muhimu yanayowahusu wabunge wote bila ubaguzi wa aina yoyote huku akiahidi kuwalinda wabunge wa upinzani walioko Bungeni

“Ndugu zetu wa upinzani mlioko humu ndani mna haki kabisa na moja ya kazi kubwa nikayofanya ni kuhakikisha kwamba na ninyi mnasikika tena vizuri zaidi, lazima tusikike wote.” Ameongeza Spika Ndugai

Amewataka wabunge wasome na kuzifahamu vizuri kanuni, sheria na taratibu mbalimbali za Bunge ambazo zitasaidia kuboresha nidhamu na kusimamia shughuli za kila siku Bungeni

“ Ninaomba sana tusome kanuni na tuzipitie kwa makini na tuzielewe kwa sababu humu ndani hatuwezi kwenda sawa bila kuzijua kanuni kwa hiyo tuzisome, tuzipitie na tuzielewe na baada ya Bunge hili tumeandaa semina ambazo zitatusaidia kutufungua macho na kutusaidia sisi kama wabunge kujua nafasi yetu katika jamii.” Amebainisha Ndugai


Share:

Ofisi Ya Jengo La Utawala Halmashauri Ya Wilaya Ya Busega Yakabidhiwa


Ofisi ya Jengo la Utawala la Halmashauri ya Wilaya ya Busega limekabidhiwa tayari kwa matumizi. Makabidhiano hayo yamefanyika siku ya Jumatatu tarehe 9 Novemba, 2020. Jengo la Utawala limekabidhiwa na Mkandarasi wa Ujenzi wa Jengo hilo Kampuni ya BMB kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya  Busega Anderson Njiginya, pia tukio hilo limeshuhudiwa na Mhandisi Mshauri kampuni ya NEDCo na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega.

Jengo la Utawala la Halmashauri ya Wilaya ya Busega lina jumla ya vyumba 97 ambapo jumla ya vyumba 68 vikiwa tayari kwa matumizi, ambayo ni zaidi ya asimilia 70% ya ukamilikaji wa jengo lote. Jengo la Utawala la Halmashauri ya Wilaya ya Busega lilianza kujengwa mnamo Mwaka 2015 ambapo Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliweka Jiwe la Msingi Mwaka 2016.

Aidha Jengo hilo ambalo likikamilika lote litagharimu jumla ya TZS Bilioni 4.9 linatatua changamoto ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega kukosa miundombinu na mazingira bora ya kufanyia kazi, kwani jengo linalotumika kwa sasa halikidhi idadi ya watumishi. Aidha kukabidhiwa kwa jengo hilo kunapunguza gharama ya fedha zilizokuwa zikitumika kwaajili ya kulipia jengo linalotumika kwasasa tangu hapo Halmashauri ilipoanzishwa mwaka 2013.

MWISHO.





Share:

Rais Mwinyi Akutana Na Tume Ya Uchaguzi Zanzibar


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kushoto) akizungumza na Viongozi wa Tume ya Uchaguzi  Zanzibar (ZEC) alipokutana nao leo Ikulu Jijini Zanzibar kwa ajili ya kuwashukuru na kuwapongeza kwa kazi ya kufanikisha vyema  Uchaguzi Mkuu uliopita hivi karibuni



Share:

TECNO Camon 16 Kuja Kuwapindua Wapinzani Wake.


Ni wazi kuwa katika ulimwengu wa simu janja watumiaji hawaridhiki tena na sura nzuri ya simu pekee, Mchanganyiko wa muonekano, pamoja na kazi ambazo simu huweza kufanya imekuwa sababu kubwa ya kuamua simu gani ya kununua. 

Hata hivyo, "uwezo wa kamera" kwa simu janja sasa imekuwa ni msamiati unaotumiwa sana katika tasnia hii. Kampuni nyingi za simu janja hushindana kwa bidii ili kuwa simu bora yenye sifa nzuri lakini pia yenye uwezo mkubwa wa kupiga picha. 


Hivi karibuni, kampuni nyingi zimezindua bidhaa zao mpya za simu janja, kama vile OPPO, TECNO (http://www.TECNOMobile.com), Samsung, Huawei, Vivo, Realme, Xiaomi na zingine, na hii imesadia kuwapa vijana wa leo chaguzi zaidi. Wakati huu tulichagua simu nne za hivi karibuni za Android kufanya ulinganisho na kujua ni nini kinacho fanya kazi kwa ubora Zaidi kwenye simu hizo. Simu hizo ni Pamoja na TECNO CAMON 16 Premier, Samsung A51, Huawei Y9, na OPPO A9. 


Uwezo wa kamera - kamera za mbele na nyuma
Ni ukweli usio pingika kuwa simu bora kuliko zote sokoni ni lazima iwe na kamera bora, na hapa ndipo inapokuja TECNO CAMON 16 Premier e, simu hii inakuja na kamera kuu ya Megapixel 64 MP, wakati Samsung A51 na OPPO A9 zinakuja na kamera ya kuu za hadi megapixel 48MP, huku Huawei Y9 ikiwa na kamera kuu ya 24MP.  


Mbali ya hayo, TECNO CAMON 16 Primer ina kamera ya mbele ya 48MP, wakati Samsung A51 inakuja na kamera ya mbele ya 32MP, OPPO A9 na Huawei Y9 zote zinakuja na kamera za Megapixel 16 MP. Mlinganisho huo unaonyesha wazi kuwa picha zinazopigwa na TECNO Camon Premier zitakuwa na mwanga zaidi na hivyo zitakuwa na ubora kuliko picha zinazopigwa na simu nyingine hapo juu. 


Ikiwa wewe ni mpenzi wa picha, au unatumia simu kupiga picha kwenye matukio muhimu, TECNO CAMON 16 Premier lazima itakufaa sana. Lakini pia, kama wewe ni mpenzi wa selfie, TECNO CAMON 16 Premier inakuja na kamera ya Megapixel 48 ambayo itakusaidia kupiga picha nzuri na angavu, Pia kama wewe unapenda kushiriki nyakati nzuri na marafiki au ndugu na jamaa, Camon 16 Premier inakuja na kamera ya mbele ya ziada yenye Megapixel 8 ambayo itakusaidia kuchukua picha zako ukiwa na ndugu na jamaa kwa urahisi Zaidi (Group Photo).

 
Uwezo huo mkubwa wa kupiga picha unawezeshwa na processor yenye nguvu ya Mediatek MTK G90T ambayo imetumika kwenye simu hii ya Camon 16 Premier. Processor hii inaipa nguvu simu ya Camon 16 Primier hadi kufikiwa 2.05GHz. 


Bila kujali kama ni usiku au mchana ni wazi kuwa kupata picha bora imekuwa ni jambo la muhimi, TECNO CAMON 16 Premier inakuja na teknolojia ya Super HIS na EIS+AIS, na wakati huohuo simu hii pia inakuja na teknolojia ya HIS hybrid intelligent anti-shake technology. Teknolojia zote hizi zinakusaidia kupiga picha vizuri wakati wa usiku ikiwa Pamoja na kuchukua video ambazo ni bora Zaidi bila kuwa na mitetemeko kwenye video hata kama unachuku video huku unatembea. 


Mbali na teknolojia hiyo, TECNO CAMON 16 Premier inakuja na teknolojia inayo kuwezesha kuchukua video za taratibu au Slow Motion hadi kufikia kiwango cha fremu 960. Hii yote inawezekana kutokana na simu hii kuwa na uwezo mkubwa wa processor Pamoja na RAM ya GB 8 ambayo ndio hufanya kazi hii kuwa rahisi Zaidi. 


Battery
Simu kuwa na battery yenye uwezo wa kudumu na chaji kwa muda mrefu imekuwa ni jambo la muhimu miongoni mwa watumiaji wa simu janja. TECNO CAMON 16 Premier inakuja na battery yenye uwezo wa 4500mAh ambayo pia inakuja na teknolojia ya quick charge ambayo inaweza kuchaji battery hiyo hadi asilimia 70 kwa muda wa dakika 30. 


Huu ni uwezo mkubwa sana ukilinganisha na simu za Huawei Y9 na Samsung A51 ambazo zinakuja na battery ya 4000mAh. Japokuwa Oppo A9 inayo battery kubwa ya 5000mAh, ni wazi kuwa teknolojia ya Quick charge ya TECNO CAMON 16 Premier ni bora Zaidi na salama hasa ukizingatia simu hii inakuja na teknolojia ya kuzuia simu hii kupata joto kwa haraka hasa inapokuwa inachaji kwa kutumia teknolojia ya Quick Charge.  


Kioo
TECNO CAMON 16 Premier inachukua taji pale linapo kuja swala la kioo, Simu hii inakuja na kioo kikubwa cha inch 6.85, kioo ambacho kinafaa Zaidi kwa wapenzi wa kucheza game kwenye simu, Pamoja wapenzi wa kuangalia filamu na tamthilia kwenye simu. Tofauti na simu nyingine kama Samsung A51 na OPPO A9. Camon 16 Premier inakuja na kioo chenye resolution ya 90Hz ultra-clear resolution ambayo inafanya kioo cha simu hii kuwa angavu na chenye kuonyesha rangi halisi na kufanya kazi kwa haraka Zaidi. 


Kwa sababu ya hii, TECNO CAMON 16 Premier imehamisha sehemu ya ulinzi ya fingerprint kutoka chini ya kioo na sasa sehemu hii inapatikana kwa pembeni mwa simu hii. Hii inafanya kuwa rahisi Zaidi kufungua simu yako hata kama umeshika simu yako kwa mkono mmoja. 


Hitimisho
Baada ya kulinganisha simu hizo zote kwenye mambo yote hayo ni wazi kuwa, TECNO CAMON 16 Premier ni simu bora na tofauti kati ya simu hizo nne. Simu hii inakuja na sifa zote ambazo mtumiaji makini angetamani kuzipata, ikiwa Pamoja na uwezo bora wa kudumu na chaji, kamera nzuri, kioo bora chenye kuonyesha rangi angavu, Pamoja na muundo mzuri wa kisasa, ni wazi kuwa simu hii inakuja na teknoloijia bora na sifa bora kwa gharama nafuu sana kuliko simu zote hapo juu.  


Tembelea https://www.tecno-mobile.com/tz/home/#/ kufahamu mengi zaidi kuhusiana na bidhaa zake
.




Share:

PICHA: Waziri Mkuu Mstaafu,majaliwa Aapa Kuwa Mbunge Wa Ruangwa

 Waziri Mkuu Mstaafu, na Mbunge wa Jimbo la Ruangwa Kassim Majaliwa akiapa kuwa mbunge wa Ruangwa, Bungeni Jijini Dodoma Novemba 10, 2020.

Waziri Mkuu Mstaafu, na Mbunge wa Jimbo la Ruangwa Kassim Majaliwa akipokea Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kanuni za Kudumu za Bunge kutoka kwa Katibu wa Bunge Stephen Kagaigai wakati alipoapa Bungeni Jijini Dodoma, Novemba 10, 2020.

Share:

Super Majinjas: Dawa Bora ya nguvu za Kiume


 ASILIMIA KUBWA YA WANAUME  WANAUPUNGU WA NGUVU ZA KIUME( SUPER MAJINJAS)
Ni dawa bora ya kutibu na kumaliza matatizo yote ya nguvu za kiume na sababu zake zote kama vile, ♤ kuwahi kufika kileleni dakika moja  ♤ maumbile kusinyaa na kulegea wakati wa tendo ♤ kukosa hamu ya tendo la ndoa ♤ kushindwa kurudia tendo la ndoa ♤ uume kusimama kwa kulegea ♤ uume kulegea katikati ya tendo ♤ kuathirika kwa kujichua kwa muda mrefu ♤ kuishiwa nguvu kutokana na punyeto.

Epuka aibu hii leo kwa kutumia SUPER MAJINJAS kiboko ya matatizo haya.
***********
Pia kuna MAKAKANUA ni Kiboko ya maumbile ya kiume madogo, inaboresha maumbile ya uume kwa kurefusha nan kunenepesha
***********
Kwanza fahamu sababu zinazopelekea kuwa na upungufu wa nguvu za kiume na uume mdogo.
*********
(1) kujichua (punyeto) kwa muda mrefu maana hupelekea misuli ya uume kulegea.
(2) ngiri (3) kuugua chango la uzazi kwa muda mrefu.
(4) kupungukiwa hormone za testosterone.
(5) ulaji wa vyakula vyenye mafuta mengi na visivyo na virutubisho  vya kutosha.
(6) kutokufanya mazoezi na mwenendo wa maisha.
(7) kisukari.
(8) tumbo kuunguruma na kujaa gesi.
(9) maumivu ya kiuno nk.
***********
MTINJETINJE NI
 dawa ya sukari inatibu tatizo mojakwamoja

Kwanini uhangaike? Kwanini uhuzunike?
Hii ni spesho kwa waliotumia madawa mengi bila kufanikiwa hakika hautajuta kuitumia.
WASILIANA NA:
TABIBU DITTU
SIMU NO:
📞WHATSAPP +255714448999  0789935470
Popote ulipo huduma hii inakufikia


Share:

Ndugai: Hakuna Kubebana.... Ukiwa Mbunge Bubu Umekwisha


 Spika mteule wa Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai, amewataka wabunge waliochaguliwa na wananchi kutokaa kimya ndani ya Bunge kwani wananchi wamewachagua kwa ajili ya kuwasemea changamoto na kutafutiwa ufumbuzi.

Akizungumza baada ya kuteuliwa kuwa Spika wa Bunge, Ndugai amesema, wabunge wanapaswa kujua walichokifuata ndani ya Bunge na kukaa kimya sio nidhamu bali ni kutowandekea haki wananchi waliowachagua.


“Ni kweli kabisa wabunge wengi wa bunge la 12 wanatoka CCM lakini hilo halimaanishi kwamba bunge hili sasa litakuwa la ndiyo,  ndiyo,  ndiyo wala haimaanishi kwamba bunge hili litakuwa la hapana, hapana, ni bunge ambalo naamini litatekeleza wajibu wake kama ipasavyo.

“Hakuna kubebana, niwape usia wabunge wageni na wengine waliokuwepo, ukichagua kuwa mbunge bubu, usiyesema, unayejipendekeza, husemi chochote, upoupo tu, eti ili uonekane una nidhamu kwenye chama au mahali kwingine umeliwa, usidhani kwamba jambo hilo kwa wananchi wako lina tija, utakuwa umejimaliza kwa wananchi wako."Amesema Ndugai ambaye amewahi kuwa Naibu Spika wa Bunge la 10 na Spika wa Bunge la 11.



Share:

Job Ndugai Achaguliwa Kuwa Spika wa Bunge


Job Ndugai amechaguliwa kuwa Spika wa Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Uchaguzi wa Spika, umefanyika leo Jumanne tarehe 10 Novemba 2020 bungeni jijini Dodoma katika Kikao cha kwanza, Mkutano wa kwanza wa Bunge la 12.

Mkutano huo wa uchaguzi, umesimamiwa na Mwenyekiti wa muda, William Lukuvi ambaye ni mbunge mteule wa Ismani kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo, Katibu wa Bunge, Stephen Kagaigai amesema, kura 345 zilipigwa, na Ndugai ameshinda kwa kupata kura 344 huku kura moja ya hapana, hivyo kuibuka kwa ushindi wa asilimia 99.7.

Baada ya kumaliza kutangazwa matokeo hayo, Ndugai aliapishwa na Katibu wa Bunge, Stephen Kagaigai.



Share:

Donald Trump amfuta kazi Waziri wa Ulinzi Mark Esper


Rais wa Marekani Donald Trump amemfuta kazi Waziri wa Ulinzi Mark Esper kuashiria kuwa huenda akatumia miezi yake ya mwisho madarakani baada ya kushindwa kwenye uchaguzi kufanya maamuzi ya kulipiza kisasi katika serikali yake.

 Trump alikuwa amezozana na Esper kuhusu msururu wa masuala na alikasirishwa hasa na hatua yake ya kupinga hadharani vitisho vya Trump vya matumizi ya wanajeshi katika kupambana na maandamano ya kupinga ubaguzi wa rangi baada ya polisi kumuua George Floyd mjini Minneapolis. 

Trump alisema kwenye Twitter kuwa Christopher Miller, mkurugenzi wa Kituo cha Kitaifa Kupambana na Ugaidi, anachukua usukani kama kaimu waziri wa ulinzi. 

Miller, mwenye umri wa miaka 55, amekuwa mkurugenzi wa kituo hicho tangu Agosti. Ni mwanajeshi wa zamani aliyehudumu jeshini kwa miaka 31.



Share:

Bunge La 12 Laanza Kwa Kumchagua Spika wa Bunge


Mkutano wa kwanza wa Bunge la 12 umeanza leo jijini Dodsoma  wakati Watanzania wakiwa na shauku ya kufahamu nani atateuliwa kuwa waziri mkuu wa Tanzania katika muhula wa pili wa uongozi wa Dk John Magufuli.

Kwa mujibu wa katibu wa Bunge, Stephen Kagaigai miongoni mwa shughuli zitakazofanywa katika Bunge hilo leo ni kusomwa kwa tangazo la Rais kuliitisha Bunge hilo kwa ajili ya kujadili maendeleo ya wananchi, kutunga sheria mpya pamoja na kuzibadili zilizopo.

Kagaigai alisema baada ya kusomwa kwa tangazo la Rais, utafanyika uchaguzi wa spika na naibu wake, nafasi zinazotetewa na waliokuwapo, Job Ngugai kutoka Jimbo la Kongwa na Dk Tulia Ackson aliyechaguliwa kuwakilisha Mbeya Mjini.

Baada ya uchaguzi huo na spika kula kiapo, wabunge wateule nao, wawakilishi 264 waliochaguliwa majimboni pamoja na 105 wa viti maalumu watano kutoka Baraza la Wawakilishi Zanzibar, wataapa.

Shughuli nyingine kubwa itakayofanyika leo ni kuthibitisha jina la waziri mkuu litakalowasilishwa bungeni na Rais John Magufuli.

Ingawa Rais Magufuli amewahakikishia wateule wa Serikali aliohudumu nao katika miaka mitano ya kwanza kuendelea na nafasi za uteuzi walizokuwa nazo, bado Watanzania wanasubiri kujua kama atafanya mabadiliko yoyote katika nafasi muhimu ya waziri mkuu ama la.


Share:

Mwenyekiti Wa CCM Rais Dkt.Magufuli Azungumza Na Wabunge Wateule Wa Ccm Jijini Dodoma



Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger